Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-08

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
aende
Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [2]
agizo
Alifahamisha kuwa utekelezaji wa agizo la Ewura ulianza tangu Januari 5, mwaka huu na kwamba, serikali itaendelea kusimamia maamuzi yake. [3]
aina
Alisema wanachoangalia katika upekeaji wa miasaada ni aina ya misaada na wanaoitoa. [4]
akawa
Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [5]
akiishi
Nyumbani kwake hapo alikuwa akiishi na watu kadhaa akiwemo jamaa mmoja ambaye ni mwenye ulemavu wa ngono yaani albino. [6]
akiwa
Mingine ni pamoja na Mbeya - Lwanjiro (36km) mkandarasi akiwa ni kampuni ya Kundan Singh kutoka Kenya, Isuna - Manyoni huko Singida inayojengwa na mkandarasi China Geo kutoka China. [7]
ama
Alibainisha kwamba, kama mtu anayetoa msaada atabainika kuwa aliwahi kupatikana na hatia ama kushitakiwa msaada wake hautapokelewa. [8]
amani
Mbali na kosa hilo la kutusi, upande wa Jamhuri ambao ndio mlalamikaji katika makosa yote ya jinai unaweza kuongeza na kosa la kutishia amani kwa kughadhibisha watu wengine. [9]
ana
Alisema wameamua kutoa kauli hiyo baada ya kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya chama Wilaya kuunda tume ya wajumbe wanne na kufuatilia suala hilo na baada ya kurudi ilibaini mwekezaji huyo ana matatizo. [10]
anataka
Sasa kwa maneno rahisi kabisa ni kwamba; kujieleza kila mmoja kunampa nafasi mwenzake kujua anafikira nini na anataka afanyiwe nini hasa. [11]
asasi
Matumizi ya maneno asasi na taasisi yanachanganywa. [12]
au
RAIS Jakaya Kikwete amesema amejitoa muhanga na atatumia nguvu zake zote bila huruma wala kujali walio ndani au nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya mafisadi yanafanikiwa. [13]
bahati
Kwa bahati mbaya neno maamuzi limetumika kwa muda mrefu na limekuwa na mashiko kiasi ambacho watu wengi wamelizoea na wanalichukulia kuwa ni sahihi. [14]
bali
Kuhusu wagombea kuchafuliana majina, alisema tatizo hilo haikuwa kwa wagombea wenyewe bali lilisababishwa wapambe wao. [15]
bidhaa
Lakini hivi sasa mafuta yanauzwa kati ya Sh1,450 na 1,600 kwa petroli na dizeli kutoka Sh1,300 hadi 1,500, licha ya maafisa wa Ewura kukutana mara kadhaa na wafanyabiashara wa bidhaa hiyo ambao wamekuwa wakidai kuwa hawawezi kupunguza kwa sababu waliyanunua bei ikiwa juu katika soko la dunia. [16]
chama
Aliwataka UWT kutumia uzoefu wao na kuchagua viongozi makini na wenye uzoefu na ndani ya chama na kuonya kuwa wakikosea watajuta kwa kipindi cha miaka mitano yote. [17]
chanjo
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) mwezi huu inatarajia kuanza kuifanyia majiribi chanjo mpya ya kipindupindu katika maeneo sita tofauti ya Unguja na Pemba. [18]
chetu
Chanzo chetu hakikuweza kubaini kama kiasi hicho cha fedha kinchokadiriwa kufikia Sh320 milioni kama ni sehemu ya Sh2.5 bilioni zilizoahidiwa na Dk Kawambwa kwamba zitatolewa na serikali. [19]
chombo
Maana ya asasi ni chombo kinachojumuisha watu kwa lengo maalumu hasa kwa kutoa huduma fulani. [20]
duniani
MIUNDOMBINU ni miongoni mwa masuala muhimu duniani kote hasa katika kuleta maendeleo na kukuza uchumi. [21]
es
Serikali inakusanya takwimu za bei ya mafuta, zikikamilika, kazi ya kuwachukulia hatua itaanza mara moja," alisema Ngeleja alipohojiwa na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. [22]
fidia
Akizungumzia changamoto zinazoukabili mradi huo, waziri huyo anasema kubwa ni tatizo la ujenzi holela na kuongeza kuwa serikali itatoa fidia kwa wale wote watakaothirika na uboreshawaji wa mradi huo. [23]
foleni
Kumbe jamaa mwenyewe alikuwa anatafuta nishani ya kiatu peke yake kwa kujaribu kuzuia kila gari linalotaka kuruka foleni. [24]
fulani
Kwa mfano timu za Bara, Simba na Yanga hazishindwi kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya michuano ya kimataifa na hata ya ligi ya nyumbani kwa sababu zina wafadhili, ambao kwa kiasi fulani wanasaidia kupunguza matatizo ya kiuchumi ndani ya timu hizo," alisema. [25]
gani
Hata hivyo alisema kama kuna mtu anaona kuna haja ya kufanyia mabadiliko kwenye kwenye katiba hiyo alitoa hoja na aelekeza ni kipengele gani anafikiri kinafaa kufanyiwa marekebisho hayo na kwamba hatua zitachukuliwa kama kutakuwa na umuhimu wa kufanya hivyo kwa kukifanyia marekebisho kipengele hicho. [26]
haja
MWENYEKITI wa kamati ya kudumu ya bunge ya katiba sheria na utawala bora, George Lubeleje amepinga kitendo cha baadhi ya wanaharakati na wanasiasa wa vyama vya upinzani wanaodai katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania inatakiwa kuandikwa upya kwa madai kuwa katiba iliyopo ni nzuri na inakidhi haja. [27]
hajui
Kauli hiyo ilionekana kumchanganya sana Kazim, akawa hajui la kufanya. [28]
hao
Kanuni ya kuwabana wafanyabiashara hao ilitatangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) na utekelezaji wake utaanza baada ya kutangazwa kwenye gazeti la Serikali. [29]
hapa
Waumini kadhaa wa msiki mkuu wa mkoani hapa wanaendelea kulaani taarifa wanazodai kuwa si sahihi ambazo maafisa wa polisi walipewa wakizihusisha na mgogoro wa msikiti huo. [30]
hapo
Stars imesaliwa na mchezo mmoja dhidi ya Uganda hapo kesho Ijumaa kwenye uwanja wa Nakivubo, huku Rwanda ikikwaana na Zanzibar yenye pointi nne. [31]
hasa
Maeneo yote ambayo yako katika mazingira machafu ndiko ugonjwa huo hulipuka na kuwaathiri wakazi wake na hasa sehemu zenye maji machafu yanayotoka vyooni na sehemu nyingine chafu. [32]
hata
Habari hizo zilisema hata hivyo watuhumiwa hao wamekana kuwa na marafiki wa nje na kwamba na hata kama wangekuwa nao si kosa kwa mujibu wa sheria za nchi. [33]
hawa
Lakini nikaja kugundua kuwa ile ya wale kuongea ndiyo dawa yenyewe tofauti tu ni kwamba huenda hawa watu hawakuwa wawazi baina yao wakiwa pekee yao, labda mmoja alishindwa kujieleza. [34]
hawezi
Sasa narudia kusema; usiogope kumwambia mwezako unavyotaka akufanyie kwani asipofanya usimlaumu kwa kuwa hawezi kujua. [35]
hayo
Maeneo ambayo yatanufaika na chanjo hiyo ni yale yaliyobainishwa kuwa ni sugu kwa ugonjwa huo na tayari Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Zanzibar, imeshafanya sensa ili kujua idadi ya watu wa maeneo hayo. [36]
hii
Hakuna utafiti uliofanywa kuhusu athri za chanjo hii kwa akina mama wajawazito, lakini wataaalamu wetu wameshauri kuwa asipewe," alisema mkuu huyo. [37]
hiki
Kama lingekuwa shirika la mtu binafsi, hakuna ambaye angekubali kuona linaendelea kupata hasara kiasi hiki. [38]
hivi
Hata hivyo, hivi karibuni Waziri Kawambwa aliteua timu ya watu saba itakayoongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Profesa Idrisa Mshoro, kwa ajili ya kuchunguza kiini cha matatizo ndani ya ATCL na kuishauri serikali hatua muafaka za kuchukua. [39]
hiyo
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na menejimenti hiyo, siku chache baada ya ATCL kusimamishwa kutoa huduma na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA), shirika hilo litapoteza Sh300 milioni kila siku. [40]
hizi
Dk Kishe anasema siku hizi mambo yameharibika kwani masuala yanayohusu mapenzi na mahusiano hayapaswi kusemwa hadharani. [41]
hizo
Waziri Magufuli alisema fedha hizo zilichelewa kufika na kusababisha matarajio ya mikakati ya wizara yake kutokamilika kama ilivyokusudiwa. [42]
hofu
Aliyataja matatizo mengine kuwa wananchi wa maeneo hayo hivi sasa wanaishi kwa hofu kubwa kwa kuwa wanamuogopa mwekezaji huyo. [43]
huko
Ni onesho la kufungua mwaka, Jahazi itatoa zawadi kwa wakazi wa Yombo ili kuona walichokifanya huko, Uingereza kwani burudani ilikuwa ya aina yake na Wazungu wanajua nini maana ya ëVIPí, Kipapatilo na Pajaí alisema Mdoe. [44]
huku
Ushindi huo umeifanya Stars kufikisha pointi sita na kuongoza kundi kwa muda, huku kiungo wake, Athuman Idd akinyemelea ufungaji bora kwa mabao mawili aliyonayo. [45]
huu
Kutokana na hali hiyo, shirika limepata hasara ya zaidi ya Sh9.3 bilioni na ikiendelea hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu, hasara itaongezeka na kufikia Sh16.2 bilioni. [46]
huwa
Katika mukhtadha wa kujifunza ni ukweli unaosikitisha kwamba wanafunzi wa lugha huwa ni wepesi kujifunza matusi kwa haraka kuliko maneno mengine katika lugha husika. [47]
huyo
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, awamu ya pili ya inatarajiwa kuanza Febuari 7 hadi 16, mwaka huu. [48]
huyu
Huyu kafanya hivi huyu kafanya hivi kumbe huyu aliamua kwenda kufanya hivi baada ya kushindwa kumuelewa mwenzake hivi, ushanifaham. [49]
ikawa
Sasa kutokana na kuona nywele kutoka juu zilikuwa zikiingia katika vyakula, waliamua kubadilishana, hoteli ikawa ghorofa ya juu na kinyozi akahamia chini. [50]
ikiwemo
Tatizo hili limekuwa likizikwaza nchi nyingi za Afrika, Tanzania ikiwemo na kusababisha shughuli za kuinua uchumi kutofikiwa kwa wakati. [51]
ila
Mimi siwezi kusema vazi fulani halifai kuvaa ila vazi linafaa kwa mahali husika; Katika sentensi hii neno lisilofaa hapa ni kuvaa. [52]
ile
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ile ile, huku Danny Mrwanda na Mrisho Ngassa wakiwa kivutio kikubwa kutokana na kushambulia kwa kasi na kuwatoa jasho mabeki wa Rwanda ambao walilazimika kutumia nguvu nyingi na ubabe. [53]
ina
Kocha wa Rwanda ambayo ina pointi tatu, Branco Tucak alisema kwamba anajipanga kwa mchezo ujao dhidi ya Zanzibar, lakini akasifu jinsi Stars ilivyokuwa ikikaba vizuri. [54]
ingawa
Alisema ingawa hakuna utafiti uliofanywa kuhusu madhara ambayo wanawake wajawazito wanaweza kuyapata kwa kutumia chanjo hiyo, lakini wataalamu wa afya wameshauri wasipewe. [55]
ingefaa
Kwa hiyo ingefaa iandikwe Mchakato wa mafanikio na matatizo ya Yanga. [56]
isipokuwa
Mkuu wa kampeni hiyo katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Abdulhamid Ameir Saleh, alisema chanjo hiyo itakuwa tofauti na chanjo nyingine kwa kwamba, itawashirikisha watu wote isipokuwa wanawake wajawazito. [57]
iwe
Tunaona ufisadi wa wengine na kutetea wa kwetu, lakini tulio wengi tulikubali kwamba hata kama ni kuonyeshana tako, na iwe hivyo hadi ushuzi utufanye sisi sote tuone aibu. [58]
jua
Na kama hato jua basi hawezi kukuridhisha na kama hatokuridhisha jua hutofurahisha na kama hatofurahia basi mengine ndiyo haya yatokanayo. [59]
juzi
Djibout yenye pointi moja tayari imeshaaga mashindano hayo juzi baada ya kuchapwa na Kenya huku ikiwa ndio timu pekee kwenye kundi B na michuano hii iliyofungwa mabao tisa hadi sasa. [60]
kabisa
Mara nyingi tunakosea kuliandika ipasavyo kutokana na kusahau au kutojua kabisa tofauti zake. [61]
kama
Kama ni mikakati ya kulijenga upya, ilianza miaka mitatu iliyopita na kama hivyo ndivyo, tunatakiwa kujiuliza kwamba, tatizo ni nini ua liko wapi?" alihoji. [62]
kata
Aliwataka watanzania kushirikiana na serikali katika kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo hivyo kuanzia kwenye kaya mitaa kata hadi taifa ili kuhakikisha wahusika wa mauaji hayo wanapatikana na wanakosa nafasi ya kuendeleza vitendoi vyao viovu kwa watu hao. [63]
kati
Ngeleja alisema wafanyabiashara wanaouza mafuta kwa bei ya juu, hawana njia yoyote ya kujitetea kwa sababu kanuni inayotumika kuwabana ilijadiliwa na kukubaliwa katika kikao cha pamoja kati yao na Ewura na watumiaji wa mafuta. [64]
kibao
Lazima zipo kibao, si tu maharamia kuwatambua maharamia wenzao. [65]
kigeni
Na miongoni mwa mikakati yake ni kuleta kocha wa kigeni. [66]
kikosi
Julio ndio kocha pekee aliyefukuzwa, Benzisk aliondoka mwenyewe baada ya kushindwa kazi, alimaliza mzunguko wa kwanza bila kuwa na kikosi cha kwanza, kocha gani anayecheza mechi 11 bila kuwa na kikosi cha kwanza,?" alihoji Dalali. [67]
kile
Mwaka jana timu ya soka ya Miembeni, ambayo ilikuwa ikiwakirisha Zanzimbar katika michuano ya klabu bingwa Afrika ilijitoa katika michuano hiyo kwa kile kilichodaiwa kutokuwa na fedha za kusafiria. [68]
kina
Akizungumza na Mwananchi, Mwenyekiti wa Moro United, Abdul Sauko alisema kwa sasa wanajadili kwa kina juu ya suala hilo kabla ya kulitolea uamuzi wa kuendelea kushiriki katika michuano hiyo au kujiondoka na kurudi kambini kujiandaa na ligi kuu. [69]
kisheria
Naye mmiliki wa kitalu hicho, Rayn Shallon akizungumzia suala hilo, alisema eneo hilo ni lake na kwamba anamiliki kisheria. [70]
kitalu
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ulanga kimeitaka serikali kumuondoa mmiliki wa kitalu cha uwindaji cha Wildlife Footprints kilichopo katika kata za Iragua na Itete kwa kukiuka masharti aliyopewa. [71]
kocha
Baada ya mchezo huo kocha wa Stars, Marcio Maximo alisema kwamba alijua Rwanda ni wagumu ndio maana akawaelekeza wachezaji wake kukaba kwa nguvu mwanzo mwisho. [72]
kote
Katika kuhakikisha kuwa viwango vipya vinatekelezwa, juzi Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, aliwatahadharisha wauzaji wa mafuta nchini kote kuhakikisha kuwa wanashusha bei ya mafuta, vinginevyo atakayeshindwa kufanya hivyo baada ya tangazo hilo kutolewa katika Gazeti la Serikali, watakuwa wamefutiwa leseni ya kufanya biashara hiyo. [73]
kufa
Wakati wanaendelea kuangalia ile picha aliingia daktari aliyekuwa akimwangalia Kazim na kumwomba waziri afupishe mazungumzo, badala yake wamsake yule mvumbuzi wa dawa kwani isingepita saa 12 kabla ya Kazim kufa ikiwa hatapata ile dawa. [74]
kuingia
Nafasi ya Sudan kupenya na kuingia nusu fainali ni majaliwa kwani inahitaji kushinda mabao mengi huku ikisubiri matokeo ya mechi nyingine. [75]
kuinua
Alisema Chama cha Soka visiwani humo (ZFA), kinatakiwa kushirikiana na timu hizo kuhakikisha zinapata wafadhili, ambao watasaidi kupunguza matatizo ya kiuchumi na kuinua soka la zanzibar. [76]
kuja
Akizungumzia lengo la ujenzi wa barabara hizo, Waziri Kawambwa anasema ni kupunguza kero ya muda mrefu na kunyamazisha kilio sugu cha wananchi kuhusu msongamano wa magari, hasa kuja katika maeneo ya katikati ya jiji la Dar es Salaam. [77]
kukamatwa
Alisema kutokana na hali hiyo, wananchi wa vijiji hivyo, wakiliona gari wanakimbia kwa hofu ya kukamatwa na kufunguliwa mashitaka. [78]
kukutana
Tutatoa tamko kesho (leo) kama tutarudi kwa ajili ya maandalizi ya mechi yetu ya mzunguko wa pili au la, lakini leo tumepanga kukutana viongozi "alisema Sauko. [79]
kule
Ndio ndugu, mimi naitwa Kazim ni mwenye mgodi wa madini ya almasi kule Mwadui, tatizo ni kwamba hali kwa sasa imekuwa mbaya mno, nimechanganyikiwa hapa hata sijui la kufanya,” alisema akiomba ushauri. [80]
kulia
Badala yake viongozi nao waliungana na wananchi kulia kuwa wafanyabishara hawa ndio chanzo cha kupanda kwa gharama za maisha. [81]
kulinda
Aliionya CCM iangalie uwezekano wa kupunguza matumizi makubwa ya fedha wakati wa michakato ya uchaguzi ili kulinda heshima ya chama hicho kikongwe. [82]
kumuua
Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [83]
kuna
Ofisa mmoja wa Wizara ya Miundombinu ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, aliliambia gazeti hili kuwa kuna mikakati mizuri ya kulisuka upya shirika hilo iliyopangwa miaka mitatu iliyopita, lakini utekelezaji ni hafifu. [84]
kurudi
Hata hivyo mvutano huo ulimalizwa kwa waumini hao kuruhusiwa kurudi nyumbani na siku iliyofuata kwenda tena polisi. [85]
kutoka
Juhudi za kumpata ufafanuzi kutoka kwa Ofisa Mkuu Mtendaji wa ATCL, David Mattaka, hazikufanikiwa jana kwa kuwa alikuwa kwenye kikao cha menejimenti na wajumbe wa bodi. [86]
kuua
Kipindupindu kiwekewe mikakati madhubuti UGONJWA wa kipindupindu ambao kwa karibu miongo mitatu unaonekana kulowea nchini kwetu, unaendelea kuua Watanzania, kama ilivyotokea wilayani Ulanga, Mkoa wa Morogoro ambako watu sita wamefariki na wengine kulazwa kutokana na kuugua ugonjwa huo. [87]
kuuza
Ngeleja alisema kitendo cha kuendelea kuuza kwa bei ya juu zaidi ya iliyopangwa ni kuyasaliti makubaliano waliyoafikiana awali wakati wa kupanga kanuni itakayowawezesha kukokotoa bei stahili za mafuta nchini. [88]
kuvaliwa
Ilitakiwa litumike neno kuvaliwa kwani mtu ndiye aliyetenda kitendo cha kuvaa ambapo vazi limetendewa kitendo cha kuvaliwa. [89]
kuzuia
Kwa hiyo mwandishi alikuwa na nia ya kutumia neno kudhibiti kwa maana ya kulinda au kuzuia unyanyasaji wa kijinsia. [90]
kwake
Kwa sababu unapokaa kusikiliza kesi namna ile, unakaa kusikia wawili wakibishana huenda kuhusu vitu ambavyo kila mtu amevibeba kifuani kwake na pale inakuwa kama nafasi ya watu wawili wakitua mizigo yao. [91]
kwani
Hata hivyo Waziri Masha aliwaomba wananchi wasiwe na wasiwasi juu ya misaada hiyo kwani lengo lake ni kuimarisha ulinzi ndani ya nchi yao na kwamba wakati mwingine hata hiyo misaada inayotolewa haipelekwi katika maeneo wanayotoka wataoa misaada. [92]
kwanza
Chanjo hiyo ambayo ni kwanza nchini Tanzania, ni mkakati wa serikali ya Zanzibar katika kukabiliana na ugonjwa huo ambao mara kwa mara umekuwa ukiwasumbua wakaziwa visiwa hivyo. [93]
la
KIASI cha Sh2.5 bilioni kilichotolewa na serikali kwa ajili ya kulinusuru Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) zimeleezwa kuwa ni kidogo ikilinganishwa na mahitaji halisi ya kuliwezsha shirika hilo kuanza kufanya kazi yake kikamilifu. [94]
lengo
Rajab alisema siku za nyuma, wizara hiyo ilikuwa ikitoa mafunzo ya jinsi ya kuepukana na kipindupindu lakini sasa, imebuni njia nyingine kwa lengo la kutokomeza maradhi hayo. [95]
lenye
Timu ya Mtibwa imepokelewa kwa shangwe na vifijo; Neno lenye mushkeli hapa ni kupokelewa. [96]
leo
Wakati huo huo, taarifa za kuaminika zilieleza kuwa wafanyakazi wa ATCL wataanza kulipwa mishaahara yao ya Novemba na Desemba wakati wowote kuanzia leo baada ya kupatikana kwa fedha. [97]
ligi
Alitoa wito kwa wapenzi wa soka mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa taifa kushuhudia maandalizi ya timu zao kabla ya kuanza kwa ligi kuu mzunguko wa pili. [98]
lina
Alisema kila jambo lina utaratibu wake na kwamba akitokea mtu mwenye ushahidi wa kutosha kuhusina na vitendo hivyo viovu, ni vema akawasiliana na vyombo vinavyohusika ili kutoa ushahidi wake utakaosaidia kuwakamata watuhumiwa. [99]
liwe
Ilitakiwa liwe kutarajia au kutazamia. [100]
lugha
Ninachunguza matumizi ya maneno na miundo ya sentensi kwa lengo la kuwatanabaisha waandishi na wasomaji kuwa ufasaha wa lugha ni jambo la kuzingatiwa ili tuweze kuulinda utamaduni wetu tulioachiwa na wazee wetu pamoja na kuuendeleza kwa ajili ya vizazi vijavyo. [101]
maadili
Kimsingi Dk Kishe alikuwa akizungumzia maadili, kanuni za maadili na matumizi ya lugha kwa jumla. [102]
mada
Katika mkutano huo, mada zilikuwa motomoto huku wajumbe wakichangamsha mkutano huo kwa kuchangia pamoja na kuchanganua. [103]
mafuta
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja amewataka wananchi kuondoa wasiwasi juu wafanyabiashara wanaouza mafuta kwa bei ya juu, kwa sababu baada ya siku chache, serikali itaanza kuwashughulikia kikamilifu. [104]
magumu
Kwa hiyo hatusemi taasisi ya kuwahudumia wajane au watoto wanaoishi katika mazingira magumu. [105]
maombi
UPANDE wa mashitaka katika kesi ya wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inayomkabili aliyekuwa mfanyakazi wa benki hiyo Jonathan Munisi, umepinga maombi ya kutaka mshitakiwa huyo aunganishwe na kesi nyingine. [106]
mara
Alifafanua kuwa kinachoonekana ni kwamba, serikali inaliendesha shirika hilo kisiasa zaidi kuliko utekelezaji, ndio maana kila mara linayumbayumba licha ya kuwepo mipango mizuri ya kuliboresha. [107]
matusi
Mathalan, matumizi ya lugha za matusi. [108]
mbali
Alisema kuwa ili kutoa burudani zaidi kundi hilo limeandaa mashindano ya kucheza miondoko mbali mbali, aliyomo katika vibwagizo vya nyimbo zao kali. [109]
mbele
Wakili wa serikali, Fredrick Manyanda, alidai mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi ,Ady Lyamuya, kuwa wanapinga kwa sababu maombi hayo yamewasilishwa kinyume cha sheria. [110]
meno
Baada ya serikali kuunda Ewura ilionekana kuwa haina meno na kwamba haingeweza kuwa na nguvu za kufanya kazi zake vyema, hata hivyo, serikali ilisikia kilio cha wananchi kuipatia meno Ewura baada ya kufanyia marekebisho sheria ya nishati bungeni. [111]
mfumo
Masha alifahamisha kuwa walianzaisha mfumo wa ulimzi jamii ili kuongeza nguvu kukabiliana na uhalifu inazidi kuongezeka nchini. [112]
mila
Katika mchakato mzima wa uundaji wa sheria mbalimbali, dhana ya mazingira hugusa maeneo mengi zaidi ikiwa ni pamoja na hali ya kisiasa, kiuchumi na wakati mwingine hata kijiografia, lakini zaidi ni muhimu kuhusisha na kuzingatia mila na desturi za jamii husika ambayo kwa ajili yake sheria husika inakusudiwa kutungwa au kuundwa. [113]
mimi
Katiba iliyopo ni nzuri, tena ni kutokana na ubora wake ndiyo maana iliruhusu mfumo wa vyama vingi hapa nchini, mimi binafisi napinga kitendo cha baadhi ya watu wanayoipinga katiba hii na kudai iandikwe upya kutokana na kwamba katiba hii ni nzuri na inakidhi mahitaji tuliyonayo kwa sasa,"alisema Lubeleje. [114]
mingi
Foleni katika barabara mbalimbali za jiji hili kubwa zaidi nchini umekuwa ukisababisha wakazi wake wengi kupoteza muda mwingi njiani na hivyo kuharibu mipango mingi ya uzalishaji mali na hata huduma za kijamii. [115]
miradi
Anasema mpango huu unaungana na miradi mingine ambayo inaendea kutekelezwa katika jiji la Dar es Salaam ambayo inahusisha ujenzi wa Barabara ya Sam Nujoma unaotekelezwa na kampuni ya Chico na kusimamiwa na kampuni ya Norplan. [116]
misaada
Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha aliliambia gazeti hili jana alipoulizwa kama misaada inayotelolea na wafanyabiashara haitakwamisha utendaji kazi wa jeshi hilo. [117]
mjini
Kikwete alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa saba wa Jumuia ya wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) katika ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma. [118]
mke
Wengine ni Mama Maria Nyerere, mke wa Rais, Salma Kikwete, Mama Fatuma Karume, Mama Sitti Mwinyi na mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda. [119]
mkoani
WAUMINI wa dini ya kiislamu wanaoendelea kuhojiwa na makachero wa polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za ugaidi wamelalamika kupotezewa muda wao na kwamba maswali wanayoulizwa hayawahusu. [120]
mno
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [121]
moto
Magoto alisema licha ya kuchukua maeneo hayo pia mwekezaji huyo alichoma moto nyumba vibanda zaidi ya 62 za wakazi hao na kuwapiga na kuwafungulia mashitaka kwamba wamevamia eneo lake. [122]
moyo
Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [123]
mradi
Dk Kawambwa anasema barabara zitakazohusika katika mradi huu zitasaidia watumia magari ambao wanaishi pembezoni mwa jiji ambao husafiri kwenda upande mwingine wa jiji. [124]
mrefu
Alisema kwamba, sababu zinazoendelea kutolewa na wafanyabiasha hao juu ya kuwa na hifadhi ya mafuta ya muda mrefu, hazina msingi bali ni tamaa yao ya kutaka kujiongezea faida. [125]
msaidizi
Jamaa huyo ambaye alikuwa kama msaidizi wake wa karibu, alikuwa akimuwakilisha katika kazi mbalimbali na ndiye aliyekuwa ana siri zake nyingi. [126]
mtindo
Wangekamata magari na kuyakalisha pale nusu saa, huu mtindo ungekoma papohapo. [127]
muda
Awali akimkaribisha Rais Kikwete Mwenyekiti wa UWT anayemaliza muda wake, Anna Abdalah, alimuomba asimame imara katika kuhakikisha kuwa mafisadi wote wanafikishwa katika vyombo vya dola ili sheria iweze kuchukua mkondo wake. [128]
mumewe
Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [129]
mwandishi
Ukweli ni kwamba mwandishi alikuwa na lengo la kutumia neno kudhibiti. [130]
mwito
Akizungumza suala la mauaji ya Albino alitoa mwito kwa watanzania wote kushiriki katika kukomesha vitendo hivyo kwa kuwafichua wahusika wa mauaji hayo. [131]
nami
Ndugu yangu nakupa pole sana, yaani ni bora ungewasiliana nami kabla ya kwenda huko, kwani ukweli ni kwamba dawa imegunduliwa nchini na jamaa mmoja tena ni albino, rudi wahi mapema usipoteze muda wako huko,” alimsisitizia. [132]
nao
Kuwachunguza mafisadi ni kazi ngumu na inahitaji gharama kubwa, lakini kusema kweli ni lazima nitapambana nao kwa kufuata utaratibu kupitia kwa vyombo husika," alisema Kikwete. [133]
naye
Milovan tuliutofautiana naye kimaslahi, alitaka mshahara mkubwa na sisi hatukuwa na uwezo wa kumlipa kwa kuwa hatukuwa na mdhamini wakati huo, na Talib tulikuwa na makubaliano ya kufundisha kwenye michuano ya Tusker tu. [134]
nchi
Akizitaja nchi ambazo zimewahi kutumia chanjo hiyo ya Dukoral kutoka Swaziland kuwa ni India, Sudan, Msumbiji, Afrika Kusini, Uganda na Indonesia. [135]
ndiye
Alisema katiba hiyo ambayo ndiye mama wa sheria hapa nchini iliandikwa mwaka 1977 na kufanyiwa mabadiliko ya mara kwa mara na kusisitiza kuwa kutokana na ubora wake haiwezi kuandikwa upya kama inavyopendekezwa na baadhi ya wanaharakati na wanasiasa wa vyama vya upinzani hapa nchini. [136]
nia
Serikali kuu ilikaa na viongozi wa jiji la Dar es Salaam na kuamua kubuni wazo la kuandaa mradi huu kwa nia ya kulipatia ufumbuzi tatizo la msongamano wa magari barabarani ambapo tulikubaliana kuunda kamati maalum kwa ajili ya kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati," anasema. [137]
nusu
Kama ilivyo kwa kundi A zilipo Kilimanjaro Stars na Zanzibar, hatma ya timu zitakazofuzu hatua ya nusu fainali kwenye kundi B itabainika katika mechi hizo zilizopangwa kufanyika Kampala badala ya Jinja. [138]
ofisi
Mahakama ya rufaa ofisi za Dodoma ilikataa rufaa yake kwa kuridhika kuwa ni kweli kuwa, mbali na kosa la kutumia lugha ya matusi dhidi ya askari jeshi hao, lakini pia mrufani alionekana kutaka kusababisha fujo na uvunjaji wa amani kwa kuwatukana askari jeshi watu ambao saikolojia ya kazi yao huwaelekeza katika matumizi ya nguvu na kipigo kwa yeyote mkorofi jambo ambalo kama lingetokea bila shaka lingesabaisha kuvunjika kabisa kwa amani ya eneo husika, kwani matusi huchukiza. [139]
pake
Pamoja na hayo, binafsi, sikuwahi kulisikia neno mchapalo, lakini Mwenyekiti wa Mkutano huo, Bakari Hamad Rashid ambaye ni Kamishna wa Utamaduni Zanzibar, alikuwa akiliweka mahala pake kiasi cha kukubalika. [140]
pale
Alisema serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuhakikisha watu hao wanalindwa na kwamba maisha yao yanakuwa salama na kwamba hivi karibuni imewapatia simu ili kurahisisha mawasiliona pale wanapobaini kuna hali ya kujitokeza kwa uharamia huo na kuwataka wanachi kuungamkono juhudi hizo kwa vitendo. [141]
pekee
Katika mchezo wa pili Uganda iligeuza hasusa Somali kwa kuitandika mabao 4-0 huku mshambuliaji Tony Maweje akipachika mabao mawili pekee yake. [142]
picha
Ikabidi kwa kumtia moyo, ikabidi aende kwenye ofisi ambayo alikuwa akifanyia utafiti huo na kufanikiwa kupata picha yake. [143]
potofu
Aidha alitoa mwito kwa mashirika mbalimbali na taasisi za dini kuendela kutoa elimu kwa watu kuoindokana na imani potofu ya kishirikiana ambayo huwasukuma kufanya mauaji hayo kwa visingizio vya kupata utajiri. [144]
rais
Abdalah alisema kama rais atatumia mamlaka yake ni wazi kuwa CCM itakuwa safi na serikali yake kwa ujumla na kwamba, waliochukua fedha za walipakodi wakiwajibishwa utakuwa ni mfano kwa wengine. [145]
rasmi
Dk Kishe alikuwa kivutio kutokana na umahiri wake wa kusheheresha matumizi ya maneno yasiyo rasmi ambayo alisema kwamba kuna baadhi ya wanajamii wamekuwa wakiyatoa makavu makavu bila y kutanguliza neno ashakum. [146]
redio
Dk Kishe alimaliza kusema kuwa Bakita imekuwa mstari wa mbele katika kuelimisha na kuainisha matumizi ya Kiswahili ikiwemo kuandaliwa vipindi mbalimbali vya redio na televisheni, kuwepo na makala za kuelimisha katika magazeti. [147]
roho
Nakufa, mkuu wa polisi unaniua, sawa mimi nimemuua albino, lakini wewe unaniua mimi kwa kunipiga kibao, imeandika wapi kwamba muharifu apigwe, kabla ya kufikishwa mahakamani,” alisema Kazim huku akikata roho. [148]
rufaa
Kwa mfano, katika shauri la rufaa kati ya John Sima dhidi ya Jamhuri, mrufani ambaye alipatikana na hatia ya matumizi ya lugha ya matusi dhidi ya askari wawili wa jeshi pamoja na mama mwenye nyumba wake, alikuwa akipinga hukumu iliyotolewa dhidi yake kwa kosa hilo la matumizi ya lugha za matusi dhidi ya askari jeshi hao. [149]
saa
Ratiba ya mkutano huo inaonyesha kuwa ni siku ya ufunguzi na upigaji kura kwa wajumbe ambapo asubuhi ya leo wataanza na semina kuhusu mambo ya UKIMWI na saa tisa mchana matokeo ya uchaguzi huo yataanza kutolewa na kisha mkutano huo kufungwa. [150]
sana
Ninachoangalia sasa ni kupanga kwa mashambulizi kwa mchezo ujao najua utakuwa mgumu sana kwa vile Uganda wako imara na wako nyumbani. [151]
sasa
Hata hivyo, mpaka sasa limeshindwa kuanza kutoka huduma kutokana na ukosefu wa fedha. [152]
sauti
Sikiliza Kazim, usinitukane tafadhari, mimi ni mtu mwenye heshima zangu, nakusaidia tu, usiniletee shida, kama vipi rudi kule India tuone kama utapona, kosa langu ni nini?” alijibu waziri kwa sauti ya hasira. [153]
sekta
Katika mkutano huo uliokutanisha maafisa utamaduni zaidi ya 200 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar, na wadau mbalimbali wa sekta hiyo nchini, mkazo wake ulikuwa hamasa za utekelezaji wa dodoso za mkutano mkuu wa tano uliofanyika Dodoma. [154]
si
Rais alisema kuwa vita dhidi ya mafisadi ni ngumu na kwamba inahitaji gharama kubwa, kuwa kelele zinazotolewa na viongozi wa vyama vya upinzani na baadhi ya watu wakitegemea kuwa akitajwa mtu basi ni lazima afikishwe mahakamani si sahihi. [155]
sifa
Taarifa zilizoenea sehemu mbalimbali nchini; na hata kukamatwa na kushtakiwa mahakamani kwa mganga mmoja wa jadi kwa tuhuma za kukutwa na vifaa mbalimbali vya hospitalini na madawa kadhaa, zinadhihirisha kuwa vifaa hivyo sasa vinatumiwa na watu wasio na sifa kutumia vifaa hivyo kutibu wagonjwa. [156]
soko
SERIKALI sasa imedhamiria kusimamia bei za mafuta baada ya kuingilia kati utekelezaji wa agizo la Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji nchini (Ewura), la kuwataka wauzaji wote wa nishati hiyo kushusha bei kulingana na viwango vilivyowekwa vinavyooana na bei ya sasa katika soko la dunia. [157]
tatu
Alifahamisha kuwa Tanzania ni ya tatu kwa uzalishaji wa mazao yanayotokana na bahari narani Afrika, lakini inaingiza asilimia 4.7 tu katika pato la taifa. [158]
tiba
VIFAA vya tiba hospitalini sasa inaonekana kutumbukia mikononi mwa watu wasiostahili ambao hawana ujuzi wa taaluma ya uganga na udaktari wa kusomea kutoka taasisi zinazotambulika. [159]
tu
Hivi karibuni, Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa alisema kuwa serikali imefuta madeni yote ya ATCL, lakini taarifa zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa tamko hilo ni la maneno tu kwa sababu halijafanyiwa utekelezaji. [160]
tumekuwa
KWA muda mrefu Watanzania tumekuwa katika matatizo makubwa ya kupanda kwa bei ya mafuta, ambayo ilisababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la duniani. [161]
tuna
Hivi karibuni tulipokea msaada wa simu za mkononi kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino na tumewapa namba maalumu itakayowasaidia kuitaarifu jeshi la polisi hapa jijini Dar es Salaam na tuna angalia utaratibu wa kuzisambaza simu hizo nchi nzima," alifahamisha. [162]
tuzo
Lakini kwa kuwa sisi ni watu wa ukweli na uwazi, tumejiweka wenyewe ndani ya tuzo la tako. [163]
uchungu
Kwa nini wengine wafaidi tu, sisi waishiwa tusifaidi? Tumefurahi kuona kwamba wako wengi wenye uchungu wa nchi yao. [164]
uhai
Kitendo cha ATCL kusimamisha huduma zake tangu Desemba 8, mwaka jana, kinafanya shirika hilo kuendelea kupata hasara, jambo ambalo ni hatari kwa uhai wa shirika hilo. [165]
uko
Alisema kuwa zipo sheria mbalimbali ambapo zinaonekana kupitwa na wakati, hivyo utaratibu wa kuzibadilisha uko mbioni ili kutoa haki sawa kwa wanawake na wanaume. [166]
umma
Hata hivyo, suala la kukabiliana na ugonjwa huo linatakiwa kuchukuliwa na viongozi mbalimbali wa umma na taasisi zote za kijamii katika kuhimiza na kusimamia utoaji wa elimu ya afya na usafi wa mazingira, ambao ndiyo chanzo na kichocheo kikubwa cha mlipuko wa ugonjwa huo. [167]
usiku
Siku moja usiku akiwa nyumbani alitafakari sana hali ngumu ya maisha ambayo angeanza kuishi. [168]
vifaa
Mkurugenzi huyo alisema wizara imekwishakamilisha maandalizi yote kuhusu chanjo hiyo, ikiwa ni pamoja na mafunzo kwa watendaji na vifaa vitakavyotumika. [169]
vijana
Aghalabu matumizi ya lugha hii hufanywa na vijana na wakati mwingine hata watu wazima na hasa baada ya kughadhibika. [170]
vipi
Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni,” alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [171]
vita
Alisema kwa ukali: "Nipo tayari, nimejitoa muhanga kuhakikisha vita dhidi ya ufisadi inafanikiwa kwa faida ya Watanzania wote. [172]
viungo
Kwa mfano, katika kujifunza lugha na elimu inayohusiana na viungo vya kijinsia. [173]
vyake
Mratibu wa onesho hilo, Said Mdoe wa Screen Masters alisema kuwa onyesho hilo ni maalum kwa wakazi wa Yombo na vitongoji vyake. [174]
vyote
Tunaelewa kwamba, karibu vifaa vyote muhimu vya hospitali, mbali na sindano na vingine vidogo, haviuzwi kwa mtu yeyote isipokuwa walipewa vibali kutokana na taaluma zao. [175]
wa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa ATCL, Balozi Mustapha Nyang’anyi alilithibitishia Mwananchi jana kuwa, bila mtaji huo kupatikana, itakuwa ndoto kwa shirika hilo kuweza kuanza tena huduma zake. [176]
wadau
Mkutano huo ulijumuisha wadau mbalimbali wa utamaduni, wakiwemo maafisa utamaduni zaidi ya 200 kutoka wilaya mbalimbali za Tanzania Bara na Zanzibar. [177]
wale
Nitaendelea kupambana na mafisadi kwa nguvu zote, kinachotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha kuwa kunakuwepo ushahidi wa kutosha kwa wale wote wanaokamatwa na kufikishwa mahakamani," alisema Kikwete. [178]
walimu
Na siyo walimu tu. [179]
wangu
Nilijua itakuwa ngumu ndio maana nikawaambia wasimuachie mtu acheze mpira, wao wanauzoefu wa kumiliki zaidi kuliko sisi na nashukuru wachezaji wangu wamenielewa ndio maana tumeshinda,"alisema Mbrazil huyo. [180]
wao
Balozi Nyang'anyi alikataa kuzungumzia kauli iliyotolewa na Dk Kawambwa, lakini alisisitiza kuwa fedha ambazo wanadaiwa na mawakala wao bado hazijalipwa. [181]
wapo
Mpaka sasa Simba ndio waliotuthibitishia kuwa wapo tayari kucheza nao Januari 15, bado tunaendelea kuwasiliana na Yanga ambao tunataka wacheze nao Januari 14," alisema Bakhresa. [182]
watakuwa
Alisema wanawake ambao watakuwa wamependeza sana, watapewa zawadi maalum. [183]
wazazi
Tunasema, watoto wanawategemea wazazi kwa matunzo yao, au Tunategemea sana mvua kwa kilimo chetu. [184]
wengi
Habari hizo zilidai kuwa katika siku ya kwanza ya kuwahoji waislamu hao hao kulijitokeza mvutano uliotokana na baadhi ya maofisa wa polisi kutaka watuhumiwa wawekwe rumande, lakini wengi wakipinga kuwa watu hao hawakuwa na makosa. [185]
wewe
Ni vizuri kuongea kutokana na tofauti zenu, na kujaribu kuzungumzia wenyewe mambo ambayo wewe unayo moyoni kuhusu mwenzio ili kwa wakati wake ajaribu kuchuja na kujifunza kukuridhisha. [186]
wiki
Akizungumza jijini jana Mwenyekiti wa timu hiyo Hassan Dalali alisema kocha huyo aliyetua nchini wiki iliyopita atatia saini mkataba wa kuifundisha timu hiyo leo kwenye hoteli ya Regency jijini. [187]
yangu
Ni kweli ninafanya kazi, lakini si yangu, utajiri wangu umepungua, nilikuwa nataka kununuaq ndege binafsi ya kutembelea, kwa hali ya kipato changu cha sasa, sina uwezo wa kufanya hivyo, mbaya zaidi tayari nilishatamba kwa watu kwamba nitanunua ndege, nisipomnunua wataniona mimi ni maskini” alijisemea. [188]
yenu
Ndugu yenu kutoka pande hizi naomba niendelee kuwashukuru ninyi wasomaji wangu kwa hamasa na changamoto mnnazonipa. [189]
yetu
Tayari tumewasilisha mikakati yetu, tumelenga zaidi kuleta mapinduzi ya maendelea katika mchezo wa riadha, tunaamini kwa kushirikiana na wizara yenye dhamana hiyo tutabadilisha kwa kiasi kikubwa muonekano wa mchezo huu kwa sasa,"Alisema Musomi. [190]
yeye
Na ni kwa sababu hiyo mtu moja huyo amekuwa akiweka kifuani na kuhesabu makosa ya mwenzie bila ya yeye kujijua kuwa, kwa kufanya hivyo anakosea pia. [191]
yeyote
SERIKALI imesema Jeshi la Polisi nchini haliwezi kuogopa kumchukulia hatua mfanyabiashara au kiongozi yeyote aliyeko au aliyetoka madarakani atakayefana makosa. [192]
yuko
Anasema tayari kazi ya kubaini maeneo zitakapopita barabara husika imekwishafanyika hivyo yeyote atakayeanza ujenzi mpya katika maeneo hayo yuko katika hatari ya kuingia hasara ya kutolipwa fidia yoyote na majengo yake kuondolewa. [193]
yule
Hakuna jambo la kukufanya tusikutangaze kama mgunduzi wa dawa kuponya kansa kwenye moyo, dawa yako tulimpa hadi mtoto wa rais na amepona, rais anataka akuone kukushukuru na kupanga sherehe kubwa ya uzinduzi wa dawa hii ya aina yake,” alisema waziri wa afya wa nchi hiyo siku moja alipokutana na kijana yule mwenye ulemavu wa ngozi. [194]
za
Balozi Nyang'anyi alitaja vikwazo vingine vinavyozidi kulinyanyasa shirika hilo kuwa ni deni la Sh19, bilioni wanalodaiwa na mawakala mbalimbali ambao walichangia huduma kadhaa za uendeshaji wa shirika, siku za nyuma. [195]
zake
Ili shirika hilo liweze kurejesha huduma zake katika hali ya kawaida, zinatakiwa zaidi ya Sh 7.1 bilioni. [196]
zako
Endapo nguvu na bidiii zaidi utazielekeza kwenye shughuli zako mwaka huu unaweza kuufurahia na kama sivyo basi utaununia. [197]
zenu
Zaidi nataka niwatakie mwaka mwema wenye baraka kwenu na kwa familia zenu, nataka pia niwakumbushe kuwa huu unaweza kuwa mwaka wa neema kwa watakao jishughulisha. [198]
zetu
Kimsingi kwa mujibu wa mila na desturi zetu za kitanzania, ni mwiko au haipendezi kutumia maneno mabaya yenye asili ya matusi katika maongezi ya kawaida. [199]
zina
Kundi hilo lina utata mkubwa kutokana na tofauti ndogo iliyopo baina ya timu za Kenya, Zambia na Burundi ambazo zote zina nafasi. [200]