Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-02-05

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
acha
Kama hii hapa chini We Makengeza, Wewe ni mwanamume au la? Kama ni mwanamume, acha kutoa viliovilio vyako vya kipuuzi kila siku maana naona unaanza kuwaambukiza hata wengine. [2]
aende
Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [3]
ajabu
Migomo na maandamano ya ajabu ajabu inatukera sana, na hii ni changamoto nyingine kubwa katika kufikia lengo la kuboresha elimu yetu. [4]
akawa
Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [5]
akitokea
RAIS Jakaya Kikwete amerejea nchini jana akitokea Addis Ababa, Ethiopia kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika(AU) akiwa mwenyekiti wa umoja huo aliyemaliza muda wake. [6]
albino
BARAZA la Habari Tanzania (MCT), limeanzisha mchakato wa kufuatilia mwenendo wa magazeti katika kuandika habari zinazohusu mauaji ya albino, jinsia, watoto na maadili ya uandishi kwa jumla, ili kubaini mapungufu na kuyafanyia kazi. [7]
alidakia
Mwishiwa mwingine alidakia. [8]
alimjibu
Pinda alimjibu kuwa Dk. [9]
ambako
Baitwa alisema maofisa hao walimzuia akiwa katika hatua za mwisho uwanjani kwa madai hakuwa na viza ya Marekani na Uingereza ambako alikuwa akipita tu. [10]
ambapo
Kitandula alisema mikopo hiyo imeweza kunufaisha Watanzania 63,211 ambapo kati ya watu hao 58% ni wanawake. [11]
ana
Kwa upande wake, Gaudiozi Ishengoma, ambaye ni wakili wa mshtakiwa wa pili Christopher Bageni, aliieleza mahakama hiyo kuwa ni jukumu la upande wa mashtaka kuthibitisha kuwa mshtakiwa ana hatia ama la, lakini kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa haumfanyi mshatakiwa kusimama na kujitetea. [12]
anaweza
Waziri Mkuu anaweza kujihakikishia hili kwa kupitia kwenye vitengo mbalimbali kufanya uhakiki wa wataalamu, kujua wangapi wanajua nini, na kwa uwezo gani. [13]
angalau
Ndio maana naipongeza serikali ya awamu ya nne ya kutambua umuhimu wa kuongeza kiwango cha elimu ili angalau Watanzania wengi wakahitimu kidato cha nne. [14]
angalia
Hebu angalia kadi za wenyewe. [15]
au
Katika mashahidi hawa wote hakuna hata mmoja aliyeweza kumuunganisha Zombe na mauaji hayo ama akiwa ofisini au katika eneo la mauaji. [16]
bado
WAKATI uongozi wa Yanga ukidai kuwa Yusuf Manji bado ni mfadhili wao, habari zilizopo ni kwamba Manji ameondoa udhamini wake wa asilimilia 100 katika klabu hiyo. [17]
baina
HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro huenda ikaingia katika mgogoro na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Morogoro Vijijini, baada ya Manispaa hiyo, kuuza kiwanja cha CCM, hali ambayo imeanza kuleta mvutano baina ya pande hizo mbili. [18]
baiskeli
KAMPUNI ya Simu ya Vodacom imekabidhi baiskeli tatu kwa waendesha Baiskeli watatu kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kimataifa ya Baiskeli kwa nchi za Afrika ya Mashariki ambayo yatafanyika Februari nane Nairobi, Kenya. [19]
bila
Kama mahakama itatilia maanani sheria itamwachia huru mshtakiwa wa pili bila kumtaka kutoa maelezo yoyote,” alidai Ishengoma. [20]
bima
Shirika hilo, lililokuwa na haki peke za kuendesha shughuli za bima nchini tangu mwaka 1967 wakati serikali ilipotaifisha mashirika binafsi, lilianza kuyumba mwaka 2000, miaka miwili baada ya serikali kulegeza masharti ya biashara na likatimua zaidi ya wafanyakazi 700 ili kupunguza gharama za uendeshaji, lakini tatizo la ufanisi linaonekana kuendelea. [21]
cha
Katika chokonoachokonoa za waandishi wa habari, ilibainika kuwa moja ya hoja ambayo jana ilikuwa ijadiliwe kwenye kikao cha Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ni hoja binafsi ya Mbunge wa Karatu, Willbrod Slaa dhidi ya tuhuma zinazomkabili Masha. [22]
chake
Kama mwenyekiti wa umoja huo, Rais Kikwete alifanikiwa kusimamia utekelezaji wa mambo mbalimbali yanayolikumba Bara la Afrika na kufanikiwa kuyapatia ufumbuzi baadhi yake na hasa kushiriki kikamilifu kutatua migogoro ya kisiasa iliyotokea katika kipindi chake. [23]
chakula
Maadhimisho hayo yalienda sanjari na watoto wanaougua saratani waliolazwa katika taasisi hiyo kushiriki katika michezo na chakula cha pamoja kwenye viwanja vya taasisi hiyo. [24]
chozi
Kocha huyo alionyesha hasira na kukaribia kumwaga chozi baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo huo. [25]
darasa
Wilaya ya Meatu mkoani Shinyanga imejipanga vilivyo ili kuzuia kuendelea kufanya vibaya katika matokeo ya darasa la saba baada ya wilaya hii kuweka mikakati ya kuinua kiwango cha elimu. [26]
dira
Vijana mnatakiwa kuwa na dira kwa sababu serikali ina dira yake, wizara zina dira zake na mashirika yana dira zao. [27]
dunia
Endapo angefananikiwa kupanda mlima huo ambao ni moja kati ya milima saba mirefu duniani angeweka historia ya dunia kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kupeperusha bendera ya Tanzania katika ramani ya dunia. [28]
es
MAWAKILI wa washitakiwa wa kesi ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara watatu wa madini na dereva teksi wa Manzese Dar es Salaam, jana waliisihi mahakama kuu kuwaachia huru washtakiwa wao kwa madai katika ushahidi uliotolewa unaonyesha hawana kesi ya kujibu. [29]
familia
Kayumba akitokea familia masikini anafaulu kuingia sekondari lakini anashindwa kuendelea kutokana na kukosa pesa ilhali jirani yake Emmy anayetoka familia inayojiweza anasonga mbele. [30]
fulani
Ni lazima ubora wa mfumo wa elimu, pia upimwe kwa kuangalia wananchi waliohitimu kiwango fulani cha elimu wanaitumiaje elimu, hata kidogo waliyoipata, kwa kujiongezea maarifa au kuzalisha maarifa mapya. [31]
gani
Slaa ameharakisha kuuliza swali hilo na kwamba alipaswa kusubiri hadi mwisho wa mchakato na kuona serikali itakuwa imechukua hatua gani. [32]
hadi
Alisema ushahidi uliotolewa na mashahidi wa kwanza hadi wa saba unaelezea jinsi marehemu walivyokamatwa na si jinsi walivyouawa. [33]
hajui
Katika ushahidi, PW36 hajui ni kwa nini DCI aliamua washtakiwe wachache kwani walikuwa ni wengi. [34]
hana
Katika kuishawishi mahakama kuwa Zombe hana kesi ya kujibu Msemwa aliieleza mahakama hiyo kuwa baada ya mauaji hayo kutokea, timu mbili za uchunguzi pamoja na Tume ya Rais iliyokuwa chini ya Jaji Musa Kipenka, ziliundwa ambazo kwa pamoja zilimuona Zombe kuwa hana hatia. [35]
hapa
Tume ya Kipenka, ambayo ilikuwa na wajumbe waliobobea katika masuala ya upelelezi, ilihoji mashahidi zaidi ya 100 na hawa 37 waliotoa ushahidi hapa ni miongoni mwao, lakini matokeo yake ilisema jumla ya askari polisi 15 washitakiwe na Zombe hakuwa na kesi,” alidai Msemwa. [36]
hasa
Mchakato huo umeelezwa kuwa utasaidia kuboresha taaluma ya uandishi wa habari hizo hasa baada ya kubaini mapungufu yatakayojitokeza na kuimarisha stadi sehemu yenye ubora. [37]
hatua
Masha anadaiwa kuingilia mchakato wa utoaji zabuni ya uchapishaji wa vitambulisho vya taifa kwa kutaka kurejeshwa kwa kampuni ambayo ilienguliwa katika hatua za awali, kitu ambacho kinaelezwa kuwa ni ukiukwaji wa Sheria ya Manunuzi ya Umma. [38]
hawezi
Dusan Kondic wa Yanga alieleza kuwa hawezi kuuzungumzia mchezo wowote hadi abakiwe na mchezo mmoja kabla ya kutangaza ubingwa. [39]
hicho
Katika hotuba yake baada ya makampuni hayo kurejesha fedha, Rais Kikwete alisema kiasi hicho kilichorejeshwa kipelekwe Wizara ya Kilimo na Chakula, lakini kauli yake ikaonekana kuwa kero kwa baadhi ya wabunge waliosema kuwa bunge ndilo linaloidhinisha matumizi ya serikali. [40]
hii
Kwa kesi kama hii utambuzi wa watuhumiwa ni jambo la muhimu sana. [41]
hili
Upande wa Mashtaka katika shauri hili unategemea sana maelezo ya washtakiwa wa 11 na wa 12 ambao wanashitakiwa pamoja na Zombe. [42]
hivi
Tunatarajia kukutana hivi karibuni ili tupange mikakati ya chama chetu kwa mwaka huu, lakini pia tunataka kuona idadi ya wachezaji gofu wanawake inaongezeka kwani bado tunaidadi ndogo ya washiriki,"alisema Malaba. [43]
hivyo
Msemwa alidai hata hivyo ushahidi wa mshtakiwa Rashid Lema (11) kwamba Bageni aliwaleza kuwa Zombe alikuwa ameagiza wafanyabiashara wachinjwe ni wa kusikia. [44]
hizi
Hata hivyo, kumekuwa na baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo wakilalamika kuwa hawapati posho za kutosha siku hizi kila wanapocheza mechi kutokanana na kuwepo kwa hali hiyo. [45]
hizo
Tuhuma hizo zimeifanya kamati hiyo kumuita Masha kwa ajili ya mahojiano, huku umma ukisubiri kwa hamu matokeo ya usaili huo. [46]
hospitali
Alihangahaika kwenye hospitali nyingi bila mafanikio. [47]
huko
Alisema baada ya kuingia kambini jana timu hiyo inatarajiwa kuondoka kesho kwenda Zanzibar na itakuwa huko hadi Jumapili na kabla ya kurudi Dar es Salaam itakuwa na mechi baina ya wachezaji wa Stars ambao watagawanywa katika vikosi viwili, kile cha kwanza cha timu hiyo na kikosi cha pili katika uwanja wa Mao Tsetung. [48]
huo
Alidai kwa kusema: “Upande wa mashtaka umetumia maelezo yao mbele ya timu ya polisi iliyowahoji na mbele ya mlinzi wa amani, hata hivyo upande huo umeshindwa kuthibitisha iwapo watuhumiwa walikiri kuhusika na kosa ingawa wameeleza kuwa walifika msitu wa Pande na kushuhudia mauaji yakitendeka. [49]
huu
Kwa mujibu wa kanuni hii, naruhusiwa kupunguza orodha ya wachangiaji na kufanya iwe ni fupi ili waziri mhusika aweze kuhitimisha muswada huu kwani kama tutaacha wote wachangie, ni hakika kuwa hatutaweza kuuhitimisha. [50]
huwa
Wadau hao wamesema kuwa wanafunzi wengi wanaokwenda kwenye shule za binafsi na zile za mashirika ya dini wengi wao huwa hawakuchaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari kwa shule za serikali hivyo hata uwezo wao ni mdogo hali ambayo inawafanya wapate muda wa kuandaliwa kabla ya kujiunga na kidato cha kwanza. [51]
huyo
Mbunge huyo alisema kuwa pato lililotokana na fedha za EPA lilikuwa ni pato jipya ambalo serikali ilipaswa kupeleka bungeni kwanza kama pato la ziada ndipo kuweka na maombi maalumu ya kutaka kuzitumia. [52]
huyu
Kama tuna jamii ya wahitimu wa viwango vile ambavyo mara baada ya kumaliza shule wakatoa talaka kwa vitabu na tabia ya usomaji; na kuwa, kwa mfano, mtu amesoma uchumi, lakini alipoajiriwa benki hajiendelezi tena kusoma, na hatimaye kubakiwa na ujuzi wa kuendesha benki, na kule nyumbani hana hata kamaktaba, ila CD za muziki na sinema tu, sidhani kama mtu huyu hatahitaji tena semina kumkumbusha kuhusu mabadiliko yanayojitokeza katika taaluma yake ya uchumi. [53]
ikiwa
Hata hivyo, Mwakalebela alisema kuwa timu hiyo ya taifa itaondoka hapa nchini Februari 19 kuelekea Ivory Coast kwa ajili ya fainali hizo ikiwa na wachezaji 23 na benchi la ufundi lenye watu sita na viongozi wa TFF, na viongozi wa serikali. [54]
ila
Sasa kama hakuna hujuma ni kwa nini wengine wabaki,? Nina imani hawa hawakuhusika ila wasiokuwepo ndio waliohusika na kuwafanya hawa kuwa kafara kwa matakwa ya wakubwa,” alidai Magafu. [55]
ile
Mbali na kuwa na uwezo wa kuchukua hatua, mamlaka hiyo piya itakuwa na uwezo wa kusitisha zabuni yoyote ile pale itakapobainika kuwa kanuni zimekiukwa. [56]
ili
Katika kesi za jinai, ili mshtakiwa aweze kusimama mahakamani kujitetea ni lazima ushahidi ulioletwa uwe ni mkubwa. [57]
imara
Mchezo huo mkali ulishuhudia timu hizo zikishambuliana na kusaka mabao na pointi, lakini safu za ulinzi za timu hizo zilikaa imara na kujaribu kuondosha hatari zote. [58]
ina
Alipoulizwa kuhusu hali hiyo, mkurugenzi huyo alisema wizara ina taarifa kuhusu maadhimisho hayo na kwamba hali hiyo inaonyesha jinsi taifa lisivyo na mwamko katika mapambano na saratani. [59]
juu
Msemwa aliongeza kuwa hata mashahidi kadhaa waliotoa ushahidi mahakamani hapo wakiwemo maafisa wa juu wa polisi waliochunguza tukio hilo na Mkurugenzi wa Mashtaka, Elieza Feleshi walithibitisha kuwa Zombe hakustahili kushtakiwa. [60]
juzi
Inawezekanaje mtu aliyekufa kupata fundisho?" alisema katika hotuba yake tulivu kwenye Hospitali ya Nairobi juzi. [61]
kabisa
Lakini kwa Tanzania tunapozungumzia kuhusu warsha tunazungumzia wingi wa wananchi ambao wamemaliza darasa la saba, au hawakusoma kabisa. [62]
kadi
Maana, jamani, hizi kadi za biashara ni kama ibada ya dini. [63]
kali
Mchezaji wa zamani wa Yanga, Kudra Omari alikaribia kuipa bao timu yake dakika ya tatu ya mchezo huo kwa shuti kali ambalo hata hivyo lilipaa na kutoka nje. [64]
kama
Hoja na ombi langu ni kwamba ushahidi wa namna hiyo usingepokelewa mahakamani,” alidai Msemwa na kuongeza kuwa hata ushahidi uliotolewa na mashahidi wengine mahakamani hapo kuwa alimuona Zombe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hauwezi kumtia hatiani katika kosa zito kama hilo. [65]
kambi
Eneo ambalo Manji ilitangazwa kujikita katika udhamini wake ni kulipia kambi, mishahara ya wachezaji, makocha, fedha za uendeshaji wa timu, posho za safari na gharama za usafiri wa ndani na nje wa timu. [66]
kansa
Ngoma alisema zaidi ya watoto milioni 3 wenye uzito mkubwa duniani, wanaugua kansa kila mwaka na kwa Tanzania kuna zaidi ya watoto 2030 wanaougua ugonjwa huo. [67]
kauli
BUNGE limepitisha kwa kauli moja ombi la serikali la kutaka nyongeza ya bajeti ya Sh 53 bilioni licha ya kuwa na vijembe vya hapa na pale kuonyesha kuwa ilikuwa ni lazima bajeti hiyo kupitishwa. [68]
kiasi
Serikali iliomba fedha hizo zilizorudishwa na makampuni yaliyoiba kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) zitumike katika nyongeza ya bajeti ya mwaka 2008/2009. Fedha hizo zilirejeshwa na baadhi ya makampuni yaliyoitikia wito wa Rais Jakaya Kikwete kutaka yarejeshe kiasi cha Sh133 bilioni zilizoibiwa kwenye akaunti hiyo. [69]
kibao
Tunafurahi sana kuona kwamba angalau mmoja wa wale tuliowaona kuwa na roho ya korosho, ambao hawajali mateso ya wananchi ili mradi wanapata posho zao, na marupurupu kibao, na uwezo wa kufisadi wapendavyo, tunafurahi kuona kwamba angalau mmoja wao ameonyesha hali ya kuhuzunika, hata hali ya kushikwa na hasira kutokana na hali hii. [70]
kidato
Katika mtihani wa kidato cha pili mwaka jana, Mbele anatamba kwamba watoto wote waliofanya mtihani walifaulu. [71]
kijana
Ndiyo maana wakitumia mwavuli wa Bunge Kivuli la Vijana ambalo lilifanyika hivi karibuni Dar es Salaam wanafunzi nao walijadili nafasi, wajibu na fursa ya kila kijana kushiriki katika uboreshwaji wa elimu nchini. [72]
kila
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, katibu mtendaji wa MCT, Kajubi Mukangaja alisema zoezi hilo litafanyika kila baada ya miezi mitatu na kutoa ripoti ambayo itasaidia katika utendaji wa kazi kwa waandishi. [73]
kile
Slaa hakuridhika na majibu hayo na badala yake alieleza kuwa serikali inapaswa kuingilia mchakato huo unaotumia kanuni za manunuzi kwa umma na siyo kuuachia hadi hali iharibike, lakini Spika Sitta aliingilia kati na kutaka lisijibiwe kwa kile alichoeleza ni kuzusha malumbano. [74]
kimataifa
Kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan aliikosesha bao timu yake, dakika ya 43 kwa shuti kali ambalo lilipanguliwa na kipa Mzungu Obren Curkovic. [75]
kina
Kituo hicho kina watoto yatima 178 na wajane 72 ambao wote hupata mahitaji ya malazi, mavazi na elimu katika eneo moja. [76]
kuacha
Pamoja na serikali kuingilia kati, tunawashauri wananchi kuliona tatizo hili kuwa kubwa, hivyo kuchukua tahadhari kwa kutunza chakula kidogo walichonacho, ikiwa ni pamoja na kuacha kutumia nafaka kupikia pombe na kuwauzia wafanyabiashara wanaosafirisha kwa magendo kwenda nje ya nchi. [77]
kuahidi
Jax akizungumza mara baada ya kukabidhiwa baiskeli hizo alipongeza Vodacom kwa msaada huo na kuahidi timu hiyo itakwenda Kenya kufanya vizuri. [78]
kuajiri
Aidha, taratibu za kuajiri upya wafanyakazi tayari zimefanyika kulingana na mahitaji ya shirika," alisema Dk. [79]
kuanza
Alisema wameamua kuanza na matukio hayo ambayo yaliitikisa nchi mwaka jana. [80]
kudai
Unajua watu wengi wanajua haki zao lakini wanashindwa kujua njia za kuzipata na hivyo kuamua kutumia vurugu kudai haki hizo," anafafanua. [81]
kufa
Wakati wanaendelea kuangalia ile picha aliingia daktari aliyekuwa akimwangalia Kazim na kumwomba waziri afupishe mazungumzo, badala yake wamsake yule mvumbuzi wa dawa kwani isingepita saa 12 kabla ya Kazim kufa ikiwa hatapata ile dawa. [82]
kufika
Alisema mkurugenzi huyo aliamua kumtuma Kaimu ofisa mipango wa manispaa hiyo,Mwaisile Lukas kufika eneo hilo ili kujionea ujenzi huo. [83]
kufundishia
Sababu kubwa ni kuwa kule kwenye taasisi zetu hakuna vifaa vya kufundishia, wala wataalamu na muda wa kutosha wa kuweza kujifundisha mambo haya. [84]
kuishi
Siku moja usiku akiwa nyumbani alitafakari sana hali ngumu ya maisha ambayo angeanza kuishi. [85]
kuja
Madega alisema katika taarifa yake kwamba mahusiano mazuri na mdhamini ndiyo yaliyofunguia milango na kuingia wadhamini wengine kujitokeza na kuja kuidhamini klabu kwani kwa sasa Yanga ipo juu. [86]
kujadili
Imefahamika jana pia kuwa mdhamini huyo na viongozi wa Yanga walikuwa na kikao juzi kujadili pamoja na mambo mengine, jinsi ya kulipa deni hilo. [87]
kula
Alisema wazazi wanapaswa kuwajengea watoto mfumo wa maisha unaojali afya na kujikinga dhidi ya saratani kwa kuwapa nafasi ya kucheza na kula vyakula vinavyofaa kwa mujibu wa kanuni za afya. [88]
kule
Je, wataalamu wetu kule shuleni wanakwenda sambamba, katika mafunzo yao, na mabadiliko haya katika masoko ya bidhaa ya TEHAMA? Ninachosema hapa ni kuwa kama nchi yetu, kama zilivyo nchi nyingi za dunia ya tatu, haitajiingiza katika uzalishaji wa maarifa na elimu kwa matumizi ya wananchi wake, na kuwa taasisi za elimu vikawa vitovu vya maarifa mapya ili wahitimu wetu watoke wakiwa sio tu washika vyeti, bali wazalishaji elimu na maarifa mapya, huenda tunaweza kupunguza utegemezi wa nje na kupunguza mahitaji ya warsha kwa ajili ya wataalamu wetu. [89]
kuliko
Baadhi ya wabunge walionekana kuwa walikuwa na mpango wa kupinga hoja hiyo kwa kile walichoeleza kuwa mpango wa serikali ulikuwa na manufaa zaidi kwa wafanyabiashara kuliko wakulima. [90]
kumbe
Maelezo haya ya askari huyu, yalinishangaza, sikutegemea kusikia kwamba kumbe mauaji haya yanaendelea kuwepo kutokana na uzembe wa watendaji wetu kusimamia majukumu yao. [91]
kumuua
Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [92]
kuna
Lakini katika shauri hili kuna ushahidi wa mazingira na si wa moja kwa moja, kuthibitisha mshtakiwa wa pili na wenzake kuwa wauaji wa marehemu. [93]
kupingwa
Mambo kama hayo na mengineyo ndiyo yanayoibuliwa na kupingwa kwa nguvu zote katika siku ya wanawake duniani. [94]
kushindwa
Magafu alidai maelezo ya shahidi wa 25 na wa 26 pamoja na maelezo ya washtakiwa wa 11 na wa 12 ulitengenezwa na upande wa mashtaka baada ya kushindwa kuwaunganisha watuhumiwa kwa kosa wanalotuhumiwa. [95]
kusikia
Walisema ushahidi wote uliotolewa ni wa kusikia tu na si wa kushuhudia kosa likitendeka. [96]
kusoma
Mafanikio makubwa yaliyopatikana hadi sasa ni vijana hao kuwa na uhakika wa kusoma muda wote bila kukatishwa masomo kutokana na sababu yoyote ile. [97]
kuwepo
Baadhi ya wabunge waliochangia katika muswada huo walionekana kuwa na wasiwasi wa namna fedha hizo zitakavyotumika na wengi waliomba matumizi hayo yatolewe ufafanuzi katika mkutano wa bunge ili kuwepo na uhakika zaidi. [98]
kuzuia
Kama angekuwa mwanamke kwenye Wizara ya Mambo ya Usalama, angeweza kuzuia ajali. [99]
kwake
Madai mengi dhidi ya asasi binafsi yamesababisha serikali kutoa tamko la kusudio la kuzifuatilia na kuzifunga ambazo zitakuwa zinakiuka malengo ya kuanzishwa au kusajiliwa kwake. [100]
la
Mawakili wa washtakiwa wote waliieleza mahakama kuwa kati ya watu 37 waliotoa ushahidi mahakamani hapo, hakuna shahidi hata mmoja aliyeweza kuithibitishia mahakama hiyo jinsi washtakiwa hao walivyotenda kosa la mauaji hayo. [101]
labda
Baba alikuwa na wasiwasi kwamba labda mwanaye angemdharau lakini mimi nilimcheka. [102]
lake
Kauli ya Mwamwaja imekuja siku chache baada ya Baraza la Waganga na Watafiti wa Tiba Asilia nchini, kutishia kumpeleka Mahakamani waziri Pinda kutokana na agizo lake la kufunga kwa muda leseni za Tiba asili. [103]
leo
Hivyo mahakama inalazimika kujiuliza ni nani walihusika katika mauaji haya maana hadi leo tuko gizani,” alidai Magafu. [104]
letu
Hali hii inatahadharisha kwamba, taifa linahitaji kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na njaa inayoweza kulidhoofisha taifa letu. [105]
licha
Akizungumzia utata wa ushahidi, Magafu, licha ya kuileza mahakama kuwa kuna mashahidi waliieleza mahakama kuwa kulikuwa na mapigano kati ya polisi na majambazi, alidai inasikitisha kuwa katika mashahidi hao wengine wanasema mauaji yalifanyika Sinza na wengine msitu wa Pande. [106]
ligi
Wakati Mkurugenzi wa Ligi Kuu ya England, Phil Lines alisema, "Tunaona ni mafanikio makubwa kufikia makubaliano harana na Multichoice ili watu wa Kusini mwa Jangwa la Sahara waendelee kuona ligi hii. [107]
lugha
Mafunzo hayo yalilenga kuwapa stadi wanafunzi hao wayazoee mazingira na lugha ya kufundishia kabla ya kuanza mafunzo kamili ambayo masomo yote isipokuwa Kiswahili na mawasiliano ya kila siku ni kwa Kiingereza. [108]
maana
Hapana shaka kuwa hawa ndio walioua maana hakuna ushahidi unaowaunganisha hawa walioko mahakamani hapa. [109]
mafao
Kibola alieleza kuwa wafanyakazi wote wa shirika hilo lililoanzishwa mwaka 1963 wameachishwa kazi na walitarajiwa kulipwa mafao yao kuanzia jana. [110]
maisha
Dk Kisyombe amesema Mkopo wa Sh bilioni moja uliotolewa na SELF wameupata kwa wakati muafaka; na kwamba mkopo huo utawasaidia kuboresha maisha ya wakinamama ambao ndio wateja wao. [111]
maiti
Baba mmoja akaniambia mtoto wake akamshtukiza akilia mbele ya luninga kwa kuona maelfu ya maiti yaliyorundikana. [112]
makala
Lakini wanapohitimu, nawahakikishia wasomaji wa makala, wanafunzi wote kama sio wengi, watakuwa hawawezi kufanya hivyo. [113]
makao
Inadaiwa baadhi ya asasi hazina hata ofisi wala makao yanayoeleweka na pia inadaiwa zinatumia matatizo ya watoto yatima au wale waishio katika mazingira magumu kujinufaisha. [114]
mapema
Akizungumzia suala hilo ofisa mipango wa manispaa hiyo, alisema manispaa yake ilishaweka pingamizi hilo mapema  katika hatua za awali na kwamba, kwa sasa wapo katika majadiliano kuona jinsi gani ya kutatua mgogoro huo. [115]
mapya
Tunapozungumia ongezeko la warsha, semina na kadhalika tujiulize kama mfumo wetu wa elimu una uwezo wa kuzalisha maarifa mapya. [116]
mara
Mwananchi iliripoti kwa mara ya kwanza Jumatatu iliyopita juu ya utata wa udhamini huo wa Manji katika klabu hiyo na hata kuikopesha fedha wakati ikijiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Etoile d'Or Mirontsy ya Comoro. [117]
matukio
Tumeanzisha mchakato wa kufanya utafiti juu ya matukio yanayojitokeza nchini na kuyatolea taarifa yake kila baada ya miezi mitatu. [118]
mdhamini
Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega alisema jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa Manji bado ni mdhamini mkuu na mafanikio yote ya klabu ni yametokana na udhamini wake. [119]
mdogo
Pia huficha ukweli kuwa uwezo wa walimu wengi ni mdogo na hufanya kazi katika mazingira magumu. [120]
mfupi
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [121]
miezi
Msemaji wa wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja, alisema wizara inatarajia kutangaza utaratibu mpya kuhusu leseni za waganga hao wa jadi ambao wamempa waziri mkuu, miezi miwili kubadili kauli yake. [122]
migomo
Mdoe aliwashukia wanafunzi wanaoabudu migomo na maandamano ya mara kwa mara akiitaja kuwa ni miongoni mwa mambo yanayokwamisha dhamira iliyopo ya kuboresha hali ya elimu kwa vijana nchini. [123]
mikoa
Pinda alitoa kauli hiyo alipokuwa ziarani mikoa ya Kaskazini kujionea mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambayo watu wanaamini kuwa yanatokana na imani za kishirikiana zinazowahusisha waganga wa jadi. [124]
mimi
NIANZE kwa kusema kuwa mimi naungana na Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda kuhusu katazo lake la warsha, semina, kongamano, mafunzo, semina elekezi na majina mengine mengi yenye kusudio moja kama lengo lake ni kudhibiti matumizi yasiyo ya faida ya fedha za wavuja jasho. [125]
minne
Baadaye utaratibu huo ulibadilika mafunzo yakawa yanatolewa kwa kipindi cha mwaka mzima kabla ya mwanafunzi kuanza rasmi kuhesabu miaka minne ya kuwa sekondari kwa ajili ya kidato cha kwanza hadi cha nne. [126]
misingi
Hivyo naiomba mahakama imwachie huru mshtakiwa wa pili kwa misingi kuwa hana kesi ya kujibu. [127]
mkewe
RAIS wa Kenya, Mwai Kibaki na mkewe wametofautiana hadharani kuhusu suala la nani wa kulaumiwa katika matukio mawili ya moto yaliyosababisha karibu watu 1456 kupoteza maisha. [128]
mkuu
Naye Mkurugenzi mkuu wa SELFINA Dk Victoria Kisyombe ameishukuru SELF kwa kuiamini SELFINA. Dk Kisyombe ameendelea kusema kuwa SELF imekuwa na uhusiano mzuri na Asasi ya SELFINA tangu mwaka 2002, na katika kipindi hicho SELFINA imefaidika kwa kujengewa uwezo wa kifedha, mafunzo na ukarabati wa ofisi ili kuweza kutoa huduma zake kwa ufanisi. [129]
mno
Pili kama waziri katika mkutano wake na makamanda hao wageamua kutoa kiasi fulani cha pesa kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwa wauaji au waganga wa kienyeji, naamini wote wangenaswa kirahisi mno. [130]
mrefu
NDOTO ya Mtanzania, Respicius Baitwa, wa mjini Moshi kwenda kupanda mlima Aconcagua wa Argentina ambao ni mrefu kuliko yote Amerika Kusini imeyeyuka baada ya kuzuiwa Uwanja wa ndege nchini Kenya. [131]
msaidizi
Jamaa huyo ambaye alikuwa kama msaidizi wake wa karibu, alikuwa akimuwakilisha katika kazi mbalimbali na ndiye aliyekuwa ana siri zake nyingi. [132]
mstari
Katika hilo alikuwa mstari wa mbele na kukubali kupeleka wanajeshi wa Tanzania kushiriki katika operesheni hiyo. [133]
muda
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imesema itatolea taarifa rasmi kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu kuzifunga kwa muda leseni za waganga wa jadi. [134]
mwa
KAMPUNI ya Multichoice imefanikiwa kupata haki za kuonyesha moja kwa moja mechi za Ligi Kuu ya England kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, awali haki hizo zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Gateaway Broadcating Service (GTV) ya Uingereza ambayo inadai imefilisika. [135]
mwezi
Ligi hiyo imeahirishwa kwa muda hadi Machi ili kuipa nafasi timu ya taifa, Stars kujiandaa na michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) zitakazofanyika nchini Ivory Coast baadaye mwezi huu. [136]
mzazi
Watoto yatima yaani wasio na baba na mama na waishio katika mazingira magumu hulipiwa gharama zote na asasi hiyo wakati wale wenye mzazi mmoja hupata punguzo. [137]
nao
Kwa hiyo rai yangu ni kwamba washtakiwa wote waachiwe huru kwa kuwa inaonekana hawana hatia wala kesi ya kujibu isipokuwa mshtakiwa wa 11 na wa 12 kama mahakama itaona kuna ushahidi wa kutosha ndiyo, lakini yawezekana nao walidanganywa,” alidai Magafu. [138]
naye
Katika sheria zetu hakuna kifungu kinachosema mtu akishuhudia kosa linatendeka hata kama ni la mauaji basi naye anakuwa na hatia,” alidai. [139]
ndani
MASHABIKI na wadau mbalimbali wa soka nchini wanaotaka kwenda kuishangilia timu ya taifa ( Taifa Stars) katika fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) watalazimika kulipa dola 1,167, karibuShilingi 1,571, 400 za Kitanzania. [140]
ndio
Hakuna ubishi kuwa watu walikufa, lakini upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kuwa washtakiwa ndio waliowaua,” alidai. [141]
ndiye
Lucas alikiri kuwepo na mapungufu katika kutoa umiliki wa kiwanja hicho kwa watu wawili na kwamba halmashauri hiyo, inatambua kuwa CCM ndiye mmiliki halali wa kiwanja,kwani mmiliki wa pili ameanza kumiliki mwaka jana. [142]
ndugu
Katika kesi hiyo, Zombe na wenzake wanatuhumiwa kuwaua kwa makusudi wafanyabiashara watatu wa madini kutoka wilaya ya Mahenge mkoani Morogoro ambao ni Sabinus Chigumbi, maarufu kama Jongo, na ndugu yake Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe Juma na dereva teksi wa Manzese jijini Dar es Salaam. [143]
ngapi
Wanaonibisha, waniambie wameangalia kweli kadi ngapi katika hizo alizopewa katika miezi sita iliyopita. [144]
ni
Wakitoa hoja zao za kuishawishi mahakama kuamini kuwa washtakiwa hao hawana kesi ya kujibu, mawakili hao kwa nyakati tofauti waliieleza mahakama hiyo kuwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo hauwahusishi na tuhuma za mauaji hayo moja kwa moja na badala yake ni ushahidi wa mazingira tu. [145]
nia
Aliongeza kuwa ingawa Zombe yuko mahakamani, hakustahili kuwa mshtakiwa bali alistahili kuwa shahidi huku akidai kuwa ameshitakiwa kwa nia mbaya tu. [146]
nini
Naye Wakili Majura Magafu aliieleza mahakama kuwa hata mashahidi waliotoa ushahidi mahakamani hapo hawakuweza kuwatambua askari waliofika katika eneo la tukio na kuhoji ni kwa nini halikuwahi kufanyika gwaride la utambuzi kwa kosa kubwa kama hilo. [147]
niwe
Lakini wangapi wameonyesha nia ya kwenda kuona hawa wahanga wenyewe na kutafuta usuluhisho? Nakumbuka msemo mmoja wa hayati Trevor Huddleston aliyekuwa mstari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi 'bora niwe na damu mkononi kuliko maji kama Pilato'.’ 'Una maana gani?' 'Namaanisha hivyo. [148]
nyingi
Ikumbuke kwamba, tatizo hili si la Tanzania peke yake, bali limezikumba nchi nyingi barani Afrika. [149]
nyingine
Kibola akizungumzia huduma za shirika hilo ambazo ni pamoja na bima ya maisha na nyingine. [150]
nzuri
Naikubali kazi yake nzuri anayoifanya kwenye ofisi yangu," Kibaki aliongeza akiwa pamoja na Saitoti na mawaziri wengine. [151]
ofisi
Naye Wakili wa Serikali kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Vicent Tango ametoa wito kwa SELFINA kuendelea kuwa wateja wazuri kwa kuzingatia masharti ya mkataba kwa mkopo husika. [152]
one
HALIKUWA jambo la ajabu kukuta baadhi ya shule za sekondari za binafsi na za dini zikitoa mafunzo ya awali ya sekondari kwa wanafunzi wake maarufu kwa Kiingereza kama Pre form one. [153]
picha
Alisema mchakato huo kwa mwaka huu utaanzia kwenye magazeti kwa kuangalia umakini, usahihi, mapungufu ya habari pamoja na picha zinazochapishwa kuhusu mambo hayo. [154]
rangi
Ninafundisha pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kozi ambazo mwanafunzi anatakiwa kujua kupiga picha za video, kuhariri habari au picha kwa ajili ya televisheni au redio; kuchanganya rangi kwa ajili ya maigizo ya jukwaani, sinema au televisheni, aweze kupiga picha za analogi na za "digital", waweze kutengeneza sinema au vipindi vya redio, au waweze kutengeneza kurasa za tovuti na kusanifu kurasa za magazeti. [155]
roho
Wanaume wa kweli tutamwelewaje? Narudia kusema, mwanasiasa anapaswa kuwa na roho ngumu kama jabali ya Mwanza. [156]
saa
Hakuna kitu," alisema mfanyakazi mmoja ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alipozungumza na Mwananchi majira ya saa 11:00 jioni. [157]
sasa
Katika swali la msingi, Faki aliitaka serikali kutoa maelezo ya maboresho ya mfumo wa manunuzi wa umma kwa kuzingatia kuwa umekuwa ukilalamikiwa kwa sababu taratibu za sasa haziko wazi na zinaruhusu ufisadi. [158]
sawa
Imekuwa vizuri mechi zote za ligi hii kuchezwa Dar es Salaam, hivyo nadhani TFF itakuwa makini zaidi kuhakikisha mambo yote yanakwenda sawa,"alisema Agila. [159]
sekta
Waziri Mkuu wa Bunge hilo lililoshirikisha vijana kutoka vyuo na shule mbalimbali za Dar es Salaam, Christopher Mdoe anasema, kuingia kwa siasa katika sekta ya elimu kumechangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa ubora wa elimu nchini na akaiomba serikali na wanasiasa kuacha mchezo wa kuingiza siasa shuleni. [160]
shida
Baadhi ya walezi na wazazi hawakuona shida yoyote wala gharama waliyotumia kuwapeleka watoto wao kwenye shule hizo. [161]
si
Mawakili hao pia waliuchambua ushahidi uliotolewa dhidi ya wateja wao na kuieleza mahakama kuwa unajichanganya kwa maelezo kuwa mashahidi hao wamekuwa wakipingana katika maelezo yao, jambo ambalo mawakili hao walisema linaacha utata kwa mahakama kujua ushahidi upi ni wa kweli na upi si wa kweli. [162]
sio
Alikunwa na vijana hao kwa kuonesha kivitendo dira waliyonayo kwa kujikusanya kupitia Bunge Kivuli la Vijana ambalo linawapa njia ya kujiandaa kuja kuwa viongozi wa kuzitumikia jamii zao sio kwa cheo tu bali kwa kazi. [163]
soka
Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu alisema jana jijini Dar es Salaam kwamba wanajisikia faraja kurejesha ligi hiyo maarufu kwa wapenda soka wa Tanzania hasa baada ya kupata haki hizo. [164]
somo
Pia shule ina kompyuta 30 kwa ajili ya kufundisha somo la teknolojia ya habari na mawasiliano. [165]
suala
Lakini shahidi hawa watatu hawakuwahi kupelekwa katika gwaride la utambuzi ingawa uchunguzi wa suala hilo ulifanywa na maafisa wa juu wa polisi. [166]
tabia
Aliwataka wabunge kuwa makini kwa kuhakikisha kuwa hawaelezi chochote kilichojadiliwa kwenye kamati hizo kwa kuwa katika siku za karibuni kumekuwepo na tabia hiyo. [167]
tayari
Katika swali la msingi, alitaka kujua hatua ambazo serikali inachukua dhidi ya Masha baada ya kuonekana kukiuka taratibu za manunuzi kwa kulazimisha kampuni ambayo tayari iliondolewa kwenye mchakato, irejeshwe. [168]
tiba
Kwa mujibu wa Mwamwaja suala la leseni la waganga wa jadi limefika rasmi wizarani na wizara inalifanyia kazi kwa kuandaa utaratibu mbadala kwa kuwa ndio yenye dhamana ya kutoa leseni za tiba ya kisayansi na tiba za jadi. [169]
tuna
Pia shule inawapa nafasi hata wale watoto ambao sio yatima tuna unafuu wa ada kwani lengo letu si biashara ila kuwapatia elimu watoto wote wa Kitanzania bila kubagua wakoje na wanaishije," amesisitiza Mbele. [170]
ujenzi
Alisema baada ya kufuatilia, walikuta mtu huyo ameanza kujenga na ndipo walipoamua kutoa taarifa katika manispaa hiyo na kuamua kuweka pingamizi la kuzuia ujenzi katika kiwanja hicho. [171]
ujumla
Alisema kampuni hiyo imewadhamini waendesha baiskeli hao kama sehemu ya mchango wake katika maendeleo ya michezo na jamii kwa ujumla wake. [172]
uko
Sasa Kazim ujue kwamba uko chini ya ulinzi, kwa sababu ni mgonjwa sana tutakufunga pindu hapa wakati tunaangalia namna ya kukufanyia, uko chini ya ulinzi,” alisema mkuu wa jeshi la polisi ambaye alionekana kusononeka sana kwa kifo cha yule mvumbuzi wa dawa. [173]
upya
SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC), ambalo ni kongwe na kubwa kuliko taasisi zote zinazotoa huduma hiyo nchini, jana lilianza kutekeleza mchakato wa kuachisha kazi wafanyakazi wake wote na kuwaajiri upya ili liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. [174]
ushindi
Katika kipindi hicho, kila timu ilijitihadi kusaka bao, lakini bila mafanikio, ingawa kwa kiasi kikubwa Yanga ilionyesha zaidi dhamira ya kupata ushindi na kuhitaji ushindi katika mechi mbili ili kujitangaza bingwa. [175]
usiku
Kuonyesha kweli imeanza kazi, Multichoice imetangaza mechi zitakazoonyesha na Super Sport 7 wikiendi hii, wakianza na Jumamosi Manchester City v Middlesborough saa 9:45 Alasiri, Chelsea v Hull City Saa 12 jioni na Liverpool v Portsmouth saa 2:30 usiku. [176]
utoro
Mikakati mingine ya wilaya ni kudhibiti utoro wa wanafunzi ili kuhakikisha wanafunzi wote wanafika na kuingia darasani na pia kuhakikisha wanaoandikishwa darasa la kwanza wanamaliza darasa la saba. [177]
vema
Shoga ni vema ukafahamu kuwa yapo mambo mengi yanayowakabili wanawake duniani, hayo ndiyo yanayoibuliwa katika siku hii inayoadhimishwa kimataifa ingawa kila nchi inaweza kuwa na kauli mbiu yake kutegemeana na changamoto zilizomo ndani ya nchi husika. [178]
vifaa
Hukimbilia dawa hiyo kama njia ya kuficha udhaifu wa serikali yenyewe kushawishi ujenzi wa shule nyingi bila walimu wa kutosha na vifaa. [179]
vile
Licha ya kukubaliana na kauli hiyo, mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe alisimama na kutumia zaidi vifungu vya katiba ya Jamhuri ya Muungano na vile vya kanuni za bunge akisema kuwa baadhi ya vifungu vilikiukwa katika kuwasilishwa kwa muswada huo. [180]
vipi
Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni,” alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [181]
vita
Siku ya wanawake Duniani ilipata msukumo mpya mwaka 1915 yalipofanywa maandamano makubwa huko Bern Switzerland yakishinikiza kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia. [182]
vitabu
Pamoja na uchanga huo shule imekamilika kwa maana kuna maabara kwa ajili ya kuwezesha wanafunzi kujifunza masomo ya sayansi bila matatizo na kuna maktaba inayotoa fursa wanafunzi kusoma vitabu vya ziada. [183]
vituo
Mbele anatoa ushauri kwa serikali iangalie uwezekano wa kuvipatia ruzuku vituo ambavyo vinashughulikia kuwasomesha watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu hapa nchini ili watoto wengi zaidi wasikose haki hiyo ya msingi maishani. [184]
vumbi
Fainali hizo cha CHAN, zitaanza kutimua vumbi kuanzia Februari 22 hadi Machi 8 nchini Ivory Coast. [185]
vya
SPIKA wa Bunge, Samweli Sitta amewaonya wajumbe wa kamati za kudumu za bunge kutotoa taarifa kwa waandishi wa habari katika siku ambayo Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ilikuwa inamuhoji Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurence Masha, kuhusu zabuni ya uchapishaji vitambulisho vya utaifa. [186]
vyake
Kweli wale watu walimuua yule albino na kwenda na viungo vyake kwenye maeneo ya biashara. [187]
wakuu
Afisa uhusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ambao ni wadhamini wakuu wa Stars, Teddy Mapunda alisema kuwa maandalizi ya timu hiyo yamekamilika kwa kiasi kikubwa na wako bega kwa bega kuakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika fainali hizo. [188]
wangu
Napenda kumhakikishia waziri wangu wa usalama, Mhe. [189]
wapi
Kama semina hiyo ingekuwa na matunda tugeona mawaziri wakifanya kazi kama mchwa kumsaidia rais, lakini wapi hawana lolote wamebaki kupiga siasa tu. [190]
wapo
Alidai katika mashahidi hao wapo wanaosema marehemu aliuawa katika ukuta wa Sinza Posta, lakini wengine wakaeleza kuwa mauaji yalifanyika katika msitu wa Pande Mbezi Luis. [191]
wasio
Pili inawahudumia wajane na tatu imejenga Shule ya Sekondari ya Tushikamane kwa ajili ya watoto inaowalea na wengine wasio yatima. [192]
wetu
Bila shaka mafanikio yaliyopo yanatokana na uongozi madhubuti uliokuwepo ambao unashirikiana vizuri na mdhamini wetu pamoja na mdhamini mwingine, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)," ilisema sehemu ya taarifa ya Madega. [193]
wewe
Je, wewe kijana wa Tanzania una dira gani? Na unatumia juhudi gani ili kufikia dira hiyo?" alihoji na kuongeza kuwa serikali inatambua umuhimu na mchango wa vijana katika nchi kwa kuwapa nafasi ya kujadili na kuhoji mambo yanayoendelea ndani na nje ya nchi. [194]
wiki
Moja ya habari ambazo ziliandikwa na vyombo vya habari wiki hii ni juu ya taarifa kuwa Masha aliingilia mpango wa utoaji wa zabuni ya uchapishaji wa vitambulisho vya taifa, kwa kutaka moja ya kampuni zilizoondolewa katika hatua za awali za mchakato irejeshwe. [195]
yapo
Sitta alikataa swali hilo lisijibiwe kwa maelezo kuwa masuala yote mawili yapo kwenye uchunguzi na kwamba kuingilia kunaweza kuathiri mikakati hiyo. [196]
yetu
Hayo yote yanaonyesha jinsi alivyokusudia kulisaidia bara hili na tunaamini mchango wake utaendelea kuwa kielelezo na kumbukumbu kwa vizazi vijavyo, hivyo kuijengea heshima nchi yetu mbele ya jumuiya ya kimataifa. [197]
yeye
Alisisitiza kuwa yeye kama spika wa bunge atahakikisha kuwa atakayekiuka kanuni hizo anachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria hizo zinazoliongoza bunge. [198]
yeyote
Katika hali ya kushangaza maadhimisho hayo yalifanyika bila kuwepo kwa mwakilishi yeyote wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, tofauti na ilivyozoeleka katika maadhimisho mengine kama vile ya Siku ya Ukimwi Duniani. [199]
zamani
Imeelezwa ofa hiyo italenga kuwalahisishia wateja wa zamani wa GTV ambao sasa watalazimika kununua king'amuzi tu na baada ya hapo watatumia madishi yao ya zamani ingawa watalazimika kufanya marekebisho kidogo tu ili waendelee kujinafasi kwa raha zao. [200]