Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-01

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


achukue
Haisemi nani achukue hatua, wala kwa vipi. [1]
aina
FUVU la kichwa cha binadamu limekutwa nyumbani kwa mfanya biashara maarufu wa Maili moja mjini Kibaha, Ally Msuya maarufu kwa jina la Puku likiwa limehifadhiwa kwenye ndoo ndogo aina ya Sadolini iliyokuwa na mafuta ya kupikia yanayojulikana kwa jina la samli. [2]
ajira
Profesa Lipumba anasema, serikali iliahidi ajira milioni mbili kwa Watanzania lakini hadi sasa mwaka wa tatu unaondoka huo inaona aibu hata kuzungumzia kipengele hicho. [3]
ama
Katibu wa matajiri hao wa mafuta nchini, Bisarara alisema akiba yao inatosha na kwamba hakuna haja ya wananchi ama serikali kuwa na wasiwasi kwamba bidhaa hiyo inaweza kupungua. [4]
ambaye
Kaimu kamanda wa polisi, Kilongo tukio hilo lilitokea Desemba 30, 2008 na kumtaja aliyeuawa kuwa ni Mwandu Mayala, 40, mkazi wa kijiji cha Ihalo ambaye anadaiwa kuiba mpunga huo mali ya Zakaria Shija. [5]
amekuwa
Kocha huyo aliyeshiriki upangaji wa ratiba hiyo jijini Abidjan, Ivory Coast Alhamisi iliyopita alisema kuwa siku zote amekuwa akiwakumbusha wachezaji wake kucheza kwa kujituma bila ya kuangalia aina ya timu, kitu ambacho anasema wamemwelewa na kuondoa hofu waliyokuwa nayo awali. [6]
ampe
CCM kuwa ni kwa nini asichague moja, yaani "ya Kaisari ampe Kaisari, na ya Mungu ampe Mungu" na akimtuhumu kuwa na urafiki wa karibu na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na wenzake. [7]
ana
Akijitetea kabla ya hukumu hiyo, Kulyama alidai apunguziwe adhabu kwa sababu ana familia inayomtegemea na wazazi na kwamba tayari ameshapoteza kazi, lakini utetezi wake ulitupiliwa mbali na hakimu huyo. [8]
asije
Alisema kuwa kuna watu ambao wamekuwa wakitangaza kuwa Mwinyi asije kufanya uzinduzi wa kampeni na asipofanya hivyo atachafuliwa. [9]
au
Ni ukweli ulio wazi kuwa katika mwaka huu tunaoumaliza sasa baadhi yetu tumekuwa tunafanya vitendo au kutoa kauli ambazo zilikuwa zinalielekeza taifa kubaya," alisema Kikwete. [10]
bado
Baada ya kuangalia kumbukumbu za mahakama Hakimu Kabate alimweleza Rama kuwa upelelezi bado haujakamilika na kumtaka aulize swali lingine. [11]
baina
Yanga ilifungiwa miaka mitatu pamoja na kutozwa faini baada ya kususa mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa baina yake na Simba, Agosti mwaka jana. [12]
bali
Kimsingi siungi mkono si tu kwa sababu Mkapa ni wa kusini bali alivyoliongoza taifa," alisema Athumani akimzungumzia Mkapa ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Lupaso wilayani Masasi. [13]
bao
Zambia iliyoingia katika michuano hiyo kama mwalikwa baada ya Eritrea kujitoa, ilianza kupata bao katika dakika ya 25 lililofungwa na Given Singuluma. [14]
barua
Katibu wa Ujumbe wa watu walikwenda kuwasilisha barua ya madai hayo kwenye Ofisi za Mwakilishi Mkazai Umoja wa Mataifa, Hamad Ali Mussa alisema wanataka kisiwa hicho kiwe na mamlaka yake kama vilivyo visiwa vinavyounda utawala wa Comoro. [15]
basi
Hivyo kama Mzee Mwinyi naye alitenda kosa wakati wa utawala wake, basi atachukuliwa hatua. [16]
bei
Basi mheshimiwa hakimu naomba hela nikanunue soda maana kila siku nasikia soda zimepanda bei lakini mimi sijawahi kunywa,"alisema Rama. [17]
bila
Nilifurahi kumsikia Rais Kikwete akisema hatamshitaki Mkapa, bila shaka aliona mbali. [18]
binafsi
Tena tulikuwa tunafanya hivyo kwa ajili ya kuendeleza manufaa binafsi ya kisiasa. [19]
bora
Lakini, hali ingekuwa bora zaidi kama uchumi wa dunia usingepata misukosuko. [20]
cha
Tumeunda kikosi-kazi kinachojumuisha Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa cha kuendesha mapambano haya," alisema Kikwete. [21]
chake
Alisema mauaji hayo ni ya mateso na hayana sababu ya kwa kuwa chanzo chake ni cha kipuuzi na kwamba wanaoamini kuwa wakipata viungo vya albino watatajirika, waganga na wauaji serikali itawabana. [22]
chuo
Mwezi mmoja baadaye uongozi wa chuo uliwarejesha wanafunzi wote isipokuwa wanafunzi 56 walioesemekana kuwa vinara wa kuwashinikiza wenzao kugoma. [23]
dana
Kwa mujibu wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo wanafunzi hao walitaka kukabidhiwa rasmi hosteli za chuo hicho zilizopo mtaa wa Chole jijini Dar es Salaam ambazo kwa muda mrefu uongozi wa chuo umekuwa ukiwapiga dana dana na kushindwa kuwakabidhi kama yalivyokuwa makubaliano ya awali. [24]
dhahabu
Mramba, waziri mkongwe aliyepata kushika wizara nyeti kwenye serikali za awamu zote nne, na Yona, aliyeshika wizara kwenye serikali za awamu mbili, walipandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kutumia vibaya ofisi kwa kuiruhusu kampuni ya M/S Alex Stewart (Assayers) ya Uingereza kuingia mkataba wa kudhibiti madini ya dhahabu kinyume cha sheria. [25]
dhati
Na hapa ndipo kunapokuja umuhimu wa kuwa na ushirikiano katika taasisi za siasa, hasa vyama vya upinzani kama kweli vinania ya dhati ya kukiondoa CCM madarakani. [26]
dola
Wakati bei ya mafuta ikipanda nchini, hali ni tofauti katika soko la dunia ambako nishati hiyo imeshuka kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita baada ya kupanda kwa kasi hadi kufikia dola 140 za Kimarekani kwa pipa mwezi Julai. [27]
elimu
Mkurugenzi wa vijana wa Chadema, John Mnyika ndiye aliyekuwa wa kwanza kuusisimua umati huo, baada ya kuwataka wananchi hao kumuuliza mgombea wa ubunge wa CCM, Mchungaji Luckson Mwanjali, kiwango chake cha elimu na kuwa ana uwezo gani wa kuwasaidia. [28]
email
Binafsi kwa wale wote walionikumbuka kwa mwaka mzima iwe ni kwa email, barua, kwa kupigia simu, kunitumia meseji ama hata hao walio nibip nikapata hisia kuwa walikuwa wananifikiria na wananikumbuka kwa namna moja ama nyingine imenionyesha wanajali kiasi kama hicho, naomba niseme ahsanteni sana. [29]
endapo
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mbeya, Nawabu Mulla alitoa onyo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari kuwa wabunge wa CCM wagawanyika na kuwa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi atakashifiwa endapo atahudhuria uzinduzi huo. [30]
eneo
Wakiwa wenye utulivu mkubwa, wakiongozwa na nyimbo za kuhamasishana huku wakilindwa na ulinzi mkali wa polisi katika mkutano huo uliofanyika katika kata ya Utengule Usongwe, wakazi wa eneo hilo walionekana kila wakati wakimshangilia mgombea huyo. [31]
es
Wakati fulani wanafunzi wa sekondari waliandamana hadi ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, wakirusha maneno makali dhidi ya serikali, wakidiriki kuiita kuwa ni ya kisanii. [32]
furaha
Tuna furaha kuona wenzetu Zambia wamekubali mwaliko wetu licha ya kualikwa dakika za mwisho baada ya Eritrea kujitoa," alieleza Musonye. [33]
fursa
Mmiliki wa kampuni inayoagiza mafuta ya GBP, Salim Baabde alisema kuwa walifunga ofisi katika kipindi cha sikukuu ili kuwapa wafanyakazi wao fursa ya kusheherekea Krismasi na familia zao. [34]
fuvu
Kwa mujibu wa mashuhuda na majirani walisema kuwa fuvu hilo ambalo lilikuwa limehifadhiwa kwenye kisadolini kidogo lilikuwa limehifadhiwa ndani ya mafuta aina ya Samli ili lisiweze kutoa harufu kali ya uozo ndani ya nyumba hiyo kwa kipindi chote ambacho ililengwa kikae humo. [35]
gani
Baadhi ya vurugu hizo zilihusishwa na vyama vya kisiasa, ingawa havikuwekwa bayana kama ambavyo Rais Kikwete hakuweka bayana vitendo hivyo vya uchochezi vilifanywa na watu gani. [36]
gari
Mtapendekezaje kwamba sisi tupewe tuzo ya tako kwa kuthamini gari kuliko kompyuta. [37]
gumzo
Michuano hiyo inafunguliwa rasmi mjini hapa, mahali ambako gumzo katika mitaa na mabasi ya abiria ni kuhusu mashindano hayo ambayo timu ya Tanzania, Kilimanjaro Stars imekuwa gumzo. [38]
hadhi
Lakini, hali ya uwanja wa michezo wa Bugembe mjini hapa ambako ufunguzi ulifanyika ilizua malalamiko kutoka kwa timu zinazoshiriki michuano hiyo kuwa haufai na hauna hadhi inayolingana na michezo yenyewe. [39]
hakuna
Mwenyekiti huyo pia alisema kuwa Halmashauri ya Kuu ya CCM mkoani Mbeya inakanusha chama hicho kimegawanyika, akisema kuwa, hakuna wabunge waliogawanyika ndani ya chama hicho. [40]
hali
Akizungumzia hali ya uchumi alisema "kwa jumla hali ya uchumi wa nchi yetu kwa mwaka 2008 ilikuwa ya kiwango cha kuridhisha. [41]
halisi
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Haruna Lipumba anasema, ripoti hiyo si sahihi kulingana na hali halisi ya maisha ya Watanzania na kwamba imelenga zaidi katika kupotosha. [42]
hana
Semboja Hajji kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam anasema, hana hakika kuwa takwimu hizo ni sahihi, lakini anasema hata kama ni sahihi hakuna tofauti yoyote kwa kuwa hata katika bajeti zilizopita takwimu hizo za kukua kwa uchumi zilitajwa. [43]
hao
Alisema wakiwa katika harakati za kusafirisha mali hizo, walizingirwa na wananchi wenye hasira kali na wenzao wawili kupigwa vibaya hadi kufa na baadaye kuchomwa moto, wakati washitakiwa hao wawili waliokolewa na polisi na kufikishwa mahakamani kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha. [44]
hapo
Kwa hiyo, ofisi inaandaa utaratibu ili wale waheshimiwa wabunge ambao hawajazipata fomu hizo, sasa wazichukue kutoka Ofisi ya Spika mara moja na kuzirejesha hapo haraka inavyowezekana," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ya Ofisi ya Bunge. [45]
haraka
Taarifa hiyo ilisema kutokana na hali hiyo, ofisi ya Bunge inaandaa utaratibu utakaowezesha wabunge ambao hawajapata fomu hizo kuzipata na kuzirejesha haraka inavyowezekana. [46]
hasa
Naomba Watanzania wenzangu wote na hasa wanasiasa wenzangu tuyatambue hayo na tujiepushe nayo. [47]
hata
Vitendo hivyo havitavumiliwa hata kidogo. [48]
hawana
Semboja anafafanua kuwa, kukua kwa mauzo ya nje nchini Tanzania si jambo la kujisifu kwamba serikali imepiga hatua, kwa sababu bidhaa nyingi zinazouzwa nje ni za kampuni za nje na kwamba Watanzania hawana bidhaa wanazouza nje ya nchi. [49]
hicho
Mgombea wa Chadema, Sambwee Shitambala ameenguliwa kwenye kinyang'anyiro hicho cha kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mbunge wa CCM, Richard Nyaulawa, aliyefariki kwa ugonjwa, lakini amekata rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambayo inatarajiwa kutangaza uamuzi kesho. [50]
hii
Leo hii tukisema wangapi wanamuunga mkono Mkapa tutawapata wengi kuliko wachache wanavyofikiri. [51]
hiki
Nimewaeleza wachezaji wangu wawe makini kwani hiki ni kipimo kikubwa kwao kwa michuano ijayo iliyo mbele yao. [52]
hisia
Mwaka 2008 tumeshuhudia wananchi wakionyesha hisia zao wazi wazi kwa nia mbalimbali, lakini pia tunmeona jinsi serikali ikiwajibika kwa njia moja au nyingine. [53]
hofu
Kitendo cha wamiliki wa vituo vya mafuta kinapaswa kukemewa kwani wanawasababishia wananchi hofu ya maisha. [54]
hoja
Wilbroad Slaa ameahidi kuwasilisha hoja ya kutaka Mkapa, aliyeongoza nchi kwa vipindi viwili (1995-2005), apandishwe kizimbani kujibu tuhuma za kufanya makosa wakati akiwa Ikulu, huku kiongozi wa upinzani Bungeni, Hamad Rashid, akiahidi kuwasilisha hoja ya kutaka kiongozi huyo aondolewe kinga ili aweze kupandishwe kizimbani. [55]
huo
Naomba makundi ya kijamii yatambue ukweli huo na waache kuwaendekeza wanasiasa hasidi. [56]
idadi
Alifafanua kuwa endapo watakuwa wakisaidiana katika maeneo ambayo chama Fulani kinaonekana kuwa na nguvu na chama hicho kikashinda, idadi ya vitu bungeni itahesabiwa kwa chama kimoja kilichoshinda kiti hicho hata kama nyuma yake kulikuwa na mchango mkubwa wa vyama vingine. [57]
ikiwa
Tunaumaliza mwaka nchi ikiwa tulivu. [58]
ile
Alisema wamiliki hao wako chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) na ndiyo waliowapa leseni ya kufanya biashara kama ambavyo mamlaka hiyo ilivyotoa leseni kwa waagizaji hao hivyo bado wana mamlaka ya kuwadhibiti kwa namna yoyote ile ili tatizo la aina hiyo isije ikajitokeza tena. [59]
ili
Ni matumaini yangu kuwa tutajiepusha na mambo hayo katika mwaka 2009. Nawasihi viongozi wenzangu wa kisiasa na wa kijamii tubadilike, tuweke mbele maslahi ya taifa ili tuiepushe nchi yetu na mabalaa ambayo baadhi ya wenzetu yaliwakuta. [60]
ilianza
Awali, Zambia 'Chipolopolo' ilianza vizuri baada ya kuitandika Djibouti mabao 3-0 katika machezo wa ufunguzi uliofanyika katika Uwanja wa Bugembe uliopo, Jinja, kilometa 80 kutoka Kampala. [61]
imara
Bwalya, nahodha wa zamani wa Zambia aliyecheza soka ya kulipwa nchini Ubelgiji , Amerika Kusini, alisema kuwa huo utakuwa mtihani mzuri kwa vijana wake ambao watacheza na timu imara kama Tanzania, Uganda, Sudan, Rwanda na Kenya. [62]
imeanza
Kwa upande wao baadhi ya majirani walisema wameshitushwa na tukio hilo la kishirikina na kwamba wamesikitishwa kwani kutokana na ukaribu wao na mfanyabiashara huyo imani yao imeanza kuondoka kwa kutoaminiana tena katika shughuli zao za kila siku. [63]
inadai
Ripoti hiyo, ambayo imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuchapishwa katika Magazeti ya serikali, inadai kuwa uchumi wa Tanzania ndani ya kipindi cha miaka miatatu ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete unapeta kulingana na viashiria kadhaa ambavyo inavitaja. [64]
iwe
Hakimu Issa Magori alitoa hukumu hiyo kwa mhasibu huyo msaidizi wa zamani wa Jeshi la Polisi, ili iwe fundisho kwa watu wengine wote wanaofikiria kufanya makosa kama hayo. [65]
jijini
WATANI wa jadi, Simba na Yanga wamepangiwa kuchezwa Aprili 19 au 23 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu. [66]
jipya
Kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri Baada ya Waziri Mkuu kujiuzulu, Rais Jakaya Kikwete alilazimika kulivunja baraza lake la mawaziri na baada ya kutafakari kwa kipindi cha zaidi ya wiki moja, hatimaye Rais aliunda Baraza jipya la mawaziri na kumteua Mizengo Peter Pinda kuwa Waziri Mkuu. [67]
juzi
Hakimu magori alitoa hukumu hiyo juzi baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa mahakamani na upande wa mashitaka. [68]
kadhalika
Hali kadhalika kwa rais wetu atakapomaliza muda wake, kama alitenda kosa naye atashitakiwa," alisema Mohammed Omari. [69]
kashfa
Lowassa hakujiuzulu peke yake, bali aliambatana na mawaziri Nazir Karamagi aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini na Dk Ibrahim Msabaha aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki kufuatia kuhusishwa kwao katika kashfa ya Richmond. [70]
kata
Katika tukio jingine, jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa tukio moja la kuuawa mtu mmoja kwa tuhuma za kuiba gunia mbili za mpunga, katika kijiji cha Ihalo kata ya Kwesela wilaya ya Shinyanga. [71]
kawaida
Ni kipindi ambacho kilikuwa na shinikizo, wasiwasi mkubwa nchini, lakini sasa taifa limerudia hali yake kawaida," alisema Rais Kikwete na kuongeza: "Uamuzi ule ulileta mashaka makubwa sana, ulileta mtikisiko nchini. [72]
kazi
Akizungumzia mauaji ya albino Rais Kikwete alisema serikali inaendelea na mapambano kuhakikisha inatokomeza mauaji hayo na kwamba imeunda kikosi kazi kuendesha mapambano hayo. [73]
kiasi
KOCHA wa Taifa Stars, Marcio Maximo amesema kuwa majina ya nchi na historia zao za nyuma hazimpi taAbu kiasi cha kumfanya ashindwe kufanya vizuri wakati wa michuano ya Afrika ya wachezaji wa ligi za ndani(CHAN) iliyopangwa kufanyika Februari mwakani nchini Ivory Coast. [74]
kila
Tutafanya kila tuwezavyo kurekebisha mambo ili huduma hizo ziboreshwe na kuwafanya watumiaji kufurahi. [75]
kile
Tuache vitendo vya kuchochea ghasia kwa kisingizio chochote kile. [76]
kina
Hivi sasa wanaendelea na uchunguzi wa kina nchi nzima kuwatambua wahalifu na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria. [77]
kinga
Wakati shinikizao la kutaka Mkapa aondolewe kinga na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za makosa anayodaiwa kufanya akiwa Ikulu, wabunge na wananchi wa mkoani Mtwara na wananchi kuibuka na kumtetea. [78]
kisha
Kutokana na matusi hayo ukichanganya na kuwa alikuwa amekolea kinywaji Mrema ambaye alikuwa amepandisha hasira alichomoa kisu alichokuwa nacho kisha akamchoma mkono wa kushoto na damu kuanza kuvuja kwa wingi,"kilisema chanzo kimoja. [79]
kiti
Alisema kuwa katika kikao hicho cha halmashauri kilichofanyika jana, wamejipanga kuhakikisha kila mbunge anapangiwa majukumu yake katika kuhakikisha CCM inatetea vizuri kiti hicho kilichoachwa wazi na mbunge wake, Richard Nyaulawa. [80]
kiwe
Zaidi ya wananchi 10,000 wa Kisiwa cha Pemba, wameuomba Umoja wa Mataifa (UN) uilazimishe Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibadili muundo wa sasa wa serikali utakaoruhusu visiwa vya Unguja na Pemba, kila kimoja kiwe na serikali yake. [81]
klabu
Awali, timu zilipangwa kukutana Aprili 12, imesogezwa mbele kwa ajili ya michuano ya timu ya taifa na klabu bingwa Afrika. [82]
kocha
Baada ya mchezo huo, kocha mkuu wa Zambia, Herne Renald alilalamika uwanja wa Bugembe kuwa ni mbovu na mkavu akiulinganisha na ule wa Chuo Kikuu cha Zambia. [83]
kodi
Mara baada ya Uchaguzi mkuu wa 1995 waliokuwa mawaziri wa fedha Simon Mbilinyi na Naibu wake Kilontsi Mporogomyi walilazimika kung'oka kwa kilichodaiwa kutoa misamaha ya kodi. [84]
kombe
Kaijage alizitaja mechi nyingine ambazo huenda zikabadilishwa kuwa ya Moro United na Kagera Sugar ambayo zinatakiwa kucheza Aprili 20, lakini mabadiliko zaidi itategemea kama Yanga itafanikiwa kuingia raundi ya pili na Prisons kushindwa kufanya vizuri katika michuano ya kombe la Shirikisho. [85]
koo
Na kama desturi ilivyo, mwenye pendekezo lazima alainishe koo za waishiwa, pamoja na kutoa posho la tako (si tuzo la tako). [86]
kosa
Hakimu huyo, baada ya kuridhika na ushahidi, alitoa adhabu hiyo ya miaka mitatu jela kwa kila kosa ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaofanya makosa kama hayo. [87]
kuagiza
Aliongeza kuwa moja ya sababu zinazoongeza hofu ya kukosekana kwa mafuta ni hatua ya waagizaji na wamiliki wa vituo vya mafuta nchini kuagiza mafuta kidogo kutokana na bei ya bidhaa hiyo kuyumba. [88]
kucheza
Alisema kuwa kutokana na wachezaji wengi wa Simba na Yanga kuwa katika timu ya Kilimanjaro Stars ambayo inashiriki michuano ya Chalenji inayoendelea Uganda na kuisha Januari 13,mechi za klabu hizo, zilizotakiwa kucheza Januari 10, sasa zitachezwa Januari 21 kwa Simba kucheza na Villa Squad na Yanga itacheza na Prisons mjini Mbeya. [89]
kufikishwa
Tayari watu 91 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani. [90]
kufoka
Bila hata kutoa tuzo ya tume kwa ajili yetu, alianza kufoka moja kwa moja. [91]
kuiunga
KOCHA Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Marcio Maximo amewataka Watanzania kuiunga mkono timu hiyo ambayo imeondoka jana kwenda Uganda kushiriki michuano ya Chalenji ambayo imeanza kutimua vumbi jana. [92]
kujiuzulu
Tukio kubwa kabisa mwaka huu ni lile la kujiuzulu Waziri Mkuu Edward Lowassa. [93]
kukusanya
Serikali ilisema imefanikiwa kukusanya zaidi ya Sh 50 bilioni zilizorejeshwa na watuhumiwa wa ufisadi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT). [94]
kuleta
Alisema kutoka na utendaji aliouita kuwa mahiri wa Mkapa wakati wa uongozi wake, umewafanya Watanzania wengi kumuunga mkono hadi sasa na kwamba kitendo cha kumshitaki ni udhalilishaji ambao unaweza kuleta mgawanyiko katika umoja wa kitaifa uliopo. [95]
kulipa
Anakubali kuwa, kiwango cha mauzo ya nje kimeongezeka, lakini anasema, kinatokana na madini hasa dhahabu na bei yake katika soko la dunia jambo ambalo halimfaidishi hata kidogo raia wa kawaida kwa kuwa makampuni yanayozalisha na kuuza madini nchini yanakwepa kulipa kodi. [96]
kuna
Mulla alisema kuwa, endapo kuna vyama vya upinzani vitatimiza lengo lao la kumkashifu kiongozi huyo, CCM haitakubali kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai na hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa. [97]
kununua
Pesa za kununua shangingi moja zinatosha kununua kompyuta kwa watu zaidi ya thelathini pamoja na kulipa gharama zote za mtandao. [98]
kuomba
Kabla ya kuomba hela ya soda, Rama aliulalamikia upande wa mashitaka kwa kuchelewa kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo. [99]
kuuza
WAAGIZAJI wakubwa wa mafuta nchini wamewakana na wamiliki wa vituo vya kuuza nishati hiyo na kushangazwa na kitendo cha kupandisha bei kiholela wakati wa sikukuu ya Krismas kwa kisingizio cha uadimu wa mafuta baada ya meli kuzuiwa na maharamia wa Kisomali. [100]
kuwa
Hii inathibitisha kuwa nchi inaweza kuwa tulivu isipokuwa pale ambapo baadhi yetu tutakapokuwa tumeamua kuwa isiwe hivyo. [101]
kuzungumza
Kocha wa Kenya, Francis Kimanzi aligoma kuzungumza mchezo huo, lakini Owino na wenzake walionekana wakimzonga mwamuzi Ally Kalyango wa Uganda. [102]
kwao
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kila timu ikitaka ama kuongeza bao au kusawazisha, lakini milango ilikuwa ni migumu na mabekiwa timu zote walikuwa makini kuondoa hatari zilizoekekezwa kwao. [103]
kwenu
Na kwa maana hiyo naomba nichukue fursa hii tena kuwashukuru wasomaji wote wa makala zangu na zaidi niseme ni fahari iliyoje kupata kusikia kutoka kwenu. [104]
la
Katika mwaka 2008 uliomalizika jana taifa lilishuhudia matukio mbalimbali- maandamano na migomo ya wafanyakazi, wanafunzi wa vyuo vikuu, wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mapigano ya kikabilila mkoani na fujo katika kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime mkoani Mara. [105]
lake
Hakuna taasisi iliyoonesha ushirikiano katika mambo yake ikashindwa kufikia lengo lake, liwe la kisiasa, kiuchumi, kibiashara na kadhalika. [106]
leo
Aidha habari ambazo gazeti hili imezipata kutoka ndani ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinasema rufaa ya Shitambala itatolewa leo saa 4:00 asubuhi. [107]
licha
Sisi hatuwezi kuchukua polisi na kwenda kuwakamata licha ya ukweli kuwa ongezeko hilo linawaumiza wananchi. [108]
ligi
Alisema ratiba ya raundi ya pili imezingatia mashindano mbalimbali kama klabu bingwa Afrika na shirikisho, michuanio ya fainali ya wachezaji wanaocheza ligi ya ndani ( CHAN). [109]
madai
Askari hao walijitambulisha kwa mama huyo na kumtaka awaruhusu kufanya upekuzi ndani ya nyumba kitendo ambacho mama huyo alikipinga vikali kwa madai kuwa mumewe hayupo, lakini Polisi walimuhakikishia usalama wa mali zake hata hivyo mke huyo aligoma kabisa kuwaruhusu kuingia ndani kwa upekuzi. [110]
madeni
Ni mwezi huo huo wa Februari, baada ya sakata la Richmond, lilizuka kwa kasi kubwa suala la wale waliochota fedha kutoka akaunti ya madeni ya nje ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA). [111]
maendeleo
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema jana kuwa katika kikao hicho walijadili mambo muhimu ya maendeleo ya soka la Afrika Mashariki na Kati. [112]
mafanikio
Matumani hayo kwa kiasi kikubwa yalichochewa na mafanikio ya kuwa na nguvu ya pamoja iliyochangia kukiondoa madarakani chama cha KANU nchini Kenya na kukiingiza chama kilichokuwa na muunganiko wa vyama mbalimbali vya upinzani nchini humo cha NARC Kenya. [113]
makini
Alipowasilisha rufani yake juzi Shitambala alisema kuwa, msimamizi wa uchaguzi hakusoma kwa makini maelezo yake na kuyazingatia kikamilifu kabla ya kufanya maamuzi ya kumuengua. [114]
makubwa
Hata hivyo, kocha huyo alisema pamoja na matumaini makubwa aliyonayo kwa kikosi chake, bado Watanzania watatakiwa kuiunga mkono hata pale michuano hiyo itakapoanza akiwataka wale wenye uwezo wa kusafiri kufanya hivyo ili kwenda kuishangilia timu hiyo. [115]
mama
Ramadhan na mama yake Hadija Ally wanadaiwa kuwa Aprili 24 mwaka huu walimuua mtoto Salome Yohana (3) ambapo Rama alikamatwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwa na kichwa cha mtoto huyo. [116]
manaibu
Alipotangaza Baraza jipya iligundulika kuwa Mawaziri tisa na manaibu mawaziri nane, walipoteza nyadhifa zao. [117]
mara
Alisema kuwa, mara nyingi kumekuwepo kambi za vijana wa CCM kwa ajili ya kujifunza itikadi za chama hicho na kwamba kambi hiyo ni kwa ajili ya shughuli za vijana. [118]
masikini
Lipumba anafafanua kuwa, ripoti hiyo inatofautiana na ripoti ya serikali ya Novemba/Desemba mwaka huu, ambayo yenyewe inaonyesha kuwa watu masikini wameongezeka kutoka 11.7 milioni 2005 hadi 12.7 milioni 2007, na kuongeza kuwa kuna ongezeko la watu milioni moja ambao ni masikini. [119]
matatizo
Yapo matatizo ya uendeshaji ambayo yamesababisha huduma zitolewazo ATCL kuwa za kiwango kisichoridhisha,” alisema Rais Kikwete. [120]
mfumuko
Profesa Lipumba anasema kwamba hali ya mfumuko wa bei inayotangazwa katika ripoti mbalimbali za serikali ni mara mbili zaidi ya hali halisi ya mfumuko wa bei za bidhaa muhimu nchini. [121]
mgomo
Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, latangaza kuwasimamisha masomo kwa muda usiojulikana, wanafunzi wa shahada ya kwanza kufuatia mgomo waliouitisha kuishinikiza serikali iwaongezee fedha za mikopo. [122]
mistari
Rais Kikwete kupitia hotuba yake hiyo alisema kuwa amedhamiria kumaliza kabisa mpasuko wa kisiasa katika visiwa vya Unguja na Pemba ambapo alisema kuwa unatokana na sababu za kihistoria za wananchi wa kisiwa hicho kusimama kwenye mistari yao ya kihistoria wakati wa mapambano ya kujitawala. [123]
mke
POLISI wilayani hapa wanamshikilia mkazi wa kitongoji cha Kobhetimo kijiji cha Nyansurumuti kata ya Kisaka tarafa ya Ngoreme maarufu kwa majina ya Mrema Mantago Nkoba (28) kwa tuhuma za kumchoma kisu na kusababisha kifo cha mdogo wake baada ya kumtuhumu kuwa na uhusiano wa mapenzi na mke wake. [124]
moja
Katika tukio jingine, mahakama hiyo imewahukumu watu wawili, Richard Mhoja, 29, mkazi wa Mshikamano na Bundala Mahona, 28, mkazi wa Nhelegani katika Manispaa ya Shinyanga, kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja kwa kosa la kuvunja na kuiba duka vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh 607,000 kwenye duka moja. [125]
mpango
WAKATI Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) likikamilisha mpango maalum wa kuinua kiwango cha mchezo huo, utekelezaji wake unatarajia kukamilika baada ya miaka nane, imeelezwa. [126]
mpya
Kuhusu utekelezaji wa kazi za Bunge kwa mwaka huu mpya wa 2009, Spika Sitta alisema atahakikisha unafuata katiba na sheria. [127]
mwa
Miongoni mwa tuhuma za Mkapa, ambaye anasifika kwa kuinua uchumi baada ya kuukuta kwenye hali mbaya, ni kujiuzia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya kwa bei nafuu akitumia kampuni ya Tan Power Resources anayoimulika pamoja na waziri wa zamani wa nishati na madini, Daniel Yona wakati akiwa rais. [128]
mwisho
Spika Sitta alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na gazeti hili kuhusu urejeshwaji wa fomu hizo ambao tarehe yake ya mwisho ilikuwa jana. [129]
na
Rais alitoa onyo hilo katika hotuba yake ya salaam za Mwaka Mpya wa 2009 kwa wananchi, aliyoitoa jana kupitia vyombo vya habari, akizungumzia changamoto kadhaa za mwaka 2009 na mikakati ya serikali yake kukabiliana nazo baada ya mikakati ya mwaka 2008 kuathiriwa na kuporomoka kwa uchumi wa nchi tajiri kutokana na kuyumba kwa taasisi za kifedha. [130]
nani
Katika soka ya sasa hutakiwi kuangalia unacheza na nani, jambo la msingi ni kuwa tayari wakati wote kukabiliana na yeyote, hivyo kitendo cha kukutana na mwenyeji na hata hizo timu nyingine si tatizo au unaweza kuangalia ni vipi tuliweza kuikabili na kuimudu Cameroon. [131]
nao
Kamanda huyo alisema baada ya mzozo wa muda mrefu kama wa dakika 10 hivi mama huyo aliamua kuwaruhusu kufanya upekuzi huku akishirikiana nao kwa kuwafungulia chumba kimoja baada ya kingine na ndipo walipokuta fuvu hilo likiwa limehifadhiwa kwenye ndoo kidogo ikiwa imefunikwa na mafuta mengi ya samli ili isionekana kama kuna kitu kingine zaidi ya samli hiyo. [132]
naye
Morumbe Mantago(22) ambaye ni mdogo wake naye mkazi wa kijijini hapo. [133]
ndio
Tunaangalia jinsi ya kuiandaa Taifa Stars kwa vile ndio inawakilisha ukanda wetu na kikao kimeshauri kwamba timu hiyo ipatiwe maandalizi ya kutosha ili ituwakilishe sawasawa,îalisema Musonye. [134]
ndipo
Alisema mtuhumiwa huyo alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kuanzia mwaka 1992 hadi 1999 wakati wizi huo ulipogunduliwa na ndipo alipokamatwa na kufikishwa mahakamani. [135]
ndivyo
Lakini ndivyo tulivyo. [136]
ndiyo
Sitta aliongeza kuwa, wamewasiliana na Ofisi ya Kamishna wa Maadili na kueleza hali hiyo na ndiyo sababu ofisi yake imetoa tamko kuwataka wabunge wasiopata fomu hizo kuzifuata ofisini kwake. [137]
ngono
Habari hizo zinadai kuwa hali hiyo iliendelea huku wakiwa wanakunywa ambapo marehemu anadaiwa kumtukana kaka yake akimujumuisha na mke wake Nyabuke Mrema (24) ambaye anahusishwa naye katika masuala ya ngono. [138]
nia
Kilichofatia baada ya hapo ndio kinachotia hofu kuwa kama kweli vyama vya upinzani vilikuwa na nia ya dhati ya kuungana na kuwa na nguvu ya pamoja dhidi ya chama tawala, kwani mambo yalianza kwenda mrama wakati wa hekaheka za uchaguzi mdogo katika jimbo la Tarime kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Chacha Wangwe. [139]
njaa
Katika tukio jingine, timu ya Kenya, Harambee Stars ikiwa na wachezaji wa Yanga, Joseph Shikokoti, John Baraza juzi ililala njaa Jumatatu ilipokwenda Jinja kwenye hoteli ya Triangle kwa kuwa hakukuwa na taarifa kwa uongozi wa hoteli. [140]
nje
Alisema baada ya kukuta fuvu hilo polisi walikitoa kindoo hicho nje ambako muda huo tayari majirani na watu wengine waliosikia uwepo wa tukio hilo waliwa wameshafika kushuhudia upekuzi huo na askari waliwaruhusu kuangalia ndani ya sadolini hiyo ili waweze kuona kilichokuwa kikifanyika ndani ya nyumba hiyo. [141]
nne
Hatari yake ni kwamba wanafunzi watakaopitia mazingira hayo watamaliza kidato cha nne bila ya kuwa na elimu inayolingana na kiwango hicho. [142]
nyeti
Hali hiyo ilisababisha Rais Kikwete kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, Daudi Ballali kutokana na kushindwa kudhibiti upotevu wa fedha hizo akiwa kama kiongozi mkuu wa taasisi hiyo nyeti ya umma. [143]
nzuri
Jamani Mkapa amelitumikia taifa hili na kuliacha katika hali nzuri. [144]
ona
Lakini ona Wakorea sasa na hakuna ambaye atatambia saa za Kikorea. [145]
ovyo
Uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 aliyekuwa Waziri wa Biashara na Viwanda Iddi Simba aliondolewa madarakani baada ya kubainika alitoa ovyo vibali vya uagizaji sukari nje ya nchi. [146]
papo
Waziri Mkuu aliyasema hayo wakati akijibu maswali ya papo kwa papo. [147]
pato
Baadhi ya viashiria vilivyoainishwa katika ripoti hiyo kuwa vimefanikiwa sana ni pamoja pato la taifa, pato la serikali, mauzo ya nje, pato la mtu mmoja mmoja na miradi mipya iliyofunguliwa na kusajiliwa. [148]
pia
Rais pia alisema serikali imekusudia kulifanyia marekebisho shirika hilo katika mwaka 2009, ili liweze kutoa huduma ipasavyo. [149]
pili
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Mbeya,kimevionya vyama vya upinzani vyenye lengo la kumchafua rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Mbeya Vijijini. [150]
rasilimali
Matumizi makubwa ya fedha yanayofanywa na vyama vya siasa wakati wa kampeni za uchaguzi ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma. [151]
rasmi
Mgeni rasmi katika mchezo wa Uganda na Zanzibar atakuwa Janet Museveni, mbunge na mke wa Rais Yoweri Museveni. [152]
ripoti
Kwa mujibu wa ripoti hiyo serikali inajigamba na kujinasibu kuwa uchumi wa Tanzania unapeta ndani ya kipindi hicho cha miaka mitatu. [153]
sera
Sisi Wabunge tupo kwa ajili ya kuifanyia marekebisho katiba, kutunga sera na sheria," alisema Sinani na akaongeza kusema: "(Suala la hoja binafsi) Likiletwa tutalijadili, lakini pamoja na majukumu hayo sidhani kama ni busara kuifanyia marekebisho katiba kila kukicha, hasa pale unapomlenga mtu fulani. [154]
shida
Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam juzi, Maximo alisema kuwa umaarufu wa nchi alizopangiwa nazo haumpi shida kwani soka ni mchezo unaochezwa kwa vitendo na si maneno. [155]
si
Akizungumzia matokeo ya darasa la saba Kikwete alisema matokeo hayo si ya kuridhisha katika miaka miwili iliyopita na kuwa ameiagiza wizara husika kufanya uchunguzi wa sababu za kushuka kwake, pamoja na kuzitafutia ufumbuzi, kazi ambayo itasimamiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. [156]
sisi
Siku chache kabla ya sikukuu ya Krismasi baadhi ya wafanyabiashara walihofia kutokea kwa uhaba wa mafuta baada ya kuwepo taarifa kwamba nchi jirani hazina mafuta, hivyo wakalazimika kupandisha bei ya bidhaa hiyo kiholela ingawa sisi kwa ujumla wetu kila mmoja ana akiba itakayoweza kutumika kwa siku 25 na kabla hayajamalizika meli za mafuta zitakuwa zimeshawasili nchini," alisema Hirani. [157]
soko
Alisema serikali itatumia nguvu nyingi katika kuhami na kukuza uchumi na kwamba,serikali itaendelea kushirikiana na Benki Kuu kuzuia athari za soko la fedha duniani zisilifikie taifa na iwapo zitalifikia, makali yake yawe nafuu. [158]
tako
HE jamani, mambo ya nishani ya viatu na tuzo la tako yameleta ubishi mkubwa sana. [159]
tamaa
Msemo huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuinua maendeleo ya watu mbalimbali hasa pale kunapoonekana kuna vikwazo ambavyo vinakatisha tamaa, na hivyo kufanya baadhi ya watu au kikundi cha watu kuanza kujitenga kwa ama kukatishwa tamaa, ama kuona mambo hayatakuwa kama wanavyofikiria. [160]
tangu
Hapa nchini tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, kumekuwa na ushindani dhaifu dhidi ya chama tawala CCM katika chaguzi zote zilizofanyika tangu mwaka 1995 ulipofanyika uchaguzi mkuu chini ya mfumo wa vyama vingi. [161]
tathmini
Wenzetu Rwanda, Kenya, Uganda wanakimbia wakati sisi ndio kwanza tunajikongoja na tunajisifu uchumi unakua, lakini ukifanya tathmini ya kina utagundua kuwa badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma," anasema Dk. [162]
tatu
Ndivyo unavyoweza kufupisha kitendo cha baadhi ya wabunge na wananchi wa mkoani Mtwara kujitokeza hadharani na kumtetea rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa. [163]
teke
Hili teke linalotujia wazee limepindua ulimwengu maana sasa ni watoto na vijana wanaojua si sisi wazee. [164]
tena
Hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 14 mwakani itakapotajwa tena. [165]
timu
Mwakyoma alisema taarifa hizo timu ya askari ilitembelea eneo la nyumba hiyo ambapo hata hivyo hawakufanikiwa kumkuta mfanyabiashara huyo na badala yake walimkuta mke wake aitwaye Mwanaidi Ramadhani (25). [166]
tu
Si hilo tu amefanya mengi ambayo anastahili kuheshimiwa na kuachwa apumzike. [167]
tukiwa
Nahodha Henry Joseph alieleza:"Uungwaji mkono ambao mmetupa tukiwa Taifa Stars, unahitaji ili tuweze kulileta kombe ambalo Tanzania imelikosa kwa muda mrefu. [168]
tume
Hata hivyo sisi waishiwa tulifaidi sana maana tulikuwa tumeshajiteua kuwa tume ya tuzo. [169]
tuna
Hakuna mgawanyiko ndani ya chama chetu cha CCM na hakuna wabunge waliogawanyika wote ni kitu kimoja na tumejipanga vizuri na tunamwomba Mwenyezi Mungu atusaidie ili tuweze kupata ushindi kwa asilimia kubwa na tuna imani kuwa tutashinda," alisema. [170]
ufisadi
Meghji na Mramba, wamepoteza nyadhifa zao wiki chache baada ya kuibuka kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya shilingi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo ni taasisi ya umma iliyo chini ya wizara waliyokuwa wakiiongoza kwa nyakati tofauti. [171]
ukanda
Musonye alisema katika kikao hicho walizungumzia maendeleo ya soka la vijana kwenye ukanda wao pamoja na maandalizi ya Taifa Stars inayoshiriki fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN). [172]
ule
Katika maelezo yake, Spika Sitta alisema kuwa mfumo uliotumika mwaka jana kuwafikishia wabunge fomu hizo kwa kuzituma majimboni mwao umesababisha usumbufu, tofauti na ule wa miaka iliyopita wakati wabunge walipokuwa wakigawiwa fomu hizo kwenye kikao chao cha mwezi Novemba. [173]
umma
Rais alitaja taasisi nyingine za umma ambazo utendaji wake ulikuwa mbaya ni Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA). [174]
vifaa
Haitoshi kuwa na vyumba vya madarasa kama vifaa vya kufundishia havipo au havitoshi, na hakuna walimu wa kutosha. [175]
vumbi
Yanga itafanikiwa kuingia raundi ya pili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika inayotarajiwa kutimua vumbi Februari Mwishoni kwa kuanza na timu kutoka Comoro. [176]
vyao
Baraza, George Owno , wote wa Yanga hawakuonyesha viwango vyao, Joseph Shikokoti alikuwa benchi. [177]
wadau
Ripoti hiyo imewashitua wadau mbalimbali wa masuala ya kisiasa, kidiplomasia na kiuchumi nchini ambao wanasema kuwa ripoti hiyo inapotosha umma wa Watanzania kwa kuwa haijazungumzia uhalisia wa uchumi wa nchi. [178]
waheshimiwa
Imebainika sasa kwamba baadhi ya waheshimiwa wabunge hawakuzipata fomu hizo. [179]
wakisema
Watu waliotoa maoni yao kuhusu hilo walionyesha kuridhishwa kwao na kitendo cha serikali kuwapandisha kizimbani mawaziri wawili wa zamani wanaotuhumiwa kwa vitendo vya ufisadi, huku baadhi wakisema kuwa bado wengi zaidi wanatakiwa kufikishwa mbele ya mkono wa sheria. [180]
wala
Suala la mafuta kupanda ni suala la wamiliki wa vituo vya mafuta wala halihusiani na sikukuu za Krismas ama sisi kufunga ofisi wakati wa sikukuu na wala lisihusishwe na suala la maharamia wa Kisomali, bali ni maamuzi ya wamiliki wa vituo vya mafuta ya kupandisha bei kwa sababu wanazozifahamu. [181]
walio
Baada ya kuwapelekea walimu katika vituo hivi, Armstrong anakiri kuwepo kwa mabadiliko makubwa ya kimtazamo kuhusu elimu kwa Wahadzabe walio wengi. [182]
wangu
Wakati naanza kuifundisha Stars wachezaji wangu walikuwa na hofu pale watakapokutana na Cameroon au timu yoyote, lakini niliwaambaia waondoe kitu hicho na kusikiliza maelekezo yangu, nafikiri walifanya nini kwenye michezo iliyiopita,"alisema. [183]
wao
Alizungumza masuala mengi yakiwemo ya sheria zilizotumika kumuondoa na akazikosoa na hatimaye aliwataka wananchi wawe wavumilivu, hata kama rufaa yao haitakubaliwa kwa kuwa atawaachia wananchi wenyewe waamue hatima ya mustakabali wao ingawa pia aliwahakikishia kuwa haki yao lazima wataipata. [184]
wasiwe
Tunakiri kwamba akiba yetu inatosha hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi. [185]
wengi
PAMOJA na kuwekewa pingamizi na hatimaye kuenguliwa kwa mgombea wake wa ubunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kiliendelea kupiga kampeni katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na watu wengi. [186]
wenyeji
Katika michuano hiyo, Stars imepangwa Kundi A ikiwa na wenyeji wa michuano hiyo, Ivory Coast pamoja na Senegal na Zambia. [187]
wetu
Navionya vyama vya upinzani vinavyosema kuwa vitamkashifu rais wetu mstaafu wa awamu ya pili wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi katika jimbo la Mbeya Vijijini, kuwa hatutakubaliana na vitendo hivyo. [188]
wewe
Hiyo itakupa nafasi ya kuona wewe ni mtu muhimu kiasi gani na huenda ikawa nafasi nyingine kwako kumshukuru tena Muumba. [189]
wiki
Katika makubaliano yetu ya kupanga bei tumeafikiana mambo mawili moja ni kukutana na Ewura kwa ajili ya kubadili takwimu za bei ya mafuta nchini na suala la pili ni kukutana kila wiki mara mbili - Alhamisi na Jumatatu- kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali, likiwemo suala la hali ya bidhaa hiyo," alifafanua Bisarara. [190]
yeye
Katika mahojino ya tukio hilo mke wa mfanyabiashara huyo alikiri fuvu hilo kukutwa ndani ya kisadolini lakini alisema hajui kichwa hicho kilifikaje kwani hata yeye ameshitushwa na tukio la askari kukuta fuvu hilo. [191]
yote
Ingawaje Rais mwenyewe amekuwa akipita na kujigamba kuwa wananchi wasiwe na hofu itakapofika 2010 yote aliyoyaahidi yatatekelezwa lakini muda umeshakuwa kikwazo kwake. [192]
zake
CCM inatarajia kuzindua kampeni zake za ubunge Januari 4 kwenye kijiji cha Ilembo kilicho tarafa ya Isangati, ikiongozwa na rais huyo wa serikali ya awamu ya pili. [193]
zao
WABUNGE wametakiwa kurejesha fomu za tamko la mali zao walizopatiwa na Ofisi ya Kamishna wa Maadili ndani ya siku 14 kuanzia leo, Spika wa Bunge Samuel Sitta amesema. [194]
zenu
Meseji zenu, email zenu zilinipa nguvu ya kuendelea na kila siku nilikuwa nasema hilo. [195]
zetu
Kwa mwaka mpya wa 2009, tutafanya kazi zetu tukiweka umuhimu katika kufuata sheria na katiba ya nchi. [196]
zichukuliwe
Hatua zichukuliwe dhidi ya warsha zisizo na maana. [197]
zile
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Muhammed Seif Khatib alisema harakati hizo hazina tofauti na zile zilizoongozwa na Kanal Bacar wa visiwa vya Anjourn nchini Comoro. [198]
zisizo
Anasema kuwa, serikali inapoangalia kipengele cha ajira huangalia zaidi katika ajira zisizo rasmi, jambo ambalo ni kinyume na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwapatia Watanzania ajira milioni mbili. [199]
zoezi
Hata hivyo, jana Ofisi ya Bunge ilitoa taarifa inayobainisha kuwa baadhi ya wabunge hawakuzipata fomu hizo kama ilivyokusudiwa na Ofisi ya Kamishna wa Maadili mwenye dhamana na zoezi hilo. [200]