Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-11

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
aende
Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [2]
aina
Pia alisema ili kukabiliana na wizi huo kampuni wazabuni ziliboresha usafirishaji kwa kubadilisha aina ya magari pamoja na kutumia mfumo wa magari hayo kusafiri pamoja katika msafara maalum. [3]
ajabu
Yaani wanahofia kwamba sisi tukiachiwa tunaweza kuwafanyia kitu cha ajabu,îalisema Meshack. [4]
akawa
Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [5]
akina
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Afya na Ustawi wa Jamii wa SMZ, Juma Rajab amesema kutokana na tahadhari ya kiafya, wanawake wajawazito hawatapewa dawa hiyo kwa kuwa, bado hakuna taarifa za utafiti wa madhara yake kwa akina mama wajawazito. [6]
akiuza
Wakati akiuza chapati, pia alikuwa akiuza mboga za majani. [7]
albamu
Mwaka 2002 aliachia albamu yake ya pili Juslisen (Just Listen), nyimbo mbili kutoka katika albamu hiyo zilishika nafasi ya kwanza katika chati za Billboard. [8]
albino
Nyumbani kwake hapo alikuwa akiishi na watu kadhaa akiwemo jamaa mmoja ambaye ni mwenye ulemavu wa ngono yaani albino. [9]
alikutana
Mkuu huyo alisema juzi Ijumaa alikutana na wafungwa pamoja na mahabusu wa gereza hilo kusikiliza malalamiko yao yanatokana na kutokubali mabadiliko ya uongozi. [10]
alitoa
Mtangi alitoa siku saba kwa watuhumiwa kuikamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria. [11]
ama
Mwaka 2003 shule yake ilianza kutoa wanafunzi wa darasa la saba na kushuhudia 'kimbunga' cha kufaulu kwani wanafunzi wote walichaguliwa kujiunga na shule za sekondari na tangu hapo shule hiyo imekuwa ikishika ama nafasi ya kwanza au ya pili katika Manispaa ya Iringa. [12]
ambae
Mchezaji huyo ambae juzi alihudhuria kikao cha maandalizi ya michezo ya nusu fainali za leo, alisema kwamba timu zilikuwa zikihangaika kutafuta makosa ya Stars. [13]
ambalo
Kabla ya kuitwa uwanja wa ndege, Kileo alikuwa ameomba kukutana na wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya katika ofisi za chama jambo ambalo pia lilikwama. [14]
ana
Lakini wanaoruka hivi wanaona kwamba kila mtu ana haki ya kuruka foleni apendavyo kwa sababu yeye ni rais mtarajiwa hata kama ni rais wa mende nyumbani kwake. [15]
anasema
Mbunifu wa mitindo maarufu nchini Fatma Amour Hamad, anasema katika mitindo kila kitambaa kina thamani, cha muhimu ni namna mbunifu anavyoamua kuelekeza nguvu zake. [16]
anaweza
Na ili kuwasaidia hawa ambao hawatujali kabisa, waliona kwamba kila mtu anaweza kuchora sababu nyingine ya kupandisha bei ya mafuta kwenye matako yake. [17]
angalia
Nasikia unamjua, ni huyu hapa angalia vizuri picha, kama unajua anapatikana wapi, nitaagiza hata magari mengine yamsake maeneo hayo, nitaomba hata jamaa yangu mmoja usalama wa taifa mstaafu mwenye uwezo mkubwa katika masuala ya kupeleleza atusaidie kumpata,” alisema waziri. [18]
au
Kwa mujibu wa sheria hiyo ambayo imechapishwa katika gazeti la serikali la Januari 9, mwaka huu kifungu cha 4 (3)(a) mtu yeyote ambaye atauza mafuta kwa bei iliyo juu zaidi ya ile iliyopangwa na mamlaka atapigwa faini isiyopungua Sh3 milioni au kifungo kisichopungua miaka mitano au adhabu zote kwa pamoja. [19]
bado
Meneja Mawasiliano huyo wa Barrick, alikiri kuwapo kwa wizi wa mchanga mwaka jana na kwamba polisi walilazimika kufanya oparesheni na baadhi ya watu walikamatwa na kuburuzwa kortini na kesi zao bado zinaendelea. [20]
bali
Aliongeza kuwa kitendo hicho kimewasikitisha viongozi na wanachama wa CUF kwa ujumla na kwamba sio hawana uwezo wa kujibu mashambulizi hayo bali wanathamini amani na utulivu wa nchi ya Tanzania. [21]
bara
Katibu wa Tume ya Uchaguzi wa CUF Tanzania bara, Moele Kuchilungulo alisema mwanachama huyo alivamiwa kwenye gereji ambako alienda kupeleka gari la mbunge wa Viti maalum kwa ajili ya matengenezo. [22]
beki
KILIMANJARO Stars ikicheza bila ya nahodha wake na beki tegemeo, Shadrack Nsajigwa na Kelvin Yondani leo mchana inashuka kwenye uwanja wa Namboole kuivaa Kenya katika moja ya mchezo wa nusu fainali za Kombe la Chalenji. [23]
bidhaa
Kupanda huku kwa bei ya mafuta duniani kulitumiwa vibaya na baadhi ya wafanyabiashara nchini kuendelea kuuza mafuta hayo kwa bei ya juu hata baada ya bidhaa hiyo kushuka katika soko la dunia. [24]
cha
KIAMA kiama cha wafanyabiashara wa mafuta kimefika baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuchapisha katika Gazeti la Serikali adhabu zitakazowakumba watakaokiuka bei za mafuta zilizopangwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura). [25]
dunia
Hii kwetu ni changamoto na kwa wapenzi wa riadha kwani sasa ni wakati wa kujitangaza zaidi dunia huku tukiweza kuibua vipaji vingine kwenye mchezo huu hapa nchini," alisema Nyambui. [26]
es
Hivi karibuni Ewura ilitoa mwongoza unaotaka kiwango cha juu cha bei ya mafuta kuwa Sh1,166 kwa lita ya petroli na Sh1,271 kwa bei ya dizeli kwa jijiji la Dar es Salaam, lakini wamiliki hao wa mafuta walionekana kukaidi mwongozo huo kwa madai kuwa walikuwa na akiba ya mafuta waliyonunua kwa bei ya juu. [27]
eti
Haya, haya, haya, wapo ambao wamediriki hata kutuita sisi waishiwa kuwa ni mafisadi, eti tumekunywa na kunywaga ushuru wa watu hadi asubuhi siku ya mwaka mpya. [28]
fani
MATUMIZI ya vitambaa mbalimbali katika mitindo ndio msingi katika kuboresha na kukuza fani ya mitindo. [29]
foleni
Kumbe jamaa mwenyewe alikuwa anatafuta nishani ya kiatu peke yake kwa kujaribu kuzuia kila gari linalotaka kuruka foleni. [30]
gani
Wasanii wa filamu bado hawajielewi = wao ni akina nani na wana nafasi gani katika kufanya Watanzania wavutiwe na kazi zao, ndio maana mpaka sasa hakuna chama kinachowasimamia wasanii wa sanaa hii hapa nchini na wanaoweza kuunda chama hicho ni wasanii wenyewe," anasema Simalenga. [31]
hadi
Kwa mafuta ya taa, lita inatakiwa kuuzwa kwa kati ya Sh 814 na Sh875. Kwa sasa mafuta ya taa yanauzwa hadi Sh1,200 kwa lita. [32]
haina
Baada ya serikali kuunda Ewura ilionekana kuwa haina meno na kwamba haingeweza kuwa na nguvu za kufanya kazi zake vyema, hata hivyo, serikali ilisikia kilio cha wananchi kuipatia meno Ewura baada ya kufanyia marekebisho sheria ya nishati bungeni. [33]
hajui
Kauli hiyo ilionekana kumchanganya sana Kazim, akawa hajui la kufanya. [34]
hapa
VIONGOZI sita wa kamati ya ujenzi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), wilayani hapa wanatuhumiwa kushiriki katika njama za kuiba mifuko saba ya saruji katika mradi wa ujenzi wa daraja la kijiji cha Kwemdimu kata ya Kisiwani, wilayani hapa. [35]
hapo
Ni kitu cha kusikitisha na cha kushangaza kwa kweli ndugu waandishi, kwani walipofika ndani ya ofisi hizo za CCM walianza kumpiga na kumuumiza vibaya huku wakimhoji kuwa ni kwanini yupo hapo gereji na bendera ya CUF," alisema Kuchilungulo. [36]
haraka
Wanyancha alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya kulishughulikia hilo kwa haraka iwezekanavyo. [37]
haswa
Mechi hizo zinatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa haswa kutokana na viwango vya timu hizo ambazo licha ya kujuana, lakini zimekuwa zikihofiana na kila mmoja anamuombea mwenzake mabaya. [38]
hatimaye
Pia ni kielelezo kuwa watoto wengi wataishia kufeli mtihani wa kidato cha nne na hatimaye kushindwa kuendelea kidato cha tano na sita. [39]
hawa
Nawaagiza kuhakikisha watu hawa wanakamatwa na kubanwa ili warejeshe fedha na vifaa walivyoiba," alisema mbunge huyo. [40]
hawezi
Sasa narudia kusema; usiogope kumwambia mwezako unavyotaka akufanyie kwani asipofanya usimlaumu kwa kuwa hawezi kujua. [41]
hayo
Mara baada ya maneno hayo, Rais Kikwete aliaga na kuondoka na kuwaacha wana CCM wakiwa wameduwaa. [42]
hii
Pia hatua hii inaifanya Ewura ambayo ilikuwa inaonekana kama kibogoyo sasa kuwa na meno ya kusimamia vyema huduma ya mafuta. [43]
hili
Habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili juzi, zinasema kuwa katika ujio wake, Malecela ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM, ataungana na Kamati ya Kampeni ya CCM iliyoko tangu kuzinduliwa kwake Januari 4, mwaka huu. [44]
hilo
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya hapatikana kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo kwani simu yake ya mkononi haikupatikani. [45]
hizi
Wameitwa uwanja wa ndege katibu na mwenyekiti hivyo sasa hatujui nani atagawa tena hizi pikipiki," alisema kiongozi mmoja wa CCM wilaya. [46]
hizo
Kinyume na matarajio ya viongozi wa CCM Wilaya ya Arusha walioandaa hafla kubwa ya ugawaji wa pikipipiki hizo Kikwete aliwakatalia na kuwataka wazigawe wenyewe. [47]
homoni
Tezi hizi huongozwa na kiungo muhimu sana kiitwacho homoni. [48]
huenda
Kwa sababu unapokaa kusikiliza kesi namna ile, unakaa kusikia wawili wakibishana huenda kuhusu vitu ambavyo kila mtu amevibeba kifuani kwake na pale inakuwa kama nafasi ya watu wawili wakitua mizigo yao. [49]
huko
Wewe kakwambia nani jambo hili?" alihoji Malecela na kuendelea: "Sina mpango wa kwenda Mbeya kwa sababu vijana waliokuwako huko wanatosha, tafadhali check vizuri na chanzo chako cha habari," alisema. [50]
huwa
Wakati mwingine wanawake huwa tunapitia magumu sana, nilipopata matatizo katika familia yangu sikukata tamaa, nilijipa moyo kuwa kama niliweza mwanzo kwa kuuza chapati na mboga nitaweza tena kutimiza ndoto yangu," anasema. [51]
huyu
Tatizo ni kuwa Mkuu huyu mpya wa Gereza alipoingia aliamua kunyoosha mambo aliyokuta yakiendeshwa kinyume na taratibu na miongozo ya jeshi letu na hata magereza nyingine haziyaeandeshi hivyo,"alisema Mallya. [52]
idadi
Kwa ujumla, matokeo hayo ni changamoto kwa serikali kufanya utafiti wa kina wa jinsi ya kuboresha elimu ya sekondari ili iende sambamba na juhudi za kuongeza idadi ya shule ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa nafasi za kidato cha kwanza ikilinganishwa na miaka ya nyumba. [53]
ijayo
BEKI wa Kilimanjaro Stars ambaye atalazimika kukaa nje wiki moja ijayo, amebainisha kwamba Kenya na Uganda zinawaogopa. [54]
ila
Tulivamiwa wakati timu inatoka uwanjani, lakini bahati nzuri hakuna mchezaji yoyote aliyeumizwa, kila mtu yupo salama ila kwenye kikao cha maandalizi ya mechi za kesho(leo) walidai kuna shabiki kaumizwa na wachezaji wetu, kitu ambacho si cha kweli," alisema Leopord Mukebezi ambaye ni meneja wa Stars. [55]
ili
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu alisema sheria za kuwabana wauzaji ili wafuate mwongozo huo tayari zilikuwa zimekamilika na kwamba taasisi yake ilikuwa imewasilisha kwa mwanasheria mkuu wa serikali ili iwekwe kwenye gazeti la serikali kitu ambacho hivi sasa kimefanyika. [56]
iliyopo
Kwa sasa ni mmiliki wa Shule ya Kimataifa ya Ster iliyopo Mjini Iringa na Living Stone iliyopo Njombe. [57]
ina
Tunajua kwamba, serikali ina majukumu mengi kwa ajili ya maendeleo ya taifa, lakini kuna umuhimu wa kulifufua kikamilifu shirika hilo, ambalo kwa ujumla ni kurunzi ya taifa letu katika medani ya usafirishaji duniani. [58]
inatakiwa
Kwa mujibu wa mwongozo huo, bei ya mafuta kwa Jiji la Dar es Salaam inatakiwa kuwa Sh 1,166 kwa lita moja ya petroli na Sh 1,249 kwa lita moja ya dizeli. [59]
iwe
Kwa upande wa mafuta ya dizeli kwa jiji la Dar es Salaam, dizeli yenye ubora wa 500ppm inatakiwa iwe Sh1,271 kwa lita na ikipanda bei ya kikomo iwe ni Sh 1,366. Kwa dizeli yenye ubora wa 5000ppm inatakiwa iuzwe kwa Sh 1,305 na ikipanda bei ya kikomo iwe ni 1,403 kwa lita. [60]
jengo
Baada ya miezi kadhaa,Msambatavangu anasema alifungua shule ya chekechea, Mchepuo wa Kiingereza iliyokuwa ikiitwa Livingstone baada ya kupata jengo kwa gharama nafuu, wilayani Njombe, mkoani Iringa. [61]
jua
Hali ya hewa ya hapa ni ya joto kali na jua mchana ambalo halitofautiani na lile la Dar es Salaam wanapoishi wachezaji wengi wa Stars. [62]
kabla
Mwongozo uliotolewa na Ewura kabla ya sheria ya adhabu kwa watakaokiuka mwongozo huo kuwekwa kwenye gazeti la serikali ulikuwa unaeleza kuwa bei hiyo ilitakiwa kuanza kutumika mara baada ya kutangazwa katika gazeti la serikali. [63]
kadi
Yondani mwenye kadi nyekundu atakosa mchezo wa leo kama ilivyokuwa kwa Shadrack Nsajigwa mwenye kadi mbili za njano. [64]
kafanya
Hapa Uingereza mmoja wa wapishi maarufu, Jamie Oliver kafanya kampeni ya watoto mashuleni kupikiwa chakula bora. [65]
kansa
Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [66]
kasi
Tazama nyuma ulikokotoka na mbele unakokwenda ili uone tofauti iliyopo ndio uweze kupima kasi unayotakiwa uende ili mambo yako yaende vizuri. [67]
kati
Kiwango hicho ni cha chini ukilinganisha na bei ya sasa katika vituo vya mafuta jijini Dar es Salaam ambayo ni kati ya Sh1, 230 na 1,450 kwa lita moja ya petroli na kati ya Sh1,300 na Sh1,500 kwa lita moja ya dizeli kwa baadhi ya vituo vya mafuta huku vituo vingine vikiwa tayari vimeanza kushusha bei. [68]
kauli
Bosi huyo alitoa kauli hiyo mbele ya waandishi wa habari za michezo wa Tanzania walioko jijini hapa, alipokuwa akizungumzia wachezaji wanaocheza Tanzania. [69]
kiasi
Hata hivyo, taarifa hiyo hakutoa sababu za wananfunzi hao kufeli kiasi hicho mwaka huo. [70]
kichwa
Baada ya kosakosa hizo Polisi Moro walijiuliza na kurekebisha makosa yao ambapo katika dakika ya 42 Fred Agai aliiwapatia maafande hao bao kwa kichwa akimalizia krosi ya beki wa kushoto Masumbuko Hassan. [71]
kidato
JUZI Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, ilitangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha pili uliofanya jana na kuonyesha kiwango cha ufualu kimeendela kushika. [72]
kikamilifu
Kutokuwepo kwake kutanirahisishia kazi sana, lakini mimi nitamtumia Fred Ojuang leo kikamilifu. [73]
kikao
Juzi Chadema ilianza kudhihirisha kwa vitendo msimamo wake huo baada ya mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kugomea kikao cha vyama vya upinzani kilichoitishwa kujadili mchakato wa uchaguzi huo na kufanyika kwenye ofisi za CUF zilizoko Buruguni jijini Dar es Salaam. [74]
kikundi
Mbali na kuwa msanii pia Simalenga pia ni Rais wa Wanafunzi katika Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ) anaposomea Stashahada ya Uandishi na Katibu Mkuu wa kikundi chake cha Kaole. [75]
kikuu
NILIANZA kwa kuuza chapati na mboga za majani, nikapanda taratibu, sasa natarajia kufungua chuo kikuu. [76]
kile
Lakini pia miundombinu ni mizuri, nimeshuhudia uwanja mzuri wa kisasa ambao ni uwanja wa kujivunia katika ukanda wa Afrika mashariki na kati, unaleta changamoto katika maendeleo ya soka, kwa sababu huwezi kupata mafanikio bila kuwa viwanja kama kile," alisema Phiri. [77]
kimataifa
Shirikisho la riadha duniani (IAAF) litashirikiana na Tanzania katika kuutangaza uwanja huu kwani umeonekena kuwa na ubora wa kisasa zaidi na wenye hadhi ya kimataifa zaidi. [78]
kina
Sheikh Yahya alisema kila kitu kina dalili zake na kwamba dalili ya CCM kukwama katika uchaguzi wa 2010 zimekwishaonekana. [79]
kote
Taalib Johnson ndilo jina lake halisi lakini anajulikana zaidi duniani kote kwa jina la Musiq Soulchild. [80]
kufahamu
Mimi nashindwa kufahamu mawasiliano haya kutopatikana tatizo hili tunaomba sana tuondoshewe," alilalamika Hamad Issa wa Chake Chake. [81]
kuhusu
Hata hivyo, akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Barrick, Tewel Tewel, alisema kuwa hana taarifa zozote kuhusu suala hilo kwani kwa sasa yupo likizo. [82]
kuja
Mwenyekiti huyo aliyaweka hadharani majina ya wanaotuhumiwa baada ya wananchi kuja juu na kutaka watajwe na wachukuliwe hatua. [83]
kujua
Sasa kwa maneno rahisi kabisa ni kwamba; kujieleza kila mmoja kunampa nafasi mwenzake kujua anafikira nini na anataka afanyiwe nini hasa. [84]
kula
WAFUNGWA na mahabusu wa Gereza Kuu la Maweni Jijini Tanga wapo katika vuguvugu la kutaka kuendesha mgomo wa kula kushinikiza mkuu mpya wa gereza hilo ahamishwe wakidai anawanyanyasa. [85]
kule
Mchezo wa mwisho Tanzania imetufunga kule Dar es Salaam mabao 2-0, lakini tunaingia uwanjani na mawazo mapya. [86]
kumbe
Huyu kafanya hivi huyu kafanya hivi kumbe huyu aliamua kwenda kufanya hivi baada ya kushindwa kumuelewa mwenzake hivi, ushanifaham. [87]
kumpiga
WATU wanoadiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wanadaiwa kumshambulia kwa kumpiga na kumuumiza mwanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), Philipo Mbwiga katika katika eneo la Mbalizi Mbeya Vijijini. [88]
kumuua
Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [89]
kupewa
Hivyo ni baadhi ya vipaji alivyonavyo msanii huyu mwenye malengo ya kuingia kwenye siasa, ambaye anasema mbali na kuzaliwa na kukulia katika maisha yanayomwezesha kuyajua vizuri maisha ya Watanzania na vipaumbele wanavyositahili kupewa pia kazi zake za sanaa zimemwezesha kuyasoma vizuri maisha ya wananchi wa Tanzania. [90]
kusema
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, SAC Editha Mallya alikiri kuwepo kwa vuguvugu hilo na kusema kuwa ameingilia kati na hatua za kulituliza zinaendelea. [91]
kutaka
Katika hali inayoonyesha kutaka kujiimarisha zaidi, CUF kimefanikiwa kuvishawishi vyama vya NCCR-Mageuzi, TLP na PPT-Maendeleo kumuunga mkono mgombea wake, Daudi Mponzi. [92]
kutusaidia
Chakula bora na mazoezi ni mawili ya msingi yanayoweza kutusaidia kupambana na matatizo ya kisukari. [93]
kuu
Phiri aliyerejea Simba mwishoni mwa wiki iliyopita, aliwahi kuifundisha timu hiyo mwaka 2004, aliondoka na kurejea tena mwaka 2005 aliweza kuipa mafanikio Simba kwa kutwaa makombe mbalimbali kama la Tusker na ligi kuu ya Tanzania bara. [94]
kuua
Tunapongeza juhudi zilizofanywa na SMZ kukabiliana na kipindupindu kwa kutafuta njia moja wapo ya kudumu dhidi ya ugonjwa huo sugu unaoendelea kuua watu, hasa katika maeneo yanayotawaliwa na uchafu. [95]
kuuza
Kuchapishwa kwa sheria hiyo katika gazeti la serikali kulikokuwa kunasubiriwa kwa hamu na wadau wa mafuta nchini ni kitanzi kwa wafanyabiashara ambao wamekaidi kukubali kuuza mafuta kwa bei iliyopangwa. [96]
kwao
Naye katibu Mkuu wa Shirikisho la riadha nchini Suleiman Nyambui alisema wanashukuru kwa utarabu huo uliowekwa na Serikali kwani ni moja ya changamoto kwao ya kuweza kusonga mbele zaidi na kujulikana kimataifa katika mchezo wa riadha. [97]
kwenda
Kifungu cha 7(7) kinaeleza kuwa, mtu yeyote atakayekiuka kipengele cha 7 (5) na 7 (6) na kwenda kinyume, atapatikana na hatia na atapigwa faini isiyopungua Sh3 milioni au kifungo kisichopungua miaka mitano au adhabu zote mbili kwa wakati mmoja. [98]
la
Alisema ameziona pikipiki hizo, lakini hatazigawa kwa kuwa hana muda kutokana na kuwahi uwanja wa ndege na akawaachia jukumu la kuzigawa viongozi wenyewe wa CCM wa Wilaya ya Arusha. [99]
labda
HATA kama nitaendelea kuwa kwenye sanaa labda nitakuwa kama kiongozi pale nitakapohitajika, lakini sitarajii kuendelea kuwa msanii kwa muda mrefu, natarajia kuachana kabisa na sanaa hii," NI kauli ya nadra sana kusikika kutoka kwa mtu anayependa kazi yake. [100]
lake
Hatahivyo; Mchezaji mmoja wa Stars ambae jina lake halikufahamika maramoja alitupa chupa kupitia dirishani na kumuumiza shabiki mmoja. [101]
langu
Nilipomaliza sekondari, sikua njia nyingine ya kujikwamua kiuchumi, lakini kwa sababu mama yangu alikuwa na hoteli, nilitumia mwanya huo kutengeneza chapati na kuziuza, ilimradi lengo langu litimie," anasema. [102]
lengo
Alisema amekuja kwa lengo na kuhakiki uwekaji wa Zulia la kisasa kwa ajili ya mchezo wa riadha na katika vipimo walivyofanya wameona uwanja huo umekamilika kwa ajili ya kazi hiyo ambayo tayari maandalizi ya uwekaji yameanza kufanyika na wataalam watakaoweka Zulia hilo. [103]
leo
Malecela aliyewahi kulalamika kuwa anatumiwa kama tingangatinga linalotumika katika ujenzi wa barabara na kuzuiwa kuitumia ikishakamilika, anatarajiwa kuungana na kampeni za CCM leo baada ya kuwasili mkoani Mbeya jana jioni, katika safari iliyogubikwa na usiri mzito ndani ya chama. [104]
licha
Juzi, Malecela alikanusha kujiunga na kampeni za CCM mkoani Mbeya licha ya vyanzo vya uhakika kulidokeza gazeti hili kuwa tayari maandalizi yamefanywa kumpokea jana jioni. [105]
lugha
Nikiwa Kilakala sikuweza kuongea Kingereza, lakini walikuwepo watoto waliokuwa wakiongea lugha hiyo vizuri kwa sababu walisoma shule za Kiingereza, hili lilinipa msukumo wa kuanzisha shule ya mchepuo wa Kiingereza," anasema. [106]
maigizo
Kauli hii haikutoka kwa mwingine, bali kwa msanii maarufu wa maigizo kutoka Kaole Sanaa Group-Simon Peter Simalenga ambaye kwa wapenzi wa maigizo anakwqenda kwa jina la Simalenga. [107]
majira
Mbali na mchezo huo utakaopigwa majira ya saa 6.30 mchana na kuonyeshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni ya kulipiwa cha GTV, Uganda itacheza na Burundi saa 9.30 Alasiri. [108]
makubwa
KWA muda mrefu Watanzania tumekuwa katika matatizo makubwa ya kupanda kwa bei ya mafuta, ambayo ilisababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la duniani. [109]
mapambo
Pamoja na kutengenezwa kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini mara nyingi mavazi haya hunakshiwa kwa kutumia mapambo yanayopatikana katika mazingira ya Kitanzania au Kiafrika zaidi. [110]
mapema
MTAALAM kutoka Shirikisho la riadha duniani (IAAF), John Velzien amethibitisha ubora wa sehemu ya kuwekea Zulia kwa ajili ya kukimbilia kwenye uwanja Mkuu na amesema vipimo vimekamilika tayari kwa kazi hiyo kuanza mapema wiki ijayo jijini Dar es Salaam. [111]
matako
Wajibiwe hao na matako matupu, pamoja na matrafiki ambao wanaangalia tu bila kuchukua hatua yoyote. [112]
mauaji
Kwenye gazeti moja liliandika kichwa cha habari kikubwa kuwa ”Siri ya mauaji ya albino yafichuka, ni kiungo kimoja kuuzwa milioni 100”...alisoma taarifa hiyo na kusema kama gazeti limeandika hivi bila shaka kuna ukweli dhidi ya madai haya kwamba mtu anaweza kuwa tajiri kwa kutumia viungo vya binadamu. [113]
mawili
Iko chini ya ubongo katikati ya masikio yako mawili. [114]
mazuri
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mpambano huo Syori alisema kuwa ushindi hayo ni matokeo ya maandalizi mazuri aliyokuwa nayo na kuongeza kuwa hiyo itakuwa changamoto ya kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya vijana ya Afrika yatakayofanyika nchini Morocco hapo baadaye. [115]
mbele
Majina ya viongozi hao yalitajwa hadharani na Mwenyekiti wa kijiji cha Kwemdimu, Francis Mnkai katika mkutano wa hadhara mbele ya mbunge wa jimbo la Muheza, Hebet Mtangi. [116]
mbinu
Habari hizo zinasema kuwa Malecela mwenye uzoefu wa kuongoza na kushinda chaguzi ndogo ndani ya chama hicho, sasa ndiye atakayekuwa kiongozi wa kupanga mbinu na harakati za ushindi wa CCM katika kinyang'anyiro hicho cha kuziba pengo la ubunge lililoachwa wazi na marehemu Richard Nyaulawa. [117]
mchana
Sherehe zilizokuwa zifanyike jana mchana katika Kijiji cha Kojani Mkoa wa Kaskazini Pemba. [118]
mfumo
Pia wamedai mkuu huyo alibadilisha mfumo wa vyakula na kwamba mara kwa mara wamekuwa wakipewa chakula kibovu ambacho hakistahili kuliwa na binadamu. [119]
mgonjwa
Huu huwapata zaidi vijana chini ya miaka 35. Wa pili (Type 2) huwakumba wenye miaka 40 kuendelea; na unaweza kuwepo mwilini bila mgonjwa kutambua. [120]
mimi
Mungu wangu nisaidie mimi," alilalamika. [121]
miti
Fatma anasema amekuwa akibuni mavazi kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini kwa mfano ngozi, magamba ya miti magunia, vitambaa vya jinja n. [122]
mjini
Wizi huo unfanyika zaidi katika vijiji vya Segese Wilya ya kahama na Ziba wilayani Igunga, Tinde Shinyanga Vijijini na Kahama mjini. [123]
mno
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [124]
moto
Baadaye wakiwa njiani wanampeleka kituoni, walipigiwa simu na Ikulu kuwa kuna watu wamechoma moto kwa pasi Ikulu. [125]
moyo
Katibu Mkuu Yusuf Makamba aliliambia gazeti hili jana kuwa, CCM haiwezi kuvunjwa moyo na utabiri huo kwa kuwa Sheikh Yahya ni binadamu anayeweza kutumia busara zake kusema anachoamini kuwa kweli. [126]
mtaji
Anasema matatizo hayo (hakuyataja) yalimfanya ashindwe kuendeleza ndoto yake Njombe, hivyo aliamua kuhamia Manispaa ya Iringa akiwa na mtaji kuanzisha shule nyingine, huku ile ya kwanza akiiendeleza mumewe. [127]
muziki
Hii ilitokana na mapenzi yake ya muziki lakini baadaye alipoamua kufanya muziki kama kazi alijibatiza jina la Soulchild, kutokana na mapenzi yake kwa muziki wa Soul. [128]
mwa
Miongoni mwa madai yanayotolewa na wafungwa na mahubusu hao ni kuwa mkuu wa gereza amewanyang'anya vyombo walivyokuwa wakivitumia kwa vyakula, wameanyang'anywa mabusati ya kuswalia na kuwa vyakula wanavyopelekewa na ndugu zao hupokonywa kabla ya kuwafikia. [129]
na
RAIS Jakaya Kikwete jana alikwepa kugawa pikipiki 19 zilizonunuliwa na wafanyabiashara na viongozi wa CCM wilaya ya Arusha kwa ajili ya watendaji wa chama hicho huku akiwataka wawe makini na misaada. [130]
nao
Siwezi kukubaliana na utabiri wa Sheikh Yahya kwa sababu yeye sio Mungu na kama watu wanaweza kuamini utabiri wake na kukubaliana nao basi. [131]
nataka
Nilipoisikia nilijikuta nataka kufahamu zaidi juu yake. [132]
naye
Beki Meshack Abel naye bado ni majeruhi na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki moja. [133]
nayo
Alisema katika mkutano wake na wafungwa hao aliwasomea utaratibu wanaotakiwa kuufuata na kuwafafanulia kwamba kuna baadhi ya mambo yalikuwa yakiendeshwa kinyume, hivyo inabidi waachane nayo. [134]
ndio
Siangalii rekodi kwamba Tanzania kamfunga Kenya mara ngapi mimi hii timu ndio nimepewa karibuni. [135]
ndivyo
Farasi unampeleka kunywa maji lakini anashindwa kuyanywa basi hivyo ndivyo mchezo ulivyo watoto tumewafundisha lakini wameshindwa kufanya vizuri lakini tunashukuru angalau tumepata nafasi nne mpaka sasaalisema Mvita. [136]
ndiyo
Kama Sheikh Yahya ametoa utabiri huo na mimi ninatabiri hivyo sasa tuone nani mkweli katika utabiri wake," alisema Makamba na kuongeza: "Huu sio wakati wa kutabiri ni wakati wa kuzungumzia maendeleo ya chama lakini kama unaona suala la utabiri wa Sheikh Yahya ndiyo la muhimu, ukaandike kwamba Makamba kasema Sheikh Yahya sio Mungu na siwezi kukubaliana na utabiri wake. [137]
ndoa
Alipofikia muda wa kuolewa, anasema alipata mume ambaye walishirikiana ipasavyo katika kuendeleza mradi wao; lakini baada ya miaka kadhaa alipata matatizo katika ndoa yake. [138]
ngumu
Siku moja usiku akiwa nyumbani alitafakari sana hali ngumu ya maisha ambayo angeanza kuishi. [139]
ni
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Arusha, Semmy Kiondo ambaye alikuwa kiongozi pekee wa wilaya aliyebaki katika ofisi hiyo jana, alisema msemaji wa kilichotokea ni katibu wa wilaya. [140]
nia
Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa alisema msimamo wa Chadema dhidi ya ushirikiano wa upinzani uko wazi kwamba imejitoa baada ya kuona hakuna nia ya dhati katika umoja huo. [141]
nini
Kwa upande wa sanaa ya filamu ambayo inashabihiana na hii ya maigizo, Simalenge anawalaumu wadau wa sanaa hiyo kuwa bado hawajajua wajibu wao na wanapaswa wafanye nini ili waweze kuifikisha sanaa katika ngazi ambayo itawafanya Watanzaia wajivunie filamu zinazotengenezwa hapa nchini. [142]
nk
Ingawa ina udogo wa choroko, tezi hii ina kazi takribani kumi- kusaidia kukua, mtiririko wa maji na damu, mimba, ngono, hedhi na uzazi; urefu na ufupi, unene na wembamba, kuchambua chakula mwilini, nk. [143]
nusu
TASAF ilituma Sh30 milioni kwa ajili ya mradi ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita sita na nusu pamoja na kutengenza daraja na kuweka makaravati. [144]
nyinyi
Sijui kama nyinyi waishiwa ni wasomi au la. [145]
nyoka
Kama wahenga walivyonena, mtoto wa nyoka ni nyoka, msanii huyo anataka kuibwaga sanaa kufuata kazi ya baba yake-mzee Simalenga, ambaye ni mwanasiasa wa siku nyingi aliyewahi kuwa Mbunge wa Njombe kwenye miaka ya 70 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalim Julius Nyerere. [146]
ovyo
Hata hivyo, pamoja na juhudi hizo tunaomba chanjo hiyo isichukuliwe kuwa suluhisho la maambukizo ya ugonjwa huo na hatimaye kuanza kuacha kutunza mazingira kiafya, ikiwamo kuchemsha maji ya kunywa, kujenga vyoo na kuvitumia, kuziba mifereji na maji machafu kuzagaa ovyo mitaani na utunzaji wa majalala ambako ndiko masikani ya vidudu vya ugonjwa huo. [147]
peke
Habari zilizopatikana zinaelezeza kuwa madereva hao wanaosafirisha mchanga kutoka Mgodi wa Kakora-Bulyanhulu mkoani Shinyanga kwenda jijini Dar es Salaam, wamekuwa wakisafiri usiku wakiwa peke yao ili waweze kusimama njiani na kupakua mchanga huo. [148]
pia
Ni kweli hatuwezi kujenga chama bila ya kuwa na rasilimali bora, lakini pia msitafute rasilimali zitakazowaletea matatizo," alisema Rais Kikwete bila ya kufafanua. [149]
pili
Mchezo mwingine baina ya Uganda na Burundi unatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa vile Burundi haichoki na hushambulia dakika zote za mchezo tofauti na Uganda ambayo kipindi cha pili huchoka haswa ikiwa na bao. [150]
polisi
Ametoa wito kwa jeshi la polisi kuongeza ulinzi wa kutosha ili kuimarisha usalama wa wananchi na wanachama wa CUF pamoja na kura zao. [151]
redio
Kabla ya kuwa Katibu Mkuu wa kikundi hicho Simalenga aliwahi kuwa katibu msaidizi wa kikundi hicho kwa kuteuliwa tangu mwaka 2001, pia msanii huyu aliyezaliwa miaka 32 iliyopita ni mwandaaji wa kipindi cha Njia Panda katika redio maarufu ya Clouds FM ya jijini Dar es Salaam. [152]
roho
Nakufa, mkuu wa polisi unaniua, sawa mimi nimemuua albino, lakini wewe unaniua mimi kwa kunipiga kibao, imeandika wapi kwamba muharifu apigwe, kabla ya kufikishwa mahakamani,” alisema Kazim huku akikata roho. [153]
saa
Hadi saa 17:30 jioni hakuna kiongozi yoyote wa CCM ambaye alikubali kugawa pikipiki hizo na hivyo kuwaacha makatibu kata wa CCM waliotakiwa kuchukua pikipiki hizo wakihangaika kujichagulia kila mtu ya kwake. [154]
sauti
Sikiliza Kazim, usinitukane tafadhari, mimi ni mtu mwenye heshima zangu, nakusaidia tu, usiniletee shida, kama vipi rudi kule India tuone kama utapona, kosa langu ni nini?” alijibu waziri kwa sauti ya hasira. [155]
sawa
Na wangapi watakuwa wameharibika kwa sababu ya kurundikwa mahali penye jengo lakini pasipo na wajenzi? Ni sawa na kupanda miti wakati wa kiangazi na kutegemea itastawi. [156]
shida
Umempata?” alidakia Kazim, aliyekuwa akizungumza kwa shida. [157]
shuti
Kipindi cha pili Polisi waliongeza mshambulizi na kupata bao la pili kupitia Nicholaus Kapipe dakika ya 54 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na mlinda mlango wa Kagera, Odo Nombo kuzuia shuti la Detla Thomas. [158]
si
Kama kuna makosa yatatuliwe kwa njia za kiserikali na si mtu kujiwekea utaratibu wa kuwaibia watu na serikali," alilalamika Dk. [159]
sijui
Ndio ndugu, mimi naitwa Kazim ni mwenye mgodi wa madini ya almasi kule Mwadui, tatizo ni kwamba hali kwa sasa imekuwa mbaya mno, nimechanganyikiwa hapa hata sijui la kufanya,” alisema akiomba ushauri. [160]
sio
Siwezi kuzungumzia suala la kualikwa au kutoalikwa lakini hata kama tungealikwa tusingehudhuria kwa sababu sisi tunaungana na vyama makini vyenye ukweli na sio muungano wa kinafiki," alisema Dk Slaa. [161]
soka
KOCHA wa timu ya Simba Patrick Phiri amesifu hatua iliyopiga Tanzania katika medani ya soka nchini na kuongeza kuwa endapo jitihada zikiongezeka Tanzania itakuwa mbali katika miaka mitatu ijayo kwenye medani ya soka. [162]
soko
Katika kipindi cha hivi karibuni wabunifu mbalimbali wa mavazi wamekuwa wakitumia mitindo tofauti kwa kutumia vitambaa vilivyokuwa kwenye chati ya juu, lengo likiwa ni kuteka soko la ndani na nje ya nchi. [163]
sugu
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na SMZ, chanjo hiyo ni ya kwanza kutolewa nchini Tanzania na kwamba, wameshaandaa maeneo maalumu ya kufanyia majaribio hayo, ambayo ni yale yenye matatizo sugu ya ugonjwa huo visiwani humo na watu 5,000 wakiwemo watu wazima na watoto wanaotarajiwa kuchanjwa. [164]
tamaa
Nia yangu ilikuwa ni kufungua shule, nilitumia fedha yangu kwa uangalifu sana, na sikuwa na tamaa hata kidogo. [165]
tatu
Dakika tano baadaye Kessy aliyekuwa akiwasumbua mabeki wa Kagera kila wakati alipiga shuti kali lililokwenda moja kwa moja wavuni na kuandika bao la tatu. [166]
tezi
Kati ya vidude ni tezi mbili ndogo, zinazofanya kazi mbili muhimu-ufahamu na mawasiliano. [167]
tu
Hali hiyo ilijitokeza mara baada ya Rais Kikwete kufika katika ofisi za wilaya hiyo na kuonekana kubadilika sura na kutumia dakika tano tu katika hotuba yake na kuondoka. [168]
tuzo
Mbali na hatua hizo, amewahi kushinda tuzo za BET, ASCAP, BMI, na Soul Train; pia amewahi kupendekezwa mara kadhaa kuwania tuzo mbalimbali kama vile MTV, American Music Awards, NAACP na tuzo za Grammy. [169]
ualimu
Tayari ameshapanga hata dhahada ambazo chuo chake kitatoa-ujasiliamali, kompyuta na ualimu. [170]
uchungu
Kwa nini wengine wafaidi tu, sisi waishiwa tusifaidi? Tumefurahi kuona kwamba wako wengi wenye uchungu wa nchi yao. [171]
ujao
Kuhusu kutembelea na mkuu wa mkoa, alisema wamempangia ziara ya kutembelea kila gereza na mkoa huo mara baada ya kurudi kutoka ungeni mwezi ujao. [172]
ukiwa
Aliweza hayo mwenyewe? "Mungu alinisaidia sana, shule ilisikika sehemu kubwa, nikapata wanafunzi na kuajiri walimu wengi zaidi huku msimamo wangu ukiwa ule ule wa kutokuwa na tamaa na kutumia vyema pesa ninayoita. [173]
ule
Watu walioshuhudia biashara hiyo ikifanyika wanasema kuwa madereva wasikuwa waaminifu kwa kushirikiana na wafanyabishara hao kutoka Mwanza na Shinyanga wamekuwa wakichota mchanga wa dhahabu na kurudishia wa kawaida, ili kufidia ule waliouuza. [174]
unene
Amel B. El Tayeb kawataka wananchi wa Dubai kufanya mazoezi, kupunguza unene kwa kuacha kula vyakula vyenye mafuta mafuta na kuvuta sigara. [175]
vingi
Anasema alikuwa mwaminifu katika biashara hivyo ndogo hali iliyomsaidia kuongeza mtaji wake na kuanza kupika vitafunio vingi zaidi ambavyo aliweza kuvisambaza katika haoteli mbalimbali. [176]
vipi
Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni,” alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [177]
vya
Hata hivyo, wengi waliitafsiri hali hiyo na makundi ndani ya CCM Mkoa wa Arusha hasa yaliyotokana na uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho mwaka jana, huku wengine wakisema ni sehemu ya juhudi za rais kupambana na vitendo vya ufisadi. [178]
vyao
Pia kifungu cha 7(6) kinaeleza kuwa wauzaji wa mafuta wanatakiwa kuweka bei za mafuta katika mabango yalivyowekwa barabarani katika vituo vyao na ni lazima vionyeshe bei vizuri bila kuficha, kuonyesha punguzo na promosheni zinazofanywa na vituo hivyo. [179]
vyote
Kwani utajiri na mali ni kigezo cha kupatikana Serikali ya vyama vyote. [180]
wake
Hata hivyo, katika hali ya kuonyesha kukerwa na alichokibaini Rais Kikwete, ilidaiwa baadaye kuwa aliwaita uwanja wa ndege Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha, Kileo na Katibu wake, Mohamed Nyawenga. [181]
wako
Lakini Nurdin Bakar na Henry Joseph wako tayari kuziba nafasi zao unajua uzuri wa wachezaji wa Stars wanajua sana, wanacheza nafasi zaidi ya moja. [182]
wale
Lakini nikaja kugundua kuwa ile ya wale kuongea ndiyo dawa yenyewe tofauti tu ni kwamba huenda hawa watu hawakuwa wawazi baina yao wakiwa pekee yao, labda mmoja alishindwa kujieleza. [183]
wameleta
Watu wameleta mapendekezo yao. [184]
wana
Rais Kikwete pia aliwataka wana CCM Wilaya ya Arusha kuanza kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa. [185]
wangu
Mimi nilikuwa nawatazama wazee wangu wakihangaika na baba mdogo. [186]
wao
Hata hivyo pingamizi la CUF na CCM dhidi ya Shitambala, limeonekana kukikwaza Chadema baada ya chama hicho kujitoa kwenye ushirikiano huo na kutangaza hadharani juzi kuwa hakitamuunga mkono mgombea wa CUF kwa kuwa umoja wao ni wa kinafiki. [187]
wapi
Ndiyo maana tukiamka mara nyingine hatujitambui tulikuwa wapi. [188]
watu
Mara baada ya Rais Kikwete kuondoka watu walikusanyika katika makundi katika viwanja wa CCM na wengi walionekana kumpongeza Rais kwa kutojiingiza katika ugawaji wa pikipiki hizo. [189]
wetu
Kesho tunategemea mchezo mgumu, lakini nimewatengeneza vizuri wachezaji wangu tayari kuhakikisha kwamba tunashinda na mkakati wetu ni ule ule kucheza fainali za haya mashindano. [190]
wewe
Ni vizuri kuongea kutokana na tofauti zenu, na kujaribu kuzungumzia wenyewe mambo ambayo wewe unayo moyoni kuhusu mwenzio ili kwa wakati wake ajaribu kuchuja na kujifunza kukuridhisha. [191]
yaani
Yule Nsajigwa ni hatari sana nimekuwa nikimfuatilia alikuwa ananipa presha sana yaani kwa utafiti wangu niliofanya hakuna beki kama yeye sasa hivi Afrika Mashariki,î alisema Kimanzi. [192]
yao
Alisema kwa wauzaji ambao hawatafuata mwongozo huo, adhabu yao ni faini ambayo kiwango cha chini ni Sh3 milioni au kunyanganywa leseni ya uuzaji wa mafuta. [193]
yenu
Ndugu yenu kutoka pande hizi naomba niendelee kuwashukuru ninyi wasomaji wangu kwa hamasa na changamoto mnnazonipa. [194]
yetu
Kwa Tanzania kukosa chombo muhimu cha usafiri wa anga kama hicho ni aibu na kinarudisha nyuma maendeleo na hata kuitangaza nchi yetu kibiashara na utalii katika duniani. [195]
yote
Salma ambaye alikuwa akiwekewa dripu mikono yote miwili alisema tatizo la kuchelewa kupata kuokolewa pia limechangia kwa wengi wao kupoteza maisha. [196]
yule
Hakuna jambo la kukufanya tusikutangaze kama mgunduzi wa dawa kuponya kansa kwenye moyo, dawa yako tulimpa hadi mtoto wa rais na amepona, rais anataka akuone kukushukuru na kupanga sherehe kubwa ya uzinduzi wa dawa hii ya aina yake,” alisema waziri wa afya wa nchi hiyo siku moja alipokutana na kijana yule mwenye ulemavu wa ngozi. [197]
zake
Wamedai kuwa hawaridhiki na uongozi wa mkuu huyo kwa kuwa amebadaili mambo mengi aliyoyakuta na kuweka amri zake za kikandamizaji. [198]
zako
Endapo nguvu na bidiii zaidi utazielekeza kwenye shughuli zako mwaka huu unaweza kuufurahia na kama sivyo basi utaununia. [199]
zenu
Zaidi nataka niwatakie mwaka mwema wenye baraka kwenu na kwa familia zenu, nataka pia niwakumbushe kuwa huu unaweza kuwa mwaka wa neema kwa watakao jishughulisha. [200]