Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-05

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
aende
Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [2]
agizo
Ilionekana dhahiri kuwa mgambo wale walikuwa wameshaamua kutekeleza kama ni agizo au uamuzi wao huo. [3]
aina
Sitaki uniulize maswali ya kipuuzi na wala sitaki unifananishe na Kivuitu kwa sababu Kivuitu ni wa Kenya na mimi ni Jaji Makame wa Tanzania na Tanzania si Kenya, hivyo naomba usitishe maswali ya aina hiyo. [4]
akawa
Kocha huyo aligeuka kituko juzi mjini Jinja baada ya kukosa usafiri wa kurejea jijini Kampala ambako ni umbali wa kilomita 85 na akawa anasimamisha kila gari nje ya uwanja wa Bugembe. [5]
akiwa
Nalimaha ndiye kinara wa mabao akiwa amepachika matatu. [6]
ama
Kuhusu suala la vurugu kutokea wakati wa kampeni hizo ama kuwepo kwa malalamiko kuhusu kampeni za Operesheni Sangara, Jaji Makame alisema sheria na kanuni za tume yake haziwezi kutumika katika vurugu baina ya vyama visivyo shiriki katika uchaguzi na vile vinavyoshiriki bali watakaohusika katika vurugu hizo hushughulikiwa na Jeshi la Polisi. [7]
amri
Makamba alisema kutokana na Mbowe kukiuka, amri hiyo imemrudia mgombea wake, Shitambala ambaye ameenguliwa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa "hamheshimu baba na mama yake, kwa kuwa Mwinyi ni baba yake. [8]
ana
Alifafanua kuwa kutokana na maandalizi mazuri waliyofanya katika uchaguzi huo wa Mbeya Vijijini, ana hakika shughuli za kampeni zitafanyika vizuri na hatimaye uchaguzi utafanyika katika tarehe iliyopangwa. [9]
anasema
Profesa Chris Peter Maina wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anasema kuwa pamoja na serikali kuhusika kwa kiasi kikubwa katika vitendo vya uvunjifu wa amani, wananchi nao wanahusika kwa kiwango kikubwa. [10]
au
Hiyo ni kazi ya polisi; ndio wenye jukumu la kuhakikisha kwamba, vurugu hizo hazitokei na endapo zitatokea wataamua sheria ichukue mkondo wake au la,” aliongeza mwenyekiti huyo. [11]
bado
Shule nyingi tulizozikagua tumekuta vitabu bado na vipya na baadhi havijagongwa mihuri lakini cha kushangaza ni pale baadhi ya shule tumekuta matumizi makubwa ya fedha za kununulia vitabu yamefanyika lakini vitabu vyenyewe hatukuviona, alisema. [12]
bao
ZAMBIA na Burundi zimetoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Kundi B wa michuano ya Chalenji uliofanyika mapema jana mjini hapa huku kocha wa Zambia, Herve Renald akiwakoromea waamuzi kwa kuchezesha kwa upendeleo. [13]
bila
Wanafunzi wanaomaliza darasa la saba mkoani Shinyanga ni asilimia 70 pekee na asilimia 30 wanaobakia wanapotea bila kufahamika walipo. [14]
binafsi
Kikubwa zaidi ambacho Watanzania tunatakiwa kukifanya ni kuiona michezo kama wajibu wetu, tuichangie na si kuiacha kwa wadhamini, wafadhili ambao wengine wana maslahi binafsi kama ambavyo imekuwa ikifanyika katika klabu zetu zikiwamo maarufu, Simba, Yanga. [15]
chanzo
Haiwezekani kila mara wawe chanzo au wahusishwe na vurugu. [16]
chawa
Pamoja na jitihada zote hizo bado kikulacho kilibaki nguoni! Pamoja na kunyoosha kaptura na sketi zao wakiziwekea “mapanga” yaliyonyooka, bado hawakuwa na ufahamu kwamba katika mapindo ya nguo zao kulikuwa na chawa. [17]
chochote
Alisema kwa Rais Kikwete, Wazanzibari si chochote kwa kuwa ameshindwa kushughulikia kero za msingi na badala yake amewatelekeza kwa miaka mitatu yote ya utawala wake. [18]
chuki
Hata hivyo, nadhani badala ya kuendelea kuwalaumu na kujenga chuki dhidi yao, tuwaombe viongozi wa manispaa na jiji la Dar es Salaam kwa ujumla na wale wote wanaosimamia ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba mgambo wanapata mafunzo thabiti ya kazi zao. [19]
es
Akizungumza na Mwananchi jana jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Lewis Makame alisema operesheni Sangara haihusiani kabisa na uchaguzi kwa sababu chama hicho hakina mgombea katika uchaguzi huo. [20]
eti
Nani atakayekupiga eti kwa sababu tu umevaa fulana ya chama cha MDC (chama kikuu cha upinzani Zimbawe - Movement for Democratic Change) na ukahudhuria mkutano wao. [21]
fujo
Siku hizi huwezi kusikia watu wakizungumzia mambo ya siasa, nadhani tumeona picha za waathirika wa fujo kwenye maeneo ya vijijini, kwa hiyo hakuna anayependa kuishia kwenye hali hiyo. [22]
fupi
Katika hatua nyingine, afisa elimu wa mkoa wa Shinyanga, Eva Lopa alisema wanafunzi wa darasa la saba mwaka huu hawatakuwa na likizo fupi ya mwezi wa tatu wala likizo ndefu ya mwezi Julai na badala yake watabaki shuleni wakiendelea na masomo ili kufidia upotevu mkubwa wa vipindi uliojitokeza. [23]
gani
Hata hivyo, Chadema haikudokeza kuwa ingezungumzia mambo gani kuhusu Mwinyi ambaye aliongoza nchi baada ya muasisi na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kung'atuka. [24]
hadi
Moja ya kanuni za tume ya uchaguzi ni kusimamia vyama vinavyoshiriki katika kampeni hadi siku ya uchaguzi na moja ya mambo tunayoyatazama wakati huo, ni mahusiano baina ya vyama vinavyoshiriki uchaguzi. [25]
hajui
Kauli hiyo ilionekana kumchanganya sana Kazim, akawa hajui la kufanya. [26]
hakuna
Matokeo kama haya yanapaswa kuwa fundisho kwa wachezaji na wadau wote kwa ujumla, kila mtu anapaswa kujua kwamba hakuna mechi rahisi,” alisema kocha huyo. [27]
hana
Naye naibu katibu mkuu wa CUF, Zanzibar Juma Duni Haji alisema Rais Jakaya ameshindwa kufanya ziara visiwani Zanzibar kwa kuwa, anaona aibu hana la kuwaambia Wazanzibari kuhusu muafaka. [28]
hao
Alisema badala ya Ewura kuwashutumu wafanyabiashara hao kwa kusema wanajipangia bei ya mafuta kwa matakwa yao, Ewura wanatakiwa kukaa na wahusika hao kufanya majadiliano ili kujua vikwazo vinavyowafanya wafanyabiashara hao kutoshusha bei ya mafuta hata kama katika soko la dunia bei iko chini. [29]
hapa
Tangu mwezi Julai mwaka jana wakati bei ya mafuta ilipopanda hadi dola 147 za kimarekani, ambayo ni ya juu kuliko zote katika historia ya soko la nishati hiyo, bei ya mafuta nchini imekuwa ikipanda hapa nchini bila kushuka wakati katika soko la dunia imeshuka hadi chini ya dola 40 za kimarekani kwa sasa. [30]
hasa
Ni jambo ambalo haliingii akilini kusikia kuwa klabu hiyo pamoja na Yanga wakati mwingine zinalia njaa, hasa pale inapokuwa wadhamini au wafadhili wamejitoa au kujiweka kando. [31]
haswa
Tulipokuwa shule ya msingi huko vijijini tulijifunza maana haswa ya methali ya Kikulacho Kinguoni Mwako. [32]
hata
Mwenyekiti huyo alitoa kauli hiyo siku moja baada ya katibu mkuu wa Chadema, Dk Wilibrod Slaa kusema kuwa wataendelea na ratiba yao ya Operesheni Sangara kwa sababu walishaanza harakati hizo mapema hata kabla ya uchaguzi huo kuwepo. [33]
hatia
Kitendo cha jeshi la polisi kutumika vibaya katika uchaguzi huo ni ishara kuwa, jeshi hili linatumika kisiasa zaidi kwa kupendelea watu fulani, hadi kupelekea kuvunja haki za kibinadamu kwa kuwamwagia maji ya pilipili na kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia," anasema Profesa Maina. [34]
hawa
Bila ya kupambana na uhalifu, wananchi watakosa amani kwani usalama wao na mali zao vitakuwa rehani, lakini sasa wanachokifanya hawa mgambo kukamata watu ovyo na kuwapiga hakiwezi kuungwa mkono. [35]
hawezi
Sasa narudia kusema; usiogope kumwambia mwezako unavyotaka akufanyie kwani asipofanya usimlaumu kwa kuwa hawezi kujua. [36]
hii
Katika shule ya msingi Ditima wilayani Bariadi, wanafunzi wa darasa la tatu na nne walifundishwa somo la historia vipindi vinne tu kati ya 92 tangu shule ifunguliwe Januari mwaka 2008... katika shule ya Igaga wilayani Kishapu vipindi vilivyopotea kuanzia Januari hadi Novemba 2008 ni 5,193 kwa masomo yote shule nzima na katika shule ya Ikonda iliyopo Shinyanga Vijijini, somo la maarifa darasa la sita halijafundishwa kwa miezi minne tangu mwezi Mei hadi Oktoba 2008... hali hii haikubaliki, alisema. [37]
hiki
Kitendo hiki kinaashiria kuwa baadhi ya wawekezaji hawa hawana sifa kwani wanapaswa kuwa na teknolojia ya kisasa na uwezo wa kifedha kuendesha shirika kubwa kama hilo. [38]
hili
Sasa kama ni Mbowe amefanya kosa hili mwaka 2010, si tayari anakuwa ameshairahisishia njia CCM,” alisema Duni. [39]
hilo
Badala yake, Mwinyi alisisitiza amani, mshikamano na maendeleo ya wilaya ya Mbeya Vijijini, akiwataka wananchi wa eneo hilo kuhakikisha wanabakia na mshikamano wakati wanasiasa watakapoondoka jimboni humo baada ya purukushani za uchaguzi. [40]
hivi
Barua za waliovuliwa vyeo zinaandaliwa baada ya kikao maalumu kinachotarajiwa kufanyika hivi karibuni. [41]
hiyo
Kwa sababu hiyo nawaombeni viongozi wa vyama vya siasa, mshindane kwa sera msitumie matusi, ubabe, kejeli, dharau na uongo kama njia ya kampeni. [42]
hizi
Huu ni ushamba na kupitwa na wakati, haiwezekani wazungu wakatufanyia kila kitu yaani kwa mfano timu ya kwanza anayochezea Didier Drogba au Kalou Salomon ifundishwe na Mzungu na hii ya pili nayo ninyang’anywe apewe mzungu, akili gani hizi. [43]
hofu
TIMU ya soka ya Prisons ya Mbeya imewatoa hofu mashabiki wa soka nchini juu ya ushiriki wao katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF ) na kuahidi kuwa watajitahidi kufanya vizuri kadri ya uwezo wao. [44]
hospitali
Alihangahaika kwenye hospitali nyingi bila mafanikio. [45]
huko
Jibu ni rahisi, kuwa tofauti na huko Ulaya, ugonjwa kwa upande wa Simba ni kuachiwa kwa wadhamini au wafadhili na wakati mwingine makundi ya wanachama kuwa na sauti kubwa, ushawishi kiasi cha kuingilia hata benchi la ufundi, kazi ambayo ni ya kitaalam, kiasi cha kuwakatisha tamaa makocha. [46]
huo
Akihutubia umati uliofika kwenye mkutano huo, Mwinyi alisema kuwa uungwana wa viongozi wa vyama vya siasa utawapa matumaini na utulivu wananchi wa Mbeya Vijijini na kuwawezesha kumchagua wanayemuamini kuwa anaweza kutatua matatizo yao kwa kutumia sera za chama chake. [47]
huu
Hata hivyo, kauli ya Dk Slaa ilionekana kuongeza wasiwasi kwa baadhi ya wanachama kwamba, mikutano yao ya kampeni ingekosa baraka za tume wakati huu ambao vyama vinavyoshiriki vinaendelea na kampeni za kunadi wagombea wao. [48]
huwa
Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF), Hamad Rashid, ambaye pia ni mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni, alisema kikubwa na cha msingi ni kwamba hotuba za rais za mwisho wa mwezi au mwaka na katika sherehe na maadhimisho mbalimbali, huwa hagusii kero za Wazanzibari kwa undani. [49]
huyu
Nafuu nyingine anayoweza kujipatia mtu huyu ni kufungua kesi ya madai dhidi ya wote waliofungua au kusababisha kifungo hicho na mwisho, katika mazingira fulani ya kisheria, mtu aliyefungiwa isivyo halali anaweza kupata nafuu kwa msaada wa mahakama kutoa hati maalum ya kisheria ijulikanayo kama 'Habeas Corpus' kuamuru kuachiwa wakati au kupisha hatua nyingine za kimahakama kuendelea ili kuthibitisha au kutengua uhalali wa kifungo chake hicho. [50]
ila
Mwisho nakusihi tu kuwa Usiogope kusema, ila ujue pakusemea. [51]
ile
Jana, gumzo la mashabiki lilikuwa ni kwenye mechi ya wanandugu, Kili Stars na Zanzibar Heroes, pia ile baina ya Rwanda na Somalia ambayo itachezwa majira ya saa 7.45 mchana katika Uwanja wa Nakivubo mjini hapa. [52]
ili
Mwinyi alisema vyama vyote vya siasa nchini lazima vilenge katika kutoa majibu ya kisera kwa matatizo yanayowakabili wananchi ili kuwaletea maendeleo yatakayowafanya kuwa na maisha bora. [53]
ina
Maximo alisema kwamba bado Tanzania ina mechi tatu dhidi ya Zanzibar, Rwanda na Uganda ambazo matokeo yake yataiwezesha kufuzu kwa hatua ya pili. [54]
iwe
KIPIGO cha Somalia kimemnyima raha na kumpotezea utulivu kocha wa Kilimanjaro Stars Marcio Maximo, lakini amewaambia mashabiki wasichanganyiwe bali iwe fundisho na iongezwe mikakati kwa mechi tatu zijazo. [55]
jengo
Hivyo hawa wanaoona kwamba jengo peke yake ni elimu wamepata nafasi ya tatu katika tuzo lakini ni tako tarajiwa tu kwa sababu wana siku chache za kujirekebisha. [56]
jua
Stars inaingia uwanjani baada ya Jumamosi kulazwa bao 1-0 na timu isiyo na makao, mfumo, Somalia katika mchezo wake wa kwanza uliofanyika mchana wakati wa jua kali. [57]
juu
Akizungumza mara baada ya kukagua daraja hilo, Waziri Membe alisema licha ya kuchelewa kulikosababishwa na kutowasili mapema kwa vifaa hivyo, serikali inafurahishwa na mwenendo mzima wa kazi hiyo kwa kuwa inatekelezwa kwa utaalamu wa hali ya juu. [58]
juzi
Stars ilikuwa gumzo juzi jioni mjini hapa baada ya kufungwa bao 1-0 na Somalia ambayo mashabiki wengi wamekuwa wakiibeza. [59]
kampuni
Daraja hilo linajengwa na kampuni ya Geo-Engineering Coopration kutoka Jamhuri ya Watu wa China. [60]
kansa
Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [61]
kasi
Tazama nyuma ulikokotoka na mbele unakokwenda ili uone tofauti iliyopo ndio uweze kupima kasi unayotakiwa uende ili mambo yako yaende vizuri. [62]
kati
Endapo msuguano kati ya vyama hivyo utajitokeza, tume ya uchaguzi inaweza kuviita kwa ajili ya usuluhishi. [63]
kesi
Inaweza kutokea kama mara nyingi inavyokuwa kwa raia wenye chuki kati yao, mmoja wao kumfungulia mashtaka ya uongo na hatimaye polisi kwa shinikizo lake kumtia nguvuni ili aweze kujibu mashtaka hayo ambayo baadaye mbele ya mahakama ya sheria huonekana si ya msingi na hivyo aliyeshitakiwa kuachiwa huru kwa kukosa au kuonekana hana kesi ya kujibu. [64]
kifungo
Mtu anaweza kuwekwa chini ya ulinzi au kifungo kisicho halali kutokana na sababu mbili au zaidi. [65]
kigeni
Lakini, ikiangaliwa kwa umakini, Simba ni klabu ambayo inaongoza kwa kuajiri na pengine kutimua makocha, wazawa au wale wa kigeni. [66]
kila
Guninita alisema kwa kufanya hivyo hakutakuwepo makundi ndani ya chama na hali ya ubaguzi wa wenye fedha na maskini utakwisha na badala yake, chama kitaongozwa kwa usawa kutokana na kila mtu kuwa na haki ya kugombea uongozi bila kuangalia hali yake ya kiuchumi. [67]
kilikuwa
Hivyo ni juu ya mlalamikiwa kuithibitishia mahakama kuwa kifungo hicho kilikuwa halali. [68]
kisasa
Si staili ya kisasa hii ni udhaifu kwa timu, wana kazi kubwa sana ya kutengeneza timu itakayocheza mpira, mpira si kuzuia. [69]
kitendo
Tukio lingine ambalo hakika halitasahaulika lililowashangaza wapenzi wengi wa soka nchini kitendo ambacho kilifanywa na wachezaji wa kigeni wa kimataifa kutoka Nigeria wa klabu ya Simba kumpiga kwa kiatu aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Krasimir Bezinski kwa kile kilichodaiwa kutowapanga wachezaji hao katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Yanga. [70]
kituo
Nakumbuka aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yussuf Makamba aliwahi kuagiza hatua kali za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya mgambo walimtandika mkazi mmoja wa jiji na tukio hilo kuripotiwa katika kituo kimoja cha televisheni. [71]
klabu
SIMBA ni mojawapo ya klabu kubwa na maarufu ya soka hapa nchini ambayo ina historia ndefu ya mafanikio katika medani ya mchezo wa soka. [72]
kocha
Katika mchezo wa leo huenda kocha huyo akawaanzisha kwa pamoja kwenye ushambuliaji, Mrisho Ngassa, Danny Mrwanda na Mussa Mgosi ambao katika mechi dhidi ya Somalia walichachafya kipindi cha pili. [73]
kosa
Akizungumza kwa njia ya simu na Mwananchi jana, naibu katibu mkuu wa CUF- Zanzibar, Juma Duni Haji alisema Chadema haina budi kukishukuru chama chake kwa kuwazindua na kuwaelimisha kosa lao la kizembe lililofanywa na mtu ambaye ni msomi na mwanasheria. [74]
kote
Ni miaka 60 sasa tangu kuanza maadhimisho ya Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu duniani kote, matendo ya uvunjifu wa haki za kibinadamu yamekuwa yakiongezeka duniani kote. [75]
kuanza
Katika mchezo huo, kipindi cha kwanza ilicheza zaidi kwa kujihami na kuzuia zaidi ya kushambulia, lakini kipindi cha pili ikabadili na kuanza kucheza kwa pasi fupi fupi. [76]
kufa
Wakati wanaendelea kuangalia ile picha aliingia daktari aliyekuwa akimwangalia Kazim na kumwomba waziri afupishe mazungumzo, badala yake wamsake yule mvumbuzi wa dawa kwani isingepita saa 12 kabla ya Kazim kufa ikiwa hatapata ile dawa. [77]
kufanya
Mmoja wa wadau waliofuatilia suala hilo katika wilaya moja tu ya Bariadi, Suleiman Monata alikieleza kikao hicho kuwa baadhi ya wakuu wa shule wanashirikiana na wenye maduka ya vitabu na maafisa elimu wa wilaya, kuhujumu fedha za kununulia vitabu kwa kufanya maonyesho tu shuleni kwenye kamati za shule na baadaye vitabu hivyo hurejeshwa madukani. [78]
kuishi
Pamoja na kutii maagizo makali ya walimu, wanafunzi wale walibaki kuishi kwa mazoea ya kuwaridhisha wakaguzi. [79]
kuja
Habari zilisema kuwa basi hilo dogo lilikuwa likitokea Marangu-Moshi Vijini kuja mjini Moshi na lori lilikuwa likija mjini Moshi na inaelezwa kwamba, dereva wa basi dogo alishindwa kulimudu basi hilo na kuligonga kwa nyuma lori hilo. [80]
kukutana
Hivyo walipanga muda wa kukutana. [81]
kula
Siku nyingine nilitamani kula tambi, nikidhani ni bei nafuu na kwamba ningeweza kununua. [82]
kule
Ukifuatilia mchakato mzima kuanzia kule vidudu unagundua mara moja kwamba mfumo wetu wa elimu unajaribu kuridhisha wakaguzi. [83]
kulia
Badala yake viongozi nao waliungana na wananchi kulia kuwa wafanyabishara hawa ndio chanzo cha kupanda kwa gharama za maisha. [84]
kuliko
Awamu ya nne ya serikali ya Kikwete imekuwa ikikumbwa na lawama za mara kwa mara kwa kufanya ziara za nje zaidi kuliko za ndani ikiwa ni pamoja na kushughulikia migogoro ya nje zaidi na kudharau ya ndani. [85]
kumbe
Huyu kafanya hivi huyu kafanya hivi kumbe huyu aliamua kwenda kufanya hivi baada ya kushindwa kumuelewa mwenzake hivi, ushanifaham. [86]
kumuua
Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [87]
kuna
Si katika ziara zake tu bali hata katika hotuba zake hazungumzii kwa undani kero za wazanzibari, kuna mambo 47 ya Muungano lakini hayagusii,” alisema Mohammed. [88]
kundi
Ivory Coast ambao ni wenyeji wa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani(CHAN) imepangwa kundi moja na Taifa Stars, Zambia na Senegal. [89]
kuona
Msimamizi wa ujenzi wa daraja hilo, Alloyce Mutagurwa alisema hayo wakati akitoa maelezo yake kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe aliyetembelea kuona maendeleo ya kazi ya ujenzi wa daraja hilo. [90]
kupitia
Ninamshukuru Chambi Chachage kwa changamoto aliyonipa kupitia Tafakuri Tunduizi. [91]
kura
Alisema wananchi wa Mbeya hawaitaki tena CCM kwa kuwa wana tatizo la mbolea na wanapofika katika maghala ya mbolea wanadaiwa vitambulisho vya kura. [92]
kuruka
Kumbe jamaa mwenyewe alikuwa anatafuta nishani ya kiatu peke yake kwa kujaribu kuzuia kila gari linalotaka kuruka foleni. [93]
kutetea
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia amefanikiwa kutetea nafasi yake ya uenyekiti wa taifa wa chama hicho. [94]
kutii
Lakini jitihada zao ziliishia katika kutii tu maagizo na kumridhisha mkaguzi (mwalimu wa zamu au mwalimu mkuu). [95]
kuu
WATU 10 wamefariki dunia papo hapo na wengine kumi kujeruhiwa vibaya, baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kuligonga kwa nyuma lori la mizigo katika eneo la Mabungo barabara kuu ya Moshi- Dar es Salaam. [96]
kuua
Ni suala la kawaida kuua albino na damu zao au viungo vyao tunavitumia kwenye shughuli hizo za uchimbaji madini na uvuvi, watu wengi wanafanya hivyo. [97]
kuuza
KAMPUNI ya kuuza mafuta ya BP imepingana na uamuzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) ya kuweka ukomo wa bei ya juu ya mafuta baada ya bidhaa hiyo kupanda ghafla katika kipindi cha sikukuu ya Krismasi. [98]
kuzingatia
Tunanunua mafuta kutoka nje kwa bei kubwa na tunalazimika kuyauza kwa kuzingatia bei tuliyonunulia. [99]
kwani
Akizungumza jijini jana, mwenyekiti wa timu hiyo, Dk Salum Chambuso alisema wapenzi wa soka wasiwe na hofu na juu ushiriki wao kwenye michuano ya kombe la Shirikisho kwani timu hiyo inaendelea kujipanga kikamilifu kuhakikisha inashinda mchezo huo ili wapate nafasi ya kusonga mbele. [100]
kwao
Tunaamini kwamba lengo la kuwepo kwao ni kuhakikisha sheria kanuni na taratibu zilizowekwa na manispaa zao hazikiukwi na sio vinginevyo. [101]
kweli
Kwa baadhi ya watu hapa jijini wana wasiwasi kama kweli hawa ni askari waliofunzwa na wakawiva katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo au ni vijana tu wa kihuni wanaokusanywa na kuvalishwa sare Ili waonekane askari. [102]
kwetu
Sasa kuwazindua kwetu kusitafsiriwe kuwa ni uadui,” alisema Duni. [103]
la
Mbeya Vijijini inaendelea kuwa na sega la amani, umoja, upendo na mshikamano. [104]
labda
Lakini nikaja kugundua kuwa ile ya wale kuongea ndiyo dawa yenyewe tofauti tu ni kwamba huenda hawa watu hawakuwa wawazi baina yao wakiwa pekee yao, labda mmoja alishindwa kujieleza. [105]
lake
Hata hivyo, chama hicho kilisema kuwa kitaendelea na mikutano ya Operesheni Sangara, ambayo lengo lake limekuwa likielezewa na chama hicho kuwa ni kufagia ufisadi na kurejesha maadili ya taifa ambayo yamepotezwa na baadhi ya watu wenye ubinafsi. [106]
lao
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama wa mkoa na taifa, ikiwa ni pamoja na makamu mweyekiti wa CCM, Pius Msekwa, Nape Nnauye, Tambwe Hiza na baadhi ya wabunge wa mkoa wa Mbeya huku bendi ya TOT ilishindwa kuhudhuria katika uzinduzi huo kutokana na gari lao kuharibika njiani. [107]
leo
Aliwaahidi Wazanzibari kuwa ataushughulikia mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar kabla ya mwaka 2008, leo ni 2009 hana alichokifanya. [108]
ligi
Prisons inaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi msimu uliopita ambapo Yanga ilitwaa ubingwa. [109]
lita
Kiwango hicho ni cha chini kulinganisha na bei ya sasa ambayo ni kati ya Sh1,400 na Sh 1,600 kwa lita moja ya petroli na kati ya Sh1,300 na Sh1,400 kwa lita moja ya dizeli. [110]
lolote
Aliishangaa Chadema kuwa pamoja na kuwa na uzoefu wa miaka 15 katika chaguzi za vyama vingi, bado inafanya kosa la kizembe na kushindwa hata na mgombea wa SAU ambaye alisema hana uzoefu, lakini ameweza kujaza fomu bila ya tatizo lolote. [111]
maana
Ndio maana anaona aibu kwa kuwa hana hata cha kuwaeleza Wazanzibari,” alisema Duni. [112]
madai
HIVI karibuni niliwashuhudia askari wa mgambo wakivamia nyumba za baadhi ya wakazi tu wa Uwanja wa Ndege kwa madai kuwa wanasaka wafanyabishara ndogo ndogo maarufu kwa jina la wamachinga. [113]
maji
Mbali ya maduka hayo pia mgambo hao waliingia katika majumba ya watu, niliwashuhudia wakiwapiga watu bila hata ya kuuliza, wakimwaga maji yaliyokuwa yamehifadhi katika ndoo na kuzichukua. [114]
mara
Sababu nyingine iliyotajwa kuzorotesha taalumu mkoani Shinyanga ni pamoja na vitabu vingi vinavyonunuliwa kwenye maduka ya vitabu na wakuu wa shule kufungiwa kwenye maboksi ofisini na baadaye hurejeshwa tena kwenye maduka hayo kuuzwa kwa mara ya pili huku wanafunzi wakibaki bila vitabu. [115]
mawili
Anafuatiwa na Given Singuluma wa Zambia, mawili na Gatoto Erick, pia wa Burundi, mwenye mabao mawili. [116]
mbele
Alisema ili chama kisonge mbele kinahitaji viongozi wenye kufuata maadili ya uongozi na katiba na si kuongoza chama kwa matakwa ya watu fulani kwa maslahi yao. [117]
mengi
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusiana na ukiukaji wa maadili unaofanywa na mgambo hawa. [118]
meno
RAPA na mwimbaji mahiri wa bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga,Pepeta International', Khalid Chuma 'Chokoraa', amesema ameuanza vibaya mwaka huu baada ya kuvunjika meno mawili katika mkesha wa mwaka mpya. [119]
mno
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [120]
moja
Lakini ninahitaji jambo moja mlielewe. [121]
moto
Nyumbani kwake kunawaka moto anazima moto kwa jirani,” alisema Mohammed. [122]
moyo
Hisia hizi za wasiwasi zimekuwa zikizidi kila siku kufuatia matendo yanayofanywa na askari hawa ambao wengi wao ni vijana ambao kwa hali ilivyo inaonekana wanmekosa moyo wa ubinadamu. [123]
moyoni
Amani ilikuwa imetawala moyoni. [124]
mrefu
KWA muda mrefu Watanzania tumekuwa katika matatizo makubwa ya kupanda kwa bei ya mafuta, ambayo ilisababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la duniani. [125]
msaidizi
Jamaa huyo ambaye alikuwa kama msaidizi wake wa karibu, alikuwa akimuwakilisha katika kazi mbalimbali na ndiye aliyekuwa ana siri zake nyingi. [126]
mtindo
Wangekamata magari na kuyakalisha pale nusu saa, huu mtindo ungekoma papohapo. [127]
muda
Ewura iliwasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu mwongozo wa bei za nishati hiyo, ikitaka petroli iuzwe hadi Sh1,166 wakati bei ya dizeli iuzwe hadi Sh1,300. Mwanasheria Mkuu anatarajiwa kutangaza katika gazeti la serikali muda wowote ili wafanyabiashara wote wa nishati hiyo wauze kulingana na bei hiyo elekezi. [128]
mumewe
Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [129]
mwa
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Yohana Balele alisema hayo wakati wa kikao cha tathmini ya elimu kilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini Shinyanga na kuwakutanisha wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa idara na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu. [130]
mwema
Hakuna mwananchi mwenye kupenda maadili, yaani raia mwema ambaye anaweza kupinga jitihada za kusaka wahalifu, hata siku moja. [131]
mwezi
Akizungumzia kuhusu upotevu wa vipindi ulioonekana katika ukaguzi uliofanywa na idara ya ukaguzi wa shule, kuanzia mwezi Mei hadi Septemba mwaka jana, mkuu huyo wa mkoa alieleza kukerwa na maelfu ya vipindi vilivyopotea bila ya wanafunzi kufundishwa huku walimu husika wakilipwa mishahara yao kama kawaida. [132]
mzuri
Nimeona wana kipa mzuri, Mohamed Abdallah hawakupaswa kufanya walivyofanya,”alisema Mwesigwa akionyesha kukerwa na mchezo wao. [133]
na
Mwinyi, ambaye anajulikana kama 'Mzee Ruksa' kutokana na kuongoza nchi wakati wa mageuzi yaliyoruhusu ushindani wa vyama vya kisiasa, hakuonyesha unazi kwa CCM wala mgombea wake wakati alipozindua kampeni za chama hicho jana katika kata ya Kijiji cha Ilembo kilicho tarafa ya Isangati wilayani Mbeya Vijijini. [134]
nalo
Jingine ambalo nalo ni kumbukumbu kwa soka ni timu ya taifa ya vijana ya Copa Coca Cola iliyofanikiwa kuibuka mabingwa wa dunia katika michuano ambayo ilikuwa ikishirikisha vijana kutoka nchi na mabara mbalimbali wenye umri chini ya miaka 17 iliyofanyika Brazil mwezi Juni. [135]
namna
Imeripotiwa kuwa wizara hiyo imekuwa ikiendesha vikao mbalimbali vya kuangalia namna ya kuondoa kero hizo za Muungano, ingawa utendaji wake bado haujaridhisha wengi. [136]
nao
Tutakabiliana nao kadri inavyowezekana kuhakikisha kwamba tunawashinda tupate uhakika wa kwenda hatua ya pili mapema,”aliongeza. [137]
naye
Aliongea kwa muda, usiku huo, baadaye alichukua simu yake ya mkononi na kumpigia mmoja wa wale watu waliokuwa wakisimamia biashara zake na kumuomba namba ya mtu yeyote anayeendesha biashara hiyo ya madini ili azungumze naye. [138]
nayo
Lakini mkurugenzi wa kampuni ya mafuta ya BP alisema bei hizo hazitekelezeki kwa kuwa wameshanunua mafuta waliyo nayo sasa kwa bei kubwa. [139]
ndege
Ni kweli ninafanya kazi, lakini si yangu, utajiri wangu umepungua, nilikuwa nataka kununuaq ndege binafsi ya kutembelea, kwa hali ya kipato changu cha sasa, sina uwezo wa kufanya hivyo, mbaya zaidi tayari nilishatamba kwa watu kwamba nitanunua ndege, nisipomnunua wataniona mimi ni maskini” alijisemea. [140]
ndiyo
Hali hiyo ndiyo msingi wa maendeleo yatakayoleta maisha bora kwa wananchi wa Mbeya Vijijini," alisema. [141]
ndogo
Kwa sababu hiyo hatuwezi kuyachukua mafuta tuliyoyanunua kwa bei ya juu na kuyauza kwa bei ndogo. [142]
nguvu
Kocha huyo alisema kwamba watatumia nguvu kubwa na juhudi kuhakikisha wanapata pointi muhimu na atafanya mabadiliko kadhaa kwenye safu ya ushambuliaji. [143]
ni
Iwe ni mwiko kuchafuana na kitachotoa majibu sahihi ya matatizo yanayowakabili wananchi wa Mbeya Vijijini ni ubora wa sera, si matusi, wala ubabe, si kejeli wala vijembe na uongo,” alisema Mwinyi ambaye aliongoza nchi kwa vipindi viwili (mwaka 1985/90 na 1990/95). [144]
nje
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng'hoboko aliliambia Mwananchi kwa simu jana kuwa, ingawa yuko nje ya mkoa wa Kilimanjaro, lakini amejulishwa kuhusu ajali hiyo mbaya iliyotokea saa mbili kamili usiku. [145]
ofisi
Guninita alisema hayo wakati akifungua semina ya siku mbili ya Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM), iliyofanyika jana kwenye ofisi ya chama hicho wilayani Ilala jijini Dar es Salaam. [146]
panga
Unapiga pasi kaptura kumwonyesha mkaguzi kuwa “panga” lile lisingepatikana kama hukupiga nguo pasi. [147]
pasi
Bao hilo liliwekwa kimiani na Roger Kola aliyepokea pasi ya Jonas Kakuwaha ambaye alipiga shuti lililomshinda kipa wa Burundi, Vladimir Niyonkuru, anayeichezea Azam FC ya Dar es Salaam. [148]
peke
Siko peke yangu ninayefikiria hivi. [149]
pia
Kikao hicho pia kiliarifiwa kuhusu ukaguzi ambao uliwabaini wanafunzi 159 wa darasa la tatu hadi la nne katika shule tatu za Kiloleli (Kishapu), Azimio (Shinyanga Manispaa) na Ilolabashi (Shinyanga Vijijini) ambao hawajui kusoma wala kuandika. [150]
picha
Huo mchezo ni hatari sana, sijui wala sipati picha itakuwaje. [151]
pindo
Hivyo watoto wale walipiga pasi kutengeneza upanga wa kumdhihirishia mkaguzi kuwa walikuwa wametii maagizo lakini hawakufanikiwa kukiondoa kiwalacho! Kilibaki katika pindo za nguo zao. [152]
raia
Phiri, aliyewahi kuinoa Simba, anachukua nafasi ya Krasmir Bezinski, raia wa Bulgaria, aliyekuwa akisaidiwa na Jamhuri Kihwelo, mzawa. [153]
saba
Zoezi hilo litaendelea kwa wakuu wote wa idara walioshindwa kutimiza majukumu yao ya kusimamia sekta ya elimu kwenye maeneo yao kiasi cha kusababisha mkoa huu, kushika nafasi ya mwisho kitaifa katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana. [154]
sana
Katika umoja wenu itunzeni imani yenu kama mboni za macho yenu; waonyesheni wanasiasa kwamba mnawapenda sana lakini wakati huohuo mnaipenda zaidi Wilaya ya Mbeya Vijijini,” alisema. [155]
sasa
Hivi sasa tumeanza kutandika jamvi na tayari nguzo nne kati ya 12 tumeshaanza kuzilaza kama unavyoona,” alisema Mutagurwa. [156]
shule
SERIKALI mkoani Shinyanga imewavua madaraka walimu wakuu 35 wa shule za msingi na waratibu watatu wa elimu wa kata kwa tuhuma za uzembe wa kushindwa kufuatilia vyema majukumu yao ya kusimamia taaluma mashuleni. [157]
sio
Hatukutegemea kama shindano hili lingefanikiwa kiasi kile , lakini ninalotaka kusisiza kuwakumbushia mabinti wetu kwamba urembi sio uzuri wa sura na umbo pekee bali wanatakiwa kuwa wachangamfu kiakili wakati wote, "alisema Balozi Leanare. [158]
siri
Siyo siri kuwa klabu hiyo, pia inajivunia kuwa na rekodi nzuri ya mafanikio makubwa pengine kuliko zote katika Tanzania. [159]
sisi
Ni mchezo mgumu sana kwa vile sisi ni ndugu na kila mmoja ana shida ya kusonga mbele,”alisema Badr, ambaye ni Mmisri. [160]
sketi
Eneo la kwanza walilojikuna wanafunzi wale lilikuwa kiunoni, pale inapofungiwa vifungo vya kushikilia kaptura au sketi. [161]
soko
Kongoro alisema kuwa wafanyabiashara wa mafuta nchini wanalazimika kuuza nishati hiyo kwa bei ya sasa kufidia gharama za kununua nishati hiyo kutoka nje, kwa sababu mafuta waliyonayo sasa hawakuyanunua kwa bei ya sasa ya soko la dunia. [162]
sura
Kipigo cha Somalia kilionekana kumchanganya Maximo juzi jioni na wakati alipokuwa akiifuatilia mechi ya pili baina ya Zanzibar na Uganda alikuwa amekunja sura na kuonekana mtu mwenye mawazo tofauti na kawaida yake. [163]
taasisi
Hatua hii ya Ewura inatuonyesha kwamba, taasisi nyingi za serikali zilizopewa mamlaka ya kusimamia huduma fulani kama zikiamua kufanya kazi yake sawasawa inawezekana matatizo mengi nchini yakamalizika. [164]
tako
Lakini kwa kuwa sisi ni watu wa ukweli na uwazi, tumejiweka wenyewe ndani ya tuzo la tako. [165]
tamko
Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake Kurasini jijini Dar es Salaam, mkurugenzi huyo, Engelordt Kongoro alisema tamko hilo halikuzingatia hali halisi ya biashara hiyo nchini. [166]
tofauti
Ukiachana na matukio hayo, vijana wa Zambia walicheza mpira wa hali ya juu tofauti na mechi zake mbili za awali. [167]
tu
Nchi yetu ni kubwa kwa urefu na upana kwa hiyo maendeleo hayana budi kusambaa polepole hayawezi kuenea kwa haraka tu kama vile chumvi katika mchuzi. [168]
tumekuwa
Namna nyingine ambayo tumekuwa tukifanya mambo kwa mazoea ni kushindwa kutambua vyema maana haswa ya elimu. [169]
ubingwa
Naapa, hakuna kocha yoyote mzungu atachukua ubingwa pale Ivory Coast. [170]
uchungu
Kwa nini wengine wafaidi tu, sisi waishiwa tusifaidi? Tumefurahi kuona kwamba wako wengi wenye uchungu wa nchi yao. [171]
ujue
Nina kuomba uniulize maswali yanayohusiana na uchaguzi wa Mbeya na si vinginevyo ama ulitaka tuipendelee Chadema ndipo ujue tumetenda haki. [172]
uko
Sasa Kazim ujue kwamba uko chini ya ulinzi, kwa sababu ni mgonjwa sana tutakufunga pindu hapa wakati tunaangalia namna ya kukufanyia, uko chini ya ulinzi,” alisema mkuu wa jeshi la polisi ambaye alionekana kusononeka sana kwa kifo cha yule mvumbuzi wa dawa. [173]
ukweli
Kuhoji mazoea ni muhimu kutokana na ukweli kwamba Kikulacho, Kinguoni Mwako. [174]
usafi
Wanafunzi wale walihudhuria vyema madarasani ambapo walifundishwa pia masuala ya usafi. [175]
utafiti
Haki ya Mungu ningependa kufanya utafiti. [176]
uvuvi
Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [177]
vijana
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Dar es Salaam, John Guninita amewataka vijana kuwafichua watu aliodai wanakigawa chama kwa kukiweka katika makundi ya wenye fedha na maskini. [178]
vipi
Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni,” alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [179]
vitu
Alisema Ewura kama wahusika wanaoshughulikia nishati ya mafuta nchini, wanatakiwa kabla ya kuzungumza chochote, waangalie hali hii kuliko kukurupuka na kuzungumza vitu visivyotekelezeka. [180]
vyao
Katika vikao vya namna ile utasikia wazee wakisema kikao hiki kinabaraka! baraka ile ni ya wele wawili wanaojaribu kuzungumza mambo yaliyo jaa vifuani kwao na kisha kuunganisha tena wakiwa wanaanza maisha mapya yaliyokunjua vifua vyao. [181]
vyombo
Kila Mzimbabwe aliyefuatilia vyombo vya habari kuhusu mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika Misri kwa hamu kubwa alifuatilia uchaguzi wa Ijumaa ile. [182]
wale
Mwandaaji wa shindano hilo kutoka Kampuni ya MD Rena Events Ltd, Rena Callist aliishukuru Serikali ya Burundi kwa ushirikiano wake na kuahidi kutumia sehemu ya mapato yaliyopatikana katika shindano hilo kwa kusaidia watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa kuanzia katika nchi hiyo kabla ya kwenda nchi nyingine. [183]
wao
Mikutano ya Chadema haiwezi kuathiri hali ya kampeni za uchaguzi kwa sababu Chadema haina mgombea na sheria za uchaguzi hazizungumzii chama ambacho hakihusiki katika uchaguzi, hivyo wao wako huru kuendelea na ratiba yao kama walivyoipanga,” alisema Jaji Makame. [184]
wapi
Akizungumzia kuhusu faini ya milioni tatu iliyotangazwa na mamlaka hiyo kwa kampuni itakayokiuka amri ya kushusha bei, Kongoro alisema wao hawawezi kuilipa kwa sababu hawajui wataitoa wapi. [185]
wapo
Haya, haya, haya, wapo ambao wamediriki hata kutuita sisi waishiwa kuwa ni mafisadi, eti tumekunywa na kunywaga ushuru wa watu hadi asubuhi siku ya mwaka mpya. [186]
wazi
Na kila siku kabla ya kuingia darasani wanafunzi wote tulijipanga katika mistari iliyonyooka eneo la wazi kwa ajili ya gwaride la kukaguliwa usafi. [187]
wenyewe
Hapa sababu kubwa huwa ni raia wenyewe. [188]
wetu
Hakikisheni kwamba wakati wanasisaa wetu wanapoondoka Mbeya Vijijini baada ya kampeni, nyinyi mnabaki kuwa kitu kimoja. [189]
wewe
Ni vizuri kuongea kutokana na tofauti zenu, na kujaribu kuzungumzia wenyewe mambo ambayo wewe unayo moyoni kuhusu mwenzio ili kwa wakati wake ajaribu kuchuja na kujifunza kukuridhisha. [190]
yale
Akizungumza baada ya kutambulishwa kwa wananchi mgombea wa CCM, Luckson Mwanjale aliwataka wananchi wa Jimbo la Mbeya Vijijini kumchagua ili aweze kutekeleza yale ambayo hayati Richard Nyaulawa aliyaacha. [191]
yenye
Zanzibar Heroes yenye pointi nne kwenye michuano hiyo ya Chalenji inakwaana na Stars ambayo haina pointi yoyote leo saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Nakivubo. [192]
yeye
Akizungumza na Mwananchi, kocha huyo alisema: Namshukuru Mungu pamoja na bidii zangu kwani yeye ndiye hugawa riziki ya mtu,ushirikiano na wachezaji wangu ndio umenifanya kuwa hivi. [193]
yeyote
Msimwogope mtu yeyote mnayemwona anaenda kinyume na katiba. [194]
yule
Hakuna jambo la kukufanya tusikutangaze kama mgunduzi wa dawa kuponya kansa kwenye moyo, dawa yako tulimpa hadi mtoto wa rais na amepona, rais anataka akuone kukushukuru na kupanga sherehe kubwa ya uzinduzi wa dawa hii ya aina yake,” alisema waziri wa afya wa nchi hiyo siku moja alipokutana na kijana yule mwenye ulemavu wa ngozi. [195]
zake
MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame amekiruhusu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuendelea na mikutano yake ya kampeni zake za Operesheni Sangara mkoani Mbeya ili zisiathiri harakati za uchaguzi wa ubunge unaoendelea katika mkoa huo. [196]
zako
Endapo nguvu na bidiii zaidi utazielekeza kwenye shughuli zako mwaka huu unaweza kuufurahia na kama sivyo basi utaununia. [197]
zao
Waziri Membe alisema kukamilika kwa Daraja la Umoja itakuwa ni ukombozi mkubwa wa mawasiliano ya usafiri, si kwa wananchi wa nchi hizo mbili tu, bali hata nchi nyingine za Sadc kwa kuwa zitaweza kusafirishia bidhaa zao mbalimbali kwa njia ya barabara. [198]
zetu
Lakini pasi zetu hazifiki katika pindo za nguo ambamo ndimo kikulacho kimejificha. [199]
zote
Ewura imeshaeleza kuwa mfanyabiashara atakayekiuka bei hiyo atalipishwa faini ya Sh3 milioni au kufutiwa leseni au kupewa adhabu zote mbili kwa pamoja. [200]