Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-02-19

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aa
Lakini waheshimiwa wenzetu wametuelewa ndiyo maana wameweza kung’aa kama Mungu, na kung’aka kama Mungu na kuamuru kama Mungu mwenyewe. [1]
aina
RAIS Jakaya Kikwete amewataka wakuu wa elimu nchini kurudisha, haraka iwezekanavyo, utaratibu wa shule zote kutumia vitabu vya aina moja vya kufundishia, badala ya mtindo wa sasa wa kila shule kutumia aina yake ya vitabu. [2]
akaona
Mungu akaangalia akaona ni vyema. [3]
akaunti
Tuhuma hizo zinadai kuwa fedha zilizoibwa zilitoka katika akaunti ya Chama cha Wafanyakazi wa Viwandani, biashara, Taasisi za fedha,, Huduma na Ushauri- tawi la kampuni ya Simu Tanzania (Tuico-TTCL) ambazo ziliingizwa kwenye akaunti ya Tucta na baadaye kuripotiwa kuyeyuka kinyemela. [4]
akawa
Kihistoria siku hii ilianza kusherehekewa kwa ajili ya kumkumbuka mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mtakatifu Valentino, ambaye aliuawa kwa kukiuka matakwa ya watawala wa wakati wake, kwa sababu alikemea baadhi ya mila zao na akawa anafungisha ndoa kisiri siri zilizokuwa zimepigwa marufuku kwa wakati huo. [5]
alfajiri
Timu hiyo inaondoka leo alfajiri kwenda Ivory Coast tayari kwa michuano ya Afrika Fainali za Afrika kwa wachezaji wa Ndani ( CHAN) zitakazoanza Februari 22 hadi Machi 8 nchini humo. [6]
ana
Alipoulizwa kuhusu kauli za Dk Kitine, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Sophia Simba, alisema: "Ni maoni yake, ana uhuru wa kutoa maoni, I respect him (namheshimu), Dk Kitine ni mtu ambaye ametumikia serikali kwa muda mrefu. [7]
angalau
Kutoa fedha kwa ajili ya michezo si jambo baya lakini kuna kila haja pia ya kuweka mwelekeo mpya utakaoiwezesha jamii yetu angalau isaidiwe kwa kujengewa miundombinu na huduma nyingine muhimu. [8]
au
Kwa msisitizo, alisema kuna baadhi ya viongozi serikalini, wakiwemo mawaziri wanapewa kiasi kidogo cha fedha kama Sh 20 milioni na kuachia zabuni au maliasili za nchi ambazo wabakaji uchumi hujipatia kiasi cha fedha kama Sh4 bilioni. [9]
awe
SERIKALI inatarajia kuzalisha megawati 500 za umeme utakaotokana na makaa yam awe ya Ngaka mkoani Mtwara, ambao utaingizwa katika gridi ya Taifa. [10]
bado
Alisema maadili yameporomoka kuanzia ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kutoa mfano kwamba, waziri anajiuzulu wadhifa wake kwa tuhuma kama hizo, lakini bado anabaki kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na mbunge. [11]
bali
Alisema kutokana na mvua hizo kuwa za muda, wakulima katika maeneo yenye misimu miwili ya kilimo, hawapaswi kutumia mvua hizo kupanda mazao bali wanatakiwa kusubiri mvua za masika. [12]
bila
Simba alisema matatizo mengi makubwa yakiwemo ya tuhuma za ufisadi zinazoibuka sasa mizizi yake ni nyuma, lakini serikali iliyopo madarakani imeamua kuendesha nchi kwa uwazi bila kuficha mambo. [13]
bunge
Ilikuwa vigumu kuamini kama kweli sababu zilizotolewa kuwa ndizo zilizozuia bunge kujadili mambo muhimu katika mustakbali wa nchi. [14]
busara
Sioni busara yoyote kwa kila mwalimu mkuu kuchagua aina ya kitabu anachotaka. [15]
chachu
Naye nahodha wa Stars, Shadrack Nsajigwa alisema vifaa wanazopata kutoka kwa wadhamini wao ni kama chachu ya kufanya vizuri katika fainali hizo ilikulipa fadhila wanazowafanyia. [16]
chake
Sasa kila shule inacho kitabu chake cha kufundishia. [17]
changu
Sonza: Kwa kuwa kilikuwa ni kituo changu cha kazi, hivyo nilijua tumepongezwa kwa ujumla. [18]
debe
Iddi alisema katika Kijiji cha Bangalala, kila kaya, ilipewa debe moja la mahindi na kwamba yaliiobaki, viongozi hao, waliwatangazia wananchi kwamba mahindi ya bure yameisha na yaliyobaki yalikuwa yakiuzwa Sh 5000 kwa debe na fedha hizo, zilizokusanywa zilikuwa zilikuwa ni kwa ajili ya usafirishaji, ulinzi na upakuaji. [19]
dhidi
Tanzania itaanza kucheza Jumatatu dhidi ya Senegal. [20]
duni
Sehemu ya tatu ni ile ya huduma kutowafikia watumishi wanaoishi na VVU, hasa wale watumishi wa kada za chini ambao mishahara yao ni duni na uwezo wa kujikimu katika hali ya kuwa na virusi hivyo ni mdogo, hususan kwa upande wa gharama za chakula na usafiri. [21]
dunia
CHAMA cha ngumi Tanzania (PST), kimesema hakitakuwa tayari kuruhusu pambano kati ya bondia Francis Cheka anayeshikilia mkanda wa dunia wa ICB na mabondia Kalama Nyirawila na Mada Maugo kutokana na mabondia hao kutokuwa na uwezo. [22]
enzi
Mfano mzuri ni Mgodi wa Mwadui, uliojengwa enzi za ukoloni. [23]
es
Akizungumza katika mkutano maalumu na baadhi ya vyombo vya habari katika mgahawa wa Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam jana, Dk Kitine alionya kwamba, uchumi na maliasili za taifa zimeshikwa na wageni, huku Watanzania walio wengi wakifanya kazi za udereva, ufagiaji barabarani, kazi za ndani na mashambani. [24]
eti
Mhali gani jamani?, Jumamosi yetu ndo' hii imewadia, tofauti na jumaamosi zingine za kila siku nimeambiwa eti hii ni ya wapendanao, kama hivyo ndivyo, yote kheri. [25]
faida
Tunashukuru kuwa wawekezaji wameamua kuingia huko labda ni kwa sababu Rais Jakaya Kikwete alihimiza hivyo au yawezekana kwa kufanya hivyo, wao hujitangaza zaidi na kupata faida. [26]
fainali
Tanzania ni kati ya timu zinazoshiriki fainali hizo ikiwa Kundi A pamoja na wenyeji Ivory Coast, Zambia na Senegal. [27]
ghafla
Alisema hali ya hewa hubadikoa ghafla na mvua kubwa inaweza kunyesha wakati wowote kutokana na mabadiko hayo hivyop watu kuendelea kuishi kwenye maeno hayo ni kuhatarisha maisha yao. [28]
haiwezi
Kazi hii ya uandishi wa vitabu vya kufundishia haiwezi kuachiwa aliyemaliza shule ya msingi au sekondari. [29]
haja
Kuhusu hoja na haja ya maprofesa nchini kuandika vitabu kwa ajili ya kufundishia, Rais alisema haoni sababu kwa nini wasomi hao hawaandiki vitabu kwa sababu wao ndio bongo kali zaidi nchini. [30]
hapa
Mwipopo: Mimi nasema uliyotoa huko ni tofauti na uliyoyaongea hapa. [31]
hapo
Kauli hizo nzito za Dk Kitine zimekuja wakati nchi pia ikiwa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu hapo mwakani, huku makundi yanayowania madaraka yakiwa yanapigana vikumbo. [32]
hatua
Alisisitiza kuwa hata hatua ya kufikisha baadhi ya vigogo mahakamani ni moja ya mafanikio makubwa katika harakati za kuimarisha utawala bora. [33]
hawana
Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti wachezaji hao walisema wanaamini kutokuwepo kwao katika kikosi kinachoelekea Ivory Coast leo si kwamba hawana kiwango bali ni moja kati ya maamuzi yaliyofanywa na Mbrazili Maximo. [34]
hayo
Hata hivyo, alisema kwamba, ingawa anaheshimu maoni hayo ya Dk Kitine na ambayo serikali itayachukua kuyafanyia kazi, bado ana imani serikali inafanya kazi kubwa katika kuimarisha misingi ya utawala bora. [35]
hazina
Bila shaka hii inatokana na kutokuwepo kwa mikakati mizuri ya kutumia hazina hiyo, labda kwa sababu ya utawala kutokuwa na mipango ya kuwawezesha wananchi wake kutumia maliasili hizo kwa manufaa ya maisha yao. [36]
hewa
Mkurugenzi wa shughuli za utabiri wa hali ya hewa, Mohamed Matitu aliliambia gazeti hili jana kuwa, ingawa mvua hizo ni za muda mfupi, athari zake zinaweza kuwa kubwa kwa wakazi wa mabondeni. [37]
hicho
Pamoja na kuuza chakula hicho, Watendaji hao pia wanatuhumiwa kukiuka taratibu za kugawa mahindi hayo,baada ya kuyagawa katika kila kata badala ya watu waliokumbwa na baa la njaa na majina yao kupitishwa na mkutano mkuu wa kijiji. [38]
hii
Nchi hii imeoza, wapo wakubwa wanakula rushwa, lakini nani kafungwa?" alihoji. [39]
hiki
Tumesimamisha maonyesho yetu, kwa kipindi hiki nawataka mashabiki wetu kuwa watulivu na wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu,” alisema Gurumo. [40]
hili
Mosi alimuuliza kama haoni kuwa kitendo cha kukubali kupongezwa kwa sababu ambazo hakuzijua ndiko kulikomfanya asimamishwe kizimbani alisema: "Mtakatifu Jaji hili ndilo lililoniponza. [41]
hilo
Akitoa ushahidi wake mbele ya mahakama hiyo, Saro alidai kuwa, alifika katika eneo hilo akiwa na Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi cha Urafiki, ASP Ahmed Makelle pamoja na PW Jane Andrew. [42]
hivi
Waziri Khatib alifahamisha kwamba, serikali imechukua hatua ya kuomba michango kutoka taasisi na makampuni yatakayokuwa tayari kufadhili sherehe hizo, kwa sababu hivi sasa haina fedha za kufanyia maandalizi hayo. [43]
hiyo
Dk Kitine alifafanua kwamba, kama Idara hiyo haitakuwa na nafasi katika kumsaidia rais kupata viongozi bora, ni dhahiri nchi itaendelea kutikiswa na viongozi wasio waadilifu ambao watalazimika kujiuzulu. [44]
hizi
Si kwamba kocha hajaona kiwango changu katika kuchagua wachezaji wanakwenda kushiriki katika fainali hizi. [45]
hofu
Mnh!? Mwenzangu naogopa hivi unavyoniona na upekupeku wangu wote huu lakini sikuwahi kunasa hata mara moja” Chawote akamweleza Siwema hofu yake. [46]
huo
Kauli ya Dk Kitine ambaye alishika wadhifa huo wa Ukurugenzi katikaIdara ya Usalama wa Taifa, wakati serikali ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, imetolewa wakati nchi ikiwa imegubikwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ya ufisadi na vita ya chini kwa chini ya kugombea madaraka. [47]
huu
Alisema huu ni wakati ambapo Idara ya Usalama wa Taifa inapaswa kuwa nguzo na mhimili imara wa kuhakikisha viongozi wanaopatikana serikalini wakiwemo mawaziri, wanakuwa waadilifu ili kulinda masilahi ya taifa. [48]
huyu
Sonza: Aliyeandika maelezo yangu siye huyu, yule alikuwa Inspekta lakini hapa inaonekana ni Sajenti kwa hiyo siye. [49]
ibilisi
Tunaona nchi nyingine zikielekea kukutana na ibilisi lakini sisi ni tofauti. [50]
ikawa
Ikawa asubuhi ikawa jioni siku ya kwanza. [51]
ila
Juzi Sonza ambaye ni miongoni mwa askari wa kituo cha Polisi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema, hakuhusika na mauaji ila kilichompoza ni kuwa miongoni mwa watu waliopongezwa na Zombe baada ya tukio hilo. [52]
ile
Mwipopo: Hebu ieleze mahakama ni lipi hukulisema siku ile. [53]
ilivyo
Kutokana na hali ilivyo sasa; viongozi wa serikali wamekuwa wakishangaa jinsi taasisi za dini zinavyoendeshwa na baadhi ya watu kinyume cha maadili yao na hatimaye kuwashauri watumishi wa Mungu kuwasaidia wenzao waache kufanya mambo ya aibu. [54]
ina
Alisema: "Anaamini timu hiyo imekamilika kwani ina kocha mzuri ina wachezaji wazuri inamashabiki wazuri ambao wanataka ushindi kutoka Ivory Coast. [55]
inapata
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF) Fredrick Mwakalebela alisema kwa upande wao wanawashukuru wadhamini kwani wanajitaidi kuhakikisha timu inapata mahitaji muhimu. [56]
itatoa
Akizungumzia mvua ya Masika ambayo ndiyo mvua ya kupandia kwa wakulima wa maeneo yanayolima mara mbili kwa mwaka, alisema mamlaka hiyo itatoa taarifa yake mwanzoni mwa mwezi marchi mwaka huu. [57]
iwapo
Alipoulizwa na waandishi wa habari iwapo kampuni au taasisi hizo hazitajitokeza kufadhili maandalizi hayo itakuwaje, alisema ana uhakika zitajitokeza. [58]
iwe
Zamani tulikuwa na sera ya kitabu kimoja cha kufundishia kwa shule zote nchini bila kujali mwanafunzi yuko shule gani, iwe hapa Dar es Salaam au Ngara au Mbinga. [59]
iweze
Maximo alisema ili timu hiyo iweze kufanya vizuri inahitaji ushirikiano mkubwa nje na ndani ya uwanja kwani yeye ameijenga timu kushirikiana ndani ya uwanja. [60]
jukumu
MAKAMPUNI ya uwekezaji nchini, yanalo jukumu la kushiriki katika harakati za kuondoa umaskini. [61]
juu
Akionekana ni mwenye uchungu na uzalendo wa hali ya juu na nchi hii, alisema kuporomoka kwa fikra za utaifa, maadili ya viongozi wa umma, misingi imara ya uongozi kwa ujumla, kumeifikisha nchi katika kiwango cha rushwa kubwa ya kutisha. [62]
juzi
Rai hiyo ilitolewa juzi na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole, alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM, katika Kata ya Rotya, wilayani Karatu. [63]
kabla
Hata hivyo, kabla ya Saro kupanda kizimbani mshtakiwa wa tisa katika kesi hiyo, PC Michael Sonza, alijitetea kuwa kuwepo kwake kwenye sherehe ya kupongezwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, ACP Abdallah Zombe, ndicho kilichomfanya ashtakiwe. [64]
kaka
Manyema iliyokuwa ikiongozwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba Julius Mrope na kaka yake Patric Mrope ilishindwa kupenya kabisa ukuta wa Majimaji uliokuwa imara kuzuia hatari zote zinazokwenda langoni. [65]
kama
Nimewaiteni kuzungumzia mustakabali wa nchi yetu, kama mnavyofahamu mimi nimeshika nafasi mbalimbali nyeti kuanzia wakati wa Mwalimu," alifahamisha. [66]
kamati
Wengine ni makamu mwenyekiti wa Kijiji cha Bangalala na wajumbe wawili wa kamati ya kugawa chakula hicho katika kijiji cha Bangalala. [67]
kasi
Zaidi ya hapo, tunaomba mamlaka zinazohusika kuweka utaratibu unaoelweka kwa ajili ya kudhibiti na kusimamia utoaji wa huduma hiyo, ili jamii inufaike na isaidie kuongeza kasi ya maendele nchini. [68]
kata
Albino aliyeuawa ametambulika kwa jina la Yunis Bahati (14) mkazi wa kijiji cha Butonga kata ya Sima wilayani Sengerema hivyo kufanya tukio hilo kuwa la pili huku la kwanza likiwa limetendeka siku 26 zilizopita wakati waziri mkuu Pinda alipokuwa ziarani mkoani Mwanza. [69]
kati
Yaani sasa imefika mahali ambapo elimu ya watoto wetu inategemea makubaliano kati ya mwalimu mkuu na mzabuni. [70]
kila
Sherehe hizo ni za kutimiza miaka 45 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo husherehekewa Aprili 26, kila mwaka. [71]
kile
Sonza: Nilichokisema ni kile nilichokieleza hapa. [72]
kiwanja
Katibu huyo alivitaja viwanja vitakavyotumika katika ligi hiyo kuwa ni kiwanja cha Ruaha wilayani Kilosa, Mvomero na kiwanja cha Kivuma kilichopo Morogoro Vijijini ambapo kila kiwanja kutakuwa na timu sita zitakazotoa washindi wawili na kupatikana timu sita zitakazoshiriki hatua ya fainali zitakazochezwa Manispaa ya Morogoro. [73]
kocha
Akizungumza baada ya kutaja kikosi hicho juzi wakati timu hiyo ilipokuwa ikikabidhiwa bendera ya taifa , kocha mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo alisema mafanikio waliyoyapata wachezaji wa timu ya taifa yanasaidia kujenga kizazi kijacho cha wachezaji mpira wa miguu nchini. [74]
kote
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa juzi, kwa vyombo vya habari na Kampuni ya Seacom inayotekeleza mradia huo, baada ya mradui huukukamilika; teknolojia hiyo ya kisasa itawawezesha Watanzania kuingia katika mfumo rahisi wa mawasiliano ya simu duniani kote. [75]
kuamini
Hii inatokana na wengi wao kuamini kuwa kwa kuwa wameoana basi wapo katika usalama. [76]
kufa
Kwanza akaagiza mbu na minyoo na kila aina ya virusi ife lakini kwa kuwa walikuwa wameingiliwa na ibilisi wakakataa kufa. [77]
kufika
Ikumbukwe kuwa, maeneo kama yale ya migodini, kulikuwa na wachimbaji wadogo wadogo waliokuwa wakijipatia fedha za kujikimu lakini baada ya wao kufika nchini, hali imekuwa tofauti na kuwazidishia machungu ya maisha. [78]
kufikia
Alisema timu zote ambazo zitashindwa kuwasilisha fomu za usajili hadi kufikia leo zitaondolewa katika mashindano hayo ikiwa pamoja na kupewa adhabu kali kulikangana taratibu za chama hicho. [79]
kuja
Lakini natoa wito kwa watu wanaoishi bondeni kuhama katika maeneo hayo kwani hali ya hewa hubadilika mara kwa mara na wakati mwingine mvua kubwa inaweza kuja na kusababisha athari kwa wakazi hao,"alisema Matitu. [80]
kujadili
WIKI hii Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lilihitimisha mkutano wake uliokuwa ukifanyika mjini Dodoma na kutoka bila ya kujadili mambo muhimu yaliyokuwa yakisubiriwa na wananchi ili kujua hatima yake. [81]
kuku
Mimi naweza kutengeneza vazi la manyoya ambalo ukivaa unaweza kufanana na mnyama au ndege yoyote kama kuku, simba na wengine wengi pia ninaimba na kucheza nyimbo za makabila mbalimbali. [82]
kumaliza
Baada ya kumaliza elimu ya msingi hakuchaguliwa kuendelea ndipo alipoamua kujikita katika sanaa. [83]
kumi
KESI ya mauaji ya wafanyabiashara wa Mahenge, mkoani Morogoro inayowakabili waliokuwa maafisa na askari wa jeshi la polisi, jana iliendelea kuvuta hisia za watu baada ya mtuhumiwa wa kumi, Abeneth Saro, ambaye alikuwa askari katika Kituo cha Polisi Urafiki, kuieleza Mahakama Kuu kuwa alifika katika eneo la tukio na kuwaona wafanyabiashara hao wakiwa hai. [84]
kundi
Jirani yetu, Mzee Rashid Chongo aliunda kikundi cha ngoma za asili na sarakasi mjini Shinyanya, na kundi hilo lilifahamika kwa jina la Nguzo Nane Cultural. [85]
kupima
Vilevile, unaelezea umuhimu wa kupima na kupata ushauri kama haki ya kila mtumishi, na itolewe bure katika hospitali zinazochaguliwa na waajiri. [86]
kutegemea
Kuhusu haja ya kuleta utulivu katika mfumo wa elimu kwa kuwa na mitaala inayoeleweka na kukubalika, mkutano umekubaliana kulingalia jambo hilo badala ya sasa ambako kuna mitaala ya kila aina kutegemea na lengo la kila shule. [87]
kutumia
Alionyesha kushangazwa na kutokamatwa kwa baadhi ya watu ambao wanafahamika dhahiri kwamba, wameiba fedha kwa kutumia makampuni katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT). [88]
kutumika
Jockel alisema utafiti huo pia umebaini kuwa umeme utakaozalishwa, unaweza kutumika kwa shughuli mbalimbali zinazofanywa na wananchi. [89]
kuu
Waraka huu una faida kuu mbili, ya kwanza ni kwamba unasaidia kuwahamasisha watu kujitokeza kupima na kupata huduma na hivyo kupunguza kasi ya kuenea kwa Ukimwi. [90]
kuuza
HALMASHAURI ya Wilaya ya Same mkoani wa Kilimanjaro imewasimamisha maafisa watendaji wa kata wanne kutokana na tuhuma za kuuza mahindi yaliyotolewa na serikali kwa ajili ya kusaidia waathirka wa njaa wilayani hapa. [91]
kwake
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Muungano, Muhammed Seif Khatib wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, jijini Dar es Salaam. [92]
kwangu
Sonza: Mtukufu Jaji si ya kwangu haya. [93]
kweli
Hii ni sera yetu au tumeletewa na mtu mwingine? Na kwa kweli katika hili hatuna sababu ya kumfurahisha mtu yeyote. [94]
kwelikweli
Umepitwa na wakati kwelikweli ndiyo maana unashindwa kuelewa tunachosema. [95]
la
Hata hao akina Mramba (Basil), ambao wamekamatwa ni sawa na tone la maji katika bahari. [96]
lake
Akiongozwa na Wakili wake Majura Magafu, alidai kuwa maelezo hayo binafsi yanaweza kupatikana katika faili lake la ajira ambalo liko makao makuu ya polisi. [97]
leo
WADHAMINI wa Taifa Stars Kampuni ya Bia ya Serengeti pamoja na Banki ya NMB wametoa jezi mpya kwa timu ya Taifa inayoondoka leo jioni kwenda Ivory Coast. [98]
lini
Kweli, hata enzi zile sikuweza kubisha na nilijitahidi kuandika, kutahadharisha lakini tangu lini wanene wasikie? Vumbi ya zulia zao zimeshaziba masikio yao. [99]
lipo
Ni wazi kuwa makampuni haya, yana mtizamo wa kibiashara zaidi na kuliacha jambo la msingi ambalo lipo mbele yao na ambalo halikwepeki, kama kujishughulisha na kuisaidia jamii ambayo ndiyo wadau wao wakubwa (social responsibility). [100]
maafa
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imewashauri wakazi wa mabondeni kuhama kuepuka maafa yanayoweza kutokea kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. [101]
maamuzi
WASHAMBULIAJI Uhuru Selemani na Jabir Aziz wamesema kutoitwa kwao na kocha Marcio Maximo katika kikosi cha Timu ya Taifa kinachokwendwa Ivory Coast si kiwango kidogo bali ni maamuzi ya kocha huyo. [102]
macho
Lakini katika hali ya kushangaza kabisa, makampuni haya yameziba masikio na kufumba macho. [103]
madudu
Ni wazi kwamba serikali imeshindwa kuwasilisha masuala hayo mbele ya bunge kwa kuogopa moto ambao unaweza kuibuka na kutokana na madudu yaliyopo, katika mikataba hiyo. [104]
maeneo
Sonza: Ni Changanyikeni, Makongo Juu, Survey, Mlalakuwa na maeneo ya Barabara ya Sam Nujoma kuelekea Mwenge. [105]
magofu
Akaona kwamba watoto wengi walikuwa wanakufa hata kabla ya kufika kwenye magofu yale yaliyoitwa shule. [106]
makusudio
Pengine walioianzisha siku hii walikuwa na makusudio mazuri tu. [107]
maovu
Tunaamini kwamba, wajibu wa taasisi za dini na watumishi wake ni kuwafanya watu waache matendo maovu na kuishi maisha yanayompendeza Mungu, ili baadaye wapate rehema na uzima wa milele. [108]
mapungufu
Lakini ukweli ni kwamba utelekezaji wake una mapungufu makubwa. [109]
mashabiki
Majimaji maarufu kama wana Lizombe walionyesha kandanda la hali ya juu lililowafanya mashabiki uwanja mzima kuwakubali na kushangiliwa kila wakati huku Manyema ya Dar es Salaam wakionekana kama wageni. [110]
masuala
Lakini jamii inapoona wanaowahubiria kuacha maovu wanafanya hayo hayo, huchanganyikiwa na wenye imani ndogo huachana kabisa na masuala ya dini. [111]
mavazi
Huyu ni msanii ambaye utengenezaji wake wa mavazi ya kisanii ya manyoya ya ndege vimempa umaarufu mkubwa. [112]
mbali
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Leodegar Tenga alisema mbali' na fedha hizo zilizochangwa, kamati hiyo imeshatumia kiasi cha milioni 250 katika kuisaidia huduma mbali'mbali za timu ya taifa. [113]
mdogo
Kwanza ni uelewa mdogo au kutokuwepo uelewa kabisa kwa watumishi wa serikali kuhusu waraka huu. [114]
mfumo
Pia ameagiza kuimarisha utulivu katika mfumo wa elimu kwa kuweka mitaala inayoeleweka badala ya hali ya sasa ambapo shule mbalimbali zinakuwa na mitaala tofauti kulingana na malengo ya kila shule. [115]
mguu
Januari 21 mwaka huu ikiwa ni baada ya siku 26, albino Jonas Maduka (47) aliuawa saa tatu usiku na wauaji kutoweka na mguu wake ambapo alifariki kutokana na kutokwa damu kutoka katika jeraha lake la mguu. [116]
mikoani
Alisema katika maadhimisho hayo kutakuwa na vijana wapanda baiskeli wa kujitolea wasiopungua 25 kutoka mikoani. [117]
mitatu
Rais Kikwete alisema hayo jana katika mkutano na wakuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake nchini, ikiwa ni mfululizo wa mikutano ya kutathmini utendaji wa Serikali ya awamu ya nne katika miaka mitatu iliyopita. [118]
miungu
Ni wapendwa wa Mungu, ni wapenzi wa Mungu, ni miungu kabisa na sisi. [119]
mke
Maina ambaye ameacha mke na watoto wa wawili alitunga kibao kumuimbia mke wake, Mama Cossy ambacho hakijatoka. [120]
mlo
Chawote akawa mlevi wa kupindukia hadi kupuuza mlo na malazi yake, si kujali afya yake kwa mlo na maradhi tu, bali hata namna ya kulifikiria tendo la kujamiana hasa katika zama hizi za Ukimwi, kuna nyakati akawa anabakwa na kundi la wahuni lakini fahamu zake hazikumtuma kuerevuka, pia hakuwa na utaratibu wa kujichunguza mwili wake. [121]
morari
Alisema pia, zinawapa morari ya kufanya vizuri kwani kila anachokipata wanapata kutoka kwa wadhamini wao na ameaidi kurudi na ushindi. [122]
mwaka
SERIKALI imeamua kuomba michango kutoka taasisi na kampuni binafsi nchini kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Muungano zinazotarajiwa kufanyika Aprili 26, mwaka huu. [123]
mwezi
Mwipopo: Je, ni mwishoni mwa mwezi Januari ulipokwenda kuhojiwa?.. maana jana ulisema uliitwa kuhojiwa mwishoni mwa mwezi huo. [124]
mzima
Mkurugezi wa halmashauri hiyo, Iddi alisema tayari tume iliundwa kuchunguza mchakato mzima wa kugawa chakula hicho, na endapo ikibainika kwamba walikiuka taratibu, voingozi hao, watafikishwa mahakamani. [125]
na
MKURUGENZI Mkuu wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa, ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Makete na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), katika serikali ya awamu ya tatu, Dk Hassy Kitine ameonya kwamba, uchafu na wizi mkubwa wa rasilimali za taifa, mustakabali mbaya wa kisiasa na hali ngumu ya uchumi vinavyoikabili nchi, vinahatarisha usalama wa taifa. [126]
nafuu
Alisema, mradi huo utakamilika katika muda ulipangwa kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kupata huduma nafuu za umeme. [127]
nao
Alisema wachezaji ambao amewachagua kwenye timu ya taifa lakini hataenda nao Ivory Coast alifanya hivyo ili kuwapa motisha na kwamba anajua atakuja kuwatumia au wanafaa kutumika katika timu ya Taifa kwa hiyo wasikate tamaa bali waendelee na mazoezi kwani mafanikio ya Stars ni mwanzo wa kukua na kujulikana soka la Tanzania kimataifa. [128]
navigator
MSIE = navigator. [129]
nayo
Makampuni haya yanayokuja kuwekeza hapa nchini, yanapaswa kuisaidia jamii ili nayo ihisi kuwa angalau inapata huduma muhimu na zinazokwenda sambamba na faida zinazopatikana katika makampuni hayo hapa nchini. [130]
ndivyo
Hivyo ndivyo ilivyo pia kwa Ramadhan Mchemba (28), maarufu kwa jina la Lovii Lovii. [131]
ndiye
Sonza: Niliokwisha kuwataja, mimi, James, Mabula, Nyangelela, Festu na Noel ambaye ndiye alikuwa dereva. [132]
ndoa
Naye Mshauri Nasaha wa Angaza, Peace Kayoza anasema kuwa kampeni hiyo ya upimaji kwa wapenzi wanaoshiriki kitendo cha ndoa, imefanikiwa kwani siku ya Valentine pekee walifanikiwa kupima watu 50 katika kituo cha Angaza kilichopo Amref, Dar es Salaam pekee. [133]
ng
Kama ambavyo kwa dini ya Wamaasai, Mmaasai hawezi kuiba ng’ombe kwa sababu Mungu wake kasema ng’ombe wote ni mali yake, vivyo hivyo hata kwa wanene wetu. [134]
ngazi
Sonza: OCS pia ni ngazi ya juu kumueleza. [135]
ni
Akifafanua na wakati mwingine akionyesha msisitizo kwa kugonga meza, Dk Kitine ambaye ni mchumi na aliyewahi kuwa waziri katika serikali ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa alisema, Watanzania wazawa wenye utajiri halali hawafiki hata watano. [136]
nia
Mlundwa alisema kumpiganisha Cheka na mabondia hao ni sawa na kumkosea heshima na hasa baada ya kutwaa ubingwa wa dunia na kuwataka mabondia hao kama wana nia ya kweli ya kupambana na bondia huyo kwanza wapambane wao na mshindia atakayepatikana ndipo aombe kucheza na Cheka. [137]
nilipata
Hapo nilipata barua ya mwalimu mmoja. [138]
nina
Siwezi kujizuzulu, sioni sababu ya kujiuzulu, nakwenda likizo ya mwezi mmoja nitarudi, kujiuzulu inafaa na lazima iwapo mtu amehusika na tuhuma, lakini mimi nina hakika sihusiki na tuhuma hizo," alisema Ngulla. [139]
nyingine
Katika hatua nyingine Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars walichangishana zaidi ya kiasi cha dola za Marekani 95,000 kwa ajili ya shughuli maalum za kuisaidia timu ya Taifa. [140]
nzuri
Japokuwa tayari wananchi wameshafahamu umuhimu wa rasilimali hizo bado hawajapewa fursa nzuri ya kuzifanyia kazi na huu ni muda muafaka kwa serikali kuangalia nini kifanyike ili fursa hizo kwa wazawa zipatikane. [141]
pa
Alisema katika kipindi cha mwisho wa serikali ya Mkapa, nchi ilivurugika kiasi kwamba, hadi sasa haijulikani pa kuanzia ili kuweza kuisafisha kwani imeoza kutokana na kukosa misingi imara ya uongozi iliyoachwa na Mwalimu Nyerere. [142]
safi
Maximo alisema timu yake haiendi Ivory Coast kushiriki tu, bali wanakwenda kushindana na Watanzania wategemee kuona kandanda safi na yenye matokeo mazuri kwani TFF na wadhamini wanaoisaidia timu wameshirikiana vya kutosha. [143]
sare
Waziri Khatib alisema, kampuni au taasisi itakayojitokeza kufadhili maandalizi ya sherehe hizo kwa kutoa sare, inaruhusiwa kuweka nembo yake kwa lengo la kujitangaza kibiashara. [144]
sauti
Akaamuru miwarsha yote, na semina vyote vipigwe marufuku ili pesa zitumike kununua matrekta, lakini alisikia tu sauti ya vicheko ikitoka kwenye magari. [145]
screen
Width = screen. [146]
sheria
Sika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano, Samuel Siita aliwatangazia wabunge kabla ya kuahirishwa kwa bunge hilo kuwa, sababu kubwa iliyofanya hoja nyingi zisijadiliwe bungeni ni kutokana na sehemu kubwa ya masuala hayo yanashughulikiwa na vyombo vyingine vya sheria. [147]
si
Vijana watakaopenda kushiriki wajitokeze kwa hiari yao na si kwa kuwalazimisha, ndio maana tumesema tutashirikisha wananchi kutoka mikoa yote nchini kwa kila wilaya kutoa vijana watatu," alifahamisha Khatib. [148]
sioni
Mimi siyo mwalimu, mimi mwalimu tu wa jeshi, lakini sioni busara katika hilo. [149]
sisi
Shikamaneni, acheni mgawanyiko tutashinda Karatu na sisi mkoa tutawapa kila ushirikiano katika uchaguzi ujao,"alisema Nangole. [150]
siyo
Hata hivyo, licha ya Saro kukubali kutoa maelezo katika timu ya polisi na kwenye Tume ya Kipenka, aliyakana kuwa siyo yake. [151]
suala
Kuhusu tuhuma za udhaifu katika uendaji na matumizi mabaya ya fedha, Ngulla alisema suala hilo halimwingii akilini kwa kuwa chini ya uongozi wake miaka mitano ya kwanza na hata sasa amekuwa akitoa taarifa za fedha za kila mwaka baada ya ukaguzi kufanyika. [152]
tarehe
Sonza: Sikumbuki tarehe. [153]
tatizo
Mradi huo, utasaidia kupunguza tatizo la umeme kwa wananchi. [154]
tena
Katika hatua nyingine, Mlundwa alisema chama chake hakipendi kuona Matumla na Cheka wakirudiana tena baada ya kupambana mara nne huku Cheka akishinda mipambano mitatu kati ya hiyo. [155]
trekta
Mungu akaagiza, trekta ziwepo. [156]
tu
Ilielezwa kwenye mkutano huo, kuwa sera ya kuwepo kwa vitabu vya kufundishia vya aina moja iliondolewa mwaka 1992, ikaanzishwa sera huria ya vitabu vingi vya kufundishia, lakini hatua hiyo ilikuwa ya majaribio na ya muda tu. [157]
uendeshaji
Nyingine ni uendeshaji usioridhisha wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), na utendaji wa kazi usioridhisha wa Kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services (Ticts)) na taarifa kuhusu uendeshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL). [158]
ukata
Naam! Sisi maskini tutakatika na ukata tu hata baada ya kukata roho lakini matajiri wataukata kama walivyoukata hapahapa. [159]
ukweli
Tuwe wawazi na kuambizana ukweli. [160]
ule
Katika jamii nyingine ambazo wananchi wanaelewa haki zao za msingi kama kule wilayani Tarime, mkoani Mara, hali imekuwa ni ngumu kwa wawekezaji katika migodi iliyopo huko kama ule wa Nyamhongo, na hali tete pia iliwahi kuripotiwa katika migodi mingine kama wa Bulyang’hulu. [161]
usajili
CHAMA cha Soka mkoa wa Morogoro, MRFA, kimesema leo ni siku ya mwisho ya kuchukua fomu za usajili kwa ajili ya Ligi Daraja la Kwanza mkoa Morogoro. [162]
utafiti
Mkurugenzi Mkuu wa Tancoal,Fergus Jockel alisema jana kuwa, utafiti wamebaini kuwa,makaa hayo yanaweza kuzalisha umeme wa uhakika zaidi. [163]
uzazi
Kuna makabila kama Wachaga, ambayo akina mama hawapewi nafasi kubwa kuzungumzia suala la afya ya uzazi. [164]
vazi
Mwenyewe anasema kwamba pia ni mahiri wa kufuma vazi la chui kwa kutumia katani na mtu atakayelivaa akafanana na mnyama huyo. [165]
vema
Nafahamu Idara ya Usalama wa Taifa inafanya kazi zake vizuri, lakini nafikiri ni vema ikazidi kumsaidia Rais ili tupate viongozi ambao ni waadilifu," alisisitiza. [166]
vile
Mnaingiza ukanjanja katika uandishi wa vitabu vya kufundishia wanetu badala ya kutumia watalaam wetu, wasomi wetu na taasisi zetu kama vile ile ya Taasisi ya Elimu Tanzania. [167]
viovu
KATIKA miaka ya hivi karibu baadhi ya viongozi wa dini wamejiingiza katika vitendo viovu ambavyo vinapoteza thamani ya utumishi na ushuda wao kwa wanaowaongoza, hivyo kuifanya jamii kudhani kwamba, huduma hiyo sasa ni sawa na ajira nyingine au imevamiwa na matapeli wanaotafuta mali. [168]
vipi
Shoga vipi tena mwenzetu?” alisalimia huku akisimama pembeni mwa Chawote ambaye kutokana na kusongwa na fikra hakuisikia salamu ile ya shoga yake. [169]
vituo
Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Angaza, Dk Beati Mboya anasema kuwa kampeni hii ya upimaji wa virusi vya ukimwi, inaendelea nchini kote katika vituo vya Angaza. [170]
vyema
Ndiyo maana sisi tumetumia kipindi hiki kuhamasisha wapenzi kupima ili kujua afya zao, ni vyema kujua hali ya afya zao kwa kupima wote, kwani hunufaika kwa kujua nini wafanye ili kujilinda. [171]
wadau
Ninachozungumzia hapa ni msaada wa moja kwa moja ambao makampuni haya yanapaswa kuutoa kwa jamii hii maskini ambayo ndiyo wadau wake wakubwa. [172]
wako
Alisema kwa sasa wataalumu wa mamlaka hiyo wako nchini Kenya kwa ajili ya shughuli hiyo na kusisitiza kuwa mara watakaporudi nchini mamlaka hiyo itatoa taarifa kuhusiana na mvua hiyo ambayo ndiyo mvua kubwa na ya kupandia kwa maeneo yanayolima mara mbili kwa mwaka. [173]
wala
Tunaenda huko, watakaothibitika, hatutawaonea haya wala huruma ya aina yoyote," alisisitiza Iddi ambaye pia na Katibu wa Kamati ya maafa ya wilaya hiyo. [174]
wale
Majeruhi wale na dereva wa gari la Chuo Kikuu aliulizwa kama kulikuwa na mafuta ya kutosha, akasema hayatoshi ndipo majeruhi wakahamishiwa kwenye gari la Oysterbay na kupelekwa Hospitali ya Muhimbili. [175]
walioachwa
Wachezaji walioachwa ni Omary Pazi, Jabir Aziz, Salvatory Ntebe na Uhuru Suleiman. [176]
wamiliki
Barabara ya Sam Nujoma na kutambuliwa na wamiliki wa Kampuni ya Bidco walioporwa fedha zao. [177]
wana
Utaratibu wenu ni mzuri, ni muhimu kuwajua wana CCM wenzetu katika kila shina, tawi na kata ili iwe rahisi kuandaa mipango ya ushindi wa kuanzia katika uchaguzi wa serikali za mitaa,"alisema Sanare. [178]
wao
Alisema njia pekee ya kuisafisha nchi hii ni kupata viongozi wenye fikra za utaifa, uadilifu na kuzingatia wajibu wao. [179]
wapi
Sonza: Hatukuwa tumeambiwa ni wapi tutafanya doria. [180]
wapo
Alisema kama wapo Watanzania wengine wenye fedha nyingi ni ambao wamezipata katika njia chafu ndiyo maana wamekuwa wakizificha ng'ambo. [181]
wateja
Hata hivyo, tunomba baada ya mitambo hiyo kukamilika tunufaike na huduma hiyo kwa kuunganishwa na dunia kwa gharamu nafuu kweli, yasiwe maneno ya kuvutia tu kama inavyokuwa katika huduma nyingi ambazo licha ya kupigiwa debe huishia kuwaumiza wateja wao. [182]
watu
Dk Kitine ambaye dhahiri alionekana kuchoshwa na mwenendo wa baadhi ya mambo yanayotendeka nchini, alisema watu wanazungumzia rushwa ndogo wakati wakubwa serikalini wanakula rushwa kubwa zinazoyumbisha uchumi wa nchi na kuleta ufakara kwa Watanzania. [183]
watumiaji
Mitambo mpya ya simu iwanufaishe watumiaji. [184]
waume
Anafafanua kuwa wanawake wengi wanaokwenda kupima peke yao, huogopa kuwaeleza waume wao kuwa wamepima na kukutwa na virusi vya ukimwi, kwani huogopa kuachwa. [185]
wazee
Wakati huo huo, Bawazir alisema kamati hiyo imemchagua Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya wazee ya klabu hiyo itakayokuwa na majukumu ya kusimamia mwenendo mzima wa timu hiyo katika ichakato mbalimbali ya uchaguzi, usajili na ushiriki wa mashindano yajayo. [186]
wazuri
Alisisitiza kuwa matarajio ya Watanzania kwa Taifa Stars ni wachezaji na viongozi watakuwa mabalozi wazuri na wataonyesha nidhamu ndani na nje ya uwanja, pili Watanzania wanatarajia kuona mchezo mzuri na wa ushindi na tatu ni timu isiende kushiriki tu bali timu yetu ionekane ikishindana. [187]
wewe
Kwa nini tusiwe kama wewe. [188]
wiki
BENDI ya Msondo Ngoma, imesimamisha maonyesho yake kwa wiki moja kufuatia kifo cha mwanamuziki wake, Joseph Maina aliyefariki ghafla jana kwenye daladala. [189]
wote
Matuti alitumia nafasi hiyo kutoa mwito kwa watu wanaoishi maeneo ya mabondeni kuhama kutokana na maeno hayo kuwa ya hatari wakati wote kwa maisha yao. [190]
yako
Kusema unampenda na hujui afya yako, si jambo zuri kwani haionyeshi ni kiasi gani unavyomjali mwezi wako, kama unampenda utamlinda," anasema Mrina ambaye pia ni mtaalamu wa mambo ya saikolojia. [191]
yale
Hata hivyo, aliyakana maelezo hayo kuwa siyo yale aliyoyaandika. [192]
yana
Alisema, maeneo mnegi nchini yana kiasi kikubwa cha makaa hayo, lakini hayajafanyiwa utafiti, kwamba mkakati wa shirika lake ni kuhakikisha kuwa umeme utakaozalisha hautakuwa na madhara kwa wananchi. [193]
yapo
Tuhuma zenyewe ni za jumla sana, lakini kama watu wazima wameamua niende likizo ,sawa nitakwenda likizo kupisha uchunguzi, huenda yapo wanayoyatafuta kwangu, sijui," alisema. [194]
yeye
Alidai kuwa, Makelle na Jane walishuka kwenye gari na kwenda mahali ambapo askari wa Urafiki walikuwa wamesimama wakiwahoji wafanyabiashara hao na yeye alibaki kwenye gari. [195]
yote
Akizungumza kuhusu sherehe hizo, alisema vijana zaidi ya 1,300 kutoka mikoa yote nchini wanatarajiwa kushiriki katika matembezi yatakayofanyika nchi nzima kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 45 ya Muungano. [196]
zile
Enzi zile, mtu aliweza hata kujenga nyumba ya fulusuti na kubandika tangazo nje Shule ya Sekondari ya Ahera. [197]
ziote
Akaamuru shule ziote kama uyoga, zisambae kila kata hadi kila kijiji, zikasambaa, zikasambaa hadi zikasambaratika. [198]
ziwepo
Basi Mungu akaamuru ziwepo shule zikawepo. [199]
zote
Hii ni mara ya kwanza kwa serikali kuomba msaada huo ili kufanikisha maandalizi ya sherehe hizo, kwani mara zote imekuwa ikigharamia yenyewe. [200]