Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-25

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
aende
Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [2]
afe
Si bora afe tujue moja. [3]
aina
Hata hivyo, Polisi hao walilishikilia kwa muda gari la matangazo la chama hicho aina ya Fuso kuwa lilikuwa likisababisha mikusanyiko ya watu. [4]
akawa
Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [5]
akiishi
Nyumbani kwake hapo alikuwa akiishi na watu kadhaa akiwemo jamaa mmoja ambaye ni mwenye ulemavu wa ngono yaani albino. [6]
akisema
KATIKA ukurasa wa kwanza wa gazeti hili jana, kulikuwa na habari iliyomkariri Rais Jakaya Kikwete akisema kuwa, serikali yake imesitisha ununuzi wa magari ya kifahari kwa viongozi wa serikali ili fedha zitakazopatikana zitumike kwa ajili ya kununulia matrekta kama mojawapo ya juhudi za kuinua kilimo nchini. [7]
alifoka
Sasa huo si ujinga, picha ndio nini? Picha ndio dawa,” alifoka Kazim hali iliyomfanya waziri aendelee kufadhaika na kumueleza kuwa watakachokifanya ni kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari. [8]
aliweza
Katika ziara yake hiyo ya siku moja, Pinda aliweza kutembelea soko la samaki na mboga mboga lililopo Mvumoni Jimbo la Wawi Mkoa wa Kusini Pemba linalojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF). [9]
ama
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mwanza, aliyejitambulisha kwa jina moja la Msangi alisema ofisi yake haina taarifa zaidi ya kutambua kuwa serikali imekuwa ikitoa misamaha wa kodi kwa asasi za kidini ama vyombo vya kidini na hivyo kusema iwapo jambo hilo lipo ofisi yake iltalifanyia uchunguzi. [10]
ambacho
PENGINE hakuna kitu ambacho Somalia inaweza kujivunia kwa mwaka 2009 kama kuifunga Kilimanjaro Stars iliyokuwa na kikosi kamili kwenye michuano ya Chalenji. [11]
amesema
Tayari Spika wa Bunge, Samuel Sitta amesema kama serikali itashindwa kuzungumzia suala la Kiwira katika mkutano ujao wabunge wataihoji. [12]
apewe
Mongella alisema suluhisho pekee la migogoro hiyo ni kwa wanasiasa kuheshimu maamuzi ya wapiga kura aliyeshinda apewe haki yake na alieshindwa akubali kushindwa hata kama alikuwa madarakani. [13]
au
Naye Katibu wa Tawi la CUF kisiwani Pemba, Ole Makumbi, Humo Omar Mrisho, alimtahadharisha Rais Jakaya kuangalia na kufikiria kwa makini kabla ya kutamka au kutenda jambo. [14]
baadaye
Mchezo wa kwanza wa timu hizo, umepangwa kufanyika Januari 31 na marudiano yamepangw akufanyika wiki mbili baadaye. [15]
bado
Habari zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya wabunge zinaeleza, ingawa hivi karibuni kamati za bunge zinazohusika zimekaa kujadili, lakini wanadhani bado hawajapata majibu mwafaka kutoka serikalini juu ya kiini cha matatizo yanayokabiliwa kampuni hizo na hatua zilizochukuliwa na serikali. [16]
baina
Rais emesahau kauli yake aliyowahi kuitoa kwamba suala la Zanzíbar linamnyima usingizi na kumpa shida huku akijaribu kuunganisha vyama hivyo kwa njia ya mazungumzo ili muafaka baina ya CUF na CCM upatikane"alisema Saidi. [17]
bali
Mgombea wa CUF, Daud Mponzi aliwataka wananchi leo wasibabishwe na CCM bali wampigie kura yeye ili washirikiane katika kuikomboa kiuchumi wakazi wa jimbo hilo ambao aliwaelezea kuwa wanataabika katika hali ngumu ya kimaisha kutokana na kuichagua CCM kwenye uchaguzi mkuu uliopita. [18]
baruti
Wakati huo huo, wabunge wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii waliotembelea Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya Mali Asili (WWF) waliombwa na shirika hilo kulisimamia kidete suala la kuboresha kilimo na kudhibiti uvuvi wa baruti ili kulinda amani na usalama wa nchi. [19]
baya
Mambo ya usiku wanapolala wazazi hayazuiliki, na watoto hawa wanatabia moja ya kujifunza kila jambo liwe zuri au baya, ni jukumu letu sisi wazazi kuhakikisha hatutoi nafasi yoyote kwa watoto hawa kwani kosa moja dogo linaweza kuzaa goli litakaloweza kuharibu mwenendo mzima wa maisha ya watoto wetu. [20]
bila
Nacho Chama cha CUF katika taarifa yake kwa vyombo vya habari juzi kimewataka viongozi wa ngazi za juu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, kuacha kuyatafsiri matatizo ya kisiwa hicho kisiasa bila wazingatie hali halisi ya kiuchumi waliyonayo wananchi wa kisiwa hicho. [21]
budi
Nitahakikisha michezo yote iliyobaki kwa sasa vijana wangu wanacheza kufa na kupona, ili kusaka pointi tatu muhimu na kuepuka kushuka daraja,,,,ukizingatia mzunguko huu ni wa lala salama hivyo hatuna budi kuamka na kupambana ili tuweze kusonga mbele"Alisema Minziro. [22]
chao
Kitu ambacho wananchi wa Pemba walivutiwa nacho sio tu kumwona Waziri Mkuu bali pia ni vile alivyoanza kuwashukuru wananchi waliojitokeza kumpokea na baadaye kutoa hotuba yake ya kuwataka wananchi washirikiane katika kuleta maendeleo katika kisiwa chao na mwisho alimalizia kwa kutoa fursa ya kuulizwa maswali. [23]
chote
Aliisifia CCM kuwa endapo kama itaendelea kuongoza kipindi chote itahakikisha inaboresha huduma muhimu kwa jamii ikiwa ni pamoja na elimu, afya, miundombinu, zahanati na kuhakikisha inaboresha kilimo. [24]
es
Hata hivyo, habari hizo ziliwashangaza baadhi ya wabunge waliokuwa wakihudhuria vikoa vya kamati za bunge jijini Dar es Salaam. [25]
ghafla
Nyaraka mbalimbali kutoka Bakwata mkoani Mwanza zinaonyesha kuwa Januari 3 mwaka huu, akaunti hiyo ikiwa salio la Sh 474,045.45, na ghafla ikapokea Sh 8,680,000 na kiasi hicho kutolewa siku hiyo kwenda kwa Cement Distributor. [26]
hao
Malecela aliongeza: "Katika Bunge la Tanzania kuna wabunge 319 kabla ya marehemu Nyaulawa kufariki dunia, katika hao 274 kutoka CCM na chama kisichokuwa na haya CUF 32 wote kutoka visiwani, Chadema 11 na TLP 1. Nimetoa takwimu hizi ili wananchi mjue kuwa vyama hivyo havina nguvu ya kuwaongoza na chenye nguvu ya kuleta maendeleo ni CCM pekee. [27]
hapa
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa kutokana na mtindo huo baadhi ya viongozi wa baraza hilo wanashirikiana na wafanyabiashara wa jijini hapa kununua saruji kwa jina la taasisi hiyo ya dini kwa lengo kujipatia faida nono. [28]
hapo
Naye Mbune wa Mkanyageni, Hají Saki Salí alisema, "hakuna suala mwafaka visiwani hapo na hali inaonyesha kwamba uchaguzi wa 2010 machafuko makubwa yatajitokeza hasa kutoka na kauli kama hizi ambazo zinaongeza utata kuhusu mwafaka. [29]
hasa
Wakizungumza na Mwananchi Jumapili kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi walisema hawakutegemea kama Rais Kikwete angetoa kauli hiyo hasa ikizingatiwa kwamba ndiye mtu pekee aliyekuwa kakitegemewa kunusu machafuko ya kisiasa Visiwani humo. [30]
hata
Tumemleta Mwanjali kwa watu walikuwa na matatizo na kero nyingi hususan barabara ambayo hata mimi nimeiona kwa macho yangu kuwa zinahitaji kufanyiwa matendenezo na nimehofu endapo kama mvua kubwa ikinyesha kama kunakuwa na usalama," alisema Malecela. [31]
hawa
Hii ni hatari sasa, itabidi tununue glove tuvae mikononi ili kuificha mikono yetu na hawa majangili" alisema Zulekha. [32]
hayo
Malecela alisema yeye akiwa kama Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, anawataka wakazi wa Mbeya kuachana na maneno hayo potofu na kumchagua mgombea huyo wa chama tawala. [33]
hii
Pia tulijua kuwa serikali hii haiwezi kusimamia misingi ya demokrasia kwa kufanya mwafaka wa kweli na wa haki. [34]
hiki
Kama hatuna mikakati hiyo, basi sasa ni wakati mwafaka kwa TFF, na wadau wa soka kwa ujumla kubuni mikakati hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho kuna dalili za soka letu kuanza kupanda huku kukiwa na ligi ya taifa inayolenga kuinua vipaji na viwango vya soka. [35]
hilo
Naye Mgombea Ubunge jimbo hilo, Lackson Mwanjali aliwataka wananchi wamchague kwa vile anaweza kuleta maendeleo na kwamba yeye ni Mchungaji hawezi kuwadanganya wananchi. [36]
hivi
Alisema "Sina taarifa hizo na wala kumbukumbu ya kiasi hicho cha fedha na kama tumewahi kuwa na mradi huo wa kuhitaji saruji kiasi hicho, lakini kwa vile kipindi cha siku tatu hivi nilikuwa nje ya Mwanza nitalifanyia kazi kwa kulifuatilia kwa makini," alieleza mwenyekiti huyo. [37]
huko
Nchi ikiwa na wachezaji wengi wanaosakata soka ya kulipwa nje, mbali na kuipandisha chati soka ya nchi hiyo, pia mchango wa wanasoka hao kiuchumi katika nchi husika utakuwa mkubwa kwa sababu wahusika kwa vyovyote vile wataamua kuwekeza kwenye nchi yao na si huko wanakocheza soka la kulipwa. [38]
huwa
Mbali na ubunifu huo wa mtindo ya mavazi, mwanamke huyo anajishughulisha na biashara ya vitu vya asili ambavyo huwa anavipata kutoka katika nchi za Afrika Mashariki na Kati. [39]
ijayo
MABINGWA wa Visiwa vya Comoro, Etoile d'Or Mirontsy wanawasili nchini Alhamisi ijayo tayari kwa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga utakaofanyika mwishoni mwa wiki ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. [40]
ikawa
Mfano zipo meseji watu wanatumiana "Vipi Dear!" unakuja, na hii ikawa ni meseji ya kawaida kabisa kwa mtu na mfanyakazi mwenzake kazini lakini kwako ikawa na sura nyingine tofauti kabisa na makusudiao yenyewe. [41]
ila
Yaah ni kweli tumelipokea lakini bado uchunguzi unaendelea na halijafikishwa mahakamani ila bado lipo katika kitengo cha nidhamu cha Jeshi," alithibitisha Kamanda Ng’hoboko. [42]
ile
Mwenyekiti wa Bakwata, Mkoa wa Mwanza, Idirisa Sharif alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema hana kumbukumbu za baraza lake kununua kiasi kikubwa cha saruji kwa ajili ya ujenzi wa miradi yoyote ile na hivyo ni suala geni kwake. [43]
imeanzisha
Ili kuboresha huduma kwa wakulima, Mamlaka imeanzisha vituo vya hali ya hewa na kilimo Matangatuani kisiwani Pemba, wilayani Mbozi katika Mkoa wa Mbeya na katika Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma. [44]
ina
Katika taarifa yake hiyo iliyosainiwa na Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Uhusiano ya Umma wa chama hicho, Salim Bimani, CUF ilisema tabia hiyo ina lengo la kuwakomoa wakazi wa Pemba. [45]
injili
CHESCO Kilemile ni mlemavu wa miguu ambaye aliyeamua kuhubiri injili kwa njia ya kuimba. [46]
ipo
BUNGE la Afrika limesema amani ya Afrika ipo hatarini ikiwa wanasiasa wataendelea na utamaduni wa kuanzisha vurugu baada ya chaguzi ili kushinikiza kugawana madaraka. [47]
isiwe
Waziri Mkuu amesema tofauti za kisiasa na kiitikadi isiwe sababu ya kutofanya shughuli za maendeleo kwani ikitokea hivyo nchi haiwezi kwenda kwa mtindo huo na wanaoumia kwa kukosa maendeleo ni wananchi ambao ndio waliowaweka viongozi madarakani kwa kuwachagua na kuwaamini kuwa viongozi hao watawaletea maendeleo. [48]
japo
Sio kweli kuwa kumpekuwa ni kumdhibiti na si kweli kuwa wanaume hawapekuliwi, kwa kuwa japo wengine wanadai hawajali lakini najua japo kwa siri au kwa kujua au kutokujua wanapekua. [49]
jingine
Anasema anatarajia kufanya onyesho jingine kubwa mwezi machi mwaka huu ambapo atawashirikisha wabunifu mbalimbali lakini kabla ya hapo atafanya onyesho katika tamasha la Sauti za Busara litakalofanyika Zanzibar hivi karibuni. [50]
juu
Mkutano huo wa CCM ulihudhuriwa na viogozi wa juu wa chama hicho akiwamo Makamu Mwenyekiti, Pius Msekwa. [51]
kaka
Mzazi mmoja ameniambia jambo moja lililonisikitisha kuwa watoto wawili ndugu mtu na kaka yake mmoja mwenye umri wa miaka 12, na mwingine 13 wamepeana mimba bila wenyewe kujua, yule binti mwenye miaka 12 ameulizwa akasema yeye hajui lakini amekuwa akifanya mchezo huo na kaka yake. [52]
kando
Pia Pinda katika ziara hiyo aliwakumbusha wananchi wa kisiwa hicho kuweka kando tofauti za kisiasa zilizopo kati ya Unguja na Pemba na kuwaeleza kwamba kamwe maendeleo hayawezi kupatikana visiwani Zanzibar iwapo kutakuwepo malumbano ya kiitikadi. [53]
kansa
Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [54]
karibu
Mambo ambayo yapo chini ya kamati hiyo ni Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ambayo ilisimamishwa huduma zake kwa karibu mwezi na kuanza safari zake juzi kwa kusuasua, Kampuni ya Reli (TRL) na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA). [55]
katiba
Maswali ambayo wabunge wengi wanajiuliza ni kama serikali inaweza kubadilisha katiba ili kutoa mwanya kwa sheria hiyo mpya, kwa kuwa katiba ya sasa inatambua chama kimoja kimoja. [56]
kauli
Habari zilizopatikana kutoka Kisiwa cha Pemba kinaeleza kuwa kutokana na kauli hiyo, baadhi ya wakazi wa kisiwa hicho wanaona kauli hiyo ya Kikwete ni ya kuwatangazia kuwakomoa kutokana na kutokipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika chaguzi mbalimbali. [57]
kibao
Unafikiri wale waliokatika shule za ukata wanaweza kushindana na wale wanaotoa mamilioni kwa ajili ya shule ya wanafunzi wachache na walimu kibao, na kufanya tuisheni juu mpaka wanaweza kufaulu bila hata kuelewa kitu. [58]
kile
Katibu wa Bakwata ambaye ni mmoja wa watia saini wa akaunti hiyo, Mohamedi Balla alipoulizwa kwanza alikataa kuwapo kwa suala hilo, lakini alipobanwa zaidi akakiri kununua saruji huyo kwa kile alichosema kuwa ofisi yake ilikuwa ikihitaji saruji kwa ajili ya kukamilishia mradi mmoja wa ujenzi wilayani Geita, lakini kutokana na mamlaka ya mapato kutoa maelekezo mapya kuhusiana na suala la msamaha wa kodi kwa asasi za kidini haikukamilisha ununuzi wa saruji hiyo. [59]
kisasa
Tumepata taarifa za kuwa tayari wana uwanja wa kisasa, sasa tunawataka Yanga watambue kuwa watacheza mechi mbili, hakuna kufikiria ya mwaka 47...," alisema Kaijage. [60]
kocha
Hiyo ilikuwa kidogo kwani kwa mujibu wa kocha wa Somalia, Mohamed Farah Shangwe zililipuka kila kona ya Somalia na watu kusahau matatizo yao. [61]
kona
Shangwe zilifurika kila kona kwa raia wa Somalia wanaoishi Uganda huku wengine walioko mipakani wakifunga safari kuja Kampala kusherehekea. [62]
kufa
Akizungumza na Mwananchi Jumapili baada ya mchezo wao na Polisi Dodoma, kocha huyo alisema kikubwa kwa sasa atahakikisha timu yake inacheza kufa na kupona kuhakikisha haishuki daraja na kupoteza michezo. [63]
kufanyika
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Lucas Ng’hoboko alithibitisha kukamatwa kwa Koplo huyo aliyekamatwa na gari la wizi na kwamba bado uchunguzi unaendelea kufanyika. [64]
kuja
Hata hivyo, gari hilo lilionekana lilipata ajali likiwa njiani kuja Tanzania na baada ya kuhojiwa, polisi huyo alijitetea kuwa gari hilo lililetwa na rafiki yake ambaye aliomba amsaidie kulihifadhi kwa muda. [65]
kujua
Madhara haya tunayatengeneza wenyewe bila kujua na wakati mwingine kwa kujua, ingawa kwa familia zingine kunasababishwa na hali ya kipato—kwa maana ya kushindwa kuwa na nafasi ya kutosha katika nyumba ya kuwatenganisha wasichana na wavulana. [66]
kukosa
Ziara ya Pinda imefichua jambo moja muhimu ambalo nadhani viongozi wengi hawalifahamu na iwapo litafanyiwa kazi basi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaweza kujipatia wafuasi wengi lakini kutokana na kupuuzwa kwa wanachama hao wachache waliopo ndio sababu kubwa inayofanya wananchi wa kisiwani Pemba kukosa maamuzi ya kukipenda chama hicho kama alivyobainisha Mzee Ahmad Ali Mussa ambaye alisimama kutoa maelezo wakati Waziri Mkuu alipotoa fursa ya kuuliza maswali. [67]
kukutana
Hivyo walipanga muda wa kukutana. [68]
kula
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime, Francias Kagenzi (45) amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Lindi, akikabiliwa na makosa matano, yakiwemo ya kula njama na kuisababishia halmashauri ya Nachingwea hasara ya Sh4.2 milioni. [69]
kule
Ndio ndugu, mimi naitwa Kazim ni mwenye mgodi wa madini ya almasi kule Mwadui, tatizo ni kwamba hali kwa sasa imekuwa mbaya mno, nimechanganyikiwa hapa hata sijui la kufanya,” alisema akiomba ushauri. [70]
kulinda
Awali akihutubiua mkutano huo aliwataka wanachama wa chama hicho leo kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kwamba mara baada ya kupiga kura wasiondoke kwenye vituo vya kupigia kura kulinda kura zao. [71]
kumaliza
Kwa upande wake Zakih Omari Juma Mbunge wa Viti Maalum alisema "Rais anazidisha machafuko visiwani humo badala ya kutafuta njia za kumaliza suala hilo yeye anazidi kuchochoea machafuko kwa kauli zake. [72]
kumi
Baada ya THT kumaliza kushambulia jukwaa Mwongoza shghuli aliwatambulisha vimwana hao kumi ambao ni Mwahija Omari, Sikudhani Daudi, Happy Kambona, Vivian Stephen, Halima Idd, Amina Maganga, Zena Hemed, Susan Daudi, Veronica Gabriel na Cecilia Joseph. [73]
kumuua
Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [74]
kundi
Timu hiyo inatarajiwa kuwasili na kundi la wachezaji 20 na maofisa wanane. [75]
kuona
Waziri Marmo alisema wananchi wasipate wasiwasi kuona upungufu wa chakula katika maghala ya Dodoma, Arusha na Shinyanga wakadhani kuwa chakula kitakosekana. [76]
kupeleka
Alisema, katika uchaguzi wa 2005 bunge la Afrika ndio lilikuwa limezaliwa tu na likiwa halijaanza kufanya kazi na hivyo kushindwa kupeleka waangalizi kama walivyofanya katika nchi za Zimbabwe na Ghana. [77]
kupokea
Wakati ule shule ilikuwa shule na chuo ilikuwa chuo, si choo cha kupokea uchafu wowote. [78]
kuua
Mikakati ya maandalizi ya TFF, mawakala wa ndani na klabu husika ihusishe pia nchi ambayo wachezaji hao wanakwenda kwa sababu nchi nyingine hazisaidii kuinua kiwango cha uchezaji na badala yake wahusika wanakwenda huko kuua vipaji vyao. [79]
kuwapa
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa na kuwapa nguvu wachezaji waweze kushinda mchezo huo. [80]
kwa
Mwenyekiti wa CUF, Ibrahimu Lipumba amewatahahdrisha wafuasi wake dhidi ya CCM ambayo inaweza kucheza rafu katika kura zao, huku CCM ikiendelea kulaumu vyama vya upinzani kwa kuendesha kampeni za lugha za matusi. [81]
kwani
WAKATI serikali ikihimiza ulipaji wa kodi kwa kwa maendeleo ya nchi, imebainika kuwa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoani Mwanza linakwenda kinyume na wito huo kwani limekuwa likitumia msamaha wa kodi waliopewa na serikali kuwasaidia wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu kukwepa kodi ya mamilioni ya shilingi. [82]
kwao
Watu walikuwa sehemu mbalimbali wakipeperusha bendera ya nchi wakishangilia kwa kila namna, kwa vile ilikuwa ni kitu cha ajabu kwao ambacho hawajawahi kusikia wala hawakutarajia. [83]
la
WAKAZI wa jimbo la Mbeya Vijijini, leo wanatarajia kupiga kura kumchagua mbunge wao baada ya wagombea kuhitimisha kampeni zao jana katika uchaguzi ambao umebashiriwa utakuwa wa vuta nikuvute kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF). [84]
labda
Sina hakika lakini mimi sijui labda halijafikishwa mezani kwangu" alisema Ng'hoboko. [85]
lao
Wamiliki wa kampuni inayomiliki gari hilo waliwaeleza polisi wa Tanzania kuwa wasingehitaji mlolongo mrefu wa kesi bali wapewe tu gari lao, ombi ambalo lilikubaliwa na wakuu wa Polisi wa kituo hicho. [86]
licha
KOCHA wa Polisi Dodoma, Sekilojo Chambua amesema hali ya timu yake inamchanganya, lakini bado hajakata tamaa licha ya kutoshinda hata mchezo mmoja tangu mzunguko wa pili wa Ligi Kuu uanze. [87]
ligi
Nchi hiyo imekuwa haina ligi kwa miaka kadhaa sasa kutokana na machafuko na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika miji mbalimbali. [88]
maalum
Mashindano haya ni maalum kwa ajili ya kupata washiriki bora zaidi watakaotuwakilisha katika mashindano makubnwa ndani na nje ya nchi hivyo Mikoa ijiandae mapema na kupeleka majina katika vituo," alisema Nyambui. [89]
madai
MSAFARA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana ulivunjwa wa polisi kwa madai kuwa ungesababisha vurugu. [90]
malezi
Kama nilivyogusia wiki iliyopita kuwa runinga zimeachiwa kwa kiasi kikubwa kuwa chombo cha kuwalea watoto, na kwamba malezi wanayoyapata watoto kupitia televisheni zao zimepelekea kuwaharibu kimaadili badala ya kuwajenga. [91]
mara
Mbowe mara baada ya mkutano huo aliamua kutembea kwa miguu kwenda katika ofisi cha Chadema zilizopo karibu na Stendi Kuu ya mabasi mjini hapa. [92]
matokeo
Kuhusu tuhuma hizo Jaji huyo alidai kuwa si za kweli na kuwataka washiriki wakubali matokeo kwani asiyekubali kushindwa si mshindani. [93]
matukio
Akifunga mazungumzo kati yao na wabunge, Mwakilishi Mkazi wa shirika hilo nchini, Hermen Mwageni alisema uvuvi wa baruti ni hatari kwa kuwa mabomu hayo hutumika katika matukio ya uhalifu. [94]
mfupi
Baadhi ya wasomaji walionipigia simu na wengine kunitumia ujumbe mfupi wameniambia ni vyema nikawakumbusha wazazi juu ya madhara yanayosababishwa na kuwalaza watoto wa jinsia tofauti katika chumba kimoja. [95]
mganga
Washitakiwa hao ni Afisa Afya wa wilaya hiyo, Tumaini Kagina (45), mganga mstaafu wa hospitali ya Nachingwea, Dk. [96]
mgombea
Akimnadi mgombea wa CCM jana katika Kata ya Ihengu Kijiji cha Idimi, Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, John Malecela alivilaumu vyama vya upinzani kwa kuendesha kampeni za matusi. [97]
mikoa
Hivi karibuni kumezuka taarifa ya kuwapo kwa watu katika mikoa mbalimbali ikiwamo Dodoma wanaowatafuta watu wenye alama ya herufi 'M' viganjani mwao ili kuvikata kwa imani ya kishirikina. [98]
minne
Mitambo mingine minne ya utabiri wa hali ya hewa ya RETIM na SYNERGIE mahsusi kwa mawasiliano na utabiri, imefungwa katika viwanja vinne vya ndege vya kimataifa vya Mwalimu Nyerere, Kilimanjaro, Mwanza na Zanzibar. [99]
miradi
Uchunguzi huo umebaini kwamba mpango huu umekuwa ukiendeshwa na baadhi ya viongozi wa baraza hilo kwa kushirikiana na wafanyabiashara kwa maslahi yao binafsi huku wakisingizia kuwa saruji hiyo imekuwa ikinunuliwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya Waislamu kupitia Bakwata. [100]
mirungi
Habari za uhakika kutoka ndani ya kituo hicho, zimedai kuwa taarifa za polisi huyo kujihusisha na biashara ya mirungi zilipelekwa moja kwa moja kwa Kamanda Ng’hoboko ambaye aliamuru akamatwe. [101]
miti
KWA kawaida amekuwa akibuni mavazi kwa kutumia magamba ya miti, ngozi, vipande vya magunia huku akinakshi kwa kutumia urembo wa asili. [102]
mjini
BUNGE linatarajiwa kuanza mkutano wake keshokutwa mjini hapa, huku baadhi ya wabunge wakipania kuibana serikali kuhusu suala la Richmond, Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Kampuni ya Kupakua Mizigo Bandarini (Ticts). [103]
mke
Amesema CCM ni chama jeuri na kikubwa hivyo bila ya kuwa na ofisi inayoonekana ni sawa na baba mwenye mke aliyekosa kuwa na nyumba. [104]
mkopo
Wakawalaghai na wao wadai kila mtu apewe mkopo wa elimu, hata wale wanaojiendesha hadi chuo ndani ya mashangingi. [105]
mno
Maneno ya Kikwete ni kampeni tu anayoipigia SMZ wameshaiona haina uwezo kwa kuwa hali ya Zanzibar kwa sasa ni mbaya mno, watu wamechoka na kukata tamaa," alisema Mrisho. [106]
msaidizi
Jamaa huyo ambaye alikuwa kama msaidizi wake wa karibu, alikuwa akimuwakilisha katika kazi mbalimbali na ndiye aliyekuwa ana siri zake nyingi. [107]
msingi
Fatma alizaliwa miaka ya sabini katika mkoa wa Kigoma, na kupata elimu yake ya msingi na sekondari mkoani humo. [108]
muda
KAULI ya Rais Jakaya Kikwete kuwa itawachukua muda mrefu wapinzani visiwani kuongoza dola, sasa imeonyesha wazi kupandisha hasira za wakazi wa Kisiwa cha Pemba na wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF). [109]
mujibu
Alisema kuwa hilo halikwepeki kwa kuwa kamati yake ilikuwa ikifanya kazi kwa mujibu wa sheria za bunge kwa manufaa ya Watanzania. [110]
mumewe
Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [111]
mwa
WAKATI bunge linaanza kikao chake mjini Dodoma kesho kutwa, hofu imetanda miongoni mwa wabunge kufuatia kuenea taarifa za kukatwa mikono kwa watu wenye alama ya ‘M’ viganjani mwao mkoani humo. [112]
mwenyewe
Chanzo cha kuaminika kimelidokeza Mwananchi Jumapili kuwa gari hilo lilikodishwa na mtu mmoja kutoka kampuni moja ya kukodisha magari nchini Kenya kwamba angeliendesha mwenyewe kwa safari binafsi. [113]
namba
Kiasi hicho cha fedha kiliwekwa katika akaunti namba 015101004917 iliyopo katika tawi la NBC jijini Mwanza, kabla ya kiasi hicho cha fedha kuingia akaunti hiyo ilikuwa na salio la Sh 474,045.45, lakini baada ya kuingia fedha hizo zilitolewa kwa vipindi tofauti ikilipwa kwa kampuni ya Cement Distributor. [114]
nami
Ndugu yangu nakupa pole sana, yaani ni bora ungewasiliana nami kabla ya kwenda huko, kwani ukweli ni kwamba dawa imegunduliwa nchini na jamaa mmoja tena ni albino, rudi wahi mapema usipoteze muda wako huko,” alimsisitizia. [115]
nani
Mongela alisema hayo kufuatia chaguzi nyingi kukumbwa na ghasia na hivyo kuishia katika kuunda serikali ya pamoja bila ya kujali nani ameshinda. [116]
nao
Lakini sasa kwanini tusisherehekee ushujaa? Sisi hatuna ligi, wachezaji tumewaokota tu tukavuka mpaka tukaenda Djibout kufanya mazoezi ndio tukachuja baadhi tukaja nao. [117]
navigator
MSIE = navigator. [118]
naye
Mbowe naye aliingia katika gari lake na kuanza kuondoka huku akisindikizwa na magari hayo ya Polisi akielekea katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. [119]
ndio
Mussa alisema jana kuwa wao walijua tangu awali kuwa CUF kinadanganywa na serikali ya CCM kuhusu mwafaka ndio maana wakaamua kuibua hoja ya kujitenga. [120]
ndoa
Anasema katika wimbo huo, ametumia mashairi kuwasihi kujilinda huku akiwahimiza kuvumilia mpaka watakapofunga ndoa. [121]
ngozi
Alisema wakati tatizo la kuuawa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi albino halijapungua, linazuka jengine ambalo litahsisha watu wengi kwa vile asilimia kubwa ya watanzania wana herufi 'M' katika viganja vyao. [122]
ni
Alifafanua kuwa vyama vya upinzani hususan CUF na Chadema havina sera za kuwaeleza wananchi na badala yake vimekuwa vikipika majungu ya kumkashifu mgombea wa CCM, Lackson Mwanjali kuwa hana elimu na kwamba hizo ni propaganda zisizokuwa na uwiano wa kuleta maendeleo kwa wananchi. [123]
nia
Kwa upande wa CUF, akihitimisha kampeni za mgombea wake, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba na baadhi ya viongozi wengine wa chama hicho walisema kuwa wananchi wameonyesha nia ya kufanya mageuzi ya uongozi kwa kukichagua chama cha CUF ili kutekeleza demokrasi na kupata maendeleo kupitia chama hicho. [124]
nini
Wapinzani wakipita na kukikejeli chama cha Mapinduzi kuwa hakijaleta maendeleo muwahoji kuwa na wao wamefanya nini kwa wananchi na muwajibu kuwa chama kama CUF hakina mbunge hata mmoja Tanzania Bara na hakuna ofisi ambayo inaendeshea shughuli zake zaidi ya kisiwani Zanzibar. [125]
nyumba
Gari hilo linalokadiriwa kuwa na thamani ya Sh60 Milioni lilikutwa nyumbani kwa Polisi huyo baada ya kifaa maalumu kilichofungwa katika gari hilo (Car Track) kuwaelekeza Polisi wa Kenya katika nyumba hiyo. [126]
nzuri
Kwa upande mwingine, maandalizi ya ujenzi wa kituo kingine cha hali ya hewa wilayani Babati katika Mkoa wa Manyara yamefikia hatua nzuri. [127]
pale
Utamu ulianza kuonekana pale walipoanza kuingia mmoja mmoja kuonyesha umahili wao wa kusakata sebene huku wakishangiliwa na umati mkubwa wa watu walioudhulia katika onyesho hilo. [128]
papo
Waziri Mkuu alisema amepata uzoefu mkubwa akiwa bungeni katika kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo. [129]
peke
Ni vyema tukawa na tabia ya kukubaliana na hali halisi, watoto wa kike wawekwe katika chumba cha peke yao na wa kiume vivyo hivyo. [130]
pia
Kiasi kingine cha Sh 11,085,163,00 kiliingia katika akaunti hiyo Januari 9, mwaka huu pia kilitolewa siku hiyo kununua saruji. [131]
picha
Ikabidi kwa kumtia moyo, ikabidi aende kwenye ofisi ambayo alikuwa akifanyia utafiti huo na kufanikiwa kupata picha yake. [132]
pili
KOCHA Mkuu wa timu ya Morogoro United, Fred Minziro amesema atahakikisha timu yake inafanya vizuri kuhakikisha haishuki daraja na kusaka pointi tatu muhimu katika mzunguko huu wa pili unaoendelea. [133]
rais
Alisema, maneno ya Jakaya ni ushahidi tosha kuwa rais huyo aliyetoa ahadi ya kushughulikia mpasuko wa kisiasa Zanzibar hana dhamira ya kweli ya kufanya hivyo. [134]
redio
Ilikuwa ni furaha kubwa sana baada ya watu kusikia kwenye redio ya Taifa kuwa timu yao imeshinda kwa kuifunga Tanzania, ilikuwa ni furaha isiyosimulika,"anasema Farah. [135]
runinga
BAADA ya kuandika kuhusu runinga zinavyoharibu watoto, wapenzi wasomaji wa safu hii wamenikumbusha jambo lingine ambalo sikuwahi kuligusia kabisa. [136]
saa
Naye Mwenyekiti wa Tume ya UChaguzi nchini, Jaji Lewis Makame akizungumza na waandishi wa habari jana jioni aliwataka wananchi kujitokeza kupiga kura leo kwa amani na kwamba vituo vya kupigia kura vitakuwa wazi kuanzia saa 12.00 asubuhi. [137]
sana
Hawa waganga wa jadi wanataka kuturudisha nyuma sana katika zama ujinga ambako baadhi ya watu walikuwa wakatili dhidi ya binadamu wenzao," alisema. [138]
sapoti
Sasa kushinda kwa Yanga kunatakiwa kuwa na sapoti ya mashabiki. [139]
sasa
Inadaiwa kuwa hujuma hiyo imekuwa ikifanyika kwa kipindi cha miaka mitatu sasa ambapo wafanyabiashara hao (ambao majina yao tunayo) katika kipindi cha wiki mbili mwezi huu waliwapa viongozi wa Bakwata jumla ya Sh 31,115,296 kupitia akaunti ya baraza hilo na kisha kiasi hicho cha fedha kutolewa kulipwa kwa kampuni ya kusambaza saruji ya Cement Distributor ili kununua mifuko 2,298 ya bidhaa hiyo. [140]
sawa
Alisema Kikwete amewaonyesha mwaka ujao utakuwa na vurugu na kwamba sasa tutajiweke sawa kukabiliana na hali hiyo. [141]
sekta
Wakati rais akitoa maelekezo kama hayo, ni vyema viongozi wengine wenye majukumu ya kusimamia kilimo, wakajiunga pamoja na jitihada za rais ili zoezi la kuimarisha sekta ya kilimo likafanikiwa na hivyo kuwaletea neema wakulima ambao ni wengi, lakini wanaongoza kwa umasikini nchini. [142]
sh
Hata hivyo washitakiwa walikana makosa makosa waliyosomewa na wapo nje kwa dhamana ya sh. [143]
shule
Baada ya kumaliza shule alikuwa nyumbani akijishughulisha na kazi za mikono ikiwamo ushonaji na utengenezaji wa mapambo mbalimbali kwa ajili ya wanawake. [144]
si
Hata hivyo, alisema kuwa mambo mengine wanayotarajia kuwasilisha bungeni bado si ya kuwekwa hadharani kwa sasa hadi yatakapopata kibali cha bunge. [145]
sio
Duni alisema matumizi ya nguvu sio ufumbuzi wa matatizo ya kisiasa na kama ni suluhisho basi Irael ingefanikiwa dhidi ya Wapalestine. [146]
sisi
Tunataraji kuingia kikosi kamili cha mauaji, sisi tutakachokifanya ni kuwafunga mabao mengi ili kujiweka pazuri. [147]
soka
Somalia baada ya kushinda ilicheza soka ambayo ilimkera kila shabiki wa Tanzania, kwani wachezaji wote walirudi nyuma ya mpira kuanzia dakika hiyo ya 13 ya kipindi cha kwanza. [148]
tajiri
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [149]
tamaa
Alishangaa kitendo cha Kikwete kwenda Pemba walikouawa watu katika maandamano ya Januari 26 mwaka 2001 na kuwakatisha tamaa, hata hivyo alisema wao hawatakata tamaa mpaka wanapata haki yao. [150]
tena
Kesi hiyo itatajwa tena februari 04 mwaka huu. [151]
tu
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa katika kipindi cha kuanzia Januari 3 hadi Januari 16 mwaka huu jumla ya mifuko ya saruji 2,298 ilinunuliwa na Bakwata kwa bei ya Sh 16,500 kwa kila mfuko na kisha kuiuza kwa Sh 19,000 kila mfuko na hivyo kujipatia Sh 43,651,913, hivyo kunufaika na faida tele ya Sh 12,053,572 kwa wiki mbili tu. [152]
tuna
Bado tuna nafasi ya kufanya vizuri zaidi, mechi nane zilizobaki ni nyingi iwapo tutashinda zote, ninaamini kabisa tunaweza kushinda,” alisema. [153]
tuseme
Tuondoshe tofauti zetu na tukubali kusema ukweli pale penye ukweli jitihada zisipuuzwe tutende zaidi na tuseme kidogo dhamira yetu njema itaonekana," amesisitiza Waziri Mkuu. [154]
tuzo
Katika safari yake hiyo kifani amewahi kupata tuzo mbalimbali ikiwa ni matokeo ya kutambuliwa kwa mchango mkubwa wa kazi zake katika kuendeleza utamaduni wa Mwafrika. [155]
ubunifu
Kimsingi kilichokuwa kinaangaliwa hapo ni uwezo, juhudi binafsi na ubunifu wa mshiriki katika uchezaji wa sebene hilo. [156]
ukata
Sasa Mkombozi akifanikiwa kuruka vikwazo vyote hivi, anapelekwa kwenye shule za ukata, shule za kukatisha tamaa moja kwa moja wakati akina Aimbora wanazidi kupeta ndani ya shule za wenyenchi. [157]
ukawa
Huenda ukawa umekutana na kitu ambacho kinabaki kuwa hisia zako tu tofauti na mapokezi ya kitu chenyewe. [158]
uko
Alisema vyama vya siasa vimekuwa havijali maslai ya wananchi na wananchi muwe na msimamo na msikubali kubabaishwa na vingozi wa vyama hivyo na vinapaswa kutambua kuwa ushindi uko CCM na wanapopita nyakati za usiku kuomba kura na kuwalaghai kwa kuhitaji shahada zenu za kupigia msikubali. [159]
ukoo
Ya nini kumpa matumaini wakati yeye na ukoo wake wote wameshatolewa nje katika dunia ya leo. [160]
ukweli
Huu ni ujinga tu hakuna cha ukweli wowote, na kwa ujinga huu watanzania tutaendelea kuuana hadi mwisho wa dunia kutokana na imani za kishirikina" alisema Abdallah. [161]
ule
Lakini ule ushindi umeleta faraja sana hata raia wanaoishi nje walikuwa wanatupigia simu na kutupa sapoti, nchi ilitulia kwa muda, watu wakaweza hata kushikana mikono. [162]
umma
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ni miongoni mwa taasisi za umma ambazo, kwa kipindi kilichopita, zilikuwa zinalalamikiwa sana na wananchi kutokana na huduma duni zisizokidhi matarajio ya wananchi zilizokuwa zikitolewa na taasisi hizo. [163]
una
Miongoni mwa vibao alivyotoa na ambavyo vimeonekana kufanya vizuri ni pamoja na Bwana Yesu, Hakuna Kama Wewe, Baba Yetu, Uniponye na Ulugandaganda, wimbo ambao una asili ya Kihehe. [164]
usafiri
Miongoni mwa sekta zinazonufaika na taarifa za TMA ni sekta za kiuchumi na kijamii kama vile sekta za usafiri, kilimo, maji, mazingira na ujenzi. [165]
uwezo
Alifafanua kuwa hiyo ni kampeni binafsi anayoifanyia serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwa yenyewe haina uwezo. [166]
vichwa
Waishiwa walitingisha vichwa vyao kwa uchungu sana. [167]
video
Safari yake ya uimbaji si ya muda mrefu kama ilivyo kwa wasanii wengi, yeye anasema alianza kuimba mwaka 2007-alianza kuimba nyimbo zake peke yake na kujikuta akiendelea na kufanikiwa kuikamilisha albamu ya video ambayo anatarajia kuizindua Machi mwaka huu. [168]
vipi
Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni,” alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [169]
vita
Huku wananchi wakiwa kimya wakimsikiliza Waziri Mkuu alisema: "Ili kuimarisha mafanikio hayo ya kujivunia, CCM katika kipindi hiki itatekeleza yafuatayo: kuimarisha matunda ya mwafaka kwa faida na maslahi ya Wazanzibari wote, kuendelea kupiga vita kwa nguvu zote ubaguzi wa dini, kabila, kijinsia au asili ya mtu katika utoaji wa huduma na fursa mbali mbali za kijamii pamoja na kuendeleza umoja, mshikamano, amani na utulivu miongoni mwa wananchi wote na kuimarisha jumuiya mbali mbali za maendeleo na kijamii," alisisitiza Pinda. [170]
vya
Kama ilivyo kawaida vyama vya CUF na Sau vilitupa makombora ya lawama dhidi ya CCM huku chama hicho nacho kikiwaponda wapinzani. [171]
vyao
Kufuatia hali hiyo, baadhi ya wabunge wamesema wana mpango wa kununua 'Glovu' kwa ajili ya kuvaa mikononi ili kuficha viganja vyao. [172]
wako
Madega aliiambia Mwananchi Jumapili kuwa wachezaji wake wako tayari kwa mchezo huo na anaamini watashinda. [173]
wakuu
Katika bunge lililopita serikali iliahidi kutoa taarifa za utekelezaji wa azimio la bunge lilokuwa limependekeza pamoja na mambo mengine kuwajibishwa kwa watendaji wakuu wa serikali akiwamo, Katibu mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Athur Mwakapugi, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Edward Hosea, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika. [174]
wala
Ni chama kisichokuwa na mwelekeo wala sera katika kuiongoza jamii ya kitanzania," alisema. [175]
wanaendelea
Katika kipindi husika, wanafunzi 120 wamemaliza mafunzo ya Utabiri Daraja la Tatu katika Chuo cha Hali ya Hewa cha Kigoma wakati wengine 43 wanaendelea na masomo. [176]
wanafanya
Na kwa nini wanafanya vizuri. [177]
wangu
Msimamo wangu sikubaliani kabisa na utamaduni huo,” alisema Mongella. [178]
wanne
Washiriki wote waliingia kuonyesha uwezo wao kwa pamoja huku sebene likipigwa kutoka kwa FM Academia mara mbili na baadaye wakaingia katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza na la pili walikuwa wanne wanne na la tatu walikuwa wawili. [179]
wapi
Eti wale akina Aimbora waliosoma shule za kulipia tangu chekechea hadi mwisho wa sekondari sasa wanadai kusoma bure chuoni? Wapi na wapi. [180]
watakuwa
Wakti JKT wakicheza na Tz Prisons, Pazi nao watakuwa wakonyeshana kazi na UDSM Outsiders. [181]
waume
Badala ya kumsaidia Rais kuwatumikia wananchi, wanadhani nafasi ambayo wanayo waume zao ya kuiongoza nchi ni kwa ajili ya kujinufaisha wao na ndugu zao. [182]
waweze
Alisema kesho wamepanga kuonana na Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, John Magufuli kuzungumzia suala hilo ili waweze kushauriana na kulitafutia ufumbuzi. [183]
wazazi
Changamoto nyingine ni watu wengi hasa vijana kushinmdwa kufikia malengo yao kutokana na maradhi kama vile Ukimwi na kuona kuwa umefika wakati kwa wazazi kuwanusuru watoto wao kwa kuwaeleza ukweli kuhusu ugonjwa huo. [184]
waziri
Kashfa ya Richmond Februari mwaka jana ilisababisha aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa, Waziri wa Nishati na Nadini, Nazir Karamagi na waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Ibrahim Msabaha kujizulu. [185]
waziwazi
Amour Said ambaye ni mfanyabiashara eneo la Darajani Kisiwani Unguja alisema kauli ya Rais Kikwete imeonyesha waziwazi namna alivyoshindwa kulitafutia ufumbuzi suala Zanzíbar. [186]
wenyewe
Alisema, tatizo la mpasuko wa kisiasa Zanzibar na mwafaka baina ya CCM na CUF ni la watanzania wenyewe na kwamba walikubaliana kuwa watalishughulikia wenyewe bila ya nguvu kutoka nje. [187]
wetu
Hatua ya soka la Tanzania imefikia pazuri si tu kwa mchezaji mmoja mmoja, bali pia kwa taifa ambapo kiwango cha soka kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa, FIFA kimeanza kupanda, hivyo kuongeza uwezekano wa wachezaji wetu kununuliwa nje. [188]
wewe
Uzinga mkubwa, ondokeni hapa, mbona zamani tulikuwa tukipata fedha nyingi ndio kusema mlikuwa mnaua albino? Sitaki kusikia uchafu huu, wewe ukiuawa utajisikia raha?” alisema Kazim akionekana mwenye hasira. [189]
yaani
Mwishoni mwa miaka ya 1990 yalizuka mauaji ya watu ambao ngozi zao zilichunwa na kuuzwa na katika siku za hivi karibuni yamejitokeza mauaji ya kutisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino. [190]
yako
Mwisho tu nikuachie mwenyewe na mizani yako. [191]
yapo
Ni kweli yapo mambo mbalimbali tutakayoyatolea ushauri kwa serikali, tutafanya hivyo kwa utaratibu uliopo wa kawaida," alisema Missanga. [192]
yenye
Kwa mujibu wa taarifa hizo, polisi huyo alikamatwa akiwa na bulungutu la mirungi hiyo nyumbani kwake na tayari majalada mawili ya uchunguzi yenye namba HI/RB/269/2009 na HI/IR/235/2009 yamefunguliwa. [193]
yuko
Mimi nimekaimu ofisi kutokana na meneja kuwa safari, naomba kusema kuwa jambo hili ofisi yangu imelipokea na kwa vile meneja yuko nje ya mkoa, Jumatatu (kesho) nitamkabidhi kwa ajili ya ufuatiaji zaidi," alieleza. [194]
za
Katika kuhitimisha kampeni za wagombea wao jana, vyama vinavyoshiriki katika uchaguzi huo kikiwamo cha Sau vilitupa karata yao ya mwisho katika mikutano ambayo ilihudhuriwa na wafusi wengi wa vyama hivyo huku kila kimoja kikiwahakikishia wafuasi wake kuwa kuibuka mshindi. [195]
zako
Unapompekuwa bila shaka unatafuta makosa! tuseme ukweli; hilo si jambo baya kufanya kama tayari hisia zako na ishara fulani zimeashiria kuwa huyu mtu lazima anakuwa anakutenda au kama huonyeshwi unapendwa. [196]
zetu
Kuanzia mwaka jana (2008) nimeanza kufanya maonyesho ya mavazi yangu mwenyewe ambapo huwa nawaalika wabunifu wengine kuonyesha kazi zao lengo likiwa ni kuwajulisha wa Tanzania kazi zetu tunazobuni" anasema. [197]
ziara
Kwa Pinda hii ilikuwa ziara yake ya kwanza Kisiwani Pemba tokea ateuliwe kuwa Waziri Mkuu lakini pia yeye ni waziri mkuu wa pili kulala katika kisiwa hicho ukiacha aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo Dk Salim Ahmed Salim (kwao) ambaye aliwahi kutembelea maeneo mbalimbali na kulala. [198]
zipo
Anasema kila mbunifu huwa ana malengo yake lakini ili kufikia malengo hayo zipo changamoto nyingi zinazowakabili, zikiwapo kukosekana kwa vifaa bora kwa ajili ya kufanyia shughuli zao mfano mashine na mitaji. [199]
zote
Kwetu sisi ijapokuwa tumefungwa mechi nyingine zote, lakini sisi ule ni kama ubingwa kwetu, tukiingia kwenye mashindano mengine tutafanya kitu kingine, lakini angalau nyumbani wamefurahi na hawakushangaa kuona tukifungwa mechi zingine. [200]