Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-28
Mandhari
Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz
- aaah
- Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu, alijisemea Kazim. [1]
- aende
- Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [2]
- afe
- Si bora afe tujue moja. [3]
- akawa
- Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [4]
- akina
- Sawasawa wakati akina Mkombozi wanasota kwa mguu. [5]
- ama
- Wanafunzi hao walidai kuwa mfumo unaotumiwa kuchambua uwezo wa kiuchumi wa mwanafunzi na familia yake (means testing), unawabagua na hivyo kutaka sera hiyo isitishwe ama wanafunzi wote wapewe mkopo kamili ili wamudu kusoma bila ya matatizo. [6]
- ambacho
- Jibu: Kitu kimoja ambacho kimenifurahisha katika kufikia malengo ya kazi yangu ni kuweza kushirikiana na wenzangu wote katika kuhakikisha kwamba tunafikia malengo tuliyojiwekea katika kujenga uhusiano mzuri na Tanzania. [7]
- ambako
- Mfano wa hali hii ni uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wa Kenya mwaka jana ambako tukio la uvurugaji matokeo ya uchaguzi lilifanyika waziwazi na kulazimika Rais Mwai Kibaki kutangazwa mshindi huku sherehe za kumwapisha zikianza. [8]
- ambazo
- Alizitaja kata hizo ambazo hazina shule za sekondari mkoani Rukwa kuwa ni Ugala na ilunde Ilele ,Utende Urwila Mtapenda, Ndende na Machimboni na Kibaoni na Katuma katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda. [9]
- ana
- Akiuzungumzia mchezo wa leo Phiri alisema wana kikosi chake kipo kamili na ana matumaini ya ushindi. [10]
- anasema
- Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Juma Duni Haji anasema kuwa watafanya mkutano mkubwa wa kukumbuka tukio hilo katika viwanja vya Kibandamaiti, Januari 30 mwaka huu. [11]
- au
- Pia washitakiwa hao wanatakiwa kila mmoja kutoa nusu ya fedha zilizoibwa kama dhamana, ambayo ni zaidi ya Sh50 bilioni au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha. [12]
- bado
- Hata hivyo, waashitakiwa hao walikana mashitaka na upande wa mashitaka ulidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. [13]
- baina
- Maandamano na mgomo huo ulitawaliwa na mapambano na mshikemshike mkali baina ya askari wa kutuliza ghasia wa serikali na waandamanaji huku baadhi yao wakipoteza maisha, wengine kupata ulemavu na wengine kuyahama makazi yao na kuwa wakimbizi wa kivita. [14]
- bali
- Mwambieni Rais Kikwete kuwa mauaji sio suluhu la migogoro ya kisiasa na kwamba siku zote anayetetea haki haogopi kufa, bali anayedhulumu ndie anayeogopa kufa, kwa hiyo tutaendelea kudai haki yetu na kamwe hatotufumba midomo kwa maneno wala risasi," anasistiza Duni. [15]
- bara
- Mauaji haya yalitokea wakati viongozi hawa bado wakiwa madarakani na ndio waliosimamia kwa kuleta askari kutoka Tanzania bara hivyo hawana uchochoro wa kukwepa mkono wa sheria kwa hili," anasema Mussa. [16]
- baraza
- Augustine, Dk Charles Kitima kwenye warsha ya baraza na wahariri wa vyombo vya habari iliyofanyika hivi karibuni, Dar es Salaam. [17]
- beki
- Ngassa aliyeingia kwenye marumbani na klabu yake Yanga kwa kudaiwa kumzuia asijiunge na timu ya Lov-Ham, alifunga bao lake hilo baada ya kuwapiga chenga beki wa Mtibwa, Chaha Marwa na kipa wake Shabani Kado na kutumbukiza mpira wavuni kwa shuti. [18]
- bungeni
- Lakini ufa katika ushirikiano wa vyama hivyo uliongezeka kuelekea uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini kujaza nafasi iliyoachwa na marehemu Richard Nyaulawa na unaweza kusambaratisha kambi ya upinzani bungeni. [19]
- chuoni
- Vyanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Chuo Kikuu hicho vililiambia Mwananchi jana kuwa serikali iliuagiza uongozi wa chuo kufanya mchakato huo baada ya kubaini uzembe huo wa kutodahili wanafunzi wanapowasili chuoni. [20]
- dhidi
- TANZANIA kwa mara ya kwanza imeungana na nchi wananchama wa Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya mauaji ya kikatili dhidi ya Wayahudi yaliyofanywa na utawala wa dikitekta Adolf Hitler huko Ujerumani. [21]
- dua
- Kama ilivyo kawaida kwa ndugu jamaa na marafiki wa waliopoteza maisha yao pamoja na uongozi wa CUF kila ifikapo Januari 26 na 27 hukusanyika katika maeneo mbalimbali kuwakumbuka na kuwaombea dua marehemu hao. [22]
- dunia
- Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Hassan Mwendapole, alithibitisha kutokea tukio la kudhaniwa mtumishi wao kafariki dunia na baadaye kuonekana akiwa hai na kulieleza tukio hilo kuwa ni la kushangaza na kustaajabisha. [23]
- es
- Masharti mengine ya dhamana ni kuwasilisha hati zao za kusafiria, kutosafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kuwa na kibali cha mahakama na kuripoti katika ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) saa 2:00 asubuhi kila Ijumaa. [24]
- faida
- Naye Rais wa Chama hicho John Mwangakala alilishukuru TFF kwa kuona umuhimu wa kusaidia vituo vyao ambao msaada huo utawapa fursa walimu wa vijana hao kuweza kutumia mipira hiyo kwa faida ya maendeleo ya mpira. [25]
- faini
- Mbali na adhabu hiyo katibu huyo alisema klabu hiyo pia inatakiwa kulipa kiasi cha Sh 300,000 nyingine ikiwa ni faini inayotokana na mashabiki wake kuingia uwanja kushangilia baada Yanga kupata bao na mara baada ya mchezo namba 68 kati yake na Prisons kumalizika. [26]
- garden
- MGOGORO uliopo muda mrefu kugombea kiwanja namba 951 kilichoko Mikocheni jijini Dar es Salaam kati ya mmiliki wa baa ya Rose garden, Damas Assey na mmiliki wa mradi wa Dar Village, kampuni ya ZEK Group, Zaddock Koola, umeingia katika hatua mpya. [27]
- geti
- Aidha Mwakalebela alisema kamati imeitaka klabu ya Villa Squad kulipa kiasi cha Sh 500,000 ikiwa ni faini baada ya wachezaji wake kuruka geti badala ya kupitia mlango maalumu wakati wa kuingia uwanjani katika mchezo namba 67 kati yake na Simba, huku na kulipa faini ya Sh, 300,000 ikiwa ni adhabu inayotokana na mashabiki wake kuvunja geti na kuingia uwanjani wakati wa mchezo namba 63 kati yake dhidi ya Prisons. [28]
- hajui
- Kauli hiyo ilionekana kumchanganya sana Kazim, akawa hajui la kufanya. [29]
- hao
- Washitakiwa hao walipandishwa kizimbani saa 9:00 alasiri huku Liyumba akisomewa mashitaka matatu na Kweka shitaka moja. [30]
- hapa
- Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini, Oscar Fernandez Taranco, alisema kama jamii zitaweza kuvumiliana katika tofauti zao za kiitikadi, itasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza machafuko yanayoleta maafa makubwa. [31]
- hapana
- Jibu: Hili si swali la kujibu ndiyo au hapana. [32]
- hasa
- MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Daniel Ole Njoolay, ametangaza azima yake ya kuwachukulia hatua madiwani wa CCM walioshindwa kutelekeza ilani ya chama hicho,hasa katika kuwaletea wananchi maendeleo. [33]
- hawa
- Sikiliza kaka, hili suala la udahili kufanyika ni shinikizo kutoka serikalini kwa sababu hawa wanafunzi hawakufanyiwa udahili toka awali na huu ulikuwa ni uzembe. [34]
- hayo
- Baada ya kutolewa masharti hayo mmoja wa mawakili wanaomtetea Liyumba, Alexander Kyaruzi alisimama na kuieleza mahakama kuwa wanazo hati za mali kwa ajili ya dhamana kwa mshitakiwa wa kwanza. [35]
- hii
- Tanzania inasikitishwa sana na hali hii na tunapenda kutoa pole kwa familia za wahanga wote wa mauaji hayo ya kusikitisha, ni jukumu letu sote kukemea kwa nguvu zote vitendo hivyo vya kikatili," alisema Msechu. [36]
- hili
- Mara baada ya kuanza kazi, Gavana wa sasa wa BoT, Profesa Beno Ndulu alisema atafuatilia suala hili ili kubaini kama kuna ubadhilifu katika mradi wa kujenga majengo hayo pacha na lile la Zanzibar. [37]
- hivi
- WAKATI Simba ikishuka kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salam kuvaana na Prisons, kocha wa timu hiyo Partick Phiri amekubali kuwa Yanga wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa na kusema hivi sasa wanaisaka nafasi ya pili tu. [38]
- huko
- Jana Profesa Maghembe alikaririwa na kituo kimoja cha televisheni akisema kuwa suala la udahili mpya katika vyuo vikuu vya umma lilikuwa ni muhimu kwa kuwa huko nyuma halikuwa likifanyika. [39]
- humo
- UONGOZI wa timu ya Toto African ya jijini Mwanza imewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo pamoja na uongozi wa Chama cha Soka mkoa humo (MZFA) kuendeleza mshikamano ulipo ili kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri zaidi katika mechi zake nane zilizosalia. [40]
- huo
- Katika mwaka wa fedha 2004/05, gharama za ujenzi wa mradi huo zilikadiriwa kuwa Sh238.59 bilioni, lakini hadi sasa gharama hizo zimeongezeka zaidi ya mara mbili ya makadirio ya awali. [41]
- huru
- Ndiyo maana vyama vya upinzani vinataka iundwe tume huru ya uchaguzi badala ya hiyo ambayo imeundwa na serikali huku mwenyekiti na watendaji wakuu wote wakiteuliwa na Rais. [42]
- huwa
- Mimi sikubaliani na utamaduni huu cha msingi watu waheshimu haki za wapiga kura kwani si kweli kama washindi walikuwa wawili bali huwa mmoja tu katika uchaguzi," anasema Dk. [43]
- huyu
- Kwanza ya yote kuna vitu shostito vya kuangalia; huyu mtu anakuheshimu kiasi gani anakupenda kiasi gani na anakujali kiasi gani. [44]
- ijayo
- Prisons ambayo inawakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho itatupa karata yake ya kwanza Jumapili ijayo kupambana na Walibya kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. [45]
- ikawa
- Mfano zipo meseji watu wanatumiana "Vipi Dear!" unakuja, na hii ikawa ni meseji ya kawaida kabisa kwa mtu na mfanyakazi mwenzake kazini lakini kwako ikawa na sura nyingine tofauti kabisa na makusudiao yenyewe. [46]
- ikiwa
- Wakati kesi hiyo ikiwa bado inaendelea, wastaafu hao wamemwomba Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kuwasaidia ili ifutwe. [47]
- ikulu
- Tumeona jinsi familia nzima ya rais inavyokuwa jirani yake wakati wa kiapo ili kuwashirikisha kupokea jukumu zito la kuongoza nchi wakati wakiwa wote ikulu. [48]
- ila
- Tupo bega kwa bega na timu hizi ili kuhakikisha zinafanya vizuri na kuchukua ubingwa na maandalizi yanakwenda kama yalivyopangwa isipokuwa mchezaji mmoja kutoka Yanga ambaye mpaka sasa leseni yake haijakamilika ila tumewasiliana na uongozi husika ambapo wamaahidi kulifanyia kazi mapema suala hilo,"alisema Mwakalebela. [49]
- ile
- Lakini kauli ambayo nataka zaidi kwa leo kumhusisha nayo Rais Kikwete ni ile ya kulileta tena suala la Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 na kama kawaida linapotajwa suala hilo malaika huwasisimka watu. [50]
- ili
- Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Fredrick Manyanda aliiomba mahakama wapewe muda ili wazihakiki hati hizo ili kujua kama ni halali na kupata uhakika wa thamani ya mali iliyotajwa katika hati hizo. [51]
- ilikuwa
- Alisema taarifa hiyo pia ilisema hali yake ilikuwa ni mbaya na alipelekwa hospitali ya mkoa kwa matibabu. [52]
- ilipo
- Koola anadai katika maelezo yake mahakamani kuwa, eneo ilipo baa ya Rose garden ni hifadhi ya barabara isiyostahili kuendelezwa na uwepo wa baa hiyo umeziba eneo la mradi wake. [53]
- ina
- Katibu wa Prisons, Antony Hau alisema kuwa mpaka sasa timu yake ina majeruhi saba wawili kati yao ambao ni Hashim Kaobo na Ally Yusuph wanaendelea vizuri na huenda wakacheza leo katika mechi yao na Simba. [54]
- japo
- Nafurahi kusema kwamba nami nimeweza kuchangia japo kidogo katika kujaribu kuwasaidia watu kuziendea na kuzitumia rasilimali zilizoko nchini mwao. [55]
- je
- Sisi kama wafadhili tunachoangalia ni matokeo ya matumizi ya hiyo bajeti, kwa mfano kama serikali itaamua kutumia asilimia 20 ya fedha za msaada wa bajeti katika elimu, kwa hiyo tunaangalia je ni nini matokeo yake katika sekta elimu,je, kuna ongezeko la wanafunzi wanaojiunhga na shule za msingi? Je, kuna ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na sekondari na je kiwango cha elimu kimeongezeka kwa kiasi gani? Katika sekta ya afya nayo tunangalia kama kuna upungufu wa vifo vya kinamama wajawazito na watoto wachanga, je vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano vimepungua kwa kiasi gani na je utapiamlo kwa watoto umepungua? Kwa ufupi tunaweza kusema kuwa kumekuwa na matokeo mazuri ya matumizi mazuri ya bajeti ya maendeleo lakini pia ziko sehemu ambazo changamoto bado ni kubwa, kwa mfano vifo vya kinamama wajawazito, vito vya watoto wachanga na hata kiwango cha elimu inayotolewa ikilinganishwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliomo katika darasa. [56]
- jingine
- Jambo jingine ambalo marais wa kiafrika wanapaswa kujifunza kutoka Marekani ni kutoa muda wa kuapishwa baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi. [57]
- jirani
- Kwa kweli hatuwezi tu kusikia baba na mama wanapigana nyumba ya jirani na sisi tukaenda bila ya kuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na ugomvi wao, lakini tunatarajia kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 tutatuma waangalizi wetu kwa jicho zito kuangalia uchaguzi unavyoendeshwa Zanzibar na hapo ndio tutakuwa na nafasi ya kuzungumza," anasema Dk. [58]
- jumuiya
- Akizungumza katika maadhimisho hayo jijini Dar es salaam jana, Mkurugenzi Msaidizi wa Uhusiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dora Msechu, alisema Tanzania inasikitishwa sana na tukio hilo na kwamba inaungana na jumuiya za kimataifa kupinga matukio kama hayo. [59]
- juu
- Alizitaka jumuiya mbalimbali za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoa elimu ya kutosha juu ya umuhimu wa kuwa na uvumulivu na kuthaminiana katika jamii. [60]
- juzi
- Kifo cha mtu anayefanana na mfanyakazi huyo kilitokea juzi usiku baada ya kupata ajali mbaya ya pikipiki ambayo inafanana pia na ya Mfanyakazi wa Manispaa hiyo. [61]
- kansa
- Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [62]
- karibu
- Tunapongeza msimamo uliofikiwa na viongozi hao, ila tunaomba usimamizi wa karibu ufanyike kuhakikisha kuwa walichoamua, kutokana na makubaliano ya wahusika wakuu katika mgogoro huo yanatekelezwa kama ilivyopangwa na kuhakikisha kila upande unaotoa mchango unaofaa kufanikisha hilo. [63]
- karibuni
- Hivi karibuni uongozi wa MZFA ulitangaza mikakati yake ya kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika mechi zake zote ili iendelee kuwakilisha mkoa katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara. [64]
- kata
- Hatua hiyo ilikuja baada ya Mkuu huyo wa mkoa, kupokea taarifa ya maendeleo ya elimu iliyosomwa na Ofisa Elimu wa Mkoa wa Rukwa, Elizabeth Mfinganga, ambayo ilisema kata 12 katika mkoa huo, bado hazijakamilisha ujenzi wa shule za sekondari za kata. [65]
- kati
- Kweka alidaiwa kuwa, kati ya mwaka 2001 na 2006, akiwa Meneja Mradi wa BoT, aliisababishia hasara serikali ya zaidi ya Sh221 bilioni. [66]
- kibao
- Unafikiri wale waliokatika shule za ukata wanaweza kushindana na wale wanaotoa mamilioni kwa ajili ya shule ya wanafunzi wachache na walimu kibao, na kufanya tuisheni juu mpaka wanaweza kufaulu bila hata kuelewa kitu. [67]
- kikao
- Mkurugenzi mtendaji wa halamashauri ya manispaa ya Shinyanga, Jane Mutagurwa, hakupatikana kuzungumzia tukio hilo kwa maelezo kuwa yuko kwenye kikao maalumu na watumishi wa halmashauri hiyo. [68]
- kile
- Katika kile kinachooneka kuendelezwa kwa matendo ya utovu wa nidhamu kwa mashabiki wa timu ya Yanga jana waliivamia basi walilopanda wachezaji wa Mtibwa na kuanza kulitupia mawe hadi polisi wa kuzuia ghasi walipowatawanya kwa mabomu ya machozi. [69]
- kongwe
- Inawezekana kabisa, ingawa yeye anasema kuna nafasi ndogo kwa chama cha CUF kuweza kushinda uchaguzi, na kwa kauli ya Kikwete kuendeleza dhana hiyo kongwe ya "Mapinduzi hayachezewi," ina maana kuwa CUF haitapewa Serikali. [70]
- kuacha
- Pia alisema kamati imetoa onyo kwa timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu kuacha tabia ya kumtumia mtu mmoja kusaini fomu maalumu zinazotakiwa kujazwa kabla ya mechi na badala yake kuwahusisha wahusika wote wanaotakiwa kufanya hivyo. [71]
- kuapishwa
- Mathalan nchini Kenya, baada ya uchaguzi mkuu wa 2007, Mwai Kibaki alitangazwa mshindi na kuapishwa baada ya dakika chache za kutangazwa kwake, jambo lililopingwa na Chama cha ODM na mwenyekiti wake na kutangaza maandamano na mgomo wa nchi nzima. [72]
- kufa
- WAFANYAKAZI wa Manispaa ya Shinyanga jana walipatwa na kiwewe cha mshituko baada ya kumkuta mfanyakazi mwenzao aliyedhaniwa kufa akiwa hai. [73]
- kuinua
- Aliwataka wananchi mkoani Rukwa kushirikiana, ili kwa pamoja waweze kuinua kiwango cha elimu, hatua ambayo alisema itawapa heshima kubwa. [74]
- kuja
- Akiwa kisiwani Pemba, Rais Kikwete ameelezwa kusema kuwa itakuwa ni vyema kwa wanachama wa chama cha upinzani kutoa ushirikiano na chama tawala CCM kuiletea Pemba maendeleo kwa sababu serikali wanayoitaka ya chama cha CUF inaweza ikakawia kuja lakini kubwa zaidi huenda isije kabisa. [75]
- kujadili
- Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela alisema kamati hiyo ilikutana Januari 25 na kujadili matukio hayo. [76]
- kujazwa
- Tumepokea barua inayotaka sisi kama moja na timu shiriki kukubaliana na maelekezo yaliyotolewa na shirikisho hilo kuhusu wachezaji kupimwa afya zao kabla ya kucheza na fomu hii pia itatakiwa kujazwa na daktari wa timu," alisema Mwakalebela. [77]
- kukutana
- Hivyo walipanga muda wa kukutana. [78]
- kule
- Kikwete alisema sababu kubwa ya wapinzani kushindwa ni kule kukataa kwao kukubali kuwa kumekuwa na kiasi kikubwa cha maendeleo. [79]
- kulinda
- Tutanajitahidi kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi zetu zilizosalia ili kudumisha mshikamo wetu na pia kulinda heshima ya mkoa wa Mwanza," alisema. [80]
- kumbe
- Uongozi wa manispaa hiyo ulianza maandalizi ya kuusafirisha mwili wa mfanyakazi huyo, lakini kumbe aliyefariki sio mfanyakazi wao. [81]
- kumi
- Amesema katika kajaribu kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa, mkataba walioingia na makampuni hayo utayalazimu kufanya kazi kwa nguvu ili waweze kukusanya fedha nyingi kwa sasababu kila kampuni italipwa asilimia kumi ya makusanyo yake. [82]
- kumuua
- Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [83]
- kuokoa
- Beki Nadir Haroub 'Cannavaro' alikosa bao la wazi dakika ya 62 baada ya kupiga shuti liligonga mwamba na beki wa Mtibwa kuokoa mpira huo kwenye eneo la hatari. [84]
- kuona
- Alisema hii itakuwa changamoto ya kutosha kwa wadau wengine kuona umuhimu wa kusaidia timu za vijana ambazo ni ndio chimbuko la kupata timu zilizo bora ambazo zitaiwakilisha Tanzania katika mashindano makubwa. [85]
- kuongoza
- HADI mwanzoni mwa mwaka 2008, vyama vya siasa vya upinzani vilikuwa vimejijengea heshima kwa namna vilivyokuwa vinanadi sera zao zikubaliwe na wananchi ili hatimaye kimojawapo kichaguliwe kuongoza nchi. [86]
- kupimwa
- Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Fredrick Mwakalebela alisema tayari wameletewa fomu kwa ajili ya kuthibitishwa na CAF kukubali wachezaji kupimwa na imetakiwa kuthibitishwa na daktari wa timu. [87]
- kusikia
- Mongella anasema, Bunge la Afrika haliwezi kuingilia mambo ya ndani ya nchi yoyote kwa kusikia tu katika vyombo vya habari. [88]
- kuu
- Ilipofika asubuhi nilitumiwa ujumbe mfupi wa simu, kwamba mgonjwa amefariki na ndipo nilipoamka na kwenda ofisini ili kufanya mipango ya kuutibu mwili na wakati tunaingia ofisini, mimi na Mkurugenzi wa Manispaa, Jane Mutagurwa, tulishangaa kuwaona watumishi wenzetu wakikimbia kuelekea kwenye lango kuu na baadaye tulipata taarifa kuwa tuliyemdhania kuwa amefariki dunia siye. [89]
- kuua
- Kocha wa Yanga, Dusan Kondic amemshutumu sana mwamuzi wa mchezo huo kuwa ndio wanaochangia kuua soka Tanzania. [90]
- kuwapo
- Baadhi walidai kuwapo kwa makaburi ya pamoja katika baadhi ya kambi za kijeshi kisiwani humo ili kuficha aibu na kuyumbisha idadi kamili ya waliopoteza maisha yao kutokana na maandamano hayo. [91]
- kwake
- Shahidi huyo alisema halifahamu jina la Kiloloma & Brothers ambalo namba yake ni 151025 iliyotolewa Aprili 14 mwaka 2005. Alisema sahihi iliyoko katika jina la Kiloloma & Brothers inafanana na ya kwake na kwamba wamiliki wake wametajwa kuwa ni Rajabu Maranda na Farijala Hussein. [92]
- kwangu
- Haiwezekani namba moja kutolewa kwa majina mawili tofauti ya biashara na sahihi iliyoko kwenye Kiloloma & Brother imegushiwa, inataka kufanana na ya kwangu," alisema Mahingira. [93]
- kwao
- Kufuatia taarifa hiyo Ole Njolay ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho, alisema "nimeona ulazima wa kuandika barua kwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa mkoa huu na kumtajia idadi ya madiwani ambao wamenishinda, kwa kutoshiriki kwao katika shughuli za maendeleo, zikiwemo za ujenzi wa shule za sekondari za kata, ili naye awachukulie hatua zinazostahili kwa kuzingatia mbele yetu tunakabiliwa na uchaguzi mkuu. [94]
- la
- Hakimu Msongo alikubaliana na ombi la upande wa mashitaka na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 10 mwaka huu itakapotajwa tena. [95]
- langu
- Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni, alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [96]
- lengo
- Hata hivyo chanzo hicho kilifafanua kwamba, lengo la chuo hicho kuendelea kuwapa baadhi ya wanafunzi nafasi ya upendeleo iliingia dosari baada ya serikali kuchukizwa na tabia ya baadhi ya wanafunzi kufanya fujo. [97]
- leo
- Baada ya kusikiliza hoja zote kiongozi wa jopo la mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo, Cypriana William, aliahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea kusikilizwa. [98]
- lolote
- Hata hivyo kamanda Kova alikubali ombi hilo kwa sharti kuwa wasifanye kosa lingine lolote ikiwa ni pamoja na kukusanyika bila kibali. [99]
- mabomu
- WINGA chipukizi Mrisho Ngassa akiwa kwenye harakati zake za kwenda nchini Norway, jana alifunga bao pekee kwa Yanga katika dakika ya 8 ilipoilaza Mtibwa 1-0, huku mashabiki wa timu hiyo ya Mtaa wa Jangwani wakitawanywa kwa mabomu ya machozi. [100]
- madai
- Katika kesi yake ya madai namba 29 ya mwaka 2006, Koola anataka Rose Garden, Manispaa ya Kinondoni na kampuni ya Simu 2000 iliyomwuzia eneo hilo, wamlipe Dola za Marekani 174,260 kuanzia Julai 2005 hadi kesi hiyo itakapotolewa hukumu, gharama ya kesi na malipo mengine yoyote mahakama itakavyoona inafaa. [101]
- magari
- Wastaafu hao walikamatwa Oktoba 23 mwaka jana na kufunguliwa mashitaka ya kukusanyika bila kibali na kusababisha msongamano mkubwa wa magari jijini Dar es Salaam. [102]
- malengo
- Alisema kwa sasa wana zaidi ya vituo 30 na bado wana mpango wa kuongeza vituo hivyo kwa lengo la kuvikuza na kuvipanua katika mikoa mingine ikiwa ni moja ya malengo yao ya kuinua soka la vijana. [103]
- mazuri
- Winga huyo wa Mtibwa, Uhuru alishawahi kufanya majaribio na timu hiyo nchi Norway, lakini hakuweza kufanikiwa na alikiri kutokana na kutofanya maandarizi mazuri. [104]
- mdogo
- Lakini ghafla mwishoni mwa mwaka jana, wakati wa kuelekea uchaguzi mdogo wa Jimbo la Tarime kujaza nafazi iliyoachwa wazi na marehemu Chacha Wangwe, vyama hivyo viliingiwa na mdudu wa kuvisambaratisha. [105]
- mfupi
- Akifafanua Mwendapole alisema, majira ya saa nne usiku, wakati akiwa amelala, alitumiwa ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa mfanyakazi mmoja wa Halmashauri ya Manispaa yake, aliyemtaja kwa jina moja la Asha ikimtaarifu tukio la ajali lililompata mtumishi mwenzao,Gwakila Lagile. [106]
- mganga
- Mzee tumekuja, hali ya biashara ni mbaya sana, yaani kila kukicha ni mikosi tupu hata hatujui tufanye nini, ila tunasikia kuna mtindo umezuka siku hizi watu wanaua albino, viungo vyao vinaweza kutusaidia kupata fedha tutakapokwenda kwa mganga wa jadi alisema na kupingwa vikali na Kazim. [107]
- mguu
- Kwa vile namfahamu vyema mtumishi huyo, nilishtuka sana na nilikwenda hospitali ya mkoa wa Shinyanga, niliwakuta baadhi ya watumishi wa halmashauri wakiwa mapokezi na madaktari wakichukua vipimo, nilipomwangalia mgonjwa ni kweli nilikuwa namfahamu kama mtumishi wa halmashauri yangu na alikuwa ameumia sana mguu wake wa kulia kiasikwamba ulikuwa ukining'inia akiwa amelowa tope na damu mwili mzima. [108]
- miaka
- Ziara ya Kikwete imeelezwa ni ya kutimiza ahadi yake aliyoitoa wakati alipokuja kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kumchagua kushika Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2005. Kwa maneno mengine bado kuna muendelezo wa kutoa shukurani kwa tukio hilo la miaka minne iliyopita. [109]
- mifumo
- LILIPOIBUKA wazo vyuo vikuu vya Afrika Mashariki kuwa na mtaala mmoja kufuatia kuanzishwa kwa Shirikisho la Nchi za Afrika Mashariki, baadhi ya wasomi akiwemo Profesa Josephat Rugemalira wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walipinga wazo hilo kwa madai kuwa nchi hizo zina mifumo tofauti ya elimu. [110]
- mke
- Katika mtazamo wa kiume wenyewe wanasema inawezekana kumpenda mke wangu lakini nikamtamani Heriet lakini hili halina maana kuwa ni Heriet nataka kuwa naye, bali mke wangu. [111]
- mkuu
- Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa hali inaendelea vizuri ya kudahili wanafunzi na akasisitiza kuwa muda wa kudahili unaongezwa. [112]
- mno
- Lakini mwaka jana wakati ilipotolewa taarifa maalum ya ukaguzi wa akaunti ya madeni ya nje ya benki kuu, watu walishtuka mno na ukubwa wa tatizo lenyewe, kulikuwa na tishio kwa hatima ya misaada ya kwenye bajeti ya Tanzania kwani baadhi ya washirika wa maendeleo walitishia kujitoa kuisaidia Tanzania. [113]
- mosi
- Maranda na Farijala wanadaiwa kuwa kati ya Aprili mosi na Septemba 2 mwaka 2005 mkoa wa Dar es Salaam, waliiba kutoka BoT Sh 1,864,949,294.45 baada ya kudanganya kuwa kampuni ya Kiloloma & Brothers imepewa deni na kampuni ya BC Cars Export ya Mumbai India. [114]
- mpasuko
- Anatahadharisha Jumuiya za Kimataifa na serikali kuwa kama suala la mpasuko wa kisiasa Zanzibar lisiposhughulikiwa mapema, basi uwezekano wa kutokea mauaji mengine katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ni mkubwa. [115]
- msaidizi
- Jamaa huyo ambaye alikuwa kama msaidizi wake wa karibu, alikuwa akimuwakilisha katika kazi mbalimbali na ndiye aliyekuwa ana siri zake nyingi. [116]
- mujibu
- Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk Meshak Massi, ugonjwa huo uliwakumba wakazi wa maeneo ya Nansio na Ngoma, wilayani Ukerewe na maeneo mengine yanayozunguka Jiji la Mwanza. [117]
- mumewe
- Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [118]
- mwa
- Ole-Nangoro ni mmoja wa wabunge walioingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuziba nafasi za wazi baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kiteto Benedict Losulutya mwishoni mwa mwaka 2007, hivyo sio mbunge wa siku nyingi katika bunge hilo. [119]
- mwenye
- Uhuru aliendelea kusema Henry ni mzuri sana na mtu mwenye msaada katika timu ya Taifa kwani anauwezo wa kucheza namba zote. [120]
- mzuri
- Meya huyo alisema maandalizi yote ya kumpeleka x-ray na baadaye chumba cha upasuaji yalikuwa yakiendelea vizuri kwa ushirikiano mzuri kati ya madaktari wa hospitali hiyo, daktari wa Manispaa na watumishi wa Manispaa hiyo, lakini ilipofika majira ya saa 6 usiku, aliondoka na kwenda kulala. [121]
- na
- ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Joachimu Liyumba na Meneja Mradi wa Benki hiyo, Deograthias Kweka, jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuisababishia hasara Serikali ya zaidi ya Sh 221 bilioni. [122]
- namba
- Alisema namba ya usajili wa Kiloloma & Bros Enterprises ni 151025 na kwamba ilitolewa Aprili 14 mwaka 2005,mmiliki akiwa Charles Isaack Kissa. [123]
- nani
- Na baada ya kugoma, nani kafukuzwa sasa? Ni wananchi wakati wenyenchi wanazidi kupeta. [124]
- nao
- Eti wao nao waliona Bi Elimu ni tishio kwa urithi wa kaka yake maana watoto wake walikuwa wanawazidi akili hata wale wa Bwana Aimbora. [125]
- naye
- Alipoingia katika ukumbi huo, alisimama kwa muda mrefu mlangoni kwa ndani, akizungumza na Benedicti Ole-Nangoro ambaye ni mbunge wa Kiteto (CCM) huku, baadhi ya wabunge wa CCM wakipita na kusalimiana naye kwa kukumbatiana. [126]
- ndio
- Ukweli huu basi unadhihirisha kuwa kama tutaishi kwa kuvumuliana, kilichotekelezwa na utawala wa kinazi hakitajirudia tena na hii ndio maana maadhimisho haya yanaendelea kufanyika kila mwaka" alisema Taranco. [127]
- ndiye
- Sio kushiriki tu bali mke ndiye ambaye humsaidia kumshikia msahafu wa dini rais wakati akiapa. [128]
- ngumu
- Hau alisema wanajua mechi Walibya itakuwa ngumu kupita watu wananyofikilia na wataakikisha wanapeperusha bendera ya Tanzania vizuri katika michuano hiyo. [129]
- ni
- Hakimu Msongo alitaja masharti matano ya dhamana ambayo ni kila mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali na barua zao za utambulisho zitoke kwa waajiri wao. [130]
- nia
- Ukichanganya nia misaada yote ya kimaendeleo inayopewa, bajeti ya serikali ya Tanzania ni kiasi cha dola 6 bilioni, fedha ambazo ni asilimia tatu tu ya bajeti ya mwaka ya huduma za afya nchini Uingereza. [131]
- nini
- Haikuweza kufahamika mara moja ni kwa nini mbunge huyo, alifuatwa na wabunge wengi kutoka katika chama chake (CCM na kusalimiana naye, ingawa dalili zilionyesha kuwa walikuwa wakimfariji kesi inayomsumbua. [132]
- njama
- Tunashangaa jinsi Tume ya Uchaguzi (NEC) inavyozembea kwenye usimamizi wa taratibu za uchaguzi na hasa kutunza masanduku ya kupigia kura, hali inayotafsiriwa kwamba, tume hiyo inakula njama za makusudi kukisaidia chama tawala, kwani tatizo hilo ni la muda mrefu. [133]
- nzuri
- Katika mchezo huo ambao mabingwa wa Kombe la Tusker, Mtibwa waliuanza kwa nguvu kwani katika dakika ya pili ya mchezo mshambuliaji wake Zahoro Pazi alikosa bao la wazi baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Uhuru Seleman, lakini alipaisha. [134]
- onyo
- Aliongeza shirikisho hilo limetoa onyo mapema kwa nchi zote zitakazoshiriki kuzuia wachezaji wake kutumia dawa hizo za kuongeza nguvu kwani itakapobainika wao kama viongozi wa ngazi za juu watachukua hatua za kisheria. [135]
- pale
- Mimi nimemuangalia kwa macho yangu pale hospitali, na kwa kweli wanafanana sana, kwani hata umbo lake ni lilelile la unene, na weusi wake. [136]
- pia
- Mramba anatuhumiwa kutumia vibaya madaraka yake akiwa Waziri wa Fedha wakati wa utawala wa awamu ya tatu chini ya Rais mstaafu Benjamini Mkapa na alifikishwa mahakamani pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini kwa wakati huo Daniel Yona na baadaye kufuatia na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Gray Mgonja, ambaye pia alipandishwa kizimbani kwa tuhuma za aina hiyo. [137]
- picha
- Ikabidi kwa kumtia moyo, ikabidi aende kwenye ofisi ambayo alikuwa akifanyia utafiti huo na kufanikiwa kupata picha yake. [138]
- pole
- MBUNGE wa Jimbo la Rombo, mkoani Kilimanjaro, Basili Mramba ambaye aanakabiliwa na mashtaka ya kutumia vibaya madaraka yake akiwa Waziri wa Fedha, jana aliingia katika ukumbi wa Bunge kwa huku wabunge wakionekana kumpa pole na kumkumbatia. [139]
- raia
- Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka TFF, Fredrick Mwakalebela alisema mpaka sasa tayari wamepokea leseni na majina ya timu zote mbili ya washiriki wanaoshirki mashindano hayo isipokuwa kipa huyo raia wa Serbia ambaye bado hajakamilisha taratibu hizo. [140]
- rais
- Nasema watakuwa wamepata funzo kubwa kutoka kwa Obama kutokana na ukweli kwamba shughuli ya kuapa ya Rais wa Marekani huendeshwa kwa uwazi na familia ya rais hushiriki kikamilifu. [141]
- sasa
- Habari zilizopatikana nje ya mahakama zinasema kuwa hadi sasa Sh600 bilioni, zimetumika katika ujenzi wa majengo pacha ya BoT yaliyoko jijini Dar es salaam jengo la Benki Kuu Zanzibar la Gulioni. [142]
- sawa
- Taifa Stars inatarajia kujiunga na kambi kwa ajili ya maandalizi ya mwisho Februari 3- 4 watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Zimbabwe kujiweka sawa tayari kwa fainali hizo wataanza kwa kuvaana na Senegal. [143]
- sera
- Aliongeza kutokana na kitendo cha wanafunzi hao kugomea sera ya kuchangia elimu, serikali iliamua kufuatilia rekodi za kila mwanafunzi na kubaini kwamba baadhi walikuwa hawajafanyiwa udahili. [144]
- shaka
- Kwanza kauli ya Kikwete ina alama ya vitisho ingawa vitisho hivi havionekani kukaziwa lakini hakuna shaka yoyote kuwa anayetaka kuchezea Mapinduzi atakiona maana itakuwa hajipendi na hajitaki. [145]
- shida
- Umempata? alidakia Kazim, aliyekuwa akizungumza kwa shida. [146]
- si
- Hata hivyo, idadi ndogo ya wapigakura iliyojitokeza kupiga kura, ni ishara tosha kwamba, kuna udhaifu katika mfumo wa siasa na demokrasi nchini; na si tu kwa sababu ya kukosekana na kwa elimu ya uraia kama inavyoelezwa. [147]
- sisi
- Najua Simba na Yanga ni watani wa jadi na kila timu haitaki kumuona mwenzake akishinda, lakini hapa inabidi tukubali tu kuwa kama tunataka kuikamata nafasi ya pili Yanga iendelee kushinda mechi zake na sisi pia tushinde," alilisisitiza Mzambia huyo. [148]
- sugu
- Tumeamuwa kutumia wataalam ili kuweza kukusanya madeni kutoka kwa wadaiwa sugu, majina ya wadaiwa wa zaidi ya miezi sita yatakabidhiwa kwa wataalam (makampuni ya udalali)," alisema Kaaya. [149]
- tafsiri
- Nionavyo wakati umefika hivi sasa kuwa na tafsiri mpya ya kuendeleza Mapinduzi. [150]
- tajiri
- Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [151]
- tu
- Alisema hata hivyo kuwa haitoshi tu kuwa na kumbukumbu kluhusu mauaji hayo na kwamba la msingi, ni kupinga vitendo vya mauji ya halaiki na dhana zote zinazosababisha kutokea kwake. [152]
- tupu
- Mgawanyo wa madaraka kwa kweli si suluhu kabisa la migogoro ya kisiasa barani Afrika ila ni hatari tupu," anasema Dk. [153]
- ubora
- Tunahitaji kuwa na mfumo utakaohakikisha udhibiti wa ubora wa elimu katika vyuo vyetu," alisema Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha St. [154]
- ujao
- SHIRIKISHO la soka Afrika, CAF limesema wachezaji wote watakaoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika (CHAN) watapimwa afya kabla ya kuanza kwa fainali hizo mwezi ujao na watakaobainika wanatumia dawa za kuongeza nguvu hatua za kisheria zitachukuliwa. [155]
- ukawa
- Huenda ukawa umekutana na kitu ambacho kinabaki kuwa hisia zako tu tofauti na mapokezi ya kitu chenyewe. [156]
- uko
- Awali ilitangazwa kuwa udahili ungefanyika hadi Januari 22 lakini sasa utaisha Januari 29. "Imebidi muda uongezeke kwani idadi ya wanafunzi ni kubwa na kuna wale watakaokata rufaa, pia mlango wa waziri uko wazi kwa wale wasio na uwezo wa kukamilisha malipo yote," alisema. [157]
- ukoo
- Ya nini kumpa matumaini wakati yeye na ukoo wake wote wameshatolewa nje katika dunia ya leo. [158]
- ule
- Jana viongozi hao wanaoendelea na mkutano wao walifikia hatua ya kupanga tarehe ya kumwapisha Waziri Mkuu, Morgan Tsvangirai na ya kuunda serikali ya umoja wa kitafia ili kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miezi kumi tangu matokoteo tata ya uchaguzi mkuu katika nafasi ya urais na ule wa marudio kutolewa mwaka jana. [159]
- umma
- Matumizi mabaya ya fedha za umma katika ujenzi wa majengo hayo, ni miongozi wa tuhuma zilizofichuliwa na kambi ya upinzani sambamba na ufisadi wa mabilioni katika Akaunti ya Madeni Nje (EPA), ambao ulisababisha aliyekuwa gavana wa BoT Daudi Balali kufukuzwa kazi pamoja na baadhi ya watuhumiwa wakiwemo watumishi wa benki hiyo, kufikishwa mahakamani kwa kuisababisha hasara serikali. [160]
- upo
- Utata katika suala hilo upo katika gharamaa za ujenzi wake na kampumi iliyopewa zabuni kufanya kazi hiyo. [161]
- upya
- Waziri huyo aliwataka wanafunzi hao kukamilisha haraka taratibu za kujiandikisha upya katika vyuo vyao ndani ya muda uliopangwa ili waweze kuanza masomo. [162]
- uwezo
- Chanzo kingine kutoka chuoni hapo kilifafanu kuwa uamuzi wa serikali kuamuru udahili ufanyike ni sahihim, kwa sababu uzembe uliofanywa na uongozi wa chuo ingesababisha chuo kuzalisha wasomi wasiokuwa na uwezo. [163]
- vichwa
- Anasema kinachoendelea nchini Zimbabwe ni matokeo ya vichwa ngumu ya watawala wa nchi za Afrika wanaopenda kungangania madarakani. [164]
- vifaa
- Alisema Kissa alisajili jina hilo kwa ajili ya kufanya biashara ya vifaa vya ofisini na steshenari na kwamba hajawahi kubadili jina la biashara. [165]
- vijana
- Timu za Tanzania Prison kutoka Mbeya na Yanga ndio watashiriki katika mashindano hayo ambapo vijana wa Kondic wataanza kuvaana na Wacomoro inayowasili kesho. [166]
- vile
- Haiwezekani wanafunzi wakawa wanaingia chuo kikuu kama vile wanakwenda Kariakoo (sokoni), lazima uwepo utaratibu, na ndicho tunachofanya," alisema Maghembe. [167]
- vumbi
- KIPA wa timu ya Yanga, Mserbia Obren Circovic ana hati hati ya kutoshiriki mashindano ya Klabu Bingwa Afrika yatakayoanza kutimua vumbi Jumamosi katika uwanja wa Taifa baada ya leseni yake kutokamilika kufuatia taratibu za mashindano hayo. [168]
- vyote
- Hakuna njia moja inayoweza kutumika kwa vyuo vikuu vyote, kila chuo kitengeneze mfumo wake," anaongeza. [169]
- vyuo
- WAKATI jamii ikiendelea kulalamikia udahili mpya wa wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma nchini, habari kutoka ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) zimeeleza kwamba, udahili huo unafanywa kwa agizo la Serikali baada ya kubaini kuwa awali baadhi wanafunzi walikuwa wanaanza masomo katika chuo hicho kabla ya kudahiliwa. [170]
- wadogo
- Kaaya amesema kuwa asilimia 90 ya wateja wanaodaiwa na kampuni hiyo ni wateja wadogo wadogo. [171]
- wajibu
- Ujanja alioutumia Kikwete ni kuwa CUF haiwezi kuwa na nafasi ya kushinda kwa sababu CCM imekuwa ikitimiza wajibu wake wa kuwaletea wananchi wa Zanzibar maendeleo. [172]
- wake
- Taarifa ya ukaguzi ya BoT ya mwaka 2005, minara hiyo ambayo ujenzi wake uligubikwa na utata, iliigharimu benki hiyo Sh500 bilioni. [173]
- wako
- Pia Yona na Mgonja na wako nje kwa dhamana na walishapewa ruhsua ya kwenda kuwatembelea ndugu zao nje ya Dar es Salaam. [174]
- wala
- Manispaa ya Kinondoni imeieleza mahakama katika utetezi wake kuwa haikupitisha ramani yoyote kuonyesha eneo ilipo baa ya Rose garden, hifadhi ya barabara wala kubadili matumizi ya ardhi hiyo. [175]
- wanafanya
- Na kwa nini wanafanya vizuri. [176]
- wapi
- Eti wale akina Aimbora waliosoma shule za kulipia tangu chekechea hadi mwisho wa sekondari sasa wanadai kusoma bure chuoni? Wapi na wapi. [177]
- wasi
- Hoja ya kwanza ni kuwa hivi baada ya miaka 45 bado kuna wasi wasi kuwa Mapinduzi yanaweza kuchezewa? Kama upo wasi wasi huo basi Mapinduzi yenyewe yana wasi wasi hata baada ya miaka 45 na kuambiwa kuwa yamejizatiti. [178]
- watafanya
- Aliwapa moyo mashabiki wao na kusema kuwa watafanya vizuri kwani bado wanawachezaji wazuri ambao wanawatumia sana kwa sasa kwenye Ligi Kuu ya Vodacom. [179]
- watu
- Uzoefu unaonesha kuwa mauaji ya halaiki yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na watu waliosoma ambao wanakuwa na mitazamo yao isiyokubalika kwa watu wengi," aliongeza kusema Msechu. [180]
- waume
- Badala ya kumsaidia Rais kuwatumikia wananchi, wanadhani nafasi ambayo wanayo waume zao ya kuiongoza nchi ni kwa ajili ya kujinufaisha wao na ndugu zao. [181]
- wazee
- Mussa anasema, wao kama wazee waliojitolea kutetea haki za Wapemba, tayari wameshalifikisha suala hilo katika ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) tangu Januari 16 mwaka huu na kwamba limepokelewa. [182]
- wenyewe
- Jibu: Hili ni suala ambalo watu wa Zanzibar wanapaswa walitatue wenyewe. [183]
- wetu
- Hii inatupa moyo sisi kama wadau kuhamasika pia na wadau wengine kuona umuhimu wa kutoa misaada kwa timu za vijana kama hizi kwani kwa kufanya hivyo italeta changamoto kubwa na chachu ya vijana wetu kujituma zaidi katika mashindano. [184]
- wiki
- Njoolay alitangaza msimamo huo mwishoni mwa wiki iliyopita, alipokuwa akizungumza katika kikao cha wadau wa elimu mkoani Rukwa. [185]
- wote
- Alisema kabla chuo hakijafunguwa kulikuwa na wanafunzi walioshindwa kuliopa ada ambao walipewa upendeleo maalumu wa kulipa taratibu huku wakiendelea na masomo kabla ya udahili kufanyika, kwa sababu udahili ukifanyika wanafunzi wote wasiolipa ada hawatakiwei kuwepo chuoni. [186]
- yake
- Katika taarifa yake ya mwaka wa fedha 2005/06, BoT ilisema hadi kufikia Juni 2006, miradi hiyo ilikwishatengewa Sh430 bilioni. [187]
- yako
- Mwisho tu nikuachie mwenyewe na mizani yako. [188]
- yangu
- Jina la Kiloloma & Bros Enterprises nalitambua kwa sababu kuna sahihi yangu katika hati ya usajili wa jina la biashara," alisema Mahingira. [189]
- yao
- Katika hali hiyo haikuweza kufahamika mara moja Mramba na Ole-Nangoro walikuwa wakizungumza kitu gani, kwa muda mrefu mlangoni hapo hadi mazungumzo yao yalipokatizwa na sauti iliyoashiria kuwa Spika wa Bunge alikuwa anaingia katika ukumbi huo. [190]
- yeye
- Alisema yeye alianza kuwaarifu wafanyakazi wenzake wa kuhusu ajali hiyo na uongozi ukachukua hatua ya kufuatilia. [191]
- yuko
- Hivi sasa yuko nje kwa dhamana na mahakama ilimpa ruhusa ya siku 29 kuanzia Januari 3 hadi Februari 2, mwaka huu kwa ajili ya kwenda kusalimia ndugu, kutembelea jimbo lake na kuhudhuria mkutano wa bunge. [192]
- yule
- Si vyema kukaa katika fikra kongwe kuwa anayeweza kuendeleza Mapinduzi ni yule yule aliyeyaleta wala kwamba Mapinduzi yenyewe yanaweza kufa kwa sababu tu ya kuondoka madarakani chama kilichoyaleta. [193]
- yupo
- Ofisa biashara huyo alisema ilipofika usiku huo wa manane, Gwakila Lagije, aliposikia taarifa za kifo chake wakati yeye yupo hai nyumbani, alianza kuhangaika kupiga simu kuwajulisha wafanyakazi wenzake kuwa yeye yupo salama na kusisitiza kwamba walikuwa wakimfananisha. [194]
- zake
- KATIKA kujiimarisha zaidi kiuchumi na jitihada za kuboresha huduma zake kwa jamii, Kampuni ya Usambazaji maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani (Dawasco), imepanga kutumia makampuni ya udalali kukusanya deni la Sh23 bilioni kutoka kwa wateja wake. [195]
- zangu
- Sikiliza Kazim, usinitukane tafadhari, mimi ni mtu mwenye heshima zangu, nakusaidia tu, usiniletee shida, kama vipi rudi kule India tuone kama utapona, kosa langu ni nini? alijibu waziri kwa sauti ya hasira. [196]
- zetu
- Lazima wapunguzwe nguvu kwa sababu ukiangalia msimamo timu nyingi pointi tunakaribiana sana hivyo kama sisi tutashinda mechi zetu tutazidi kwenda juu zaidi na hao wengine inabidi wafungwe ili tusonge mbele kirahisi. [197]
- ziara
- RAIS Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi alikuwa na ziara ya siku kadhaa katika mikoa mitano ya Zanzibar akifanya kazi za kiserikali na pia za kichama. [198]
- ziko
- Bado uchunguzi unaendelea na pia zipo kesi ambazo tayari ziko mahakamani, tunatarajia kwamba sheria na haki itafuata mkondo wake. [199]
- zito
- Sisi (PAP) kwa mfano Zimbabwe tulipeleka waangalizi wetu, tena kwa jicho zito sana na waliporudi tulitoa taarifa yetu kwamba uchaguzi haukuwa huru wala wa haki lakini tukapuuzwa matokeo yake ndiyo haya mnayoyaona," analaumu. [200]