Nenda kwa yaliyomo

sauti

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru

Kiswahili

[hariri]
Uwakilishi wa wimbi la sauti

Nomino

[hariri]

sauti (sauti)

  1. milio ya watu au kelele zitokanazo na vitu vinapogongana.

== ngeli ==i-/zi-

aina za sauti za Kiswahili

[hariri]
  1. irabu. Irabu za Kiswahili ni tano: a, e, i, o, u. Katika kufafanua irabu tunazigawa kuzingatia viungo viwili: ulimi na mdomo. Kuzingatia ulimi tunapata irabu ya mbele, irabu ya kati na irabu za nyuma. Irabu za mbele ni i na e, hutamkwa kwa kuitumia sehemu ya mbele ya ulimi. Irabu ya kati ni a, hutamkwa kwa kuitumia sehemu ya kati ya ulimi. Irabu za nyuma ni u na o, irabu hizi hutamkiwa sehemu ya nyuma ya ulimi. Irabu a, e na i hutamkwa midomo ikiwa imetandazwa. Irabu o na u hutamkwa midomo ikiwa imeviringwa
  2. konsonanti: b, ch, d, dh, f, g, gh, h, j, k, l, m, n, ng, ng', p, r, s, sh, t, th, v, w, y, z. Katika kutamka konsonanti hewa inapopitia kinywani kutoka mapafuni huzuiliwa na

Tofauti kati ya irabu na konsonanti ni kwamba wakati wa kuzitamka irabu hewa haizuiwi mahali popote ilihali wakati wa kuzitamka konsonanti hewa huzuiwa kwenye ala mbalimbali za kutamkia.


Tafsiri

[hariri]