Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-22

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah 
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
aende 
Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [2]
aina 
Vyote hivi muhimu sana na hivyo tutaendelea kusaka raslimali za maendeleo popote tunapoweza na kwa kutumia kila aina ya mbinu. [3]
akawa 
Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [4]
alianza 
Rais Kikwete alianza ziara ya Tanzania Visiwani juzi, katika Mkoa wa Kaskazini Pemba na jana, alimaliza ziara ya kisiwa cha Pemba kwa kutembelea mkoa wa Kusini Pemba. [5]
alifoka 
Sasa huo si ujinga, picha ndio nini? Picha ndio dawa,” alifoka Kazim hali iliyomfanya waziri aendelee kufadhaika na kumueleza kuwa watakachokifanya ni kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari. [6]
ama 
Sisi hatuna kumbukumbu zinazoonyesha kuwa kuna hati ya kitalu namba 87, iliyotolewa kwa mtu ama watu katika eneo la Kipawa. [7]
ambako 
Mwaka 1980 alijiunga na chuo cha Kays cha nchini Uingereza ambako alihitimu stashahada ya ubunifu wa mitindo. [8]
ambao 
Rais ametoa ufafanuzi huo wakati alipofungua mradi wa tanki la maji kwenye kijiji cha Kengeja, mradi ambao umegharimiwa na serikali ya Japan na utakaowanufaisha kiasi cha watu 19, 000 wa kijiji hicho na maeneo ya jirani. [9]
ambaye 
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Boaz ambaye alikuwa katika eneo la tukio pamoja na Mkuu wa wilaya Arumeru, Wawa Lali, Mkuu wa wilaya ya Arusha, Evance Balama na maafisa kadhaa wa polisi alisema bado chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana. [10]
ana 
Moita alidai pia kuwa ana taarifa za kuaminika kwamba mshitakiwa wa pili ameandaa maandamano nchi nzima yanayotarajiwa kufanyika Januari 24, mwaka huu wakati hajatoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika na masuala ya ulinzi. [11]
asasi 
WABUNGE wamelalamikia kukithiri kwa asasi zisizo za kiserikali (Azaki) ambazo hazina ofisi licha ya kwamba, zimesajiliwa kuihudumia jamii. [12]
au 
Ilieleza kuwa mtu yeyote anayedai ni mmiliki wa kiwanja hicho ni muongo kwa sababu kumbukumbu zao zinaonyesha kuwa hakuna mtu au kampuni iliyoomba umiliki wa viwanja hivyo. [13]
baina 
Mmoja alikuwa analipiwa daraja A na mwingine C, hivyo kusababisha mkanganyiko baina ya wanafunzi hao. [14]
balozi 
Balozi wa Misri nchini, Wael Nasr alisema jana katika mahojiano maalum na gazeti hili kuwa hakubaliani na hatua ya balozi za nje kuzungumzia masuala ya ndani ya Tanzania kwa kuwa hii ni kinyume cha sheria za kimataifa za kidiplomasia. [15]
beki 
Dakika ya 17, beki Juma Jabu alitaka kujifunga mwenyewe, baada ya kumrudishia vibaya mpira kipa wake Ally Mustafa. [16]
bila 
Ni kweli hata sisi tumegundua utata huo, tunaufanyia uchunguzi na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria," alisema Mahingila bila kufafanua adhabu zinazoweza kutolewa kwa wamiliki wa kampuni hiyo. [17]
bukta 
Eti beki alimvuta bukta. [18]
bungeni 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Naibu Makamu wa Chuo anayeshughulikia utawala, Profesa Yunus Mgaya alisema kuwa wanachosubiri wao ni kuona kuwa Waziri Maghembe anaiwasilisha bungeni ili ijadiliwa na kupitishwa. [19]
bwana 
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na bwana mmoja aitwaye John Gottman unasema: namna vile watu wanavyogombana unaweza kujua ni kiasi gani watu wanapendana halikadhalika utaweza kujua ni maamuzi yatokanayo. [20]
cha 
Hata hivyo, mmoja wa maofisa waandamizi wa idara hiyo, alisema kwa kuwa NMC tayari imekufa yeyote atakeyekuwa anakimiliki viwanja hivyo kwa hati iliyotolewa mwaka 1980, itakuwa ni kinyume cha sheria na anapaswa aombe umilikishwaji. [21]
chake 
Kutokana na kuwepo kwa taarifa hizo, Jeshi la Magereza limetuma kikosi chake malum cha kupambana na Ghasia ambacho kimeimarisha ulinzi kwa kushirikiana na Askari Magereza wa Gereza hilo la Karanga. [22]
chongo 
Kweli ushabiki ni chongo. [23]
dhana 
Epuka dhana na kusikiliza maneno ya watu. [24]
dogo 
Katika tukio hilo, basi dogo lililokuwa na abiria lilitumbukia katika mto huo na kusabaisha vifo na wengine kujeruhiwa. [25]
duni 
Mama huyo ambaye ni mbunifu wa mitindo aliyedumu katika fani hiyo kwa muda mrefu zaidi, anasema elimu duni na kutoelewa umuhimu wa mitindo nchini ndiyo tatizo kubwa, kwani jamii ya kitanzania haina uelewa kabisa. [26]
es 
UTATA umezidi kugubika sakata la umiliki wa Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd, baada ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kusema haina kumbukumbu za umiliki wa kampuni hiyo katika kitalu namba 87, Kipawa, jijini Dar es Salaam. [27]
eti 
Hata wale waliotishia kuwashitaki viongozi wa CHADEMA eti kwa kuwadhalilisha sasa wamebaki vichwa chini. [28]
faida 
Kabla sijaeleza sababu ambazo naona zinasababisha kushuka kwa e-government nchini, labda nitaje faida za mpango huu. [29]
fani 
Asia Idarous ambaye ni mkongwe katika fani ya ubunifu wa mitindo hapa nchini, anasema hiyo fani inayoweza kutumika kama shughuli ya kujikwamua kiuchumi, ikiwa muhusika atakuwa makini katika kufanya kazi zake. [30]
gani 
Unapoanza kufungwa sio kwamba tayari umepoteza mchezo unatakiwa kutulia na kurekebisha makosa yako na baadaye kuangalia ni namna gani unaweza kupata ushindi hivi ndivyo ninavyotaka tukafanye hata tutakapoenda Ivory Coast. [31]
hadi 
Akizungumza wakati wa kukagua ujenzi wa barabara ya lami kutoka Jondeni hadi kufikia Makombeni, Kisiwani Pemba, katika siku ya pili ya ziara yake ya siku sita Tanzania Visiwani, Rais Kikwete alisema kuwa mawazo ya kusimamisha ununuzi wa magari ya serikali ni jitihada za serikali yake kuinua hali ya kilimo nchini. [32]
hajui 
Kauli hiyo ilionekana kumchanganya sana Kazim, akawa hajui la kufanya. [33]
hao 
Kuhusu ziara za nje, Rais alisema kuwa hatua ya viongozi wa Tanzania kutembelea nchi za nje siyo kupoteza wakati wala fedha, bali ni jitihada za viongozi hao kujazia raslimali za maendeleo ya Tanzania. [34]
hapa 
Alisema kuwa Ibrahim ambaye ni miongoni mwa wachezaji watatu kutoka hapa nchini wataowakilisha kanda ya Afrika Mashariki, alifanikiwa kupata nafasi ya kwenda nchini humo baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya vijana yaliyofanyika Agosti mwaka jana. [35]
haraka 
Akizungumza na Mwananchi mwenyekiti huyo alisema kutangulia si kufika na haraka haraka haina baraka. [36]
hasa 
Tunajua kuwa mahakama ni chombo huru kinachoongozwa kwa sheria na taratibu zake wakati wa kuendesha shughuli zake na hasa kesi. [37]
hasira 
Ilidaiwa wanafunzi hao walibeba mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali ambao ulikuwa umejielekeza kuleta hasira na kujenga chuki kwa watu wengine. [38]
hati 
Msemaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ndeny Ulomi aliliambia Mwananchi jana kuwa hawana kumbukumbu zinazoonyesha hati ya kiwanja namba 87, eneo la Kipawa. [39]
hawa 
Tusipotoka kwenda kuwaona watu hawa, watashughulika na wale ambao wamekwenda na wamewaona. [40]
hii 
Wakati anakutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa wizara ya fedha na mipango ya uchumi kuhusu tathmini ya utendaji wa serikali yake katika miaka mitano iliyopita, Rais Kikwete aliuelekeza uongozi wa wizara hiyo Jumatatu wiki hii mjini Dar Es Salaam kuchukua hatua za kusimamisha ununuzi wa magari ya Serikali, ili kuokoa fedha za kuwekeza katika kilimo. [41]
hili 
Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Temeke ililithibitishia gazeti hili kuwa hakuna kiwanja kilichotolewa kwa jina la kitalu namba 87, Kipawa. [42]
hizi 
Lengo letu ni kupitisha sheria na sera ambazo zitazisajili Azaki chini ya mwavuli mmoja na si vinginevyo ingawa siku hizi, baadhi ya Azaki zinaanzishwa bila malengo," alisema. [43]
hospitali 
Majeruhi ambao hadi jana walikuwa wamelazwa katika hospitali hiyo ni Josepheni Boniface, Scolactica Samson na Maria Apolonary. [44]
huduma 
Inasikitisha kuona kwamba, wakati serikali ikijitahidi kufanya kampeni ya kupunguza vifo vya wanawake vinavyotokana na matatizo ya uzazi kwa sababu ya kukosa huduma ya uzazi, baadhi ya watu wanawazuia wake zao wasiende kliniki. [45]
hujui 
Kwa kuwa hujui aliyekuletea ana nia gani na mumeo. [46]
hujuma 
Kwa kutumia mwanya huo huo wa serikali kulala kusimamia mambo mengi muhimu, watumishi wengi wa umma wamejipata madaraka ya kufanya mambo ambayo kwa uhakika ni hujuma dhidi ya serikali yao. [47]
huko 
Alisema baada ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), kubinafsishwa, nyaraka zote za madeni ya biashara zilizokuwa huko, zilihamishwa. [48]
huku 
Nashukuru Mungu nipo salama ingawa naumwa, lakini sijui na siamini kama kweli nipo salama, kwa kuwa nilichokushuhudia kabla sijapoteza fahamu ni Land Rover kutaka kulipita gari kubwa na ghfafla tukatumbukia mtoni," alisema Valeria huku akilia. [49]
huna 
Ama unaota unahisi unakusaliti na huna uhakika, na huenda hujamuuliza. [50]
huo 
Mwananchi lilipowasiliana na Msajili wa Makampuni, Esteriano Mahingila kuhusu utata huo, alisema watafanyia uchunguzi wa kina na kuchukua hatua wahusika kwa mujibu wa taarifa hizo. [51]
hutumia 
Sasa ukikuta timu ambazo saikolojia yao ipo katika hali nzuri hutumia nafasi hiyo kujipanga na hatimaye kupata ushindi kirahisi"anasema Maximo. [52]
huu 
Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Kenyela mbele ya hakimu mkazi, Victoria Nongwa kuwa wanafunzi hao walitenda kosa hilo Januari 19 mwaka huu saa 3:45 asubuhi katika maeneo ya chuo hicho. [53]
huyo 
Shahidi huyo ambaye ni Mkuu wa Mipango Kazi wa BOT, alisema hayo alipokuwa akitoa ushahidi wa kesi hiyo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. [54]
huyu 
Kuna huyu Yassin Saleh na Tumaini Martin chama kinafanya mipango ya kuwapeleka nchini Kenya, kwa mafunzo zaidi kabla ya kwenda Morocco,"alisema Mvita. [55]
idadi 
TPA imeeleza sababu nyingine ya kupungua shehena hizo kuwa ni Tazara kushindwa kuhudumia shehena nyingine za mbolea na mafuta na kupungua kwa uwezo waTrl kunakotokana na idadi ndogo ya injini na mabehewa yake na mtaji mdogo wa TPA katika kuwekeza. [56]
ijayo 
Kipa huyo raia wa Uganda alikili kuwa na udhaifa wa mipira ya aina hiyo, hivyo ameamua kuanza mazoezi ya kutaka kuondoa tatizo hilo haraka kabla ya mechi ijayo. [57]
ikawa 
Na inawezekana ikawa hujui nini kamwambia mumeo kuhusu wewe. [58]
ikiwa 
Rais Kikwete ametoa ufafanuzi huo kwa wananchi baada ya kuwa ameambiwa na wananchi katika eneo hilo kuwa walikuwa na mahitaji ya pembejeo ikiwa ni pamoja na tretka za kilimo. [59]
ila 
Huwa tunaendesha semina mbalimbali kwa waamuzi, lakini idadi imekuwa ndogo sana na wengi wanaokuja ndio hao marefa tulionao ambao wengi ni wanajeshi na ukweli ni kwamba wanachezesha vizuri tu hao wanaolalamika mbona timu zao zikishinda huwa hatusikii malamiko yao ila wanapofungwa ndio wanajua kuongea ? kifupi ni kwamba hakuna upendeleo wowote Kili RBA," alisema Mbaga. [60]
ile 
MWENYEKITI wa timu ya Simba, Hassan Dalali amesema ule mkakati wa kuifukuzia Yanga katika harakati za ubingwa umeanza rasmi na kwa ufanisi, kwani michezo yao tisa iliyobaki lazima washinde na hawataki kukubali sare ya aina yoyote ile. [61]
ili 
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa serikali yake inatafakari kusimamisha ununuzi wa magari ya serikali kwa muda, ili fedha zitakazookolewa katika zoezi hilo zitumike kununua matreka kwa ajili ya kuinua kilimo nchini. [62]
ina 
Wakati huo huo, Hussein Issa na Patricia Kimelemeta wanaripoti kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimekiri kuwa sera ya uchangiaji wa elimu kwa vyuo vikuu nchini ina upungufu ambao yanahitaji kufanyiwa marekebisho. [63]
ipo 
Kipawa ipo Ilala. [64]
itoe 
Mheshimiwa hakimu mashahidi wawili waliobaki ni wagonjwa na mmoja amezuiliwa kusafiri kwa kuwa ni mzee, tunaomba mahakama itoe amri itakayosaidia kuwapata mashahidi," alisema Lukosi. [65]
iweze 
Ni wajibu wa upande wa mashitaka kutafuta mashahidi, ili kesi iweze kuendelea na kama wameshindwa wafunge kesi yao ili upande wa utetezi, turuhusiwe kuleta utetezi kwa mujibu wa sheria,"alisema Mgongolwa. [66]
kada 
SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inayomkabili kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na wafanyakazi watatu wa BoT, Peter Noni ameieleza Mahakama kuwa, ripoti ya madeni yaliyohakikiwa bila kulipwa, ilikabidhiwa kwa washitakiwa ambao ni wafanyakazi wa benki hiyo. [67]
kali 
Mussa Hassan Mgosi aliwainua mashabiki wake kwa kuachia shuti kali lililomshinda kipa wa Villa Squad na kujaa wavuni dakika ya 22 baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Juma Nyoso. [68]
kambi 
MCHEZA tenisi wa Tanzania, Shaaban Ibrahim aliyefanikiwa kucheza fainali ya michuano ya tenisi Kanda ya Mashariki anatarajia kuondoka nchini Januari 31 kwenda Afrika Kusini kuweka kambi, kabla ya kushiriki Michuano ya Tenisi ya Afrika kwa Vijana iliyopangwa kufanyika Machi nchini Morocco. [69]
kanda 
Huku hayo yakiendelea Tumsifu Sanga anaripoti kuwa Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova alisema hatatoa kibali cha kuandamana kwa wanafuzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam mpaka atakapopata uhakika wa hali ya usalama barabarani kwa siku hiyo. [70]
kansa 
Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [71]
kati 
Kiwanja namba 87 eneo la viwanda Kipawa ni moja kati ya viwanja vilivyomilikishwa kwa National Milling Corporation (NMC), S LP 9502 Dar es Salaam," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. [72]
kiasi 
Inakisiwa kuwa serikali inaweza kuokoa kiasi cha kikubwa na kuridhisha cha fedha kwa uamuzi wa kusimamisha ununuzi wa magari katika serikali. [73]
kibao 
Jamaa kauaaaa, kabakaaaaa, kafisadiiiiiii, kafanya kufuru kibao zinazopingana kabisa na msahafu wa dini yake, lakini badala ya kumkemea twamtetea. [74]
kile 
Hata hivyo CHADEMA wamekataa ombi hilo kwa kile walichosema kuwa, ushirikianao wa vyama hivyo ulishakufa tangu wakati wa uchaguzi wa Tarime. [75]
kisha 
Mkurugenzi Mkuu wa Azaki, Marcel Katumba, alikiri kuwepo tatizo hilo na kwamba, baadhi ya asasi hizo, zinawasilisha moja kwa moja maombi kwa wahisani na kupata fedha kisha kuzitumia zinavyotaka. [76]
kitakuwa 
Naye mkurugenzi wa msanii huyo, Hartmann Mbilinyi anasema Steve anatarajia kutengenezewa kipindi ambacho kitakuwa ni fungakazi kwa sanaa ya vichekesho ambayo inaonekana kupata umaarufu mkubwa hapa nchini. [77]
kocha 
Naye kocha wa Villa, Ken Mwaisabula alisema amekubali matokeo, kwani anaamini kufungwa ni sehemu ya mchezo na washambuliaji wake hawakuwa makini katika umaliziaji. [78]
kote 
Lengo kubwa la kuigawa Tanzania katika kanda sita ni kuhakikisha tunapata urahisi kiutendaji ili mikakati yote ambayo tayari tumesha ipitisha iweze kote nchini. [79]
kuambiwa 
Ugomvi mwingi wa wanawake wengi unatokana na maneno ya kuambiwa ama kudhania. [80]
kuandika 
Hata hivyo Hakimu Kente alisema kwa sababu washitakiwa hao hawawataji kwa majina askari magereza, mahakama hiyo isingeweza kutoa onyo kwa askari hata wasiohusika bali itakachokifanya ni kuandika barua ikimwelekeza mkuu wa Magereza kuhakikisha mshitakiwa huyo wa kwanza anapatiwa matibabu. [81]
kubuni 
Wapinzani mnapaswa mwende kwa wananchi na kubuni mbinu ambazo zitawavutia wananchi ili kujiunga. [82]
kubwa 
Mamia ya wakazi wa Arusha na vitongoji vyake jana walikusanyika katika hospitali ya mkoa kutambua miili ya waliofariki na majeruhi hivyo kusababisha vurugu kubwa kutoka na kila mmoja kutaka kuingia katika hospitali hiyo. [83]
kuchokwa 
Afadhali hata mpira maana hatimaye mashabiki wataanza kudai mabadiliko lakini katika siasa, watu watashabikia weeeeeeeeeeeee huku chama fulani kimeshapondwa badala ya kupendwa, kimechekwa na kuchokwa na hata kuchukiwa kutokana na kuchakaa kwake. [84]
kufa 
Wakati wanaendelea kuangalia ile picha aliingia daktari aliyekuwa akimwangalia Kazim na kumwomba waziri afupishe mazungumzo, badala yake wamsake yule mvumbuzi wa dawa kwani isingepita saa 12 kabla ya Kazim kufa ikiwa hatapata ile dawa. [85]
kuja 
Jingine ni Land Rover lililokuwa linatoka Tengeru kuja Arusha, gari dogo la abiria lililokuwa linatoka Arusha kwenda Moshi na lori aina Scania lililokuwa na shehena ya chupa za soda. [86]
kujaribu 
Kujua na kujaribu kutumia njia sahihi ya kugombana kutasaidia kutatua migogoro yenu. [87]
kujua 
Na kwa sababu ya kukosa ubunifu, vyama hivi vya upinzani vinajikuta vikifanya kazi ya CCM. Yaani vinatumiwa kwa kujua au kwa kutokujua na CCM ili kuangamiza upinzani nchini. [88]
kukosa 
BAADHI ya wachezaji wanaoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu mkoa wa Dar es Salaam, Kili RBA wamesema moja ya sababu zinazochangia mchezo huo kukosa mwelekeo ni upendeleo wa wazi unaofanywa na baadhi ya marefa. [89]
kule 
Hii ni nafasi aliyoipata mwaka jana kwenye mashindano ya vijana kutokana na kufanya kwake vizuri, hivyo atakuwa kule kwa mafunzo ya mwezi mmoja kabla ya kuelekea Morocco. [90]
kumbe 
Zaidi ya yote kumbe alikuwa amechukua mkopo benki baada ya biashara zake kumchanganyia, ili kuboresha zaidi, akiamini kuwa kwa namna alivyokuwa akipata fedha angeweza kulipa deni ndani ya muda mfupi. [91]
kumuua 
Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [92]
kundi 
Vyanzo mbalimbali vya kuaminika vimelidokeza Mwananchi jana kuwa kundi la watuhumiwa hatari kutoka Kenya liliingia nchini Januari 6 mwaka huu kwa lengo la kuwatorosha baadhi ya watuhumiwa raia wa Kenya. [93]
kushona 
Amefahamisha kuwa amekuwa akichora kila anachobuni na kisha kushona mavazi yanayowezatumika katika shughuli mbalimbali. [94]
kuu 
Hata hivyo, alisema manispaa haiwezi kumchukulia hatua yoyote kwa sababu mmiliki ni serikali kuu, hivyo ni moja ya raslimali ambazo iliyokuwa Tume ya Rais ya Kubinafsisha Mashirika ya Umma (PSRC) ilipaswa kuwa na taarifa zinazohusu viwanja hivyo. [95]
kuua 
Ni suala la kawaida kuua albino na damu zao au viungo vyao tunavitumia kwenye shughuli hizo za uchimbaji madini na uvuvi, watu wengi wanafanya hivyo. [96]
kuwa 
Mbali na wizara hiyo, manispaa ya Temeke nayo imesema kuwa kitalu hicho kilichoelezwa na Wakala wa Serikali wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) katika usajili wa Kagoda, kuwa ndipo yalikuwa makao makuu ya kampuni hiyo hakiko katika eneo la manispaa hiyo. [97]
kuweka 
Katika hatua nyingine, Balozi Nasr alisema Rais Kikwete ni mfano wa kiongozi aliyefanikiwa na kuweka historia katika kuuongoza Umoja wa Afrika (AU) wakati akiwa mwenyekiti wa umoja huo. [98]
kuzidi 
Lakini mara nyingi kunyamaza ni kuzidi kuzidisha matatizo. [99]
kwa 
Hii inafuatia taarifa zilizotolewa na Brela kwa waandishi wa habari juzi jijini Dar es Salaam kwamba kampuni ya Kagoda inapatikana kwenye kiwanja kilichopo kitalu namba 87 eneo la Kipawa, wilayani Temeke. [100]
kwake 
Alibainisha kuwa kumbukumbu za usajili wa kampuni ya Kagoda zilichukuliwa ofisini kwake kwa maagizo ya kamati iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kwa uchunguzi baada ya kampuni hiyo kuhusishwa na kashfa ya ufisadi wa Sh40 bilioni za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA). [101]
kwenda 
Aliondoka kwenda Kisiwa cha Unguja kuendelea na ziara yake. [102]
langu 
Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni,” alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [103]
lao 
Aliendelea kusema ya kuwa alichokishuhudia yeye ni kuona gari lao likipunguza mwendo na kwamba, gari aina ya Land Rover lilikuwa linataka kulipitia lori aina ya Scania na ghafla alisikia kishindo kikubwa na basi walilokuwa wanasafira lilitumbukia mtoni. [104]
lazima 
Ikumbukwe kuwa ndani ya gereza hilo kuna mtuhumiwa hatari ambaye aliwahi kuingia katika gereza moja huko Kenya na kuwatoa washirika wake sasa lazima tuchukue tahadhari zote,"alidokeza. [105]
leo 
Hata hivyo, upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Mabere Marando uliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi leo, ili wakajadiliane na wateja wao kwanza. [106]
ligi 
Alisema hakuna jambo la kuizuia Simba kushindwa kutimiza malengo yake kwa sasa na kuwataka mashabiki na wanachama wake kuondoa wasiwasi kwa kuwa, wao watamaliza ligi wakiwa vinara si ya pili au ya tatu, hizo ni nafasi za timu nyingine si Simba. [107]
linatoka 
Magari ambayo yalihusika katika ajali hiyo ni basi la abiria aina ya Fuso la kampuni Lim Safari lililokuwa linatoka Arusha kwenda Moshi. [108]
lolote 
Viongozi hawa wamekaa madarakani kwa muda mrefu lakini hakuna lolote wanalofanya. [109]
maana 
Kocha wa Simba Patrick Phiri alisema timu yake imecheza vizuri, ndiyo maana walishinda na anaamini wataendelea kufanya vizuri. [110]
macho 
Aliongeza kuwa 'mbali na kuchaguliwa katika kikosi hiyo aitoshi bali na kupata namba ili nionekane na mawalaka wa kimataifa na kushawishika kwa uwezo wangu kwani ninaamini macho na masikio yote duniani yatakuwa yameelekezwa huko Ivory Coast ambapo kutakuwa pia na mawakala mbalimbali wanaotafuta wachezaji. [111]
majina 
Hata hivyo alishindwa kuwataja majina askari hao wa magereza kutoka Dar Es Salaam wanaoendesha vitendo hivyo, lakini aliiomba Mahakama itoe kibali akapatiwe matibabu kutokana na maumivu anayoyasikia kichwani na kifuani. [112]
maombi 
Kenyela aliwasilisha maombi kupinga dhamana kwa washitakiwa. [113]
mara 
Hata hivyo, Ulomi alishauri Mwananchi kuwasiliana na manispaa husika kwa kuwa mchakato wa umilikishaji wa viwanja mara nyingi huanzia kwenye halmashauri. [114]
mfupi 
Anasema kuwa muda uliopo ni mfupi mno kabla ya kwenda Afrika Magharibi hivyo ni muhimu basi wachezaji waliomo katika kikosi chake wakaishi kulingana na maadali ya mchezaji soka ili kulinda viwango vyao lakini pia kwavile muda mwingi watakuwa katika klabu zao ni muhimu wakafata maelekezo ya walimu wao kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamemsaidia kwa kiasi kikubwa. [115]
mgao 
Bandari ya Dar es Salaam imepoteza kiasi kikubwa cha mgao wake wa soko (Market share) kwa bandari shindani ya Mombasa," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. [116]
mimi 
Hata ningekuwa mimi nisingekubali kushirikiana na wanasiasa kama hawa. [117]
minne 
Ripoti hiyo ya miaka minne iliyopita inaonyesha kuwa Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya 127 mwaka 2005 hadi 147 mwaka jana. [118]
misitu 
Maadhimisho ya siku hiyo yaliyoanza kuadhimishwa mwaka 2001 yamekuja huku kukiwa na taarifa kuwa sekta ya misitu imekuwa ikikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo upoteaji wa miti. [119]
miti 
JANUARI Mosi mwaka huu ilikuwa ni siku ya taifa ya kupanda miti. [120]
mkali 
Hata hivyo, udahili chuoni hapo unaendelea chini ya ulinzi mkali wa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na mafisa wa usalama wa taifa waliotanda kila eneo. [121]
mkuu 
Mfano ameweza kusaidia Comoro kwa njia za kisasa bila kumwaga damu, Kenya pia aliingilia kati mgogoro uliotokea baada ya uchaguzi mkuu wa 2007. Hapana shaka yeye ni mfano wa kuigwa katika utatuzi wa matatizo ya Bara la Afrika," alisema balozi Nasr. [122]
mno 
Ni mapema mno kusema chanzo cha ajali hiyo, vijana wanagu wanaendelea kutoa miili na kuyaondoa magari katika eneo hili; tutatoa taarifa mara baada ya kazi ya uokoaji kukamilika," alisema Kamanda Boaz. [123]
msaidizi 
Jamaa huyo ambaye alikuwa kama msaidizi wake wa karibu, alikuwa akimuwakilisha katika kazi mbalimbali na ndiye aliyekuwa ana siri zake nyingi. [124]
mtandao 
Kuna baadhi ya wasomaji wataanza kujiuliza e-government ni nini? Hizi ni huduma ambazo zinatolewa na serikali kwa wananchi wake kwa njia ya kompyuta ambayo imeunganishwa katika mtandao wa internet. [125]
mto 
WATU 15 wamefariki dunia na wengine 12 wamejeruhiwa vibaya baada ya magari matano kupata ajali katika daraja la mto Nduruma, wilayani Arumeru, Arusha jana mchana. [126]
muda 
Ilifafanua kuwa hati ya umiliki wa kiwanja hicho ilitolewa kwa barua ya toleo, yenye kumbukumbu namba ILA/11984/1/DSM ya Oktoba 3, 1980 iliyoonyesha kuwa mmiliki atakuwa nacho kwa muda wa miaka 99 kwa ajili ya matumizi ya viwanda. [127]
mume 
Wanaonyanyasa wanawake wachukuliwe hatua kali LEO katika gazeti hili tumechapisha habari kuhusu tukio la mama mmoja mkazi wa Kijiji cha Iyumbu kilichoko Kata ya Mugungira, wilayani Singida, kunusurika kuuawa na mume wake baada ya kumkata kwa panga kutokana na kukaidi amri yake ya kumzuia kuhudhuria kliniki ya ujauzito. [128]
mumeo 
Kubeba ulichoambiwa ukakitumia kama fimbo ya kumhukumu mumeo ni makosa makubwa. [129]
mumewe 
Mama huyo ambaye hivi sasa amelazwa hospitalini akitibiwa majeraha hayo, alinusurika kuuawa baada ya mume wake kumwona mama yake mzazi akirejea kutoka kisimani kuchota maji na baada ya kutenda kosa hilo mumewe alitorokea kusikojulikana. [130]
mwa 
Alisema Azaki zinapaswa kufanya kazi bega kwa bega na serikali, kwa kuwasilisha ripoti za kazi kila inapofika mwishoni mwa mwaka. [131]
mzazi 
Alisema kubainika kwa tatizo hilo kulitokana na fomu mbili za wanafunzi mapacha ambao wanalipiwa na mzazi mmoja huku kila mwanafunzi akiwa na daraja lake la malipo. [132]
naamini 
Naheshimu uhuru wa Tanzania, naamini katika haki, sikubali hatua ya balozi yoyote wa nje kuzungumzia mambo ya ndani ya Tanzania. [133]
nami 
Hivyo ndiyo nami nikafikia hatua ya kujiuliza swali hili kuhusiana na nchi yetu kushuka. [134]
nani 
Mbrazil huyo anasema kuwa soka ya dunia ya sasa imebadilika mpira hauchezwi kwa kuangalia rekodi za nyuma kwamba nani na nani wamefanya nini siku zilizopita kwani kila mmoja hutaka kufikia malengo aliyojiwekea. [135]
nao 
Wabuni mikakati yao wenyewe ili nao wainuke, siyo kuitegemea CHADEMA. CHADEMA wao wameanza, vyama vingine vifuate. [136]
naye 
Anasema Stive ana kipaji ndiyo maana kampuni yake imeamua kufanya naye kazi kwa ukaribu, ili kuweza kufanya mipango yake ya kukuza sanaa yake kimataifa inafanikiwa, na ulimwengu ufahamu kuwa mbali na soka pia Tanzania kunavipaji vingine. [137]
ndio 
Tafadhali wasiliana na Ilala ndio watakaokuwa na taarifa za kiwanja hicho," alisema Chawala. [138]
ndugu 
Chanzo kimoja ndani ya Gereza, kimefahamisha kuwa karibu kila siku kumekuwa kukifanyika upekuzi katika vyumba vya mahabusu na utaratibu wa baadhi ya mahabusu kupelekewa chakula na ndugu zao umefutwa. [139]
ngumu 
Siku moja usiku akiwa nyumbani alitafakari sana hali ngumu ya maisha ambayo angeanza kuishi. [140]
nyumbani 
Siku moja Kazim akiwa amejipumzisha nyumbani, alifuatwa na watu wale waliokuwa wakisimamia biashara zake za uvuvi wa samaki na uchimbaji wa madini. [141]
onyo 
Wakili Median Mwale anayewatetea baadhi ya washitakiwa katika kesi hiyo wakiwemo Wakenya aliiambia Mahakama kuwa wateja wake wamemuarifu juu ya kuwepo kikosi hicho maalumu kinachofanya mambo hayo ya unyanyasaji na kuiomba mahakama itoe onyo kwa mkuu wa Gereza la Karanga kwa niaba ya askari hao. [142]
pale 
Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini(Uvejuta), Silinde David alisema maandamano yao yatabaki pale pale hata kama viongozi wao wamekamatwa. [143]
picha 
Tukio pia hili linatupa picha kwamba, elimu ya afya ya uzazi bado watu wengi hawajaipata nchini hususan maeneo ya vijijini, hivyo pamoja na harakati za kupiga vita ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake, elimu ya uzazi itolewe kwa wanaume wote hasa wa vijijini. [144]
poa 
Na kwa kuwa Makengeza Enterprises haitaki watu wapekue baadaye na kupata funza badala ya mafunzo, viatu maalum vitauzwa kwa bei poa hapohapo kwenye tamasha. [145]
programu 
Hadi awamu ya kwanza ya programu hiyo ilipomalizika mwaka jana, mafanikio yaliyopatikana na kidogo. [146]
rafiki 
Ninaye rafiki yangu ambaye alikuwa mpigania uhuru wa Afrika Kusini. [147]
rais 
Alisema mahusiano yanayojengwa na Rais Kikwete, yanaashiria kurejea kama iliyokuwa wakati wa utawala wa hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na rais wa kwanza wa Misri, hayati Gamal Nasir na kwamba anatamani kuona yakirejea kabla hajafa. [148]
rekodi 
Akizungumza na Mwananchi jana Mgosi alisema anafanya hivyo ili ajiweke katika rekodi nzuri na kujihakikishia namba katika kikosi cha timu ya taifa ambacho kitakwenda kwenye fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani nchini Ivory Coast mwezi ujao. [149]
roho 
Nakufa, mkuu wa polisi unaniua, sawa mimi nimemuua albino, lakini wewe unaniua mimi kwa kunipiga kibao, imeandika wapi kwamba muharifu apigwe, kabla ya kufikishwa mahakamani,” alisema Kazim huku akikata roho. [150]
ruhusa 
Nongwa alisema washitakiwa pia hawaruhusiwi kwenda kwenye maeneo ya chuo kikuu bila ruhusa ya mahakama na hawaruhusiwi kufanya mikutano bila ruhusa kutoka mamlaka husika na watatakiwa kuripoti kituo cha polisi Oysterbay kila Ijumaa asubuhi. [151]
saa 
Ajali hiyo ambayo ilisababishwa kufungwa kwa barabara ya Arusha, Moshi kuanzia mchana hadi saa 12 jioni ilitokea baada na magari hayo kukutana katika daraja hilo jembamba na kugongana. [152]
sanaa 
Anasema yeye binafsi amepania kuboresha sanaa yake na kuipenyeza katika soko la kimataifa. [153]
sasa 
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Ilala kwa gazeti hili ilisema baada ya kuchunguza kumbukumbu za mafaili ya umilikishaji wa viwanja, ilibaini kuwa kiwanja kilichoko katika kitalu namba 87, Kipawa kilikuwa kinamilikiwa na lililokuwa Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC) ambalo sasa limekwishakufa. [154]
sauti 
Jina laStive Nyerere limetokana na sanaa yake kwa kuwa alianza usanii kwa kuingiza sauti ya Baba wa Taifa ,Mwalimu Julius Nyerere. [155]
sawa 
MISRI imepinga tabia ya mabalozi wa nchi za nje kuzungumzia mambo ya ndani ya Tanzania, akisema kufanya hivyo ni sawa na kuingilia uhuru na haki ya taifa. [156]
sekta 
Rais Kikwete tayari ametoa maelekezo kuhusu suala hilo la kusimamisha ununuzi wa magari ili kupata fedha za kuwekeza katika sekta ya kilimo. [157]
semina 
Wakizungumza katika semina ya mafunzo ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii jijini Dar es Salaam juzi, wabunge hao walisema, asasi hizo ni nyingi na zinaendelea kuongezeka. [158]
shida 
Ndipo hapo tunaona shida ya ushabiki. [159]
si 
Kamanda Kova alisema Jeshi lake limepokea barua ya wanafunzi hao ikilitaka jeshi la polisi kutoa ulinzi siku ya Jumamosi katika maandamano ya wanafunzi hao kupinga sera ya uchangiaji wa elimu ya juu ombi lao litafanyiwa kazi kwa muda wa masaa 48 na uwezekano wa kukataliwa ama kukubaliwa upo na si kuhusiana na maandamano kwa kuwa hawakuomba kibali cha kuandamana. [160]
sifa 
Kwa hiyo, kwa sifa ya Tanzania ilivyo, tangu eeeeenzi za mwalimu, tutasimama upande gani? Upande wa wanaonyanyaswa. [161]
sio 
Majeruhi wengine ni Sloyce Joachim, Elia Abdalah, Dismas Patrece na Isack Angalili ambao wote bado hali zao sio nzuri na baadhi walitarajiwa kufanyiwa upasuaji. [162]
soka 
Alisema huu ndiyo wakati wa kutimiza ndoto zake za kucheza katika mataifa yaliyoendelea kisoka barani Afrika na Ulaya, kwani nafasi hiyo imepatikana huwenda isipatikane tena, hivyo ni lazima aonyeshe juhudi kwani kila kukicha kikosi kinabadilika na vijana wanakuja juu sana katika soka. [163]
taasisi 
Vile vile sababu nyingine ambayo inasababisha teknolojia hii muhimu kutotumika ipasavyo ni pamoja na kukosekana kwa sera na mipango madhubuti ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama), katika taasisi za serikali. [164]
tajiri 
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [165]
tangu 
Amri hiyo ilitolewa kabla ya shahidi wa kwanza katika kesi inayomkabili kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM); na wafanyakazi watatu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuhusiana na tuhuma za wizi wa fedha za EPA hajaanza kutoa ushahidi na kuwafanya waandishi ambao walikuwa mahakamani hapo kupigwa na butwaa kutokana na ukweli kwamba, tangu mwanzo kesi hizo hawajawahi kupewa ama kudaiwa vibali. [166]
tatu 
Hii ni mara ya tatu kwa ajali mbaya kutokea katika eneo hilo ndani ya kipindi kisichozidi miezi sita. [167]
tena 
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 5 mwaka huu itakapotajwa tena. [168]
tu 
Nawaomba mashabiki na wapenzi wetu wasiwe na wasiwasi kabisa, kwani matunda na harakati zetu zinaanza kutimia, msife moyo kuona kuwa Yanga bado wamebakiza michezo tu itangaze ubingwa kwani mpira unadunda," alisema Dalali. [169]
tuna 
Sisi tuna mikakati yetu tuliyojipangia wenyewe wanasimba kuhakikisha tunachukuwa ubingwa wa ligi hii ya Vodacom mwaka huu licha ya kuwa nyuma kidogo kwa pointi kadhaa, lakini tunahakikisha michezo yetu tisa iliyobaki tunashinda yote, hatutoi hata sare ya aina yoyote ile, kwani sasa tumeazimia kuwa kazi ni moja tu," alimaliza Dalali. [170]
ujumla 
Kwa ujumla, tunalaani vikali kitendo hicho cha kinyama na unyanyasaji, kwani kinaonyesha wazi bado kuna baadhi ya wanaume wanaendelea kuwafanyia ukatili wanawake, kinyume cha sheria na haki za binadamu. [171]
uko 
Mimi sikisemi chama chochote kile maana ushabiki huo uko kote kote, kwa chama cha zama zile hadi chama cha zama hizi. [172]
vema 
Katika kusisitiza maandalizi ya Yanga kwa ajili ya michuano hiyo TFF juzi kupitia msemaji wake Florian Kaijage walitakaa mabingwa hao kutojisahau na mafanikio yao walioyapata kwa sasa na badala yake wajiandaa vema kwa mchezo huo dhidi ya Etoile d'Or Minonstry. [173]
viatu 
Kutakuwepo na sanamu kubwa ya Kichaka na wote mtapewa nafasi ya kuitupia viatu kwa nguvu zote. [174]
vile 
Idarous amewahi kufanya kazi mbalimbali zilizokuwa na mafanikio makubwa, kama vile kuandaa onyesho la Miss Victoria lililofanyika 1987 na Shyrose Banji aliibuka kidedea. [175]
vipi 
Mambo vipi mashosto. [176]
vita 
Nasr alisema vita dhidi ya ufisadi ni ya ndani na haipaswi kuingiliwa na nchi yoyote ya nje na na akisisitiza kuwa Tanzania ni nchi imara yenye uhuru wake na uwezo wa kuamua na kutekeleza mambo yake. [177]
vya 
Alisema kuwa maendeleo ya Tanzania yana sura mbili ya vyanzo vya raslimali. [178]
vyema 
Steve Mengere maarufu kwa jina la Stive Nyerere, anasema mwaka mpya wa 2009 ni mwaka wa mabadiliko kwake na anasema ni vyema kwa wasanii wenzake kuboresha kila kitu katika maisha kuanzia katika kazi za usanii, maisha, tabia na mavazi. [179]
vyote 
Hivi vyote vinapungua kwa kiasi kikubwa chini ya utaratibu huu. [180]
wake 
Mheshimiwa hakimu tunaomba kesi iahirishwe hadi kesho (leo) ili tukapate ufafanuzi juu ya Data base na uhifadhi wake," alisema Marando. [181]
wako 
Sasa Chadema wameanza Operesheni Sangara, wameshavuruga mikoa ya kanda ya Ziwa na sasa wako jijini Dar es Salaam. [182]
wala 
Gazeti hili lilipofutilia katika Manispaa ya Ilala, maafisa walisema hawana kumbukumbu wala taarifa za kiwanja hicho. [183]
wangu 
Mheshimiwa Hakimu nihakikishiwe usalama wangu, sisi Wakenya tunadhulumiwa sana Gerezani ,"alilalamika Mshitakiwa huyo na kuungwa mkono na mshitakiwa wanne, Ex- F. 940 PC Nathaniel Manyama ambaye ni Polisi aliyefukuzwa kazi baada ya tuhuma hizo. [184]
wao 
Afisa Uhusiano wa manispaa hiyo, Lynn Chawala alisema kuwa eneo la Kipawa liko Manispaa ya Ilala, hivyo taarifa za kiwanja hicho watakuwa nazo wao. [185]
wapi 
Upo hapo! Kuwa makini kumsikiliza kunakupa nafasi ya kujua umekosea wapi au tatizo liko wapi na kurekebisha ikibidi. [186]
wapo 
Katika gereza hilo, wapo Wakenya 12 wanaotuhumiwa kwa matukio kadhaa ya uhalifu likiwemo la uporaji wa Sh5.3 bilioni mali ya Benki ya NBC Tawi la Moshi inayowakabili raia wanane wa Kenya. [187]
wawe 
Na sasa si suala la Waislamu tu, wawe Waislamu wenzetu au Waislamu waleee. [188]
wenu 
Wakati mwingine unaweza kukuta jambo kubwa mliligombania linakuwa dogo kutokana na uelewa wenu kwa kila moja wenu. [189]
wenzetu 
Sisi tutafanya maandamano hata kama wenzetu wamekamatwa," alisisitiza. [190]
wote 
Wengine ni Mtawa, Anastazia, Mchungaji Peter Maina, David Ngunda na Alice Kinga wote wakazi wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro. [191]
yao 
Jeshi la polisi lina taratibu zake wao waliomba kupewa ulinzi hawakuomba kibali cha kufanya maandamano, hivyo tunatarajia kujadili barua yao ya kuomba ulizni na si maandamano kwa kuwa barua yao tumeipata na tunaifanyia kazi ndani ya masaa 48 na tutawapa jibu la barua yao kulingana na hali ya usalama itakavyokuwa siku hiyo," alisema Kamanda Kova. [192]
yenu 
Inachokupasa ufahamu kuwa kuziba kauli katika suala ambalo limekuudhi hupelekea madhara makubwa mbeleni katika mahusiano yenu na huenda ikaathirika afya yako. [193]
yote 
Wakili wa upande wa utetezi, Flugency Massawe alipinga hoja hizo kwa madai kuwa makosa yote wanashitakiwa nayo washitakiwa yanastahili dhamana na kwamba, hakuna kiapo kinachoendana na kosa la washitakiwa. [194]
yuko 
Huyu yuko kwenye upande wa madini. [195]
yule 
Na ni vyema ukaongea naye ili upate ukweli kwa kusema wasiwasi wako, au kile ulichoambiwa kwa kumkutanisha na yule aliyesema itasaidia kuondoa migogoro yenu. [196]
zaidi 
Alisema katika utawala wake Rais Kikwete, amekuwa mfano wa kuigwa ndani na nje ya nchi yake na uwepo wake madaraka unaonyesha kurejesha mahusiano mazuri zaidi na nchi jirani. [197]
zako 
Zipo hizi hisia wakati mwingine za kumchukia bila kujua sababu, lakini sababu ni kwamba dhana zako ndizo zinakupeleka huko. [198]
zetu 
Moja ni nguvu zetu wenyewe, na sura ya pili ni nguvu za marafiki watu. [199]
zote 
Baada ya kusikiliza hoja zote hakimu Nongwa alitupilia mbali hoja za upande wa mashitaka kwa kuwa washitakiwa bado ni watuhumiwa, hadi mahakama itakapothibitisha kosa lao. [200]