Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-31

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
aende
Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [2]
afe
Si bora afe tujue moja. [3]
aina
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova waliofariki dunia katika ajali hiyo mbaya iliyohusisha magari malori mawili na basi dogo aina ya Toyota Hiace ni Maiko Msagila (33) na John Steven (32) ambao ni wafanyabiashara na Ally Issa (37), ambaye ni mkazi wa Ukonga, jijini. [4]
aishi
Kwa sababu naye hakuwa na mtoto, licha ya kuwa na wake wawili, aliamua kumchukua Kazim aishi naye. [5]
ajuza
Ongezeko hilo linafuatia kuuawa kwa kupigwa mshale, kwa ajuza Khanga Lekupele (100). [6]
akawa
Mchizi kabla ya kuingia biznes kubwa kama za kuwa na butiki hivi, ..alikuwa mtu wa mishen'tauni, lakini mara mbili tatu hivi akawa kadakwa na ma'afande, akatia akili, akaanza kuuza mitumba, ndio mambo yakaenda, ..mdogo mdogo mpaka kapata butiki. [7]
albamu
Muba alisema ya kwamba albamu ipo kwenye maadalizi makubwa kwakuwa mpaka sasa bado nyimbo nne ili kuweza kuikamilisha, anatarajia kuizindua siku ya Valentine. [8]
alifuatwa
Siku moja Kazim akiwa amejipumzisha nyumbani, alifuatwa na watu wale waliokuwa wakisimamia biashara zake za uvuvi wa samaki na uchimbaji wa madini. [9]
alisoma
Siku moja baada ya kukutana na jamaa huyo alisoma taarifa kwenye gazeti moja kwamba kuna biashara kubwa ya kununua viungo vya albino kwa ajili ya machimbo ya madini na biashara ya uvuvi. [10]
aliwahi
Kuna wakati aliwahi kupewa mtihani wa kidato cha sita, alifanya na kufaulu vizuri. [11]
ama
Hatudhani Yanga na Prisons wakawadharau ama kucheza chini ya kiwango na kushindwa kupata ushindi. [12]
amani
Mwaka 1917 kwa mara ya kwanza siku ya wanawake duniani iliadhimishwa Machi 8, siku hiyo wanawake waliandamana kwa madai ya kutaka ëamani na mkate,í kwa kuwa kulikuwa na vita hakukuwa na amani, hivyo hata upatikanaji wa chakula ulikuwa wa shida. [13]
ambae
MCHEZAJI wa zamani wa timu ya West Ham ya England, Tommy Tailer ambae ni mtaalam na mkufunzi wa shule za vijana za mchezo za soka anatarajia kuchukua vijana wa tatu kutoka kituo cha Tanzania soccer academy kwa ajili ya kwenda kuwafanyia majaribio katika klabu ya Peterbough United iliyopo England. [14]
ambazo
Kampeni zilitawaliwa na vituko vya mashabiki kupigwa, bendera za CUF kuchanwa, masunduku ya kura kukutwa kwa watendaji wa CCM, FFU kuwatisha wananchi na kasoro nyingine nyingi ambazo CUF imeziripoti kwa msimamizi wa uchaguzi na polisi," alisema Profesa Lipumba. [15]
ana
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Cheka alisema ana uhakika wa asilimia 100 ya kushinda mpambano huo kutokana na aina ya mazoezi anayoyapata kwa mwalimu wake Abdalah Saleh (Komando) pamoja na kutambua udhaifu wa Rashid Matumla. [16]
au
Miongoni mwa kasoro hizo ni zinazokataza wananchi kuingia kwenye maeneo ya hifadhi, jambo ambalo lilielezewa kuwa ni kuzuia haki ya wakazi wa maeneo karibu na hifadhi kutofanya shughuli zozote ikiwemo kutafuta kuni au majani. [17]
bado
Hata hivyo rufaa hiyo bado haijapangiwa jaji wa kuisikiliza. [18]
bahati
Akafunga ofisi hizo za kuziweka kwenye majengo yake ambayo kwa bahati mbaya yalikuwa nje ya mji. [19]
baina
Wakati huo huo,idadi ya watu waliokufa katika mapigano baina ya wakulima na wafugaji wa Kata ya Pangwi, imeongezeka na kufika wanane. [20]
bali
Alifafanua kuwa kulingana na taratibu za awali, Tanzania ilikuwa hainufaiki na biashara hiyo ya utalii bali wageni wanaomiliki vitalu na ndio maana bunge liliona hilo likataka hali hiyo irekebishwe. [21]
band
Ndiko kazi kubwa inakokwenda kufanyika, litapigwa live la kufa mtu huku watu maarufu, pamoja na wengi wa nyadhifa mbali mbali wakiwa wanaiangalia, shoo ya kwanza itakuwa ni maalum kwa mashabiki, kama shukrani kwa kijana, kwa kumvumilia na kuendelea kuwa shabiki wa Top band. [22]
baraza
Nahodha alisema tatizo la uchafu wa mji wa Zanzibar, linatokana na baraza kutokuwa makini na si ukosefu wa vitendea kazi, kama ilivyoelezwa na baadhi ya wajumbe wa baraza la wawakilishi. [23]
bila
Masharti mengine ya dhamana ni kuwasilisha hati zao za kusafiria, kutosafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kuwa na kibali cha Mahakama, na kuripoti ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kila saa 2:00 asubuhi ya kila Ijumaa. [24]
biznes
Yaani kwa kuwa washkaji zake wengi mademu, kutokana na biznes anayofanya. [25]
cha
Kipengele kingine kilichoonekana kuwakera wapinzani ni cha kumtaka mtuhumiwa aliyekamatwa ndani ya hifadhi kuwa ndiye anayepaswa kuithibitishia mahakama kuwa hakutenda kosa, badala ya mpango wa kawaida ambao mlalalmikaji ndiye anayepaswa kuthibitisha katika kiwango cha kuiondolea mashaka mahakama kwamba, mtuhumiwa alitenda kosa hilo. [26]
chacha
Nilikuwa nafanya muziki huku nasoma, na bendi yangu ya kwanza ilikuwa nikilimanjaro chacha bendi, ambayo nilianza kuimba mwaka 1961" anafafanuwa Gurumo. [27]
chake
Alisema kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi wa Mbeya Vijijini na wapigakura wengi kutojitokeza kupiga kura, kumetokana na udhaifu wa tume hiyo, katika kusimamia uhuru na haki katika chaguzi. [28]
darasani
Kila alichofundishwa kilikuwa ni kama vile alishawahi kufundishwa mara nyingi, kwani alikuwa ana uwezo wa ajabu mno darasani, hadi wanafunzi wa madarasa ya juu wakawa wanakwenda kwake kuomba kufundishwa baadhi ya mambo ambayo hawakuwa wakiyajua. [29]
es
WATU tisa wamefariki dunia na wengine zaidia ya kumi kujeruhiwa vibaya katika ajali mbaya ya gari iliyotokea jana majira ya saa kumi alfajiri, eneo ya Jet katika Barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam. [30]
fulani
Kipaji siku zote hakijifichi,ingawa sikuwa nafikiria kuwa muimbaji hata siku moja lakini niliamua kufanya kitu fulani ili kuweza kuangalia kama kweli watu wanayoniambia,nashukuru Mungu kwamba niliweza kutengeneza wimbo wangu wa kwanza 'Brenda' lakini sikuweza kuupeleka redio sikuwa najiamini kiivyo,nakiri hilo" Alisema Muba. [31]
gani
MSANII ni kioo cha jamii, hivyo msanii yeyote anapaswa kuzingatia hili na kujua yeye ni nani na ana nafasi gani na pia ana msaada gani kwa jamii katika kufikisha ujumbe, ingawa walio wengi huhofia, pia inawezekana kabisa huenda wakawa hawajui nini cha kufanya. [32]
hadi
Bunge hadi jana jioni lilikuwa linajadili muswada wa sheria ya wanyamapori ambao ulipingwa vikali na wabunge wa upinzani, kwa maelezo kuwa baadhi ya vifungu viko vinawanyima haki wazawa. [33]
haina
Kwanza waziri mwenyewe ni albino, kama ataniambia mambo yasiyoeleweka, nitatuma watu tumuue viungo vyake tuvipeleke kwenye biashara, ambayo hadi sasa bado haina mafanikio licha ya kuua yule albino ambaye alikuwa msaidizi wangu wa karibu,” alijisemea. [34]
halina
Wakili wa serikali, Boniface Stanslaus alisema pingamizi la Magafu halina msingi kwani hata katika sheria inayotumika kusajili majina ya biashara hakuna sharti lolote linaloonyesha kwamba, kitabu hicho ni lazima kiandikwe kimetoka Brela. [35]
hana
Vyanzo mbalimbali vya habari kutoka mahakamani hapo vilidai kuwa baadhi ya ndugu wa mtuhumiwa walifika mahakamani hapo kushughulikia dhamana ya yake, lakini walipoelezwa kuwa Hakimu Mkazi Hadija Msongo, ambaye anasikiliza kesi hiyo hana jalada la kesi, walikataa kuondoka mahakamani hapo. [36]
hao
Katika utetezi wake, Mwangunga aliomba radhi kwa hatua yake hiyo na kufafanua kwamba, aliona kuwa kusimamisha ghafla kwa shughuli za uwindaji, kungesababisha hasara kwa taifa na hata kuathiri biashara hiyo, hivyo akanona ipo haja ya kuwaongezea muda wafanyabiashara hao ili baada ya hapo miongozo hiyo ianze kutumika. [37]
hapa
Kama hapa tungetekeleza kanuni kisawasawa hivi sasa waziri (Mwangunga) angepelekwa Keko (gerezani) akakae huko siku saba," alionya Zitto. [38]
haraka
Uwaziri ni nafasi nzito, walijari, saa mbili baadaye taarifa ikarushwa kwenye vituo vingi vya redio na televisheni kuwa mvumbuzi wa dawa ya kansa ya moyo na damu kwa ujumla, anatafutwa na waziri, atakayemkuta awasiliane na waziri haraka iwezekanavyo au afike hospitali kuu ya taifa. [39]
hasa
Akizungumza na waandishi wa habari jana mchezaji huyo alisema lengo lake hasa ni kuhakikisha kituo hiko kinatimiza malengo yake ya kutengeneza wachezaji vijana wenye vipaji ili waweze kucheza soka la kulipwa barani Ulaya. [40]
hayo
Shuhuda mwingine ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kwamba baada ya ajali ya malori hayo kutokea wahusika hawakuweka alama zozote barabarani kuashiria kuwa kuna ajali, hivyo dereva wa daladala iliyokuwa ikipita nusu saa baada ya malori hayo kugongana hakuona kitu hivyo aliligonga lori hilo na kuliburuza mbele kidogo kutokana na kasi aliyokuwa anakwenda. [41]
hicho
Kuna watu walikuja wakasema kuwa ni ndugu wa Liyumba wamekuja kufuatilia dhamana, lakini walipoambiwa kuwa jalada limepelekwa kwa incharge (Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi) walikataa kuondoka," kilisema chanzo hicho. [42]
hii
Liyumba na Kweka ambao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jumanne wiki hii bado wanasota rumande kwa kukosa dhamana. [43]
hili
Jaji Makame aliliambia gazeti hili jana kuwa tume yake haihusiki na matukio yote aliyoyaeleza Profesa Lipumba na kwamba uchaguzi huo ulifanyika chini ya msimamizi maalum. [44]
hizi
Mashindano haya yatakuwa ni hatua ya maandarizi ya timu hizi mbili yaani timu ya Dar es Salaam na Mzizima ambazo zitashiriki katika michuano ya ngumi za majiji ya Tanzania ambayo ni Mwanza,Mbeya,Tanga,Arusha na Dar es Salaam ambapo Dar es Salaam ikiwa ni wenyeji wa mashindano hayo itaziingiza timu tano ikiwa ni Timu ya jiji,Kinondoni,Ilala,Temeke na Mzizima. [45]
hospitali
Alihangahaika kwenye hospitali nyingi bila mafanikio. [46]
huku
Shuhuda huyo alisema kuwa kati ya abiria 18 waliokuwa kwenye basi hilo wawili tu ndio walikuwa nafuu huku wengie wakiwa wamumia vibaya ukiachia mbali waliokufa ambao miili yao iliharibiwa vibaya. [47]
huo
Shahidi huyo C 8565, Sajin Othman ambaye ni mtaalamu wa kuchunguza nyaraka katika maabara ya idara ya upelelezi jeshi la polisi alikuwa akitoa ushahidi huo, jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. [48]
huu
Baada baada ya hapo, William aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 2 mwaka huu ili kutoa muda kwa upande wa utetezi kupitia baadhi ya nyaraka zilizofanyiwa uchunguzi na shahidi wa tano katika kesi hiyo. [49]
huwa
Unajua madra huwa tunafundishwa mambo mengi ikiwemo kuimba, kwa hiyo mimi ndiko hasa nilipo jifunzia mambo ya muziki" anasema Gurumo Lakini mbali na Madrasa Gurumo anasema, muziki nikipaji alichorithi kutoka kwa mama yake mzazi ambaye alikuwa mwimbaji wa ngoma za asili. [50]
huyu
Pia msanii huyu huyu ni msaada mkubwa sana kwa jamii kama anajitambua yeye ni nani. [51]
ikawa
Ikiwa ameweza elezea hali halisi ya maisha ya mlalahoi, wengi wanamini huenda hiyo ikawa ni njia sahihi ya kufikisha ujumbe kwa viongozi wetu ambao leo hii wamepoteza uaminifu miongoni mwa jamii. [52]
ila
MAENDELEO ya soka duniani hayapimwi kwa matokeo ya mechi uwanjani tu ila ni mazingira yote kuanzia timu, klabu, viwanja, uongozi bora na mashabiki. [53]
ile
Othman alidai kuwa saini iliyoko katika cheti cha usajili cha kampuni ya Kiloloma & Brothers ambayo inadaiwa kufanana na ile ya afisa mtendaji mkuu wa Wakala wa Usajili wa Majina ya Biashara na Kampuni (Brela), Esteriano Mahingira hazifanani. [54]
ili
Hoja ya Dk Mzindakaya, ambayo iliungwa mkono na wabunge wengi, ilikuwa inaweka wazi kuwa bunge liliamuru vibali vilivyokuwa vinatumika viishie 2009 ili kuanzia 2010 taratibu mpya zisizo za kuiba mapato ya serikali zitumike. [55]
ina
Tanzania ina vipaji vingi ikiwemo mpira wa miguu lengo langu la kuchukua wachezaji hawa ni kuwapeleka kwenye kituo cha kufundisha soka kilichopo England kwa kuwafanyika majaribio katika klabu yetu na endapo watafuzu vizuri basi watapata nafasi ya kujinga na ligi daraja la kwanza katika klabu ya Peterbough,"alisema Tommy. [56]
ishu
Jamaa anauza duka la pamba za kidemu, mademu ndo' wateja wake, basi wana kila wakimuona ameibuka kiwanja, labda mademu wawili watatu wanaibuka kumpa hai, wanaanza kusambaza ishu kwamba, ...mchizi kicheche kwa sana nini. [57]
jazi
Gurumo alikaa kilimanjaro chacha bendi kwa takribani miaka mitatu ambapo mwaka 1963 alijiunga na kilwa jazi, ambapo alikaa kwa mwaka mmoja. [58]
jibu
Hata hivyo, wastaafu hao walidai kuwa, tangu suala hilo lilipofika kwa Mkulo hakuna jibu lolote walilopata, hivyo kuamua kumwandikia barua Kandoro ili awawezeshe kuonana Kikwete. [59]
jumla
Katika mashindano hayo ya 13 yanayoshirikisha jumla ya klabu 52 michezo 21 inatazamiwa kuchezwa wikiendi hii ikiwemo mechi dhidi ya Miembeni ya Zanzibar na Monomotapa ya Zimbabwe itakayopigwa leo,ugenini. [60]
juu
Ni hatari kwa mahakama yako tukufu kupokea kielelezo kama hiki kwa sababu ndani kuna majina tu ya makampuni hakuna hata sahihi na hata karatasi ya juu ya kitabu hiki ni ya kupachikwa kwa stika," alisema Magafu. [61]
juzi
MAJALADA ya kesi za watuhumiwa wa wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na dhamana ya aliyekuwa Mkurugenzi na Utawala wa BoT, Joachim Liyumba, juzi yalizua kizaazaa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusababisha askari wa kutuliza ghasia kumwagwa mahakamani hapo. [62]
kabla
Alidai kuwa utoaji wa vitalu hupaswa kufanywa miaka miwili kabla ya kuanza biashara, ili kutoa nafasi ya mmiliki kutafuta wawindaji hivyo utekelezaji wa maazimio ya bunge ungeweza kulisababishia taifa hasara. [63]
kali
Natoa wito kwa madereva wote wanaoendesha magari kwa kutofuata sheria za usalama barabarani na wale wanaokatisha njia walizopangiwa waache, kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yao," alisema Kamanda Kova. [64]
kana
Kila somo ambalo walikuwa wakimfundisha alikuwa akilielewa vizuri mno na kwa haraka, kana kwamba ni mtoto ambaye alikuwa akifundishwa kwa miaka mingi masomo hayo. [65]
kansa
Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [66]
karibuni
Alisema ng'ombe hao waliibwa katika mapigano ya hivi karibuni kati ya wakulima na wafugaji wa Kata ya Pangwi, wilayani Kilindi. [67]
kasi
Kamanda Kova aliwaambia waandishi wa habari kuwa ajali hiyo mbaya iliyotokea katika njia panda ya Jet na barabara ya Nyerere ilisababishwa na uzembe wa dereva wa daladala ambalo lilikuwa katika mwendo kasi na hatimaye kuligonga tela lori aina ya Scania lililokuwa limeanguka katika barabara hiyo baada ya kugongana na lori la mchanga aina ya Fuso. [68]
kata
Nae Katibu wa chama hicho, Athumani Juma aliongeza kwa kuiomba Serikali kutoa Semina elekezi kwa Wakuu wa mikoa, manispaa, miji, wilaya, halmashauri na kata kuhusu tiba hiyo asili kwa jamii. [69]
kibao
Mpoto anafahamika zaidi kwa kuimba mashairi yake hasa ya kisiasa ambayo mara nyingi yamekuwa na tafsiri nyingi kwa mashabiki wake, lakini kutokana na kibao chake hiki ambacho anaonekana kuuchimba zaidi ufisadi katika mashairi yake ya mwanzo. [70]
kibaya
Wengi wanashindwa kutambua majukumu yaliyopo mbele yao na kibaya zaidi wake na watoto wao tumeshuhudia wakiigeuza ikulu eneo la kufanyia biashara na kupora raslimali za wananchi kwa kivuli cha Rais. [71]
kijana
Akizungumza jijini jana kocha mkuu wa Tenis nchini Salum Mvita alisema kijana huyo ataondoka siku hiyo badala ya Januari 30 kama ilivyo pangwa. [72]
kocha
Alisema vijana hao watakwenda kufundishwa chini ya kocha John Ferguson ambae ni mdogo wa kocha Manchester United, Alex Ferguson. [73]
kuandika
Wachezaji wa Prisons ya Bara ambayo kesho ipo kazi wamesema kesho watakuwa kwenye wakati mgumu wa kutaka kurekebisha makosa yao katika Ligi hiyo na kuandika historia mpya. [74]
kubwa
Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa vikali na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) kwa maelezo kuwa historia inaonyesha kuwa Tanzania imekuwa ikipata hasara kubwa kupitia biashara ya utoaji wa vitalu. [75]
kuelewa
Unafikiri wale waliokatika shule za ukata wanaweza kushindana na wale wanaotoa mamilioni kwa ajili ya shule ya wanafunzi wachache na walimu kibao, na kufanya tuisheni juu mpaka wanaweza kufaulu bila hata kuelewa kitu. [76]
kufa
Baada ya kusubiri kwa kipindi kirefu sana, na zoezi kali la kufa mtu kufanywa katikati ya kitongoji kilichobeba jina la wilaya, hatimaye ngoma uwanjani leo, watu wanatarajia kupata mambo ambayo walikata tamaa kabisa kuyapata. [77]
kufika
Mtafaruku huoulitokea baada ya askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) kufika mahakamani hapo na kuanza kuwafukuza watu baada ya kutaarifiwa na uongozi wa mahakama kuhusu watu waliokuwa wanagoma kuondoka katika eneo hilo. [78]
kuhusu
Akiomba radhi kuhusu kosa hilo, Waziri Mwangunga alijitetea kuwa hakufanya hivyo kwa kulidharau bunge bali kwa utashi wake pamoja na ushauri wa wataalamu wake. [79]
kuimarisha
Kwa mujibu wa chanzo hicho, Kova alimpigia simu Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Kenyela ili kuimarisha ulinzi mahakamani hapo. [80]
kuimba
Ikiwa walio wengi wamejikita zaidi katika kuimba nyimbo ambazo zinalenga zaidi mahusiano hasa ya kimapenzi na kusahau nafasi zao katika jamii. [81]
kuishi
Siku moja usiku akiwa nyumbani alitafakari sana hali ngumu ya maisha ambayo angeanza kuishi. [82]
kuja
Tumeweka kiingilio kidogo katika mchezo huu ili kuwashawi mashabiki kuja kwa wingi kuishangilia timu yao ili iweze kufanya vizuri na kuibuka na ushindi,"alisema Kaijage. [83]
kukaa
TFF wanatakiwa kuwa wakali kwani kama hali hii ikiachwa, itaota mizizi na kitu cha kushangaza ni viongozi wa Yanga kukaa kimya bila ya kusema chochote, kupinga au hata kulaani kitendo cha mashabiki wao. [84]
kuku
Tumbo kali jana kashikwa na kuku wa jirani, lakini cha ajabu inaelezwa ushahidi wa mwizi wa kuku hadi atakapokamatwa na mnofu au mchuzi wa kuku" ni baadhi ya tungo hizo. [85]
kukutana
Hivyo walipanga muda wa kukutana. [86]
kule
Tangu alipokuwa katika shindano la BSS Aboubakar Mzuri alikuwa akiota kuimba mpaka kufikia kiwango cha Q Chief, umeona bwana, na kwa kweli akiimba huyu mtoto, kuanzia sura yake sauti na hata kule kunata na sauti yake kama uko nje ya ukumbi waweza sema mtoto wa kibondei Q Chief anaimba ndani huko, na ukiingia utamkuta kijana ambaye ghafla waweza sema, ..labda mdogo wake wanavyoshabihiana. [87]
kumuua
Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [88]
kuona
Naye Zacharia Osanga anaripoti kuwa, watu walioshuhudia ajali hiyo walisema daladala hiyo ilikuwa katika mwendo wa kasi jambo lililomfanya dereva ashindwe kuidhibiti baada ya kuona lori lililokuwa limeanguka katika barabara ya Nyerere. [89]
kupingwa
Mambo kama hayo na mengineyo ndiyo yanayoibuliwa na kupingwa kwa nguvu zote katika siku ya wanawake duniani. [90]
kusikia
Baada ya kusikia tangazo hilo, nilishindwa kuvumilia maana ningebaki nyumbani peke yangu ningelia sana. [91]
kutakuwa
Mbali na kuwa na pambano hilo pia siku hiyo kutakuwa na mapambano ya utangulizi kati ya mabondia ya Morogoro na Dar es Salaam kati ya Deo Njiku na Hemed Chilambo,Hamis Ajali na Abdalah Gobeto, James John atapambana na Jackson Jovin na Shaban Madilu atazichapa na Alex Dewa. [92]
kuu
MAWAKILI wanaomtetea aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Joachim Liyumba na Meneja mradi wa Benki hiyo, Deogratias Kweka ambao wanatuhumiwa kuisababishia hasara Serikali ya zaidi ya Sh 221 bilioni wameamua kukata rufaa mahakama kuu kupinga masharti ya dhamana. [93]
kuua
Ni suala la kawaida kuua albino na damu zao au viungo vyao tunavitumia kwenye shughuli hizo za uchimbaji madini na uvuvi, watu wengi wanafanya hivyo. [94]
kuwapa
Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega alisema wameamua kuweka viingilio vya chini kuwapa nafasi mashabiki wake wengi kushudia mchezo huu. [95]
kwani
Hata hivyo, alidai kuwa daladala hilo halikuwa limesajiliwa kwa njia hiyo kwani lilitakiwa kusafirisha abiria kwa njia ya Mabibo/Muhimbili na kwamba muda wa leseni (TLB) yake ulikuwa umekwisha tangu Machi 3, 2007, hivyo lilikuwa likifanya safari za usiku kwa kuiba. [96]
kwao
Naye Mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la soka nchini Sunday Kayuni alisema hii kwao ni changamoto nzuri kwa maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini hasa kwa vijana wadogo pia itasaidia kuitangaza Tanzania kimichezo. [97]
kwenda
WATU 18 wametiwa mbaroni mkoani Tanga, kwa tuhuma za kusafirisha ng'ombe 07 wa wizi, kutoka Kilindi kwenda Kilosa, mkoani Morogoro. [98]
la
Alikemea vikali tabia hiyo na kutaka iwe fundisho kwa wengine na kwamba, atakayefanya kosa kama hilo afike bungeni akiwa na barua ya kujiuzulu la sivyo sheria itumike ambayo ni kumfunga jela kwa siku saba. [99]
labda
Katika mashairi hayo ameweza kuelezea kuwa hilo ni tatizo "wala siwachongei bali kama mkiamua kuwafukuza wafukuzeni wote, majengo yafugiwe kuku labda ndilo tutaloliweza" ni baadhi ya mashairi ya msanii huyo. [100]
lake
Kamanda Kova, alisema dereva wa Fuso aliyekimbia mara baada ya ajali hiyo anasakwa na jeshi lake ili kufikishwa katika vyombo vya sheria kujibu mashitaka yatakayomkabili, hivyo kumtaka ajisalimishe kabla ya kutiwa mbaroni. [101]
lami
Pamoja na uchafu wa mitaani, Juma pia alilalamikia kuondolewa kwa mchanga katika barabara za lami, jambo ambalo alisema linachangia katika kuharibu miundombinu. [102]
lao
Katika madai yao ya msingi wastaafu hao wanadai kuwa Mkulo ameshindwa kutekeleza ombi lao la kutaka kamati yao ikutane na serikali kujadili kwa pamoja malipo ya mafao yao. [103]
leo
TIMU pekee yenye kipa mzungu Afrika Mashariki na kikosi ghali zaidi nchini na makocha watatu wa kigeni, leo inashuka kwenye uwanja wa Taifa kuivaa Etoile d'or ya Comorro katika msimu mpya wa Ligi ya Mabingwa Afrika. [104]
liko
Jina la Kiloloma & Bros Enterprise nalifahamu na hata kwenye daftari la kumbukumbu la Brela liko," alisema Kitambi. [105]
live
Vitu live, sauti mwanana na vitu kibao vya kushangaza. [106]
lugha
Kumbe walimtibua badala ya kumtibu na Bi Elimu mwenyewe alikuwa analalamika sana kwa nini anateswa na hao wanaojidai kumtibu katika lugha ambayo hata kuielewa haielewi. [107]
maamuzi
Mwishoni kabisa Mpoto aliweza kuelezea baadhi ya watumishi ambao huchukua maamuzi yao wao wenyewe na hatimaye kuwasingizia baadhi ya watu ambao hawana utetezi na kuwaangamiza. [108]
madai
Hata hivyo, wakili anayewatetea washitakiwa hao, Majura Magafu alipinga kitabu hicho cha kumbukumbu ya majina ya kampuni kisipokelewe mahakamani hapo kama kielelezo, kwa madai kuwa kimeandaliwa kukidhi matakwa ya kesi hiyo. [109]
madini
Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [110]
maiti
Maiti za marehemu hao zimehifadhiwa katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Amana na majeruhi wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hali zao zinaendelea vizuri. [111]
majiji
CHAMA cha mchezo wa ngumi za ridhaa Mkoa wa Dar es Salaam (DABA) kinatarajia kufanya mashindano kwa jiji la Dar es Salaam ambapo watazishirikisha timu kutoka katika majeshi ya ulinzi na usalama ikiwa ni maandalizi ya ngumi za majiji ya Tanzania. [112]
makali
Tunadhani, Kamati ya mashindano iwe na makali hasa ili iwe fundisho kwa wengine. [113]
matokeo
Siku moja baada ya Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo hayo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejigamba kwamba asilimia 65 ya watu ambao hawakujitokeza kupiga kura, ni watu waliotaka kikipigia kura chama hicho. [114]
mazuri
Mpira ndivyo ulivyo, tutajitahidi kurekebisha makosa hao Walibya hatuwajui lakini tutapambana nao uwanjani na tunaamini matokeo yatakuwa mazuri, tutashangaza,"alisema mshambuliaji mkongwe Oswald Morris. [115]
mdogo
Uchaguzi mdogo wa ubunge Mbeya Vijijini ulifanyika Januari 25 mwaka huu ambapo watu waliopiga kura walikuwa 44,855 kati ya 127780 waliojiandikisha. [116]
mgumu
Miembeni ambayo mwaka jana haikufanya vizuri leo itakuwa na mtihani mgumu, lakini inapewa nafasi kubwa ya kuanza vizuri kutokana na muundo wa kikosi cha sasa ambacho kimesheheni vijana kama ilivyo kwa wenzao wa Mundu ambayo wachezaji wake hawana uzoefu wowote kimataifa. [117]
mguu
Sawasawa wakati akina Mkombozi wanasota kwa mguu. [118]
michuano
Prisons ambayo ni wawakilishi wa Bara kwenye michuano hiyo ya Shirikisho, watasubiri hadi kesho kuivaa Khalij Sert ya Libya jijini Dar es Salaam. [119]
mimi
Nijuavyo mimi msanii ana nafasi kubwa ya kuweza kufanya kazi zake kwa uhuru ikiwa tu hatavunja sheria za nchi. [120]
mingi
Msanii huyu aliweza kuimba wimbo unaohusiana na mambo ya kisiasa 'Salam kwa mjomba ambao pia uliweza kujenga maswali pamoja na minong'ono mingi miongoni mwa jamii. [121]
mji
Waziri kiongozi alitoa ahadi hiyo jana alipokuwa akitoa ufafanuzi kufuatia swali la msingi la Mwakilishi wa Nungwi (CCM), Ame Ussi Juma, aliyetaka kujua namna serikali inavyoshughulikia tatizo la uchafu katika mitaa ya mji wa Zanzibar. [122]
mke
Sio kushiriki tu bali mke ndiye ambaye humsaidia kumshikia msahafu wa dini rais wakati akiapa. [123]
mmoja
Sisi tulishtukia mapolisi wamekuja wakaanza kutuondoa kinguvu na watu wote waliokuwepo hapa mahakamani," alisema mmoja wa wafanyakazi wa Kisutu ambaye hakupenda kutaja jina lake. [124]
mno
Kwetu sisi hapa Afrika, hali ni tofauti mno, mke huwa hapewi nafasi yoyote ya karibu wakati rais akiapa, lakini pia hata familia za rais wengi wanapoingia madarakani huwa haizifahamiki sawa sawa. [125]
mumewe
Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [126]
na
MBUNGE wa Kwela (CCM), Dk Christant Mzindaka, maarufu kama "mzee wa mabomu", ameibuka bungeni na kueleza kusikitishwa na uzembe uliofanywa na Waziri wa Maliasili, Shamsa Mwangunga kwa kuwaongezea muda wamiliki wa vitalu vya uwinfaji katika hifadhi za taifa kinyume na maagizo ya bunge. [127]
nami
Ndugu yangu nakupa pole sana, yaani ni bora ungewasiliana nami kabla ya kwenda huko, kwani ukweli ni kwamba dawa imegunduliwa nchini na jamaa mmoja tena ni albino, rudi wahi mapema usipoteze muda wako huko,” alimsisitizia. [128]
nao
Mwangia ambaye alifika eneo hilo la ajali muda mfupi anasema kuwa walikuta miili ya abiria ikiwa imekatika katika, lakini walifanikiwa kuwanasua majeruhi wawili ambao nao walikuwa wameumia vibaya kichwa. [129]
naye
Kutokana na malipo ya mafao ya wastaafu hao kushughulikiwa na Wizara ya fedha, Kandoro naye alimuandikia barua waziri Mkulo akimwomba ili kamati ya wastaafu hao kama walivyoomba ikutane na serikali kujadili kwa pamoja malipo yao. [130]
ndilo
Ikiwa suala hilo ndilo ambalo limeshika kasi sana hivi sasa katika nchi yetu, amefanikiwa kufafanua kiundani zaidi na kuyaanika wazi maisha ya Mtanzania halisi ambaye hali yake kiuchumi inazidi kuyumba kila kukicha. [131]
ngumi
Wanachama wa mchezo wa ngumi za ridhaa nchini wamewataka wadau wa mchezo huo kujitokeza kwa wingi katika mkutano ulioitishwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) utafanyika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. [132]
ni
Vile vile, alikemewa vikali kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuigonganisha mihimili miwili, bunge na serikali kwa maana kwamba, akiwa na madaraka ya kiserikali iliyowekwa madarakani na wananchi alipuuzia maagizo ya bunge, ambalo ni mwakilishi wa wananchi katika kutunga sheria za nchi. [133]
nini
Hivi ni kweli Lipumba hajui kama kama tume imeshatoa masanduku, anayepaswa kuyatunza ni msamamizi wa uchaguzi," alihoji na kuendelea " Hata kama masanduku yalikutwa kwa balozi, baada ya kuyakagua polisi walikuta nini ndani yake. [134]
njama
Tena naona ndiyo njama zao za kuwanyima wananchi nafasi ya kusoma. [135]
nyingi
Katika ajali hiyo baadhi ya maiti zilipasuka vichwa na nyingine zilipondeka baadhi ya viungo na kusababisha hali uokoaji kutokana na damu nyingi iliyomwagika na jinsi zilivyoharibiwa. [136]
nzito
SIKU chache baada ya Chama cha Wananchi (CUF), kushindwa katika uchaguzi wa Mbeya Vijijini, mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, ameibua shutuma nzito dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) na kumtaka mwenyekiti wake, Jaji Lewis Makame, ajiuzulu. [137]
ofisi
Kuhusu ulinzi kuimarishwa katika kesi za EPA ni wajibu wa siku zote na ulinzi katika ofisi za serikali ni lazima uimarishwe," alisema Lyamuya. [138]
pale
Hata hivyo kabla ya kutoa leseni serikali iorodheshe maduka na vifaa nyote vinavyo tumiwa na waganga asili/tiba na aina ya tiba wanazotoa ili pale panapotokea jambo lolote linalo kiuka tiba hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao na si wote. [139]
pambano
Yanga inaonekana kujipanga kikamilifu kwa pambano la leo huku viongozi wakisisitiza kwamba wamewaandaa vizuri kisaikolojia wachezaji kwa ajili ya ushindi wa uhakika ili kurahisisha kazi ugenini kwenye marudiano. [140]
pia
Alidai pia maandishi yasiyobishaniwa na yale yanayobishaniwa yaliyoko katika nyaraka mbalimbali yanafanana na ya mshitakiwa wa pili Rajabu Maranda. [141]
picha
Ikabidi kwa kumtia moyo, ikabidi aende kwenye ofisi ambayo alikuwa akifanyia utafiti huo na kufanikiwa kupata picha yake. [142]
pili
Kwa ujumla hoja zote za Dk Mzindakaya ziliungwa mkono na katika kuhitimisha alifuta pendekeo za pili, ambacho kilikuwa kinalitaka bunge limwadhibu Mangunga. [143]
pole
Anawapa pole wafiwa wote waliomtarajia lakini anawaambia kwamba upande wa Bi Elimu mwenyewe, kweli Mwenyezi Mungu amemrehemu maana maumivu yake yalikuwa makali sana na alikuwa anadhoofika siku hadi siku licha ya madaktari wa uongo na kweli waliokuwa wanadai kumtibu. [144]
polisi
Naye Hakimu Lyamuya alipoulizwa kuhusu hilo, alisema askari polisi walifika mahakamani hapo kuimarisha hali ya ulinzi na usalama na kwamba hilo ni jambo la kawaida. [145]
rais
Akizungumza na Mwananchi Mwenyekiti wa Wastaafu hao, Nathaniel Mlaki alisema baada ya kuona hawapewi jibu la kuridhisha na Waziri wa fedha, wameamua kumwandikia barua mkuu huyo wa mkoa wakimtaka awasiliane na rais ili waweze kuonana naye. [146]
redio
Katika tafiti yangu wananchi wengi hupata ahueni mara tu wasikiapo wimbo huu ukiimbwa katika redio mbalimbali hasa wawapo kwenye daladala asubuhi wakielekea makazini, kwani huanzisha mjadala na wengi wanajipa moyo kwamba viongozi wameyasikia. [147]
robo
Akizungumza na Mwananchi, Mkurugenzi wa chama cha mpira wa kikapu mkoani Dar es Salaam (BD), Mbaga Mwambona alisema mpaka sasa timu nane zimefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali katika ligi hiyo inayochezwa kwa muundo wa mashindano huku timu zikigawanywa kwa makundi. [148]
roho
Nakufa, mkuu wa polisi unaniua, sawa mimi nimemuua albino, lakini wewe unaniua mimi kwa kunipiga kibao, imeandika wapi kwamba muharifu apigwe, kabla ya kufikishwa mahakamani,” alisema Kazim huku akikata roho. [149]
safi
Nahisi tatizo linalotukabili si la vitendea kazi, ni ufanisi wa kazi yenyewe na kutotimiza wajibu wetu, nchi yetu ni masikini na hatuna uwezo wa kununua magari ya mamilioni kwa ajili ya kufanyia usafi, lakini kweli hatuwezi kutumia mifagio, kuuwezesha mji wetu kuwa safi," alisema Nahodha. [150]
salaam
Mwenyekiti huyo alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelez, Jijini Dar es salaam, kuelezea kuwa hawahusiki na mauaji ya maalubino. [151]
sana
Alisema mechi hiyo itakuwa ngumu sana kwani wanacheza dhidi ya timu ambayo hawaijui, lakini watahakikisha wanatoka na ushindi mkubwa kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele mechi ya marudiano. [152]
sh
Shirikisho la soka Tanzania limetangaza kiingilio cha sh. [153]
sherehe
Mfano wa hali hii ni uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wa Kenya mwaka jana ambako tukio la uvurugaji matokeo ya uchaguzi lilifanyika waziwazi na kulazimika Rais Mwai Kibaki kutangazwa mshindi huku sherehe za kumwapisha zikianza. [154]
shosti
Leo mwezi unatimia shosti ushajiuliza umefanya nini cha maana? Au wewe ni kati ya wale wanaoka chobiso kuchunguza ya watu wakati yakwao yanawashinda. [155]
si
Kamanda Kenyela alipoulizwa kuhusu sakata hilo, alisema alipigiwa simu na bosi akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake na kuelezwa kuwa hali si shwari mahakamani hapo, lakini aliporudi alikuta watu wote wameshaondoka. [156]
sio
Sababu za matatizo hayo sio tume kwani imefanya kila liwezalo ikiwamo kutoa elimu ya uchaguzi katika vijiji vyote vya Mbeya ambako huenda Lipumba hakufika. [157]
sisi
Hapa kuna sababu nyingine, na sisi tunaungana na watu wanaosema kuwa uchache wa wapigakura umetokana na Chadema kuenguliwa kwenye uchaguzi huo," alisema. [158]
staili
Huu tunasema ni uhuni uliotukuka na tunalaani staili hii ya mashabiki wa Yanga ya kushangilia kizamani. [159]
suala
Akizungumzia suala hilo, Jaji Makame alimpuuza Profesa Lipumba akisema, anongea asichokijua. [160]
tajiri
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [161]
tatu
Mpambano huo kati ya Francis Cheka na Rashid Matumla ëSnake Boyí utakuwa ni wa tatu kuwakutanisha mabondia hao huku Cheka akishinda mawili na matumla akishinda pambano moja. [162]
tena
LIGI ya mpira wa kikapu mkoa wa Dar es Salaam, Kili RBA inaendelea tena leo katika uwanja wa ndani wa Taifa kumakizia mzunguko wa kwanza. [163]
tiba
MWENYEKITI wa Chama cha Utabibu wa dawa za asili nchini, Simba A. Simba ameitaka Serikali kurudisha leseni za waganga zilizofungiwa kwa madai ya kuhusika na mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino) na vikongwe kwa kuwa asilimia 65 ya wananchi nchini wanategemea waganga wa tiba asili. [164]
tu
Zitto alisema kumbukumbu za serikali zinaonyesha kuwa mwaka 2006, walikuwa wametarajia kukusanya Sh15 bilioni lakini walikusanya Sh7 bilioni tu. [165]
uhuni
TFF ikomeshe uhuni huu wa mashabiki. [166]
ukata
Sasa Mkombozi akifanikiwa kuruka vikwazo vyote hivi, anapelekwa kwenye shule za ukata, shule za kukatisha tamaa moja kwa moja wakati akina Aimbora wanazidi kupeta ndani ya shule za wenyenchi. [167]
ukoo
Ya nini kumpa matumaini wakati yeye na ukoo wake wote wameshatolewa nje katika dunia ya leo. [168]
ule
Wewe unakumbuka eeeeenzi za Mwalimu? Wakati ule shule zilizotamba, shule zilizoshindana kwa nguvu zote zilikuwa shule za wananchi. [169]
umri
Mshindi huyo ataiwakilisha Tanzania kwa umri wa miaka chini ya 14 ya Afrika nchini Morocco mbapo katika mashindano hayo hayo washindi wengine wawili kwa kupitia umri wa miaka 16 walipata nafasi kwa ajiri ya michuano ya Afrika itakayo fanyika nchini Morucco. [170]
upya
Ni Top Band Jumamosi hii inajimwaga uwanjani, kukuletea songi mpya na zile ulizozizoea, huku ikiwa imesukwa upya na kuwekwa vionjo ambavyo vitakusababisha wewe na wenzio wawili watatu kutothubutu kuiulizia ilipo itakapofika siku ya wikiendi. [171]
usafi
WAZIRI Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Shamsi Vuai Nahodha, ameahidi kuwa ofisi yake itashirikiana na Baraza la Manispaa ya Zanzibar, kusimamia shughuli za usafi katika manispaa hiyo. [172]
uzinduzi
Alisema mafanikio yaliyoanza kujitokeza baada ya uzinduzi wa kampeni ya usafi wa mji wa Zanzibar, yamedhihirisha kuwa kama watu watajipanga, mji huo unaweza kuwa safi. [173]
vema
Kama msanii ambaye anatambua umuhimu wa elimu ameweza kuelezea matatizo ambayo yanawakabili walimu hasa wa shule za msingi ambao wananyonywa katika mishahara yao na wanashindwa kujiendesha vema kimaisha. [174]
vipi
Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni,” alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [175]
vita
Siku ya wanawake Duniani ilipata msukumo mpya mwaka 1915 yalipofanywa maandamano makubwa huko Bern Switzerland yakishinikiza kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia. [176]
vyake
Kweli wale watu walimuua yule albino na kwenda na viungo vyake kwenye maeneo ya biashara. [177]
vyao
Waishiwa walitingisha vichwa vyao kwa uchungu sana. [178]
waanzishe
Siku moja akiwa nyumbani kwake alifuatwa na watu wawili walikumueleza kuwa waanzishe biashara ya kuchimba madini kama njia ya kupata fedha kwa wingi na kwa haraka. [179]
wala
Alisema ingawa hiyo ndiyo sababu ya msingi, halalamiki kwani Chadema iliondolewa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi na wala isingekuwa vyema tume kukiuka sheria hiyo kwa sababu ya kuuhamasisha uchaguzi huo. [180]
wana
Madega aliwataka wana Yanga kujitokeza kwa wingi uwanjani na kuishangilia timu yao ilikuipa nguvu na morali ya kufanya vizuri na kuiongezea klabu yao mapato. [181]
wanafanya
Na kwa nini wanafanya vizuri. [182]
wangapi
HIVI wangapi mlisikia tangazo la kifo juzi? Mimi nilishtuka kweli. [183]
wao
Mmoja wa mawakili hao, Oscar Msechu alisema jana kuwa wamefikia hatua hiyo ili kuomba mteja wao apunguziwe masharti ya dhamana kwani kiasi cha fedha kilichotakiwa na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ni kikubwa. [184]
wapi
Eti wale akina Aimbora waliosoma shule za kulipia tangu chekechea hadi mwisho wa sekondari sasa wanadai kusoma bure chuoni? Wapi na wapi. [185]
watu
Kamanda Kova aliwataja watu nane waliojeruhiwa waliokuwa katika daladala ni mkazi wa Gongo la Mboto, Saimoni Silvester (27), mkazi wa Mwenge, Karunde Osambi (34), mkazi wa Makongo Juu, Eva Joseph (28). [186]
waume
Badala ya kumsaidia Rais kuwatumikia wananchi, wanadhani nafasi ambayo wanayo waume zao ya kuiongoza nchi ni kwa ajili ya kujinufaisha wao na ndugu zao. [187]
wawapo
Ameelezea vitendo vya walimu wengi kuamua kufanya biashara wawapo makazini kutokana na kipato kidogo wanachokipata ambacho kinashindwa kukidhi mahitaji ya wao na familia zao. [188]
waweze
WASTAAFU wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamemuandikia barua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro wakimtaka awasaidie waweze kuonana na Rais Jakaya Kikwete kupeleka malalamiko yao dhidi ya Waziri wa Fedha Uchumi na Mipango, Mustafa Mkulo. [189]
wazazi
WENGI wanamfahamu kama Gurumo, lakini jina alilopewa na wazazi wake alipozaliwa mwaka 1940 ni Muhidini Mwalimu Mohamedi. [190]
wezi
Wale wezi wenzake walipoona hakuna mawasiliano yoyote kutoka kwa Kazim waliondoka, hawakuwa na habari naye tena. [191]
wimbo
Msanii huyu aliyefanikiwa kufanya vizuri na wimbo wake uliovuma hivi sasa 'Nikipata nauli' ambao amemshirikisha Banana Zorro, Licha ya kushirikishwa katika wimbo wa Salamu zangu mjomba na kumfunika Irene Sanga ambaye alikuwa mtunzi. [192]
yake
Mwangunga aliamriwa kusimamisha vibali vilivyotolewa na wizara yake kwa wawindaji badala ya kuisha mwaka 2012 vifikie ukomo 2010, ili kuanzia hapotaratibu mpya za uwindaji zianze kutekelezwa. [193]
yao
Wengine ni Maiko Maujiro, Agustino Yohana, Elly Athumani, Alfonsi Golesh na wanaume wawili ambao hawakutambuliwa majina yao. [194]
yapo
Mabaki ya daladala hiyo yapo kituo cha Polisi cha Buguruni jijini. [195]
yetu
Wiki ijayo tutalishungulikia suala la usafi wa mji kwa kugawana kazi kati yetu na wafanyakazi wa Baraza la Manispaa ya Zanzibar, mwenyewe nitasimamia kazi hiyo tuone kama hatutaweza," alisema Nahodha. [196]
yuko
Bwana Jamhuri Mwananchi anafurahi kutangaza kwamba Bi Elimu Mkombozi hajafa bali yuko mahututi. [197]
yule
Alisema wapiga kura hao waligoma kupiga kura kwa sababu walimkosa yule waliyetarajia kumchagua ambaye ni mgombea wa chama hicho alienguliwa katika kinyang'anyiro hicho Sambwee Shitambala. [198]
zaidi
Kwa mujibu wa Profesa Lipumba, Daftari la wapigakura lilikuwa na udhaifu mkubwa uliojitokeza kwa majina ya watu waliofariki dunia kuendelea kuwepo na wengine kujiandikisha zaidi ya mara moja. [199]
zile
Nililetewa nyaraka mbalimbali nizichunguze zikiwemo zile ziizokuwa zinabishaniwa na zisizobishaniwa na nimegundua kuwa sahihi ya Mahingira iligushiwa," alidai Othman. [200]