Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-02-20
Mandhari
Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz
- aendako
- Maneno ya kule yangeondolewa na neno aendapo ilingerekebishwa na kuwa aendako. [1]
- aina
- Lakini pia walisema wazo la Rais Jakaya Kikwete kutaka vitabu vya kufundishia watoto katika Shule za msingi na sekondari viwe vya aina moja ni zuri. [2]
- akaona
- Mungu akaangalia akaona ni vyema. [3]
- alitoa
- Hakimu Msongo alitoa ruhusa ya siku mbili Februari 18 na 19 kwa ajili ya upande wa Jamhuri kumchukua mshitakiwa huyo na kwamba wakati wa upelelezi, mshitakiwa ataruhusiwa kuwa na mawakili wake binafsi. [4]
- ambako
- Mashahidi hao waliieleza mahakama kuwa washitakiwa hao walikwenda kuwaonesha mahali ambako mauaji hayo yalifanyika katika msitu huo,na baada ya ushahidi wao huo,waliiongoza mahakama kwenda katika eneo la tukio hilo katika msitu huo. [5]
- ambapo
- Uamuzi huo uliushangaza upande wa mashitaka ambapo mwendesha mashitaka wa serikali, Justus Mulokozi, alipinga uamuzi huo wa mshitakiwa kupewa dhamana kwa hati ambayo haikutimiza kiwango cha fedha kilichopangwa na mahakama. [6]
- ambavyo
- Na hii inabaki kuwa sababu ndoa nyingi zinaterereka kwa kuwa wanawake wanashindwa kujipendekeza na kuwanyenyekea waume zao kila siku kama vile ambavyo wengi wanafanya katika siku kama hii. [7]
- ambaye
- Akizungumzia suala hilo, Ali Issa ambaye aliteuliwa kukaimu nafasi ya Isaack, alikiri kuwa tayari ameshaanza kazi hiyo. [8]
- anasema
- Mtaita anasema vyanzo vya maji ya Mserereko kwa sasa vinazalisha asilimia 50 ya mita za ujazo 6,000 ambazo huzalishwa wakati wa hali ya kawaida na kuvifanya vyanzo hivyo kushindwa kuchangia asilimia 30 ya mita za ujazo zinazozalishwa na Moruwasa kwa wateja wake. [9]
- au
- Baada ya mawakili hao wa utetezi Jaji Masati alimpa nafasi kiongozi wa Jopo la mawakili wa serikali, Wakili wa kujitegemea Revocatus Mgaya Mtaki,kama ana pingamizi au maoni yoyote kuhusiana na maombi ya mawakili wa utetezi. [10]
- awe
- Maana ya kulea ni kumtunza na kumfundisha mtoto mpaka akue na aweze kujitegemea na awe na maadili mazuri. [11]
- badala
- Walimu pamoja na wizara inatoa zabuni kwa watu wasiokuwa na uwezo kwa sababu ya maslahi zaidi bila kujali ubora wa vitabu vitakavyozalishwa badala yake wanajali kupata cha juu katika kazi hiyo. [12]
- bali
- Wakati wa kusoma hati hizo wakili Ndusyepo hakutaja namba wala mahali iliko bali alitaja jina lililoko kwenye hati husika. [13]
- bonus
- Mwenyekiti wa kamati ya majadiliano ya chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Viwanda na Biashara (Tuico), Iddi Mbona, alisema uongozi wa NBC umeshindwa kulipa nyongeza ya bonus kwa wafanyakazi kama inavyoelezwa katika mkataba wa hali bora kazini. [14]
- bunge
- Kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri ya jiji, mbali ya wajumbe wengine pia kilihudhuriwa na Rais wa bunge la Afrika Balozi Gerturde Mongella ambaye miaka ya 1983 na 1984 alikuwa mwenyekiti wa tume ya serikali iliyojulikana kama Tume ya Mongella iliyofanya utafiti kuhusina na mauaji ya wazee vikongwenchini. [15]
- bungeni
- Sika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano, Samuel Siita aliwatangazia wabunge kabla ya kuahirishwa kwa bunge hilo kuwa, sababu kubwa iliyofanya hoja nyingi zisijadiliwe bungeni ni kutokana na sehemu kubwa ya masuala hayo yanashughulikiwa na vyombo vyingine vya sheria. [16]
- cha
- Alisema mshitakiwa atatakiwa kutimiza masharti ya dhamana ya kiasi kilichobaki cha Sh 54,417,344,800.23 endapo mahakama itaona kuwa hati hizo zina kasoro. [17]
- demokrasia
- Kiongozi au Chama kuzungumzia maoni ya mtu binafsi ni kuvunjavunja demokrasia, mtazamo na maoni ya mtu. [18]
- duni
- Sehemu ya tatu ni ile ya huduma kutowafikia watumishi wanaoishi na VVU, hasa wale watumishi wa kada za chini ambao mishahara yao ni duni na uwezo wa kujikimu katika hali ya kuwa na virusi hivyo ni mdogo, hususan kwa upande wa gharama za chakula na usafiri. [19]
- enzi
- Lakini ilikuwa dhahiri kwamba zile shule nyingi za watu binafsi enzi zile zisingeweza kufanikiwa hata kidogo. [20]
- es
- Habari zilizolifikia gazeti hili jana, zimesema kuwa uamuzi wa kumwengua Katibu Mkuu huyo, umefikiwa na kikao cha Kamati ya Utekelezaji kilichofanyika siku mbili kuanzia Jumanne chini ya Mwenyekiti wa umoja huo Masauni Hamad Masauni katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM zilizoko Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam. [21]
- eti
- Hatutaacha kuzungumzia suala hili nyeti la kuhujumu mali ya umma kwa vile eti sisi ni viongozi wa dini. [22]
- feki
- Sababu nyingine aliyoitoa Profesa Safari ni kuhusu suala la manunuzi ya vitabu vya maprofesa ambapo alisema kwamba serikali haitaki kutoa fedha kwa ajili ya kununulia vitabu badala yake wanakimbilia kununua vitabu feki kwa bei nafuu ili mradi wapate cha juu. [23]
- fulani
- Lakini kama wangekuwa na wafadhili ambao kwa kiasi fulani wangeweza kusaidia katika maandalizi, hakika aibu hii ya kutolewa mwanzoni kabisa mwa mashindano hayo isingetokea kila wakati kwa sababu wangeweza kufanya maandalizi mazuri. [24]
- gani
- Masuala kama ni kiasi gani cha fedha zinazopangwa kwa ajili ya huduma hizo, zinakwenda wapi, zinatumikaje na zinamfikaje mlengwa, kila mtumishi anapaswa kuyafahamu. [25]
- halifai
- Neno kunajisiwa limetumika vibaya na halifai katika muktadha huu kwani lina maana maalumu. [26]
- hao
- Wadhamini hao walikamatwa majira ya saa 6 mchana na kuwekwa mahabusu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi walipoachiwa saa 10:47 jioni. [27]
- hapa
- Mtukufu Jaji,kama nilivyoomba jana mahakama yako inipe nafasi ya kwenda kuonana na mshitakiwa wa 11 kama anaweza kufika mahakamani kutoa ushahidi,nilifanya hivyo,lakini hali yake bado hairidhishi kuja kutoa ushahidi mahakamani hapa leo wala kesho. [28]
- hapo
- MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana ilishindwa kusikiliza ushahidi wa mshitakiwa wa 12 DC. Rajabu Bakari baada ya mshitakiwa wa 11 DC Rashid Lema kushindwa kufika mahakamani hapo kwa ajili ya kutoa ushahidi wake. [29]
- hati
- Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Tabu Mzee alisema kuwa, walipokea hati kwa ajili ya kumkamata Liyumba na wadhamini wake lakini hawajafanikiwa kumpata Liyumba. [30]
- hicho
- Mwenyekiti huyo alitaja sababu zilizokwamisha mkutano huo kuwa pamoja na kitendo cha uongozi wa benki kuwahamisha viongozi wa Tuico, kwenye matawi yao bila kupata ushauri na uongozi wa chama hicho makao makuu. [31]
- hii
- Alisema kwa mujibu wa taratibu za mahakama awamu hii ilikuwa inashia leo na kwamba kisheria hawawezi kuendelea. [32]
- hiki
- Akizungumza katika eneo la tukio Kiongozi wa bendi hiyo Maaalim Mwihidini Gurumo aliwataka wapenzi na mashabiki wa bendi hiyo kuwa watulivu katika kipingi hiki kigumu huku uongozi wake ukitafakari namna na kulikabili pengo hilo ambalo alidai ni kubwa mno. [33]
- hili
- Sisi kama serikali tunashangaa, tutakaa kujadili suala hili na kulitolea maamuzi kupitia ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali," alisema Mulokozi. [34]
- hivi
- Akizungumza na Mwananchi hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Bushiri alisema kuwa klabu nyingi visiwani humo hazina vitega uchumi wala wafadhili hali inayosababisha timu hizo kushindwa kufanya maandalizi ya kutosha katika michuano ya kimataifa. [35]
- hivyo
- Hata hivyo alikiri juu ya kuandamwa na tuhuma hizo na kusema kuwa, waliozianzisha walikuwa na tafsiri tofauti. [36]
- hizi
- Ukimwi kupata huduma hizi na hivyo kurefusha maisha yao na kuendela kuwa nguvu kazi ya taifa. [37]
- hovyo
- Sasa huko wanapotupeleka bila hata ya kutuwekea huduma kama hizo wanategemea nini zaidi ya uharibifu wa mazingira kwa kujisaidia hovyo. [38]
- huduma
- Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Leodegar Tenga alisema mbali na fedha hizo zilizochangwa, kamati hiyo imeshatumia kiasi cha milioni 250 katika kuisaidia huduma mbalimbali za timu ya taifa. [39]
- huko
- Tukumbuke kuwa msomaji wa magazeti ni mwananchi wa kawaida akiwemo huyo wa darasa la saba huko kijijini au mitaani ambako hakuna kamusi za Kiswahili. [40]
- huu
- Liyumba na Kweka walipandishwa kizimbani Januari 27, mwaka huu kwa tuhuma za kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh 221 bilioni. [41]
- huwa
- Wakati mwingine huwa nakata tamaa kutokana na ukosefu wa fedha kwani zana za sanaa nazitoa mbali na kwa kwa bei kubwa. [42]
- huyo
- Wakati akitoa uamuzi wa dhamana ya Liyumba, Hakimu Msongo alisema mshitakiwa huyo atakuwa nje kwa dhamana ya Sh 882 milioni wakati mahakama ikijiridhisha na hati nyingine zilizopingwa na upande wa mashitaka. [43]
- huyu
- Ushindi wa mwanamitindo huyu si tu kwa manufaa yake binafsi bali ameweza kuitangaza Tanzania kimataifa hasa kwa upande wa utalii wetu ameweza kutuwakilisha vizuri. [44]
- ibilisi
- Tunaona nchi nyingine zikielekea kukutana na ibilisi lakini sisi ni tofauti. [45]
- ife
- Siseme siku hii ife lakini ninachotaka kusema mimi; hivi kweli hatuwezi kusherehekea siku hii kila siku ya maisha yetu kwa kuhuisha upya ndoa zetu na waume zetu, ila kila siku iwe siku ya wapendano!? Kwa sababu ukweli utabaki kuwa wanaopendana ni wale waliooana. [46]
- ikawa
- Ikawa asubuhi ikawa jioni siku ya kwanza. [47]
- ikiwa
- Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wakuu wa Wizara ya elimu na ufundi na taasisi zake nchini ikiwa ni mfululizo wa mkutano wa kutathimini utendaji wa serikali ya awamu ya nne katika miaka mitatu iliyopita. [48]
- ila
- Haileweki kumchojoa ni kufanya nini ila msomaji anaweza kubuni maana ya neno hilo. [49]
- ile
- Pale Chausiku alipomchojoa ile bukta yake na kuanza kuutemebeza ulimi wake wa moto. [50]
- ili
- Baada ya kumtuimua Isaack, nafasi ya Kaimu Katibu wa UVCCM, inashikiliwa na Ally Issa, ili kupisha uchunguzi huru dhidi ya tuhuma zinazomkabili. [51]
- ina
- Anasema Moruwasa kwa kushirikiana na Wizara ya Maji na Umwagiliaji ina mpango wa kuboresha miundombinu yake na kuongeza uzalishaji wa maji chini ya Mradi wa Millennium Challenge Goal (MCC). [52]
- inatarajia
- Mamlaka hiyo inatarajia baada ya mradi huo kukamilika uzalishaji utaongezeka hadi kufikia mita za ujazo 33,000 kwa siku. [53]
- ingeandikwa
- Kwa hiyo ingeandikwa, namna ya kumdhibiti na siyo namna na kumdhibiti. [54]
- ingefaa
- Kwa hiyo ingefaa iandikwe, Uhuru wa habari umechafuliwa au umeharibiwa. [55]
- iwe
- Nidhamu, nidhamu, nidhamu, hicho ndio kitu kikubwa sana kwenu, nidhamu ndani ya uwanja na nje, heshimu kila mmoja, wasikilizeni waamuzi, usibishane na mwamuzi, nahodha ndiye anayepaswa kuongea na mwamuzi pale anapokosea ili kuepusha kadi za mara kwa mara, tupo ugenini hivyo nidhamu lazima iwe mbele," alihasa. [56]
- iweje
- Sasa jiulize, iweje usafiri wa mabasi unaweza kukukwaza mtu? Mwandishi alikuwa na maana ya kumtatiza au kumchanganya kimawazo. [57]
- je
- Tunaomba serikali isitishe mpango huu na kufanya uchunguzi wa kina, kwani iwapo serikali itavunja na baadaye kubainikwa kuwa nyumba ya mganga huyo aliyevunjiwa siyo mhusika hajihusishi na ramli na anastahili kurejeshewa leseni, je atarejeshewa fidia? alihoji Mwenyekiti huyo. [58]
- jengo
- Kwa mujibu wa habari hizo, Isaak anatuhumiwa kuingia mkataba na wafanyabiashara wa jengo la Makao Makuu ya UVCCM bila kuijulisha Kamati ya Utekelezaji na Baraza Kuu la umoja huo jambo ambalo ni kinyume na utaratibu. [59]
- juu
- Wakizungumza nje ya mahakama, mawakili hao walisema wataijadili na ofisi ya mwanasheria mkuu itatoa maoni yake juu ya suala hilo. [60]
- juzi
- Alisema hayo juzi katika kipindi maalumu kilichorushwa hewani na Televisheni ya Channel 10 ya jijini Dar es Salaam saa 3:30 usiku. [61]
- kabla
- Kwa mujibu wa kanuni za UVCCM, kabla ya mikataba kutiwa saini, inatakiwa kupitia kwenye Kamati ya Utekelezaji, Baraza Kuu na Baraza la Wadhamini. [62]
- kadhaa
- Mashabiki kadhaa kutoka Kenya na Watanzania wachache walijitokeza kuilaki Stars huku baadhi ya wenyeji wa hapa wakionyesha kuifurahia kwamba wamewahi kusikia taarifa zake jinsi ilivyoitesa Cameroon ambao wao ni wapinzani wao na kamwe hawapendi kufungwa na timu hiyo au Nigeria. [63]
- kali
- Victor Mwambo ndiye aliyeanza kuwainua vitini mashabiki wa Mwanza dakika ya tisa ya mchezo baada ya kuachia fataki kali lililojaa wavuni moja kwa moja na kuwaacha mabeki wa Nyerere wakishangaa. [64]
- kamwe
- Baada ya kuwasili, Stars iliyopitia Nairobi, Kenya na Douala, Cameroon katika saa ya zaidi ya saa saba, Kocha wake Marcio Maximo alisema wana imani kubwa ya kufanya vizuri ingawa alisisitiza suala la ushindani litakua ni kubwa na kamwe hawaogopi. [65]
- kasi
- ASKOFU wa Kanisa la Pentekoste lililoko Ubungo Kibangu Dar es Salaam, Antony Lusekelo, amekemea ufisadi na mauaji ya albino na kuitaka Serikali iongeze kasi kukabiliana na matatizo hayo kwa kuwa yanahujumu uchumi. [66]
- kata
- MAKAMU Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu Thomas Darabe amewashutumu viongozi wa kijiji cha Qangded katika kata ya Baray kufuatia matumizi mabaya ya Sh33 milioni za mradi shirikishi wa maendeleo ya kilimo nchini (PADEP). [67]
- kati
- Tanzania ni kati ya timu zinazoshiriki fainali hizo ikiwa Kundi A pamoja na wenyeji Ivory Coast, Zambia na Senegal. [68]
- kiada
- BAADHI ya Maprofesa na Wahadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaan (UDSM) wamesema wengi wanashindwa kutunga na kuandika vitabu vya kiada kwa sababu ya kukithiri kwa ufisadi katika sekta ya elimu. [69]
- kiafya
- Msafiri aliyasema hayo mbele ya Jaji wa Mahakama ya Rufaa Salum Masati,baada ya kuileza mahakama kuwa hali kiafya ya DC. Lema haimruhusu kufika mahakamani hapo kutoa ushadi na akaiomba mahakama iahirishe shauri hilo hadi hapo baadaye. [70]
- kikamilifu
- Hata hivyo, tunadhabni kwamba watendaji hao walikuwa na wasimamizi wao wakati wa kugawa chakula hicho, ambao walitakiwa kufuatilia kikamilifu utekelezaji wake. [71]
- kile
- Habari za kuahirishwa kwa kesi hiyo zilianza kusikika mapema jambo ambalo lilianzisha mjadala wa chini kwa chini miongoni mwa wasikilizaji na hata wanahabari,ambao walikuwa wakisubiri kwa hamu sana kumuona mshitakiwa huyo wa 11 na kumsikiliza kile ambacho angekisema katika ushahidi wake wa utetezi. [72]
- kingine
- Kikundi kimoja kitagombana na kingine, mtu na mtu kama ilivyo katika maeneo haya kwa hivi sasa. [73]
- kisha
- Jaji Masati alikubaliana na maelezo ya Wakili Msafiri kisha akampa nafasi wakili wa Mshitkwa wa 13 DC. Festus Gwabisabi,Rongino Myovela kwa ajili ya kumuongoza mshitakiwa huyo kuanza kutoa ushahidi wake. [74]
- kocha
- Akizungumza jijini jana kocha Muhesa alisema ana uzoefu mkubwa na timu hiyo hivyo hajaona timu yoyote ambayo itaweza kumzuia asitimize malengo yake. [75]
- kufanya
- Mafisadi wanadidimiza uchumi kwani fedha na mali wanazochukua zingeweza kuzalisha na kufanya mambo ya kimaendeleo, alisema. [76]
- kuhusu
- Tulishauandikia uongozi wa NBC kuhusu mkutano huo, lakini jana uongozi huo haukutokea,alisema Mbona. [77]
- kujuzwa
- Wanafunzi wa Mzizima Aga Khan walitembelea na kujuzwa Uhuru Publications Limited (UPL). [78]
- kule
- Dereva alikuwa makini kuendesha gari huku akiwa amekaza macho kuelekea mbele ya kule aendapo. [79]
- kulea
- Pamoja na kulea ladha, viungo vinasaidia pia katika tiba. [80]
- kumdhibiti
- Ilielezwa kuwa wabunge wa CCM walikuwa wakitafuta msimamo wa pamoja wa namna na kumdhibiti Dk Slaa. [81]
- kuna
- Hii ni sehemu tu ya shughuli za ukarabati wa jengo na wala sikumpangisha mtu, alisema Isaack nakubainisha kuwa katika shughuli za ujenzi zinazofanyika katika eneo hilo, kuna wanaokarabati jengo na wanaojenga eneo la wazi nyuma yake. [82]
- kundi
- Mashabiki hao wameonyesha kuishabikia Tanzania na kutaka iifunge Senegal wakitamba wanataka kupona ikosonga hadi nusu fainali pamoja na Ivory Coast zikitokea kundi A ambalo timu nyingine ni Zambia na Senegal. [83]
- kupima
- Vilevile, unaelezea umuhimu wa kupima na kupata ushauri kama haki ya kila mtumishi, na itolewe bure katika hospitali zinazochaguliwa na waajiri. [84]
- kupona
- Vitendo vya kutojali utu wa mtu na kusisitiza maslahi binafsi, vitatupeleka pabaya kwani njia ya watu wanyonge kupona ni nyembamba sana , alisema. [85]
- kusimamia
- Viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia elimu ya watoto wetu ndio waliovuruga. [86]
- kutolewa
- Hamu hiyo inatokana na ushahidi uliowahi kutolewa mahakamani hapo na mashahidi wa upande wa mashitaka ambao waliieleza mahakama hiyo kuwa washitakiwa wa 11 na wa 12 ndio walioeleza ukweli wa mauaji ya wafanyabaishara hao mahali na jinsi yalivyofanyika. [87]
- kuuza
- GAZETI hili jana lilichapisha habari kuhusu maafisa watendaji kata waliosimamishwa kazi na Halmashauri ya Wilaya ya Same, mkoani Kiliomanjaro kwa tuhuma za kuuza na kukiuka taratibu za kugawa mahindi yaliyotolewa na serikali kwa ajili ya watu walioathirika na njaa katika eneo hilo. [88]
- kwake
- Mkuu wa Wilaya ya Karatu Methew Sodoyek alipoulizwa kwa njia ya simu alisema ni kweli tatizo hilo lilifika mezani kwake na liliundiwa kamati kuchunguza na watakaobanika kuhusika hatua za kisheria zitachukua mkondo wake. [89]
- la
- Baada ya maelezo hayo, Hakimu Msongo aliahirisha kesi hiyo hadi leo saa 8 mchana kwa kuwa jalada halisi la kesi hiyo limeitwa mahakama kuu na kuwataka wadhamini hao wafike muda huo. [90]
- lake
- Lakini kama nilivyosema mwanzo tunajua kilichotuleta huku na kila mtu anajua jukumu lake. [91]
- leseni
- Mmoja wa mawakili wanaomtetea Liyumba, Hudson Ndusyepo alisoma hati na leseni za makazi kwa maeneo ambayo hayajapimwa, lakini upande wa mashitaka ulikubali hati moja ambayo ni ya nyumba ya Liyumba iliyoko Mbezi Juu yenye thamani ya Sh 882 milioni. [92]
- lina
- Kundi B lina timu za Ghana, Libya, Zimbabwe na DR Congo ambazo mbili zitavuka hadi nusu fainali na kucheza timu mbili za kundi A kutafuta mbnili ambazo zitasonga fainali. [93]
- lipo
- Tatizo lipo kwenye uvunjaji wa nyumba zao, jambo hili halina sababu ya maana ambayo itasaidia kupunguza mauaji haya. [94]
- mabasi
- Kuna jambo ambalo kwa muda mrefu lilikuwa likinikwaza hasa kuhusu usafiri wa mabasi. [95]
- madudu
- Ni wazi kwamba serikali imeshindwa kuwasilisha masuala hayo mbele ya bunge kwa kuogopa moto ambao unaweza kuibuka na kutokana na madudu yaliyopo, katika mikataba hiyo. [96]
- magofu
- Akaona kwamba watoto wengi walikuwa wanakufa hata kabla ya kufika kwenye magofu yale yaliyoitwa shule. [97]
- makao
- Isaack alieleza kuwa katika shughuli za ukarabati wa jengo la UVCCM makao makuu, baadhi ya mafundi waliweka vifaa katika chumba kimoja cha jengo hilo na baadhi ya wanachama wakatafsiri kuwa wamepangishwa. [98]
- makini
- Ameitaka Serikali kushughulikia matatizo hayo kwa makini zaidi kulikomesha lisiendelee kudidimiza uchumi wa nchi. [99]
- manabii
- Na ili kuthibitisha kwamba wanene wanafuata njia ya kweli, wako manabii wetu ambao wameunganisha mimbari na jukwaa. [100]
- mapungufu
- Lakini ukweli ni kwamba utelekezaji wake una mapungufu makubwa. [101]
- mapya
- Tangu wakati huo, watu wengi walianza kupata shauku ya kupima na kujua hali yao ya afya na pia kuelewa kwa kina kuhusu ugonjwa huo na namna ya kujikinga ili kuzuia maambukizo mapya. [102]
- mara
- Wakati mjadala huo ukiendelea chini kwa chini,mara mawakili wa pande zote waliingia katika chumba cha mahakama na kuvaa majoho yao hali iliyoashiria kazi kuanza,hivyo kuwafanya wasikilizaji kujiweka tayari. [103]
- mashindano
- Akizungumza na Mwananchi jana Katibu Mkuu wa chama cha mchezo huo hapa nchini Issa Mtalako alisema mashindano hayo makubwa yameandaliwa na Shirikisho la dunia la mchezo wa meza (ITTF). [104]
- matatu
- Baadhi ya wasomi waliozungumzia suala hilo ni Profesa Abdallah Safari ambaye alisema kwamba maprofesa wanauwezo wa kutunga vitabu, lakini kuna matatizo makubwa matatu yanayosababisha wasipate mwamko wa kutunga vitabu hapa nchini. [105]
- mavazi
- Huyu ni msanii ambaye utengenezaji wake wa mavazi ya kisanii ya manyoya ya ndege vimempa umaarufu mkubwa. [106]
- mayowe
- Kwa mfano, mwandishi ameandika, Ghafla Mwajuma aliguta mayowe yaliyomfamya Kitenga kugeuka haraka nyuma na kumwangalia yule msichana. [107]
- mazuri
- TAIFA Stars jana iliwasili mjini Abidjan na kupewa mapokezi makubwa na wenyeji hali iliyofanya wachezaji waseme kuwa wana deni kubwa la kuonyesha uwezo wao baada ya kuanza na mapokezi mazuri kutoka kwa wenyeji wao. [108]
- mbele
- Kabla ya wadhamini hao kuachiwa waliingizwa mahakamani saa 10:30 jioni mbele ya Hakimu Mkazi Hadija Msongo. [109]
- mbinu
- Amekitaka Chama cha Soka visiwani Zanzibar (ZFA), kutafu mbinu mbadara za kuweza kuzisaidi timu za visiwani humo kupata wafadhili kwa ajili ya manufaa ya soka la Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. [110]
- mdogo
- Kwanza ni uelewa mdogo au kutokuwepo uelewa kabisa kwa watumishi wa serikali kuhusu waraka huu. [111]
- mgawo
- UKAME mkubwa ulioikumba Manispaa ya Morogoro umesababisha uhaba mkubwa wa maji, hali iliyoilazimu Mamlaka ya Majisafi na Majitaka ya Manispaa hiyo (Moruwasa) kutangaza mgawo mkubwa wa maji kwa wateja wake. [112]
- mimi
- Hiyo ndiyo iliyokuwa chachu ya mimi kuipenda sanaa hiyo. [113]
- miungu
- Ni wapendwa wa Mungu, ni wapenzi wa Mungu, ni miungu kabisa na sisi. [114]
- mjini
- Darabe ambaye pia ni diwani wa kata ya Baray kwa tiketi ya Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), aliyasema hayo jana kwa waandishi wa Habari katika ofisi za wilaya ya chama chake zilizopo mjini hapa. [115]
- mno
- Tunakwenda Ivory Coast kusaka ushindi tu, acha kucheza na jukwaa 'mashabiki' sawa, wanakufurahia, lakini unajisahau mno, cheza mpira kwa manufaa ya timu yako. [116]
- mradi
- Alisema kutoa maoni ni haki ya kila mtanzania ambayo amepewa kikatiba ili mradi asivunje sheria, na kuongeza kuwa Kitine ametumia haki yake ya kikatiba. [117]
- mwa
- Katika ushahidi wao mashahidi hao ambao waliieleza mahakama kuwa walikuwa ni miongoni mwa wapelelezi wa timu iliyoundwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jeneral (IGP) Saidi Mwema ndio waliowahoji washitakiwa hao wawili na kwamba waliwaeleza ukweli kuwa wafanyabiashara hao walikamatwa wakiwa hai na kwenda kuuliwa katika msitu wa Pande ulioko Mbezi Luis. [118]
- mwenendo
- Gaudioz Ishengoma: Mtukufu Jaji nami naunga mkono hoja na naomba tupatiwe mwenendo wa shauri hili. [119]
- mzima
- Lakini kinachokusudiwa ni mfumo mzima wa kupata madini. [120]
- mzuri
- Akizungumza na Mwananchi jana katika hoteli ya Regency, Msasani, Msekwa alisema "Sioni kama ni utaratibu mzuri kutolea maoni yaliyotolewa na mtu mwingine. [121]
- na
- MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeagiza Mkurugenzi wa zamani wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba aliyeachiwa kwa dhamana siku tatu zilizopita akamatwe pamoja na wadhamini Wadhamini wake ambao ni wafanyakazi wa BoT Benjamin Nduguru (mhasibu wa benki hiyo) na Agaterus Oto (afisa usalama wa ndani wa benki hiyo) walikamatwa jana na kuachiwa muda mfupi baadaye, lakini Liyumba hakupatikana. [122]
- nao
- Wakili Msafiri: Mtukufu Jaji,kwa jinsi nilivyozungumza nao kuna maneno ambayo ni lazima kwanza mshitakiwa wa 11 ayatamke kwa kinywa chake ndipo mshitakiwa wa 12 aweze kutoa ushahidi wake. [123]
- nayo
- Double O, Sambruma na baadaye Juwata iliyokuja kuwa OTTU sasa Msondo Ngoma ambayo aliyodumu nayo mpaka mauti yalipomkuta. [124]
- ndivyo
- Hivyo ndivyo ilivyo pia kwa Ramadhan Mchemba (28), maarufu kwa jina la Lovii Lovii. [125]
- ndiyo
- Mambo haya ndiyo yaliyosababisha wadau wa elimu nchini kupigia kelele wakitaka utulivu katika mfumo wa elimu, urejeshwe kwa kuweka mitaala inayoeleweka badala ya hali ya sasa. [126]
- ndoa
- Naye Mshauri Nasaha wa Angaza, Peace Kayoza anasema kuwa kampeni hiyo ya upimaji kwa wapenzi wanaoshiriki kitendo cha ndoa, imefanikiwa kwani siku ya Valentine pekee walifanikiwa kupima watu 50 katika kituo cha Angaza kilichopo Amref, Dar es Salaam pekee. [127]
- ndugu
- Katika kesi hiyo Zombe na wenzake wanatuhumiwa kuwaua kwa makusudi wafanyabiashara watatu wa madini Sabinus Sabinus Chigumbi maarufu kama Jongo na ndugu yake Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe Juma Ndugu,dereva teksiManzese jijini Dar es Salaam. [128]
- ng
- Hati nyingi tulizoziangalia zina mali zisizodumu kama kuku, ngombe na mbuzi na hazimtambulishi mtu aliyefanya uthamini, hakuna hata mihuri tuna wasiwasi zisije zikawa za mitaani," alisema Mulokozi. [129]
- ngono
- Ni kitendo kibaya anachoweza kufanyiwa mtu (cha ngono) bila ridhaa yake. [130]
- ngozi
- Akitangaza uamuzi huo na nakala zake kusambazwa jana kwa vyombo vya habari Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Clement Mabina aliitaka Serikali kusitisha mpango huo mpaka utakapofanyika uchunguzi wa kutosha juu ya wahusika halisi wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). [131]
- nia
- Alisema naamini timu yangu itafanya vizuri kwenye michuano hii kwa kuwa tulifanya maandalizi ya kutosha kwa nia ya kuibuka mabingwa. [132]
- ningewapa
- Siku ya wanafunzi kuingia katika hizi shule ningewapa mtihani. [133]
- nini
- Jaji:Ni kwa nini tusiendelee na mshitakiwa wa 12? Alihoji Jaji Masatti baada ya Wakili Msafiri kuomba kesi hiyo iahirishwe kutokana na DC Lema kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi. [134]
- noti
- Nasikia hivi karibuni watawaomba waheshimiwa wapepee noti zao za posho za mipasho huko makalio makuu ili kuthibitisha kwamba na wao wanaelekea mbinguni potelea mbali kama sisi tusio na noti za kupepea tunafuata njia nyingine. [135]
- nusu
- Stars imewasili kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Felix Houphoet Boigny jijini hapa saa tisa na nusu ikiwa ni saa tatu nyuma kwa saa za Tanzania na kupata mapokezi yaliyoongozwa na msafara wa askari wawili wenye pikipiki kukatisha jiji la hadi kwenye hoteli ya Golf waliyopangiwa kilomita takribani 10 kutoka katikati ya jiji. [136]
- nzuri
- Haijawahi kutokea dunia kuona uzuri wa bajeti unatangazwa kwa kutumia mamilioni ya fedha wananchi kutuma watu mikoani kushwishi wananchi waione ni nzuri. [137]
- pia
- Wakili wa DC Lema,ambaye pia ni wakili wa DC.Bakari,Denis Msafiri aliieleza mahakama kuwa DC. Bakari hawezi kutoa ushahidi wake kabla ya DC. Lema kwa kuna maneno ambayo ni lazima DC. Lema ayatamke kwanza kwa kinywa chake ndipo DC. Bakari aweze kutoa ushahidi wake. [138]
- pili
- Katika hatua nyingine mahakama hiyo imekubali upande wa Jamhuri kumchukua mshitakiwa wa pili, Deograthias Kweka kwa ajili ya upelelezi na kwamba upelelezi ufanyike wakati wa saa za kazi. [139]
- ramli
- Akielezea tamko hilo Mwenyekiti wa Chama hicho tawala mkoa, alisema hawana pingamizi na ufutaji wa leseni za waganga wa jadi kwa vile ni njia sahihi ya kuchuja na kusajili wapya na kwamba watakaobainika kuwa wanapiga ramli ambazo ni chanzo cha mauaji haya basi wanapaswa kufutiwa leseni zao kabisa. [140]
- sana
- DC.Lema na DC. Bakari ni mashaidi muhimu sana katika kesi hiyo kwa kuwa kutokana na ushadhi uliotolewa mahakamani hapo na shahidi wa 30 Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tabora ACP Mmari na shahidi wa 36, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Signey Mkumbi kutoka makao makuu ya polisi. [141]
- sauti
- Maana ya kuguta ni kuita kwa sauti ya juu au kupiga kekele. [142]
- sawa
- Amesema yeye akiwa Kiongozi wa CCM hawezi kujadili maoni ya binafsi ya mtu kwani ni sawa na kuingilia haki yake. [143]
- sera
- Kilichoshuhudiwa na jamii, kwa kile kilichoonekana kama huduma na sera ya elimu kubinafsishwa, ni kila shule kujiamulia, siyo tu mitaala na vitabu vya kiada, bali hata malengo ya kila shule yakawa tofauti. [144]
- sharti
- Ili iwafikie wahitaji, sharti waigharimikie kulingana na kiwango wanachohitaji kukisomea. [145]
- shule
- Juzi,akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Rais Kikwete aliwashambulia maprofesa nchini kwa kushindwa kutunga vitabu vya kusoma wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na kuwataka waamke ili kuisaidia jamii. [146]
- si
- Aliongeza kuwa kwa maoni yake binafsi CCM haitazungumzia maoni ya mtu binafsi na wala si utaratibu mzuri kwa viongozi kuzungumzia na kutolea kauli maoni ya watu. [147]
- sindano
- Anasema kuwa katika kufuma manyoya hayo, hutumia kamba na sindano kubwa za mkono na humchukua wakati mwingine miezi kadhaa kukamilisha kazi yake. [148]
- siyo
- Hiyo siyo kweli. [149]
- soka
- Maximo alisema kila mchezaji inampasa kujua kuwa amekwenda Ivory Coast kushindana si kucheza soka la kufurahisha mashabiki hivyo kila mchezaji ajitume kwa bidii na kuipigania taifa lake wafike fainali. [150]
- somo
- Kwanza jamii ilishuhudia baadhi ya masomo muhimu yakiondolewa katika mfumo wa ufundishaji shuleni na kufanywa ya ufundi halafu mengine yakaunganishwa kuwa somo moja. [151]
- tamaa
- Wakizungumza jana na Mwananchi kwa nyakati tofauti, wasomi hao walisema wana uwezo wa kutunga vitabu vingi na vyenye ubora kulingana na elimu ya Tanzania, lakini rushwa inawakatisha tamaa ya kutunga vitabu. [152]
- tatizo
- Sababu inayofanya serikali ishindwe kutatua tatizo hilo ni suala la ufisadi uliozagaa serikalini na taasisi zake kwani kila kukicha wanawaza maslahi binafsi katika zabuni za utungaji wa vitabu, alisema Profesa Kanywanyi. [153]
- tena
- Baada ya kusilikiza hoja za pande zote hizo,Jaji Masatti aliridhia hoja na maombi ya mawakili hao wa utetezi na hivyo kuahirisha kesi hiyo hadi hapo itakapangwa tena na msajili wa mahakama. [154]
- tishio
- Ufisadi kwenye madini ya dhahabu sasa ni tishio. [155]
- trekta
- Mungu akaagiza, trekta ziwepo. [156]
- tu
- Kwa sasa nimetoka tu kidogo ofisini niko maeneo ya Kariakoo, alisema Issack wakati akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu. [157]
- uendeshaji
- Nyingine ni uendeshaji usioridhisha wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), na utendaji wa kazi usioridhisha wa Kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services (Ticts)) na taarifa kuhusu uendeshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL). [158]
- uhakika
- Shaka lina maana ya wasiwasi kutokuwa na uhakika na kitu. [159]
- ujazo
- Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na wataalamu wa Moruwasa, kiwango cha maji kinachozalishwa na mamlaka hiyo kimeshuka kutoka mita za ujazo 25,000 hadi kufikia 22,000 kwa siku kutoka katika vyanzo vyake vyote. [160]
- ukame
- Mgawo huo ulioanza Januari 6, ulitokana na vyanzo vya maji ya mserereko vya Mambogo, Vituli, Kigurunyembe, Mgolole na Bwawa la Mindu kupunguza uzalishaji wake, huku vyanzo vingine vikionekana kukauka kabisa kutokana na ukame. [161]
- ukata
- Naam! Sisi maskini tutakatika na ukata tu hata baada ya kukata roho lakini matajiri wataukata kama walivyoukata hapahapa. [162]
- umma
- Askofu huyo amewataka mafisadi, wauaji wa albino na wezi wa rasilimali za umma, kujishusha na kumgeukia Mungu, kabla laana haijashuka juu yao. [163]
- una
- Nape alidai kuwa baraza hilo na kumtaka mwenyekiti wake, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiuzulu, kwa madai kuwa mchakato wa ukarabati wa jengo hilo una harufu ya rushwa. [164]
- uongozi
- BAADHI ya wafanyakazi wa Benki ya NBC, wametishia kuupeleka mahakamani, uongozi wa benki hiyo kwa tuhuma za kushindwa kutekeleza madai yao. [165]
- upya
- MGOGORO upya unafukuta ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapiduzi (UVCCM) baada ya Kaimu Katibu wake Mkuu, Isaack Francis, kuenguliwa kwenye madaraka kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali na matumizi mabya ya madaraka. [166]
- utu
- Kuhusu mauaji ya albino, askofu Lusekelo alisema kunahitajika jitihada za makusudi kukomesha vitendo hivyo kulinda utu wa binadamu. [167]
- uzazi
- Kuna makabila kama Wachaga, ambayo akina mama hawapewi nafasi kubwa kuzungumzia suala la afya ya uzazi. [168]
- vazi
- Mwenyewe anasema kwamba pia ni mahiri wa kufuma vazi la chui kwa kutumia katani na mtu atakayelivaa akafanana na mnyama huyo. [169]
- vita
- Mara kadhaa nimekuwa nikizugumza kwamba vita kuu ya tatu ya dunia itakuwa ni ya kugombea maji. [170]
- vya
- Baada ya kesi hiyo kuahirishwa,wananchi waliokuwa wamefika mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo walionekana wamejikusanya vikundi vikundi katika viwanja vya mahakama hiyo huku kila mmoja akiwa na maoni yake kuhusiana na hatua ya kesi hiyo kuahirishwa hasa juu ya hatima ya ushahidi wa mshitakiwa wa 11 ambaye hali yake ni mbaya kiafya kutokana na maradhi yanayomkabili. [171]
- vyema
- Ndiyo maana sisi tumetumia kipindi hiki kuhamasisha wapenzi kupima ili kujua afya zao, ni vyema kujua hali ya afya zao kwa kupima wote, kwani hunufaika kwa kujua nini wafanye ili kujilinda. [172]
- wadau
- KUANZIA mwanzoni mwa miaka ya 1990 wadau wa elimu nchini wamekuwa wakilalamikia mambo mengi yaliyoachwa yajiendeshe bila kudhibitiwa. [173]
- wako
- Hatuna nia ya kuwatetea watuhumiwa hao, bali kwa kufuata misingi ya uwajibikaji, waliokuwa wanasimamia utwekelezaji mpango wa kugawa chakula kwa niaba ya halmashauri, walitakiwa kufutilia kwa karibu wakiwemo madiwani ambao wako karibu nao. [174]
- wakulima
- Mbali ya tatizo hilo kusababishwa na uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji ya mserereko, sababu nyingine inayoelezwa na Mkurugenzi huyo wa Moruwasa ni uchepushaji maji unaofanywa katika safu za Milima ya Uluguru na wakulima wa mbogamboga. [175]
- wale
- Sababu zinazoelezwa na mamlaka kusababisha ukame ni pamoja na uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanywa na baadhi ya wakazi wa manispaa hiyo hasa wale waishio katika safu za Milima ya Uluguru. [176]
- walio
- Watu wengi wanadhani kwamba wapendanao ni wale tu walio katika mapenzi yaani boyfriend na girlfriend pekee. [177]
- waliopo
- Anasema kuwa ili kuwafikia watu wengi zaidi, wameamua kupeleka huduma hizo kwa watu waliopo katika maeneo maalumu kama shuleni, migodini n. [178]
- wana
- Hamu kubwa ilikua ni kusikia kama washitakiwa hao wataendelea kuyakubali maelezo ya ushahidi huo na kama wana kitu siri nyingine wanazozijua ambazo wangezifunua kuhusiana na mauji,au wangeuakana ushahidi huo. [179]
- wapi
- Kutokana na hali hiyo washitakiwa hao ndio pekee wanaoatazamiwa kupasua ukweli wote kuhusiana na mauaji hayo baada ya washitakiwa wengine waliokwisha kujitetea mahakamani hapo kukana kuwa hawahusiki na wala hawajui ni wapi wafanyabiashara hao walikouliwa. [180]
- wapime
- Kampeni hiyo ya upimaji inayoendelea nchi nzima, ina lengo la kuwataka wapenzi wapime na kujua afya zao, kwani kwa kufanya hivyo wataonyesha ni jinsi gani wanavyojali. [181]
- wapo
- Hii inatokana na wengi wao kuamini kuwa kwa kuwa wameoana basi wapo katika usalama. [182]
- watu
- Taarifa zinasema kuwa, baada ya kumwengua Isaack, kamati imeunda tume ya watu watano inayoongozwa na Ridhiwan Kikwete kuchunguza tuhuma hizo. [183]
- wawe
- Wito wangu kwa wapenzi na mashabiki wetu ni kwamba wawe watulivu tunajua tupo katika kipindi kigumu sana, lakini sisi kama viongozi wa bendi tutajitahidi kulikabili pengo hili kubwa kadri ya uwezo wetu," alisema Maalim Gurumo. [184]
- wewe
- Maximo alimwita Ngassa na kumwambia wewe ni mchezaji mzuri, lakini mara nyingi amekuwa akicheza na jukwaa badala ya kucheza kwa kuisaidia timu. [185]
- wiki
- Katika tukio hilo wanamuziki wa bendi mbalimbali, wabunge na viongozi wa serikali walijitokeza kuuaga mwili wa marehemu Maina aliyefariki ghafla Jumatano wiki hii na taarifa ilizozipata Mwananchi kutoka hospitalini hapo zilieleza kuwa kifo cha mwanamuziki huyo kilitokana na shinikizo la damu. [186]
- wote
- Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Masauni Hamad Masauni hakupatikana ili kufafanua suala hilo jana baada ya simu yake ya mkononi kuita muda wote bila kupokelewa. [187]
- yake
- Hatua ya kukamatwa kwa Liyumba na wadhamini wake imekuja siku mbili baada ya Liyumba kuachiwa kwa dhamana ya Sh 882 milioni ambayo ni thamani ya nyumba yake iliyoko Mbezi Juu. [188]
- yako
- Taarifa za ndani ya kikao cha kamati ya utekelezaji zilieleza kuwa, baadhi ya wajumbe walikuja juu na kutaka Isaack afukuzwa kazi moja kwa moja kwa sababu maelezo juu ya tuhuma zake yako wazi. [189]
- yale
- Wanaume walikuwa wakivuja jasho kuchacharika kumaliza mzigo wa magunia 230. Hii ina maana kuwa wanaume walikuwa wanajitahidi kuyabeba yale magunia kwa bidii ili wayamalize haraka. [190]
- yaliyokuwa
- Moja ya mashindano ambayo aliwahi kushiriki na kushinda ni yale yaliyokuwa yakiandaliwa katika ukumbi wa Night Park, Uwanja wa Ndege Dar es Salaam yaliyojulikana kama African Style na kuibuka na ushindi. [191]
- yetu
- Maprofesa wanatunga vitabu lakini wapiga chapa wanachapisha vitabu vyetu na kuviuza bila ya idhini yetu lakini sheria haichukuwi mkondo wake ipasavyo. [192]
- yuko
- Kweka bado yuko rumande baada ya kukosa dhamana. [193]
- yule
- Baada ya kuongea na Ngassa, Maximo alimgeukia Jerry na kumwambia mshambuliaji mzuri ni yule anayejua kuwakimbia mabeki kila wakati na kutafuta nafasi ya kufunga si kutaka kushindano nguvu. [194]
- za
- Akizungumza nje ya mahakama, Mzee alisema tangu jana hati ilipotolewa wamekuwa wanafanya jitihada za kumtafuta Liyumba bila mafanikio na kwamba, bado wanaendelea kumtafuta. [195]
- zawadi
- Anasema kuwa, ili kuwavutia watu wengi zaidi kupima virusi, zawadi mbalimbali kama vile fulana, kalamu, miamvuli n. [196]
- zetu
- Juhudi kubwa tunazifanya kujikita zaidi kwenye jamii, kwani kwa sasa tumeziwezesha ofisi zetu za kanda kwa kuzipa uwezo wa kujiendesha bila ya kutegemea makao makuu, kwa kufanya hivyo wananchi wanajipatia huduma kwa ubora zaidi bila ya kutegemea makao makuu. [197]
- zile
- Enzi zile, mtu aliweza hata kujenga nyumba ya fulusuti na kubandika tangazo nje Shule ya Sekondari ya Ahera. [198]
- ziote
- Akaamuru shule ziote kama uyoga, zisambae kila kata hadi kila kijiji, zikasambaa, zikasambaa hadi zikasambaratika. [199]
- ziwepo
- Basi Mungu akaamuru ziwepo shule zikawepo. [200]