Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-09

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aina
Alisema hatua hiyo ilikuja baada ya kuhusishwa na wizi wa gari aina ya Isuzu Tipper yenye namba za usajili UAL 071E iliyokuwa imeobwa Nansana, Kampala, Desemba 27 mwaka jana. [1]
alidai
Mwendesha Mashtaka wa serikali Michael Mugabe, alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Novemba 17 mwaka jana. [2]
ama
Vilevile Sheikh Yahya alisema kuwa mwaka 2010 utakuwa mwaka wa vifo na kukwama kwa viongozi wanaoiba mali au kura katika chaguzi ama kwa ugonjwa au kutekwa nyara. [3]
amani
Mbali na kosa hilo la kutusi, upande wa Jamhuri ambao ndio mlalamikaji katika makosa yote ya jinai unaweza kuongeza na kosa la kutishia amani kwa kughadhibisha watu wengine. [4]
ana
Danny ana maumivu fulani nina wasiwasi sana na lakini mpaka kesho (leo) asubuhi nitajua lakini hana hali mbaya sanaanasema Daktari wa timu, Juma Sufian. [5]
asasi
Matumizi ya maneno asasi na taasisi yanachanganywa. [6]
au
Chiligati aliwatoa wasiwasi wananchi wa kudhulumiwa haki yao ya kupata vitambulisho hivyo, kusumbuliwa au kunyanyaswa na kusema atahakikisha kila Mtanzania wa kweli anakuwa nacho na asiyestahili hakipati. [7]
awe
Alifafanua kuwa kiongozi wa serikali hiyo ya muungano wa vyama lazima awe anafanya kazi katika serikali hii ya awamu ya nne na kukaribia kumaliza muda wake. [8]
bado
Kuhusu mvutano uliokuwapo kati yake na Mengi akijibu maswali ya waandishi Masha alisema, suala Mengi halijakwisha kwani bado wanasubiri ushahidi wake aliosema ili waweze kufuatilia tuhuma alizotoa. [9]
bahati
Kwa bahati mbaya neno maamuzi limetumika kwa muda mrefu na limekuwa na mashiko kiasi ambacho watu wengi wamelizoea na wanalichukulia kuwa ni sahihi. [10]
baina
Mazungumzo baina ya CCM na CUF yaliingia kwenye mtafaruku baada ya chama hicho cha upinzani kutangaza kuwa kimejitoa kwa kuwa wenzao wanakiuka makubaliano. [11]
bali
Katika hotuba hiyo, Green alisema, CCM na CUF havipaswi kuwekeana uadui bali vinapaswa kujadiliana na kuangalia mfumo ambao utamaliza tatizo la kisiasa Zanzibar hasa ikizingatiwa kuwa vyama vyote vina wafuasi wanaolingana. [12]
beki
MASHABIKI na wadau wa soka wa hapa wanahofia kwamba huenda beki wao, Andy Mwesigwa akashindwa kumdhibiti Danny Mrwanda na akasababisha penalti. [13]
bidhaa
Kupanda huku kwa bei ya mafuta duniani kulitumiwa vibaya na baadhi ya wafanyabiashara nchini kuendelea kuuza mafuta hayo kwa bei ya juu hata baada ya bidhaa hiyo kushuka katika soko la dunia. [14]
bila
WAZIRI wa Mambo ya Ndani Lawrence Masha, ameendeleza ngonjera katika suala la vitambulisho vya uraia kwa kusema vitaanza kutolewa mwaka huu bila kutaja siku, mwezi wala tarehe ya kutolewa kwa vitambulisho hivyo. [15]
chama
Hakuna chama kinachoshinda madaraka kwa asilimia 100. Hakuna chama kilicho nje kabisa ya mfumo wa madaraka. [16]
chanjo
Chanjo ya kipindupindu isiwalemaze wananchi JUZI Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ilitangaza kuwa Januari17, mwaka huu itaanza kuifanyia majaribio chanjo mpya ya ugonjwa wa kipindupindu katika visiwa vya Unguja na Pemba, ikiwa ni juhudi zake za kutokomeza ugonjwa huo visiwani humo. [17]
chombo
Kwa Tanzania kukosa chombo muhimu cha usafiri wa anga kama hicho ni aibu na kinarudisha nyuma maendeleo na hata kuitangaza nchi yetu kibiashara na utalii katika duniani. [18]
dalili
Sheikh Yahya alisema kila kitu kina dalili zake na kwamba dalili ya CCM kukwama katika uchaguzi wa 2010 zimekwishaonekana. [19]
dhidi
Kuna majibizano makali kutoka kwa baadhi ya wafuasi kwenda kila upande wa siasa dhidi ya wapinzani wao. [20]
dizeli
Kwa upande wa mafuta ya dizeli bei iliyopo kwenye mabango ya vituo vingi vya mafuta inaonyesha kuwa ni Sh. [21]
enka
Meshack Abel anasumbuliwa na enka na hatacheza leo lakini nafasi yake imezibwa kikamilifu na Kelvin Yondani ambae amekuwa kama pacha wa Salum Sued. [22]
es
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Masha alisema mamlaka ya vitambulisho hivyo imeshaundwa na matarajio ni kuwa, vitambulisho vitaanza kutolewa mwaka huu. [23]
eti
Haya, haya, haya, wapo ambao wamediriki hata kutuita sisi waishiwa kuwa ni mafisadi, eti tumekunywa na kunywaga ushuru wa watu hadi asubuhi siku ya mwaka mpya. [24]
fidia
Akizungumzia changamoto zinazoukabili mradi huo, waziri huyo anasema kubwa ni tatizo la ujenzi holela na kuongeza kuwa serikali itatoa fidia kwa wale wote watakaothirika na uboreshawaji wa mradi huo. [25]
foleni
Kumbe jamaa mwenyewe alikuwa anatafuta nishani ya kiatu peke yake kwa kujaribu kuzuia kila gari linalotaka kuruka foleni. [26]
hadi
Uchaguzi huo ulisimamiwa Seif Khatib akisaidiwa na Dk Abdalah Kigoda na Yusuf Omary Mzee ambao walikuwepo katika mkutano huo tangu juzi hadi jana ulipofungwa. [27]
haina
Aliesma kuwa hali ikiendeea namna hiyo UWT itakuwa haina mwelekeo kabisa na haionyeshi mfano bora kwa jumuiya zingine kutokana na kutawaliwa na matusi wakati wa kampeni. [28]
haja
Hivyo, kuna haja kuwa na utaratibu au kampeni maalumu ya kuwasaka watu wa aina hiyo kuanzia kwenye maduka ya dawa hadi kwa waganga wa jadi na wanaopatikana navyo wachukuliwe hatua za kisheria. [29]
halafu
Nimewaambia wachezaji kila mtu asimame na mtu kuanzia mwanzo mpaka mwisho, wasitoe nafasi wachezee mpira, watulie halafu wanapanga mashambulizi. [30]
hana
Alisema, baada ya kupata malalamiko hayo, alienda kumwuliza Afisa Mtendaji wa kata kuhusu utaratibu huo lakini afisa huyo alisema haupo na wala hana taarifa. [31]
hao
Alisema changamoto kubwa ni uhalifu wa mauaji ya albino ambapo alisema kuwa, serikali itapambana na kufanya kila iwezalo kuhakikisha wauaji hao wanadibitiwa. [32]
hapo
Kabla ya hapo, Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania bara, Pius Msekwa alimtaka Simba kutumia uzoefu alionao kutoka Ikulu kuwasaidia wanawake wenzake, kuhakikisha kuwa wanapata haki zao ya kimsingi. [33]
haraka
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasilianio Ikulu baada ya mazungumzo ya Rais Kikwete na mabalozi hao, ilisema, rais amezitaka Palestina na Israel kutafuta haraka njia za kukomesha mapigano yanayoendelea huko Gaza. [34]
hata
Kwa upande wake, Janet Kahama aliuponda uchaguzi huo na kusema kuwa ulikuwa na kasoro nyingi yakiwemo matusi amabayo hayaelezeki na kwamba, hata mumewe alitukanwa kwa ajili yake. [35]
hatua
Katika hatua nyingine, Green alifafanua kuwa kitendo cha Marekani kusaidia wananchi wa Tanzania ni sehemu ya kupunguza uhasama nchini mwake. [36]
hawa
Ukiangalia hawa Uganda ni hatari sana kwenye krosi tumejiandaa kikamilifu kukabiliana na hilo kwa vile tunajua kwamba wana wachezaji wengi warefu. [37]
hawezi
Sasa narudia kusema; usiogope kumwambia mwezako unavyotaka akufanyie kwani asipofanya usimlaumu kwa kuwa hawezi kujua. [38]
hayo
Kahama ambae alifika ukimbini muda mfupi kabla ya matokeo hayo alionyesha kutokuridhika kabisa na jinsi mchakato uchaguzi ulivyoendeshwa. [39]
hii
Huu ni mwaka wa 2009 ambayo jumla ni 11, awamu hii ya nne chini ya uongoz i wa CCM ni miaka 47 ambayo 4+7 = 11. Kwa hiyo herufi ya kumi ni J na ya 11 K yaani JK ndie mshindi" alitabiri sheikh Yahya. [40]
hiki
Inawezekana ni kutokana na kusahau mahitaji ya mila na desturi zetu, kizazi cha sasa hasa hiki cha muongo huu wa mwaka kati ya 2000 na kuelekea 2010, kimeshamiri katika kuruhusu vinywa vyao kutamka maneno hayo machafu mahala popote na kwa mtu yeyote bila ya woga. [41]
hili
Baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, walikiri kuwa miongoni mwao tayari wameenda benki na kuthibitisha kuwa mishahara imeingia kwenye 'akaunti' zao. [42]
hivi
Alisema, hadi hivi sasa zaidi ya watuhumiwa 100 wa mauaji ya albino wamekamatwa na mashauri yao yako katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa kisheria. [43]
hizi
Nawahakikishieni kwamba shughuli hizi za kati ya watu na watu zinaondoa uhasama wa kisiasa nchini Marekani," alisema Green akibainisha miradi mbalimbali inayofanywa na nchi yake nchini. [44]
hizo
Aliwatoa hofu Watanzania akisema kuwa hata baada ya Rais Bush kumaliza muda wake, Rais Obama naye utaendelea juhudi hizo za kuisaidia Tanzania. [45]
huko
Walitengeneza funguo bandia na baada ya mmiliki wa gari hilo kuliweka katika eneo la kupaki huko Nansana, watu hao walirejea na kuwadanganya walinzi kuwa mmiliki amewatuma kuichukua gari hiyo," alinena Nabakooba. [46]
huku
Muda wa kutangazo matoke, Ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma, ulipofanyika mkutano huo ulitulia kimya huku wajumbe wakisubira jina mshindi. [47]
humo
BALOZI wa Marekani nchini, Mark Green, ameibua upya hoja ya serikali ya mseto visiwani Zanzibar na kuonya kuwa maumivu ya kisiasa visiwani humo msingi wake ni uadui uliopo kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF). [48]
husika
Anasema tayari kazi ya kubaini maeneo zitakapopita barabara husika imekwishafanyika hivyo yeyote atakayeanza ujenzi mpya katika maeneo hayo yuko katika hatari ya kuingia hasara ya kutolipwa fidia yoyote na majengo yake kuondolewa. [49]
huu
Alidokeza kuwa viongozi wana wajibu wa kuwaelekeza wafuasi wao juu ya ukweli huu na kuwasahihisha wale wanaoweka maslahi ya chama mbele badala ya maslahi ya wananchi. [50]
huwa
Katika mukhtadha wa kujifunza ni ukweli unaosikitisha kwamba wanafunzi wa lugha huwa ni wepesi kujifunza matusi kwa haraka kuliko maneno mengine katika lugha husika. [51]
huyu
Huyu kafanya hivi huyu kafanya hivi kumbe huyu aliamua kwenda kufanya hivi baada ya kushindwa kumuelewa mwenzake hivi, ushanifaham. [52]
ikiwa
Akizungumzia ripoti ya mafanikio ya miaka mitatu ya serikali ya awamu ya nne kwa wizara yake Masha alisema kuwa, wizara hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na msongamano wa wafungwa magerezani, wahamiaji haramu na kuongezeka kwa uhalifu. [53]
iko
Stars ambayo leo inavaana na Uganda kwenye mechi ya kufuzu kucheza nusu fainali za Chalenji, iko kundi A la michuano ya fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(CHAN). [54]
ila
Alisema historia ya Zanzibar haitofautiani na ile ya Marekani, ila walichokifanya wao katika kuondoa tofauti zao ni kuwa na mfumo wa kugawana madaraka na ndio hadi sasa umeweza kujenga umoja wa taifa hilo lenye nguvu duniani. [55]
ili
Alisema macho ya wizara hiyo yangeelekezwa zaidi katika utambulisho huo ili kuhakikisha unafanywa kwa umakini. [56]
imetoa
Wiki iliyopita, Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa alisema kuwa serikali imetoa Sh2.5 bilioni kwa ATCL, ambapo Sh320 milioni zitatumika kulipa mishahara ya wafanyakazi na kiasi kitakachobakia ni kwa ajili ya kulisaidia shirika kuanza tena huduma zake baada ya kuzisimamisha tangu Desemba 8, mwaka jana. [57]
ina
Akizungumza na balozi wa Israel, Kikwete alisema," ni kweli Israel ina haki ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Hamas, lakini bado taifa hilo limetumia nguvu nyingi katika kulipiza kisasi. [58]
inatakiwa
Kwa hiyo inatakiwa kuwa, Mimi siwezi kusema vazi fulani halifai kuvaliwa ila vazi linafaa kwa mahali husika. [59]
ingefaa
Kwa hiyo ingefaa iandikwe Mchakato wa mafanikio na matatizo ya Yanga. [60]
iwe
Tunaona ufisadi wa wengine na kutetea wa kwetu, lakini tulio wengi tulikubali kwamba hata kama ni kuonyeshana tako, na iwe hivyo hadi ushuzi utufanye sisi sote tuone aibu. [61]
jamani
HAYA haya jamani. [62]
jua
Na kama hato jua basi hawezi kukuridhisha na kama hatokuridhisha jua hutofurahisha na kama hatofurahia basi mengine ndiyo haya yatokanayo. [63]
jumla
Masha alisema kwa upande wa jeshi la polisi jumla ya askari 44 wamefukuzwa kazi kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa na wanne kesi zao zinaendelea Mahakamani. [64]
kadi
Rekodi zangu zinaonyesha kwamba hao kila mmoja ana kadi moja nina wachezaji kama sita ambao wana kadi za njano,îalifafanua Maximo akijibu suala hilo. [65]
kama
Mimi namshukuru mume, watoto wangu na familia yangu kwa ujumla maana uchaguzi ulikuwa ni mgumu haijapata kutokea na kusema kweli uchaguzi ulikuwa na rafu nyingi sana, hata hivyo kama mshindi kapatikana basi tutamuunga mkono kwa dhati," alisema mama Kahama. [66]
kambi
Nataka wazoee mazingira ya kambi na maisha ya timu ya Taifa ili wakati tukitoka Ivory Coast nitakapobadili kikosi wasiwe wageni. [67]
kanuni
Akizungumza katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika baada ya Kamati ya Maendeleo ya Kata, Mstaahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Jerome Bwanausi, amesema kitendo hicho ni ukiukwaji wa kanuni, taratibu na sheria za manispaa. [68]
kasi
Uganda ambayo katika mechi dhidi ya Somalia ilionekana kubadilika, mashabiki wake wameshtushwa na kipigo ilichotoa Stars wanaogopa zaidi safu ya ushambuliaji iliyojaa wachezaji wenye kasi. [69]
kata
Hayo yalielezwa juzi katika mkutano wa hadhara wa meya wa manispaa ya Temeke Jerome Bwanausi na wakazi wa kata ya Mbagala Kuu uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mbagala Kuu. [70]
kati
Akitangaza matokea ya uchaguzi huo, mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Seif Khatibu alimtangaza Simba kuwa alikuwa amepata kura 470 sawa na asilimia 54.5 ya kura zote zilizopigwa na kuwaacha washindani wake, Janet Kahama aliyepata kura 383 sawa na asilimia 48.4 na Joyce Masunga aliyeambulia kura 10 sawa na asilimia 1.1 kati ya kura halali 862 zilizopigwa. [71]
kauli
Balozi Nyang'anyi alikataa kuzungumzia kauli iliyotolewa na Dk Kawambwa, lakini alisisitiza kuwa fedha ambazo wanadaiwa na mawakala wao bado hazijalipwa. [72]
kiafya
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Afya na Ustawi wa Jamii wa SMZ, Juma Rajab amesema kutokana na tahadhari ya kiafya, wanawake wajawazito hawatapewa dawa hiyo kwa kuwa, bado hakuna taarifa za utafiti wa madhara yake kwa akina mama wajawazito. [73]
kiasi
Nashawishika kusema kwamba kiasi kikubwa cha maumivu ya kisiasa ya Zanzibar yametokana CCM kukitenga CUF kisiasa," alisema Green. [74]
kikao
Mara nyingi nimekuwa nikipata bahati ya kuwepo kwenye kikao cha usuluhishi wa migogoro mingi ya wanandoa. [75]
kila
Hakuna kiongozi atakayeweza kuendesha kila kitu anavyotaka yeye milele. [76]
kilo
Alisema, mbali na hilo jeshi la polisi kwa ushirikiano na vyombo vingine vya dola, limekamata watuhumiwa 22,092 na kilo 133 za dawa za kulevya za viwandani na jumla ya watuhumiwa 19,409 walikamatwa na kilo 512,898 za bangi na ekari 653 za mashamba ya bangi zimeteketezwa. [77]
kina
Hatua hiyo ilikuja baada ya polisi kuomba kibali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Mwanza, ili kufukua kaburi hilo na kupata mwili wa marehemu kwa ajili ya kuufanyia uchunguzi wa kina. [78]
kinga
Kwa hiyo basi, tunawaomaba wananchi wa Zanzibar kuendelea na juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo, kwa kuzingatia kanuni za afya ambazo ndiyo kinga pekee muhimu kwa ugonjwa huo. [79]
kuanza
Pamoja na hali hiyo, baadhi ya wafanyabiashara wameonekana kuanza kushusha bei hiyo. [80]
kuingia
Kocha huyo alisema kwamba wamepanga timu hiyo kuingia kambini Februari 2 jijini Dar es Salaam kujiandaa na safari ya Ivory Coast. [81]
kuja
Alisema aliombwa kuja nchini kwa mara nyingine na marafiki zake wa Simba aliowaacha hapa na kuelezwa kuwa Simba haifanyi vizuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu. [82]
kujifunza
Kwa mfano, katika kujifunza lugha na elimu inayohusiana na viungo vya kijinsia. [83]
kujua
Hii ni timu ya Taifa kila mtu anapaswa kujituma kwa kujua kwamba aliyeko ndani ya timu anaweza kutoka muda wowote akaingia mwingine. [84]
kulia
Badala yake viongozi nao waliungana na wananchi kulia kuwa wafanyabishara hawa ndio chanzo cha kupanda kwa gharama za maisha. [85]
kuliko
Mpaka sasa wafanyabiashara wa vituo vya OilCom wanaendelea kuuza mafuta kwa bei ya juu kuliko vituo vya kampuni nyingine jijini Dar es Salaam, kwa kuuza petroli Sh1,600 na dizeli Sh1,450 kwa lita. [86]
kulinda
Kuthibiti lina maana ya kuwa ya kweli, kuwa ya kuaminika ambapo kudhibiti ina maana ya kulinda, kutia mkononi, kutunza. [87]
kuna
Ukweli ni kwamba kuna majambazi wengi wa magari ambao wana uhusiano naye wa karibu. [88]
kundi
Haipaswi kundi moja la kisiasa lijisikie limetengwa na Serikali. [89]
kupokewa
Neno sahihi ni kupokewa. [90]
kusahau
Ambacho hatuwezi kusahau safari hii ni ushindi wa kishujaa dhidi ya Kilimanjaro Stars. [91]
kutoa
Ofisi ya mradi wa vitambulisho imepatikana, mratibu wa mradi ameteuliwa na mchakato wa kumpata mkandarasi wa kutoa vitambulisho unaendelea," alisema Masha. [92]
kuu
Ni kawaida nchini Marekani kwa chama kimoja kuongoza Serikali kuu wakati chama kingine kikiongoza Bunge. [93]
kuua
Tunapongeza juhudi zilizofanywa na SMZ kukabiliana na kipindupindu kwa kutafuta njia moja wapo ya kudumu dhidi ya ugonjwa huo sugu unaoendelea kuua watu, hasa katika maeneo yanayotawaliwa na uchafu. [94]
kuuza
PAMOJA na jitihada za serikali kuwataka wafanyabiashara wa mafuta nchini, kushusha bei ya nishati hiyo, wauzaji wa jijini Dar es Salaam, wameendelea kukaidi amri hiyo kwa kuendelea kuuza mafuta kwa bei ya juu. [95]
kuvaliwa
Ilitakiwa litumike neno kuvaliwa kwani mtu ndiye aliyetenda kitendo cha kuvaa ambapo vazi limetendewa kitendo cha kuvaliwa. [96]
kuwapatia
Baadhi ya wananchi ambao walitegemea kuwa serikali itafanya kila namna kuwapatia kipato bila hata ya kujishughulisha katika kazi. [97]
kuwepo
Rais Kikwete pia alisisitiza msimamo wa Tanzania wa kutaka kuwepo kwa mataifa ya Israel na Palestina katika eneo hilo la Mashariki ya Kati. [98]
kuzuia
Kwa hiyo mwandishi alikuwa na nia ya kutumia neno kudhibiti kwa maana ya kulinda au kuzuia unyanyasaji wa kijinsia. [99]
kwake
Suala la CCM kushirikiana na Chama cha Demokrasia (DP) katika uchaguzi mdogo wa Tarime ni udhaifu na dalili tosha juu ya kushindwa kwake," alisema Sheikh Yahya. [100]
kwao
Kwa upande wa idara ya uhamiaji Masha alisema, jumla ya wahamiaji haramu 7,568 walikamatwa hapa nchini na kati yao 5,712 walifukuzwa nchini na wengine 1,856 ambao ni wasomali 62 na Waethiopia 1,236 wanaendelea kuzuiliwa katika Magereza mbalimbali wakisubiri kurejeshwa kwao. [101]
la
Simba aliuomba mkutano mkuu wa saba kumkubalia Anna Abdalah kuwa mjumbe wa kudumu wa Baraza Kuu la UWT na kukubaliwa na wajumbe wote. [102]
labda
Lakini nikaja kugundua kuwa ile ya wale kuongea ndiyo dawa yenyewe tofauti tu ni kwamba huenda hawa watu hawakuwa wawazi baina yao wakiwa pekee yao, labda mmoja alishindwa kujieleza. [103]
lazima
Ni lazima kueleza hapa kuwa Serikali inalaani vikali mauaji haya na itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa wauaji wanadhibitiwa," alisema Masha. [104]
lengo
SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limeijibu klabu ya Mtibwa Sugar kuwa haijawahi, haina na haitakuwa na lengo la kutoa tamko kwa ajili ya kumdhalilisha mtu, kundi la watu au wanachama wake kama ilivyo kwa timu hiyo. [105]
leo
Mpinzani wa leo anaweza kuwa rafiki wa kesho. [106]
leseni
ATCL lilinyang'anywa leseni ya kurusha ndege na TCAA baada ya kubaini kasoro kadhaa kwenye nyaraka zake za uendeshaji, lakini mwishoni mwa mwezi uliopita, ilirejeshwa. [107]
ligi
Kocha mpya wa timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi Mzambia, Patrick Phiri jana alitia saini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha timu hiyo huku akiwahakikishia wapenzi na wanachama sasa Simba itarudi kwenye nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi. [108]
liko
Eneo la Gaza Palestina, liko chini ya Hamas wakati eneo la Ukanda wa Magharibi, liko chini ya Chama cha PLO kinachoongozwa na Rais Mahmoud Abbas. [109]
lina
Kundi hilo lina timu za Senegal, Zambia na wenyeji Ivory Coast. [110]
lita
Ufuatiliaji wa bei ya mafuta jijini hapa uliofanywa na Mwananchi, unaonyesha kuwa vituo vingi vya mauzo vinauza mafuta ya petroli kwa bei kati ya Sh1,600 hadi Sh1,400 kwa lita kinyume na bei ya Sh 1,166 iliyopangwa na serikali. [111]
liwe
Ilitakiwa liwe kutarajia au kutazamia. [112]
lugha
Ninachunguza matumizi ya maneno na miundo ya sentensi kwa lengo la kuwatanabaisha waandishi na wasomaji kuwa ufasaha wa lugha ni jambo la kuzingatiwa ili tuweze kuulinda utamaduni wetu tulioachiwa na wazee wetu pamoja na kuuendeleza kwa ajili ya vizazi vijavyo. [113]
maadili
Kimsingi Dk Kishe alikuwa akizungumzia maadili, kanuni za maadili na matumizi ya lugha kwa jumla. [114]
maafisa
Mkutano huo ulijumuisha wadau mbalimbali wa utamaduni, wakiwemo maafisa utamaduni zaidi ya 200 kutoka wilaya mbalimbali za Tanzania Bara na Zanzibar. [115]
mada
Katika mkutano huo, mada zilikuwa motomoto huku wajumbe wakichangamsha mkutano huo kwa kuchangia pamoja na kuchanganua. [116]
madai
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow, alisema uchunguzi huo unalenga katika kupata ushaidi juu ya madai kuwa marehemu alikufa kwa kipigo cha mama yake wa kambo. [117]
madogo
Kuhusu maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ambayo inatarajia kuanza Januari 10, Mapunda alisema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha makosa madogo madogo ambayo yaliyojitokeza katika raundi ya kwanza hayatokei tena. [118]
maeneo
Shirika la ndege ni moja ya vivutio vikubwa vya utalii, kwa sababu kuwepo kwake kunaweza kuwahamisha watalii kuja nchini kwa kuwa na uhakika wa usafiri katika maeneo mbalimbali, ndani ya nchi na hata kutoka nje. [119]
magari
MCHUNGAJI Mkuu wa Kanisa la Kawuku Miracle Center wilayani Wakiso,Uganda, Godfrey Kizito, amekiri kujihusisha na wizi wa magari na kuyauza katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. [120]
magumu
Kwa hiyo hatusemi taasisi ya kuwahudumia wajane au watoto wanaoishi katika mazingira magumu. [121]
maharamia
Eti meli zinatekwa nyara na maharamia. [122]
mahitaji
Hii ndiyo sababu ya sheria kuwa na tabia ya kubadilika mara kwa mara kutegemea na mahitaji ya wakati na mazingira. [123]
majira
Waganda katika mchezo wa leo wa kumalizia kundi B,utakaochezwa kwenye uwanja wa Nakivubo mjini Kampala Uganda majira ya saa 10 jioni. [124]
marufuku
Nikiwa kiongozi wa halmashauri hii ninapiga marufuku kitendo hicho kwani ni ni kinyume na utaratibu wa manispaa. [125]
mashambulizi
Tafuteni njia zote zinazowezekana na za haraka ili kukomesha mara moja mashambulizi haya. [126]
meno
Baada ya serikali kuunda Ewura ilionekana kuwa haina meno na kwamba haingeweza kuwa na nguvu za kufanya kazi zake vyema, hata hivyo, serikali ilisikia kilio cha wananchi kuipatia meno Ewura baada ya kufanyia marekebisho sheria ya nishati bungeni. [127]
miaka
Vitambulisho hivyo vingegharimu kiasi cha dola za Kimarekani 155 milioni sawa na Sh183 bilioni za Kitanzania miaka hiyo. [128]
mila
Katika mchakato mzima wa uundaji wa sheria mbalimbali, dhana ya mazingira hugusa maeneo mengi zaidi ikiwa ni pamoja na hali ya kisiasa, kiuchumi na wakati mwingine hata kijiografia, lakini zaidi ni muhimu kuhusisha na kuzingatia mila na desturi za jamii husika ambayo kwa ajili yake sheria husika inakusudiwa kutungwa au kuundwa. [129]
mimi
Afande, nyie ndio mnaotakiwa kukumbuka idadi ya magari niliyoyaiba kwa kuwa mmekuwa mkiweka kumbukumbu kuhusu mimi, mnaniuliza ni magari mangapi ninayofikiri ninakumbuka nimeiba," alihoji mchungaji Kizito. [130]
mingi
Kaimu mkuu wa RRU, Asuman Mugenyi, alisema Mchungaji Kizito amekuwa akituhumiwa kwa wizi wa magari nchini Uganda kwa miaka mingi na kuyauza DRC, na kwamba amekiri kwa Polisi kuwa amekuwa akifanyakazi hiyo kwa miaka 15 sasa. [131]
mkuu
Kwa upande wa wawakilishi wa jumuiya za CCM walioshinda na Martha Mlata ambae atakuwa ni mwakilishi kwa Jumuiya ya wazazi na upande wa vijana alichaguliwa Shy-Rose Bhanji ambaye alimshinda mbali mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Halima Dendego. [132]
mmoja
MABALOZI wa nchi za Israel na Palestina jana walipishana Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati kila mmoja akimfuata Rais Jakaya Kikwete, kwa mazungumzo na utambulisho. [133]
mwa
Kwa sababu hiyo, Green alivishawishi CCM na CUF, kuacha uadui na badala yake kurejea kwenye meza ya mazungumzo ya muafaka wa kisiasa hasa ikizingatiwa kuwa chokochoko za kisiasa zimetawala miongoni mwa wafuasi wao. [134]
mwenyewe
Sikatai tulihitaji pesa za ziada na mimi mwenyewe nimefanya tuisheni. [135]
mzuri
Wachezaji hawa wameonyesha ushirikiano mzuri kuanzia mechi ya awali na wamekuwa tishio kubwa kwa Waganda. [136]
na
Kwa ujumla, wimbo huo uliambatana na shamrashamra na wanawake waliokuwa kwenye Mkutano Mkuu wa Saba wa UWT, licha ya matatokoe kutokuwa tayari, uliaashiria wazi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba alikuwa ameshinda na hatimaye akwa hivyo. [137]
nao
Katibu Mtendaji wa Basata, Gonche Materego, anasema: "Hatuwezi kukwepa utandawazi na tutakabiliana nao. [138]
naye
Rais Mteule Obama naye amefanya hivyo hivyo," alibainisha Green. [139]
ndani
Aidha, amesema kuwa serikali hiyo ya muungano wa vyama itaongozwa na rais aliyepo madarakani Jakaya Kikwete kutokana upinzani aliouonyesha ndani ya Chama na serikali yake. [140]
ni
Kwa upande wa wajumbe wa Baraza Kuu kutoka Tanzania bara walioshinda ni Bety Machangu, Magret Mkanga, Sifa Swai, kutoka Zanzibar ni Ratifa Nasoro, Subira Ally, Mtumwa Yusufu, Lilian Limo na Catherin Nao. [141]
nia
Serikali kuu ilikaa na viongozi wa jiji la Dar es Salaam na kuamua kubuni wazo la kuandaa mradi huu kwa nia ya kulipatia ufumbuzi tatizo la msongamano wa magari barabarani ambapo tulikubaliana kuunda kamati maalum kwa ajili ya kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati," anasema. [142]
nini
Naamini vijana wangu na najua watafanya kazi niliyowaagiza, ni kama tumeshaingia nusu fainali sare ni nzuri kwetu lakini nimewaambia wachezaji wangu washinde kwa vile sielewi nini kinaweza kutokea. [143]
njano
Mawazo yao ni kwamba Haruna Moshi na Shadrack Nsajigwa hawatacheza leo kwa kuwa wanakadi mbili za njano kila mmoja kitu ambacho si sahihi na kitawashangaza uwanjani. [144]
nusu
Katika mchezo wa kuwania kufuzu nusu fainali ya kombe la Chalenji, ambao asilimia hamsini ya Stars wana malaria, Uganda haina cha kupoteza lakini Stars inahitaji ushindi huku ikisikilizia matokeo ya mechi ya nyingine. [145]
nyinyi
Sijui kama nyinyi waishiwa ni wasomi au la. [146]
nyuma
Alitaja vikwazo vingine vinavyolikabili shirika hilo kuwa ni deni la Sh19, bilioni wanalodaiwa na mawakala mbalimbali ambao walichangia huduma kadhaa za uendeshaji siku za nyuma. [147]
pake
Pamoja na hayo, binafsi, sikuwahi kulisikia neno mchapalo, lakini Mwenyekiti wa Mkutano huo, Bakari Hamad Rashid ambaye ni Kamishna wa Utamaduni Zanzibar, alikuwa akiliweka mahala pake kiasi cha kukubalika. [148]
pale
Kwa sababu unapokaa kusikiliza kesi namna ile, unakaa kusikia wawili wakibishana huenda kuhusu vitu ambavyo kila mtu amevibeba kifuani kwake na pale inakuwa kama nafasi ya watu wawili wakitua mizigo yao. [149]
pekee
Nafasi ya Makamu wa Mwenyekiti ilikwendaka kwa Asha Bakari Makame ambaye alikuwa mgombea pekee, aliyepata kura 736 sawa na asilimia 60.3 na kura 70 zilimkataa. [150]
pia
Zoezi la ufukuaji mati hiyo pia limeshuhudiwa na aliyekuwa baba mlezi wa mtoto huyo Mambya Simon pamoja na viongozi wa serikali za mtaa na Kamati ya Maafa ya Mtaa wa Mabatini walikokuwa wakiishi. [151]
pili
Zanzibar ina mategemeo makubwa ya kufuzu hatua ya pili na wachezaji wake walisema jana kwamba hawana presha yoyote na Rwanda. [152]
rais
Miongoni mwa miradi hiyo ambayo ilipewa msukumo mkubwa na rais anayemaliza muda wake, George Bush ni mpango wa kupambana na Ukimwi, Malaria na Millennium Challenge ambao utaboresha miradi mbalimbali ukiwepo wa kuboresha na kuunganisha umeme Unguja na Pemba. [153]
rasmi
Dk Kishe alikuwa kivutio kutokana na umahiri wake wa kusheheresha matumizi ya maneno yasiyo rasmi ambayo alisema kwamba kuna baadhi ya wanajamii wamekuwa wakiyatoa makavu makavu bila y kutanguliza neno ashakum. [154]
rufaa
Kwa mfano, katika shauri la rufaa kati ya John Sima dhidi ya Jamhuri, mrufani ambaye alipatikana na hatia ya matumizi ya lugha ya matusi dhidi ya askari wawili wa jeshi pamoja na mama mwenye nyumba wake, alikuwa akipinga hukumu iliyotolewa dhidi yake kwa kosa hilo la matumizi ya lugha za matusi dhidi ya askari jeshi hao. [155]
saa
Mtoto huyo alifariki dunia Novemba 19 mwaka jana na kuzikwa siku Iliyofuatia katika makaburi ya Nyasaka na kaburika lake lilifukuliwa saa 5:34 ya asubuhi ya jana chini ya usimamizi wa Inspekta wa Polisi Inongu Kinasa. [156]
sanaa
Kingine ambacho kilikuwa cha kuvutia ni mvutano wa baadhi ya maafisa utamaduni kuafiki kazi za waganga wa jadi zichukuliwe kama sanaa huku upande mwingine ukipinga kwa kuwa ile ni taaluma kamili ya uganga na masuala ya utamaduni hayapo. [157]
seti
Katika michezo mingine iliyokutanisha mchezaji moja moja, Syori Lauri wa Burundi akiibuka kifua mbele kwa kumfunga Lidya Ndagilire wa Uganda kwa seti 2,0 ikiwa 6-1,6-1 na Nadia Fernand wa Kenya akimwondoa Mtanzania Vaileth Peter kwa seti 2.1 na matokeo yakiwa 1-6,7-5,na 6-3, huku Yasini Shaaban wa Tanzania akiibuka kidedea kwa kumtoa Taeme Gabresarasiye wa Ethiopia kwa 6-3,6-4 na kumfanya mtanzania huyo kuendelea kusonga mbele. [158]
shule
BAADHI ya walimu wakuu wa shule za msingi zilizoko katika manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, wanawatoza wanafunzi waliofaulu darasa la saba Sh5000, ili wawape barua za utambulisho wa kujiunga na sekondari, Imeelezwa. [159]
si
Aliendelea kuwa, lazima awe si muoga kufichua waovu na bila kusita kuwakamata waovu wa fedha za umma hata kama ni kutoka katika chama, serikali au rafiki yake. [160]
sifa
Taarifa zilizoenea sehemu mbalimbali nchini; na hata kukamatwa na kushtakiwa mahakamani kwa mganga mmoja wa jadi kwa tuhuma za kukutwa na vifaa mbalimbali vya hospitalini na madawa kadhaa, zinadhihirisha kuwa vifaa hivyo sasa vinatumiwa na watu wasio na sifa kutumia vifaa hivyo kutibu wagonjwa. [161]
sio
Kwa namna yoyote ile, fanyeni majadiliano, midahalo na ikibidi bishaneni katika kutafuta njia sahihi kwa ajili ya Zanzibar, lakini ikumbukwe kwamba wapinzani wa kisiasa sio maadui," alisisitiza Green. [162]
sisi
Lakini sisi tuko nyumbani tunapaswa kuwaonyesha mashabiki wetu kwamba tuko tayari kwa ubingwa na matokeo mazuri ya kuwafurahisha kama wenyeji,îalisema kocha huyo na kusisitiza kwamba hawataki kupoteza uelekeo wao. [163]
soko
KWA muda mrefu Watanzania tumekuwa katika matatizo makubwa ya kupanda kwa bei ya mafuta, ambayo ilisababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la duniani. [164]
sugu
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na SMZ, chanjo hiyo ni ya kwanza kutolewa nchini Tanzania na kwamba, wameshaandaa maeneo maalumu ya kufanyia majaribio hayo, ambayo ni yale yenye matatizo sugu ya ugonjwa huo visiwani humo na watu 5,000 wakiwemo watu wazima na watoto wanaotarajiwa kuchanjwa. [165]
tatu
Farah alisema kikosi chake kilistahili kuishia kwenye hatua hiyo kwa vile ikiwa na pointi tatu kwa vile haina ligi wala mfumo wa kueleweka. [166]
tiba
VIFAA vya tiba hospitalini sasa inaonekana kutumbukia mikononi mwa watu wasiostahili ambao hawana ujuzi wa taaluma ya uganga na udaktari wa kusomea kutoka taasisi zinazotambulika. [167]
tu
Hivi karibuni, Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa alisema kuwa serikali imefuta madeni yote ya ATCL, lakini taarifa zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa tamko hilo ni la maneno tu kwa sababu halijafanyiwa utekelezaji. [168]
tuzo
Lakini kwa kuwa sisi ni watu wa ukweli na uwazi, tumejiweka wenyewe ndani ya tuzo la tako. [169]
uamuzi
Neno maamuzi lilitakiwa liwe uamuzi. [170]
ubovu
Pamoja na wananchi kujitahidi katika shughuli zao za kuwaingizia kipato kikwazo kimekuwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine kutokana na ubovu wa barabara au miundombinu mingine. [171]
uchungu
Kwa nini wengine wafaidi tu, sisi waishiwa tusifaidi? Tumefurahi kuona kwamba wako wengi wenye uchungu wa nchi yao. [172]
uhai
Ni hatari kwa mganga wa jadi asiyejua madhara ya dawa ya malaria kama ALU, kutumia kutibu wagonjwa wake, kwani huhatarisha maisha ya wateja wake, ambao wanaweza kupoteza uhai au kupata madhara mengine ya kiafya, ikiwamo kuifanya miili yao kuwa sugu kutokana kutumia dawa bila vipimo maalumu na sahihi kuthibitisha ugonjwa wake na kiwango cha tiba. [173]
ujao
Serikali ya miaka ya 2010 ni ya muungano wa vyama, uchaguzi ujao hautakua na wizi wa kura kama vile ilivyokuwa awali, vyama vya Upinzani kulaumiana na chama Tawala. [174]
ukitoa
Lakini Ngassa yupo kwenye hali nzuri na wachezaji wengine wanaendelea na mazoezi kama kawaida ukitoa Meshack. [175]
umri
Lakini Phiri alisema kikosi alichokiona Zanzibar ni kizuri kinachoundwa na vijana wenye umri mdogo ambacho ana imani wakiungana na wenzao waliopo Uganda Simba itakuwa hatari kama ilivyokuwa zamani. [176]
vazi
Mimi siwezi kusema vazi fulani halifai kuvaa ila vazi linafaa kwa mahali husika; Katika sentensi hii neno lisilofaa hapa ni kuvaa. [177]
vigumu
Mwaka 2006 aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi John Chiligati alisema, vitambulisho vya uraia vingetolewa kwa Watanzania mwaka 2007 na kwamba ingekuwa vigumu kughushiwa. [178]
vya
Hali ya hewa kisiasa hapa visiwani itaimarika iwapo viongozi wa vyama vikuu vya kisiasa watatangaza hadharani kwamba wanawaheshimu wapinzani wao kama ni Wazanzibari na Watazania walio wazalendo. [179]
wa
Hivi ndivyo walivyokuwa wakiimba baadhi ya akina mama katika baadhi ya mitaa ya mji wa Dodoma jana kabla ya matokeo uchaguzi wa Mwenyejkiti wa Jumumia ya wananwake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) taifa kutangazwa. [180]
wakiwemo
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana mjini hapa wadau hao wakiwemo waandishi wa habari walionyesha hofu dhidi ya beki huyo kwa madai kuwa anapaniki. [181]
wako
Tunawajua katika namba saba na nane wako vizuri sana, kuna wachezaji kama Bengo Stephen, Tonny Mawejje, Massa Geofrey ni hatari sana na hatupaswi kuwapa nafasi kabisa. [182]
wameleta
Watu wameleta mapendekezo yao. [183]
wapo
Alisema alienda Zanzibar kuiangalia timu hiyo inayoshiriki michuano ya kombe la Mapinduzi, lakini alidai kuwa si rahisi kuzungumzia matatizo ya yaliyopelekea kufanya vibaya kwenye mzunguko wa kwanza kwa kuwa wachezaji wengi wapo na timu ya taifa ya Tanzania bara kwenye michuano ya Chalenji nchini Uganda. [184]
wawili
Nimepokea malalamiko kutoka kwa wazazi wawili ambao watoto wao walikuwa wakisoma katika shule za msingi Mtoni Kijichi na Bwawani. [185]
wengi
Watu wengi walitafsiri vibaya nilipotoa siku saba Mengi awasilishe ushahidi wake, tulikuwa tunataka tupate ushahidi huo ili tuweze kufuatilia tuhuma alizotoa, siku saba zimepita na hakuleta ushahidi lakini bado suala halijakwisha tunasubiri awasilishe ushahidi ili tufuatilie," alisema Masha. [186]
wetu
Wakati fulani huko nyuma baadhi ya watoa habari wetu waliwahi kukamatwa kwenye eneo hilo na waliachiwa baada ya Uganda kuingilia kati. [187]
wewe
Ni vizuri kuongea kutokana na tofauti zenu, na kujaribu kuzungumzia wenyewe mambo ambayo wewe unayo moyoni kuhusu mwenzio ili kwa wakati wake ajaribu kuchuja na kujifunza kukuridhisha. [188]
wiki
Mathalani, wiki iliyopita vituo vya BP, vilikuwa vinauza petroli kwa Sh1,470 na jana bei hiyo ilikuwa Sh1,402 kwa lita na dizeli kushuka kutoka Sh1,450 mpaka Sh1,233 kwa lita. [189]
wote
Akihutubia mkuwatano huyo baada ya kutangazwa mshindi, Mwenyekiti mpya alisema kuwa atashirikiana na wajumbe wote pamoja na kuandaa semina kwa wote waliochaguliwa kushika nafasi mbali mbali katika umoja huo. [190]
yenu
Kama kuonyesha hasira yenu, tayari mmefanya vya kutosha. [191]
yetu
Maoni yetu ni kwamba lazima mtafute njia za haraka kukomesha jambo hilo vinginevyo msimamo wa dunia utawageuka. [192]
yuko
Aklitoa shukurani baada ya matokeo ya uchaguzi huo kutangazwa, Joyce Masungu aliyewania nafasi ya mwenyekiti, aliaahidi kushirikiana na mama Simba akisema kuwa yuko tayari kufanya kazi za UWT na CCM wakati wowote atakapotumwa na mwenyekiti wake. [193]
yupo
Meya huyo yupo kwenye ziara ya kukagua shughuli za maendeleo na kusikiliza kero za wananchi katika kata zote 24 za manispaa ya Temeke. [194]
za
Hali hiyo pamoja na pilipilika za maandali sherehe ya kumpongeza zilizoashiria kuwa baada ya matokea kutangazwa kungekuwa na haflakubwa ya kumpongeza waziri huyo kwa ushindi wake. [195]
zake
HATIMAYE wafanyakazi wapatao 300 wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), wameanza kulipwa malimbikizo ya mishahara yao ya Novemba na Desemba, mwaka jana, huku hatima ya kuanza safari zake ikiwa bado haijulikani. [196]
zangu
Lakini pamoja na jitihada zangu kudhibiti tatizo hilo wazazi wameendelea kulalamika kutozwa fedha kwa barua hizo," alisema. [197]
zenu
Zaidi nataka niwatakie mwaka mwema wenye baraka kwenu na kwa familia zenu, nataka pia niwakumbushe kuwa huu unaweza kuwa mwaka wa neema kwa watakao jishughulisha. [198]
zetu
Kimsingi kwa mujibu wa mila na desturi zetu za kitanzania, ni mwiko au haipendezi kutumia maneno mabaya yenye asili ya matusi katika maongezi ya kawaida. [199]
zipo
Hata hivyo, anasema kuwa kamati zipo isipokuwa wanakosa fedha za ruzuku katika utekelezaji wa majukumu yake. [200]