Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-27

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
aende
Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [2]
afe
Si bora afe tujue moja. [3]
aina
BAADA ya Rais Jakaya Kikwete kusema kuwa, wanaobeza maendeleo yaliyoletwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ni walevi wa pombe ya kienyeji aina ya tende, Chama cha Wananchi (CUF), kimesema amekikejeli kwa wananchi na kumtaka asipime maendeleo kwa kuangalia barabara, bali maisha ya watu. [4]
akawa
Najua bado kuna watu ambao wanaamini viongozi tumemzuia Ngassa kujiunga na timu hiyo, lakini si kweli kwani haiwezekani wakala akawa anazungumza na vyombo vya habari tu bila sisi kujua. [5]
akina
Sawasawa wakati akina Mkombozi wanasota kwa mguu. [6]
akisema
Juzi rais Kikwete alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa wanaobeza maendeleo yaliyoletwa na SMZ na Serikali ya Muungano kuwa ni walevi wa pombe ya kienyeji aina ya tende. [7]
albino
Nyumbani kwake hapo alikuwa akiishi na watu kadhaa akiwemo jamaa mmoja ambaye ni mwenye ulemavu wa ngono yaani albino. [8]
alikwenda
Baada ya kuhitimu alikwenda kufundisha Butimba. [9]
ama
Unajua wasituendeshe, kama wanaona hatufai na wanataka kutubagua, waache kutuita kwenye mikutano yao, ama tusiripoti kabisa mechi hii, lakini si kutuwekea vikwazo vya kadi. [10]
amani
Licha ya kuwepo mgongano katika mchakato mzima wa kinyang’anyiro hicho, tunawashukuru wananchi wa Mbeya Vijijini kwa kumaliza uchaguzi huo bila vurugu za kutishia amani, maisha na uharibifu wa mali kama ilivyowahi kutokea katika majimbo mengine. [11]
ambao
Alisema wataalam hao ambao hupelekwa sehemu mbalimbali nchini, huwasaidia wananchi wa kawaida kuanziasha vikundi na miradi ya maendeleo ili waweze kujikimu na maisha. [12]
anatakiwa
Madega alisema taarifa zilizopo ni kwamba mchezaji huyo anatakiwa na klabu ya Lov-ham ya Norway kwa ajili ya majaribio ya wiki moja. [13]
au
Tunataka atueleze kama kampuni iliyonunua Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira ni yake, mkewe, watoto wake na rafiki yake Yona au la?" alihoji Dk Slaa. [14]
bado
Lipumba alituhumu kuwa ikiwa ni miaka nane sasa tangu kutokkea kwa maafa hayo, bado tume za uchaguzi zinaendelea kujenga mazingira ya kutokuwa na chaguzi huru na za haki. [15]
baina
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema kukwamishwa kwa juhudi za kuleta mwafaka baina yao na CCM Zanzibar kwa mara ya tatu, ili kuepusha maafa kama yalitokea Januari 26 na 27 mwaka 2001 kisiwani Pemba, ni ishara tosha kwamba Chama hicho hakikujifunza chochote kutokana na maafa hayo. [16]
bandari
Alisema zoezi hilo la dharula litaanza kufuatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kuagiza kupunguza msongamano wa makontena ili kuirejesha bandari hiyo kuwa katika hali yake ya awali. [17]
baraza
Augustine, Dk Charles Kitima kwenye warsha ya baraza na wahariri wa vyombo vya habari iliyofanyika hivi karibuni, Dar es Salaam. [18]
baya
Mambo ya usiku wanapolala wazazi hayazuiliki, na watoto hawa wanatabia moja ya kujifunza kila jambo liwe zuri au baya, ni jukumu letu sisi wazazi kuhakikisha hatutoi nafasi yoyote kwa watoto hawa kwani kosa moja dogo linaweza kuzaa goli litakaloweza kuharibu mwenendo mzima wa maisha ya watoto wetu. [19]
bila
Alikumbusha kuwa, ahadi ya hayati Mzee Abeid Amani Karume kwa Wazanzibari kuhusu kupata elimu, maji na afya bila ya malipo ilikufa pamoja naye, kwani mpaka sasa hakuna hata kimoja kati ya hivyo kinachotolewa bila ya malipo. [20]
es
Alalamika kuwa, kuna tatizo kubwa la kiutendaji ndani ya tume, kwani watendaji wake waandamizi wako Dar es Salaam badala ya kuwepo maeneo yote ya wapigakura ili kubaini matatizo hayo mapema. [21]
faida
Hayo ndiyo tunayotaka kusikia kwa faida ya wananchi, kwani ni haki kujua," alisema Dk Slaa. [22]
fani
Aliongeza kuwa wizara hiyo pia inajivunia idadi kubwa ya vyuo tisa vya ustawi wa jamii na 53 vya maendeleo ya wananchi vilivyopo nchini, ambavyo husaidia kutoa wataalam katika fani za maendeleo ya jamii. [23]
gani
Tutafanya nao mazungumo tukubaliana ni kiasi gani aweze kuuzwa, sisi hatutaki ubabaishaji hapa kama kuna mchezaji anatakiwa ni lazima klabu ijue na sheria zifuatwe," alisisitiza Madega. [24]
ghafla
Wakishapewa mikopo wale waliosomeshwa shule za wenyenchi kuanzia chekechea, hao ndio walazimishwe kuthibitisha kwamba baba zao wamekuwa maskini ghafla baada ya kulipa miaka yote ile. [25]
hajui
Wakizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, viongozi wa ngazi za juu wa CUF walisema, Rais Kikwete hajui maana ya maendeleo kwa kuwa anayapima kwa kutumia barabara badala ya kuangalia maisha ya watu. [26]
hapa
Tabia ya baba kutosahihishwa ndiyo imetufikisha hapa tulipo," alisema Dk Slaa. [27]
hapo
Kwa mfano katika kijiji cha Ikukwa ilikuwa ni siku ya chama chetu kufanya mkutano hapo na CCM ikawa na ratiba katika eneo hilo. [28]
hasa
Alisema hatua ya askofu huyo na viongozi wengine wa dini hasa makanisa si sahihi, kwani inaendeleza utaratibu wa zamani wa kutomwonya au kumwambia ukweli mkubwa anapokosea. [29]
hata
Mwenyekiti huyo alibainisha matatizo yaliyojitokeza siku ya kupiga kura kuwa ni pamoja na vituo vingi kutokuwa na majina ya wapigakura na kwamba, hata sehemu ambayo yalibandikwa hayakuwa sahihi. [30]
hawa
Tena kibaya zaidi ni wapinzani hawa wanapokuwa hawasikilizwi hata pale wanapokosoa mambo ambayo yanaonekana dhahiri kuwa yanaweza kulipeleka taifa pabaya. [31]
hii
SMZ, CCM na ZEC hawakutosheka na maafa ya Januari 2001 na sasa wameamua kuanaandaa janga jingine, ambalo lazima Watanzania walipinge na walizuie kwa nguvu zao zote lakini sisi Chama cha CUF tunachukua fursa hii kuungana na kila raia wa nchi hii kuomboleza maafa haya ambayo yameendelea kuwa aibu kubwa kwa taifa letu" alisema. [32]
hili
Sisi hatumchukii ila tunataka kujua ukweli, kama alipokuwa Ikulu, akiwa Rais wa taifa hili alifanya biashara na kuuza mali ya Watanzania. [33]
hivi
Awali Katibu mtendaji wa Chama cha wakulima cha KCGA na RCGA Gracian Madafu alililieleza gazeti hili kuwa hivi karibuni kumezuka migogoro kwa wakulima inayosababishwa na SBT kwa kusimamia usajili wa utitiri wa vyama visivyo na wanachama kinyume na makubaliano. [34]
hiyo
Mwananchi wa Kijiji cha Msituni, Kata ya Iwindi, Ezekieli John alituambia kwamba hawezi kupiga kura kwa sababu shahada yake ilichukuliwa na balozi wa nyumba kumi na taarifa hiyo tumeipeleka polisi," alilalamika Profesa Lipumba. [35]
hizi
Lakini sisi tumeshazishtukia kauli hizi ni za kilaghai, zinalenga na kujipendekeza kwa SMZ na Rais Amani ili wanyonye petroli yetu, hatukubali," alidai Duni. [36]
hizo
Alisema rais kapotoka na anapaswa kujirekebisha kwa kuwa yeye kama kiongozi wa Watanzania wote, hapaswi kutoa kauli za kejeli na kinafiki kama hizo. [37]
hofu
Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana, wakati akitoa maoni kuhusu kauli ya Mkapa aliyotoa mkoani Iringa Jumapili iliyopita, akiwaonya wanasiasa kuacha fitina, chuki, majungu, udini na ukabila kwa hofu kwamba nchi inaweza kuingia katika machafuko. [38]
hospitali
Alihangahaika kwenye hospitali nyingi bila mafanikio. [39]
huku
Aidha kimeitaka serikali ya Jamhuri ya Muungano Iseme basi kwa ukandamizaji wa haki za binaadamu huku kikiitaka tume za ucvhaguzi kusema basi kusimamia chaguzi zisizokidhi viwango vya demokrasia kwa maslahi ya wachache. [40]
humo
Naye Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alisema, malengo ya ziara ya Kikwete visiwani humo mwaka huu ni kuwakejeli wananchi na si vinginevyo. [41]
huru
Profesa Lipumba alisema kuwa, kuna umuhimu mkubwa wa kuwepo kwa tume huru ambayo itaweza kufanya kazi kwa kuhakikisha inafika maeneo ya vijijini ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya uraia ili wananchi wote wapate haki ya kupiga kura. [42]
huu
Zaidi ya hayo nashangaa kwa nini azungumzie hayo wakati huu anapokabiliwa na tuhuma za kufanya biashara Ikulu," alisema Dk Slaa. [43]
huwa
Pia, Madega aliongeza kuwa Yanga si Academia ambayo inakuza vipaji vya wachezaji bali inapokuwa ikisajili huwa inazingatia zaidi maslai yake na kuendelea kufanya vizuri kwenye michezo yake. [44]
huyu
Kwanza ya yote kuna vitu shostito vya kuangalia; huyu mtu anakuheshimu kiasi gani anakupenda kiasi gani na anakujali kiasi gani. [45]
ila
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa amesema hakuna Mtanzania anayemchukia Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, ila malalamiko yao dhidi yake ni kutaka kujua ukweli kuhusu mambo yanayomhusu. [46]
ile
Aliponda kwamba, serikali ya Muungano na ile ya Zanzibar haijafanya chochote kwa fedha zao na kwamba hata barabara zinazosemwa zimejengwa kwa fedha za wahisani. [47]
ili
Alisema kuwa kwa sasa wanaandaa utaratibu wa kuwasiliana na wanasheria wa chama chao ili kupata ushauri wa hatua za kuchukuliwa. [48]
ina
Naye Meneja Masoko wa Coca Cola, Alpha Joseph alisema kampuni yao ina nia ya dhati ya kuwaendeleza vijana kisoka katika ngazi mbalimbali kuanzia Wilaya hadi kimataifa ili kuweza kuiletea sifa Tanzania kwa kupata vipaji vya kutosha vya soka. [49]
ingawa
Madhara haya tunayatengeneza wenyewe bila kujua na wakati mwingine kwa kujua, ingawa kwa familia zingine kunasababishwa na hali ya kipato—kwa maana ya kushindwa kuwa na nafasi ya kutosha katika nyumba ya kuwatenganisha wasichana na wavulana. [50]
ipo
Aliishutumu kauli za Kikwete kuwa ni za kilaghai na kwamba, zinalenga kujipendekeza kwa SMZ na Rais Amani Karume ili petroli ambayo ipo Zanzibar iweze kunyonywa na upande mmoja wa Muungano. [51]
itacheza
Ghana sasa itacheza na mshindi wa pili wa Kundi B, wakati Cameroon itacheza na mshindi wa kundi hilo. [52]
iwe
Ninachosubiri kwenda Norway, iwe ni majaribio au mkataba ila nataka kucheza Ulaya hiyo ni ndoto yangu. [53]
japo
Sio kweli kuwa kumpekuwa ni kumdhibiti na si kweli kuwa wanaume hawapekuliwi, kwa kuwa japo wengine wanadai hawajali lakini najua japo kwa siri au kwa kujua au kutokujua wanapekua. [54]
juu
Hizo siasa za chuki, majungu, fitina, ukabila na udini zitaisha akiwaweka wazi Watanzania juu ya umiliki wa Mgodi wa Kiwira. [55]
juzi
Huko Nungwi alikopewa kofia ya kiua juzi kaulizwa swali mbele ya wananchi kwamba, kuna hoteli nyingi za kitalii, lakini mbona wafanyakazi wote wanatoka Kenya na Uganda kwa sababu ya elimu? Lakini hakujibu. [56]
kabisa
Mwafaka uliofikiwa baina ya vyama vya CUF na CCM baada ya maafa haya, ulikusudia kukimaliza kama si kukizika kabisa chanzo cha maafa hayo lakini CCM hawakuta kuheshimu" alisema. [57]
kabla
Aliongeza kuwa, wananchi wa Tanzania wanataka kusikia kauli ya rais huyo mstaafu, kwa kuwa mgodi wa Kiwira ulikuwa ni mali yao kabla ya kuuzwa. [58]
kaka
Mzazi mmoja ameniambia jambo moja lililonisikitisha kuwa watoto wawili ndugu mtu na kaka yake mmoja mwenye umri wa miaka 12, na mwingine 13 wamepeana mimba bila wenyewe kujua, yule binti mwenye miaka 12 ameulizwa akasema yeye hajui lakini amekuwa akifanya mchezo huo na kaka yake. [59]
kama
Alisema kwa kitendo kama hicho makanisa yanaweza kufika pabaya, kwa kurukia mambo na kusifu watu wakimezea mate michango ya fedha. [60]
kanisa
Mkapa alinukuliwa na vyombo vya habari jana akizungumza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Walolesi la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Iringa alipokaribishwa na Askofu Dayosisi hiyo, Dk Owdenburg Mdegella kuwasalimia waumini. [61]
kansa
Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [62]
kavu
Aidha alisema kuwa licha ya zoezi hilo kuwepo ni lazima wenye mizigo wachangie kiasi kidogo cha fedha ili kuwezesha kuhamisha makontena hayo hadi kwenye bandari kavu (ICDs) na kwamba gharama hizo zimeangaliwa kwa umakini. [63]
kazini
Mwanga alitunga vitabu vyote kwa Kiingereza, lakini bado hakuacha msimamo wake kwamba Kiswahili kina nafasi kubwa katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora kwa sababu ndiyo lugha wanayoifahamu zaidi na ndiyo inayotumiwa wanapokuwa kazini. [64]
kibao
Unafikiri wale waliokatika shule za ukata wanaweza kushindana na wale wanaotoa mamilioni kwa ajili ya shule ya wanafunzi wachache na walimu kibao, na kufanya tuisheni juu mpaka wanaweza kufaulu bila hata kuelewa kitu. [65]
kidogo
Hii ni kusema kwamba hawakujifunza hata kidogo kwa yale ambayo Serikali yake iliyafanya mwaka 200" alisema profesa Lipumba. [66]
kikao
Imefafanua kwamba kikao hicho kitatanguluwa na kikao cha Asasi ya Kisiasa, Amani na Usalama ya SADC, ambacho kitakutanisha nchi tatu wananchama wa Asasi hiyo chini ya uenyekiti wa swaziland. [67]
kila
Tatizo hapa ni wananchi, hawafahamu kuwa maisha bora yanatafutwa na wao wenyewe, ndiyo maana kila wakati wanailaumu serikali badala ya kujenga hoja za kuishinikiza kuwajenga mazingira yatakayowezesha kupata maisha bora kwao. [68]
kisasa
Wafadhili hao pia wasaidie vifaa vya michezo vya kisasa zaidi ikiwa pamoja na kuwawezesha wachezaji kukaa kambini kwa muda mrefu zaidi kwa ajili ya mafunzo. [69]
kitabu
Alipokuwa anahitimu shahada yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1971, Mwanga aliandika tasnifu ambayo mhadhiri wake Prof John Higgins alipendekeza iwe kitabu. [70]
kiua
Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Juma Duni Haji, alihoji kama maendeleo yanapimwa kwa kuangalia barabara na kuvalishwa kofia ya kiua (maua) na wananchi wa Nungwi basi wanampongeza rais. [71]
kiume
Mara nyingi nimekuwa nikibuni mavazi ya kike na ya kiume na hata mavazi ya watoto, yote yakiwa na mitindo tofauti tofauti tena kwa kutumia vitu vya asili na vitambaa vya jinja, kaniki nk. [72]
kocha
Wakati Yanga ikitaraji kuibuka na ushindi kesho kocha wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga amekataa na kusema kuwa Yanga lazima wapigwe tu. [73]
kombe
Rwanda imemaliza ikiwa na pointi nne bado niweza kufuzu kwa kombe la Dunia endapo Misri itawafunga vinara wa Kundi B, Afrika Kusini na Nigeria ikifungwa na Ivory Coast. [74]
kote
Pia Waziri Sitta alisema kutokana na juhudi za wizara yake, vyama vya kuweka na kukopa (Saccos) nchini kote vimeonyesha kuleta mafanikio na maendeleo ya hali ya juu kwa jamii kuliko kutumia benki. [75]
kuandaa
Ni jambo lililo wazi kuwa asilimia kubwa ya wachezaji wa kikapu nchini ni wanafunzi ambao katika hali ya kujifunza wanakuwa wepesi kuelewa, Hivyo kama BD na TBF watajipanga vizuri na kuandaa mikakati ya kueleweka, ni wazi kuwa watapata wadhamini ambao watauendeleza mchezo huo. [76]
kuanza
Wakati huo huo, kesi ya wizi wa fedha za EPA, inayowakabili, Farijala Hussein na Rajabu Maranda inatarajiwa kuanza kusikilizwa leo katika mahakama hiyo. [77]
kubuni
Malengo yangu ya baadaye ni kuwa mbunifu mwenye mafanikio makubwa kwa kubuni nguo zitakazoweza kushindana kwenye soko nje ya Afrika. [78]
kubwa
Profesa Ibrahim alisema kuwa, tatizo kubwa ambalo ndilo lililochangia watu wachache kutojitokeza kupiga kura ni watendaji wa vijiji na kata kuzuia shahada za wapigakura kwa kisingizio cha kuwapa vocha za mbolea ya ruzuku. [79]
kufa
Mwanga aliyewahi kuwa rais wa kwanza wa Chama cha Wachapishaji Vitabu nchini (PATA) hakuacha kusema hadharani sononeko lake kuhusu mabadiliko ya fani ya uchapishaji vitabu kufuatia kuanzishwa kwa sera ya vitabu vya kiada ya mwaka 1991 na kuibuka kwa utandawazi vitu vilivyochangia kufa kwa wachapishaji wazawa waliokuwa wakiheshimika na hata kuwa na kipato kizuri siku za nyuma. [80]
kuishi
Nyota hao walitoa mafunzo ya mchezo huo na kuwahamasisha vijana kuishi kwa kujiamini pamoja na kutambua afya zao. [81]
kuja
Alipoisoma akaniambia hii tasnifu inaweza kuja kuwa kitabu kama nitakiongeza zaidi maelezo," alisema Mwanga na kuongeza. [82]
kulala
Na ndio maana mwaka mmoja na miezi minne baadaye Mwenyezi Mungu amemwita kwenda kulala katika nyumba ya milele. [83]
kule
Watu kama mawaziri, wakuu wa wilaya na wabunge wanapohangaika kweli kweli kuwa wajumbe wa NEC wanatafuta nini kule?" alihoji na kuongeza. [84]
kumpa
Akademiki Mwenyenchi ambaye inasemekana alikuwa anaona hakuna haja ya kumpa Bi Elimu hata punje ya mchele na badala yake achukue chakula chote yeye mwenyewe. [85]
kumuua
Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [86]
kundi
Ghana iliwafunga wenyeji Rwanda 2-0 na kumaliza vinara wa kundi wakiwa na pointi saba huku Cameroon iliwafungasha vilago Mali 3-0 na kufikisha pointi tano. [87]
kupitia
Kuweka fedha kupitia Saccos inasaidia zaidi kuliko kuziweka benki, hivyo kutokana na hali hiyo tunahimiza jamii kujiunga kwa wingi katika vikundi vya kuweka na kukopa," alisema Sitta. [88]
kupokea
Wakati ule shule ilikuwa shule na chuo ilikuwa chuo, si choo cha kupokea uchafu wowote. [89]
kusaka
Akielezea kuhusu maafisa maendeleo ya jamii katika wizara yake, alisema maafisa wanaokaa ofisini wakati wote hawafai katika juhudi za kusaka maendeleo ya jamii katika ngazi ya mkoa, wilaya, tarafa, kata hadi vijijini, hivyo wanapaswa kuwajibishwa. [90]
kusoma
Anesema baada ya kumalizika kwa mkataba wake aliamua kuanza kusoma kozi mbalimbali za ukocha lakini pia akitafuta kazi nyingine tofauti na ukocha ili aweze kujikim kimaisha. [91]
kuua
Ni suala la kawaida kuua albino na damu zao au viungo vyao tunavitumia kwenye shughuli hizo za uchimbaji madini na uvuvi, watu wengi wanafanya hivyo. [92]
kwake
Alisema, hiyo yote ni kwa kuwa CCM ilihisi kuwa utekelezwaji wa mwafaka haukuwa na maslahi kwake viongozi wa Serikali wakaanza kuhujumu hatua kwa hatua na hatimaye wakauvunja kkabisa. [93]
la
WAKATI Tume ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini ikimtangaza mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mchungaji Luckson Mwanjali kuwa mshindi, Chama cha Wananchi (CUF), kimeyakataa matokeo hayo. [94]
lake
Mpongoliana alisema mwezi Machi, 2005 alichaguliwa kuwa mjumbe wa nyumba kumi na kwamba, moja ya majukumu aliyopewa ni kuwatambua wakazi wa eneo lake. [95]
langu
Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni,” alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [96]
lazima
Yule Askofu wa Iringa aliyemtetea Mkapa kuwa anazushiwa, lazima awaombe radhi Watanzania, kwa sababu amewakosea," alisema Dk Slaa. [97]
lengo
Kuanzia mwaka jana (2008) nimeanza kufanya maonyesho ya mavazi yangu mwenyewe ambapo huwa nawaalika wabunifu wengine kuonyesha kazi zao lengo likiwa ni kuwajulisha wa Tanzania kazi zetu tunazobuni" anasema. [98]
leo
Baba kutoambiwa akikosea hiyo ni tabia ya zamani na mbaya, haifai katika ulimwengu wa leo. [99]
ligi
Timu hiyo inashikiria nafasi ya 12 ikiwa na pointi 34 kwenye msimamo wa ligi wenye timu 16 za daraja la kwanza. [100]
likiwa
Baraza lilianzishwa mwaka 1980 likiwa na dhima ya kuratibu na kuviwezesha vyuo na wadau kuendeleza sekta ya elimu ya juu kwa nchi za Afrika Mashariki. [101]
lina
Kwa sasa likifanya kazi zake kama chombo cha Umoja wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC), baraza lina vyuo wanachama 66 kutoka nchi za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda. [102]
lingine
BAADA ya kuandika kuhusu runinga zinavyoharibu watoto, wapenzi wasomaji wa safu hii wamenikumbusha jambo lingine ambalo sikuwahi kuligusia kabisa. [103]
mahiri
Mafanikio hayo ni pamoja na ziara ya wachezaji mahiri wa Ligi ya kikapu nchini Marekani (NBA) Jennifer Azzi na Matt Bonner wanaotokea Klabu ya San Antonio Spurs. [104]
makusudi
Uchaguzi wa mwanzo wa 1995 ulitawaliwa na mapungufu ya makusudi na ukamalizika kwa tume ya Zanzibar (ZEC) kulazimisha ushindi kwa Dkt. [105]
mauaji
Kwenye gazeti moja liliandika kichwa cha habari kikubwa kuwa ”Siri ya mauaji ya albino yafichuka, ni kiungo kimoja kuuzwa milioni 100”...alisoma taarifa hiyo na kusema kama gazeti limeandika hivi bila shaka kuna ukweli dhidi ya madai haya kwamba mtu anaweza kuwa tajiri kwa kutumia viungo vya binadamu. [106]
mbali
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbali mbali kuhusu winga huyo kutakiwa na klabu Lov-ham ya nchini Norway, lakini uongozi wa Yanga hautaki kutoa ruhusa kwa nyota huyo kwa sababu kemkem. [107]
mbele
Alifafanua kuwa anayepaswa kujisafisha mwenyewe mbele ya watu aliowaongoza ni Mkapa na si askofu huyo. [108]
mbunifu
Huyu ni Fatma Amour, mbunifu mahiri wa mitindo hapa nchini. [109]
mfumo
WAKATI Kampuni ya Vinywaji baridi ya Cocacola ikizindua mashindano yake kwa Sh450milioni, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, BMT, Iddi Kipingu amesema elimu ya soka wanayopatiwa wachezaji iandane sambamba na ya kitaaluma ili kuleta mabadiliko ya mfumo wa soka hapa nchini. [110]
mfupi
Baadhi ya wasomaji walionipigia simu na wengine kunitumia ujumbe mfupi wameniambia ni vyema nikawakumbusha wazazi juu ya madhara yanayosababishwa na kuwalaza watoto wa jinsia tofauti katika chumba kimoja. [111]
mguu
Mziba amezaliwa miaka 47 iliyopita mkoa wa Kigoma ambapo alinza kucheza soka akiwa shule ya msingi mwanzoni mwa miaka ya 70 na alisitaafu kucheza soka mwaka 1997 baada ya kusumbuliwa na matatizo ya goti la mguu wa kushoto ambalo aliumia mwaka 1989 katika mechi iliyo zikutanisha timu za Yanga na AFC Leopard ya Kenya iliyopigwa katika uwanja wa Shekh Amli Abed jijini Arusha. [112]
miezi
Akizungumza na waandishi Habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Forodha nchini, Otieno Igogo, alisema pamoja na makubaliano ya kupunguza msongamano huo, watahakikisha kuwa msongamano huo umekwisha ndani ya miezi mitatu kuanzia Januari 26 mwaka huu. [113]
mikoa
Katika hatua nyingine Rais Kikwete amevunja rekodi ya kuwa rais wa kwanza kukamilisha ziara ya mikoa yote 26 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi kifupi cha miaka mitatu tangu alipoingia madarakani. [114]
mimi
Wakala ataendelea kujadiliana na uongozi na mimi nitaambiwa mwisho kabisa. [115]
minne
Mchezo huo ambao utakuwa ni mmoja wa michezo minne tu ambayo Yanga itahitaji kushinda ili itangaze ubingwa mapema wakati pia mchezo wa leo utakuwa ni moja ya maandalizi kwa watoto hao wa Jangwani kabla ya kuivaa Etoile d'Or Mirontsy ya Comoro kwenye michuano ya Afrika. [116]
mitatu
Hoja hiyo ilitolewa jana na waziri huyo, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo kuzungumzia mafanikio ya wizara yake kwa muda wa miaka mitatu ikiwa katika Serikali ya awamu ya nne. [117]
miti
KWA kawaida amekuwa akibuni mavazi kwa kutumia magamba ya miti, ngozi, vipande vya magunia huku akinakshi kwa kutumia urembo wa asili. [118]
miwa
Akizungumza na mwananchi jijini Dar es salaam jana Mligwa alisema sera ya serikali kuhusu suala la miwa ipo wazi hivyo SBT inatakiwa kufuata majukumu yake kama vile kuhakikisha kuwa inasimamia udhibiti wa Sukari ndani na nje ya nchi pamoja na maslahi ya wakulima na wenyeviwanda bila kuchochea mgogoro wowote. [119]
mjumbe
Shahidi huyo, Nestory Mpongoliana ambaye ni mjumbe wa nyumba kumi, Mburahati Kigogo alikuwa akitoa ushahidi jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. [120]
mke
Katika mtazamo wa kiume wenyewe wanasema inawezekana kumpenda mke wangu lakini nikamtamani Heriet lakini hili halina maana kuwa ni Heriet nataka kuwa naye, bali mke wangu. [121]
mno
Kwetu sisi hapa Afrika, hali ni tofauti mno, mke huwa hapewi nafasi yoyote ya karibu wakati rais akiapa, lakini pia hata familia za rais wengi wanapoingia madarakani huwa haizifahamiki sawa sawa. [122]
mpango
Hata hivyo kwa mujibu wa Dk Kitima ambaye ni mmoja wa wajumbe wanaosimamia mpango huo, vyuo vikuu bado vinasuasua kutekeleza mpango hasa eneo la udhibiti wa ubora kwa chuo kimoja kimoja. [123]
mrefu
Tunashangaa jinsi Tume ya Uchaguzi (NEC) inavyozembea kwenye usimamizi wa taratibu za uchaguzi na hasa kutunza masanduku ya kupigia kura, hali inayotafsiriwa kwamba, tume hiyo inakula njama za makusudi kukisaidia chama tawala, kwani tatizo hilo ni la muda mrefu. [124]
muda
Anachofanya ni kujaribu kupoteza muda na kuwapamba wananchi wasahau hoja ya msingi iliyopo sasa," alisema Dk Slaa. [125]
mumewe
Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [126]
mwaka
Duni alisema Januari 30, mwaka huu watafanya mkutano mkubwa katika viwanja vya Kibanda Maiti, Zanzibar ambako wanakusudia kumwelewesha Rais Kikwete maana ya maendeleo. [127]
na
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya matokeo ya awali kutangazwa, Mwenyekiti wa CUF, Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba alisema chama chake hakiyatambui matokeo hayo kutokana na kuwepo kwa kasoro nyingi kuanzia wakati wa kampeni na siku ya upigaji kura. [128]
nami
Nilimjua kama mchapakazi aliyejua kutofautisha kati ya maslahi binafsi na yale ya umma," anasema Wassira alipozungumza nami kwa njia ya simu. [129]
nani
Na baada ya kugoma, nani kafukuzwa sasa? Ni wananchi wakati wenyenchi wanazidi kupeta. [130]
nao
Alisema, uchaguzi wa 2005 nao ulifuata mkondo wa chaguzi mbili zilizotangulia na kwamba kilichozuia maafa yasitokee mwaka huo ni busara za uongozi wa CUF na sio serikali ya jamhuri ya muungano chini ya rais mstaafu Mkapa. [131]
nayo
Lakini pamoja na changamoto ya bei tunayokabiliana nayo katika soko la dunia, tunatoa pia changamoto kwa viwanda vyetu nchini kuzalisha bidhaa zenye ubora na za aina mbalimbali na si kuzalisha kanga na vitenge pekee, alisema. [132]
ndio
Herve alisema analazimika kufanya kazi ya ziada kukabiliana na muda uliopo na mechi yao ya ufunguzi dhidi ya wenyeji ndio inampa presha zaidi. [133]
ndoto
Naye Mrisho Ngassa alipoulizwa kuhusu hilo alisema yeye kwa sasa ameliacha suala hilo kwa wakala wake wajadiliane na uongozi wa Yanga kufanikisha ndoto yake ya kucheza Ulaya. [134]
ngumu
Kazi yangu inakuwa ngumu sana ila wakirudi muda wowote milango ipo wazi na ningekuwa mwenye furaha zaidi. [135]
ni
Alisema matatizo ya awali ni pamoja na kampeni za CUF kuingiliwa na viongozi wa kampeni na kutoa mfano kuwa, katika kata ya Ikukwa baada ya chama hicho kufanya mkutano wao, CCM walitumia watu hao hao waliokuwa katika mkutano huo, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa kampeni za uchaguzi. [136]
nilikuwa
Mimi wakati huo nilikuwa mkuu wa mkoa wa Mara. [137]
nk
Kwa waliopitia elimu ya sekondari hasa miaka ya 1980 na 1990 hawakosi kukumbuka vitabu kama ‘Mastering 40 English Structures’, 'English for Secondary Schools’ na ‘English Tenses' nk. [138]
ofisi
Baada ya kufuzu nilifanya kazi katika ofisi mbalimbali kama katibu muhtasi, lakini kutokana na maslahi duni niliamua kuachana na kazi za kuajiriwa na kujiajiri mwenyewe," anasema. [139]
pale
Alisema kuwa siasa za chuki, majungu, fitina, ukabila na udini anaozungumzia Mkapa utaisha pale atakapowaweka wazi Watanzania kuhusu tuhuma zinazomkabili. [140]
pekee
Alisema njia pekee ni wananchi kuibana Serikali ili iweze kujenga mazingira ya kuwauwezesha kupata maisha bora badala ya kufikiria jinsi watakavyoyapata na kuilamu serikali. [141]
pia
Dk Slaa pia alimtaka Askofu Mdegella kuwaomba radhi Watanzania kwa kitendo chake cha kumtetea na kumsifu Mkapa. [142]
picha
Alisema kuwa matatizo mengine ni pamoja na kupigwa kwa mwanachama wao na wafuasi wa CCM, kushushiwa bendera pamoja na kuchana picha ya mgombea wao. [143]
pili
Akitoa ushahidi wiki iliyopita, shahidi wa pili katika kesi hiyo ambaye ni Msajili Msaidizi wa Wakala wa Usajili wa Makampuni (Brela), Andrew Mkapa alisema Jaffar Hussein Jaffar aliorodheshwa katika jalada la usajili wa kampuni ya Rashhaz kama mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo. [144]
rais
Hatumchukii Mkapa, hakuna mtu anayemchukia, yeye ni rais mstaafu, tunachotaka ni kuwa aache blaablaa za kupotosha hoja. [145]
saa
Uwaziri ni nafasi nzito, walijari, saa mbili baadaye taarifa ikarushwa kwenye vituo vingi vya redio na televisheni kuwa mvumbuzi wa dawa ya kansa ya moyo na damu kwa ujumla, anatafutwa na waziri, atakayemkuta awasiliane na waziri haraka iwezekanavyo au afike hospitali kuu ya taifa. [146]
sana
Tuna ari kubwa tunajua tuko ugenini na mambo yanaweza kuwa mgumu, lakini uwanja huo tumeuzoea ni kama wa Manungu hivyo lolote linaweza kutokea, Yanga hawatishi sana tunajua wanaongoza ligi, sisi tumekuja kushindana hivyo tuna uwezo wa kuwafunga. [147]
sauti
Sikiliza Kazim, usinitukane tafadhari, mimi ni mtu mwenye heshima zangu, nakusaidia tu, usiniletee shida, kama vipi rudi kule India tuone kama utapona, kosa langu ni nini?” alijibu waziri kwa sauti ya hasira. [148]
sekta
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na wadau wa sekta ya nguo nchini, Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. [149]
sherehe
Mfano wa hali hii ni uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wa Kenya mwaka jana ambako tukio la uvurugaji matokeo ya uchaguzi lilifanyika waziwazi na kulazimika Rais Mwai Kibaki kutangazwa mshindi huku sherehe za kumwapisha zikianza. [150]
shule
Mashindano haya ambayo ni ya tatu kufanyika yataanzia ngazi ya Wilaya,Mkoa na baadae Taifa yanatarajia kuanza mwezi ujao katika ngazi ya Wilaya na fomu hizo zitajazwa na wachezaji wa shule za Sekondari, shule maalum za soka nchini pamoja na timu za mitaani. [151]
si
Unajua, tume haiwezi kumwadhibu mkurugenzi wa wilaya ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi kwa kuwa yeye si mwajiriwa wa tume, bali ni mkubwa wake wa kisiasa ambaye ni mkuu wa Wilaya ambaye ana uwezo kumshawishi atakavyo, ikiwamo kuhakikisha CCM inapata ushindi," alisema. [152]
sijui
Ni vyema pia kwa wazazi kutopuuza kila jambo mfano unakuta baba na mama wanalala na mtoto wao wa miaka mitatu na kuendelea, sijui hapa unatarajia nini kama si kujifunza mambo tofauti. [153]
sio
Salmin Amour na uchaguzi wa 2000 sio tu kuwa ulitawaliwa na mapungufu, bali ulivuuka vipimo vya chini vya chaguzi, kiasi ya kwamba waangalizi wa ndani na nje waliuita ‘aibu kwa demokrasia" alisema Profesa Lipumba. [154]
sisi
Lakini cha kushangaza tulipomaliza mkutano wetu na wao wakaingia na kufanya mkutano katika eneo hilo hilo ambalo sisi tulikuwa tumewakusanya watu," alilalamika Lipumba. [155]
soka
WAKATI mwenyekiti wa Yanga, Iman Madega akikanusha kumzuia Mrisho Ngassa kwenda Norway kucheza soka la kulipwa na kudai kuwa maslahi ya klabu ni lazima yaangaliwe, mchezaji huyo amedai anachosubili sasa ni kwenda Ulaya tu. [156]
soko
KUFUATIA kuwepo kwa mgogoro wa kiuchumi duniani, bei ya pamba katika soko la dunia imeshuka kwa kiasi kikubwa na kusababisha kurundikana kwa zao hilo hapa nchini. [157]
tajiri
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [158]
tatu
SHAHIDI wa tatu katika kesi ya wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inayomkabili Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na wafanyakazi watatu wa BoT ameshindwa kumtambua mkurugenzi wa kampuni ya mshitakiwa wa kwanza. [159]
tena
Alifafanua kuwa pia watanzania wapaswa kujiuliza ikiwa kweli serikali ya Muuungano na ile ya Zanzibar zina dhamira na nia thabiti ya kutokuyarudia tena yale yale. [160]
tu
Barabara zote zilizopo Zanzibar ambazo rais anasema kuwa ni maendeleo, kwa ubora hazikaribii hata barabara moja tu ya kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma. [161]
tuzo
Katika safari yake hiyo kifani amewahi kupata tuzo mbalimbali ikiwa ni matokeo ya kutambuliwa kwa mchango mkubwa wa kazi zake katika kuendeleza utamaduni wa Mwafrika. [162]
uchumi
Mary Nagu, alisema hali hiyo itasababisha madhara katika uchumi wa Tanzania. [163]
ujao
Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Mawasiliano Ikulu, Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika anayemaliza muda wake mwapema mwezi ujao ataungananna viongozi wengine wa SADC kujadili hali ilivyo nchini Zimbabwe baada ya kukwama kupatikana kwa ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa nchini humo. [164]
ukata
Mratibu wa AFC, Jerald Munishi aliliambia Mwananchi jana kuwa timu hiyo inakabiliwa na ukata mkubwa kiuchumi hivyo maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya hatua ya pili ya Ligi daraja la kwanza kuwa ya kusuasua. [165]
ukawa
Huenda ukawa umekutana na kitu ambacho kinabaki kuwa hisia zako tu tofauti na mapokezi ya kitu chenyewe. [166]
ukoo
Ya nini kumpa matumaini wakati yeye na ukoo wake wote wameshatolewa nje katika dunia ya leo. [167]
ule
Sitakosea nikieleza kuwa kwa hali ilivyokuwa wakati ule, na hata yeye mwenyewe alivyokuwa akisema kwa masihara, siku za kuishi kwa Mzee Mwanga zilikuwa zinahesabika. [168]
umekutana
Umepekuwa umekutana na kitu umekiamini sivyo kwa kiherehere chako cha kusaka mambo. [169]
urithi
Hivyo ni miongoni mwa vitabu vyake takriban 23 alivyoviandika na kuvichapisha vinavyotoa ushahidi wa urithi wa taaluma aliouacha Mwanga kwa Watanzania. [170]
uwanja
MABINGWA watetezi Yanga inashuka dimbani leo kucheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro kabla ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi hii dhidi ya Etoile d'Or Mirontsy, huku wapinzani wao Simba wataonyeshana kazi na Prisons kesho kwenye uwanja huo wa Taifa. [171]
vema
Alifafanua kuwa Mkapa anapaswa kuwaambia wananchi kama tuhuma zinazomkabili ni kweli au uongo na kwamba, akithibitisha ni uongo ni vema, lakini ikiwa ni kweli basi sheria ichukue mkondo wake badala ya kuendeleza maneno aliyoyaita blaablaa ambazo hazitamsaidia. [172]
vya
Aliongeza kuwa, katika baadhi ya vijijini vya kata za Ilembo na Santilya vituo vilikuwa na umbali wa kilomita saba hadi kumi kutoka maeneo wanayoishi wananchi, hivyo kusababisha baadhi yao kushindwa kupiga kura. [173]
vyao
Wanataka kutuua ili walete vitabu vyao. [174]
vyema
Ni vyema changamoto kama hizo zikafanyiwa kazi kwa kuwa utafutaji wa wataalamu wa mchezo huo si kazi ngumu ila ni suala la mipango ,kuzingatia na umakini tu. [175]
wakuu
Ndiyo maana vyama vya upinzani vinataka iundwe tume huru ya uchaguzi badala ya hiyo ambayo imeundwa na serikali huku mwenyekiti na watendaji wakuu wote wakiteuliwa na Rais. [176]
wale
Tusiishie kwenye vijana 20 wale wa juu pekee wanaochaguliwa kwenye mashindano haya katika kuwaendeleza bali kila mmoja ambaye ana uwezo wa kuwainua na wale wanaobaki kuweza kufanya hivyo," alisema Kipingu. [177]
wana
Wapinzani pia ni watoto wa taifa hili na wana sehemu ya kuchangia maendeleo. [178]
wanafanya
Na kwa nini wanafanya vizuri. [179]
wapi
Eti wale akina Aimbora waliosoma shule za kulipia tangu chekechea hadi mwisho wa sekondari sasa wanadai kusoma bure chuoni? Wapi na wapi. [180]
waume
Badala ya kumsaidia Rais kuwatumikia wananchi, wanadhani nafasi ambayo wanayo waume zao ya kuiongoza nchi ni kwa ajili ya kujinufaisha wao na ndugu zao. [181]
wazazi
Changamoto nyingine ni watu wengi hasa vijana kushinmdwa kufikia malengo yao kutokana na maradhi kama vile Ukimwi na kuona kuwa umefika wakati kwa wazazi kuwanusuru watoto wao kwa kuwaeleza ukweli kuhusu ugonjwa huo. [182]
wazo
LILIPOIBUKA wazo vyuo vikuu vya Afrika Mashariki kuwa na mtaala mmoja kufuatia kuanzishwa kwa Shirikisho la Nchi za Afrika Mashariki, baadhi ya wasomi akiwemo Profesa Josephat Rugemalira wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walipinga wazo hilo kwa madai kuwa nchi hizo zina mifumo tofauti ya elimu. [183]
wengi
Zambia ambayo ipo kundi A na Tanzania na wenyeji, ni wachezaji 2o tu waliowasili kambini kati ya 25 walioteuliwa ambao wengi wao walikuwa na kikosi kilichoshiriki Chalenji hivikaribuni nchini Uganda. [184]
wenye
Waziri huyo alisema pia kuwa hadi sasa kuna mabeli karibu 240,000 ambayo yamerundikana kwani yamekosa wanunuzi na hivyo kuwaomba wenye viwanda vya nguo kununua pamba hiyo. [185]
wewe
Uzinga mkubwa, ondokeni hapa, mbona zamani tulikuwa tukipata fedha nyingi ndio kusema mlikuwa mnaua albino? Sitaki kusikia uchafu huu, wewe ukiuawa utajisikia raha?” alisema Kazim akionekana mwenye hasira. [186]
wiki
Katika ziara yake ya wiki mbili Unguja na Pemba, Rais Kikwete amejikuta akipandisha hasira na chuki za wananchi wa visiwa hivyo kutokana na kauli zake, ambazo zimetafsiriwa kuwa ni za kuwakejeli wananchi na kuongeza mpasuko wa kisiasa visiwani humo. [187]
yaani
Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [188]
yako
Haya ni makampuni makubwa yako kila mahali duniani hatuwezi kushindana nayo. [189]
yale
Juhudi nyingi za kuepusha yale yaliyotokea Pemba 2001 zimefanyika kwa mara tatu lakini wenzetu CCM wamekuwa wakizikwamisha. [190]
yote
Siku ya kupiga kura tulifanikiwa kuwakamata vijana wakiwa na masanduku ya kupigia kura, hivyo hayo yote ni mlolongo wa kasoro ambazo zimejitokeza na kutufanya sisi tusiyakubali matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi," alisema. [191]
yoyote
Alizitaka taasisi kubwa za kimataifa za fedha kuwa na udhibiti katika masuala yote ya fedha ili kuhakikisha kuwa hali kama hiyo inadhibitiwa kulinda uchumi wa nchi masikini ambazo hazihusiki kwa namna yoyote na kutokea kwa mtikisiko wa uchumi duniani. [192]
yuko
Bwana Jamhuri Mwananchi anafurahi kutangaza kwamba Bi Elimu Mkombozi hajafa bali yuko mahututi. [193]
yule
Nilihitimu shahada yangu ya kwanza ya Sayansi ya Lugha mwaka 1971. Wakati namalizia niliandika tasnifu yangu nikaiwasilisha kwa mhadhiri wangu, Mwingereza yule alikuwa anaitwa Prof. [194]
zako
Unapompekuwa bila shaka unatafuta makosa! tuseme ukweli; hilo si jambo baya kufanya kama tayari hisia zako na ishara fulani zimeashiria kuwa huyu mtu lazima anakuwa anakutenda au kama huonyeshwi unapendwa. [195]
zangu
Ndugu zangu hakuna fakhari yoyote kuyakumbuka na kuyakumbushia matukio haya machafu katika nchi yetu ambayo yaliiacha historia yake iliyotukuka ikiwa imejeruhika vibaya" alisema. [196]
zetu
Aidha aliilaumu CCM kuwa imekuwa ikiharibu chaguzi mbalimbali tangu mwaka huo na kuongezea hisabu ya chaguzi zetu zisizokidhi vigezo vya kidemokrasia ya dunia. [197]
ziara
Walisema inaonekana Rais Kikwete amefanya ziara hiyo kwenda kuwakejeli kwamba ni walevi wa pombe aina ya tende. [198]
zipo
Anasema kila mbunifu huwa ana malengo yake lakini ili kufikia malengo hayo zipo changamoto nyingi zinazowakabili, zikiwapo kukosekana kwa vifaa bora kwa ajili ya kufanyia shughuli zao mfano mashine na mitaji. [199]
zote
Hata hivyo, alisema CCM waliomba msamaha baada ya suala hilo kufikishwa Tume ya Uchaguzi na kuzikutanisha pande zote mbili. [200]