Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-06

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
aelewe
Anaongeza kuwa kimsingi ili mwanafunzi aweze kuwa na msingi mzuri wa lugha ni lazima afundishwe na aelewe hatua zote nne za kujifunza lugha hiyo kitu ambacho hakifanyiki na kama kinafanyika basi si kwa shule zote hasa za vijijini. [2]
aende
Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [3]
akawa
Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [4]
ama
Katika mabadaliko hayo, kama Tanzania tumekuwa tukijitahidi kukahikisha tunakwenda nayo sambamba ama kama ni kuwa nyuma basi isiwe mbali sana, na katika hilo serikali imekuwa na mikakati mingi katika sera zake za elimu ili mradi tu kuhakikisha haibaki nyuma. [5]
ambao
Wengine, kwa mujibu wa kamanda huyo, ni Itendele Awadhi (45), Zaidi Kichawele(30), Jabir Ramadhan (30), Amir Mamdali (28) ambao ni wakazi wa Mwanga na utingo wa gari hilo ambaye hajatambuliwa hadi sasa. [6]
amepoteza
Hata hivyo barua ilipokuja ilimweleza kuwa alikuwa amepoteza sifa za kuwa mwanafunzi wa shule. [7]
ana
Lakini, kocha huyo amesema pia kuwa mshambuliaji wa Tanzania, Jerry Tegete ana akili, lakini hana nguvu ndio maana hatakuwa na madhara kwao. [8]
anataka
Sasa kwa maneno rahisi kabisa ni kwamba; kujieleza kila mmoja kunampa nafasi mwenzake kujua anafikira nini na anataka afanyiwe nini hasa. [9]
asaini
Alisema kuwa jana walitaka kocha huyo asaini mkataba huo, lakini wakagundua kulikuwa na upungufu ambao walitakiwa kuurekebisha kabla ya kocha huyo kusaini. [10]
au
Kwa mujibu wa Ewura wale watakaobainika kukiuka bei hizo mpya, watakabiliwa na adhabu ya kunyang'anywa leseni au kulipishwa faini ya Sh3 milioni au kupewa adhabu zote mbili. [11]
awe
Kweli suala la mgombea wa Chaema kuondolewa limetuumiza sana tulikuwa tunampenda na bado tunampenda na tunamuhitaji awe mbunge wetu kwani ndiye tuliyemdhania kuwa angeleta mabadiliko katika jimbo hili. [12]
bado
Akizungumza na 'Mwananchi' Imamu wa Msikiti Mkuu wa Bondeni Mohamad Hambal alisema kuwa mpaka jana saa kumi na moja jioni waumini wenzao walikuwa bado wanashikiliwa na kwamba inadaiwa kuwa wanahusihwa na tuhuma za ugaidi. [13]
baina
Mpango wa kuchangia elimu wilayani Serengeti ni utekelezaji wa maazimio ya mkutano baina ya madiwani wa Serengeti na wakazi wa wilaya hiyo na wale wa mkoa wa Mara wanaoishi jijini Dar es Salaam. [14]
bali
Alisema kitendo hicho hakiotamuathiri bali wanamkomaza kisiasa na kwamba endapo kama angeteuliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo angelepeleka maendeleo. [15]
bao
Katika mechi hiyo iliyotawaliwa na vijana wa Marcio Maximo, Kili Stars ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Danny Mrwanda katika dakika ya 13 baada ya kuunganisha krosi ya Kigi Makasi. [16]
baridi
Mkakati huo umeanza kutekelezwa kupitia uhamasishaji maalum unaofanywa na Mamlaka hiyo kwa watu wanaojihusisha na biashara ya dawa baridi nchini. [17]
barua
Baada ya juhudi zote walizofanya kukutana na uongozi kufeli, kwa pamoja waliamua kuandika barua ya maoni na kuipeleka gazetini. [18]
cha
Mapema mwaka huu Ewura ilitoa mwongoza unataoka kiwango cha juu cha bei ya mafuta kuwa Sh1,166 kwa lita ya Petroli na Sh1,271 kwa bei ya dizeli. [19]
chanzo
Kwa mujibu wa kamanda huyo chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva aliyekuwa akiendesha Toyota Hiace. [20]
chao
WANANCHI wa Kitongoji cha Kwedihuo katika Kijiji cha Kwandugwa wilayani Handeni, wameiomba serikali, ikipe kitongoji chao hadhi ya kuwa kijiji, ili kupanua wigo wa eneo la utawala. [21]
chombo
Baadhi ya wauzaji wa mafuta wamekuwa wakidai kuwa bei zilizotajwa na Ewura hazitekelezeki kwa kuwa walishanunua mafuta kwa bei ya juu na hivyo kuanza kuiuza kwa bei iliyotangazwa na chombo hicho itakuwa ni kuingia hasara. [22]
dhidi
Timu hiyo, kesho itacheza mechi yake ya tatu dhidi ya Rwanda 'Amavubi' yenye pointi tatu baada ya jana kuitungua Somalia kwa mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa mchana kwenye uwanja huo. [23]
dogo
WATU 11 wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kutoka kwenye sherehe ya ubarikio kuligonga kwa nyuma lori lililokuwa limeegeshwa pembeni kwenye Barabara ya Himo eneo la Uchira. [24]
es
Sh1,450 na Sh1,600 kwa lita moja wakati dizeli inauzwa kati ya Sh1,300 hadi Sh1,500 Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Waziri Ngeleja alisema kukaidi agizo lililotolewa na Ewura ni kuidharau serikali. [25]
foleni
Kumbe jamaa mwenyewe alikuwa anatafuta nishani ya kiatu peke yake kwa kujaribu kuzuia kila gari linalotaka kuruka foleni. [26]
gari
Alisema gari hilo lilikuwa limebeba wanafamilia waliokuwa wametoka kwenye sherehe ya ubarikio katika eneo la Longoi wilayani Hai mkoani hapa, kuelekea wilayani Mwanga na kwamba liligonga lori aina ya Volvo ambalo imedaiwa lilikuwa limeegeshwa pembeni kidogo kwenye barabara hiyo. [27]
gazeti
Mwongozo huo wa Ewura unaeleza kuwa bei hiyo inatakiwa kuanza kutumika mara baada ya kutangazwa katika gazeti la serikali. [28]
hajui
Kauli hiyo ilionekana kumchanganya sana Kazim, akawa hajui la kufanya. [29]
halafu
Ukiangalia jinsi wanavyocheza unaona ni watu ambao muda wowote lolote linaweza kutokea halafu wanacheza kitimu wana kasi ya mashambulizi. [30]
hali
Aliwataja waliojeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCM C kuwa ni Madole Adinani (20), Rukia Fadhili (20), Farijala Abdulla (26), Asumina Khamis(50) ambao ni wakazi Kiruru wilayani Mwanga na kuwa hali zao ni mbaya. [31]
halisi
Watu watashuhudia mpira halisi wa Kiafrika ambao wameukosa, wamezoea kuwaona kina Drogba (Didier), Michael Essien, lakini sasa wanakuja wapya. [32]
hana
Baadhi ya maduka ya dawa baridi utakuta dawa zilizopitwa na wakati, mhudumu hana taaluma na biashara yenyewe inaendeshwa bila vibali wala leseni,"alisema Simwanza. [33]
hao
Waziri alitoa kauli hiyo siku moja baada ya tarehe iliyotangazwa na Ewura kuanza kutumika bila mafanikio yeyote huku wafanyabiashara hao wakiendelea kuuza mafuta kwa bei kubwa. [34]
hapo
Chifu huyo alisema kuwa Mbunge Shiwa ndiye aliwaletea wazo la kujenga Shule ya Sekondari ya Ilembo na kwamba baada ya hapo tangu mwaka juzi wamekuwa wakichangishwa fedha kila mara kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, lakini hakuna kinachoendelea. [35]
haraka
Mkakati huo unalenga katika kuhakikisha kuwa kila kata, inakamilisha haraka ujenzi wa vyumba vya madarasa, ili kuwawezesha wanafunzi hao, kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu. [36]
hasa
Aidha, unalenga katika kuibua vipaji vya Watanzania katika michezo hasa kwa vijana katika maeneo mbalimbali hasa vijijini na maeneo machache ya mijini katika mwaka huu. [37]
hatua
Alifikia hatua ya kuwekwa nguzo na bahati mbaya akafariki dunia kabla ya kulimalizia," alisema. [38]
hawa
Tunashangaa sana waumini wenzetu kushikiliwa na kuhojiwa bila sababu za msingi na wanaowahoji wametoka Dar es salaam, inatupa wasiwasi hawa askari walipewa taarifa zisizo sahihi na hakuna muumini wetu anayejihusisha na ugaidi," alisema Mohamad. [39]
hayo
Mboma aliyasema hayo juzi wakati akiwashukuru wananchi katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho za kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo hilo. [40]
hazina
Ufundishaji wa jinsi hiyo kwa nchi yetu ni mgumu kwani shule nyingi hazina vifaa maalum vya kuwasaidia walimu kufundisha na somo likaeleweka. [41]
hii
Aliongeza kuwa hii ni biashara huria hivyo atakayeona hawezi kuifanya katika kiwango hicho kilichowekwa na Ewura, anaweza kujiondoa kwani wafanyabiashara ni wengi na wanataka kufanya biashara hiyo hapa nchini. [42]
hiki
Alisema vyama vya upinzani vinatakiwa kuangaliwa kwa umakini na kwamba kipindi hiki cha kampeni wanaanza kupita katika mikoa kuomba kura kwa wananchi na kutoa lugha chafu badala ya kujenga sera itakayoweza kukubalika kwa jamii na kwamba jamii inapaswa kutambua baadhi ya Vyama vya upizanzani havina ofisi za kuendeshea shughuli na kwamba watambue maendeleo hayaletwa kwa kasfa bali kwa sera ya chama husika. [43]
hizi
Wachezaji hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakidai kwamba mechi mbili za mwanzo dhidi ya Sudan na Zambia ndizo zilikuwa zikiwanyima usingizi, hizi nyingine wana hakika watashinda. [44]
hofu
TIMU ya soka ya Prisons imewatoa hofu mashabiki wa soka nchini kuhusu ushiriki wake katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) na kueleza kuwa watajitahidi kufanya vizuri kadri ya uwezo wao. [45]
hovyo
Watu wanaongea Kingereza kwa umakini mkubwa ili wasifanye makosa, wanaogopa kuchekwa lakini lugha ya Kiswahili watu wanaiongea hovyo hovyo, hawajali kama wanakosea au la kwa kuwa hakuna mtu wa kuwacheka. [46]
huko
Katika kipindi cha miezi minne iliyopita, bei hiyo imeporomoka kwa kasi hadi kufikia dola 38 kwa pipa, lakini kushuka huko kwa bei ya mafuta katika soko la dunia hakujaathiri bei ya nishati hiyo hapa nchini. [47]
huna
Kama umeangalia vizuri wakiingia kwenye boksi lako ni hatari sana na kama huna ukuta mzuri utapata madhara makubwa, halafu wanatumia nafasi vizuri. [48]
huwezi
Si timu ya kubeza kama Senegal, huwezi kuifananisha Tanzania na Senegal, Senegal wengi hawatumii akili, lakini wana nguvu sana na wakambiza bila malengo. [49]
huyo
Kamanda huyo aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Fadhil Mohamed(60), Awadhi Bakari(30), Mganga Shaban(30), Elizabeth Makwesa(40), Hamidu Jumanne (20) na Wairina Hamisi (45) wakazi wa wilaya ya Mwanga. [50]
huyu
Baada ya kuondoka Mbunge Shiwa, kuna wabunge wa CCM walikuwepo lakini hakuna walilotufanyia kama huyu wa mwisho. [51]
ila
Mwisho nakusihi tu kuwa Usiogope kusema, ila ujue pakusemea. [52]
ile
Akimzungumzia Tegete baada ya kumuona katika mechi dhidi ya Somalia, kocha huyo alisema: ìAnacheza legelege sana ndio maana ile nafasi inamshinda, anahitaji kuwa na nguvu sana na kupewa mazoezi magumu awe na madhara. [53]
ili
Siku moja kabla ya sikukuu ya Krismasi, bei ya mafuta aina ya petroli ilipanda ghafla hadi kufikia Sh1,800 kwa lita jijini Dar es salaam, wakati mikoani ilipanda hadi kufikia Sh2,500 kwa lita na wauzaji mafuta walijitetea kuwa shehena zao za mafuta zilichelewa kutokana na meli kuhofia kupita pwani ya Somalia ambako maharamia wa Kisomali wamekuwa wakiteka meli na kudau fedha nyingi ili waziachie. [54]
ilianza
Ukiachana na madai hayo ya uongozi wa Zanzibar Heroes, Kili Stars ambayo ilianza michuano ya Chalenji kwa kufungwa na Somalia bao 1-0, jana ilionyesha soka ya uhakika na kujiamini kwa kiasi kikubwa. [55]
ina
Kwa mujibu wa mwalimu huyo, kwa sasa shule ina walimu wawili tu. [56]
iwe
Kwa upande wa mafuta ya dizeli kwa jiji la Dar es Salaam, dizeli yenye ubora wa 500ppm inatakiwa iwe Sh1,271 kwa lita na ikipanda bei ya kikomo kiwe ni Sh 1,366. Kwa dizeli yenye ubora wa 5000ppm inatakiwa iuzwe kwa Sh 1,305 na ikipanda bei ya kikomo iwe ni 1,403 kwa lita. [57]
jamani
HAYA haya jamani. [58]
jengo
Waratibu wa mchezo huo, Kanda ya Ziwa, Godfrey Gatabazi ambaye ni Mkurugenzi wa New Age Communictions na Mkuu wa Utawala wa Fedha, Kanda ya Ziwa, Lameck Mchuma walisema hayo katika uzinduzi wa mchezo huo jengo la Shirika la Mfuko wa Pensheni wa Mashrika ya Umma (PPF) jijini Mwanza. [59]
jua
Stars inaingia uwanjani baada ya Jumamosi kulazwa bao 1-0 na timu isiyo na makao, mfumo, Somalia katika mchezo wake wa kwanza uliofanyika mchana wakati wa jua kali. [60]
juzi
Hiyo haitakuwa biashara tena," alisema mkurugenzi wa kampuni maarufu ya BP, Engelort Kongoro alipozungumza na waandishi juzi. [61]
kabisa
Mandaalizi yanaendelea vizuri kabisa, kwa upande wetu viongozi tunaendelea na mikakati yetu kuhakikisha timu inashinda mechi zake tano za kwanza ili tuweze kutangaza ubingwa mapema zaidi kabla ya kumalizika kwa ligi," alisema. [62]
kali
TIMU ya soka ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars jana ilizinduka katika michuano ya Chalenji baada ya kupata ushindi wa kwanza kwa kuichapa Zanzibar Heroes kwa mabao 2-1 katika mechi kali na yenye ushindani iliyochezwa kwenye uwanja mbovu wa Nakivubo mjini hapa. [63]
karibu
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kwedihuo, katika kitongoji hicho Spita Spita, alimuomba Dk,Kigoda kumsaidia kufuatilia kwa karibu tatizo la idadi ndogo ya walimu. [64]
kata
Wakiongea na Mwananchi, baadhi ya wananchi wa kata ya Ilembo walisema kuwa kitendo cha kuondolewa mgombea wa Chadema ni sawa na kunyang`anywa tonge la ugali mdomoni kwa kuwa hali hiyo imewasikitisha sana. [65]
kibao
Lazima zipo kibao, si tu maharamia kuwatambua maharamia wenzao. [66]
kike
Akizundua mpango huo katika tarafa ya Rogoro, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo John Ng’oina alisema lengo la mpango huo ni kujenga bweni moja katika kila shule ya sekondari ya kata ili kupunguza tabia ya sasa ya wanafunzi wa kike kupanga vyumba mitaani. [67]
kile
MWEZI Julai mwaka jana kijana Abdillah Omar na wenzake watatu waliamua kutumia haki yao ya kidemokrasia kusema kile walichokuwa hawapendezeshwi nacho shuleni. [68]
kilio
Wameonya kuwa kama serikali itashindwa kusikiliza kilio chao,hawatapiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa, utakaofanyika baadaye mwaka huu. [69]
kina
Wananchi hao walidai kuwa kitongoji chao kina sifa zote za kukifanya kuwa kijiji na kwamba wakati sasa umefika wa kukipatia hadhi hiyo ili kuharakisha maendeleo. [70]
kituo
Aliendelea kueleza kwamba askari hao mgambo waliendelea kumpiga vibaya kabla ya wananchi kujitokeza na kusaidia kumwokoa na kumkimbiza katika kituo kidogo cha afya kilichopo kata ya Ipinda, ambako anasema hakuweza kupatiwa matibabu mazuri kabla ya ndugu zake kumuhamishia katika hospitali kuu ya wilaya kwa matibabu zaidi. [71]
kosa
Nasema hili kwa sababu inashangaza kuona kundi ndogo la wafanyabiashara wa mafuta nchini limeigeuza serikali kama mtoto anavyoweza kumchezea babu yake akijua kwamba hawezi kuadhibiwa kwa kosa lolote analoweza kumfanyia. [72]
kote
Tunawashauri watendaji wa serikali nchini kote kujega utamaduni kwa kufanya ufuatiliaji, badala ya kuchukua hatua baada ya mambo kuhabaribika, kwani maamuzi ya namna hiyo, mara nyingi huchukuliwa kwa jazba bila kuzingatia matatizo mengine yanayoweza kuchangia matokeo mabaya. [73]
kuacha
Kinachotakiwa ni kwa wachezaji kucheza kwa kujiamini, kuacha kufanya makosa ya kijinga ambayo yanawapa nafasi wapinzani wao kuyatumia na kuwaadhibu kwa mabao. [74]
kuamua
Tumejaribu kutathmini ushiriki wetu kwenye michuano ya Tusker na kuamua kufanya maboresho kwa kumchukua kocha Mshindo Msolla ili kuongeza nguvu kwenye benchi la ufundi. [75]
kucheza
Kocha Marcio Maximo aliwasifu wachezaji wake kwa kucheza vizuri, lakini alisema kuwa walipoteza umakini baada ya Zanzibar kupata bao la kusawazisha. [76]
kufa
Wakati wanaendelea kuangalia ile picha aliingia daktari aliyekuwa akimwangalia Kazim na kumwomba waziri afupishe mazungumzo, badala yake wamsake yule mvumbuzi wa dawa kwani isingepita saa 12 kabla ya Kazim kufa ikiwa hatapata ile dawa. [77]
kuinoa
WAKATI uongozi wa Simba ukieleza kuwa kocha Mzambia Patrick Phiri atasaini mkataba wa kuinoa timu yao katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Alhamisi katika mgahawa wa Food World jijini Dar es Salaam kuna habari kuwa mkataba huo tayari umesaini. [78]
kuja
Hivyo kwa niaba ya machifu wenzangu na wananchi, hatuitaki CCM... tunamsubiria Sambwee Shitambala mwaka ujao, ndiyo maana nimeamu kuja huku kuwaeleza," alisema. [79]
kujua
Kimsingi nilifukuzwa shule kuanzia Novemba 25 mwaka huu (2008) kwa sababu niliamua kuisema katika gazeti ili umma uweze kujua huduma mbovu zinazotolewa na shule Mungumaji ambayo ni ya serikali," anaeleza sababu ya kufukuzwa shule. [80]
kula
Burundi na Zambia zinaongoza kwenye msimamo wa kundi B kila moja ikiwa na pointi nne, ili kujiweka pazuri na kuendelea kula matoke ya mjini Jinja, Kenya inapaswa kushinda leo. [81]
kule
Ndio ndugu, mimi naitwa Kazim ni mwenye mgodi wa madini ya almasi kule Mwadui, tatizo ni kwamba hali kwa sasa imekuwa mbaya mno, nimechanganyikiwa hapa hata sijui la kufanya,” alisema akiomba ushauri. [82]
kulia
Badala yake viongozi nao waliungana na wananchi kulia kuwa wafanyabishara hawa ndio chanzo cha kupanda kwa gharama za maisha. [83]
kuliko
Walisema wao wamekuwa wakijituma zaidi kuliko watu wa vitongoji vingine vya eneo hilo na kwamba ni vizuri serikali sasa ikaheshimu mchango wao. [84]
kumbe
Huyu kafanya hivi huyu kafanya hivi kumbe huyu aliamua kwenda kufanya hivi baada ya kushindwa kumuelewa mwenzake hivi, ushanifaham. [85]
kumuua
Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [86]
kupiga
Nadhani ninyi mtakuwa mashahidi; kurasa hii nitaiboresha na zaidi ni kwamba nimeadhimia kupiga hatua. [87]
kutetea
Naiomba wizara, taasisi za kutetea haki za binadamu na asasi nyingine zinisaidie kupata shule nyingine ili niendelee na masomo. [88]
kuu
Lazaro (28) amelazwa katika hospitali kuu ya wilaya hiyo baada ya kupingwa vibaya nakundi kubwa la askari mgambo waliokuwa wakifuatilia kwake mchango wa ujenzi wamadarasa ya shule ya sekondari. [89]
kuua
Ni suala la kawaida kuua albino na damu zao au viungo vyao tunavitumia kwenye shughuli hizo za uchimbaji madini na uvuvi, watu wengi wanafanya hivyo. [90]
kuzaa
Tunasikitika tu kwamba huu uchungu hauishii katika kuzaa jamii mpya inayoongozwa na viongozi waadilifu. [91]
kwa
Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja huku wauzaji wengi wa mafuta wakiwa wamekaidi agizo la Ewura la kutaka mafuta yaanze kuuzwa kwa bei hizo mpya kuanzia jana wakati likisubiriwa tangazo rasmi kwenye Gazeti la Serikali. [92]
kwetu
Sudan na Zambia zilikuwa mechi ngumu sana kwetu, lakini nakuhakikishia hizo mbili nyingine zilizobaki tunashinda,îalisema Njoroge. [93]
la
SERIKALI imetahadharisha wafanyabiashara wanaouza mafuta kuwa wale watakaoshindwa kufuata bei elekezi iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) mara baada ya tangazo la serikali kutolewa, watakuwa wamefutiwa leseni zao za biashara. [94]
labda
Lakini nikaja kugundua kuwa ile ya wale kuongea ndiyo dawa yenyewe tofauti tu ni kwamba huenda hawa watu hawakuwa wawazi baina yao wakiwa pekee yao, labda mmoja alishindwa kujieleza. [95]
lake
Kamanda huyo alisema mara baada ya ajali hiyo madereva wote wawili walikimbia lakini, jana asubuhi dereva wa lori alijisalimisha polisi na kuwa jeshi lake linaendelea na uchunguzi ili kumtia mbaroni dereva wa Hiace na mara upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani. [96]
langu
Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni,” alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [97]
lao
Alisema kuwa wao ni wanachama wa CCM na wana kadi za CCM, lakini dhamira yao ilikuwa ni kumchagua mgombea wa Chadema kwa kuwa ndiye alikuwa chaguo lao hivyo kwa sasa hawana la kufanya. [98]
lengo
Gatabazi aliwaambia waandishi wa habari kuwa michezo hiyo inatarajiwa kuanza Januari 7 kwa lengo la kuiweka jamii pamoja kupitia mtandao wa Vodacom Tanzania katika kuinua na kufufua michezo nchini. [99]
leo
Zamani mlikuwa mnasema Ewura hawana meno, leo hii wamepata meno nendeni mkaiambie jamii kwamba Ewura wana meno na wameanza kung'ata na hivi karibuni mtaanza kusikia waliong’atwa na kupata idadi yao kwa sababu takwimu zipo na maafsa wameshaanza kazi ya kufuatilia wale walioanza kukaidi amri hiyo,"alizidi kufafanua. [100]
licha
Je, wajibu wa wakaguzi wa elimu ni nini? Inakuwaje tatizo lijulikane baada ya matokeo mabaya, na ndipo mkoa uamke na kufanya utafiti wa kupata mchawi? Hatua hiyo ya zimamoto haikustahili kuchukuliwa sasa, kwa sababu tunaamini kwamba, kama mkoa huo ungefanya vizuri licha ya udhaifu huo kuwepo, mambo yangekuwa shwari. [101]
macho
Matokeo ya darasa la saba yaliyotangazwa mwishoni mwa mwaka jana yanazidi kuonesha ni jinsi gani serikali inavyozidi kufumbia macho ushauri na mawazo mbalimbali yanayotolewa kwani matokeo yameonesha kuwa kiwango cha ufaulu kwa masomo ya Kiingereza na Hisabati kinazidi kuporomoka. [102]
madai
Katika tukio lingine, baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kideleko walimuomba Dk Kigoda aondoke na Kaimu Mkuu wa shule hiyo kwa madai ya kushindwa kuwalea wanafunzi wa shule hiyo tangu alipokabidhiwa madaraka miaka mitatu iliyopita. [103]
maduka
Afisa Uhusiano Gaudensia Simwanza aliliambia gazeti hili jana kuwa mkakati huo umekuja kufuatia ongezeko la makosa katika uendeshaji wa biashara ya dawa baridi yanayofanywa na wamiliki wa maduka ya dawa hizo. [104]
magari
Watu wanapita kwa kasi ya alQaeda, na kuzuia magari upande wa pili na pia kufanya hata foleni ya kwenda mjini ikwamekwame. [105]
magumu
Mimi nimetumia muda wangu mwingi kuziangalia timu zote kama mwanamichezo, nazijua lakini ninachoweza kukuambia ni kwamba mashindano yatakuwa magumu na yenye ushindani. [106]
maisha
Aliitaja mikoa itayoshiriki michezo hiyo kuwa ni, Tabora, Kigoma, Kagera, Mara, Shinyanga na Mwanza ambapo alisema kuwa Vodacom Tanzania inalenga kuleta mabadiliko ya maisha ya Watanzania miongoni mwa wanafamilia ya watu zaidi ya milioni tano. [107]
maji
Novemba 10 mwaka jana, wanafunzi wa shule hiyo walichoma shule hiyo wakidai uongozi wa shule unawacheleweshea chakula cha mchana ambacho uongozi wa shule ulidai kilichelewa kutokana na shule hiyo kukabiliwa na tatizo la maji. [108]
maoni
ALIYEKUWA Mkuu wa Majeshi Nchini, Meja Jenerali, Robert Mboma, amesema anaamini kitambi alicho nacho kimesababisha kushindwa katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) za ubunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini. [109]
mapya
Inawezekana kabisa Kiswahili kutumika kama njia ya kufundishia shuleni kwani kina misamiati na istilahi nyingi sana za kisayansi na teknolojia na pia utohoaji wa maneno mapya unaendelea. [110]
mbali
Ninashukuru kwa kuanza vizuri katika mashindano haya ni mwanzo mzuri ambao ninaamini nitafika mbali," Onyacha. [111]
mbele
Baruti alisema basi hilo dogo lilikuwa kwenye mwendo kasi na kwamba lilipojaribu kulipita gari lililokuwa mbele, haikuwezekana kwa kuwa kulikuwa na gari nyingine mbele hivyo kuligonga lori hilo. [112]
mfano
Alitoa mfano wa fedha za mwezi Oktoba ambazo hadi kufikia mwezi Desemba 2008 hazikuwa zimefika shuleni. [113]
mfupi
Anaishauri serikali kuzingatia umuhimu wa kuwapeleka walimu wake katika mafunzo ya muda mfupi kitu kitakachowasaidia wenyewe na wanafunzi wanaowafundisha. [114]
michezo
Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 30 baada ya kushinda michezo 10 na kupoteza mechi moja katika mzunguko wa kwanza. [115]
mingi
Alisema maduka mingi ya dawa baridi nchini hayana leseni wala vibali vya biashara hiyo huku wafanyakazi wake wakiwa hawana sifa na wala taalum inayokidhi kufanya kazi hiyo. [116]
miti
Omari anasema mbali na kusimamishwa shule alipewa adhabu ya kumwagilia maji miti saba shuleni hapo hadi itakapokuwa mikubwa. [117]
mkoa
Habari zaidi zinasema kuwa mfanyabiashara aliyehojiwa kwa saa kadhaa akihisiwa kufadhili mtandao huo aliachiwa mara baada ya kuhojiwa na wapelelezi hao kutoka nje ya mkoa wa Arusha. [118]
mkuu
Baadhi ya viongozi wapya wa msikiti mkuu mkoani Arusha wanashikiliwa na kuhojiwa na wapelelezi kutoka jijini Dar es salaam kwa tuhuma za ugaidi. [119]
mno
Pia, aliwasifu wachezaji wawili wa Stars, Cannavaro na Abdi Kassim ambao alisema waliisumbua mno ngome yake. [120]
moyo
Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [121]
mtindo
Wangekamata magari na kuyakalisha pale nusu saa, huu mtindo ungekoma papohapo. [122]
muda
Mechi hiyo ilianza huku mvua kubwa ikinyesha kwa muda mrefu katika kipindi cha kwanza, lakini iliendelea vizuri baada ya mvua hiyo kukatika katika kipindi cha pili. [123]
mujibu
Kwa mujibu wa mwongozo huo, bei ya mafuta kwa jiji la Dar es Salaam inatakiwa kuwa Sh1,166 kwa lita moja ya petroli na Sh 1,249 kwa lita moja ya dizeli. [124]
mumewe
Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [125]
mwa
Wananchi hao walitoa raia hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, walipokuwa wakizungumza na Mbunge wa Handeni, Dk Abdallah Kigoda. [126]
namna
Tunadhani kwamba, kama vikao vya namna hiyo vingekuwa vinafanyika mara kwa mara hali hiyo isingekuwa hivyo. [127]
nani
Matokeo yake, Hassanoo alisema utasainiwa mbele ya mdhamini wao, TBL akieleza: "Sisi si wahuni bwana lazima wadhamini wetu wajue tumesaini mkataba wa miaka mingapi na nani. [128]
nao
CUF wamekuja hapa tumewasikiliza sera zao na tunawasubiri kuona sera zao ni nini kama tunaona nao hawaturidhishi, basi tutajua la kufanya," alisema mmoja wao. [129]
nchi
Kamwe serikali haitawavumilia wafanyabiashara watakaokaidi agizo hilo kwa sababu nchi inaongozwa kwa sheria na haiongozwi na wafanyabiashara wala kwa utashi wa mtu," alisema Waziri Ngeleja. [130]
ndefu
SIMBA ni mojawapo ya klabu kubwa na maarufu ya soka hapa nchini ambayo ina historia ndefu ya mafanikio katika medani ya mchezo wa soka. [131]
ndogo
Kwa sababu hiyo hatuwezi kuyachukua mafuta tuliyoyanunua kwa bei ya juu na kuyauza kwa bei ndogo. [132]
ngazi
Makamba, alisema hakuna haja ya wananchi kukichagua chama cha Chadema na CUF kutokana na kuonyesha nidhamu yao na kwamba hawana uwezo wa kuleta maendeleo kutokana na kuonyesha wazi kashfa ya kumtukana kiongozi wa ngazi za juu ambaye aliwahi kuongoza nchi. [133]
nje
Wanadai kuwa bei waliyonunulia bidhaa hiyo nje ni kubwa na ni tofauti na iliyopo sasa kwenye soko la dunia. [134]
njia
Mzee Mwinyi aliwataka wanaogombea na viongozi wa vyama vya siasa kushindana kwa sera badala ya matusi, kejeli, ubabe na uongo kama njia ya kuwashawishi wananchi kuwapa kura, ili kuwapa nafasi ya kuchagua mtu na sera sahihi kwa ajili ya maendeleo na kudumisha amani katika eneo hilo na nchi nzima kwa ujumla. [135]
nne
Mechi nyingine nne za mwanzo za Yanga ni dhidi ya Prisons, Mtibwa Sugar, Moro United na Polisi Morogoro. [136]
nyumba
Kila nyumba ambapo mtoto alichaguliwa kwenda sekondari vigelegele vikasikika. [137]
nzuri
Ni kocha aliyetoa mchango mkubwa kwa timu ya Chipolopolo tunaamini tunaamini atafanya kazi nzuri ya kukinoa kikosi cha Msimbazi na kuweza kubadilika katika kipindi hiki cha Ligi kuu kinachotarajia kuanza hivi karibuni,"alisema Almasi. [138]
pa
Nadhani inaweza kutuathiri hiyo, lakini napambana kuhakikisha kwamba wapi pa kufanyia kazi baada ya kuwaona wapinzani wangu. [139]
peke
Tulikuwa wanne lakini nimefukuzwa peke yangu kwa kuwa nilikuwa mstari wa mbele katika shughuli zote tulizofanya za kufichua uovu wa shule. [140]
pekee
Alisema katika mpango huo mpya, maduka hayo ya dawa muhimu yatauza dawa zilizothibitishwa na kusajiliwa na Mamlaka hiyo pekee na hivyo kuwa na uhakika kamili juu ya ubora, usalama na ufanisi wake. [141]
picha
Ikabidi kwa kumtia moyo, ikabidi aende kwenye ofisi ambayo alikuwa akifanyia utafiti huo na kufanikiwa kupata picha yake. [142]
pili
Athuman Idd 'Chuji' aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya nahodha Henry Joseph aliandika bao la pili katika dakika ya 78 kwa shuti kali alipopiga adhabu ndogo kwa ufundi mkubwa na kumuacha kipa wa Zanzibar, Mohammed Abdallah akilamba mchanga. [143]
pungufu
Sio tu kiasi hiki cha ruzuku kinapigiwa kelele na wadau wa elimu kuwa hakitoshi bali imegundulika kuwa katika baadhi ya maeneo nchini fedha hizo hazifiki au zinatolewa pungufu. [144]
rais
Walipohojiwa kama wangeenda kwenye mkutano huo wa uzinduzi, walisema kuwa wangeenda kwa ajili kumfahamu rais huyo mstaafu kwa kuwa hawajawahi kumuona. [145]
roho
Nakufa, mkuu wa polisi unaniua, sawa mimi nimemuua albino, lakini wewe unaniua mimi kwa kunipiga kibao, imeandika wapi kwamba muharifu apigwe, kabla ya kufikishwa mahakamani,” alisema Kazim huku akikata roho. [146]
saa
Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Ramadhani Baruti alisema, ajali hiyo ilitokea juzi saa 1.15 usiku katika eneo hilo lililo wilayani Moshi Vijijini. [147]
sare
Endapo ikitoa sare au kufungwa itakuwa haina maana kwani mchezo wa mwisho itakutana na Burundi ambayo itahitaji sare yoyote kufuzu. [148]
sasa
Kwa sasa mafuta ya taa yanauzwa hadi Sh1,200 kwa lita. [149]
sauti
Jibu ni rahisi, kuwa tofauti na huko Ulaya, ugonjwa kwa upande wa Simba ni kuachiwa kwa wadhamini au wafadhili na wakati mwingine makundi ya wanachama kuwa na sauti kubwa, ushawishi kiasi cha kuingilia hata benchi la ufundi, kazi ambayo ni ya kitaalam, kiasi cha kuwakatisha tamaa makocha. [150]
sehemu
Somalia ambayo ilianza kwa kufungwa 2-0 na Zanzibar na baadaye kuitandika Kili Stars 1-0, jana haikucheza mpira kama ilivyocheza dhidi ya Stars huku wakijitahidi kushambulia na wapinzani wao, Rwanda wakionekana kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo. [151]
sera
Walisema kuwa wanahitaji mabadiliko kwani CCM imekuwa ikiwahaidi lakini hakuna mafanikio yoyote na kwamba wamechoka na chama hicho ambcho wamekuwa wasikilza kiula mara sera zake lakini hakuna zinazotekelezwa katika eneo hilo. [152]
serikalini
CCM kuzirejesha shule hizo serikalini utafanikiwa. [153]
si
Alipoulizwa kuwa ni kwanini anamtaka Sambwee Shitambala kuwa mbunge wa jimbo la Mbeya Vijijini wakati hajawahi hata kuwaongoza na pia si mzaliwa wa tarafa hiyo ya Isangati, Chifu Mpoli alisema kuwa kutokana na jinsi alivyomuona na kutafakari anaamini anaweza kuwasaidia wananchi wake. [154]
sio
Tanzania ni timu nzuri ambayo huwezi kuidharau kwa vile imefungwa na Somalia, soka ndivyo ilivyo haya mambo yanatokea wala sio maajabu. [155]
siri
Siyo siri kuwa klabu hiyo, pia inajivunia kuwa na rekodi nzuri ya mafanikio makubwa pengine kuliko zote katika Tanzania. [156]
sisi
Wachezaji hawawezi kutupangia sisi kuwa wanamtaka kocha fulani ili awafundishe wao kwa kuwa Kondic hawamuelewi wao kazi yao ni kucheza mpira, sisi kwa upande wetu tunaona kocha mzuri na ndio katupa ubingwa mwaka jana na mwaka huu sisi ndio tupo kileleni kwa pointi 30 katika Ligi Kuu ya Vodacom, alisema Madega. [157]
somo
Jumanne Maghembe pamoja na mambo mengine alisema kuwa kiwango cha ufaulu cha wanafunzi waliofanya mtihani huo katika somo la Hisabati na Kiingereza umezidi kushuka. [158]
tajiri
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [159]
tako
Lakini kwa kuwa sisi ni watu wa ukweli na uwazi, tumejiweka wenyewe ndani ya tuzo la tako. [160]
tano
UONGOZI wa Yanga umesema unaendelea na mikakati kuhakikisha timu hiyo inashinda mechi zake tano za kwanza za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara ili kutwaa ubingwa mapema. [161]
tatu
Akizungumza kwa shida jana katika wodi namba tatu hospitali ya wilaya ya Kyela alipolazwa, Dickson alisema kuwa tukio hilo la kupigwa lilimtokea Desemba 28, mwaka jana majira ya saa 11 jioni, alipofuatwa nyumbani kwake na kukutwa na mgambo hao akiwa anagema ulanzi katika shamba lake. [162]
teknolojia
Pia umeme ambao ni muhimu sana hasa wakati huu wa teknolojia ya habari na mawasiliano bado haupatikani shuleni. [163]
timu
Katika mchezo wa awali, Rwanda 'Amavubi' iliibuka na kuitandika timu ya taifa ya Somalia mabao 3-0 katika mechi ya kombe la Chalenji iliyofanyika kwenye uwanja wa Nakivubo, mjini Kampala. [164]
tu
Kama Mbunge Yete Mwaliyego ambaye alichaguliwa mwaka 2000 huyo ndiyo hatusemi kwani alikuwa anaomba kura kwa mabavu na alifikia hata kutuambia kuwa mnichague msinichague mimi ni mbunge wenu tu na alipochaguliwa hakuonekana tena hadi naye alipofariki dunia," alisema Sipiti Solomoni wa Kijiji cha Ilembo. [165]
uchungu
Kwa nini wengine wafaidi tu, sisi waishiwa tusifaidi? Tumefurahi kuona kwamba wako wengi wenye uchungu wa nchi yao. [166]
ujao
Hata hivyo, umoja wa waagizaji mafuta ulikanusha habari hizo na kueleza kuwa akiba ya mafuta iliyopo ni kubwa kiasi cha kuweza kutosha kwa mwezi mmoja mzima ujao, kipindi ambacho walisema shehena nyingine itakuwa imeshawasili. [167]
uko
Sasa Kazim ujue kwamba uko chini ya ulinzi, kwa sababu ni mgonjwa sana tutakufunga pindu hapa wakati tunaangalia namna ya kukufanyia, uko chini ya ulinzi,” alisema mkuu wa jeshi la polisi ambaye alionekana kusononeka sana kwa kifo cha yule mvumbuzi wa dawa. [168]
ukweli
Baadhi ya waumini wa msikiti wamelaani kitendo hicho na kusema kuwa habari hizo zisizo za ukweli zimepelekwa na baadhi ya viongozi wa zamani wa msikiti huo ambao waliondolewa kwa sababu mbalimbali. [169]
umma
RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, ameudhihirishia umma wa Watanzania kwamba, kwa nafasi yake anastahili kuwa ‘Mzee wa Boma’, badala ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, kutokana na kujiepushe kwake na siasa za makundi wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) za uchaguzi mdogo katika wilaya ya Mbeya Vijiji mwishoni mwa wiki iliyopita. [170]
vifaa
Taarifa za mkuu wa mkoa huyo zinaeleza kwamba, katika shule kadhaa, ufundishaji ulikuwa hafifu kiasi ikiwamo watoto kukosa masomo kwa muda kutokana na walimu kutoingia darasani, pamoja na uzembe uliofanywa katika upatikanji wa vifaa vya kufundishia hasa vitabu. [171]
vijijini
Mboma ambaye aliwashangaza baadhi ya watu walioshuhudia uzinduzi wa kampeni hizo uliofanywa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi katika kijiji cha Ilembo Mbeya vijijini. [172]
vituo
Afisa Uhusiano huyo amewahamasisha Watanzania kutumia zaidi maduka makubwa ya dawa, zahanati, vituo vya afya, hospitali na maduka ya dawa muhimu badala ya dawa baridi kwa uhakika wa afya zao. [173]
vya
Vyama vya CCM na CUF vilibaini kasoro hizo na kuweka pingamizi ambalo lilikubaliwa na Tume ya Uchaguzi. [174]
vyake
ULIPOANZISHWA Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi (MMEM) mwaka 2002, moja ya vipengele vyake muhimu ilikuwa utoaji wa ruzuku kwa wanafunzi ili kutoa msaada kwa wanafunzi kukidhi mahitaji yao ya kielimu kama vile vifaa, vitabu na mambo mengineyo muhimu katika mchakato mzima wa kujifunza na kujisomea. [175]
vyao
Katika vikao vya namna ile utasikia wazee wakisema kikao hiki kinabaraka! baraka ile ni ya wele wawili wanaojaribu kuzungumza mambo yaliyo jaa vifuani kwao na kisha kuunganisha tena wakiwa wanaanza maisha mapya yaliyokunjua vifua vyao. [176]
vyombo
Kauli hiyo ya Madega imekuja baada ya baadhi ya vyombo vya habari (si Mwananchi) kuripoti kuwa kocha huyo wa Yanga anajiuzulu na kuwa mkurugenzi wa ufundi na timu kunolewa na kocha wa vijana wa timu hiyo. [177]
vyote
Hii ni changamoto kwa viongozi wengine wanaomfuata na wanastahili kuelewa kwamba, kwa ngazi waliyofikia wao ni walezi wa taifa na vyama vyote vya siasa, hivyo wanatakiwa kujiepusha na maeneno yanayoweza kuwagawa wananchi na kuchochea uhasama. [178]
wadau
Hii ni kwa sababu kuna mambo mengi yanayokwamisha utekelezaji wa mipango na cha kushangaza serikali imekuwa kiziwi muda wote licha ya kelele nyingi zinazotolewa na wadau mbalimbali wa elimu. [179]
wadhamini
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Simba, Hassan Othman (Hassanoo) alisema jana kuwa kocha huyo ambaye alishawahi kuinoa Simba miaka ya nyuma na kupata mafanikio makubwa atasaini mkataba huo siku hiyo mbele ya wadhamini wao, Kampuni ya Bia (TBL). [180]
wako
WACHEZAJI wa Yanga, Joseph Shikokoti, Mike Baraza, George Owino na John Njoroge pamoja na Osborne Monday wa Azam wako kwenye jaribio zito leo kwenye michuano ya Chalenji inayoendelea jijini hapa. [181]
wameleta
Watu wameleta mapendekezo yao. [182]
wangu
Mheshimiwa mbunge tunakuomba Mama Kisaka (Kaimu Mkuu wa shule) uondoke naye, hatumhitaji tena hapa Kijijini, msimfukuze kazi, lakini muondoeni, mimi mtoto wangu amefeli, lakini kwa kuwa mwalimu anashindwa kuwalea wanafunzi,sitaweza kumleta mtoto wangu," alisema Edward Mgaya. [183]
wao
Serikali imedhamilia kudhibiti tabia ya wafanyabiashara hao kupandisha bei ya mafuta kwa utashi wao ingawa ni soko huria lakini ni lazime wadhibitiwe" "Mwanzo tulidhani kwamba watazingatia sheria za nchi na kuziheshimu lakini wameshindwa hivyo basi wasijaribu kuichezea hata kidogo," alifafanua Ngeleja. [184]
wapo
Ni kweli wapo wapelelezi kutoka jijini Dar es salaam wanawahoji hawa watu na mpaka sasa sifahamu jingine lolote", alisema Kamanda Basilio. [185]
watatu
Walisema kuwa kati ya wabunge watatu waliowahi kuongoza jimbo la Mbeya Vijijini, ni Shiwa (CCM) ndiye aliyeweza kuwaletea maendeleo hivyo bado anahitaji mabadiliko na kwamba msimamo wao ni kuchagua chama pinzani. [186]
watu
Kamanda wa polisi mkoani Arusha Matei Basilio alikiri kushikiliwa kwa watu hao na kusema kuwa askari wanaowahoji wametoka jijini Dar es salaam. [187]
wazazi
Mpango huu umekuja wakati baadhi ya wazazi wilayani Serengeti wakilalamikiwa na viongozi wao kwa kutoipa elimu umuhimu na thamani hasa upande wa watoto wao wa kike. [188]
wenyeji
Nchi zinazoshiriki michuano hiyo ambayo itakayomalizika Januari 10 ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Sudan na wenyeji Tanzania. [189]
wewe
Ni vizuri kuongea kutokana na tofauti zenu, na kujaribu kuzungumzia wenyewe mambo ambayo wewe unayo moyoni kuhusu mwenzio ili kwa wakati wake ajaribu kuchuja na kujifunza kukuridhisha. [190]
wote
Aliwataja wengine kuwa ni Lukwaro Mlaha (25), Halima Mchomvu (40), Mariam Manzi (50) na Salma (48), wote wakiwa wakazi wa Mwanga na kuwa wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi na kwamba hali zao zinaendelea vizuri. [191]
yake
Halmasahauri ya Wilaya ya Mbarali, George Kagomba, alisema ujenzi wa vyumba vya madarasa katika halmashauri yake, umedorora kutokana na uzembe uliofanywa na baadhi ya watendaji. [192]
yao
Hili liko wazi na kama hawatakubaliana na suala hilo ni dhahiri kwamba watakuwa wamejiondoa katika biashara hiyo kwa sababu bei hizo zimepangwa kwa kuzingatia maslahi ya taifa, yao wenyewe na maslahi ya wananchi tena kwa kushirikiana na kampuni zinazoagiza mafuta. [193]
yenu
Ndugu yenu kutoka pande hizi naomba niendelee kuwashukuru ninyi wasomaji wangu kwa hamasa na changamoto mnnazonipa. [194]
yetu
Phiri ni kocha mzuri na tunaamini ujio wake katika timu yetu utazaa matunda na tutaweza kufanya vizuri katika mzunguko huu unaoanza hivi karibuni. [195]
yote
Kabla ya kunifuta shule walinitaka nilipe michango yote ya shule ninayodaiwa, nilikuwa nadaiwa Sh 43,000 nilipeleka nusu yake, wakakataa lakini nilipopeleka fedha kamili nikafutwa na shule, huu ni uonevu. [196]
yuko
Mbunge huyo yuko katika ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo kwa wananchi wa jimbo lake. [197]
yule
Hakuna jambo la kukufanya tusikutangaze kama mgunduzi wa dawa kuponya kansa kwenye moyo, dawa yako tulimpa hadi mtoto wa rais na amepona, rais anataka akuone kukushukuru na kupanga sherehe kubwa ya uzinduzi wa dawa hii ya aina yake,” alisema waziri wa afya wa nchi hiyo siku moja alipokutana na kijana yule mwenye ulemavu wa ngozi. [198]
zako
Endapo nguvu na bidiii zaidi utazielekeza kwenye shughuli zako mwaka huu unaweza kuufurahia na kama sivyo basi utaununia. [199]
zenu
Zaidi nataka niwatakie mwaka mwema wenye baraka kwenu na kwa familia zenu, nataka pia niwakumbushe kuwa huu unaweza kuwa mwaka wa neema kwa watakao jishughulisha. [200]