Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-12

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
acha
We mwishiwa supu acha roho mbaya. [2]
aende
Kila mwishiwa aende kujiandaa kuonyesha kipaji chake siku ile na mshindi atapewa nafasi ya kujaribu kipaji chake kwenye kituo cha runinga. [3]
aina
Michungwani aligongwa na gari aina ya lori lisilofahamika kutokana na kukimbia mara tu baada ya tukio majira ya saa 5:30 asubuhi. [4]
ajabu
Ukipita kwenye vituo utaona bei ya mafuta zilizobandikwa kwenye mbao za matangazo zikionyesha kuwa zimepungua, lakini ukweli ni kwamba ukijaza mafuta, cha ajabu utaambiwa ulipe bei ya juu," alisema mmoja wa madereva ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini. [5]
akaanza
Wakati bado tunacheka akaanza. [6]
akina
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Afya na Ustawi wa Jamii wa SMZ, Juma Rajab amesema kutokana na tahadhari ya kiafya, wanawake wajawazito hawatapewa dawa hiyo kwa kuwa, bado hakuna taarifa za utafiti wa madhara yake kwa akina mama wajawazito. [7]
aliacha
Mmoja aliacha kuangalia simu yake. [8]
alisoma
Siku moja baada ya kukutana na jamaa huyo alisoma taarifa kwenye gazeti moja kwamba kuna biashara kubwa ya kununua viungo vya albino kwa ajili ya machimbo ya madini na biashara ya uvuvi. [9]
ama
Mimi niko tayari kusuluhishwa na mtu yeyote awe wa kidini ama kiongozi wa chama, lakini kwanza lazima kijana huyo aelezwe kuwa anachokifanya nakijua na wanaomtumia kwa hilo nawajua kwa undani zaidi," alisema Sendeka. [10]
ambae
Nduga ambae alikuwa machachari miaka ya nyuma ilipokuwa Simba ikinolewa na Phiri amefurahi kupata habari kwamba klabu hiyo imemrejesha kocha huyo. [11]
ambao
Wengine ni Amir Sanyo, Salim Musa, Omar Aljabri, Napendaeli Msangi, Said Abdallah na askari polisi WP Koplo Mariam wa Muheza na askari wawili wa JWTZ, ambao ni Koplo Mbaraka Mafoni na Koplo Deo Zakaria. [12]
ana
Huyu ni Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa wa Arusha alipaswa kufanya maandamano yake mkoani Arusha hata yangekuwa kwa mabasi na malori, lakini jimboni Simanjiro kwa maandamano ni ishara ya kutosha kuwa ana lake jambo na chama Mkoa wa Arusha, kinapaswa kumwonya vinginevyo anaweza kuleta balaa kwa wapiga kura," alisema. [13]
anatoa
Mbali na wazazi wake Shabani anatoa sifa kwa makocha wake ambao umfundisha mbinu mbalimbali za mchezo huo hao sio wengine ni Martin Dzuwa na Nico Jonas kuwa ndio siri ya mafanikio yake kutokana na maelekezo yao. [14]
au
Mdoe au kwa kwa jina la utani la Osama. [15]
bado
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi ,James Mbatia alisema pamoja na juhudi zinazofanywa na serikali kupambana na ufisadi, bado chama chake hakioni kama hakuna dhamira ya kweli katika jambo hilo. [16]
baina
Mchezo mwingine baina ya Uganda na Burundi unatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa vile Burundi haichoki na hushambulia dakika zote za mchezo tofauti na Uganda ambayo kipindi cha pili huchoka haswa ikiwa na bao. [17]
bali
Si kocha huyo tu bali hata mashabiki wa soka wa nchi hiyo ambayo klabu zake kubwa ni mbili za El-Merreikh na El-Hilal ambazo zina rekodi nzuri kwenye michuano ya bara la Afrika. [18]
bashasha
Unafikiri hiki ni chama cha siasa? Tunagombea uenyekiti au kiti kizuri cha kulala huko Dodoma? Hapa wategemea bashasha si bahasha. [19]
bila
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye kongamano la kiisilamu, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam, walisema oparasheni Sangara imekuwa ikimchafua rais Jakaya Kikwete bila sababu licha ya mambo mengi mazuri, aliyoyafanya kwa taifa. [20]
binafsi
Pemba, baada ya nyumba za kulala wageni kufurika na hivyo wageni wengine kukodi nyumba za watu binafsi kwa gharama tofauti. [21]
cha
Kwa mujibu wa maelezo ya watu walioshuhudia, magogo hayo yaliwakumba abiria waliokuwa wameketi kuanzia kiti cha kwanza hadi cha mwisho katika basi la Tashriff na baadhi ya abiria waliokuwa wamesimama tayari kwa kushuka katika kituo cha Hale. [22]
chanjo
Chanjo ya kipindupindu isiwalemaze wananchi JUZI Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ilitangaza kuwa Januari17, mwaka huu itaanza kuifanyia majaribio chanjo mpya ya ugonjwa wa kipindupindu katika visiwa vya Unguja na Pemba, ikiwa ni juhudi zake za kutokomeza ugonjwa huo visiwani humo. [23]
chupa
Sekeseke hilo lilianza dakika chache kabla ya mchezo dhidi ya Uganda kumalizika ambapo mashabiki wa Uganda walianza kurusha chupa uwanjani kwa madai kuwa mwamuzi Alfred Ndinya wa Kenya anawakandamiza. [24]
dogo
Huku akitambaa kuwa na usajili mzuri katika dirisha dogo aliowasajili, akijivunia wachezaji wake kama Waganda Ben kalama, Dan Lwagaluka wengine Francis Ouma, Osbom Monday na Malegeresi Mangwa na kuhakikisha safu zote zinakamilika. [25]
enzi
Kuhusu tofauti ya mchezo huo hivi sasa na zamani Kibira anasema kuwa enzi zao walikuwa wakijituma sana katika kufanya mazoezi kwa pia wanapokuwa katika mechi kwa sababu waliani kuwa wameajiliwa kwa ajili ya kazi hiyo. [26]
es
Kwa mujibu wa habari hizo, ajali hiyo ilitokea wakati basi hilo likitoka jijini Dar es Salaam kwenda Tanga. [27]
fedheha
Lakini baada ya kutangulia kufungwa na Bara dakika ya 13 kupitia kwa Danny Mrwanda, ili kuepuka fedheha Zanzibar ilisambaratika na kuanza kucheza mpira na iliposawazisha tu dakika ya zisizozidi nne baadaye kupitia kwa Nadir Cannavaro, ikawa inashambulia kwa umakini mkubwa huku timu karibu yote ikiwa nyuma. [28]
gani
Wameingia wote wamejikusanya nyuma ya mpira sasa huwezi kujua nini lengo lao, hawataki kusogea mbele wachezaji nusu uwanja wakipoteza wamejaa kwao huwezi kufanya lolote ndio maana mpira umekosa msisimko, sielewi ni akili gani walikuwa wanatumia au ni mpira wa Bara gani wanacheza hawa jamaa,îaliongeza Bobby. [29]
haina
Lakini timu yangu imeimarika sana, tulikuwa tunacheza na timu ambazo zimejaza wachezaji wa kulipwa tu ndani, wakati Zanzibar haina hata mmoja. [30]
haja
Mara kadhaa, Kondic raia wa Serbia amekuwa akilalamika kwamba kuna haja ya kufuata sheria za Shirikisho la soka la Kimataifa (Fifa) katika kanuni za kuwachukua kwenye klabu zao badala ya kuwachukua kwa muda mrefu. [31]
halikuwa
Kocha wake, alisema tangu mwanzo wa mashindano kwamba lengo lake halikuwa ubingwa wa michuano hiyo bali kutengeneza kikosi cha vijana ambacho kitaingia kwenye mashindano ya mwaka huu na kuchukua ubingwa. [32]
halisi
Waliiomba Ewura kuingilia kati matatizo hayo ili kuwawezesha kufahamu bei halisi za nishati hiyo. [33]
hana
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Mohamed Mbonde, kuhusu madai kwamba Ole Millya ameanda Simanjiro kwa maandamano alisema hana taarifa hizo na kwamba hilo halihusiani na chama. [34]
hao
Juma Hoza mmoja wa waombolezaji hao. [35]
hapa
Akizungumza na Mwananchi jana jijini Arusha, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Basilio Matei, alisema vijana wake wanaendelea na upelelezi kuhusu tuhuma hizo kabla ya kumfikisha mahakamani Ole Sendeka. [36]
hawa
Ndio maana nitabaki na hawa nilionao na nitaongeza wachache kidogo lakini si aina ya Mwalala. [37]
hii
Katika kutekeleza operesheni hii tutakuwa na timu 10 za viongozi watakaoendesha chini ya Mwenyekiti wetu wa taifa, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu," alisema Tumbo. [38]
hiki
Rais Kikwete aliwaomba wafiwa wote wawe na moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na akawaombea waliojeruhiwa kupona haraka ili warejee katika maisha ya kawaida. [39]
hili
Napenda waislamu muelewe kuwa chama cha Chadema hakina msaada wowote juu ya uislamu na kimekumbatia udini, ukabila na ubinafisi kutokana na sababu hiyo, tutatembea nchi nzima kuwaeleza wanachi ukweli wa jambo hili na kuwataka wasikiunge mkono chama hicho,"alisema Mwaipopo. [40]
hivyo
Hata hivyo baadhi ya wafuasi wa Ole Sendeka walisusia ibaada hiyo ya shukrani kwa madai kuwa hizo ni kampeni za ubunge. [41]
hizi
Kufanyika kwa sherehe hizi kisiwani Pemba kumefungua ukurasa mpya wa historia ya serikali ya awamu ya sita, ambayo ilipoingia madarakani haijawahi kufanya sherehe kubwa kama hizo, kisiwani Pemba. [42]
hujui
Utamaduni huu shostito ni wa pwani, kama ulikuwa hujui chukua hiyo, Na ukweli ni kwamba wanawake wengi wa pwani wanajua maana ya chai ya jioni na ndiyo maana wanasifiwa kuwa wanayajua mambo. [43]
huko
Ni ukweli usiopingika kwamba, watoto wengi siku hizi, wasipofuatiliwa hawajali kabisa shule, hivyo wazazi muwe mstari wa mbele kuwahimiza kusoma, si tu kwa kuwapeleka tuisheni, kwani huko pia hufanya mambo yao wasipofuatiliwa maendeleo yao. [44]
humo
Wananchi hao walizuia magari na shughuli mbalimbali zinazofanyika katika eneo hilo la barabara, huku wakiwa wamewasha moto wa matairi njiani humo. [45]
huna
Pumbavu kabisa, huna maana wewe, sasa ni lazima ufe, mwenye siri za dawa ni huyo albino uliyemuua, mbwa kabisa wewe,” alifoka waziri kwa hasira kisha kupiga simu kwa mkuu wa jeshi la polisi ili kumkata Kazim kwa kitendo chake. [46]
huo
Wakati huo huo, Ole Millya alipokelewa kwa shangwe katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, wakati wa ibaada ya shukrani ya kuombewa baada ya kushinda nafasi hiyo. [47]
huu
Pia amewapa pole familia za wafiwa na kuwaomba wawe wastahimilivu katika wakati huu mgumu wa majonzi. [48]
huyu
Mimi siyo kocha wa visingizio, lakini huyu mwamuzi alifanya maamuzi ambayo yalikuwa yakiwaondoa wachezaji wangu mchezoni, hakuwa makini,”alisema kocha huyo kwa hasira. [49]
ijayo
BEKI wa Kilimanjaro Stars ambaye atalazimika kukaa nje wiki moja ijayo, amebainisha kwamba Kenya na Uganda zinawaogopa. [50]
ikawa
Kauli hizo za Bobby zilikuja kujirudia kwa Marcio Maximo wa Bara wakati timu yake ilipoivaa Zanzibar lakini safari hii ikawa kwa staili ya aina yake kidogo. [51]
ila
Tulivamiwa wakati timu inatoka uwanjani, lakini bahati nzuri hakuna mchezaji yoyote aliyeumizwa, kila mtu yupo salama ila kwenye kikao cha maandalizi ya mechi za kesho(leo) walidai kuna shabiki kaumizwa na wachezaji wetu, kitu ambacho si cha kweli," alisema Leopord Mukebezi ambaye ni meneja wa Stars. [52]
ile
Mmoja wa wasimamizi katika kituo cha mafuta cha MT cha mjini hapa alisema kuwa, hawezi kukataa kutokea kwa hali katika vituo vingine, lakini kwa upande wa kituo chake bei ya mafuta ni ile iliyoko katika mbao za matangazo. [53]
imara
Tathmini ya timu hiyo inaonyesha kwamba itawatumia muda mwingi kutulia na kutengeneza timu imara na tishio kama ile walioivunja baada ya kufungwa na Taifa Stars ya Tanzania. [54]
imeanza
Kama klabu imeanza maandalizi ya michuano au ligi, wachezaji wake kuwa nje kwa wiki mbili ni nyingi sana. [55]
ina
Tunajua kwamba, serikali ina majukumu mengi kwa ajili ya maendeleo ya taifa, lakini kuna umuhimu wa kulifufua kikamilifu shirika hilo, ambalo kwa ujumla ni kurunzi ya taifa letu katika medani ya usafirishaji duniani. [56]
inaweza
Hakuna timu ya taifa inaweza kukaa kambini kwa kipindi kirefu hivyo, lakini pia inategemea na makubaliano kati ya timu ya taifa na klabu zenyewe. [57]
itakuwa
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mpambano huo Syori alisema kuwa ushindi hayo ni matokeo ya maandalizi mazuri aliyokuwa nayo na kuongeza kuwa hiyo itakuwa changamoto ya kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya vijana ya Afrika yatakayofanyika nchini Morocco hapo baadaye. [58]
jua
Hali ya hewa ya hapa ni ya joto kali na jua mchana ambalo halitofautiani na lile la Dar es Salaam wanapoishi wachezaji wengi wa Stars. [59]
juu
Akizungumzia ogomvi wao na Ole Millya uliofikia hatua ya kutwangana makonde, Mbunge huyo wa Simanjiro alidai kuwa aliuanza Millya kwa maneno na vitendo na kwamba yeye alichokifanya ni kujibu mashambulizi ya hali ya juu ikiwa ni njia pekee ya kujitetea. [60]
kadi
Kukosekana kwa Nsajigwa jana mwenye kadi mbili za njano kulidhihirisha ubora wake na hamasa yake kwani safu ya ulinzi ilionekana kutojiamini huku mawasiliano yakiwa hamna kati yao. [61]
kama
Wafuasi wa Ole Millya waliimba nyimbo mbalimbali za kumpongeza na kumtaja kama Mbunge Mtarajiwa. [62]
kanda
Kwa upande wake kocha wa Tanzania, Salum Mvita alisema kushindwa kwa wachezaji wao ni kutokana na kutofuata maelekezo ya walimu wao alaongeza kuwa hata hivyo mpaka wakati huo wachezaji wake wanne walifuzu kuingia katika timu ya kanda ya Afrika Mashariki na Kati. [63]
kansa
Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [64]
kata
Mwenyekiti wetu atazindua rasmi operesheni hiyo katika Jiji kwa kuwahutubia wananchi wa kata tatu za Jimbo la Kigamboni za Mbagala Kuu, Charambe na Zakheim katika mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya Zakheim Mbagala," alisema Tumbo. [65]
kati
Walisema dizeli imekuwa ikiuzwa kwa bei ya kati ya Sh 1,274 na Sh 1,600 kwa lita moja na mafuta ya taa, yanauzwa kwa bei ya Sh 770 na Sh 800 kwa lita. [66]
kauli
Akisoma tamko la waislamu hao, kuhusu OIC na Mahakama ya Kadhi katibu wa Baraza la habari la Kiislamu Tanzania (Bahakita) Shekhe, Sadick Godigodi alisema wamekubaliana kwa kauli moja kusubiri kauli itakayopotolewa na serikali. [67]
kiasi
Hata hivyo, taarifa hiyo hakutoa sababu za wananfunzi hao kufeli kiasi hicho mwaka huo. [68]
kibao
Nakufa, mkuu wa polisi unaniua, sawa mimi nimemuua albino, lakini wewe unaniua mimi kwa kunipiga kibao, imeandika wapi kwamba muharifu apigwe, kabla ya kufikishwa mahakamani,” alisema Kazim huku akikata roho. [69]
kichwa
Baada ya kosakosa hizo Polisi Moro walijiuliza na kurekebisha makosa yao ambapo katika dakika ya 42 Fred Agai aliiwapatia maafande hao bao kwa kichwa akimalizia krosi ya beki wa kushoto Masumbuko Hassan. [70]
kikao
Alisema semina ilikuwa ikizungumzia uporwaji wa ardhi na kumwendeleza kielimu mtoto wa kike wa kimasai, lakini yeye alifika hatua ya kumshambulia na kumkashifu wazi wazi hatua iliyomfanya hata mwenyekiti wa kikao hicho Vicenti Parseko Ole Kone Mkuu wa Mkoa wa Singida, kumkatiza kwa kumweleza juu ya kutoka nje ya mada zilizopo, lakini akikaidi hilo. [71]
kila
Kwa upande wa nishati ya mafuta bei ya petroli imeteremka kutoka Sh 1,560 hadi Sh 1,435 wakati bei ya dizeli imeteremka kutoka Sh 1,680 hadi Sh 1,410 huku mafuta ya taa yakiuzwa kwa Sh 1,050 kwa kila lita moja. [72]
kimoja
Alisema operesheni hiyo katika Jiji la Dar es Salaam imesukumwa na mabadiliko ya kisiasa duniani yanayohusisha pia majiji makubwa kama Dar es Salaam, ambalo alisema linatia aibu kwa kukosa hata kiti kimoja cha udiwani wa upinzani. [73]
kina
Kwa ujumla, matokeo hayo ni changamoto kwa serikali kufanya utafiti wa kina wa jinsi ya kuboresha elimu ya sekondari ili iende sambamba na juhudi za kuongeza idadi ya shule ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa nafasi za kidato cha kwanza ikilinganishwa na miaka ya nyumba. [74]
kirefu
SUALA la malalamiko ya Kocha Mkuu wa Yanga, Dusan Kondic pamoja na uongozi wa juu wa klabu hiyo kuhusu wachezaji wake kukaa kipindi kirefu kambini wakiwa na kikosi cha timu ya taifa (Taifa Stars) limekuwa likiwagawanya mara kadhaa wadau wa soka nchini. [75]
kote
Pia amweataka makocha pamoja na waamuzi wa Netiboli kote nchini kuwa na jitihada za kuendeleza mchezo huo kwa kuanzia ngazi ya vijiji ,kata, tarafa, wilaya na mikoa. [76]
kuamua
Siku ya vipaja? Mwishiwa Supu unawaita waamuzi kwa ajili ya siku ya vipaja? Hata sisi tunaweza kuamua. [77]
kubwa
Ibada hiyo ilifanyika katika Kanisa la Usharika wa Olkesment na iliongozwa na Mchungaji Emanuel Kweka na kufuatiwa na sherehe kubwa ambayo watu wengi waliihusisha na uzinduzi wa kampeni ya Ubunge wa Simanjiro. [78]
kucheza
Kipindi cha kwanza Stars ilishangaza kutokana na morali yake kuwa chini na kucheza kwa taratibu tofauti na mechi dhidi ya Zanzibar, Rwanda na Uganda. [79]
kufanikiwa
Ibrahim Shaban Mtanzania pekee aliyeipeperusha vema bendera ya Tanzania na kufanikiwa kufika hatua ya fainali ya Michuano ya Tenisi kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa Vijana wenye Umri chini ya Miaka 14 hadi 16 na 14 kushuka chini yaliyomalizika Jumamosi kwenye Viwanja vya Gymkahan jijini Dar es Salaam. [80]
kufikishwa
Watu wengine watatu wamefariki baada ya kufikishwa hospitalini ya Magunga wilayani Korogwe. [81]
kuimba
Kweli wanaweza kuingia hivihivi? Kweli wataingia kama milolongo ya vijana wanaotafuta nafasi moja ya Ustaa wakati ambapo hata wenzao wa mitaani wanawacheka wakijaribu kuimba. [82]
kuingia
Katika hatua nyingine, Mwaipopo aliwataka viongozi wa dini za kiislamu Mashekhe na Maimamu kuingia kwenye siasa kuanzia nafasi za serikali za mitaa hadi ubunge ili kwenda kuwatetea wananchi. [83]
kuishi
Siku moja usiku akiwa nyumbani alitafakari sana hali ngumu ya maisha ambayo angeanza kuishi. [84]
kuja
Wakati sherehe hizo, zikifanyika kisiwani hapa maeneo mbali mbali kwa nyakati tofauti yamepambwa kwa bendera za kijani na njano, huku shughuli nyingi za kiuchumi zikiwa zimepata uhai mkubwa baada ya wageni kutoka Unguja na Tanzania Bara kuja kwa wingi na kusababisha mitaa mbali mbali kuwa na watu wengi. [85]
kukutana
Hivyo walipanga muda wa kukutana. [86]
kule
Mchezo wa mwisho Tanzania imetufunga kule Dar es Salaam mabao 2-0, lakini tunaingia uwanjani na mawazo mapya. [87]
kumbe
Zaidi ya yote kumbe alikuwa amechukua mkopo benki baada ya biashara zake kumchanganyia, ili kuboresha zaidi, akiamini kuwa kwa namna alivyokuwa akipata fedha angeweza kulipa deni ndani ya muda mfupi. [88]
kumi
Baadhi ya wachezaji wanaopungua kumi walipunguzwa kwenye kikosi hicho kilichokuwa tishio kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, lakini baadae likapita tena panga jingine ambalo pengine halijawahi kutokea Afrika. [89]
kumuua
Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [90]
kuna
Pia kuna watoto wawili wa kiume na watatu wa kike. [91]
kunywa
Farasi unampeleka kunywa maji lakini anashindwa kuyanywa basi hivyo ndivyo mchezo ulivyo watoto tumewafundisha lakini wameshindwa kufanya vizuri lakini tunashukuru angalau tumepata nafasi nne mpaka sasaalisema Mvita. [92]
kupitia
Operesheni hiyo ilibuniwa ghafla baada ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Tarime uliomweka madarakani mgombea wa kiti cha ubunge kupitia tiketi ya Chadema, Charles Mwera. [93]
kutinga
Stars ambayo mashabiki wa hapa walikuwa wakiipa nafasi kubwa ya kutinga fainali ilifanya vinginevyo uwanjani na sasa itacheza na Burundi kuwania nafasi ya tatu kesho. [94]
kutumia
Wapo walioshindwa kutumia nafasi pia muda wao umekwisha, hawakuweza kufanya kitu cha ajabu. [95]
kuua
Ajali hiyo imewarejesha wakazi wa Tanga katika majonzi yaliyowatokea mwaka 1998 wakati basi la iliyokuwa Kampuni ya No Challenge kupata ajali na kuua abiria zaidi ya 70.Baadaye kampuni hiyo ilibadilishwa na kuitwa Tashriff. [96]
kuwa
Waombolezaji waliojitokeza katika Hospitali ya Bombo kuangalia waliokufa katika ajali hiyo walikuwa wameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mohamed Abdulaziz ambaye alitoa salamu za rambirambi kwa waliofiwa na kuwataka kuwa na moyo wa subira. [97]
kwake
Katika salamu hizo, Waziri Mkuu ameeleza kusikitishwa kwake na ajali za kila mara na kuwatakia uponyaji wa haraka majeruhi wa ajali hiyo, iliyotokea jana usiku katika eneo la Hale mkoani humo. [98]
la
MJI wa Tanga na maeneo mengine ya jirani, jana yalizizima kwa majonzi yaliyotokana na ajali ya basi la Kampuni ya Tashriff, lililosababisha watu 27 kufa papo hapo na wengine 23 kujeruhiwa. [99]
labda
Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [100]
lao
Hali hiyo ilimfanya Naibu Waziri Mahiza aliyekuwa akisafiri na gari lake kutokea Dar es Salaam kwenda Tanga mjini kulazimika kuitisha mkutano wa ghafla wa hadhara katika eneo hilo ili kupunguza jazba zao, ambapo alifanikiwa kuwapoza wananchi hao kwa kuwaeleza kuwa suala lao litashughulikiwa na serikali. [101]
leo
RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume leo, anatarajiwa kuongoza maelfu ya wananchi wa Unguja na Pemba katika kuadhimisha miaka 45 ya Mapinduzi yanayofanyika kitaifa kisiwani Pemba huku wageni mbalimbali wakilazimika kukodi nyumba za wananchi wa kawaida baada ya nyumba za kulala wageni kufurika watu kutoka Unguja na Tanzania Bara. [102]
letu
Lengo letu ni kuhakikisha kuwa chadema inakuwa kimbilio la wanyonge katika kila ngazi ya utawala hapa nchini," alisema Tumbo. [103]
litakuwa
Kama inawezekana FA (shirikisho la soka) linawasiliana na klabu na kueleza kwamba litakuwa na wachezaji kwa kipindi kirefu zaidi. [104]
lori
Inasemekana katika ajali hiyo, basi hilo, liliuvaa upande wa kushoto wa lori lililokuwa limebeba magogo na kuegeshwa kando ya barabara. [105]
mada
Sendeka alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mgogoro uliotokea wilayani Monduli muda mfupi baada ya mapumziko ya semina ya wazee wa jadi wa kimasai (Olaigwanani), waliokuwa wakijadili mada za ardhi na nafasi ya mtoto wa kike wa jamii ya wafugaji katika elimu. [106]
madini
Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [107]
maisha
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Rais amesikitishwa na ajali hiyo, iliyogharimu maisha ya Watanzania wasiokuwa na hatia. [108]
makundi
Ule mchezo ulikuwa mgumu sana na muhimu sana kushinda kwa wachezaji wangu walikuwa wamepania sana na tungeshinda ule tungefika mbali sana kuliko hapa kwenye hatua ya makundi tulikoishia. [109]
mapema
Kutokana na hatua hiyo, waislamu hao wamesimamisha maandamano waliyokuwa wamepanga kufanyika mapema mwezi huu kwa lengo la kuishinikiza serikali kutoa tamko lake kuhusiana na Mahakama ya Kadhi na OIC na walisema kuwa watatoa kauli yao baada ya serikali kutoa tamko. [110]
matatu
Stars jana ilifanya mazoezi kwa muda wa saa mbili kwenye uwanja wa Express Fc kuanzia majira ya saa 5 asubuhi huku kocha Marcio Maximo akifanyia kazi mambo matatu. [111]
mbao
Ajali hiyo, iliua watu 27 papo hapo na ilisababishwa na basi hilo, lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Tanga baada ya kugonga lori la mbao lililokuwa limeharibika na kuegeshwa barabarani. [112]
mbovu
Mashabiki wa Tanzania wakiongozwa na Teddy Mapunda, walikuwa wakimrushia maneno Katibu wa Cecafa, Nicholaus Musonye kuhusiana na uchezeshaji mbovu. [113]
michezo
Mchezaji huyo ambae juzi alihudhuria kikao cha maandalizi ya michezo ya nusu fainali za leo, alisema kwamba timu zilikuwa zikihangaika kutafuta makosa ya Stars. [114]
mifuko
Badala ya kukaa na kufurahia kutoboka kwa mifuko na kupasuka kwa suruali yenye mifuko, kila mara wanatafuta kazi zingine za kufanya. [115]
mika
Hayo ni maneno ya Anna Kibira, mwana mama aliye tamba miaka ya 70,80 na mwanzoni mwa mika ya 90 katika mchezo wa Netibaoli akiwa na timu ya JKT Mafinga, NBC United, timu ya mkowa wa Dar es Salaam na timu ya Taifa. [116]
mikoa
Kamanda Sirro alisema hadi kufikia jana mchana miili ya watu 18 waliokufa katika ajali hiyo, ilikuwa imetambuliwa na ndugu zao waliokuwa wakiingia jijini Tanga wakitokea mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuwatambua waliokufa. [117]
mimi
Ni kocha mzuri sana anayeelewa maana ya mchezaji, mimi ananielewa nilivyo na uwezo wangu ngoja nikakutane naye kwanza halafu nitajua. [118]
mkuu
Taarifa zilizothibitishwa na mkuu wa wilaya ya Handeni, Winfrid Ligubi zinaeleza kwamba, lori hilo ambalo namba hazikupatikana mara moja liliwagonga watu hao ambao baadaye walikimbizwa katika hospitali ya Magunga wilayani Korogwe. [119]
muhimu
Kutokana na hali hiyo, aliwataka walimu wawe makini sana katika kuhifadhi mitihani kwa kuwa ni nyaraka muhimu. [120]
mumewe
Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [121]
mwa
Kwa mujibu wa Sirro, watu 14 miongoni mwa waliokufa ni wanaume na watano ni wanawake. [122]
mwezi
Alisema kutokana na ubinafisi wa chama hicho, kimeshindwa kuviunga mkono vyama vya upinzania vya Chama cha Wananchi (CUF) na Sauti ya Umma (SAU) vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya vijijini ambao unaotarajia kufanyika mwezi huu. [123]
mwishiwa
Si kila mtu anaweza kuchekesha? Kwa nini tusifanye na sisi?’ ‘Kweli kabisa mwishiwa Supu. [124]
nao
Wananchi hao walioonekana kuwa na hasira kali waliamua kuufikisha ujumbe wao kwa nguvu, ambapo licha ya kuwasha moto barabarani humo pia walirusha mawe kwa mtu yeyote aliyejitokeza kuzungumza nao ili kuwatuliza kwa kile walichodai kwamba watakubali tu kuzungumza na uongozi wa serikali ya wilaya ya Handeni. [125]
naomba
Watanzania wanapaswa kuelewa kwamba vijana wako tayari kufa kutetea heshima ya Taifa lao naomba sana wawaunge mkono kwa kila hali. [126]
naye
Yule kocha ni rafiki yangu sana alipotua tu Simba nimepata ripoti na nimepanga kwenda Dar es Salaam muda siku yoyote kuanzia sasa kufanya naye mazungumzo. [127]
nchi
Maadhimisho hayo, yatafanyika katika Uwanja wa Gombani Mkoa wa Kaskazini na kuhudhuriwa na viongozi wa kitaifa akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dk Ali Mohammed Shein, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, mawaziri, viongozi wastaafu na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini. [128]
ndio
Mwenyekiti huyo pia alisema kuwa ili kukabiliana na ufisadi wa fikra ambao ndio chanzo kikubwa cha kuwepo kwa mikataba mingi mibovu, ni vema somo la maadili likaingizwa katika mitaala ya elimu na hivyo kufundishwa katika shule zetu. [129]
ndiye
Francis Ouma anayeichezea Azam Fc ya Dar es Salaam ndiye aliyeifungia Kenya bao la kwanza dakika ya 18 kwa shuti baada ya mabeki wa Stars kujichanganya na Henry Joseph kujikuta akiumalizia mpira nyavuni. [130]
ndiyo
Lakini pia tunadhani kwamba, tangazo la serikali kwamba, mtihani huo ni wa kutimiza wajibu tu, kutokana na kusema kuwa hakuna mwanafunzi atakaye rudishwa nyumbani au kurudia mwaka akifeli, limechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza umakini kwa wanafunzi na ndiyo maana wamefeli. [131]
ngumu
Timu hiyo ilikuwa ikicheza mfumo wa kujilinda muda wote kwa kuchezesha wachezaji kumi na moja nyuma ya mpira hasa wanapokutana na timu ngumu na kocha wao alikuwa akikiri wazi kwamba amewaelekeza kufanya hivyo ili wasifungwe. [132]
ni
Habari zilisema hali ya majeruhi wawili wa ajali hiyo ni mbaya mno na wamelazwa katika Hospitali Teule ya Muheza. [133]
nia
Akitangaza rasmi nia ya kuzindua operesheni hiyo, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, Erasto Tumbo, alisema itaanzia katika Wilaya ya Temeke na hasa katika Jimbo la Kigamboni na kwamba itaongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe. [134]
nini
Tatizo langu ni nini? Chezeni mpira uwanjani acheni visingizio,”alisema Musonye mbele ya waandishi wa habari. [135]
niwe
Ni malengo ambayo nilijiwekea mapema kwamba jambo la kwanza ni kufikia hatua ya juu kabisa na pia niwe mmoja wa wachezaji watakaoiwakilisha kanda hii kule Morocco kwani itakuwa ni sehemu nzuri ya kupata uzoefu pamoja na mbinu mpya za kimchezo, kama unavyojua mashindano ya Afrika yatashirikisha mataifa mengi yakiwemo yale ambayo yapo juu kupitia mchezo huuíanasema Shabani. [136]
nusu
MAWASILIANO mabovu kwenye safu ya ulinzi pamoja na morali ya chini ni kati ya sababu zilizopelekea Kilimanjaro Stars kufungwa mabao 2-1 na Kenya jana katika mchezo wa nusu fainali ya Chalenji. [137]
ofisi
Akajenga majumba makubwa na kuyapangisha ofisi, huku mengine yakitumiwa kama nyumba za kulala wageni. [138]
pale
Heshima ya Sudan kwenye soka inapaswa kubaki pale pale na jinsi ya kulinda hicho kitu ni kwa kuwatengeneza vijana wale wengine walioshindwa kufuzu CHAN wanaonekana kama wameshazeeka,"anasema. [139]
pamoja
Wanafunzi hao kwa pamoja wanaisaidia polisi sanjari na mkuu huyo. [140]
pia
Alisema pia inashangaza na kusikitisha kuona mwenyekiti wa UVCCM mkoani Arusha anakwenda Simanjiro kwa 'mbwembwe' kubwa na msafara mzito kwa lengo la kuwashukuru wajumbe na kutoa sadaka kanisani. [141]
picha
Ikabidi kwa kumtia moyo, ikabidi aende kwenye ofisi ambayo alikuwa akifanyia utafiti huo na kufanikiwa kupata picha yake. [142]
pili
MKUU wa shule ya sekondari ya Nyawa, Wilaya ya Bariadi mkoani Shinyanga, anahojiwa na polisi baada ya mitihani ya kidato cha pili kuibwa katika shule yake. [143]
rasmi
Rais Karume atakagua gwaride rasmi lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama na kupigiwa wimbo wa taifa kabla ya kulihutubia taifa. [144]
sana
Nimesikitishwa sana na jinsi maisha ya Watanzania wenzetu yanavyondelea kupotea katika ajali za barabarani. [145]
sasa
CHAMA cha NCCR- Mageuzi, kimependekeza kuundwa kwa Tume ya Taifa ya Maridhiano na Msamaha ambayo itatumiwa na watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi na wananchi, kueleza ukweli halisi wa mambo, hatua ambayo chama hicho kimesema itasaidia kulifanya taifa kushughulikia pia mambo mengine ya maendeleo badala ya ufisadi tu kama ilivyo sasa. [146]
sawa
Kocha huyo anasema kwamba hawakutazamiwa kupoteza kombe hilo lakini wanajipanga kupata mbinu za kuweka mambo sawa. [147]
seti
Fainali ya pili iliyowakutanisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 14, Iradukunda Guyorly wa Burundi alifanikiwa kumshinda Mtanzania pekee aliyefanikiwa kuingia hatua hiyo Ibrahim Shaaban kwa seti 2-0 katika michezo 6-2,6-1katika mpambano mkali uliokuwa na ushindani mkubwa. [148]
shida
Umempata?” alidakia Kazim, aliyekuwa akizungumza kwa shida. [149]
si
Alisema kitendo cha Ole Millya kuandamana kwa magari, pikipiki, baiskeli na miguu kwenda Simanjiro kuwashukuru wajumbe aliomchagua na kutoa shukurani kanisani si cha kuungwa mkono. [150]
sifa
Mwaipopo alisema kama oparesheni Sangara ingekuwa ni ya kweli basi ingekuwa tayari kutaja baadhi ya sifa ambazo Rais Kikwete amekuwa akizifanya badala ya kumchafulia jina lake kila inaopoendesha mikutano yake. [151]
sio
Wazazi uniunga mkono kwa kila hali kama sio wao nisingeweza kuwa hapa kila wakati unipa moyo kitu ambacho kinanifanya niongeze juhudi ili niweze kuwa bora zaidi na kuiletea nchi yangu sifa na heshimaîanaongeza. [152]
sisi
Yaani wanahofia kwamba sisi tukiachiwa tunaweza kuwafanyia kitu cha ajabu,îalisema Meshack. [153]
sugu
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na SMZ, chanjo hiyo ni ya kwanza kutolewa nchini Tanzania na kwamba, wameshaandaa maeneo maalumu ya kufanyia majaribio hayo, ambayo ni yale yenye matatizo sugu ya ugonjwa huo visiwani humo na watu 5,000 wakiwemo watu wazima na watoto wanaotarajiwa kuchanjwa. [154]
suluhu
Timu hiyo ambayo ilikuwa kundi B lililokuwa mjini Jinja kwenye uwanja wa mbovu wa Bugembe, ilitoka suluhu mechi mbili na kupoteza moja na kushinda vile vile moja ya mwisho dhidi ya Zambia. [155]
tajiri
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [156]
tangu
Akizungumzia Oparasheni Sangara, alifafanua imekuwa ikichafua rais Kikwete bila ya sababu za msingi kwa kuwa rais huyo tangu ameingia madarakani amesababisha mafisadi kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya Sheria. [157]
tatizo
Pendekezo hilo linakuja wakati serikali ikiendelea na hatua za kuwafikisha mahakamani, watu mbalimbali wanaotuhumiwa kwa vitendo hivyo, lakini chama hicho cha upinzani, kimesema hakioni kama dhamira hiyo ni ya kweli katika kushughulikia tatizo hilo. [158]
tatu
Pia alisema kipindi hiki cha Rais Kikwete kumekuwa na uhuru mkubwa wa kuabudu kutokana na serikali yake kuruhusu mihadhara ya kidini ambayo, ilikuwa ikizuiliwa na serikali ya awamu ya tatu. [159]
tenisi
Ninaamini ikiwa tutapata wadhamini watakaokuwa wanatupeleka kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa Tanzania itakuwa ni moja kati ya nchi zilizopiga hatua kupitia mchezo huu wa tenisi. [160]
tiketi
MBUNGE wa Simanjiro kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Christopher Ole Sendeka, keshokutwa anatarajiwa kuburuzwa mahakamani. [161]
tu
Tanga, Nyakoro Sirro, alisema dereva wa basi hilo alitoweka mara tu baada ya ajali na kwamba, wafanyakazi wengine watatu wa basi hilo waliokuwamo wakati wa tukio, wamekufa. [162]
tufanye
Sisi ndio wenye wachezaji, tunawahitaji kwa ajili ya kujiandaa, watuache tufanye nao mazoezi na siku chache kabla ya michuano watawachukua. [163]
ujasiri
Kikwazo kikubwa kinachowasumbua ni ujasiri wa kuthubutu kuwatupa jela maswahiba wao hao, walioshiriki katika kuwaingiza madarakani kwa njia ya wizi wa kura ama kutoa rushwa. [164]
ukawa
Katiaka mashindano hayo nilionesha kiwango kikubwa sana huo ndio ukawa mwanzo wangu wa kuchaguliwa katika timu ya mukowa wa Dar es Salaam na katika timu ya Taifa. [165]
uko
Hata hivyo, hakuna shaka kwamba kama Rais Kikwete hata kuwa mwoga, ni wazi ushindi uko kwake kwa sababu yeye ana kila kitu kwanza, anashikilia dola, ana vyombo vya kumsaidia kuwakamata na kuwashtaki, hivyo kundi hilo la mafisadi litakwama. [166]
ukocha
Anesma baada ya kustaafu kufanya kazi katika benki hiyo alijiendeleza kwa kusoma kozi mbalimbali za ukocha pamoja na kozi uwamzi wa mchezo huo ambapo alifanikiwa kufikia ngazi ya juu katika kozi ya ukocha na uwamuzi. [167]
ule
Kesho tunategemea mchezo mgumu, lakini nimewatengeneza vizuri wachezaji wangu tayari kuhakikisha kwamba tunashinda na mkakati wetu ni ule ule kucheza fainali za haya mashindano. [168]
usafiri
Wananchi hao wanadai kuwa wamiliki wa baadhi ya vituo vya mafuta, wamekuwa wakibandika matangazo yanayoonyesha kuwa bei zimeshuka, lakini wanapojaza mafuta kwenye vyombo vya usafiri, wanaelezwa bei za juu. [169]
utundu
Lakini bado nafikiri huu unaweza kuwa utundu unaoweza kukutumia ukakusaidia. [170]
uwe
Chai hii shosti haihitaji digrii, au lazima uwe umezaliwa na hotelia, laahasha na wala si ngumu kutengeneza almuhimu hapa ni makusudio yaliyolengwa. [171]
uzoefu
Huwezi kusema ufungue muda wote na kushambulia ukicheza na timu kama Uganda kwa aina ya wachezaji nilionao ambao ni vijana, nilichotaka tusifungwe mabao mengi lakini vijana wapate uzoefu na kuimarika zaidi kimashindano. [172]
vile
Lakini Danny Mrwanda ambaye amekuwa machachari muda wote na tishio jijini hapa, amesema kwamba mchezo wa leo watatulia na uwezekano wa kushinda ni mkubwa kwa vile Kenya haiwapi presha. [173]
vipi
Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni,” alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [174]
vituo
BAADHI ya watu wanaomiliki vyombo ambavyo uendeshaji wake unatumia mafuta katika mji wa Morogoro, wamelalamikia baadhi ya vituo vinavyouza nishati hiyo kwa kuwarubuni. [175]
vya
Habari za uhakika toka kwa viongozi wa CCM, zimeeleza kuwa vurugu hizo huenda zikajadiliwa katika vikao vya maadili vya chama hicho hivi karibuni. [176]
vyao
Mzee tumekuja, hali ya biashara ni mbaya sana, yaani kila kukicha ni mikosi tupu hata hatujui tufanye nini, ila tunasikia kuna mtindo umezuka siku hizi watu wanaua albino, viungo vyao vinaweza kutusaidia kupata fedha tutakapokwenda kwa mganga wa jadi” alisema na kupingwa vikali na Kazim. [177]
vyenu
Hapa nawalinda kabisa na vijisenti vyenu. [178]
vyoo
Alisema wanafunzi hao, wamefutiwa matokeo baada ya kubainika kukutwa na majibu katika makaratasi, kujiandika katika nguo, mwilini na hata baadhi yao kuandika katika vyoo na kutoka katika chumba cha mtihani kwa ajili ya kuibia. [179]
waishiwa
Lo! Mimi nilidhani waishiwa watacheka na kuendelea na kujiliwaza kwao. [180]
wako
Alisema wachezaji wake wote wako katika hali nzuri na hana mchezaji yoyote aliye majeruhi kwa sasa na kuahidi washabiki wake wakae waone timu itakavyofanya vizuri msimu huu. [181]
wakuu
Kwa mujibu wa Mbatia kwa miaka mingi serikali imekuwa ikipigiwa kelele za kuwepo kwa ufisadi unaofanywa na watendaji wake wakuu serikalini, lakini imekuwa kiziwi na hata baada ya kuamka na kuanza kulishughulikia suala hilo bado kumekuwepo na usanii. [182]
wale
Katika suala hili la kupambana na ufisadi tunashauri iundwe Tume ya Maridhiano na Msahama ili watu wote walioshiriki katika ufisadi wakiwa viongozi na wale wahanga, waweze kufika mbele ya tume na kuelezea ukweli halisi” alisema Mbatia. [183]
walitoka
Wanafunzi 10 bora kitaaluma katika mtihani huo, walitoka katika shule ya sekondari ya Tabora Boys ya mjini Tabora, wanafunzi 10 bora wa kike walitoka shule mchanganyiko. [184]
wanachuma
Lakini wakati huu wengine wanachuma hivi hivi. [185]
wapo
Kimanzi alisema leo atatumia wachezaji wote wanaocheza Yanga na Azam za Dar es Salaam, Mike Baraza akiwa ni mmoja wapo kwani alimpumzisha makusudi awali. [186]
wazazi
Pamoja na kuomba mazingira ya kufundishia yaboreshwa tunawasihi walimu na wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto na kuwajengea maandalizi mazuri ya kufanya vizuri katika mitihani yao. [187]
wenyeji
Katika nusu fainali ya pili wenyeji Uganda ambao tangu juzi walikuwa wakijitamba walisambaratisha Burundi kwa kuichapa kwa mabao 5-0 katika mchezo huo uliokuwa wa upande moja zaidi. [188]
wenzao
Anaongeza kuwa ikiwa watajitokeza wafadhili ambao watakuwa wakiwagharimia gharama mbalimbali pale wanapopata mialiko ya kwenda kushiriki michuano mbalimbali basi Tanzania itaweza kupata mafanikio makubwa kupitia mchezo kwani tatizo lililoko hivi sasa ni kukosa uzoefu wa kutosha tofauti wenzao wa mataifa mengine. [189]
wewe
Kwa kumtengea chai mumeo kama ni wadizaini hii utaonyesha mapenzi makubwa na wewe pia kupata nafasi ya kuzungumza naye mipango yenu ya baadaye kama si kupenyeza zako hoja. [190]
wiki
Pemba, baada ya serikali kushusha bei ya zao hilo, kutoka Sh 5,000 hadi Sh 3,750 kwa pishi moja katika kipindi cha wiki moja iliyopita. [191]
yaani
Yule Nsajigwa ni hatari sana nimekuwa nikimfuatilia alikuwa ananipa presha sana yaani kwa utafiti wangu niliofanya hakuna beki kama yeye sasa hivi Afrika Mashariki,î alisema Kimanzi. [192]
yako
Andaa chai yako kwa umakini, chai shurti iandaliwe ikiwa na kila kikorombwezo kumpumbaza. [193]
yao
Maofisa wangu wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo na ninatarajia kwamba watakamilisha kazi yao, ili Januari 14 tumpeleke (Ole Sendeka) mahakamani,"alisema Matei. [194]
yetu
Kwa Tanzania kukosa chombo muhimu cha usafiri wa anga kama hicho ni aibu na kinarudisha nyuma maendeleo na hata kuitangaza nchi yetu kibiashara na utalii katika duniani. [195]
yuko
Huyu yuko kwenye upande wa madini. [196]
yule
Halafu nikuchekeshe zaidi ni kwamba hata yule kocha aliporudi kwenye klabu yake Merreikh. [197]
za
Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo aliyelazwa katika Hospitali ya Bombo, Hamid Swahib, ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Mayomboni wilayani Mkinga, alisema mara baada ya ajali, lilijitokeza kundi la watu waliojidai kutaka kutoa msaada wakati ni wezi wa mali za watu. [198]
zangu
Siwezi kufanya programu zangu vizuri na mara nyingi nimelazimika kuahirisha hata mazoezi. [199]
zote
Alizitaka mamlaka zote zinazohusika na masuala ya usalama barabarani kuhakikisha kwamba wasafirishaji wa abiria na mizigo wanazingatia kikamilifu sheria za usalama barabarani na kuwa makini zaidi na vyombo wanavyoviendesha, ili kuepusha ajali zinazoendelea kupoteza maisha ya watu na uharibifu wa mali. [200]