Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-03

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


achukue
Haisemi nani achukue hatua, wala kwa vipi. [1]
adhabu
Wakizungumza na Mwanachi, wanafunzi hao walisema kuwa wanasikitishwa na hatua iliyochukuliwa na uongozi kutaka kuwapa adhabu viongozi wao. [2]
afya
Mfano nchi inatoa dola milioni 120 katika miradi ya afya, katika fedha hizo wanazitumia kulipa mishahara ya wataalamu wao, kulipa gharama kubwa za kupangisha nyumba na mambo mengine meng baada ya muda wanaondoka na wataalamu wao na faida kubwa waliyoipata" alisema. [3]
aina
Ilikuwa ni vigumu kuelewa aina ya msako uliokuwa ukifanywa na mgambo hao na ndiyo maana kila mtu aliyekuwa katika eneo hilo la tukio alikuwa akizungumza lake. [4]
akili
Yaani watu wanafurika kupendekeza majina ya watu wanaostahili nishani ya viatu, kama yule mwandishi asiyeogopeshwa hata na asidi, na yule mtoto aliyemuuliza swali waziri mkuu aliyepitwa na wakati hadi akaandamwa na mashushushu eti mtoto hana akili ya kuuliza maswali kama hayo, na wale waliokaa barabarani mbele ya magari hadi shida zao ziliposikilizwa. [5]
aliongeza
Mganga aliongeza kuwa washtakiwa hao walitumia vibaya madaraka yao kwa kumualika Dk. [6]
alitaka
Mzee alitaka kukasirika kwa hiyo nilijaribu kuingilia kati. [7]
ama
Lakini naamini kwamba mgambo wengi ama hawajapatiwa elimu ya au wanalewa majukumu yao ndiyo sababu wamekuwa wakishiriki katika vitendo vingi vya udhalilishaji na ukiukaji wa haki za binadamu. [8]
amani
Bodi hiyo iliyoundwa na Meya ndiyo yenye jukumu la kusimamia utekelezaji suala hilo ikiwamo kuwatambua wafanyabiashara wenye sifa za kupangishwa, kusimamia amani na utulivu katika jengo hilo," alieleza. [9]
ambae
Kocha Maximo ambae kikosi chake kinaanza kutupa karata ya kwanza leo majira ya saa 7.30 mchana dhidi ya Somalia amesema wapinzani wake hawana cha kupoteza. [10]
amri
Tunatoa amri kwamba shauri hilo lirudishwe Mahakama Kuu na lisikilizwe mbele ya jaji mwingine," jopo hilo limesema katika uamuzi uliosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Profil Lyimo. [11]
ana
Ukiangalia Somalia ni timu nzuri ambayo inashiriki haya mashindano, lakini haina changamoto kubwa kama tulivyo sisi Tanzania,îalisema Maximo ambaye kila mmoja jijini hapa ana shauku ya kuona timu yake inachazaje. [12]
anasema
Profesa Chris Peter Maina wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anasema kuwa pamoja na serikali kuhusika kwa kiasi kikubwa katika vitendo vya uvunjifu wa amani, wananchi nao wanahusika kwa kiwango kikubwa. [13]
anaweza
Alisema kuwa katika hoja ya pili, Sheria ya Viapo, wakili anaweza kushuhudia kiapo. [14]
ardhi
Mahakama Kuu (kitengo cha ardhi) ilikosea kwa kutoliamua shauri hili katika misingi ya hoja. [15]
au
Mawakili hao Hebert Nyange, kwa niaba ya Mramba, Sam Mapande kwa niaba ya Yona, na Profesa Leonard Shaidi kwa niaba ya Mgonja, kwa nyakati tofauti waliomba mahakama ipitie tena sharti hilo na kuwapunguzia kiwango cha pesa au thamani ya hati za mali walizoziwasilisha mahakamani hapo kwa kuzingatia kanuni ya kushirikiana katika kiwango cha dhamana. [16]
awali
Kwa mabadiliko hayo, mashtaka hayo sasa yatawahusisha watuhumiwa watatu badala ya wawili kama ilivyokuwa awali. [17]
bado
Tunaweza kwenda mahakamani, lakini bado viongozi tutalijadili kwanza. [18]
baina
MCHEZO wa Kirafiki baina Simba ya jijini Dar es saalam na Coastal Union ya hapa,juzi uliingia dosari baada ya wapenzi wa soka kuvamia chumba cha mauzo na kupora fedha. [19]
bali
Alisema watu wengi wanajidanganya kuwa mauaji haya hayawahusu, alisema mapambano hayo ni ya wote kwa sababu si mapambano ya kidini wala ya kikabila, bali ni mapambano ya kupigania haki za binadamu zinazovujwa huko Ghaza. [20]
baraza
Uongozi wa serikali ya wanafunzi ulipokwenda NACTE kujua kuna tatizo gani ulijibiwa kuwa chuo kilifanya makosa kusajili wanafunzi bila kulishirikisha baraza hilo. [21]
bila
Kuna kitu Chadema inaweza ikafanya ili iendelee kuwemo kwenye uchaguzi," alisema Zitto bila ya kubainisha kitu hicho. [22]
bodi
SERIKALI imeiamuru bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuwachukulia hatua za kinidhamu wafanyakazi waliohusika katika uzembe uliosababisha shirika hilo kunyang’anywa leseni ya kurushwa ndege, huku ikitangaza mkakati wa kulihuisha. [23]
bora
Nilikuwa na kikosi cha wachezaji wengi, lakini nyie niliowachagua ndio bora zaidi, kila mmoja kwa wakati wake anapaswa kunithibitishia kwamba sikufanya makosa kumpa nafasi hii. [24]
chake
Hadidu za rejea kwa hicho kikosi kazi alizitaja kuwa ni kuweka bayana matatizo ya ATCL, chanzo chake na kuishauri serikali hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa. [25]
chama
Lakini msaidizi wake, Zitto Kabwe ndiye aliyekuwa na kauli ya matumaini kwa wafuasi wa chama hicho kilichoibuka kidedea kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime. [26]
chini
Kwa sababu hiyo, alisema serikali imeamua kuunda timu ya watu saba, ambayo itakuwa chini ya makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Profesa Idrissa Mshoro ili kutoa tathmini ya kitaalamu. [27]
chuki
Hata hivyo, nadhani badala ya kuendelea kuwalaumu na kujenga chuki dhidi yao, tuwaombe viongozi wa manispaa na jiji la Dar es Salaam kwa ujumla na wale wote wanaosimamia ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba mgambo wanapata mafunzo thabiti ya kazi zao. [28]
chuo
ZAIDI ya wanafunzi 1,000 wa mwaka wa kwanza kwenye Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wamegundulika kuwa hawana sifa za kujiunga na chuo hicho. [29]
dili
Alianza kwa kusema: "Jamani mnasikia kuwa sasa hivi albino sio 'dili' tena?" Tukaguna basi akatuuliza mnaguna nini na kusisitiza akitumia maneno ya mjini siku hizi: "habari ndiyo hiyo. [30]
dogo
Akizungumzia sakata hilo, Ngamba alisema ni kweli kwamba timu yake iliwachezesha wachezaji walioongezwa katika dirisha dogo la na watakaosajiliwa msimu ujao. [31]
dola
Hata hivyo, ATCL ilirejeshewa cheti hicho Jumanne iliyopita baada ya kukamilisha kujaza kwa usahihi nyaraka hizo za TCAA. Serikali ilitoa dola 273,000 za Marekani kwa ajili ya kufanikisha zoezi la kusahihisha dosari zilizopkuwepo kwenye nyaraka muhimu za utoaji wa huduma za ndege. [32]
elimu
Haya yote yalitokana na tabia waliyoonyesha kiasi cha wananchi wa kawaida kabisa kuhoji uwezo, elimu na busara zao katika utendaji wao wa kazi. [33]
eneo
Mmbando alimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Said Shaaban ambapo alimkabidhi hundi pamoja na seti za jezi na mipira 15 katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za wizara hiyo zilizopo eneo la migombani mjini Zanzibar. [34]
es
Akitoa uamuzi kuhusu ATCL jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Miundombinu, Dk. [35]
fedha
Mganga alisema Mramba, ambaye wakati huo alikuwa waziri wa fedha, na Yona akiwa waziri wa nishati, waliingia mkataba huo kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma na Sheria ya Madini. [36]
fujo
Siku hizi huwezi kusikia watu wakizungumzia mambo ya siasa, nadhani tumeona picha za waathirika wa fujo kwenye maeneo ya vijijini, kwa hiyo hakuna anayependa kuishia kwenye hali hiyo. [37]
gani
Naye Wakili Nyange aliiomba mahakama ifanye upya tathmini ya kiasi kinachotakiwa kutolewa baada ya washtakiwa hao kuunganishwa ili waweze kuomba kuondoa baadhi ya mali zitakazozidi, lakini akaomba wapewe muda wa kuangalia ni hati gani waweze kuziondoa kwa kuwa suala hilo limekuwa ni la ghafla. [38]
gari
Mtapendekezaje kwamba sisi tupewe tuzo ya tako kwa kuthamini gari kuliko kompyuta. [39]
hadi
Kuhusu hoja ya wagombea kama walikuwa na muda wa kutosha wa kukamilisha fomu zao za uteuzi na kuziwasilisha kwa wakati, Jaji Makame alisema kuwa kwa mujibu wa barua ya msimamizi wa uchaguzi ambayo walipatiwa makatibu wote wa vyama vya siasa wa wilaya, wagombea walitakiwa kuchukua fomu za uteuzi kuanzia Desemba 17,2008 hadi Desemba 27,2008 ambayo ilikuwa siku ya kwanza. [40]
hali
Hivyo ikagundulika kuwa kuna baadhi ya watu wanaokula rushwa kusajili wanafunzi kwa njia wanazojua na kuwapa namba za usajili bila kufuata utaratibu, hali ambayo inaharibu sifa ya chuo," alisema mtoaji habari huyo. [41]
hana
Kocha wa Zanzibar, Badr El Din alisema kwamba mchezo huo utakuwa mgumu na wachezaji hawatofautiani sana, lakini hana wasiwasi wowote. [42]
hao
Katika mashtaka hayo Mganga alisema washtakiwa hao kwa pamoja kati ya mwaka 2002 hadi 2005 wakiwa watumishi wa umma katika nafasi za uwaziri, walitumia vibaya madaraka yao kwa kuingia mkataba na kampuni ya M/S Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Uingereza, ulioiwezesha kampuni hiyo kudhibiti uzalishaji wa madini nchini. [43]
hapa
Akichangia mjadala huo kwa kutoa mfano wa Cuba, afisa ubalozi wa Cuba hapa nchin, Dionisio Hernandez, alisema nchi za magharibi daima zimekuwa na sera za unyonyaji na njia pekee ya kujinasua ni kuwa na mshikamano isiotetereka. [44]
hasa
Alisema kama nchi za Afrika zikiungana na kuwa na msimamo wa pamoja katika mambo yake na hasa kuwa na soko la pamoja, itakuwa vigumu kuingiliwa na mataifa tajiri kwa kutumia ubaguzi wa watu wachache wenye uchu wa madaraka. [45]
hata
Akizungumza baada ya Maandamano ya kupinga hayo katika Uwanja wa Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, Profesa Haroub alisema Rais Kikwete anayo nafasi ya kuwashawishi wakuu wa nchi za Afrika kulaani mauaji hayo kwa kuvunja uhusiano na Waisraeli na hata kuvunja uhusiano wa kubiashara na kiuchumi na nchi hiyo. [46]
hati
Kutokana na hatua hiyo, upande wa mashtaka, ambao jana uliongozwa na mwendesha mashtaka wa serikali, Biswalo Mganga umefanya mabadiliko katika hati ya mashtaka ya Mramba na Yona. [47]
hatia
Kitendo cha jeshi la polisi kutumika vibaya katika uchaguzi huo ni ishara kuwa, jeshi hili linatumika kisiasa zaidi kwa kupendelea watu fulani, hadi kupelekea kuvunja haki za kibinadamu kwa kuwamwagia maji ya pilipili na kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia," anasema Profesa Maina. [48]
hawa
Bila ya kupambana na uhalifu, wananchi watakosa amani kwani usalama wao na mali zao vitakuwa rehani, lakini sasa wanachokifanya hawa mgambo kukamata watu ovyo na kuwapiga hakiwezi kuungwa mkono. [49]
hawezi
Sasa narudia kusema; usiogope kumwambia mwezako unavyotaka akufanyie kwani asipofanya usimlaumu kwa kuwa hawezi kujua. [50]
hayo
Alisema kifungu cha 38 (3) (a) katika Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985 kinaeleza kuhusu wagombea ubunge pekee, hivyo kutokana na maelezo hayo jibu ni dhahiri kuwa sheria za viapo haziwezi kutumika katika viapo vya ubunge. [51]
hii
Kutokana na maelezo ya majibu ya hoja zilizoanishwa na kwa kuzingatia uamuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika rufaa ya Ernest Binna mgombea ubunge jimbo la Bunda kwa tiketi ya CUF katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Tume ya Taifa ya uchaguzi inakataa rufaa hii," alisema. [52]
hiki
Kitendo hiki kinaashiria kuwa baadhi ya wawekezaji hawa hawana sifa kwani wanapaswa kuwa na teknolojia ya kisasa na uwezo wa kifedha kuendesha shirika kubwa kama hilo. [53]
hilo
Kauli yake ililingana na ya katibu wake mkuu, Wilbroad Slaa ambaye alilitazama suala hilo kisheria zaidi. [54]
hivi
Moja ya mambo yatakayofanyika katika marekebisho ya mkataba huo ni kuangalia uwezekano wa serikali kuwa na mamlaka katika suala la utawala ndani ya TRL... hivi sasa mamlaka yote yapo chini ya Kampuni ya Reli ya India (Rites)," alisema. [55]
hiyo
Lakini jana, mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Lewis Makame aliwaambia waandishi wa habari kwenye hoteli ya Mount Livingstone kuwa baada ya kutafakari mambo makuu manne, tume yake imetupilia mbali rufaa hiyo. [56]
hizi
Hisia hizi za wasiwasi zimekuwa zikizidi kila siku kufuatia matendo yanayofanywa na askari hawa ambao wengi wao ni vijana ambao kwa hali ilivyo inaonekana wanmekosa moyo wa ubinadamu. [57]
hizo
Alisema kuwa ili kuweza kupata majibu ya hoja hizo, tume ilichambua kila hoja na kwamba katika hoja ya kwanza, tamko la mrufani (Shitambala) lililotolewa kwenye fomu zake za uteuzi halikuwa halali kwa kuwa alilifanyia kwa wakili. [58]
huenda
Mchezo wa leo ni changamoto kubwa kwa Stars kwani mashabiki wote wa hapa wamekuwa wakiizungumzia na huenda wakafurika uwanjani kutaka kuiona. [59]
huko
Hivyo ni wakati sasa kwa Wafrika kuunga kupiga vita unyama na udhalimu unaofanywa na Waisrael huko Ghaza. [60]
huku
Mramba sasa anakabiliwa na mastaka 12 badala ya mashtaka 13 ya awali, huku Mgonja akikabiliwa na mashtaka nane kama ilivyokuwa awali, wakati Yona naye anakabiliwa na mashtaka matano kama ilivyokuwa awali. [61]
huo
Mgombea huyo hakukubaliana na uamuzi huo na kukata rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. [62]
huru
Alisema kutokuwa na msimamo wa pamoja kama nchi huru za Afrika kunazipa nafasi nchi za magharibi kuendeleza utawala wao kwani wamekuwa wakitumia matatizo ya waafrika kuendeleza maslahi yao binafsi. [63]
huu
Waziri Kawambwa aliongeza kwamba bado wako kwenye majadiliano na RITES yaliyoanza mwezi Novemba mwaka jana na watakutana tena Januari mwaka huu. [64]
huwa
Kila mwaka ifikapo Januari mosi, maneno mengi husemwa kuhusu kampeni hiyo ya upandaji miti inavyoendelea, lakini baada ya tarehe hiyo kupita, na maneno hayo hupotea hadi Januari mosi nyingine au tarehe nyingine ambayo mkoa huwa umejipangia. [65]
huwezi
Watafiti wanasema huwezi kutatua tatizo kabla ya kulijua. [66]
huyu
Nafuu nyingine anayoweza kujipatia mtu huyu ni kufungua kesi ya madai dhidi ya wote waliofungua au kusababisha kifungo hicho na mwisho, katika mazingira fulani ya kisheria, mtu aliyefungiwa isivyo halali anaweza kupata nafuu kwa msaada wa mahakama kutoa hati maalum ya kisheria ijulikanayo kama 'Habeas Corpus' kuamuru kuachiwa wakati au kupisha hatua nyingine za kimahakama kuendelea ili kuthibitisha au kutengua uhalali wa kifungo chake hicho. [67]
ibaki
Kwa ukatili huu, napenda hii adhabu ya kifo ibaki pale pale kwani ni wa hali ya juu, unaoumiza wanaoathirika kwa kiwango kikubwa, kwa lugha nyepesi umepitiliza na ni unyama. [68]
idara
Inadaiwa kuwa mmoja wa wafanyakazi hao anafanya kazi idara ya manunuzi wakati taaluma yake ni ufundi, na mwigine anashikilia kitengo cha rasilimali watu wakati taaluma yake ni mawasiliano. [69]
ile
Baadhi ya waandishi tuliokuwapo pale, tulimtafuta kiongozi wa operesheni ile kujua kulikoni lakini alikataa katakata kulizungumzia suala hilo, na badala yake alitoa amri kwa askari wake akiwataka wapande katika karandinga lao pamoja na watu ambao waliwakamata wakidai kuwa ni wahalifu. [70]
iliyo
Profesa Shaidi aliiomba mahakama ikubali kuondoa hati za mali namba 186038/116 ambayo ni nyumba ya Marry Ngulume iliyo kiwanja namba 29, Ada Estate yenye thamani ya Sh. [71]
ina
Ingawa serikali pia ina hisa ya asilimia 49 katika kampuni hiyo, tatizo liko katika mkataba wa uwekezaji kwani moja ya kipengele katika mkataba huo unairuhusu RITES kuajiri wafanyakazi na katika marekebisho haya moja ya maeneo yatakayotazamwa ni suala la menejimenti ya TRL ambayo kwa sasa ina wafanyakazi wote kutoka India. [72]
jinai
KATIKA makala zilizotangulia tulijadili juu ya haki ya asili ya binadamu kuwa huru na jinsi inavyoweza kuingiliwa na utendaji au utekelezaji wa sheria ya jinai kimakosa. [73]
jinsi
Ni kwa jinsi hiyo tu, kampeni ya upandaji miti inaweza kufanyika kwa ufanisi badala ya kuwa ya maigizo ya Januari mosi. [74]
jua
Na kama hato jua basi hawezi kukuridhisha na kama hatokuridhisha jua hutofurahisha na kama hatofurahia basi mengine ndiyo haya yatokanayo. [75]
juu
Alikuwa akitoa uamuzi wa serikali baada ya kupokea maelezo ya mwenyekiti wa bodi ya ATCL, Balozi Mustapha Nyang’anyi aliyotakiwa kuyatoa katika muda wa siku saba juu ya sababu zilizosababisha shirika hilo kunyang’anywa cheti hicho na TCAA Desemba 8, mwaka jana. [76]
kabisa
Tutafungwa na timu zote unazozijua, lakini si Bara hatukubali kabisa na wala hawawezi kufanya kitu kama hicho. [77]
kali
Katika kipindi cha pili Zanzibar ilionekana kujimarisha zaidi katika nafasi ya Ulinzi ikiongozwa na Naroub Haroun 'Canavaro' na kuzuia hatari zote katika dakika ya 55 mshambuliaji wa Somalia, aliyewahi kuichezea Simba ya Tanzania, Isse Abushir alipiga shuti kali lilopita juu kidogo ya lango. [78]
kasi
Ikiwa hili litatekelezwa kwa kasi ile ile wanayoifanya katika kutimiza unyama wao, ninaamini kabisa kwamba majonzi haya tunayopata kila siku kusikia wenzetu hawa wamepoteza maisha kwa mtindo huu yatapungua kama sio kukoma kabisa. [79]
kazi
Alisema kuwa kutokana na siku hizo wagombea walikuwa na siku sita za kazi ambazo wangeweza kuzitumia katika kuwasilisha viapo vyao kwa mahakimu kwani mrufani alijua wazi kuwa siku za sikukuu na mwisho wa wiki mahakama hazifanyi kazi hivyo alitakiwa kuchukua tahadhali kwa kutumia siku ambazo mahakama zinafanya kazi. [80]
kesi
HATIMAYE katibu mkuu mstaafu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja jana aliunganishwa katika kesi inayowakabili mawaziri wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona ya matumizi mabaya ya ofisi za umma na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh11 bilioni. [81]
kiasi
Mashtaka mengine kwa washtakiwa hao ni kutoshughulikia suala la ada ya madini na kutopeleka makubaliano kwa mwanasheria mkuu wa serikali na hivyo kuipa kampuni hiyo muda wa nyongeza kabla ya kushughulikia suala la kiasi cha ada ambacho kampuni hiyo ilitakiwa kulipa. [82]
kifungo
Mtu anaweza kuwekwa chini ya ulinzi au kifungo kisicho halali kutokana na sababu mbili au zaidi. [83]
kike
Sheria ya Makosa ya Kujamiiana ya mwaka 1998, pamoja na mambo mengine, imelenga kuthibiti unyanyasaji wa kijinsia ukiwemo kuwapa mimba watoto wa kike lakini haijafanikiwa kwa kiwango kilichotarajiwa licha ya ukali wake. [84]
kina
Jopo la Stars lililoko mjini hapa halikuweza kusema sababu maalum ya kuchelewa, lakini benchi la ufundi lilidai kwamba lilikuwa likifanya maandalizi ya kina. [85]
kituo
Hata hivyo; waandaji wa mchezo huo walikuwa hawajaripoti kituo chochote cha Polisi kwa ajili ya kuchukua hatua za kuwasaka waliohusika na tukio hilo ambalo si la kimichezo. [86]
kocha
TIMU za Tanzania, Zanzibar na Kilimanjaro Stars leo zitashuku dimbani kwenye uwanja wa Nakivubo kwa nyakati tofauti, huku kocha Marcio Maximo akiwatahadhalisha :"wachezaji wake atayecheza chini ya kiwango katika mashindano haya ya Chalenji tusilaumiane. [87]
kombe
TIMU ya soka ya Simba jana iliondoka kwenda Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi ambapo leo inaanza kutupa karata yake ya kwanza kwa kucheza na Miembeni ya Zanzibar. [88]
koo
Na kama desturi ilivyo, mwenye pendekezo lazima alainishe koo za waishiwa, pamoja na kutoa posho la tako (si tuzo la tako). [89]
kosa
Baadaye Mgonja akafikishwa mahakamani peke yake Desemba 15 kwa kosa linalolingana na lile la Mramba na Yona kwa maelezo kuwa uchunguzi dhidi yake ulikuwa haujakamilika. [90]
kote
Ni miaka 60 sasa tangu kuanza maadhimisho ya Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu duniani kote, matendo ya uvunjifu wa haki za kibinadamu yamekuwa yakiongezeka duniani kote. [91]
kubaki
Kitendo hicho husababisha watoto kubaki bila malezi na kuanza kujitafutia maisha kwa njia zisizofaa, na hapo ndipo wasichana huangukia kupata mimba. [92]
kuimba
Mgambo wamewekwa kwenye vizuizi barabarani na katikati ya jiji wakisimamisha ovyo magari na kuwataka abiria kuimba na kukariri tamko hilo. [93]
kujua
Wanafunzi hao walipeleka malalamiko yao kwa uongozi wa serikali ya chuo wakitaka kujua sababu za kutokuwa na sifa za kujiunga na chuo hicho wakati walishafanya majaribio. [94]
kukemea
Wazee wanapaswa kulaumiwa kwa sababu wameshindwa kutekeleza jukumu lao la kikatiba la kuonya, kushauri na kukemea mambo yanapoanza kuharibika," alisema. [95]
kulinda
Alisema bodi hiyo imeundwa kulinda na kutekeleza haki za wafanyabiashara watakaopangishwa kwenye jengo hilo ambalo sasa bado halijakabidhiwa kwa halmashauri ya jiji. [96]
kuna
Bado kuna namna ya kufanya. [97]
kusema
Tunajidanganya kwa kusema kuwa mauaji haya hayatuhusu. [98]
kuu
Morogoro kupitia soka na kuwataka wasibweteke na ushindi huo bali wajitahidi kufanya vizuri katika ligi kuu inayotarajia kuanza baada emwezi huu. [99]
kuuaga
Kumbi mbalimbali za burudani zilifulika watu katika hekaheka za kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya huku kuwa na matukio ya kufurahisha na kuburudisha. [100]
kuvamia
Aliongeza kuwa mwaka 1997 Tanzania ilivunja uhusiano wake na Israel baada ya Waisrael kuvamia nchi za mashariki ya mbali pamoja na baadhi ya nchi za Afrika kupinga uvamizi uliokuwa na lengo la kudhulumu rasilimali za nchi hizo. [101]
kwa
Mgombea wa Chadema, Sambwee Shitambala alienguliwa na Tume ya Uchaguzi ya Mbeya Vijijini baada ya vyama vya CCM na CUF kuwasilisha pingamizi, vikidai kuwa alikiuka Sheria ya Uchaguzi kwa kuapa kwa wakili badala ya kwa hakimu. [102]
kwake
Utetezi mwingine unaoweza kutumiwa na mlalamikiwa ni pamoja na kama itatokea mlalamikaji mwenyewe kuwa ndiye chanzo cha kufungiwa kwake huko, yaani kifungo cha kujitakia, hii inafanana na msemo wa Kiswahili kwamba 'mwenye kilanga haliliwi' hivyo hana wa kumbebesha lawama kwa kuwa ni yeye ndiye aliyesababisha kufungiwa kwake. [103]
kwao
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye hoter ya Avys ipoweka kambi timu Kill Boys rais huyo wa TFF alisema hadi yake kwao watapofanikiwa kurudi na ubingwa nyumbani fedha zote dola elfu 30 watagawana wao wachezaji na mwalimu. [104]
kweli
Prof Wamba alitoa wito huo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza katika mjadala wa wazi ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, ambapo pia alizitaka nchi za Afrika kuwa na demokrasia ya kweli inayozingatia usawa na haki kwa wananchi wake. [105]
kwetu
Tuyatumie mashindano haya kwa umakini pia tunatakiwa kuthibisha mbele ya umma wa Watanzania na wapenda soka barani Afrika kuwa kufuzu kwetu kwa fainali za CHAN haikuwa bahati. [106]
la
Kwa kuwa suala hili ni la kisheria, ni vema ukatupa muda kwanza ili tulijadili kuona tutafanyaje," alisema Dk. [107]
lake
Katika ziara hiyo Nnauye aliwapa wazee hao zawadi ya vikombe vya kahawa, birika lake na fedha taslimu Sh100,000 kama ishara ya kuwataka waendelee kukutana kwenye shina hilo na kuzungumza mambo ya chama. [108]
lao
Nape alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akizungumza na wazee wa CCM wa kata ya Kiwalani katika ukumbi wa shina lao la wakereketwa la Kibuyu ambako wazee hao hukutana kwa ajili ya kunywa kahawa na kujadili siasa. [109]
leo
Hatuwezi kuwaamini watu waliotutawala na wakatufananisha na mbwa, leo hii warudi wakiwa na nia njema ya kututatulia matatizo yetu, ukweli ni kwamba wana maslahi yao binafsi ambayo yamekuwa yakituongezea migogoro isiyoisha" alisema. [110]
letu
Alisema "Makundi hayo hata sasa bado yapo kwani baadhi ya wanaCCM wanaita shina letu hili la wakereketwa kuwa shina la wahuni na wapika majungu. [111]
ligi
Tunajua Tanzania ni timu ngumu na ina wachezaji wengi wa viwango vya juu lakini njooni muone mpira,kwenye kikosi chetu mimi mwenyewe ndio nacheza ligi wengine wote hawachezi sababu ya vita lakini kazi itafanyika. [112]
maduka
Wafanyabiashara wengi hasa wa maduka katika maeneo hayo yaliyovamiwa hawakusalimika. [113]
maisha
Naamini kwa kufanya hivyo, watabadilika na kusaidia katika utoaji wa elimu kwa wakazi wa jiji kuhusu haki na wajibu wao, ili sote tufurahia matunda ya nchi hii na kuendesha maisha kwa amani na kuheshimiana. [114]
maombi
Hakimu Mwankenja alirejea tena saa 6:30 kutoa maamuzi kuhusu maombi ya upande wa utetezi, akisema kila mshtakiwa atatakiwa kuweka hati ya mali yenye thamani ya Sh. [115]
mapema
Waziri Kawambwa alisema hatua hiyo inatokana na marekebisho ya mkataba ulioanza mapema mwaka jana baada ya serikali kuunda kamati ya kupitia upya mkataba huo. [116]
mapenzi
Ngoma hizi pia huandamana na unywaji wa pombe na wavulana na wasichana huwa huru kufanya mapenzi na mtu yeyote kitu ambacho kinachochea mimba na ndoa, kwa sababu baada ya ngoma hufuatiwa na ndoa kwa wapenzi waliokutana kwenye singenge. [117]
mapya
Baadaye ndipo Mgonja alipanda kizimbani kuungana na Mramba na Yona ndipo wakasomewa mashtaka hayo mapya. [118]
mara
Haiwezekani kila mara wawe chanzo au wahusishwe na vurugu. [119]
mazao
Serikali pia inapaswa kuhakikisha uwepo wa masoko kwa ajili ya mazao ya wakulima vijijini. [120]
mazuri
Lakini, kama kawaida, watu wanapenda kuona mabaya kuliko mazuri hivyo vimependekezwa vikundi vingi sana kwa tuzo la tako. [121]
mbinu
Kuchelewa kwa Stars kuwasili mjini hapa kumechukuliwa kama ni moja ya mbinu za kimichezo huku baadhi ya mashabiki wakidhani kwamba Tanzania ina wachezaji wenye utajiri mkubwa na wanaocheza soka la kulipwa ndio maana ikachelewa kuwasili. [122]
mengi
Maeneo mengine yaliyokuwa yanasheherekea usiku huo hapa nchini ni pamoja na Makumbusho,Vatcan City Sinza, Kempisk, Movenpik Hotel, New Msasani Club, Roya Zambezi Mbeya, Splended Tanga, Kibo Kigoma, Twisters Pub na maeneo mengine mengi hapa nchini. [123]
mimi
Kila mmoja hapa anapaswa kunionyesha mimi wakati huu kwamba sikufanya makosa kwenye uteuzi wake, nataka mshinde na timu ifike mbali ndio maana sikuleta kikosi kingine hapa. [124]
mitaa
Shabani Maembe alimwambia Nnauye kwa masikitiko kuwa kushindwa kwa CCM katika mitaa ya Kiwalani, Kigilagila na Yombo katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2004, kulitokana na makundi yaliyoibuka ndani ya chama hicho kwa misingi ya ushabiki. [125]
miti
JANA ilikuwa siku ya uzinduzi wa kitaifa wa mwaka wa zoezi la upandaji miti wakati Rais Jakaya Kikwete alipoongoza kampeni hiyo kandokando ya Barabara ya Kilwa. [126]
mke
Katika Wilaya ya Tandahimba, Lindi kwa mfano, imebainika kwamba baada ya mavuno wanaume huwapa wanawake talaka kitu ambacho kinajulikana kama "kusafisha ghala," mke mpya huingizwa na yule wa zamani kufukuzwa. [127]
mkia
JUZI mkuu wa wilaya ya Korogwe alizuia likizo ya ofisa elimu wake na kutishia kumchukulia hatua za kinidhamu kutokana na wilaya hiyo kushika mkia katika matokeo ya darasa la saba. [128]
mkoa
MABINGWA wa Kombe la Tusker, Mtibwa Sugar ya Turiani mjini Morogoro, imewasili mkoani hapa na kupata mapokezi makubwa huku serikali ya mkoa ikiahidi kutoa sh 1 milioni kwa wachezaji wa timu hiyo. [129]
mnene
Waishiwa wateule, kwa nini hapa Tanzania, daima tuko upande wa watendewa kuliko watendaji? Hebu angalia maazimio mwisho wa warsha zote ambazo hatimaye mnene kwenye nguvu amesimamisha. [130]
moja
Alisisitiza kuwa serikali ipo tayari kumuwajibisha yeyote iwapo atatajwa kwenye ripoti hiyo kwa kuwa lengo ni kuhakikisha ATCL inaondokana na wingu la vikwazo na kuwa moja ya mashirika makubwa ya ndege barani Afrika. [131]
moto
Siku nne baadaye, askari polisi walivamia kijiji hicho na kuwaondoa wanakijiji hao kwa nguvu kabla ya kuharibu mali na kuchoma nyumba zao moto. [132]
moyoni
Amani ilikuwa imetawala moyoni. [133]
mpya
Mgogoro huo ulichukua sura mpya mwezi Oktoba 8 mwaka 2001 baada ya halmashauri hiyo kutoa matangazo kwa vipaza sauti, ikiwataka wananchi hao waondoke katika ardhi iliyobaki ndani ya siku nne. [134]
msomi
Naye msomi mwingine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof Issa Shivji alisema, miaka 50 iliyopita Watanzania walishirikiana na baadhi ya mataifa ya Afrika kupiga vita ukaburu na uzayuni uliofanywa na wazungu wa Afrika Kusini. [135]
muziki
Baadhi ya mashabiki wa muziki huo walisema wameamua kujiunga na kupanda jahazi kwa kuukaribisha mwaka wakiwa pamoja na kundi hilo maridadi jijini hapa. [136]
mwanamke
Sheria ya Makosa ya Kujamiiana (Sospa) ya mwaka 1998, uamuzi wa mwanamke kufanya mapenzi unaanzia miaka 18 na kuendelea. [137]
mwema
Hakuna mwananchi mwenye kupenda maadili, yaani raia mwema ambaye anaweza kupinga jitihada za kusaka wahalifu, hata siku moja. [138]
mzima
Walisema baada ya safari ndefu ya siku 360 za pilika pilika, kukamilika na kuanza safari zingine ni lazima kwa mtu kujipongeza kwa kuvuka mabonde na milima ya mwaka mzima. [139]
na
VIONGOZI na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana waliachwa wakitafakari cha kufanya baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutupilia mbali rufaa ya mgombea wao kupinga kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wa Mbeya Vijijini. [140]
nafuu
MAHAKAMA ya Rufaa imetengua uamuzi wa Mahakama ya Ardhi uliowanyima fursa ya kurejea kwenye makazi ya asili wanakijiji cha Nyamuma wilayani Serengeti na kuwapa nafuu wakazi hao ambao kwa miaka zaidi ya saba sasa wamekuwa wakipigania kurejeshwa maeneo hayo. [141]
nalo
Kwa mfano, uzembe wa kutokujua au kuzingatia aina ya kosa analoshtakiwa nalo mtu, kwa mfano, kumweka mtu ndani kwa kosa ambalo kimsingi sio la jinai. [142]
nani
Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985 imetamka bayana ni nani anayetakiwa kushuhudia tamko la kisheria kwa wagombea ubunge," alisema Jaji Makame. [143]
nao
Tanzania ina wachezaji wazoefu na mastaa, lakini mimi nina vijana wengi ambao nataka wafanye kazi, nimetoka nao mbali ndio maana nawaandaa kuwa mabingwa wa hii michuano mwakani. [144]
nayo
Naamini kwamba kila mmoja wenu anaweza ndio maana nikamjumuisha kwenye timu yangu ya ushindi, hii timu niliyokuja nayo ni kikosi cha kwanza na ndio timu yangu bora zaidi kwa hiyo nategemea mambo makubwa. [145]
nchi
WAHADHIRI waandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kutumia nafasi yake ya uenyekiti wa umoja wa Afrika kuwashawishi viongozi wa nchi za Afrika kuunga mkono katika kupinga mauaji ya Wapalestina yanayofanywa na Israel katika ukanda wa Gaza. [146]
ndio
Jaji huyo alisema kwa kuwa katika kifungu cha 38 (3) kuna neno linaloonyesha kuwa hakimu wa mahakama ya mwanzo, wilaya na mahakama za hakimu mkazi ndio wanaopaswa kushuhudia tamko hilo la kiapo, ni dhahiri kuwa wakili hapaswi kushuhudia tamko mgombea ubunge. [147]
ndiyo
Pia kimewataka viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema kukubali makosa yao kuwa ndiyo yaliyosababisha kufanyika kwa makosa wakati wa kiapo. [148]
ndoa
ATCL iliwahi kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA), lakini baadaye serikali iliona ndoa hiyo haina manufaa na kuamua kuivunja miaka mitatu iliyopita. [149]
nia
Uamuzi wa jana wa mahakama unawapa nafuu kubwa wanakikiji hao ambao kwa miaka zaidi ya saba sasa wamekuwa wakipigania kurejeshwa katika makazi yao ya asili, lakini serikali ikionesha wazi kutokuwa na nia ya kuachia ardhi hiyo. [150]
nini
Huu ndio wakati muafaka ambao nawapa, nataka ushindi sitaki mniangushe, kila mmoja nataka acheze soka tushinde kwa vile kama mnavyoona kila mtu hapa anasubiri kuona Tanzania itafanya nini. [151]
nje
Wafuasi wa Chadema hawakuweza kusogelea hoteli ya Mount Livingstone wakati Jaji Makame akitangaza uamuzi huo kutokana na kuwepo na ulinzi mkali wa maafisa wa usalama wa Jeshi la Polisi na Askari wa Kutuliza Ghasioa (FFU) waliokuwa nje ya geti la hotel hiyo. [152]
nne
Akisoma mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Hezroni Mwankenja, Mganga alisema shtaka la kwanza hadi la nne yanamhusu Mramba na Yona peke yao. [153]
nyie
Kila mchezaji hapa ana kazi ya kufanya hapa, Watanzania wana imani kubwa na nyie na wanaamini mnaweza kufanya kazi kubwa, lakini mnachopaswa kufanya pia nyie ni kuthibitisha. [154]
nyingi
Nimesikia habari nyingi sana- ambazo watu wanazizungumzia siku hizi. [155]
nyinyi
Ni nyinyi wazee mnaohitaji picha za ngono. [156]
nyota
Simba imekwenda Zanzibar bila wachezaji wake nyota wakiwemo Henry Joseph, Kelvin Yondan,Deodratius Mushi Dida, Juma Jabu, Mussa Hassan Mgosi, Meshack Abel na Haruna Moshi Boban walioko timu ya taifa mjini Kampala. [157]
ombi
Hakimu Mwankenja alikubali ombi hilo. [158]
papo
Lakini kompyuta zinadai maamuzi ya papo kwa papo. [159]
pia
Mbali na uamuzi huo, serikali pia imeamua marekebisho ya mkataba wa uwekezaji wa Kampuni ya Reli (TRL) ili kuwapa Watanzania nafasi ya kuingia katika bodi ya wakurugenzi na kuwemo kwenye menejimenti. [160]
raia
Baada ya mchezo huo kocha wa Zanzibar, Badr el Din raia wa Misri alisema kwa sasa nategeneza timu ya kutwaa ubingwa mwakani, lakini nimefurahishwa na matokeo pamoja na kiwango tulichokionyesha kwa leo. [161]
saa
Jana Mramba na Yona walipanda kizimbani saa 5:20 na baadaye Wakili Mganga akaiomba mahakama Mgonja aunganishwe katika kesi hiyo. [162]
sana
Mechi yetu na Bara itakuwa ngumu sana, lakini nakwambia utaona mwisho wa siku, tutashinda na naahidi hivyo kwa vile ninajua timu zote mbili, Zanzibar hii siyo iliyopita. [163]
sasa
Siwezi kueleza chochote kwa sasa kwa sababu tunahitaji kufanya consultations (mashauriano)," alisema mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alipotakiwa kuzungumzia hatua inayofuata baada ya Jaji Makame kutangaza uamuzi huo. [164]
shaka
Hatua ya mgambo hao ya kuingia katika majumba ya watu na kufanya watakalo bila ya kuwa na hati ya upekuzi (search warrant), ambayo hutolewa na polisi, kinatia shaka ujuzi wao na utekelezaji wa kazi zao kwa kufuata maadili. [165]
shida
Wamba alisema kuwa utajiri wa madini na nishati ya uranium waliyonayo, imekuwa kivutio kikubwa kwa nchi za magharibi kuendelea kuwatumia watu kujitajirisha na huku wananchi wakiendelea kupata shida. [166]
si
Kwa kuwa tamko limesainiwa na mtu asiyehusika, ni dhahiri kuwa tamko hilo (la kiapo) si halali na ni sababu ya kuweka pingamizi iliyotajwa katika kifungu cha 40(1) (d) cha sheria ya uchaguzi Na. [167]
sio
Akizungumza jana katika mkutano wa wafanyabiashara wadogo wa Mkoa wa Dar es Salaam, alisema baadhi ya watu wanawalaghai wenzao kuwa serikali imewateua kusimamia ugawaji wa maeneo katika jengo hilo na kuanza kukusanya fedha jambo ambalo sio kweli. [168]
sisi
Walisema kitendo cha kuwaita kwenye kamati ya nidhamu na kuwatuhumu kuwa wao ndio wanaohamasisha watu kugoma wakati sisi wanafunzi ndio wanaowatuma kuwatetea, ni kuwakandamiza. [169]
sote
Wakati umefika kwa sisi Waafrika kuonesha mshikamano wetu wa kupiga vita unyama wanaofanyiwa Wapalestina kwani mapambano yanayofanywa na Wapalestina ni mapambano yetu kwa sababu sote tunaupiga vita Ubeberu", alisema Profesa Haruob. [170]
swali
Akijibu swali kuhusu muundo wa uongozi wa kampuni hiyo na sababu za kuajiri wafanyakazi wawili kutoka India ambao hawana taaluma ya kazi wanazofanya, Dk. [171]
tako
HE jamani, mambo ya nishani ya viatu na tuzo la tako yameleta ubishi mkubwa sana. [172]
tamaa
Hapa tutaangalia hali za kukatisha tamaa na matukio ya kutisha ya mwaka uliotawaliwa na uchaguzi uliokuwa umegubiwa na utata. [173]
timu
Enrigue Sagura wa kampuni hiyo kushiriki katika kikao na kuiongezea kampuni hiyo muda wa nyongeza wa miaka miwili kabla ya majadiliano ya timu ya wataalamu wa serikali. [174]
tu
Alisema kuwa kifungu cha 46, kipengele cha 6 cha Sheria ya Uchaguzi kinaruhusu mgombea tu kutoa malalamiko kwa tume kama anaona haridhishwi na mwenendo wa uchaguzi. [175]
tuna
Hawa wenzetu hata wakipoteza hawana hasara, lakini sisi tuna deni kubwa tunatakiwa tuionyeshe hii jamii ya Afrika Mashariki na Kati kwamba tunajua mpira, ndio maana tumekwenda CHAN wao wakashindwa. [176]
uchumi
ESTHER (siyo jina lake halisi), mtaalam anayeishi na kufanyakazi katika Mji Mkuu wa Zimbabwe, Harare ameandika matukio muhimu ya mwaka 2008 akielezea jinsi anavyopambana na maisha kwenye nchi hiyo ambayo uchumi wake umeanguka vibaya. [177]
udhalimu
Alisema kuwa, hii ni kwa sababu ya unyama na udhalimu walioufanya. [178]
umri
Wapo walionaswa wakiwapiga wananchi viboko hadharani bila hata ya kujali umri na hadhi yao katika jamii. [179]
utotoni
Utafiti huo umebaini kuwa chanzo kingine cha mimba za utotoni ni ngoma za usiku. [180]
uwezo
Jaji Projest Rugazia wa Mahakama ya Ardhi alitupilia mbali ombi hilo baada ya kuridhia pingamizi la awali lililowekwa na wajibu maombi kwamba mahakama hiyo haikuwa na uwezo wa kisheria kushughulika na shauri hilo. [181]
viapo
Lakini akaongeza kuwa Sheria za Viapo zinahusu viapo na matamko ya kisheria kwa ujumla. [182]
vikundi
Lakini jioni wananchi walikuwa wamekusanyika kwenye vikundi kujadili suala hilo baada ya kupata habari kuwa Chadema haitashiriki. [183]
vita
Profesa Haroub Othman wa chuo hicho, alisema umefikia wakati kwa Waafrika kuonesha mshikamano kupiga vita unyama wanaofanyiwa Wapalestina kwani mapambano yao ni mapambano ya Afrika kwa sababu wote wanapinga vita na ubeberu. [184]
wadau
Mapokezi hayo yaliyoanzia maeneo ya Msamvu nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, na kuongozwa na Kaimu mkuu wa mkoa wa Morogoro, Athuman Mdoe, mkuu wa wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu, Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Amir Nondo , mkurugenzi wa Manispaa, Raphael Ndunguru , viongozi wa Chama cha Soka MRFA pamoja na wadau mbalimbali wa soka mkoani hapa. [185]
wale
Shukuru Kawambwa alisema kuwa wafanyakazi wanaopaswa kuwajibishwa ni wale ambao walizembea wajibu wao, hivyo kuisababishia serikali hasara kubwa. [186]
walimu
Utafiti pia umebaini upungufu mkubwa wa walimu. [187]
wameua
Kama itathibitika wameua na wao wauawe. [188]
wana
Mtu huyo alisema kuwa chuo kilipopeleka majina ya wanafunzi hao NACTE, baadhi walionekana wana sifa na wengine kukataliwa kwa kutokuwa na sifa. [189]
watu
Tumegundua kuwa mapungufu yapo maana kuna watu ambao wanahusika katika kuhakikisha kuwa ndege za ATCL zinaruka," alisema Dk. [190]
wazee
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (Nec) Nape Nnauye, amekemea makundi ndani ya chama hicho na kuwataka wazee kutumia nafasi yao ya Kikatiba kuonya na kushauri ili chama kirudi katika misingi yake. [191]
wenyewe
Hapa sababu kubwa huwa ni raia wenyewe. [192]
wewe
Ni vizuri kuongea kutokana na tofauti zenu, na kujaribu kuzungumzia wenyewe mambo ambayo wewe unayo moyoni kuhusu mwenzio ili kwa wakati wake ajaribu kuchuja na kujifunza kukuridhisha. [193]
yako
Zungu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ilala, alisema mamlaka ya kusimamia jengo hilo yako katika bodi iliyoundwa na Meya wa jiji na hakuna mtu yeyote aliyekasimiwa mamlaka hiyo hata awadanganye. [194]
yao
Katika mabadiliko hayo kwenye hati ya mashtaka ya kesi hiyo namba 1200 ya mwaka 2008, Mramba ambaye ni mshtakiwa wa kwanza amepunguziwa mashtaka wakati Yona, ambaye ni mshtakiwa wa pili, na Mgonja ambaye ni mshtakiwa wa tatu, wanaendelea kukabiliwa na mashtaka yao ya awali. [195]
yetu
Tumesikiliza matokeo ya rufaa yetu ambayo Tume ya Taifa imetupilia mbali, tunahitaji muda wa kutafakari kwa undani. [196]
yeye
Maana ya tamko au msimamo huu wa sheria ni kwamba ni wajibu wa mwenye kufungiwa au kukimbia kuithibitishia mahakama kuwa kifungo au kizuizi alichowekewa hakikuwa na uhalali wa kisheria kwa kuwa yeye si mhalifu na hahusiki na kosa aliloshtakiwa. [197]
yote
Kawambwa alisema kuwa tayari serikali imefuta madeni yote ya ndani ya ATCL na imeridhia kutoa Sh3.3bilioni kama sehemu ya kuanzia katika kulisuka upya shirika. [198]
za
Alisema hoja ya pili ni kama Sheria za Viapo (Oaths and Statutory Declarations Act, Cap 34 R.E 2002 na Notaries Public and Commissioners for Oaths Act, Cap 12 E.R. 2002) zinaweza kutumika katika suala hili na kama wagombea walikuwa na muda wa kutosha wa kukamilisha fomu zao za uteuzi na kuziwasilisha kwa wakati. [199]
zenu
Zaidi nataka niwatakie mwaka mwema wenye baraka kwenu na kwa familia zenu, nataka pia niwakumbushe kuwa huu unaweza kuwa mwaka wa neema kwa watakao jishughulisha. [200]