Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-02

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


akili
Naye Mchungaji kiongozi wa kanisa kuu hapo Ernest Kadiva alisema Tanzania inapaswa kuelewa kuwa kuna kuanguka na kuinuka hivyo ni vema wananchi wakautumia mwaka 2009 kama mwaka wa kuinuka ili mawazo ya kifisadi na mambo mengine yaliyotawala kwenye akili na mioyo ya watu wengi yakaanze kutoweka. [1]
akiwa
Mwendesha mashtaka, wakili wa serikali, Stanslaus Boniface, aliileza mahakama kuwa Mramba akiwa waziri wa fedha na Yona akiwa waziri wa nishati na madini kwa pamoja walitumia vibaya madaraka yao kwa kuingia mkataba na kampuni ya M/S Alex Stewart (Assayers ya Uingereza ulioiruhusu kudhibiti uzalishaji wa madini ya dhahabu kinyume cha sheria. [2]
ama
Watuhumiwa wote kwa sasa wako nje kwa dhamaa baada ya kukamilisha masharti mbalimbali yakiwemo kutoa ama pesa tasklimu au hati za mali zenye thamani sawa na nusu ya pesa wanazodaiwa kusababisha hasara. [3]
ambapo
Masebu alisema vituo vyote vinavyouza dizeli yenye ubora tofauti(500ppm na 5000ppm) vinatakiwa kuonyesha kwenye visima na kuuza dizeli tofauti katika kisima kama ilivyoonyesha itachukulia kama ni uchakachuaji wa mafuta ambapo adhabu kali itachukuliwa. [4]
ambayo
Hatua yao ya nne, ambayo ilisababisha viongozi nane wa Jumuiya hiyo kukamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kukusanyika bila kuwa na kibali, waliifanya Oktoba 29 baada ya kukaa katikati ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Umoja wa Mataifa kuanzia alfajiri na kusababisha msongamano mkubwa wa magari jijini Dar es Salaam. [5]
anasema
Profesa Chris Peter Maina wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anasema kuwa pamoja na serikali kuhusika kwa kiasi kikubwa katika vitendo vya uvunjifu wa amani, wananchi nao wanahusika kwa kiwango kikubwa. [6]
ang
Lakini kama serikali haitakubali kukaa na sisi kujadili malipo yetu na ikiendelea kung’ang’ania msimamo wake kuwa imeshatulipa, hatutasita, tutaendelea na harakati zetu mpaka tutakapohakikisha tumelipwa," alisema Makingi. [7]
ardhi
Wajumbe hao walisema uhaba wa ardhi ya kilimo katika wilaya hiyo,umechangiwa na hatua ya serikali ya kuwapa wawekezaji maeneo makubwa wanayoyatumika kwa kilimo cha chain a mkonge. [8]
asije
Ninaikumbuka Harare ya zamani, ambayo mashimo yalikuwa yakizibwa pale yanapotokea, wakati ambao mtu ungeweza kwenda dukani na kununua maziwa bila kupigwa muhuri wa hilo duka ili asije kununua tena. [9]
au
Sasa hapo tukiandamana au kudai mafao yetu utatuambia kuwa tunachochea vurugu wakati ni wazi kuwa madai yetu hayasikilizwi," alisema Makingi. [10]
bado
Alisema kauli kwamba baadhi ya watu wamekuwa na lengo la kujinufaisha na ghasia hizo, si kweli kwani upande wa walimu ni jambo ambalo liko wazi hadi sasa bado wanapigwa chenga na kushindwa kupata haki zao. [11]
bali
Mukoba alisema kauli hiyo ya rais inalenga kuwatisha walimu na wafanyakazi wote wanaoidai serikali madai mbalimbali na kwamba, katika matukio yote yaliyotokea mwaka jana hakuna tukio la mgomo ambalo lilikuwa la uchochezi bali yalilenga kudai haki. [12]
bao
Zanzibar iliyocheza mchezo wa kujiamia kwa dakika zote tisini iliwachukua dakika 25 kwa timu hiyo kutoka Tanzania visiwani kuandika bao kwanza kwenye mchezo ulioshudiwa na mashabiki wachache. [13]
barua
Alikiri kuwa kwa sasa shirika linakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano kama vile simu za mikononi, ‘intaneti’, na hata kampuni binafsi kusafirisha vifurushi na barua. [14]
basi
MWINJILISTI wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Tusimsahau Manoza amewataka Watanzania kuendelea kuiombea nchi amani kwa kuwa kama Mungu asingelinusuru taifa mwaka jaja basi kungelitokea machafuko makubwa. [15]
bega
Sudan ambayo imekuwa bega kwa bega na balozi wao mjini hapa, ilitoa suluhu na Kenya katika mechi ya awali kwenye uwanja wa Bugembe mjini Jinja ambako ni kilomita 80 toka Kampala ilipo Taifa Stars. [16]
bei
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(Ewura) imetoa mwongoza unaotaka kiwango cha juu cha bei ya mafuta kuwa Sh1,166 kwa lita ya Petroli na Sh1,271 kwa lita ya dizeli. [17]
benchi
Jopo la Stars lililoko mjini hapa halikuweza kusema sababu maalum ya kuchelewa, lakini benchi la ufundi lilidai kwamba lilikuwa likifanya maandalizi ya kina. [18]
bendi
Vaticani City Sinza ilikuwepo bendi ya Akudo Impact wazee wa masauti ikikonga nyoyo za washeherekeaji wa kuuaga mwaka na kukaribisha mpya, wakiwa pamoja na kundi zima la Original Komedi. [19]
bila
Mohammed alilaumu hotuba ya rais kwa kulifumbia macho suala la ajira kwa Watanzania na kuamua kubaki bubu bila ya kuzungumza chochote kuhusu ahadi hiyo, jambo ambalo alilielezea kuwa ni usaliti kwa wapiga kura. [20]
bora
Nilidhani kuwa rais atasema kuwa ataendelea kusimamia haki na utawala bora katika vitu ambavyo vinalegalega, lakini anatoa vitisho. [21]
budi
Wilaya haina budi kufanya utafiti wa kina wa tatizo la matokeo mabaya kabla ya kuanza kuadhibu watumishi bila ya hata kujua nani hasa alihusika. [22]
cha
Naye Gedius Rwiza anaripoti kuwa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kimeelezea kushangazwa kwake na kauli ya Rais Kikwete ya kuonya dhidi ya wanasiasa na vikundi vya kijamii vitakavyojihusisha na kuchochea ghasia. [23]
chanzo
Haiwezekani kila mara wawe chanzo au wahusishwe na vurugu. [24]
chuki
Hata hivyo, nadhani badala ya kuendelea kuwalaumu na kujenga chuki dhidi yao, tuwaombe viongozi wa manispaa na jiji la Dar es Salaam kwa ujumla na wale wote wanaosimamia ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba mgambo wanapata mafunzo thabiti ya kazi zao. [25]
dili
Alianza kwa kusema: "Jamani mnasikia kuwa sasa hivi albino sio 'dili' tena?" Tukaguna basi akatuuliza mnaguna nini na kusisitiza akitumia maneno ya mjini siku hizi: "habari ndiyo hiyo. [26]
dini
WACHUNGAJI wa madhehebu mbalimbali ya dini za kikristo wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kuendelea kuwashughulikia mafisadi bila woga wala kumtazama mtu machoni na kuwamaliza. [27]
dola
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Minde alisema kulingana na makadirio yaliyowahi kufanywa miaka ya nyuma, shirika hilo linatakiwa mtaji wa dola za Marekani 30 milioni na linadaiwa zaidi ya Sh8bilioni kwa ajili ya kulipa pensheni za wafanyakazi. [28]
elfu
RAIS wa shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Leodegar Tenga amekutana na wachezaji wa Kilimanjaro Stars kuwaidi kuwapa fedha zote zawadi dola elfu 30 watapochukua ubingwa wa Kombe la Chalenji. [29]
elimu
Haya yote yalitokana na tabia waliyoonyesha kiasi cha wananchi wa kawaida kabisa kuhoji uwezo, elimu na busara zao katika utendaji wao wa kazi. [30]
email
Binafsi kwa wale wote walionikumbuka kwa mwaka mzima iwe ni kwa email, barua, kwa kupigia simu, kunitumia meseji ama hata hao walio nibip nikapata hisia kuwa walikuwa wananifikiria na wananikumbuka kwa namna moja ama nyingine imenionyesha wanajali kiasi kama hicho, naomba niseme ahsanteni sana. [31]
endapo
Aliongeza Tenga kuwa endapo tutatolewa mapema na kushindi kupata ubingwa huu itakuwa ni aibu kwetu kwa sababu Watanzania wanategemea kupewa zawadi ya mwaka mpya kwa kutwaa ubingwa huu. [32]
eneo
Katika kusisitiza juu ya upandaji miti, Rais Kikwete aliwataka viongozi wa manipaa kuwa na mpango wa kuotesha miti inayofanana kulingana na uchaguzi wa maeneo kuliko hali ilivyo sasa ambapo miti tofauti tofauti inaweza kuonekana katika eneo moja hivyo jiji kutokuwa na mandhari nzuri. [33]
es
Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, kiongozi wa upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohammed (Mbunge) alisema, Rais hakupaswa kutoa kauli hiyo kwa kuwa ni jambo la kawaida katika nchi yoyote kutokea vurugu. [34]
eti
Nani atakayekupiga eti kwa sababu tu umevaa fulana ya chama cha MDC (chama kikuu cha upinzani Zimbawe - Movement for Democratic Change) na ukahudhuria mkutano wao. [35]
fujo
Siku hizi huwezi kusikia watu wakizungumzia mambo ya siasa, nadhani tumeona picha za waathirika wa fujo kwenye maeneo ya vijijini, kwa hiyo hakuna anayependa kuishia kwenye hali hiyo. [36]
fursa
Kwa vile posta ni shirika la umma na linajiendesha katika mazingira ya bila mtaji wa kutosha, alisema wadau wanapaswa kupewa fursa ya kujadili namna ya kukabiliana na changamoto hiyo ili kulinusuru shirika. [37]
gani
Hii ni amani tu, sijui alikuwa anataka kiashiria gani rais wetu?" alihoji Mohammed. [38]
gari
Mtapendekezaje kwamba sisi tupewe tuzo ya tako kwa kuthamini gari kuliko kompyuta. [39]
gazeti
Mwongozo huo wa Ewura unaeleza kuwa bei hiyo inatakiwa kuanza kutumika mara baada ya kutangazwa katika gazeti la serikali. [40]
hadhi
Wapo walionaswa wakiwapiga wananchi viboko hadharani bila hata ya kujali umri na hadhi yao katika jamii. [41]
hai
Naona watu kama hawa hawafai kuachwa hai. [42]
haja
Alisema katika kitabu cha zaburi 31 neno la Mungu linaeleza waziwazi kuwa nimekukimbilia wewe ili nisiaibike milele, hivyo ni vema wananchi wakamkimbilia Mungu ili waweze kusitiriwa haja zao kwani wakiwekwa huru watakuwa huru kwelikweli. [43]
hali
Masebu alisema baada ya uchambuzi wa kina na wa hali ya juu wa maoni yote ya wadau na baada ya kuchambua umuhimu wa kulinda maslahi ya watumiaji, bila kusababisha hasara kwa watoa huduma, Ewura imejiridhisha kuwa kuna kila sababu ya kutayarisha nyenzo muhimu za kuingilia kati kudhibiti mwenendo wa bei za mafuta wakati wowote itakapohitajika. [44]
hana
Haina maana kuwa mwekezaji mpya akija hapa nchini mwananchi wa kawaida hana haki ya kuishi katika eneo hilo, vitendo kama hivi ni uvunjaji wa haki za binadamu. [45]
hao
Wastaafu hao mpaka sasa wameshafanya matukio makubwa manne. [46]
hapa
Baada ya kufanya uhakiki huo kama madai hayo yatakuwa hayajawa tayari na mimi nasema tusije kulaumiana maana hapa naona ni kama mchezo wa paka na panya," alisema Mukoba. [47]
hasa
Pamoja na hali hiyo alisema kuwa shirika la posta likipata mtaji linaweza kujiendesha vizuri kwa faida kwa sababu bado lina fursa nyingi za kibiashara na hasa ikizingatiwa kubwa ndio lenye mtandao mkubwa nchini. [48]
hata
Alifafanua kwamba kwa kawaida zinapotolewa kauli za vitisho kama hivyo, Watananzania hufikiria kuwa ni wapinzani tu ndio walengwa, lakini ukweli ni kwamba hata chama tawala husababisha vurugu katika baadhi ya maeneo. [49]
hatia
Kitendo cha jeshi la polisi kutumika vibaya katika uchaguzi huo ni ishara kuwa, jeshi hili linatumika kisiasa zaidi kwa kupendelea watu fulani, hadi kupelekea kuvunja haki za kibinadamu kwa kuwamwagia maji ya pilipili na kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia," anasema Profesa Maina. [50]
hawa
Bila ya kupambana na uhalifu, wananchi watakosa amani kwani usalama wao na mali zao vitakuwa rehani, lakini sasa wanachokifanya hawa mgambo kukamata watu ovyo na kuwapiga hakiwezi kuungwa mkono. [51]
haya
Tuyatumie mashindano haya kwa umakini pia tunatakiwa kuthibisha mbele ya umma wa Watanzania na wapenda soka barani Afrika kuwa kufuzu kwetu kwa fainali za CHAN haikuwa bahati. [52]
hekima
Mimi nilidhani nguvu inatokana na hekima na maarifa ya yanayosemwa. [53]
hekta
Alisema kabla ya wilaya hiyo haijagawanywa na kuwa na majimbo mawili ya uchaguzi, aliwahi kufanya jitihada za kupigania ardhi kwa kuomba hekta 50 kutoka katika mashamba yaliyokuwa yakilimikiwa na mfanyabiashara Chavda. [54]
hicho
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinadai kuwa wajumbe wa tume hiyo, walianza mjadala wa rufaa hiyo mara baada ya kuwasili hotelini hapo saa 4:00 na kwamba, kulikuwa na mvutano mkubwa hadi majira ya saa 7:00 usiku wa kuamkia jana. [55]
hii
Dar es Salaam leo hii haina mahali ambapo panavutia mtu. [56]
hiki
Kitendo hiki kinaashiria kuwa baadhi ya wawekezaji hawa hawana sifa kwani wanapaswa kuwa na teknolojia ya kisasa na uwezo wa kifedha kuendesha shirika kubwa kama hilo. [57]
hili
Haa'! jamaani nini tena hii Mungu aonyeshe muujuza wake leo; sisi tuko kwenye maombi ya kuliombea taifa pamoja na vitendo viovu vya mauaji ya albino, leo mtu anakuja kufanya uharamia huo ndani ya kundi hili linalokesha kwa ajili ya kumuomba Mungu," alishangaa mshiriki mmoja na kuanza kumuomba Mungu asaidie kuepusha balaa hilo. [58]
hivi
Kama unavyojua hivi sasa suala letu linashughulikiwa na Kamanda (wa kanda maalum ya Dar es salaam, Suleiman) Kova ametuahidi kuwa atalifikisha sehemu husika na atatupatia jibu. [59]
hizi
Nyenzo zote hizi zimelenga kuiwezesha Ewura kama mdhibiti, kuingilia na kudhibiti bei wakati wowote itakavyohitajika kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu 17 cha Sheria ya Ewura," alisema Masebu. [60]
hoja
Akijibu hoja hoja hiyo mwendesha mashtaka wa serikali (PP) wakili wa serikali, Fredrick Manyanda aliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Hezron Mwankenja kuwa upelelezi dhidi ya Mgonja ulikuwa bado haujakamilika,na kwamba baadaye wanaweza kuunganishwa. [61]
huko
Utetezi mwingine unaoweza kutumiwa na mlalamikiwa ni pamoja na kama itatokea mlalamikaji mwenyewe kuwa ndiye chanzo cha kufungiwa kwake huko, yaani kifungo cha kujitakia, hii inafanana na msemo wa Kiswahili kwamba 'mwenye kilanga haliliwi' hivyo hana wa kumbebesha lawama kwa kuwa ni yeye ndiye aliyesababisha kufungiwa kwake. [62]
huku
Mjumbe wa Jumuiya hiyo, Ramadhani Makingi alisema kuwa licha ya Rais Kikwete kutoa onyo kwa wanasiasa na vikundi vya kijamii dhidi ya ghasia, hawatakubali kuona haki yao inapotea kwani hadi sasa hawajalipwa mafao yao huku serikali ikiwa imeshatoa tamko kuwa zoezi la malipo hayo limeshafanyika. [63]
huo
Aidha alisema kuwa, pamoja na kauli hiyo wanategemea kufanya mkutano mkuu mwishoni mwa mwezi huu, kufanya majumuisho ya mwenendo mzima wa ulipaji wa madai ya walimu na kuongeza kuwa baada ya kufanya uhakiki huo watatoa tamko dhidi ya serikali. [64]
huwa
Kila mwaka ifikapo Januari mosi, maneno mengi husemwa kuhusu kampeni hiyo ya upandaji miti inavyoendelea, lakini baada ya tarehe hiyo kupita, na maneno hayo hupotea hadi Januari mosi nyingine au tarehe nyingine ambayo mkoa huwa umejipangia. [65]
huyo
Hata hivyo, washiriki hao walishusha pumzi baada ya mshereheshaji kutoa ufafanuzi kuwa taarifa hizo zilikuwa zimekosewa na kufafanuwa kuwa mtoto huyo alikuwa na dada yake na kwamba mama yao alikuwa anamtaka dada yake ampelekee. [66]
huyu
Nafuu nyingine anayoweza kujipatia mtu huyu ni kufungua kesi ya madai dhidi ya wote waliofungua au kusababisha kifungo hicho na mwisho, katika mazingira fulani ya kisheria, mtu aliyefungiwa isivyo halali anaweza kupata nafuu kwa msaada wa mahakama kutoa hati maalum ya kisheria ijulikanayo kama 'Habeas Corpus' kuamuru kuachiwa wakati au kupisha hatua nyingine za kimahakama kuendelea ili kuthibitisha au kutengua uhalali wa kifungo chake hicho. [67]
ibaki
Kwa ukatili huu, napenda hii adhabu ya kifo ibaki pale pale kwani ni wa hali ya juu, unaoumiza wanaoathirika kwa kiwango kikubwa, kwa lugha nyepesi umepitiliza na ni unyama. [68]
ile
Baadhi ya waandishi tuliokuwapo pale, tulimtafuta kiongozi wa operesheni ile kujua kulikoni lakini alikataa katakata kulizungumzia suala hilo, na badala yake alitoa amri kwa askari wake akiwataka wapande katika karandinga lao pamoja na watu ambao waliwakamata wakidai kuwa ni wahalifu. [69]
ili
Alisema kuwa licha ya rais Kikwete kutoa onyo kwa wanaochochea vurugu, wapo watu wanaodai haki zao kwa hiyo serikali inatakiwa iwaangalie na sio kuwatisha ili washindwe kudai haki zao, akisema vitisho ni kinyume na sheria za haki za binadamu. [70]
iliyo
KENYA iliyo na wachezaji wanne wa timu ya Yanga ya Dar es Salaam, leo ina kazi ngumu itakapopambana na Zambia kwenye moja ya mechi za kombe la Challengi Jijini hapa. [71]
imekuwa
Ni kweli serikali imekuwa ikiahidi lakini hakuna utekelezaji. [72]
ina
Hii ina maana shirika linajiendesha katika mazingira magumu. [73]
ingawa
Kocha wa Kenya, Francis Kimanzi ingawa amekuwa mgumu kuzungumza na vyombo vya habari, wachezaji wake wamesema kwamba wanachotaka ni ushindi tu. [74]
iwe
Isiwe kwa wapinzani tu, sheria lazima iwe msumeno kwa kila mtu. [75]
jimbo
Kwa mujibu wa Bendera serikali inashindwa kutekeleza ahadi yake kwa sababu wakati huo ilikuwa inahusu kero ya jimbo moja lakini baada ya kuongezeka kwa jimbo lingine, sasa imekuwa kero ya majimbo mawili. [76]
jinai
KATIKA makala zilizotangulia tulijadili juu ya haki ya asili ya binadamu kuwa huru na jinsi inavyoweza kuingiliwa na utendaji au utekelezaji wa sheria ya jinai kimakosa. [77]
jinsi
Lakini kwa vile wametulazimisha hatuna jinsi lazima tucheze mpira lolote litakalotokea litokee, hakuna jinsi. [78]
joto
MAMBO yanazidi kuwa magumu katika mchakato wa uchaguzi mdogo wa mbunge Mbeya Vijijini baada ya kuzidi kwa matukio yanayopandisha joto zaidi la kisiasa mkoani Mbeya na hata maeneo mengine ya nchi. [79]
juhudi
Alilielezea shirika kuwa lina uhusiano mazuri na mashirika mengine ya posta duniani, lakini kama juhudi za kulijengea uwezo hazitafanyika, litashindwa kutekeleza kazi za washirika wake kikamilifu na kusababisha kuvunja uhusiano na kutoa nafasi hiyo kwa makampuni binafsi. [80]
juu
Julai 26 na Septemba 4 mwaka jana waliandamana mpaka Ikulu, Oktoba 17 walijazana nje ya ofisi za Wizara ya Fedha na Uchumi kwa nia ya kuzungumza na Naibu Waziri wa Wizara hiyo juu ya mafao yao. [81]
kampeni
Aidha tume hiyo imeagiza wagombea hao wasiendelee na mikutano ya kampeni za uchaguzi, ikibatilisha uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Juliana Malange, ambaye aliwaruhusu kufanya kampeni wakati wakisubiri majibu ya rufaa zao. [82]
kasi
Kikosi hicho cha Sudan katika mchezo uliopita kilionyesha udhaifu kweye safu ya kiungo na ushambuliaji, lakini wachezaji wake wana kasi kuliko timu iliyozoweleka. [83]
kati
Kiwango hicho ni cha chini kulinganisha na bei ya sasa ambayo ni kati ya Sh1,400 na 1,600 kwa lita moja ya petroli na kati ya Sh1,300 na Sh1,400 kwa lita moja ya dizeli. [84]
kero
Huu ni mwaka wa Mungu, ni mwaka wa matengenezo ni mwaka wa kunyanyuka, ni vema kila mtu akajiuliza kuwa alikuwa kikwazo katika kitu gani ili aweze kurekebisha badala ya kuendelea kuwa kero kwa wengine," alisema Manoza. [85]
kesi
Ingawa washtakiwa hao wanakuja tena mahakamani hapo kwa ajili ya kesi yao kutajwa, lakini huenda leo Mgonja akafutiwa mashtaka yanayomkabili peke yake na kuunganishwa na mawaziri hao wa zamani. [86]
kiasi
Mramba na Yona kwa pamoja walilazimika kutoa kiasi cha Sh. [87]
kifungo
Mtu anaweza kuwekwa chini ya ulinzi au kifungo kisicho halali kutokana na sababu mbili au zaidi. [88]
kike
Sheria ya Makosa ya Kujamiiana ya mwaka 1998, pamoja na mambo mengine, imelenga kuthibiti unyanyasaji wa kijinsia ukiwemo kuwapa mimba watoto wa kike lakini haijafanikiwa kwa kiwango kilichotarajiwa licha ya ukali wake. [89]
kimya
Katika uchaguzi, matokeo yalikuwa yametolewa kwenye kituo cha kupigia kura, kwa hiyo nimetulia kimya nikijua kwamba kulikuwa na ucheleweshaji wa makusudi wakati tayari matokeo hayo yalikuwa yakijulikana wazi. [90]
kingine
Utafiti huo umebaini kuwa chanzo kingine cha mimba za utotoni ni ngoma za usiku. [91]
kituo
Nakumbuka aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yussuf Makamba aliwahi kuagiza hatua kali za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya mgambo walimtandika mkazi mmoja wa jiji na tukio hilo kuripotiwa katika kituo kimoja cha televisheni. [92]
kocha
Hali hiyo ya kuchelewa kwa Stars imeonekana kuwachanganya wapinzani wake lakini Somalia kupitia kocha wake imedai kwamba haina mchecheto itafanya kazi ndani ya dakika tisini. [93]
koo
Na kama desturi ilivyo, mwenye pendekezo lazima alainishe koo za waishiwa, pamoja na kutoa posho la tako (si tuzo la tako). [94]
kosa
Akiongea baada ya kutoka kuhojiwa, Shitambala alisema kuwa alipata nafasi ya kutoa maelezo mengi kulingana na kosa lililosababisha aenguliwe katika uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na sheria inavyoelekeza katika masuala ya utoaji wa kiapo. [95]
kote
Alisema mauaji hayo yanaondoa heshima ya nchi na tafsiri iliyoenea kote duniani kuwa Tanzania ni nchi ya amani na kuwataka Watazania kwa kushirikiana na serikali pamoja na mashirika mbalimbali ya kupiga vita vitendo hivyo kwa nguvu zote. [96]
kufoka
Bila hata kutoa tuzo ya tume kwa ajili yetu, alianza kufoka moja kwa moja. [97]
kuimba
Mgambo wamewekwa kwenye vizuizi barabarani na katikati ya jiji wakisimamisha ovyo magari na kuwataka abiria kuimba na kukariri tamko hilo. [98]
kuja
Hata leo hii tuseme mtu anataka kuja kupumzika Dar es Salaam, hakuna sehemu ya kuvutia. [99]
kukidhi
Alisema kwa upande wake, serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Chakula iliahidi kutoa hekta 4000 za ardhi ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa eneo hilo. [100]
kula
Siku nyingine nilitamani kula tambi, nikidhani ni bei nafuu na kwamba ningeweza kununua. [101]
kulijua
Watafiti wanasema huwezi kutatua tatizo kabla ya kulijua. [102]
kuondoa
Nchi nyingi hivi sasa zipo katika mchakato ya kuondoa adhabu ya kifo lakini kutokana na hili la maalbino naomba serikali kwa sasa isitishe mpango huo wa kuondoa adhabu hiyo hadi hapo hali itakapotulia. [103]
kuu
Taarifa hiyo iliyoibuia na kuvuta hisia za umati wa watu waliokuwapo uwanjani hapo, ikiwa ni pamoja na meza kuu iliyokuwa ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Abass Kandoro aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete, ilitangazwa na mshereheshaji wa mkesha huo, James Mwang'ambe. [104]
kuuaga
Kumbi mbalimbali za burudani zilifulika watu katika hekaheka za kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya huku kuwa na matukio ya kufurahisha na kuburudisha. [105]
kuwakamata
Pamoja na vikwazo vyote hivyo vinavyochangia wasichana kukosa elimu kutokana na kupata mimba, utafiti umeonyesha kwamba, jitihada za kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wahalifu wa vitendo hivyo zinakwamishwa. [106]
kwangu
Wakati naendelea kufikiria kile nilichokisema, nilitambua kwamba nimekuwa sawa na watu ninaowalaumu kwa nguvu zetu zote, kwa chuki zote, kutokuvumilia changamoto kwangu na kuona fujo kama ndiyo suluhisho la kutatua matatizo. [107]
kwao
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye hoter ya Avys ipoweka kambi timu Kill Boys rais huyo wa TFF alisema hadi yake kwao watapofanikiwa kurudi na ubingwa nyumbani fedha zote dola elfu 30 watagawana wao wachezaji na mwalimu. [108]
kwenu
Na kwa maana hiyo naomba nichukue fursa hii tena kuwashukuru wasomaji wote wa makala zangu na zaidi niseme ni fahari iliyoje kupata kusikia kutoka kwenu. [109]
ladha
Hii inaharibu ladha ya mchezo na mpira hauendi inavyopaswa ndio maana unaona wachezaji wangu wameamua kutumia uzoefu wa mitaani. [110]
leo
Kuahirishwa kutangazwa kwa matokeo ya rufaa ya mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Sambwee Shitambala, hadi leo asubuhi, kumelimepandisha joto kwenye kinyang'anyiro cha kuziba nafasi iliyoachwa na mbunge wa CCM, Richard Nyaulawa. [111]
lina
Alilielezea jiji la Dar es Salaam kuwa lina maeneo mengi ya kuvutia ambayo hayajaendelezwa kama vile fukwe za Coco na Oysterbay. [112]
maduka
Wafanyabiashara wengi hasa wa maduka katika maeneo hayo yaliyovamiwa hawakusalimika. [113]
maji
Mbali ya maduka hayo pia mgambo hao waliingia katika majumba ya watu, niliwashuhudia wakiwapiga watu bila hata ya kuuliza, wakimwaga maji yaliyokuwa yamehifadhi katika ndoo na kuzichukua. [114]
mali
Mwaka 2007 wachungaji hao walifanya maombi kwenye uwanja huo kuomba Mungu kulinusuru taifa na watu wachache wanaojilimbikizia mali kinyume na utaratibu na kulisababishia taifa umasikini. [115]
mambo
Alisema mwaka 2009 Mungu anataka kuwaonyesha watanzania mambo yaliyo mema kama watakuwa ni watu wa kuzingatia haki, rehema na kwenda kwa unyenyekevu. [116]
maoni
Alisema mamlaka imechambua maoni ya wadau wote kwa makini na kwa kulinda maslahi ya watumiaji, watoa huduma na serikali. [117]
masoko
Serikali pia inapaswa kuhakikisha uwepo wa masoko kwa ajili ya mazao ya wakulima vijijini. [118]
matendo
Hisia hizi za wasiwasi zimekuwa zikizidi kila siku kufuatia matendo yanayofanywa na askari hawa ambao wengi wao ni vijana ambao kwa hali ilivyo inaonekana wanmekosa moyo wa ubinadamu. [119]
mazao
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake Betty Mkwasa, ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Mbunge wa Korogwe Mjini, Joel Bendera, alisema hali hiyo imesababisha wenyeji, kukosa ardhi kwa ajili ya kilimo cha kawaida cha mazao ya chakula la biashara. [120]
mbali
Nataka nitumie vyema nafasi, kipaji na umri wangu nipate nafasi ya kucheza soka mbali zaidi ya Afrika,î alisema mchezaji huyo mwenye miaka 19 anayesoma kwenye shule ya St. [121]
mbaya
Kwegyir, ambaye ni mlemavu wa ngozi na mwakilishi wa watu wenye ulemavu huo bungeni, alisema hali bado ni mbaya kwa albino kutokana na kuendelea kuwepo kwa watu wenye imani potofu wanaowawinda ili wachukue viungo vyao ambavyo inadaiwa vinatajirisha. [122]
mbinu
Bendera ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni, alisema hali hiyo inachangiwa wawakilishi wa wananchi bungeni, kutokuwa makini na kukosa mbinu za kuisaidia jamii. [123]
mema
Aliwaomba viongozi wa dini kwa kushirikiana na waamini wenye mapenzi mema kumuomba Mungu mara kwa mara kwa ajili hiyo ili kukomesha vitendo hivyo vinavyowafanya watu hao kuishi kwa mashaka kama hii siyo nchi yao. [124]
mfano
Alitoa mfano wa nchi kama Newsland ilifanikiwa kuimarisha shirika lake la Posta kupitia mijadala ya kitaifa baada ya kaathirika vibaya na teknolojia mpya za mawasiliano pamoja na utandawazi. [125]
mikoa
Burudani imeonyesha kuwa ni eneo kubwa lililoteka hisia za wengi katika sherehe za kuuaga mwaka na kukarisha mwaka, kwani kumbi zote za jiji hili pamoja na mikoa yake zilifurika watu waliofika kwa ajili ya kujipongeza wakiwa na ndugu na jamaa. [126]
mimba
TATIZO la mimba kwa wasichana wadogo limekuwa likiongezeka nchini licha ya jitihada zinazofanywa kisheria na kimaadili kupambana nalo. [127]
mjini
Hayo walisemwa na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Korogwe,kilichofanyika juzi mjini hapa. [128]
mke
Katika Wilaya ya Tandahimba, Lindi kwa mfano, imebainika kwamba baada ya mavuno wanaume huwapa wanawake talaka kitu ambacho kinajulikana kama "kusafisha ghala," mke mpya huingizwa na yule wa zamani kufukuzwa. [129]
mkia
JUZI mkuu wa wilaya ya Korogwe alizuia likizo ya ofisa elimu wake na kutishia kumchukulia hatua za kinidhamu kutokana na wilaya hiyo kushika mkia katika matokeo ya darasa la saba. [130]
mkoa
Mwongozo uliotolewa na EWURA umetaka kila mkoa kuuza mafuta kwa mujibu wa bei hizo na kwamba, mafuta yatatakiwa kushuka kwa kufuata mwongozo huo wa kila mkoa. [131]
mosi
Shamsa Mangunga alisema kuwa baada ya uzindizi huo ambao hufanyika Januari mosi kila mwaka, kila mkoa umejipangia siku maalumu ya kuotesha miti kulingana na majira ya mvua katika maeneo yao. [132]
mujibu
Kwa mujibu wa mwongozo huo, bei ya mafuta kwa Jiji la Dar es Salaam inatakiwa kuwa Sh1,166 kwa lita moja ya petroli na Sh 1,249 kwa lita moja ya dizeli. [133]
muziki
Baadhi ya mashabiki wa muziki huo walisema wameamua kujiunga na kupanda jahazi kwa kuukaribisha mwaka wakiwa pamoja na kundi hilo maridadi jijini hapa. [134]
mwa
Lakini kauli yake haijawa nzuri masikioni mwa wanasiasa ambao wanaona kuwa mwaka 2008 ulitawaliwa na vitendo vingi vya kudai haki, ikiwemo migomo na vurugu, wakisema vinathibitisha kuwa nchi haikuwa tulivu kama Rais Kikwete alivyoeleza. [135]
mwanamke
Sheria ya Makosa ya Kujamiiana (Sospa) ya mwaka 1998, uamuzi wa mwanamke kufanya mapenzi unaanzia miaka 18 na kuendelea. [136]
mwema
Hakuna mwananchi mwenye kupenda maadili, yaani raia mwema ambaye anaweza kupinga jitihada za kusaka wahalifu, hata siku moja. [137]
na
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa onyo kali dhidi ya wanaojihusisha na kuchochea ghasia nchini, akisema "tusije tukalaumiana," wanasiasa wamejibu wakisema kauli hiyo si sahihi na ni ya vitisho ambavyo haviwezi kuwazuia kufanya kazi zao. [138]
naamini
Lakini naamini kwamba mgambo wengi ama hawajapatiwa elimu ya au wanalewa majukumu yao ndiyo sababu wamekuwa wakishiriki katika vitendo vingi vya udhalilishaji na ukiukaji wa haki za binadamu. [139]
nalo
Kwa mfano, uzembe wa kutokujua au kuzingatia aina ya kosa analoshtakiwa nalo mtu, kwa mfano, kumweka mtu ndani kwa kosa ambalo kimsingi sio la jinai. [140]
namna
Alisema njia hizo ni pamoja na inayoshirikisha utayarishaji na upitishaji wa njia ya kukokotoa bei pamoja na upitishaji wa kanuni za Ewura za mwaka 2008 za namna ya kupanga bei. [141]
nao
Siku moja usiku wa manane, benki yangu ilinijulisha kuwa nimepoteza utrionea niliokuwa nao. [142]
ndefu
Walisema baada ya safari ndefu ya siku 360 za pilika pilika, kukamilika na kuanza safari zingine ni lazima kwa mtu kujipongeza kwa kuvuka mabonde na milima ya mwaka mzima. [143]
ndiyo
Pia wametuhoji kuwa wamesikia kwamba tulifanya mkutano wa kampeni, tukamjibu ndiyo kwa kuwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Mbeya Vijijini alituruhusu kuendelea na kampeni," alisema na kuongeza kuwa maamuzi hayo yalikuwa sahihi. [144]
ndoa
Utafiti umeonyesha kwamba, ngoma hizi zinachangia kwa kiasi kikubwa mimba, ndoa za utotoni na maambukizi ya virusi vya ukimwi. [145]
ndogo
HIVI karibuni niliwashuhudia askari wa mgambo wakivamia nyumba za baadhi ya wakazi tu wa Uwanja wa Ndege kwa madai kuwa wanasaka wafanyabishara ndogo ndogo maarufu kwa jina la wamachinga. [146]
ngumu
Kazi tuliyonayo hapa ni ngumu sana kila timu inataka hili kombe na sisi ni wenyeji tunapaswa kufanya kitu kuonyesha utofauti. [147]
niaba
Akitoa slaamu za mwaka mpya kwenye umati wa watu waliokuwa uwanjani hapo kwa niaba ya Rais Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abass Kandoro, aliwataka viongozi wa dini kuendelea kuisaidia serikali katika kuhakikisha amani na utulivu uliopo hapa nchini unadumishwa. [148]
nini
Nashindwa kuelewa nini mnachojadili kwenye vikao vyenu. [149]
nipo
Mimi hii ndio mashindano yangu ya kuionyesha Afrika kwamba nipo na ninafanya kazi kikamili. [150]
njia
Masebu alisema, Ewura imefikia maamuzi hayo baada ya mamlaka kupendekeza njia ya kudhibiti bei ya mafuta ya petroli na bidhaa zake. [151]
nne
Tulipanga matembezi zaidi ya mara nne tumezuiwa na polisi; tumefukuzwa kutumia uwanja wa Mnazi Mmoja; tumedai malipo yetu tukaambiwa kuwa hatukuwa wafanyakazi wa EAC bali tulikuwa vibarua; wastaafu wengine wanakufa kila siku, lakini hakuna msaada wowote tunaopata. [152]
nyinyi
Ni nyinyi wazee mnaohitaji picha za ngono. [153]
ona
Lakini ona Wakorea sasa na hakuna ambaye atatambia saa za Kikorea. [154]
papo
Lakini kompyuta zinadai maamuzi ya papo kwa papo. [155]
pia
Wote ni mashuhuda na mmeona matokeo yake Mungu amejibu," alisema Mchungaji Godfrey Emmanuel ambaye pia ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa mkesha huo. [156]
pili
Akizungumza na wachezaji Kilimanjaro Stars, Tenga alisema kuwa kuna mambo matatu ambayo angependa kuwaambia kwanza ni nidhamu,pili, mcheze vizuri na ushindi, mwisho wasigombane na waamuzi. [157]
saa
Awali ilitaarifiwa kuwa uamuzi wa rufaa ya Shitambala, ambaye alienguliwa kugombea ubunge wa Mbeya Vijijini kwa kuapa kwa wakili badala ya hakimu, ingetolewa jana saa 4:00 asubuhi. [158]
sana
Fedha zisipopatikana na shirika likaboresha huduma, litajikuta katika wakati mgumu sana miaka michache ijayo," alisema Minde ambaye alistaafu kazi Januari mwaka jana. [159]
sera
Aidha walikemea vyama vya siasa kufanya kampeni za matusi wakieleza vinalifedhehesha taifa na kwamba wanasiasa wanapaswa kutambua jamii imechoshwa na hali hiyo na kuvitaka vyama hivyo kufanya kampeni kwa kunadi sera zake. [160]
shaka
Hatua ya mgambo hao ya kuingia katika majumba ya watu na kufanya watakalo bila ya kuwa na hati ya upekuzi (search warrant), ambayo hutolewa na polisi, kinatia shaka ujuzi wao na utekelezaji wa kazi zao kwa kufuata maadili. [161]
sio
Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema wameipokea kwa mshangao kauli hiyo, kwa sababu rais wa nchi anapozungumzia migomo, anajumuisha walimu ambao wamekuwa wakidai haki zao na sio kuchochea migomo. [162]
sote
Naamini kwa kufanya hivyo, watabadilika na kusaidia katika utoaji wa elimu kwa wakazi wa jiji kuhusu haki na wajibu wao, ili sote tufurahia matunda ya nchi hii na kuendesha maisha kwa amani na kuheshimiana. [163]
sura
Mkesha huo uliopangiliwa kwa namna yakee pia uliwaombea mawaziri wote wa serikali ya Tanzania na wabunge ili Mungu awawezeshe kufanya kazi kwa manufaa ya wanachi na taifa kwa ujumla badala ya maslahi yao ili kusaidia kubadilisha sura ya Tanzania. [164]
taifa
Rai hiyo imetolewa na wachungaji hao kwenye mkesha maalumu wa kuliombea taifa uliofanyika usiku wa kuamkia jana kwenye uwanja wa zamani wa Taifa jijini Dar es Salaam. [165]
tako
HE jamani, mambo ya nishani ya viatu na tuzo la tako yameleta ubishi mkubwa sana. [166]
tamaa
Hapa tutaangalia hali za kukatisha tamaa na matukio ya kutisha ya mwaka uliotawaliwa na uchaguzi uliokuwa umegubiwa na utata. [167]
tangu
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa washtakiwa hao kukutana mahakamani hapo tangu walipofikishwa na mahakamani hapo na kusomewa mashtaka yanayowakabili. [168]
teke
Hili teke linalotujia wazee limepindua ulimwengu maana sasa ni watoto na vijana wanaojua si sisi wazee. [169]
tena
Inadaiwa kikao hicho kiliendelea tena jana asubuhi hadi saa 9:00 wakati walipowaita wagombea na kuwahoji na kumaliza saa 10:00 jioni. [170]
tu
Alisema sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano na kutiwa saini na rais zipo na kwamba hizo ndizo zinapaswa kutumika kushughulikia wanaosababisha vurugu na si kutoa vitisho tu. [171]
tume
Aliyasema hayo jana majira ya saa 10:00 jioni baada ya wagombea, walioenguliwa na msimamizi wa uchaguzi katika kinayang'anyiro cha ubunge katika Jimbo la Mbeya Vijijini na baadaye kukata rufaa, kuhojiwa na tume yake kwenye hoteli ya Mount Livingstone. [172]
uchumi
ESTHER (siyo jina lake halisi), mtaalam anayeishi na kufanyakazi katika Mji Mkuu wa Zimbabwe, Harare ameandika matukio muhimu ya mwaka 2008 akielezea jinsi anavyopambana na maisha kwenye nchi hiyo ambayo uchumi wake umeanguka vibaya. [173]
uhai
Alisema mauaji ya albino ni jambo lisilokubalika na kuwataka watu kutambua kuwa mali zinatokana na watu kujituma katika kufanya kazi na si kutoa uhai wa mtu mwingine kwa kuwa mwenye uwezo wa kutoa uhai huo ni Mungu pekee. [174]
umri
MAELFU ya watu waliokuwa wamefurika kwenye mkesha wa mwaka mpya ulioandaliwa maalumu kwa ajili ya kuliombea amani taifa uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, juzi walishikwa na butwaa baada ya kutolewa taarifa za kupotea kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino) aliyedaiwa kuwa na umri wa miaka mitatu. [175]
una
Huu si uwanja ni malisho ya ngíombe, huwezi kuwa na uwanja una mabonde kiasi kile halafu mkavu. [176]
ungo
Unaonyesha kwamba jamii nyingi bado zinapinga kitendo cha mtoto wa kike kupata elimu ya kutosha, kwa kuweka vikwazo vingi vya kumfanya asiweze kuhudhuria shule, kuunga mkono tabia ambazo zitamfanya msichana aolewe mapema hasa kwa wale waliomaliza shule za msingi madam wamevunja ungo. [177]
upungufu
Utafiti pia umebaini upungufu mkubwa wa walimu. [178]
utafiti
Ni vizuri matokeo hayo ya utafiti wa wataalam na onyo wanalolitoa likafanyiwa kazi kuendesha kampeni ya kweli ya upandaji miti. [179]
uvunjifu
Ni miaka 60 sasa tangu kuanza maadhimisho ya Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu duniani kote, matendo ya uvunjifu wa haki za kibinadamu yamekuwa yakiongezeka duniani kote. [180]
vituo
Alisema vituo vyote vya mafuta vitatakiwa kuchapisha bei za mafuta zikionekana vizuri na kila mabango yakionyesha bei inayotozwa, punguzo na vivutio vya biashara au promosheni. [181]
wa
Rais Kikwete alitoa onyo hilo juzi wakati wa hotuba yake ya salaam za mwaka mpya alipoonya wale aliowaita wanasiasa hasidi, akisema "tuache vitendo vya kuchochea ghasia kwa kisingizio chochote kile. [182]
waishiwa
Hata hivyo sisi waishiwa tulifaidi sana maana tulikuwa tumeshajiteua kuwa tume ya tuzo. [183]
wake
Tulitegemea kuwa rais angetuambia katika hotuba yake kuwa ndani ya miaka mitatu ya utawala wake amefanikiwa kutoa ajira ngapi kwa Watanzania lakini hakuligusia kabisa. [184]
wameua
Kama itathibitika wameua na wao wauawe. [185]
wanaoathirika
Watoto wa kike ndio wanaoathirika zaidi. [186]
wao
Viongozi waliokuwepo ni madiwani, wenyeviti wa mitaa pamoja na wakurugenzi wa manispaa zote tatu, wakuu wa wilaya, baadhi ya wabunge pamoja na kinara wao, Abbas Kandoro. [187]
watatu
Mkurugenzi wa ufundi na Meneja wa Sudan, Ahmed Babiker alisema jana kwamba wamekuja na wachezaji watatu tu waliokuwa kwenye kikosi kilichofungwa na Taifa Stars. [188]
watoto
Anaongeza kuwa watu 130 hufariki kila mwaka kutokana na mauaji kama haya ambayo hushuhudiwa moja kwa moja na watoto wetu, hivyo kuwajengea tabia mbaya ya kujichukulia sheria mkononi. [189]
wenyewe
Hapa sababu kubwa huwa ni raia wenyewe. [190]
wiki
Kwa sasa, sheria bado haituruhusu kuwataka wauzaji kufuata bei hiyo, lakini baada ya wiki mbili mwanasheria mkuu atakuwa ameshaiweka kwenye gazeti la serikali tayari kwa kuanza kazi," alisema Masebu. [191]
wote
Kwa chama tawala na vyama vya upinzani, yaani wanasiasa wote," alisistiza Mohammed. [192]
yako
Naamini wapo pia wale ambao wamejitoa kwa ajili yako hao nao ni watu ambao ni nyema ukawageukia kuwapa ahsante kwa kuwa mwaka unaoanza utauingia ukiwa mtu mpya. [193]
yao
Walimu waliitisha mgomo nchi nzima wakishinikiza walipwe zaidi ya Sh16 bilioni ikiwa ni malimbikizo ya malipo yao mbalimbali, hata hivyo mgomo huo ulikumbana na vizingiti mbalimbali vya mahakamani, ikiwemo amri isiyo ya kawaida ya kuuzuia mgomo iliyotolewa usiku na jaji wa Mahakama ya Kazi. [194]
yeye
Maana ya tamko au msimamo huu wa sheria ni kwamba ni wajibu wa mwenye kufungiwa au kukimbia kuithibitishia mahakama kuwa kifungo au kizuizi alichowekewa hakikuwa na uhalali wa kisheria kwa kuwa yeye si mhalifu na hahusiki na kosa aliloshtakiwa. [195]
zangu
Ndugu zangu taarifa zlizotufikia hapa zinasema kuna mtoto wa miaka mitatu mwenye ulemavu wa ngozi, amepotea," alisema Mwang'ambe. [196]
zenu
Meseji zenu, email zenu zilinipa nguvu ya kuendelea na kila siku nilikuwa nasema hilo. [197]
zile
Mgambo wanaosimama kwenye vizuizi barabarani na wale wa kwenye kambi sasa wamepungua katika maeneo mengi lakini siyo maeneo yote, mabango yametolewa kwenye mabasi, vijana sasa wanavaa fulana zenye nembo za wanamuziki wa R&B badala ya zile za RG Mugabe. [198]
zima
Baadhi ya kumbi ambazo mwananchi lilifanikiwa kufika ni pamoja na ukumbi wa Dar West Park Tabata Jijini Dar es Salaam ambapo kundi zima la Jahazi Modern Taarabu lilikuwa likitoa burudani ya kusindikiza mwaka na kukaribisha mwaka. [199]
zote
Pia wanaweza kukumbwa na adhabu zote mbili. [200]