Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-13

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
acha
We mwishiwa supu acha roho mbaya. [2]
aende
Kila mwishiwa aende kujiandaa kuonyesha kipaji chake siku ile na mshindi atapewa nafasi ya kujaribu kipaji chake kwenye kituo cha runinga. [3]
aina
Kocha wa Stars, Marcio Maximo alisema kwamba mchezo huo utakuwa mgumu na wenye kila aina ya burudani na vijana wake wako sawasawa kupambana. [4]
ajenda
Hata hivyo, katibu wa CCM Arusha, Mohamed Mbonde alisema jambo hilo halipo katika ajenda. [5]
akawa
Tena kichekesho ni kwamba kila mwishiwa akawa amebeba bahasha lililotuna. [6]
akina
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Afya na Ustawi wa Jamii wa SMZ, Juma Rajab amesema kutokana na tahadhari ya kiafya, wanawake wajawazito hawatapewa dawa hiyo kwa kuwa, bado hakuna taarifa za utafiti wa madhara yake kwa akina mama wajawazito. [7]
ama
AIBA waliagiza kuitishwa kwa uchaguzi ama kuteuliwa kwa kamati ya muda ndani ya mwezi mmoja tangu tulipofutiwa uanachama, sasa ni zaidi ya miezi mitatu imepita na hakuna anayetoa maelezo," alisema. [8]
amani
Alisema hiyo ni moja ya changamoto kubwa zinazoikabili serikali yake kwa kuwa, ndizo zitaleta amani na utulivu wa nchi na akakiri kuwepo kwa tofauti kubwa za kimtizamo baina ya vyama vya siasa, ingawa alisema ni jambo la kawaida kwa vyama kutofautiana. [9]
ana
Hata hivyo, hakuna shaka kwamba kama Rais Kikwete hata kuwa mwoga, ni wazi ushindi uko kwake kwa sababu yeye ana kila kitu kwanza, anashikilia dola, ana vyombo vya kumsaidia kuwakamata na kuwashtaki, hivyo kundi hilo la mafisadi litakwama. [10]
anatoa
Mbali na wazazi wake Shabani anatoa sifa kwa makocha wake ambao umfundisha mbinu mbalimbali za mchezo huo hao sio wengine ni Martin Dzuwa na Nico Jonas kuwa ndio siri ya mafanikio yake kutokana na maelekezo yao. [11]
au
Ewura imeeleza kuwa, imeshawasilisha bei hizo mpya kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili atangaze kwenye Gazeti la Serikali na kuanzia hapo yeyote atakayekiuka bei hiyo atakabiliwa na adhabu ya faini ya Sh3 milioni au kunyang'anywa leseni au adhabu zote mbili kwa wakati mmoja. [12]
baada
Akizungumzia muafaka wa CCM na Chama cha Wananchi (CUF), Rais Karume alitaka kuendelezwa kwa mazungumzo baina ya vyama hivyo vikuu visiwani baada ya kukwama kwa miezi kadhaa sasa. [13]
baadae
Akizungumza na Mwananchi jana Rais wa Shirikisho hilo Chacha Michael alisema wameandaa utaratibu maalum wa kuhakikisha wanawaorodhesha mabondia wote waliopo mikoani ili kupata idadi kamili na baadae kuandaa mashindano ya kulipwa katika mikoa yote hapa nchini. [14]
bado
Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Arusha, Semmy Kiondo alisema kuwa pikipiki hizo bado hazijakabidhiwa rasmi kwa makatibu kata 17 wa CCM wilayani Arusha. [15]
bali
KOCHA wa Polisi Morogoro, John Simkoko amesema ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Karega Sugar Jumamosi ni tahadhari kwa timu nyingine zinazoshiriki ligi ya Vodacom kwamba kikosi chake hakina muda wa kusubiri bali kinasaka ushindi tu. [16]
beki
Tangu juzi mashabiki pamoja na wadau mbalimbali wa hapa wamekuwa wakiisema vibaya Tanzania baada ya beki Salum Sued kuonyeshwa kadi nyekundu katikamechi ya nusu fainali dhidi ya Kenya. [17]
bila
Mafuta ya dizeli ndiyo yanayopatikana bila ya shida kwenye vituo vingi na inauzwa kwa bei iliyotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura). [18]
bunge
WADAU wa demokrasia na utawala bora nchini, wameshauri kwamba wabunge wasiteuliwe kuwa mawaziri, badala yake utafutwe utaratibu mwingine wa kuwapata mawaziri nje ya bunge. [19]
cha
Katika kipindi cha kuelekea Krismasi, petroli ilipanda ghafla na kufikia hadi Sh1,800 na wauzaji walisingizia kuwa hiyo ilitokana na shehena walizokuwa wakitegemea kushindwa kufika kwa wakati kutokana na meli zilizobeba mafuta hayo, kuhofia kupita pwani ya Somalia ambayo ina maharamia wanaoendelea kuteka meli za mizigo na kudai donge nono ili waziachie. [20]
chama
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amewataka viongozi wa chama hicho mkoani Arusha, kutoa maelezo juu ya msaada wa pikipiki 19 ambao alitakiwa kuugawa kwa watendaji katika wilaya ya Arusha. [21]
chanjo
Chanjo ya kipindupindu isiwalemaze wananchi JUZI Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ilitangaza kuwa Januari17, mwaka huu itaanza kuifanyia majaribio chanjo mpya ya ugonjwa wa kipindupindu katika visiwa vya Unguja na Pemba, ikiwa ni juhudi zake za kutokomeza ugonjwa huo visiwani humo. [22]
chochote
Kumbe yeyote aliyepeleka chochote kwa waamuzi alienguliwa kwenye shindano moja kwa moja. [23]
dereva
Juma Abdalah ambaye ni dereva wa daladala kati ya Mwenge na Kariakoo. [24]
don
Suti hilo! Yaani suruali ilikuwa mfano wa ‘don’t touch’ na tai ilikuwa inajikunja kutokana na kutumika miaka si chini ya ishirini. [25]
endapo
Alisema kuwa endapo Wazanzibari watatekeleza wito wake, wataweza kuondoa tofauti za ukabila na vyama vya siasa. [26]
enzi
Kuhusu tofauti ya mchezo huo hivi sasa na zamani Kibira anasema kuwa enzi zao walikuwa wakijituma sana katika kufanya mazoezi kwa pia wanapokuwa katika mechi kwa sababu waliani kuwa wameajiliwa kwa ajili ya kazi hiyo. [27]
es
Jana Ewura ilitangaza bei mpya za mafuta zitakazotumiwa kuanzia Januari 13. Kwa mujibu wa bei hizo, jijini Dar es salaam, petroli itauzwa kati ya Sh1,171 na Sh1,259 kwa lita, wakati dizeli itauzwa kati ya Sh1,301 na Sh1,390 kwa lita. [28]
fedheha
Lakini baada ya kutangulia kufungwa na Bara dakika ya 13 kupitia kwa Danny Mrwanda, ili kuepuka fedheha Zanzibar ilisambaratika na kuanza kucheza mpira na iliposawazisha tu dakika ya zisizozidi nne baadaye kupitia kwa Nadir Cannavaro, ikawa inashambulia kwa umakini mkubwa huku timu karibu yote ikiwa nyuma. [29]
fulani
Watuvumilie kwa kipindi fulani," anasema Maximo. [30]
haina
Akitetea hoja yake kuwa serikali inaliendesha bunge, Arfi alisema serikali inawasilisha bungeni miswada mingi ya dharura hata kama haina maslahi kwa taifa huku ikiacha mambo ya msingi yanayoigusa jamii. [31]
haja
Kuna haja ya kutenganisha utendaji wa shughuli za bunge na za serikali kwa kuepuka kuteua wabunge kuwa mawaziri," alishauri Peter Masika, ambaye ni mjumbe wa Baraza la APRM nchini. [32]
halafu
Alianza kufukuzwa kocha halafu baadae timu ikavunjwa ikaundwa upya ndio hii imekuja Chalenji hapa ikatema ubingwa tuliokuwa tunaushikilia. [33]
hana
Mathalani yeye mumeo hana kawaida hiyo ya kurudi jioni nyumbani ama kwa necha ya kazi yake basi hulazimika kuwepo kazini muda huu wa jioni, bado unaweza kuutumia muda wa usiku baada ya chakula cha jioni. [34]
hao
Ewura imewataka wauzaji wa bidhaa hiyo kuuza petroli kwa Sh1,166 kwa lita, ingawa vituo vinavyouza bidhaa hiyo vimekuwa vikiuza kwa Sh1,233 kwa lita, tofauti na bei ambayo ilikuwa ikitumiwa awali na wafanyabiashara hao ambayo ilikuwa kati ya Sh1,450 na Sh1,600 kwa lita ya petroli. [35]
hapa
Katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba mapema mwaka jana aligoma kugawa pikipiki hizo alipokuwa mkoani hapa, kutokana na kilichoelezwa kuwa ni utata wa upatikanaji wake na kutokichafua chama hicho. [36]
hasira
Zanzibar ina mikakati mibaya sana wanaharibu mpira, angalia wachezaji wangu walikuwa wakijaribu kufungua na kupanda lakini wenzetu wao wameingia na mbinu moja tu hawataki kucheza mpira wao ni kulinda tu muda wote,îalisema Bobby kwa hasira baada ya kutoka suluhu. [37]
hawa
Unajua lazima watu waelewe hawa wachezaji siyo kwamba hawana nidhamu na mimi hata siku moja sijawahi kuwafundisha wasiwe na nidhamu,"alisema Maximo. [38]
hii
Lazima serikali ichukue hatua kali kukomesha hali hii," alisema Khamis. [39]
hilo
Bei ya mafuta ya taa Wakazi wengi wa Dar es Salaam walioongea na Mwananchi, walielezea kuwa tatizo hilo ni mgomo uliopangwa na wafanyabiashara hao kama njia ya kukwamisha mkakati wa serikali wa kudhibiti bei ya mafuta. [40]
hivi
Suala la mafuta sasa hivi limeshakuwa kero, kwa kuwa vituo vingi vimegoma kuuza. [41]
hizi
Unajua ndugu yangu waswahili wanasema biashara ni asubuhi jioni mahesabu hivyo nimewaambia wachezaji wangu kwamba wacheze kwa juhudi kuanzia mechi hizi za kwamba na sio kusubiri hadi maji yawe shingoni ndiyo tuanze kutapatapa. [42]
hofu
Waingereza walikuwa wanaihami Zanzibar kutokana na hofu za watawala wa Kisultani dhidi ya Wajerumani ambao wakati huo walikuwa wakitawala Tanganyika. [43]
hotuba
Hilo lilithibitishwa na Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha aliyesema katika hotuba yake kwamba, alikuwa haamini kinachotokea jinsi watu walivyojaa uwanjani hapo, akimaanisha kuwa hakutegemea umati mkubwa. [44]
hujui
Utamaduni huu shostito ni wa pwani, kama ulikuwa hujui chukua hiyo, Na ukweli ni kwamba wanawake wengi wa pwani wanajua maana ya chai ya jioni na ndiyo maana wanasifiwa kuwa wanayajua mambo. [45]
huko
Dar-es-Salaam ambapo linachapishwa huko kupitia Unguja hadi Pemba na lilikuwa litolewe bure kwa wananchi waliokuwa kwenye Uwanja wa Gombani ulio Kisiwani Pemba. [46]
humo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Aman Abeid Karume, amewataka wananchi visiwani humo kuondoa tofauti zao zenye misingi ya ubaguzi wa Pemba na Unguja, ili kujenga nchi yenye usawa. [47]
huna
Pumbavu kabisa, huna maana wewe, sasa ni lazima ufe, mwenye siri za dawa ni huyo albino uliyemuua, mbwa kabisa wewe,” alifoka waziri kwa hasira kisha kupiga simu kwa mkuu wa jeshi la polisi ili kumkata Kazim kwa kitendo chake. [48]
huo
Mgomo huo baridi ulisababisha vituo vichache vilivyokuwa vikiuza petroli kwa bei ya Ewura kufurika magari mengi na watu wenye madumu kwa ajili ya kununua petroli ya ziada, katika wiki ambayo bei ya mafuta katika soko la dunia imezidi kuporomoka na kufikia chini ya dola 39 kwa pipa. [49]
huru
Katika ripoti hiyo iliyoandaliwa na Timu ya Ufundi ya Tathimini (TAT), ilionyesha kuwa asilimia 88 ya wananchi waliohojiwa kuhusu uhuru wa bunge, walisema liko huru na asilimia 12 wakisema haliko huru. [50]
huu
Naamini TLP, PPT-Maendeleo na NCCR-mageuzi, wamegundua kuwa CUF itapata aibu ya kuanzia mwaka 2009 kwa kushindwa vibaya kwenye uchaguzi huu na hivyo vimeamua kuja kuwasaidia CUF kubeba mzigo huo wa aibu,"alisema Nnauye. [51]
huwa
Gazeti la Zanzibar Leo, ambalo kwa kawaida huwa halina rangi, jana lilishapishwa kwa rangi na kuandikwa makala mbalimbali za maadhimisho ya miaka 45 ya Mapinduzi ya Zanzibar. [52]
huwezi
Wameingia wote wamejikusanya nyuma ya mpira sasa huwezi kujua nini lengo lao, hawataki kusogea mbele wachezaji nusu uwanja wakipoteza wamejaa kwao huwezi kufanya lolote ndio maana mpira umekosa msisimko, sielewi ni akili gani walikuwa wanatumia au ni mpira wa Bara gani wanacheza hawa jamaa,îaliongeza Bobby. [53]
huyo
Habari za uhakika toka kwa viongozi wa mkoa, ambao mwishoni mwa wiki waliandamana na Rais Kikwete kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) mara baada ya kiongozi huyo wa nchi kusita kugawa pikipiki hizo, zimeeleza kuwa Kikwete alimwagiza katibu wa CCM Arusha, Mohamed Mbonde kushughulikia suala hilo. [54]
huyu
Nasikia unamjua, ni huyu hapa angalia vizuri picha, kama unajua anapatikana wapi, nitaagiza hata magari mengine yamsake maeneo hayo, nitaomba hata jamaa yangu mmoja usalama wa taifa mstaafu mwenye uwezo mkubwa katika masuala ya kupeleleza atusaidie kumpata,” alisema waziri. [55]
idadi
Kuhusu wanafunzi ambao hawakufanya mtihani, alisema ni 11,111 na kwamba idadi hiyo ni sawa na asilimia 36.61 ya wanafunzi wote. [56]
ikawa
Kauli hizo za Bobby zilikuja kujirudia kwa Marcio Maximo wa Bara wakati timu yake ilipoivaa Zanzibar lakini safari hii ikawa kwa staili ya aina yake kidogo. [57]
ile
Mechi ambayo awali ilikuwa icheze majira ya saa 6.30 mchana imesogezwa mbele huku ile nyingine la fainali baina ya Uganda na Kenya ikichezwa saa 1.00 usiku. [58]
imara
Tathmini ya timu hiyo inaonyesha kwamba itawatumia muda mwingi kutulia na kutengeneza timu imara na tishio kama ile walioivunja baada ya kufungwa na Taifa Stars ya Tanzania. [59]
imeanza
Kama klabu imeanza maandalizi ya michuano au ligi, wachezaji wake kuwa nje kwa wiki mbili ni nyingi sana. [60]
jipya
MAAFISA wa ngazi za juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) wamezuia nakala za gazeti jipya linalomikiwa na kampuni ya Zanzibar Media Corporation la Taifa Huru lisisambazwe katika sherehe za miaka 45 ya Mapinduzi Zanzibar. [61]
jua
Hivyo wewe ukimnyooshea mwenzio kidole, jua vingine vinakugeukia wewe," alisema. [62]
juu
Katika mikoa mingine, petroli itauzwa kati ya Sh1,201 kwa bei ya chini kabisa wilayani Kibaha, hadi Sh1,535 kwa bei ya juu kabisa katika mkoa wa Kagera, wakati dizeli katika mikoa hiyo itauzwa kati ya Sh1,339 kwa bei ya chini kabisa mkoani Morogoro na Sh1,693 kwa lita, ikiwa ni bei ya juu kabisa katika mkoa wa Singida. [63]
juzi
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limesema kauli iliyotolewa juzi na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kupinga oparesheni Sangara inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), si kauli ya waislamu wote. [64]
kaimu
Akizungumzia ziara ya kaimu mufti mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Utawala alisema kuwa ziara hiyo ni sehemu ya utaratibu aliyojiwekea kaimu mufti ya kutembelea baraza katika mikoa yote Tanzania na kwamba kaimu mufti ametembelea Dodoma na Morogoro na atatembelea mikoa mingine. [65]
kali
Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo, wanaiomba serikali kuchukua hatua kali kwa wale waliokaidi na wanaogoma kuuza mafuta hayo kwa madai ya kukataa kupunguza bei. [66]
kamati
Naye mjumbe wa kamati ya utendaji ya Chama cha ngumi za ridhaa mkoa wa Arusha ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini aliiomba serikali kuiingilia kati kama BMT imeshindwa hata kuteua kamati ya muda ya kuongoza Shirikisho hilo wakati mchakato wa uchaguzi ukiandaliwa. [67]
kamili
KILIMANJARO Stars ikiwa na kikosi kamili leo jioni inaivaa Burundi katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa kombe la chalenji. [68]
kansa
Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [69]
kasi
Hata hivyo alisema hali ya mfumko wa bei haukuwa mzuri katika mwaka 2007 na hivyo kusababisha kasi ya mfumko wa bei kwa bidhaa mbalimbali na kuongeza hali ngumu ya maisha kwa wanaanchi. [70]
kiasi
Uzoefu na wenyewe haununuliwi tunapaswa kupambana kidogo kidogo, mimi sikufurahi hata kidogo kwa kadi za Yondani na Sued kwavile zimeigharimu timu lakini hawapaswi kulaumiwa kwa kiwango cha juu kiasi hicho. [71]
kibao
Nakufa, mkuu wa polisi unaniua, sawa mimi nimemuua albino, lakini wewe unaniua mimi kwa kunipiga kibao, imeandika wapi kwamba muharifu apigwe, kabla ya kufikishwa mahakamani,” alisema Kazim huku akikata roho. [72]
kila
Alisema malengo ya mapinduzi yametimizwa kwa kutekelezwa ilani ya Chama Cha Mapinduzi, kikiendeleza yale ya Afro Shirazi (ASP) kilicholeta ukombozi kwa Zanzibar katika kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania nchini. [73]
kimoja
Anapenda, muwekee na kibiskuti kimoja cha tangawizi pembeni. [74]
kina
Kwa ujumla, matokeo hayo ni changamoto kwa serikali kufanya utafiti wa kina wa jinsi ya kuboresha elimu ya sekondari ili iende sambamba na juhudi za kuongeza idadi ya shule ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa nafasi za kidato cha kwanza ikilinganishwa na miaka ya nyumba. [75]
kipaji
Na katika kutafuta kazi zingine wanashambulia kazi za watu kwa dharau kabisa wakidhani kwamba kila kitu ni rahisi, hakuna cha kipaji wala cha kusomea. [76]
kitaifa
Karume alisema hayo jana katika sherehe ya miaka 45 ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliyofanyika kwenye kisiwa cha Pemba, Zanzibar na kurushwa moja kwa moja na TBC1 kutoka Chake Chake, Pemba zilikofanyia kitaifa. [77]
kocha
Burundi tunategemea hawawezi kutusumbua sana ingawa tunajua watakamia, lakini nafasi ya tatu ni yetu,"alisema kocha huyo kwa kujiamini. [78]
kombe
Tanzania ambayo leo inacheza na Burundi kuwania nafasi ya tatu ya kombe la chalenji ndio timu pekee ya CHAN inayokwenda. [79]
kote
Pia amweataka makocha pamoja na waamuzi wa Netiboli kote nchini kuwa na jitihada za kuendeleza mchezo huo kwa kuanzia ngazi ya vijiji ,kata, tarafa, wilaya na mikoa. [80]
kuamua
Siku ya vipaja? Mwishiwa Supu unawaita waamuzi kwa ajili ya siku ya vipaja? Hata sisi tunaweza kuamua. [81]
kufa
Wakati wanaendelea kuangalia ile picha aliingia daktari aliyekuwa akimwangalia Kazim na kumwomba waziri afupishe mazungumzo, badala yake wamsake yule mvumbuzi wa dawa kwani isingepita saa 12 kabla ya Kazim kufa ikiwa hatapata ile dawa. [82]
kufanya
Tukae pamoja kwa ajili ya kujadili mambo ya maendeleo, tofauti zetu katika siasa tuziache tunapoamua kufanya mambo ya maendeleo," alisema Rais Karume. [83]
kuimba
Kweli wanaweza kuingia hivihivi? Kweli wataingia kama milolongo ya vijana wanaotafuta nafasi moja ya Ustaa wakati ambapo hata wenzao wa mitaani wanawacheka wakijaribu kuimba. [84]
kukosa
Baba paroko huyo alisema suala lililoibuka sasa la ufisadi limekuwa likiambatana na shutuma kwa watu kuwa wanahusika na ufisadi hata kama si kweli, jambo ambalo linashusha hadhi na heshima za watu wengine na kuongeza kuwa kufanya hivyo ni kukosa maadili na ni aibu kwa taifa. [85]
kukutana
Hivyo walipanga muda wa kukutana. [86]
kule
Ni malengo ambayo nilijiwekea mapema kwamba jambo la kwanza ni kufikia hatua ya juu kabisa na pia niwe mmoja wa wachezaji watakaoiwakilisha kanda hii kule Morocco kwani itakuwa ni sehemu nzuri ya kupata uzoefu pamoja na mbinu mpya za kimchezo, kama unavyojua mashindano ya Afrika yatashirikisha mataifa mengi yakiwemo yale ambayo yapo juu kupitia mchezo huuíanasema Shabani. [87]
kumbe
Zaidi ya yote kumbe alikuwa amechukua mkopo benki baada ya biashara zake kumchanganyia, ili kuboresha zaidi, akiamini kuwa kwa namna alivyokuwa akipata fedha angeweza kulipa deni ndani ya muda mfupi. [88]
kumi
SHULE tisa za sekondari za kata katika kanda ya kati, zimekuwa miongoni mwa shule kumi zilizofanya vibaya katika matokeo ya mtihani wa kidato cha pili. [89]
kumpa
Alisema tayari walikuwa wameshakuja na magazeti hayo kwa ajili ya kuyasambaza lakini mara walipigiwa simu na kutakiwa kupeleka nakala kadhaa kwa wahusika wa Wizara ya Habari na wakafanya hivyo lakini jambo la kushangaza baada ya muda alipokea simu kutoka kwa naibu katibu mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Said Shaaban akimtaka asisambaze hata nakala moja ya gazeti hilo bila ya kumpa maelezo yoyote. [90]
kumpiga
Awali beki mwingine Kelvin Yondani alionyeshwa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Uganda, Ijumaa iliyopita baada ya kumpiga machoni Bryan Umony wa Uganda. [91]
kumuua
Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [92]
kuna
Hiki kikao kilipangwa hata kabla ya hili tatizo na kuna ajenda zake. [93]
kundi
Hiyo ni rekodi ya pekee kwenye mashindano hayo ya Chalenji hususani kwa timu zilizokuwa kundi A kwani hakuna kikosi kilichopewa kadi mbili nyekundu. [94]
kuona
Wanaume wanapenda kuona wanajaliwa kwa kumtengea chai tu ya kipekee inatosha kufikisha ujumbe kuwa unamjali. [95]
kuonana
Wapi waamuzi, wapi waamuzi! Unajua ni vizuri kuonana nao kwanza. [96]
kusema
Lakini madai hayo ya Waganda yamemkera Maximo ambaye ameibuka na kusema kwamba wachezaji wake waachwe ni presha inawasumbua. [97]
kutwaa
Mipango na malengo yetu na yaleyale kutwaa ubingwa na nafikiri kazi kubwa ipo Jumanne hii. [98]
kuua
Tunapongeza juhudi zilizofanywa na SMZ kukabiliana na kipindupindu kwa kutafuta njia moja wapo ya kudumu dhidi ya ugonjwa huo sugu unaoendelea kuua watu, hasa katika maeneo yanayotawaliwa na uchafu. [99]
kuweza
Kocha wa Azam, Dos Santos anawalalamikia washambuliaji wake kuwa walikosa umakini wa kufunga mabao mengi zaidi kipindi cha kwanza, Naye Ferix Miziro alisema anawashukuru vijana wake kwa kuweza kubadilika kipindi cha pili na kuweza kusawazisha. [100]
kwake
Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Malima ilifanyika nyumbani kwake Tabata na baadaye mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kwenda Msoma mkoani Mara kwa Maziko. [101]
kwani
Nawaomba wenzangu tuondoe mambo ya uzanzibari na upemba, kwani yanaweza kutupeleka pabaya. [102]
kwao
Stephano alisema wanafunzi 6,591 ni wasichana na 4,520 ni wavulana na kwamba kushindwa kwao kufanya mtihani, kulitokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mimba, utoro na vifo. [103]
la
Lakini Wizara ya Madini na Nishati imesema inasubiri kupata taarifa kutoka kwa watendaji leo asubuhi, kabla ya kuanza kuchukua hatua kwa wote waliokiuka sheria iliyotangazwa kwenye Gazeti la Serikali kuhusu bei elekezi za mafuta, kwa mujibu wa naibu waziri kwenye wizara hiyo, Adam Malima. [104]
labda
Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [105]
lake
Angalia mechi na Uganda alivyotoka Yondani timu ilikuwa kwenye matatizo makubwa, angalia pia na Kenya kadi ya Sued imeigharimu timu lakini yote hayo tatizo lake ni lile lile presha ambayo inasababishwa na kutokuwa na uzoefu, tuwape muda. [106]
langu
Kundi langu linawasanii watatu lakini tuna mpango wa kuongezeka zaidia kulingana na nafasi," alisema. [107]
lao
Stars leo itakuwa na beki wake tegemeo Shadrack Nsajigwa pamoja na Kelvin Yondani ambao pengo lao liliigharimu timu kwenye safu ya ulinzi, lakini itwakuwa na hasara nyingine kwani Salum Sued mwenye kadi nyekundu atakuwa jukwaani. [108]
letu
Kusajiliwa kwa shiriisho letu itakuwa changamoto ya kuendeleza mchezo huu zaidi kwani tutapata fursa ya kuandaa mikakati mbalimbali kwa mabondia wetu lengo likiwa ni kuleta mabadiliko na kuandaa mapambano mbalimbali ya kulipwa hasa Mkoani ambapo ndipo vipaji vilipojificha zaidi," alisema Chacha. [109]
licha
Wakizungumza na Mwananchi jana kwa nyakati tofauti, wadau hao walishangazwa na ukimya wa BMT kuhusiana na uchaguzi wa shirikisho hilo licha ya kuagizwa kufanya hivyo katika kipindi mwezi mmoja tangu kilipofutiwa uanachama. [110]
maana
Baadhi ya wananchi waliozungumza na Mwananchi ndani ya Uwanja wa Gombani walisema kuwa, walilazimika kufika katika sherehe hizo kwa kuwa walipewa vipande vya karatasi vilivyotakiwa kusainiwa na kuhakikiwa wakati wanapotoka na kuingia uwanjani hapo ndiyo maana hawakutoka hadi mwisho. [111]
macho
Alisema maendeleo yaliofikiwa na Zanzibar ni makubwa katika kipindi cha miaka 45 na aliwataka wananchi kujivunia maendeleo hayo na kuachana na watu wenye kuyabeza ambao hawana macho ya kuyaona. [112]
madini
Kuna sheria nyingi tu zinazolalamikiwa na mambo mengine ambayo bunge limekuwa likiihimiza serikali kuyatekeleza, ukiwemo ya Ripioti ya Jaji Mark Bomani ya madini, lakini serikali imekuwa kimya tu," alisema Arfi. [113]
maeneo
Naye dereva mwingine wa daladala anayehudumia kati ya Mwenge na Tegeta, Yusuph Khamis alisema kuwa vituo vinavyouza mafuta katika maeneo hayo ni vichache ukilinganisha na wingi wa vituo. [114]
majina
Alisema kutokana na hilo wengi hujikuta wakiwa na majina makubwa ndani ya mkoa wao na kushindwa kutambulika nje ya mkoa. [115]
mbali
Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa ngazi za juu, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais, Dk Ali Mohammed Shein na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. [116]
mbele
Katika hatua nyingine msaidizi huyo wa paroko alisema kuwa wanadamu wanapaswa kuishi maisha ya ukamilifu kwa kumkaribia Mungu kwani hawajui siku ambayo wataitwa mbele ya haki. [117]
mbinu
Rais Karume aliuambia umati unaomsikiliza kwamba, kumekuwepo na mafanikio makubwa katika kuimarisha miundo mbinu katika sekta mbalimbali, ikiwemo barabara za mjini na vijijini katika visiwa vyote vya Unguja na Pemba. [118]
mdogo
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (Nec), Nape Nnauye, ameukejeri ushirikiano wa wapinzani katika kampeni za uchaguzi mdogo Mbeya Vijijini, akisema, bora vyama hivyo vimeungana kuisaidia CUF kubeba aibu ya kushindwa. [119]
mfumo
Masika alisema kitendo cha kuwateua wabunge kuwa mawaziri, kunaleta muingiliano wa maslahi jambo ambalo ni kiunyume cha mfumo wa utawala bora. [120]
mfupi
Niligundua tatizo lililokuwa linatusumbua ni pumzi na ndiyo maana kama ulikuwa unafuatilia uliweza kugundua wachezaji Tanzania walikuwa wanachoka baada ya muda mfupi lakini wenzetu walikuwa wanamudu kuwa imara wakati woteîanasema Shabani. [121]
miaka
Akihutubia kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 45 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Gombani mjini Chake Chake, Pemba, Rais Karume aliwashutumu wananchi na baadhi ya wasomi kwa kushabikia uhuru huo. [122]
mifuko
Badala ya kukaa na kufurahia kutoboka kwa mifuko na kupasuka kwa suruali yenye mifuko, kila mara wanatafuta kazi zingine za kufanya. [123]
mimi
Kwa hiyo mimi ninashauri nafasi za uwaziri ziwe zinatangazwa kwenye magazeti na watume maombi na kufanyiwa usaili au wateuliwe kwa utaratibu mwingine nje ya bunge," alisisitiza Masika. [124]
mipango
Alisema Uunguja na Upemba utaondoka endapo Wanzanzibari watakubali kuondoa tofauti zao na kukaa pamoja, kujadili mipango ya maendeleo ya nchi yao. [125]
mno
Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha na nawashukuru mno mnao zidi kuniandikia kupitia asmahmakau@mwananchi. [126]
moyo
Wazazi uniunga mkono kwa kila hali kama sio wao nisingeweza kuwa hapa kila wakati unipa moyo kitu ambacho kinanifanya niongeze juhudi ili niweze kuwa bora zaidi na kuiletea nchi yangu sifa na heshimaîanaongeza. [127]
muda
Pikipiki hizo, ambazo zilikuwa ni utekelezaji wa ahadi ya Kileo aliyotoa mara baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM mwaka 2007 na mbunge, zimekaa muda mrefu bila ya kukabidhiwa kutokana na walengwa waliokusudiwa kuzikabidhi kutopatikana. [128]
mumewe
Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [129]
mwa
Alisema kushamiri kwa demokrasia miongoni mwa wananchi ni dalili tosha ya kuwepo kwa utawala bora na kuwa, serikali itaendelea na mikakati yake kuhakikisha inaendelea kuheshimu misingi ya demokrasia na utawala bora. [130]
mwaka
Alisema pia malengo ya mapinduzi hayo ya Januari 12 mwaka 1964 yametimizwa kutokana na nchi kuondokana na ubaguzi, chuki na uhasama na kuendelea kuishi kwa umoja na mshikamano. [131]
mwishiwa
Si kila mtu anaweza kuchekesha? Kwa nini tusifanye na sisi?’ ‘Kweli kabisa mwishiwa Supu. [132]
na
HALI ya upatikanaji wa mafuta jijini, hasa petroli, inazidi kuwa mbaya kutokana na vituo vingi kutouza bidhaa hiyo kwa kile kinachoonekana kuwa, ni njama za waziwazi za wafanyabiashara ya mafuta kuikwamisha serikali kudhibiti upandaji holela wa bei ya nishati hiyo. [133]
nami
Ndugu yangu nakupa pole sana, yaani ni bora ungewasiliana nami kabla ya kwenda huko, kwani ukweli ni kwamba dawa imegunduliwa nchini na jamaa mmoja tena ni albino, rudi wahi mapema usipoteze muda wako huko,” alimsisitizia. [134]
nao
Kila mtu anayeingia uwanjani na sisi anajua Tanzania ni timu ngumu ndio maana wanakamia na kutumia hata nguvu za ziada lakini wachezaji wangu wanahitaji uzoefu kukabiliana nao. [135]
nchi
Lakini umoja wa waagizaji wa mafuta, ulipingana na maelezo hayo ukidai kuwa mafuta yaliyo kwenye akiba yangeweza kutosheleza nchi kwa kipindi cha mwezi mmoja kabla ya shehena nyingine kuingia. [136]
ndio
Kinachotokea ni kwamba presha ya mchezo inavyozidi kibinadamu wanapoteza uvumilivu, mchezaji anajikuta ameshafanya kitu ambacho hakistahili ndio maana unaona kila wakati najaribu kuwatuliza ninapoona mtu anajisahau. [137]
ndiye
Baada ya kumaliza kozi niliazisha timu yangu ambayo mimi mwenyewe ndiye kocha wa timu hiyo, pia nianza kufanya biashara ndogo ndogo kwa ajili ya kujikimu kimaisha. [138]
ndugu
Hata hivyo, baadhi ya watu, wakiwemo wanasiasa na wasomi, wamekuwa wakipinga mapinduzi hayo wakidai kuwa, yaliua baadhi ya ndugu zao na wamediriki hata kuadhimisha sherehe zao za uhuru, badala ya Mapinduzi. [139]
ngumi
SHIRIKISHO la ngumi za kulipwa hapa nchini (TPBO)limesajiliwa rasmi kwa mujibu wa sheria za maendeleo ya mchezo huo ili kusimamia na kuendeleza mchezo huo hapa nchini. [140]
nini
Sijui tatizo ni nini, lakini wengi wanajisahau kwa kujiona nyota katika redio za mkoani hapa, ndiyo maana wanabweteka na kujiona wamemaliza na baada ya muda majina yanashuka na kushindwa kujitofautisha na wasanii wanaochipukia," alisema. [141]
nyuma
Kama hakuna umoja yanaweza kutokea matatizo ambayo yatarudisha nyuma maendeleo na kuvuruga amani iliyopo. [142]
pale
Nafikiri utaona mabadiliko makubwa kwenye huu mzunguko wa pili kwani kuongezeka pale mbele kwa Sammy Kessy kumeimarisha safu yangu ya ushambuliaji na hivyo kunipa matumaini ya kufanya vizuri,"alisema kocha huyo mpole. [143]
pia
Ewura pia imetaka dizeli iuzwe kwa Sh1,271 kwa lita na karibu vituo vyote vilikuwa vinauzwa nishati hiyo kwa bei inayolingana na ya mamlaka hiyo, yaani kati ya Sh1,280 na Sh1,300 kwa lita huku vingine vikidiriki kuuza hata kwa Sh1,180 kwa lita. [144]
picha
Ikabidi kwa kumtia moyo, ikabidi aende kwenye ofisi ambayo alikuwa akifanyia utafiti huo na kufanikiwa kupata picha yake. [145]
raia
Mara kadhaa, Kondic raia wa Serbia amekuwa akilalamika kwamba kuna haja ya kufuata sheria za Shirikisho la soka la Kimataifa (Fifa) katika kanuni za kuwachukua kwenye klabu zao badala ya kuwachukua kwa muda mrefu. [146]
redio
MSANII aliyejiengua kutoka kundi la La Familia, Philip Nyandindi (0-Ten) amesema kiwango cha wasanii wa mkoa wa Morogoro kinashuka kutokana na ukweli kwamba hawaamini kama wanaweza kusimama wenyewe huku wakitegemea zaidi redio zilizopo ndani ya mkoa. [147]
ruhusa
Waziri Khatib alisema pamoja na kushangazwa na kitendo hicho, hakuona haja ya kuleta ugomvi kwa viongozi na atasubiri ruhusa kwa gazeti hilo kufunguliwa na kusambazwa. [148]
rushwa
Watawala wengi hasa wa nchi za kifarika wamekuwa wakiingia madarakani kwa njia ya rushwa hivyo inawawia vigumu kuanzisha mapambano dhidi ya rushwa. [149]
safi
Bao la kwanza la Azam FC lilifungwa na Jamal Mnyate dakika ya 36 kwa kuunganisha krosi safi iliyopigwa na Yahya Tumbo iliyowachanganya mabeki wa Moro United. [150]
sawa
Stephano alisema jumla ya watahiniwa 3,350 walifanya mtihani huo ambao ni sawa na asilimi 90.06 ya wanafunzi wote waliotarajiwa. [151]
si
Jambo hili si kweli," alisema Karume, ambaye baba yake, Abeid Karume aliongoza mapinduzi hayo yaliyouondoa utawala wa Kisultani. [152]
sio
Alisema anaamini CUF haitashinda kwenye uchaguzi huo kwani CCM imeshajipanga vya kutosha kumpata mbunge hivyo sio vibaya aibu hiyo ya kushindwa ikibebwa na wapinzani wote. [153]
soka
Alisema kuwa kuongezeka kwa mshambuliaji Sammy Kessy aliyekuwa akicheza soka uarabuni kumeimarisha safu yake ya ushambuliaji na kumpa matumaini ya kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi. [154]
suala
Lakini hakufafanua suala hilo. [155]
sugu
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na SMZ, chanjo hiyo ni ya kwanza kutolewa nchini Tanzania na kwamba, wameshaandaa maeneo maalumu ya kufanyia majaribio hayo, ambayo ni yale yenye matatizo sugu ya ugonjwa huo visiwani humo na watu 5,000 wakiwemo watu wazima na watoto wanaotarajiwa kuchanjwa. [156]
suluhu
Timu hiyo ambayo ilikuwa kundi B lililokuwa mjini Jinja kwenye uwanja wa mbovu wa Bugembe, ilitoka suluhu mechi mbili na kupoteza moja na kushinda vile vile moja ya mwisho dhidi ya Zambia. [157]
tabia
Alisema kwa kipindi kirefu kumeibuka tabia ya Wazanzibari kubaguana kwa misingi ya siasa na ukazi, hali ambayo ilisababisha mgongano na mjadala mkubwa visiwani humo. [158]
tajiri
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [159]
tatu
WIKI kadhaa baada ya askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana jimbo la Zanzibar, John Ramadhan kumpongeza rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kuwa ni mtu wa kuheshimiwa, kauli yake imeungwa mkono na kiongozi mwingine wa Kanisa Katoliki. [160]
tena
Ligi hiyo itaendelea tena Januri 16 kwa kuzikutanisha Villa Squad na Prisons ya Mbeya Wajelajelai huku Januari 17 ni kati ya Maafande wa JKT Ruvu na Yanga mechi zote zikichezwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. [161]
tenisi
Ninaamini ikiwa tutapata wadhamini watakaokuwa wanatupeleka kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa Tanzania itakuwa ni moja kati ya nchi zilizopiga hatua kupitia mchezo huu wa tenisi. [162]
tu
Ewura pia ilisema bei mpya ilitakiwa kuanza Jumatatu iliyopita na kwamba, wale ambao wamekiuka tangu kipindi hicho, sheria itawakumba mara tu Mwanasheria Mkuu atakapotangaza bei hizo kwenye Gazeti la Serikali. [163]
tuhuma
Mmoja wa wafanyabiashara hao ni mtu aliyefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuchota fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Malimbikizo ya Madeni ya Nje (EPA). [164]
tuna
Mungu na wote tuna mapungufu yetu. [165]
ujasiri
Kikwazo kikubwa kinachowasumbua ni ujasiri wa kuthubutu kuwatupa jela maswahiba wao hao, walioshiriki katika kuwaingiza madarakani kwa njia ya wizi wa kura ama kutoa rushwa. [166]
ujenzi
Alisema ujenzi wa barabara hizo umesaidia kuboresha hali za maisha ya wananchi kuwa bora na kupunguza umasikini uliokuwa unawakabili. [167]
ukanda
Wakati Uingereza ikiondoka mwaka 1963 utawala wa Zanzibar kwa Sultani wa Oman, ambaye kabla ya uhuru alitawala hadi ukanda wa pwani ya Bara. [168]
ukawa
Katiaka mashindano hayo nilionesha kiwango kikubwa sana huo ndio ukawa mwanzo wangu wa kuchaguliwa katika timu ya mukowa wa Dar es Salaam na katika timu ya Taifa. [169]
ukiwa
Maadhimisho hayo yamefanyika kisiwani Pemba wakati Uwanja wa Amaan ulio Unguja ukiwa katika matengenezo makubwa. [170]
ukocha
Anesma baada ya kustaafu kufanya kazi katika benki hiyo alijiendeleza kwa kusoma kozi mbalimbali za ukocha pamoja na kozi uwamzi wa mchezo huo ambapo alifanikiwa kufikia ngazi ya juu katika kozi ya ukocha na uwamuzi. [171]
ulio
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Karume ulio Chake Chake, zilionekakana ndege ndogo za kukodi zikitua na kuruka mithili ya daladala, wakati meli zote zilikuwa zimejaa wananchi kutoka Unguja na Tanzania Bara. [172]
upya
Msanii huyo aliongeza kuwa hajaonekana kwa muda mrefu katika muziki kwa kuwa alikuwa akijipanga upya. [173]
utundu
Lakini bado nafikiri huu unaweza kuwa utundu unaoweza kukutumia ukakusaidia. [174]
uwe
Chai hii shosti haihitaji digrii, au lazima uwe umezaliwa na hotelia, laahasha na wala si ngumu kutengeneza almuhimu hapa ni makusudio yaliyolengwa. [175]
vifaa
Alisema upungufu mkubwa wa vifaa vya kujifunzia na vya kufundishia katika shule za sekondari za wananchi, pia umechangia katika matokeo mabaya ya mtihani huo. [176]
vile
Mchezo utakuwa mgumu sana matokeo yake ni ufanisi wa mtu ndani ya dakika 90 kwa vile Kenya kama unavyoiona ni timu ambayo inazidi kupanda kiwango cha ubora kila siku,"alisema Bobby Williamson ambae ni kocha wa Uganda. [177]
vipi
Katika ibada hiyo Kambili alisema kuwa maisha ya binadamu yana mwisho wake, na kabla mwisho wa kila mwanadamu hauijafika ni vema akajiuliza anajiandaa vipi wakati atakapokufa. [178]
vya
Kuna vituo vingi sana vya kuuza mafuta katika maeneo haya, lakini mpaka sasa vinavyotoa huduma ni vichache ambavyo viko Tangi Bovu na Africana. [179]
wadau
Rais Karume alisema kitu cha msingi kwa Wazanzibari ni kuendelea kujisifia utaifa mkubwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wenye wadau wawili ambao aliwataja kuwa ni Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. [180]
waishiwa
Lo! Mimi nilidhani waishiwa watacheka na kuendelea na kujiliwaza kwao. [181]
wake
Alieleza mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na serikali yake, akitaja sekta ya maji, elimu, afya, miundombinu ya mawasiliano na barabara pamoja na utawala bora unaotekelezwa kwa vitendo chini ya utawala wake. [182]
walimu
Alisema tatizo la watoto kufanya vibaya katika mitihani, limechangiwa na upungufu mkubwa wa walimu unaoikabili mikoa ya kanda ya kati inayojumuisha Dodoma na Singida. [183]
wanachuma
Lakini wakati huu wengine wanachuma hivi hivi. [184]
wao
Ujue tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo mwakani, hivyo wako baadhi ya wanasiasa wanatumia mwanya wa majukwaa ya dini kupeleka ujumbe wao," alisema. [185]
wapate
Huwezi kusema ufungue muda wote na kushambulia ukicheza na timu kama Uganda kwa aina ya wachezaji nilionao ambao ni vijana, nilichotaka tusifungwe mabao mengi lakini vijana wapate uzoefu na kuimarika zaidi kimashindano. [186]
wapi
Utadhani bingo! Lakini wapi! Maisha yamekuwa lotto na Mungu mkubwa siku yangu itakuwapo. [187]
wapo
Kwa bahati mbaya mpaka sasa wapo baadhi ya watu wanaoamini kuwa uhuru uliotolewa na Uingereza ulikuwa kwa wananchi wa Zanzibar. [188]
watoto
Hayo yalisemwa jana na Kaimu Mkaguzi wa Elimu wa Kanda ya Kati, Festus Stephano, ambaye alisema kiwango cha watoto, kufaulu katika mwaka huu pia kimeporomoka, ikilinganishwa na mwaka jana. [189]
wavulana
Kwa mujibu wa Mkaguzi huyo wanafunzi 15,224 miongoni mwa hao ni wavulana na wengine 15,126 ni wasichana. [190]
wenzao
Anaongeza kuwa ikiwa watajitokeza wafadhili ambao watakuwa wakiwagharimia gharama mbalimbali pale wanapopata mialiko ya kwenda kushiriki michuano mbalimbali basi Tanzania itaweza kupata mafanikio makubwa kupitia mchezo kwani tatizo lililoko hivi sasa ni kukosa uzoefu wa kutosha tofauti wenzao wa mataifa mengine. [191]
wetu
Wajibu wetu ni kukaa pamoja na kujadiliana mambo ya maendeleo kwa kila nyanja bila ya kuingiza tofauti zetu za kisiasa na makazi," alisema. [192]
yako
Andaa chai yako kwa umakini, chai shurti iandaliwe ikiwa na kila kikorombwezo kumpumbaza. [193]
yao
Kama serikali ina uwezo wa kuwabana kweli na tuone makali yao. [194]
yote
Walisisitiza kwamba, uwepo mgawanyo wa madaraka baina ya mihimili ya utawala ili kuifanya mihimili yote iweze kujitegemea katika utendaji wake. [195]
yuko
Huyu yuko kwenye upande wa madini. [196]
yule
Halafu nikuchekeshe zaidi ni kwamba hata yule kocha aliporudi kwenye klabu yake Merreikh. [197]
zaidi
Jambo la msingi na muhimu zaidi katika mazingira tunayoishi. [198]
zako
Kwa kumtengea chai mumeo kama ni wadizaini hii utaonyesha mapenzi makubwa na wewe pia kupata nafasi ya kuzungumza naye mipango yenu ya baadaye kama si kupenyeza zako hoja. [199]
zangu
Siwezi kufanya programu zangu vizuri na mara nyingi nimelazimika kuahirisha hata mazoezi. [200]