Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-02-10

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


adha
Hata hivyo Shule ya Sekondari ya Azania iliyopo Ilala, Dar es Salaam imeamua kuondoa adha ya mabaki kwa kubuni matumizi mengine mazuri kwa maslahi yao. [1]
aina
Maiti hiyo ilikutwa katika maegesho ya magari yaliyo ghorofa ya kwanza ya jengo hilo, ikiwa na majeraha ya kisu sehemu ya mgongoni na kifuani na ikiwa imevunjikavunjika viungo vyake na kuhifadhiwa kwenye begi la nguo ambalo liliwekwa ndani ya buti la gari aina ya Toyota Corola iliyokuwa imeegeshwa kwenye eneo hilo. [2]
ajabu
Tena niliota ndoto ya ajabu sana na nawaomba waishiwa wasomaji wangu wanisaidie kuelewa ndoto hii. [3]
akioza
Samaki mmoja akioza, wote wameoza. [4]
alihoji
Unafikiria ni nini kitatokea," alihoji. [5]
ambalo
Jaji Masatti alisema kuwa ingawa kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, watuhumiwa walifika katika eneo la tukio wakati wa kuwakamata eneo la Sinza, hakuna ushahidi kuwa walikwenda eneo la mauaji ambalo ni Msitu wa Pande. [6]
amekuwa
Mwinyi, ambaye pia ni Mbunge wa Kwahani Zanziabr akitokea Mkuranga Pwani, ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar na wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanika, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, amekuwa akitajwa katika kinyang'anyiro cha kuingia Ikulu ya Zanzibar. [7]
ana
X anaonekana ni mtu mwenye mafanikio makubwa kwa sababu ana nyumba nzuri na ana uwezo wa kutimiza mahitaji yake yote n. [8]
anahisi
Sisi kama wanafunzi wa Azania tunajivunia kuwa na mtambo mkubwa kama huu na tunamshukuru Mkuu wa shule kwa kukubali na kuruhusu kujegwa mtambo huo shuleni hapa jambo ambalo limetusaidia hasa tunaochukua masomo ya sayansi," anaongeza Mnaku ambaye anahisi ni shule yao pekee yenye mtambo kama huo Dar es Salaam. [9]
anataka
Hakusikilizi, anataka umsikilize. [10]
anaweza
Tukikubaliana na maana hiyo basi maelezo yanayofuata ni kwamba kila mtu anaweza kuyatafasiri mafanikio katika mtazamo wake. [11]
atakuwa
Washtakiwa wengine nao walisema watakuwa na mashahidi isipokuwa mshitakiwa wa 11 ambaye alisema atakuwa shahidi mwenyewe. [12]
au
Jaji Masatti alisema Zombe kwa nafasi yake aliyokuwa nayo wakati huo ya mkuu wa upelelezi wa mkoa na kaimu kamanda wa polisi mkoani Dar es Salaam alikuwa katika nafasi nzuri ya kujua kila tukio la uhalifu lililokuwa likiendelea jijini na hata kutoa maelekezo au maagizo ambayo ni sahihi. [13]
badala
Chanzo mojawapo cha kushuka kwa ufaulu katika shule za msingi wilayani Serengeti ni wakaguzi wa elimu wa shule za msingi hawafanyi kazi yao badala yake wanajihusisha na biashara ya kuwakopesha fedha walimu wakati ni kinyume cha kazi yao," alisema Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Edward Ole Lenga. [14]
bila
Haki ya pili alisema kuwa wanaweza kutoa ushahidi bila kiapo na hivyo hawataulizwa maswali na haki ya tatu alisema ni kutoa ushahidi kwa kiapo na wataulizwa maswali na hata kuleta mashahidi kama wanao. [15]
bomba
Akiwa nchini, Rais Banda atakuwa na mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete na kutembelea bomba la mafuta la Tanzania na Zambia (Tazama). [16]
chake
Mara baada ya kuelezwa kuwa hawana kesi ya kujibu Noel alionekana akifuta chozi la furaha kwa kitambaa chake cheupe, huku Nyangelela akilengwalengwa na machozi ya furaha na kujifuta kwa viganja vyake. [17]
dhamira
Akizungumzia uamuzi wake wa kuchukua fomu Ngabo alisema kuwa hilo limetokana dhamira yake ya kweli ya kurudisha heshima ya mchezo huo nchini. [18]
dhidi
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandaro Alhamisi atakabidhi bendera kwa timu ya Prisons ya Mbeya inayoondoka kwenda Tripoli, Libya kwa ajili ya mechi yake ya maludiano ya kuwania Kombe la Shrikisho la Soka Afrika (CAF) dhidi ya timu ya Khalij Sert. [19]
dogo
Ni kama zali, kwani mchezaji huyo alisajiliwa kipindi cha dirisha dogo na kuanza kuichezea JKT Ruvu na ameonyesha kiwango kikubwa katika mechi tatu alizocheza na timu hiyo hata kumshawishi Maximo kumuongeza katka kikosi chake. [20]
es
HATIMAYE Mahakama Kuu imetegua kitendawili cha hatima ya aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoani Dar es Salaam, Abdallah Zombe na wenzake 12 baada ya kuamua kuwa, wana kesi ya kujibu katika tuhuma zinazowakabili za mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva wa teksi mmoja, huku ikiwaachia watuhumiwa watatu. [21]
faida
Nuru anasema maji yanayotoka katika mtambo huo ni mbolea mbayo inaweza kustawisha mimea ya aina yoyote na faida za mtambo huo ni kuhifadhi mazingira na pia umepunguza gharama za shule katika ununuzi wa mkaa. [22]
fulani
Kwanza miji ya Dakar na Durban ina ushirikiano na Jiji la Dar es Salaam na wao kwa kiasi fulani wamefaidika na mikutano kama hii, kwa hiyo ninaamini kabisa majadiliano haya yatatupa suluhisho la jambo la kufanya," alisema. [23]
gani
Katika mkutano wetu tutapata fursa ya kujadili jinsi gani ya kukuza vipaji vya wanafunzi kupitia michezo kwa kuwa hivi sasa hiyo ni sehemu ya ajira sawa na masomo mengine" alisema Mkono. [24]
gesi
Wanafunzi na wanajumuiya wa shule hiyo wakishirikiana na Taasisi ya Teknolojia ya Vijijini ya Dar es Salaam (ARTI-Tz) na Tume ya Sayansi na Teknolojia wametengeneza mtambo wa kutengeneza gesi (bio-gas) kutokana na mabaki ya vyakula. [25]
haitambui
Kwa serikali ambayo haitambui uchawi walimu hao watakuwa na wakati mgumu kuthibitisha ukweli huo kisayansi. [26]
hana
Alisema, kwa mujibu wa katiba ya nchini, kila mtu hana huru wa kutoa maoni na kwa hiyo, waliosambaza ujumbe huo wametiza haki yao. [27]
hao
Mahakama imeridhika kuwa washtakiwa hao watatu katika kesi hiyo namba 26 ya mwaka 2006 hawana kesi ya kujibu. [28]
hapa
WALIMU wa michezo katika shule za Sekondari wilayani hapa, wameandaa mkutano maalum utakaowawezesha kujadili mikakati ya kuendeleza pamoja na kupanga ratiba ya michuano ya kanda. [29]
hasa
Alifafanua kuwa, kama serikali haitokuwa makini na kero za walimu hasa kuhusu maslahi yao, kuna uwezekano baadhi ya walimu wengi wazuri kukimbilia shule binafsi. [30]
hatutaki
Sisi hatutaki, hatutaki lakini tutatupwa kama hao. [31]
hawa
Madiwani naomba mjue hili msiulize ni kwa nini mnasema hali ya taaluma ni mbaya, ni kwa sababu hawa mnaotegemea kusaidia kuinua elimu ndio wanaofanya biashara ya kukopesha. [32]
hayuko
Atataka umfanyie hiki umfanyie hiki lakini yeye hayuko tayari kwa lolote juu yako. [33]
hewa
Alisema mkutano huo pia utajadili matatizo yanayoikumba sekta ya utalii nchini, mabadiliko ya hali ya hewa na utunzaji wa fukwe za bahari. [34]
hii
Mwaka jana kulikuwa na migogoro mingi kati ya walimu na serikali, ambapo hadi leo hii hakuna lolote lililofanyika. [35]
hiki
Kitendo hiki kinaonyesha kuwa alikuwa akijua kilichotendeka kwa marehemu. [36]
hili
Hata hivyo, katika hili hatuhitaji kutafuta mchawi, bali ukweli ni kwamba, kuna sababu nyingi zilizochangia hali hiyo, lakini baadhi yake ni kukosa walimu wazoefu na mgogoro wa walimu na serikali uliokuwepo mwishoni mwa mwaka jana. [37]
hizi
Binafsi sichoki kumshukuru Mungu kwa hizi neema alizonijaalia nazo. [38]
hizo
Jaji Masatti, akijibu hoja za wakili wa mshtakiwa wa 11, Koplo Rashid Lema, na mshtakiwa wa 12, Koplo Rajabu Bakari, alisema ingawa katika maelezo yao waliyoyatoa kwa timu ya polisi ya upelelezi wa tukio hilo washtakiwa hao hawakubali kuwa walihusika, lakini kuna baadhi ya vigezo vinavyowahusisha na tuhuma hizo. [39]
huenda
KIUNGO mpya wa Taifa Stars, Mwinyi Kazimoto huenda 'akavaa viatu' vya Athuman Idd 'Chuji' kutokana na mchezaji huyo wa Yanga kuwa majeruhi. [40]
huko
Tumejitoa, kwani tumejaribu kwa wahisani mbalimbali, nako imeshindikana na chama hakina fungu la kutosha kupeleka huko (Rwanda) wanamichezo wetu. [41]
humo
Alisema mkutano huo utasaidia kupata njia ya kudhibiti wimbi la watu wanaotoka vijijini kwenda Dar es Salaam na kuleta ongezeko lisilokuwa la lazima jijini humo. [42]
huru
Katika kesi hiyo washitakiwa walioachiwa huru jana ni pamoja na aliyekuwa mshitakiwa namba nne F.5912 PC Noel Leonard, aliyekuwa mshitakiwa wa sita D.6440,CP Moris Nyangelela na aliyekuwa mshitakiwa wa nane E6712 CPL Felix Cedrick. [43]
huu
Washitakiwa hao walifikishwa mahakamani Januari 27, mwaka huu na hadi leo bado wako rumande kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. [44]
ijayo
Haya shostito kazi kwako, mpaka wiki ijayo usikose kupitisha tena macho hapa. [45]
ili
Sababu nyingine aliyoibainisha Jaji Masatti kuwa imemfanya Zombe awe na kesi ya kujibu ni kitendo cha kuwaita ofisini kwake washtakiwa wengine walioshiriki katika tukio hilo la kuwakamata marehemu ili kuwapongeza. [46]
ilishindwa
Mwaka jana, Tanzania pia ilishindwa kushiriki mashindano kama hayo ya Kanda ya Tano Afrika kuwania tiketi ya kushiriki Michezo ya Olimpiki. [47]
iliyoko
Stars iliyoko kambini inajiandaa kwa mchezo wa kesho wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Zimbabwe utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. [48]
imara
Wanadai japokuwa ujenzi wake ulichukua wiki mbili, kwa uzoefu wao sasa mtambo huo unaweza kutengenezwa kwa siku tatu na ukakamilika kuwa imara kwa matumizi. [49]
ina
Miji mingi ina matatizo katika utunzaji wa fukwe za bahari na miundombinu ambayo inasababisha sekta ya utalii kuwa ngumu na mabadiliko ya hewa ambayo kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na ujenzi holela wa viwanda,"alisema. [50]
iwe
Hakuna daktari anayeweza kutibu masuala ya kiroho bali ni imani zetu kila mmoja kwa imani yake ili mradi iwe ni imani halali. [51]
iweje
Kama samaki mmoja aliyeoza anaozesha tenga zima, iweje kama karibu samaki wote wameoza? Yupo samaki mwingine atakayepona kweli? Ataozeshwa na yeye. [52]
jamani
Zombe hakuonekana kuwa mchangamfu kama awali na alipofuatwa na waandishi, alisema: “Tuonane kesho jamani. [53]
jengo
SAKATA la maiti ya mtu mwenye asili ya Asia, Abdulbasiti Abdallah, 21, iliyokutwa ndani ya gari kwenye jengo la J.Mall jana lilitinga polisi wakati watu watano pia wenye asili ya Asia, wakiwemo wanawake wawili, walipokamatwa wakihusishwa na mauaji hayo. [54]
jirani
UKIONA kiongozi wa familia anapita barabarani karibu na nyumba ya jirani yake na kuanza kuporomosha matusi kweupe, wazo litakalokujia haraka haraka ni kuwa labda amelewa pombe, tende au kitu kingine. [55]
joto
Mmoja wa wapishi wa shule hiyo, Stella James anasema mtambo huo umesaidia kwa kiasi kukubwa kupunguza adha na joto ambalo lilikuwa linawatesa wakati wa kupika vyakula. [56]
juu
Kwa upande wa Bageni, Jaji Masatti alisema kulingana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kuwa ndiye alikuwa kiongozi wa msafara uliokwenda kuwakamata marehemu maeneo ya Sinza, pia naye anapaswa aieleze mahakama juu ya majibizano ya risasi kati yao (polisi) na marehemu jinsi yalivyotokea. [57]
juzi
Mshtuko wa madiwani umetokana na ukweli kwamba kiwango cha kufaulu kilishuka mwaka jana hadi kufikia asilimia 46 kutoka asilimia 53 mwaka juzi. [58]
kaa
Kwa maana hiyo kama nafsi yako inakusuta kweli utaweza kujiamini? Siamini kamwe! Na kibaya zaidi ni kwamba kaa ukisubiri siku moja kuumbuliwa kwa sababu uovu wowote siku zote huacha nyayo nyuma yake. [59]
kali
Ole Lenga ametoa onyo kwa wakaguzi hao kuhakikisha wanaacha biashara hiyo mara moja vinginevyo serikali itawachukulia hatua kali kwa kuwa wamechangia kudumaza taalum wilayani humo. [60]
kambi
TBF ilikuwa ikisaka Shilingi milioni 45 kwa ajili ya maandalizi ya michezo hiyo ikiwemo kuweka kambi timu zote za wanawake na wanaume. [61]
kamwe
Kwa maana hiyo watu kama hao hata kama watapata utajiri wa kiwango gani, hawataweza kamwe kujiamini, kwa sababu tayari wamekengeuka kimaadili na dhambi hiyo inaweza kutenguliwa kwa wao kukiri hadharani dhambi hiyo. [62]
kana
Walibainisha kuwa uamzi huo wa madiwani wanauchukulia kama wa kisiasa lakini wanatakiwa kujua chanzo cha matatizo hayo ni nini wala si kuwawekea maazimio walimu wakuu kana kwamba wao wanapenda kufelisha watoto ambao wamekaa nao kwa miaka saba. [63]
kata
Kuanzishwa kwa sekondari za kata, kulikolazimu kuwahamisha walimu wengi wazoefu kwenda kuwa walimu wakuu wa shule hizo, pamoja na waliohamia sekondari za binafsi zikiwamo seminari kufuata masilahi, kumechangia kwa kiasi kikubwa kudhoofisha ubora wa elimu katika shule za umma. [64]
kazini
Baadhi ya matukio ambayo walimu hao wanadai kuwa yalichangia kuamua kumwita mganga huyo ni uwezo wa kimiujiza wanaodai anao mwalimu huyo ambaye, kwa siku nyingi, amekuwa akilalamikiwa kuwa anawaroga walimu wenzake shuleni hapo pamoja na kuwafanya wawe wanaugua mara kwa mara wakiwa kazini shuleni hapo. [65]
kigumu
Mgogoro wa walimu uliotokea Agosti hadi Oktoba, mwaka jana wakati watoto wanajiandaa na mitihani, pia umechangia kwa kiasi kikubwa matokeo kuwa mabaya, kwani wanafunzi walikosa maandalizi ya kutosha kutokana na kukosa walimu wa kuwasaidia katika kipindi hicho kigumu. [66]
kikao
Kwa sasa kwa kuwa kuma ATM sijui wanafanyaje," alisema katika kikao cha madiwani. [67]
kile
Naomba unielewe mwandishi, andika kile nilichosema, kama kuna mtu au kikundi cha watu wameandika vipeperushi na kusambaza taarifa hizo, basi ni vema,” alisema. [68]
kilo
Kova alisema baada ya kufanya mauaji hayo, watuhumiwa waliwaadaa wanandugu kwa kuwataka kupeleka kiasi cha Dola 100,000 za Kimarekani au kilo tano za dhahabu kama masharti ya kutokutekeleza mauaji kwa ndugu yao huyo. [69]
kina
Katika kipindi hiki wanafanyia uchunguzi wa kina tabia hiyo kwa lengo la kuwachukulia hatua kali wote wanaojihusisha na biashara hiyo kwa kuwa ni kinyume cha utaratibu wa kazi na kuwa tabia hiyo inakwamisha juhudi za maendeleo ya elimu wilayani humo. [70]
kubaini
Kamanda Kova aliongeza kuwa utaratibu wa kuchunguza watuhumiwa wote utafanyika kwa kutumia DNA na Forensic ili kubaini wahusika. [71]
kubaki
Kadhalika walimu hao wanadai kwamba wakitoka benki kuchukua mishahara yao wakifika shuleni hapo fedha zinapotea kimiujiza na kubaki watupu wanapofika nyumbani jioni baada ya kazi. [72]
kubwa
Ni aibu kubwa kwa serikali, shule zake kufanya vibaya, hivyo tunaomba mikakati iandaliwe kulipatia ufumbuzi suala hilo, ili kurejesha heshima yake, kama ilivyofanyika wakati wa utawala wa awamu ya pili kurejesha hadhi na heshima ya utumishi wa umma na ofisi za serikali uliokuwa umeporomoka. [73]
kuficha
Anadiriki kutoa aibu zako nje na kuficha za kwake. [74]
kujitoa
Baadaye CUF ilitangaza kujitoa. [75]
kukosa
Cheyo alisema timu hizo za Tanzani hazitaweza kushiriki mashindano hayo nchini Rwanda kwa kukosa kiasi hicho cha fedha ambacho kilikuwa kikihitajika kwa kila hali. [76]
kumbe
Imefikia hatua wakaguzi wanakaa na vitabu vya benki kwa madai kuwa wanawadai na walimu wamekuwa hawaishi katika ofisi za wakaguzi kumbe ni kwa ajili ya mikopo si ukaguzi kama watu wanavyodhani," alisema. [77]
kunuka
Na watu katika kutafuta samaki asiyeoza walianza kunuka na wao. [78]
kuomba
Hata hivyo, mawakili wanaowatetea washitakiwa hao tayari wamewasilisha maombi Mahakama Kuu kuomba kulegezwa kwa masharti hayo ya dhamana. [79]
kuona
Kwa ujumla, inasikitisha kuona shule za serikali ambazo zilitazamiwa kuonyesha mfano mzuri, zikiwemo zinazoitwa za vipaji maalumu zimeshukuka, hivyo kuondoa thamani ya kiwango chake. [80]
kupewa
Walisema kuwa miradi mingi ya nyumba za walimu na vyumba vya madarasa imekwama licha ya kupewa fedha kutokana na madiwani hao kuchukua kandarasi hali ambayo inafanya shule nyingi kukosa walimu kutokana na sababu hiyo. [81]
kusema
Katika hatua nyingine, waziri Membe alifafanua kuhusu mambo yaliyoafikiwa katika mkutano wa Umoja wa Afrika katika kuunda serikali ya Umoja wa Afrika na kusema Umoja huo hauwezi kuundwa kama miundombinu muhimu haitaboreshwa kwanza. [82]
kutafakari
Nikajaribu kutafakari. [83]
kutaka
Kelele za kutaka kuhama ziliongezeka zaidi baada ya mganga huyo aitwaye Frank Juma Kisonga kufika na kufukua katika moja ya madarasa hayo kile kinachoonekana kuwa ni uthibitisho wa ushirikina huo. [84]
kuwaambia
Tunajisikia furaha kuwaambia mambo yetu, siri zetu, mbinu zetu tunavyohisi, tunavyojisikia tukitegemea mambo mazuri kutoka kwao. [85]
kuzuia
Na japokuwa kuna matamko kadhaa ya kuzuia walimu kujishughulisha na biashara wakati wakiwa darasani hakuna mabadiliko ya maana. [86]
kwa
Zombe na wenzake wanashtakiwa kwa tuhuma za kufanya makosa manne ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka mjini Mahenge, Morogoro- Sabinus Chigumbi, maarufu kama Jongo, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi wa Manzese jijini Dar es salaam, Juma Ndugu. [87]
kwako
Na wanakuja kwako wakiwa wanapeperusha hii bendera ya urafiki. [88]
kwamba
Kuhusu washitakiwa wengine, Jaji Masatti alisema kwa kuwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo unadhihirisha kuwa walihusika katika kuwakamata marehemu na kwamba walikuwepo katika eneo la mauaji, basi wanayo kesi ya kujibu kuielezea mahakama jinsi marehemu walivyouawa. [89]
kwao
Mwaka jana vipeperushi kama hivyo vilisambazwa vikimlenga Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano Muhamed Seif Khatib na kuna wakati fulani vilisambaza vilisambazwa vikiwataka Wapemba kuhama Unguja na kurudi kwao. [90]
kweli
Mimi kitaaluma ni mwalimu na nafundisha shule binafsi, huku wanafunzi wanafundishwa kwa asilimia 80, hiyo 20 iliyobaki ndio wanatafuta wenyewe, hii ni tofauti na shule za serikali ambako kwa siku wanaweza kufundishwa kipindi kimoja tu au viwili kati ya vipindi sita, sasa hapo unategemea mwanafunzi atafaulu kweli?" alihoji Morris. [91]
kwenda
Leo rais huyo atatembelea bomba la Tazama na Bandari ya Dar es Salaam, eneo la Kitengo cha Makontena yanayosafirishwa kwenda Zambia. [92]
la
Akitoa uamuzi huo Jaji Masatti alisema ingawa ameridhika na hoja zilizotolewa na Wakili wa Zombe, Jerome Msemwa kuwa Zombe hakuwepo katika eneo la tukio, kuna ushahidi wa kimazingira ambao unamfanya mshitakiwa huyo awe na kesi ya kujibu. [93]
lake
Mtambo huo umeunganishwa katika majiko matatu na kila jiko lina tangi lake. [94]
lengo
Mkurugenzi wa Shirika hilo, Jane McRae alisema jana katika siku ya kwanza ya mkutano huo utakaodumu kwa siku nne, kuwa, lengo la kukutana na wadau hao ni kujadili mambo ya kufanya kuliboresha jiji hilo na majiji mengine barani Afrika yenye tatizo la ongezeko la wakazi. [95]
lenye
SHIRIKA linalosaidia kukuza maendeleo ya majiji duniani lenye makao yake makuu nchini Canada, (ICSC), limekutana na wadau wa jiji la Dar es Salaam na kujadili mbinu za kuliendeleza jiji hilo. [96]
leo
KESI ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh221 bilioni inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Joachim Liyumba na Meneja Mradi wa benki hiyo, Deograthias Kweka inaendelea leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu. [97]
licha
Maulid alisema Ligi Kuu ya Zanzibar inatazamiwa kuanza hivi karibuni licha ya kuibuka kwa utata kwa upande wa udhamini wa ligi hiyo ZANTEL na klabu zinazoshiriki ligi hiyo. [98]
likioza
Tenga moja likioza, litenge, tenga moja likioza, litenge, lituuupe. [99]
maana
Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa maiti hiyo kukutwa katika gari lenye namba za usajili T546 AMH lenye rangi ya kijivu, alisema uchunguzi wa awali uliofanywa na jeshi hilo umegundua kuwa marehemu na mtuhumiwa walikuwa marafiki wa karibu kwa kipindi kirefu na wote walikuwa wafanyabiashara ndio maana waliweza kutoka pamoja siku ya kifo chake. [100]
mabao
Prisons katika mechi yake ya kwanza iliyofanyika Dar es Salaam wiki iliyopita ilikubali kipigo cha mabao 2- 0 kutoka kwa Walibya hao. [101]
mada
Ni dhahiri wengi wa wasomaji wameridhishwa na mada yenyewe ambayo leo itazungumzia sehemu ya pili kabla ya kuanza kujadili mada nyingine. [102]
majira
Akiwa ameongozana na ujumbe wa watu sita, Banda, 71, aliwasili Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Nyerere majira ya saa 6:30 mchana. [103]
makala
Mtambo huu unatumia mabaki ya chakula kama vile wali, ugali, makande na aina mbalimbali za vyakula anavyokula binadamu pamoja na matunda," anasema Mkuu wa shule hiyo Donald Sigodalilwa alipohojiwa na mwandishi wa makala haya hivi karibuni. [104]
mara
Matukio ya baadhi ya watu kusambaza taarifa na vitisho kwa vipeperushi kama hivyo katika kisiwa cha Zanzibar, yamekuwa yakitumika mara kwa mara. [105]
mashabiki
Afisa Habari wa TFF, Florian Kaijage alisema kuwa viingilio hivyo vimeangalia hali za mashabiki wote na kuwataka wajitokeze kwa wingi ili kuishangilia timu hiyo. [106]
matenga
Kandokando yake yalikuwepo matenga ya samaki na mchuuzi alikuwa anayakagua moja moja. [107]
mbali
Jambo pekee litaloweza kuleta mabadiliko hapa ni kubadili mfumo wa ligi na kwenda na wakati kwa kuangalia ligi za nchi mbali mbali duniani. [108]
mbele
LIGI ya Taifa Ngazi ya Wilaya Tanga imeendelea kutimua vumbi katika wilaya tatu za Mkoa wa Tanga kwa timu mbalimbali kusonga mbele. [109]
mbovu
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, walisema kushuka kwa kiwango cha kufaulu kwa watahiniwa kumesababishwa na sera mbovu ya elimu. [110]
mchuuzi
Kwanza nilimwona mchuuzi wa samaki akiwa amesimama mbele ya meza yake ya biashara. [111]
mdomo
Hawezi kufunga mdomo wake kuzungumza mambo yako. [112]
mema
Kwa imani hiyo inafuata kwamba iwapo watu watafanya mambo mema kwa lengo la kulinda furaha ya wenzao na wakafanya hivyo kwa nia njema hakuna yeyote awaye wala mamlaka yoyote iwezayo kuwakwaza watu wa aina hiyo. [113]
mfumo
KOCHA wa Tanzania, 'Taifa Stars' Marcio Maximo ameponda mfumo mzima wa kuendesha wa Ligi Kuu ya Zanzibar kuwa umepitwa na wakati kwa sasa. [114]
mgumu
Malalamiko ya walimu yanaungwa mkono na Ole Lenga ambaye amepiga marufuku madiwani kuchukua kandarasi wilayani humo kwa kuwa wamekuwa tatizo kwa kukwamisha miradi ya ujenzi hali ambayo inapelekea kuifanya wilaya hiyo kuwa katika wakati mgumu. [115]
midogo
Ana miradi midogo midogo inayoweza kumfanya asiuguse hata mshahara wake. [116]
miezi
Maximo alisema kwa muda wa miezi minne sasa hakuna mechi ya Ligi Kuu yoyote inayochezwa kisiwani hapa sasa utawezaje kuteua wachezaji kutoka Zanzibar ? alihoji Mbrazil huyo. [117]
mikondo
Mwaka 1967 shule hiyo ilitaifishwa na mwaka 1987 ilipanuliwa zaidi na kuwa na mikondo 28 ikiwemo 24 ya sekondari ya kawaida (O- Level) na minne ya sekondari ya juu (A-Level). [118]
mingine
Kwa mujibu wa wanafunzi hao, mtambo huo umekuwa kichocheo kikubwa kwa wanafunzi kuchukua masomo ya sayansi tofauti na awali wakati bado haujatengenezwa, kwani wengi walikuwa wanakimbia masomo ya sayansi na kuchukua michepuo mingine. [119]
miradi
Wageni hao pia watakagua miradi ya maendeleo na kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na nchi zao. [120]
mkaa
Wapishi wanaipenda kazi yao kwani sasa wanapika chakula kingi bila kuungua na joto ikilinganishwa na wanavyopikia majiko mengine ya mkaa. [121]
mkubwa
Abimeleck Mnaku na Silas Michael, wanafunzi wa kidato cha tano wanasema tangu wateuliwe kuwa wasimamizi wa mtambo huo wamekuwa wakijifunza kwa makini na ustadi mkubwa hali inayowafanya wajione kuwa nao wanaweza kutengeneza mtambo kama huo kwa matumizi yoyote. [122]
mnuko
Au hata akibaki hajaoza, bado atanuka kama wenzie maana amekaa kwenye tenga la mnuko mtupu. [123]
mrefu
Alisema moja ya njia ya kuchaguwa wachezaji ni kuangalia katika ligi, lakini kwa muda mrefu hakuna mechi au mashindano magumu yoyote yanayoendelakatika kisiwa cha Unguja na Pemba. [124]
msingi
Alisema migomo na maandamano ya walimu na wanafunzi vimechangiwa kwa kiasi kikubwa sambamba na ukosefu wa maadili kwa baadhi ya walimu na wanafunzi ambao ndio msingi wa mafanikio kielimu. [125]
mwepesi
Rafiki huyu ni mwepesi kuchukua ya kwako na kukuletea ya watu. [126]
mwingine
Alimtaja mwanamasumbwi mwingine wa zamani na mwalimu maarufu wa mchezo huo anayewania nafasi ya ukatibu mkuu kuwa ni Remmy Ngabo. [127]
naamini
Mimi ni mchezaji mwenye uwezo mdogo sana na naamini kuna wachezaji wenye uwezo mkubwa lakini nafikiri kocha ana makusudi na mimi. [128]
nao
Alisema kwa ushahidi huo, ambao pia uliungwa mkono na mashahidi watatu, Pw30, Pw31 na Pw36, haoni sababu kwa nini nao wasiwe na kesi kujibu. [129]
naomba
Kwa hiyo naomba tukubaliane juu ya maana mpya ya mafanikio ambayo yataambatana na kujiamini. [130]
ndani
Alisema kitendo cha kuwaweka ndani ndugu wa marehemu, Venance Mchami (shahidi wa nne) na Emmanuel Likonga ,waliokwenda kutambua miili ya marehemu katika Hospitali ya Muhimbili, akiwatishia kuwaua na kuwataka wampelekee Benadetha Ngonyani (Pw2) ni sababu nyingine iliyomfanya awe na kesi ya kujibu. [131]
ndicho
Hicho ndicho wazazi wanadai kinachangia matokeo mabaya ya wanafunzi shuleni. [132]
ndivyo
Mtambo huu ukipewa chakula na maji kama inavyotakiwa ndivyo unavyotoa gesi kwa wingi na ukizidishiwa chakula unavimbiwa na hivyo kushindwa kutoa gesi inayotakiwa kwa matumizi ya kawaida," anaeleza. [133]
ndiyo
Hali hiyo, uchunguzi wa ofisi ya mkuu wa wilaya unaonyesha ndiyo inakwamisha mchakato mzima wa elimu wilayani hapo. [134]
ndoo
Wakati niliona siwezi kuvumilia tena na imebaki kuoza na mimi, wakaja watu wenye ndoo za maji na kuanza kuwamwagia watu wote huku wakiimba. [135]
ni
Jaji wa Mahakama Kuu, Salum Masatti alisema mahakama hiyo imeridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kuwa Zombe, ambaye ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo na wenzake tisa wana kesi ya kujibu kuhusiana na vifo vya wafanyabiashara hao. [136]
nia
Kauli ya Hiza inafuta zaidi matarajio ya kumalizwa kwa mgogoro wa kisiasa uliokikumba kisiwa hicho baada ya matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2005, mgogoro uliosababisha CCM na CUF kuingia kwenye mazungumzo ya muafaka nia ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. [137]
niaba
Akielezea sababu za kuwaachia huru washitakiwa watatu, Jaji Masatti alikubaliana na hoja za mawakili wao- Majura Magafu kwa niaba ya mshitakiwa wa nne na wa sita, na Rongino Myovela kwa niaba ya mshitakiwa wa nane. [138]
nimeloa
Lakini wale samaki wakanicheka tu na mimi nikakuta wenye ndoo wakinilenga na mimi hadi nilijikuta nimeloa. [139]
nk
MABAKI ya vyakula mbalimbali kama makande au wali au ugali pamoja na aina mbalimbali za matunda kama ndizi au maembe nk yakiachwa ovyo huoza na kutoa harufu mbaya na kuwa kero kubwa kwa binadamu. [140]
nyama
Daktari wa Stars, Juma Sufian alisema jana kuwa huenda Chuji akaikosa mechi hiyo kwa kuwa bado anasumbuliwa na tatizo la nyama ya paja. [141]
nyota
Nchi zitakazoshiriki mashindano hayo ambayo wenyeji Rwanda wameita nyota wake wa Marekani na Canada ni Kenya, Burundi, Ethiopia, Uganda, Zambia na Sudan. [142]
paa
Ndipo hapo nikastuka na kukuta huko nje mvua inyesha na paa yangu inavuja kwa nguvu zote hadi kweli nimeloa. [143]
pale
Anakuwa rafiki yako pale anapohisi unaweza kumsaidia. [144]
picha
Nafahamu fika kuwa kuchagua marafiki ni kazi ngumu sana hasa kutokana na ukweli kwamba hawa watu wote kwa picha ya nje ni marafiki. [145]
pili
Washtakiwa wengine walioonekana wana kesi ya kujibu ni mshitakiwa wa pili ambaye ni Mrakibu wa Polisi (SP), Christopher Bageni, mshitakiwa wa tatu ambaye Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Ahmed Makelle na wa tano WP 4593 PC Jane Andrew. [146]
rais
Banda, ambaye alichaguliwa mwaka jana kuwa rais wa Zambia kutokana na kifo cha aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo, Levy Monawasa, aliwasili nchini jana na kulakiwa na Rais Kikwete kisha kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake katika uwanja wa taifa. [147]
ratiba
Baadhi ya wanafunzi walilalamikia ratiba ya masomo iliyotoka wakisema kuwa inawabana na itawafanya wasifanye vizuri katika masomo yao. [148]
saa
Wote kwa pamoja waliondoka kizimbani saa 5.40 huku wakifuatwa na ndugu zao walioonyesha furaha isiyokuwa na kifani. [149]
safi
Lazima pale juu paonekane safi. [150]
salama
Sisi hatuwezi kufanya miujiza ya kuwafanya watoto wafaulu kama shule yenye watoto zaidi ya 700 ina walimu watatu, hawana vifaa vya kujifunzia wala vya kufundishia, walimu waliopo nao wanaishi maeneo ambayo si salama kutokana na ukosefu wa nyumba, leo watarajie nini kuhusiana na matokeo, hivyo hakuna aliyeajiriwa awe mwalimu mkuu," alisema mmoja wa walimu ambaye jina lake tunalo. [151]
sana
Awali Msemaji wa chama cha soka cha Zanzibar (ZFA) Maulid Hamad Maulid alipinga wazo la Maximo na kusema si lazima kufuata mifumo ya ligi za nchi za nje kwani mfumo uliopo haujawa wa kizamani sana. [152]
sauti
Kumbe nilikuwa sitafakari bali nasema kwa sauti kana kwamba nilikuwa mwanasiasa na mimi. [153]
shosti
Na ushauri wa kupewaaa shosti. [154]
si
Mchezaji huyo leo ( jana ) ameshindwa kufanya mazoezi kabisa kwa sababu ya maumivu ya nyama ya paja, lakini baadaye tutampeleka hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi ili tujue kama ataweza kucheza mechi ya kesho au la, lakini si rahisi kwa jinsi nilivyomwona. [155]
sisi
Vyuo vingine, kwa mfano Chuo Kikuu-main campus, wamepewa fedha zote (Sh600,000), lakini sisi tumepewa nusu (Sh300,000) na bado fedha zenyewe wametucheleweshea. [156]
siyo
Historia inaonesha kwamba siyo lazima kila mwenye mafanikio awe na furaha hapo maana yangu ni kwamba mafanikio ya mtu ni kitu cha binafsi kuliko mtazamo wa jamii au wa nje yake mhusika. [157]
soka
Ni natumaini yetu kuwa tutafanya vizuri katika mechi hiyo kama wao waliwaza kutufunga nyumbani basi hata sisi tunaweza kufanya maajabu nyumbani kwani soka ni mchezo wa makosa," alisema. [158]
tabia
Alisema Februari 6 majira ya saa 3.00 usiku marehemu aliondoka na rafiki huyo wakiwa na gari yake ndogo Toyota Corola yenye rangi ya maziwa, na ilipofika saa 4.00 usiku, wazazi wa marehemu walipatwa na wasiwasi na kuanza kumtafuta Abdul Basiti kwa kuwa hakuwa na tabia ya kuchelewa. [159]
tangu
Hii ni ziara yake ya kwanza nchini tangu aingie madarakani mwaka jana. [160]
tawala
Awali CUF iliwatangazia wafuasi wake wamekubaliana na CCM kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, lakini chama hicho tawala kikasema kuwa walichokubaliana na kurudi kwa wananchi, hali iliyosababisha CUF kutangaza kujitoa. [161]
tenga
Lakini alipofika kwenye tenga la tatu akaanza kutupa samaki mmoja baada ya mwingine, maana kila mmoja alionekana kuoza. [162]
tu
Washtakiwa hao ndio walioileza timu hiyo kuwa marehemu waliuliwa katika Msitu wa Pande na kwamba wao hawakuhusika kuwaua bali walikuwa wakiangalia tu na kwamba baada ya kuuawa wao walihusika kubeba maiti hizo na kuziingiza katika gari kwa ajili ya kuzipeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili. [163]
tuna
Sisi tunashukuru kuwepo kwa mtambo huu ambao unatusaidia katika mazoezi ya vitendo na hivi sasa hakuna kitu ambacho hatukijui kuhusu biogas na tuna uwezo wa kutengeneza mahali popote tukipelekwa. [164]
uchawi
Nasema kitendo kilichofanywa kumpeleka mganga wa jadi katika shule hiyo kwa ajili ya kutoa uchawi ni kinyume cha sheria," alisema Madiga alipozunguza na mwandishi wa makala hii wiki iliyopita. [165]
uchi
Mganga huyo alivitoa vitu hivyo akiwa uchi wa mnyama katika darasa hilo la kwanza na akadai kwamba vitu hivyo viliwekwa na mwalimu huyo usiku wa manane na yeye pia akiwa uchi wa mnyama ili walimu wenzake wateseke," alisema. [166]
uhusiano
Zara ambayo inatarajia kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Zambia. [167]
ujio
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe alisema ujio wa wageni hao utakuwa wa manufaa kwa watanzania na maendeleo ya nchi kwa ujumla. [168]
ukipata
Hapo namaanisha kwamba watu wanaamini kwamba ukipata mafanikio kinachofuata ni furaha. [169]
ulafi
Hatuna ulafi, tuwatafute wasafi, hatuna ulafi tuwatafute wasafi. [170]
una
Mtambo huu una uwezo wa kuchukua kilo 12 za mabaki ya chakula na lita 40 za maji asubuhi, na jioni huwekwa kiasi hicho hicho. [171]
uongozi
Mgomo huo uliodumu kwa siku mbili ulisitishwa jana baada ya uongozi wa chuo hicho kuwaahidi wanafunzi kuwa utawapa fedha zote baada ya wiki moja. [172]
uovu
Wapo wanaotafuta umaarufu kwa kutoa michango hadharani kwa lengo la kujitangaza lakini wengi wao ni waathirika wa maradhi ya kutojiamini, dhamira zao zinawasuta kwa uovu wao. [173]
uozo
Na hapo nikajikuta nimekaa chini huku harufu ya uozo ikiwa imeniletea kizunguzungu. [174]
ushindani
Alipoulizwa atakabiliana vipi na ushindani wa namba, Kazimoto anasema: “Nitahakikisha anajitahidi na kupata namba katika kikosi cha kwanza. [175]
usiku
Kwa mujibu wa Jaji Masatti, kitendo cha Zombe kufika katika kituo cha polisi Urafiki usiku wa tukio hilo na kuulizia pesa zilizochukuliwa na washitakiwa kutoka kwa marehemu na kuonyesha kukasirika baada ya kuambiwa kuwa zilikuwa zimepungua, kinaonesha kuwa alikuwa na mawasiliano na washitakiwa wengine waliowakamata marehemu. [176]
utu
Athari za kutanguliza vitu ni kuondoa utu, kwa hakika tamaa ya vitu siku zote huondosha utu. [177]
vema
Alisema kama kuna watu wamesambaza vipeperushi hivyo ni vema tu, kwa sababu wametumia haki yao ya msingi. [178]
vigumu
Alisema kuwa miradi yote waliyopewa madiwani imetekelezwa chini ya kiwango kabisa na mingine imekwama kabisa hali ambayo inawawia vigumu madiwani kuwajibishana na hilo ni kosa kubwa kwa kuwa wanachangia kuwakatisha tamaa wananchi ambao wanachangia fedha na nguvu zao. [179]
vina
Mashitaka kama haya huzua utata katika uendeshaji wake, upande wa mashitaka ndiyo ambao inatakiwa kuthibitisha madai hayo dhidi ya mshitakiwa kwa kuwa ni vigumu kuthibitisha kwamba vitu au vifaa alivyokutwa navyo mshitakiwa ni kweli vina nguvu inayoaminiwa kuwa ni ya kishirikina. [180]
wala
Kwa kweli sina maoni yoyote kuhusu taarifa hizo, sijibu na wala sina mpango wa kujibu taarifa za vipeperushi,” alisema. [181]
wale
Wanafunzi waliosimamishwa masomo Novemba 18 mwaka jana ni wale wa shahada ya kwanza. [182]
waliooza
Ilionekana wazi kwamba waliooza zaidi ni wale wa juu, kisha wale wa juu walikuwa wameambukiza wale wa chini uozo wao. [183]
wananuka
Na hata wachuuzi wenyewe walikuwa wananuka. [184]
wangu
KWANZA naanza kwa shukrani kwa mapokeo mazuri kwa wasomaji wangu katika makala iliyopita ya "Jiamini ili uaminiwe iliyotolewa katika safu hii ya Saikolojia na Maisha. [185]
wapi
Hawa wako wapi? Lazima tushirikiane nao kurejesha hadhi ya shule za serikali kielimu,” alisema Masawe. [186]
wapo
Kwa wale tunaoamini katika dini tunaambiwa kwamba katika kila kizazi wapo walinzi wa maadili na hufanya hivyo kwa njia mbalimbali hata kwa njia za kujitoa muhanga inapobidi. [187]
wawili
Masharti mengine ni kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali na barua zao za utambulisho zitoke kwa waajiri wao. [188]
wenu
Anakuwa mwema zaidi anapokuwa na shida, katika kipindi chako cha mafanikio urafiki wenu utanoga, ukifilisika atakugeuka. [189]
wenzetu
Tuko tayari kwa lolote juu yao na tunawafanya kuwa ni wenzetu. [190]
wetu
Tunafaulisha vijana wetu na kuwaita wenye vipaji maalum na kuwapeleka katika shule zetu kama Mkwawa, Mzumbe, Tabora Wavulana kila mwaka. [191]
wiki
Mgomo huo ulitokana na wanafunzi kutoridhia kiasi cha fedha za kujikimu, kwa ukongozi kuahidi kuwapa fedha zote ndani ya wiki moja. [192]
yale
Kundi kubwa la watu waliovaa matambara, wenye nyuso zilizosinyaa kwa njaa, wakijaribu kuvuta matenga yale na kuchambua ili wapate angalau kasamaki kamoja ambako kalikuwa afadhali. [193]
yetu
Nchi yetu ni nchi ya utawala bora inayoongowa na sheria ambazo zinatungwa na Bunge na kutafsiriwa na mahakama kwa hiyo tuonane kesho tujifunze sheria. [194]
yeye
Kwa upande mwingine yupo Y ambaye yeye ni mtu mwenye mafanikio ya wastani. [195]
yule
Kati ya wageni mashuhuri watakaohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika, CAF, Issa Hayatou, Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa , Fifa, Sepp Blatter na yule wa Ulaya (Uefa), Michel Platini. [196]
zabuni
Ni marufuku kupewa zabuni ndani ya wilaya. [197]
zake
Vipeperushi hivyo visivyoonyesha jina na mahali vilikochapishwa, vikimtaka waziri huyo, kuachana na ndoto zake za kuunyemelea urais na siasa za Zanzibar kwa jumla. [198]
zangu
Naomba nichukue furasa hii kuwasabahi marafiki zangu popote mlipo. [199]
ziara
RAIS wa Zambia, Rupiah Banda amewasili nchini kwa ziara ya siku mbili. [200]