Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-14

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aina 
Katika hali isiyo ya kawaida, vituo vingi vya mafuta vilikuwa havina mafuta aina ya petroli kwa takriban siku nne, ikiwa ni siku chache baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Mafuta (Ewura) kutangaza bei mpya za bidhaa hiyo, ambayo ilipingwa vikali na wauzaji. [1]
ajira 
Kuhusu mfumo wa elimu uliopo, Rashid anasema kuwa baada ya Mapinduzi, Mzee Abeid Amani Karume alitangaza fursa sawa katika elimu ambapo ilitolewa bure kwa watoto wote na hivyo kuongeza idadi ya watu walisoma na kuongeza ajira hivyo kuinua vipato vya wananchi wake na taifa kwa ujumla. [2]
akaanza 
Wakati bado tunacheka akaanza. [3]
akawa 
Hata hivyo askari polisi, walikuwa wameshachelewa kwani vikosi vya Okello tayari vilikuwa vimeshavamia ghala hilo na muda mfupi kila mfuasi wa Okello akawa amesheheni silaha za moto. [4]
akiwa 
Lowasa akiwa kama kiongozi wa semina hiyo ya kimila, lakini akasema kwamba hawezi kuzungumzia siasa za Simanjiro," alisema Ole Sendeka. [5]
akiwemo 
Watu 21 wameshapandishwa kizimbani, akiwemo mfanyabiashara maarufu, Jeetu Patel. [6]
ama 
Seleli ambaye aliitaka serikali kuchunguza kwa kina kama mafuta hayo yapo ama hakuna ndipo wafanye utaratibu wa kufungia. [7]
ana 
Hata hivyo, Ole Sendeka alifafanua kwamba hana wasiwasi wowote kuhusu taarifa kwamba Millya ana mpango wa kugombea ubunge katika jimbo lake kwa sababu ana haki ya kikatiba kufanya hivyo. [8]
au 
Mbunge huyo alisema maisha bora kwa kila mtanzania hayamfuati mtu aliyejipumzisha baa au kwenye klabu cha pombe au anayelalamikia serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete. [9]
awe 
Kifungoni ndiko kulikomfanya awe na fikra za kimapindizi. [10]
azma 
Mgawanyiko wa jamii kitabaka na mgawanyiko huo pia ukawa na sura ya kikabila; nguvu za kiuchumi kuwa zinamilikiwa na tabaka moja lililo dogo na walio wengi wakiwa masikini; mfumo wa kumiliki ardhi ambapo ardhi ilikuwa imehodhiwa na wachache; na mfumo wa uchaguzi ambao ijapokuwa kijuujuu ulionyesha kuwa wa kidemokrasia lakini kwa hakika ulikuwa umeficha ndani azma ya kuulinda ubwanyenye na usultani. [11]
bado 
Hata hivyo, upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. [12]
baina 
Aidha, watu hao waliiba gari aina ya Land Cruiser la wakala wa majengo katika harakati za kutoroka, lakini walilitelekeza Mabibo baada ya mapambano makali baina yao na askari wa doria, askari waliokuwa wakisindikiza fedha hizo na askari wa mgambo. [13]
bashasha 
Unafikiri hiki ni chama cha siasa? Tunagombea uenyekiti au kiti kizuri cha kulala huko Dodoma? Hapa wategemea bashasha si bahasha. [14]
bia 
KAMPUNI ya bia Tanzania (TBL) imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu za soka za Simba na Yanga vyenye thamani ya Shilingi 60 milioni kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu pamoja na kuahidi kutekeleza ahadi ya kutoa mabasi kwa timu hizo. [15]
bila 
Kutokana na tukio hilo lililotokea Januari 7 mwaka huu katika kijiji hicho, Mwenyekiti Lesilwa alisema kuwa wanakijiji wake walipata shaka baada ya kuona mganga huyo (jina tunalo) akiwachangisha waganga wa jadi wa kijiji chake bila kutoa taarifa. [16]
bungeni 
MAKAMU wa mwenyekiti mstaafu wa CCM Taifa, John Samwel Malecela, amesema kuwa Tanzania nzima imekikataa Chama cha Wananchi (CUF); kutokana na kutokuwa na wabunge Bara na kupelekea hoja zao kutokubalika bungeni. [17]
cha 
Ukosefu huo wa umeme ulitokana na ukame mkubwa ulioikumba nchi kiasi cha kusababisha serikali kutafuta umeme mbadala badala ya ule unaotengenezwa katika mabwawa ya maji ambayo kwa wakati huo mengi yalikuwa hayana maji ya kutosha. [18]
changamoto 
Akizungumza jijini jana Katibu mkuu wa Yanga Lucas Kisasa alisema ushauri wa Kondic wameupokea kwa mikono miwili na kuchukulia kama changamoto katika maendeleo ya klabu hiyo. [19]
chote 
KATIKA kusherehekea miaka 45 ya Mapinduzi ya Zanzibar, suala kubwa moja linalobakia ni mafanikio yaliyopatikana katika Mapinduzi hayo katika kipindi chote hicho. [20]
dereva 
WATU wanaodhaniwa kuwa majambazi wamevamia gari lililokuwa limebeba fedha za kituo cha mafuta cha Mount Meru zikipelekwa Benki ya Standard Chartered na kumuua dereva na kujeruhi askari mmoja na mhasibu wa kituo hicho eneo la Manzese Darajani jana. [21]
dhamira 
Yumkini hiyo pia ilikuwa ndio dhamira ya wafanyaji wa Mapinduzi ya Zanzibar. [22]
dhidi 
Stars ambayo ilikuwa na wachezaji wake wote tegemeo kama Shadrack Nsajigwa na Kelvin Yondani waliokosekana katika mechi iliyopita dhidi ya Kenya, ilicheza soka la kuonekana dakika 30 za mwisho. [23]
don 
Suti hilo! Yaani suruali ilikuwa mfano wa ‘don’t touch’ na tai ilikuwa inajikunja kutokana na kutumika miaka si chini ya ishirini. [24]
es 
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Kisutu, Wariyalwande Lema, Gire alisomewa mashtaka yake na wakili wa serikali, Boniface Stanslaus ambaye alidai kuwa Machi 13 mwaka 2006 jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alighushi nyaraka akionyesha kwamba, Mohamed Gire, ambaye ni mwenyekiti wa Richmond Development Company LLC ya Texas nchini Marekani, alisaini kumruhusu Naeem Adam Gire kufanya shughuli za kampuni hiyo hapa nchini. [25]
familia 
Nyota huyo wa Manchester United alijitahidi kujizuia asitokwe na machozi wakati walipokuwa akitoa shukruni zake kwa wachezaji wenzake pamoja na familia yake. [26]
fulani 
Sasa hivi tunaona aina fulani ya mahubiri ya Imani ya Kikristo yakilenga kuimarisha imani kwa msingi wa maandiko, na sio kwa kuangalia nyakati zilizopo. [27]
gani 
Mwenyekiti huyo alisema kuwa mganga huyo pia alikutwa na fomu zaidi ya 29 ambazo anadaiwa kuwa alikuwa akizitumia kuwatoza waganga wa jadi Sh3,500 za mchango ambao haukueleweka mara moja ulilenga kufanyia kazi gani. [28]
ghala 
Okello alitoa taarifa kwamba, Mapinduzi yangeanza baada ya yeye na vikosi vyake, kuvamia kambi na ghala la silaha za Jeshi la Polisi ya Ziwani. [29]
hadi 
Kashfa hiyo, iliyoingia hadi ndani ya Bunge la Muungano, ilisababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu baada ya kuhusishwa na sakata hilo. [30]
hao 
Wakili huyo alidai kuwa, katika shtaka la nne mwezi Juni mwaka 2006, mshtakiwa alitoa taarifa za uongo kwa wajumbe wa Timu ya Majadiliano ya Serikali kwamba, Richmond ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme ili wajumbe hao waweze kuipendekeza. [31]
hapo 
Akitoa uamuzi huo jana, Hakimu Mkazi Hezron Mwankenja alisema, Mgonja amenyimwa ruhusa kutokana na barua yake aliyowasilisha mahakamani hapo kuwa na mapungufu. [32]
harakati 
Kesi ya Gire ni mwendelezo wa harakati za serikali kushughulikia tuhuma za ufisadi. [33]
hasa 
Naye Makamu mwenyekiti wa Simba Omary Gumbo alisema udhamini wa TBL umewasaidia kuwapunguzia matatizo mengi yaliyokuwa kwenye timu hiyo hasa mishahara ya wachezaji na benchi la ufundi. [34]
hata 
CUF kimekataliwa na Tanzania nzima na kwamba hata bungeni wabunge wake kutoka Pemba kwa kuwa huongea upuuzi. [35]
hati 
Katika shtaka la pili, wakili huyo alidai kuwa Machi 20 mwaka 2006 katika eneo la Ubungo Umeme, mshtakiwa alitoa hati za uongo zilizoonyesha kwamba, Mohamed Gire amezisaini kumuidhinisha kufanya shughuli za kampuni hiyo nchini. [36]
haukuwa 
Msamiati wa Mpemba na Muunguja haukuwa ukitumika wala kueleweka miaka 45 iliyopita. [37]
hayo 
Katika kesi hiyo ameunganishwa Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja kwa makosa kama hayo. [38]
hazina 
WAKATI Klabu ya Simba ikikamikilisha mchakato wa kumsaka Katibu mkuu na Mweka hazina wa kuajiriwa, watani wao wa jadi Yanga mchakato huo umechelewa kutokana na kuwepo kwa mgongano wa katiba na mkataba. [39]
hii 
Nia ya mafisadi hawa inafahamika na leo hii wameanzia kwangu kesho watahamia kwa (mbunge wa Same, Anne) Kilango na baadaye watakwenda kwa (mbunge wa Kyela, Harrison) Mwakyembe ili waweze kufanikiwa katika jitihada zao za kulimaliza kundi linalopiga vita ufisadi ndani ya CCM na kama hawatashughulikiwa kikamilifu na haraka, hali ya chama itazidi kuwa mbaya," alisema. [40]
hiki 
Tukio hilo limetokea katika kipindi hiki ambacho kuna hekaheka kila mahali nchini juu ya unyama mkubwa wanaofanyiwa walemavu wa ngozi nchini, wengi wao wanadaiwa kukatwa baadhi ya viungo vyao ili vitumike kwa imani za kishirikina. [41]
hili 
Hivyo hata katika suala hili la ufisadi siyo kwamba, CCM ndiyo mafisadi, hilo ni la mtu binafsi nawaomba msikubali kudanganywa kwa wimbo huo," alisema. [42]
hisia 
Wenye vituo vya mafuta wamekuwa na hisia kuwa Ewura itakapobadilisha bei inaweza kushuka na hivyo kupata hasara. [43]
hivi 
Alisema mafisadi hao walianza kumwandama kipindi kirefu ndani ya chama hicho na hivi sasa wamefikia hatua ya kumuangamiza kisiasa ndiyo sababu wameanza kutafuta kila sababu za kumshitaki ili afikishwe mahakamani. [44]
hotuba 
Katika hotuba yake ya sherehe za mapinduzi, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Amani Abeid Karume ameeleza jitihada za serikali hiyo katika kuhakikisha kuwa tatizo la umeme linapatiwa ufumbuzi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. [45]
hujui 
Utamaduni huu shostito ni wa pwani, kama ulikuwa hujui chukua hiyo, Na ukweli ni kwamba wanawake wengi wa pwani wanajua maana ya chai ya jioni na ndiyo maana wanasifiwa kuwa wanayajua mambo. [46]
huku 
Watenda maovu wako kila mahala hata huku Mbeya wanaposema kuwa kuna watu wanachuna ngozi, siyo kwamba wananchi wote ndiyo wanaochuna ngozi; ni baadhi ya watu ambao wamekosa maadili ndio wanaofanya unyama huo. [47]
humo 
Wakati huo huo Sendeu alisema Chama kinachohusika na mchezo huo cha nchini Malawi kimetoa ahadi ya kuipa mwaliko Tanzania kwaajili ya kushiriki mashindano mengine ya kimataifa yaliyopangwa kufanyika Marchi nchini humo. [48]
huo 
Akiongea na wahariri mwishoni mwa mwaka jana, Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwatoa hofu wananchi akisema kuwa, tuhuma nyingi za ufisadi zinashughulikiwa na kwamba katika uchunguzi huo mambo mengi mapya yamebainika. [49]
huru 
Anasema dhuluma na uonevu ndivyo viliyofanya wananchi wa visiwa hivyo kuamua kuungana na kuuondoa utawala wa Kiarabu, lakini tangu Mapinduzi serikali ya CCM imekuwa ikiendeleza ubabe wa kuhakikisha inatawala milele jambo ambalo si katika misingi ya demokrasia huru. [50]
huu 
Yona aliomba ruhusa ya siku saba ya kuanzia Januari 3 hadi 10 mwaka huu kwa ajili ya kwenda kuwaona wazazi wake. [51]
huwa 
Si kila mwanamme anapenda kunywa chai nyumbani asubuhi, na wengi huwa hawanywi chai kwa kituo asubuhi, na saa kumi si lazima iwe saa kumi kamili, hapa namaanisha jioni. [52]
idadi 
Kwa ujumla, matokeo hayo ni changamoto kwa serikali kufanya utafiti wa kina wa jinsi ya kuboresha elimu ya sekondari ili iende sambamba na juhudi za kuongeza idadi ya shule ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa nafasi za kidato cha kwanza ikilinganishwa na miaka ya nyumba. [53]
idhini 
Alisema amesikitishwa kuona mkuu huyo wa wilaya akimkatalia kukutana naye kwa maelezo kwamba, mpaka atakapopata idhini kutoka kwa viongozi wake, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Said Mecky Sadik au Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi). [54]
iko 
Moja ya njama hizo za mafisadi zilianza kuonekana siku moja baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa UV-CCM baada ya mtu asiyejulikana kuniandikia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kwa laini ya Tigo ukisema kwamba wameshaking'oa kisiki kimoja bado mimi na watafanikiwa kwa sababu hakuna haki hapa Tanzania na kwamba haki iko mbinguni. [55]
ile 
Tunafurahia kuwa wadhamini wa timu hizi, ushirikiano ni mzuri kati yetu na tunaahidi kuboresha zaidi udhamini wetu kwa mwaka huu 2009, na pia ile ahadi ya kutoa mabasi tutaitekeleza katika kipindi cha miezi miwili," alisema Shelukindo. [56]
ili 
Inadaiwa kuwa, mshtakiwa huyo alitoa taarifa hizo ili wajumbe wa bodi hiyo waipendekeze Kampuni ya Richmond kufanya kazi hiyo. [57]
iliyokuwa 
Katika Mapinduzi haya, serikali ya kisultani iliyokuwa madarakani kwa zaidi ya karne moja ilisimamishwa kwa siku moja tu. [58]
imeshuka 
Abdallah alisema mbali na hilo TBBO imeuanza mwaka mpya kwa kurudisha hadhi ya mchezo huo hapa nchini ambayo kwa miaka ya hivi karibuni imeshuka. [59]
ina 
Jana, Gire alipandishwa kizimbani majira ya saa 9:00 alasiri kujibu tuhuma za kueleza uongo kuwa Richmond ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme nchini. [60]
iwe 
Ilionao Zanzibar ni uhuru wa kuwa na serikali yake lakini isiyokuwa na nguvu za kuinua uchumi kwa kuwa hakika yake ni tawi tu la serikali nyengine, baada ya kuwa Zanzibar imefanywa iwe sehemu tu ya Tanzania (tena inayodharauliwa) na serikali yake sehemu tu ya serikali ya Tanzania (tena iliyonyimwa nguvu zote muhimu). [61]
juu 
Wakiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wajumbe wa kamati hiyo waliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali inatakiwa kuchukua jukumu la juu kwa kuwa wafanyabiashara hao hawana huruma na uchumi wa nchi. [62]
juzi 
Burundi chini ya kocha wake Gilbert Younde ambae juzi alisema Tanzania haiponi, ilipata bao la pili dakika ya 42 kupitia kwa Jafari Jumapili aliyeunganisha krosi ya Nahimana. [63]
kabla 
JIBU: Ili kujua kama malengo yake yamefikiwa kwanza yatupasa kujuwa hali ilivyokuwa kabla ya Mapinduzi. [64]
karibu 
Alisema hata alipokuwa mkoani Dodoma alikutana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye alimkaribisha ofisini kwake na kuzungumza mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wa nchi, ikiwemo kupeleka viongozi watakaoweza kuwa karibu na jamii katika maeneo ambayo wanaona CCM haina nguvu kwenye maeneo hayo. [65]
karne 
Mapinduzi hayo yaliandika historia mpya ya Zanzibar na watu wake waliokuwa chini ya utawala wa Sultan kwa zaidi ya karne moja. [66]
kasi 
Matukio ya ujambazi wa kutumia silaha yameibuka tena kwa kasi katika jiji la Dar es Salaam baada ya kupotea kwa muda ambapo Desemba 10 mwaka jana majambazi walivamia kituo cha mafuta cha Magomeni na kumuua mhasibu wake kisha kupora fedha taslim. [67]
kati 
Aidha, mapambano kati ya askari na majambazi hao, yalikuwa magumu baada ya kuamua kujichanganya katika umati mkubwa wa watu katika eneo hilo. [68]
kidato 
MFUMO mpya wa elimu nchini wa mwanafunzi kuelewa zaidi kuliko kukariri, umesababisha kushuka kwa kiwango cha kufaulu kwa waliofanya mtihani wa sekondari kidato cha pili Kanda ya Mashariki mwaka jana, imefahamika. [69]
kidogo 
Alisema tukio hilo lilitokea eneo la Manzese Darajani wakati gari hilo likisindikizwa na askari namba F8407 PC Lazaro na F8186 PC Sosthenes wa Kituo kidogo cha Polisi Urafiki. [70]
kijamii 
Mapinduzi ya Zanzibar yanaathiriwa sana na ubaguzi katika maendeleo ya siasa, uchumi na maendeleo ya kijamii. [71]
kijeshi 
Sheikh Karume na Babu hawakuwa wamejulishwa kuhusu Mapinduzi hayo ya kijeshi kwani wote walikuwa Tanganyika, lakini walirudi Zanzibar baada ya kukaribishwa na Okello. [72]
kijiji 
Mganga huyo alikamatwa na mwenyekiti wa kijiji cha Chinangali ya Pili wilayani Chamwino, Ernest Lesilwa kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji chake. [73]
kisiwani 
Kutokana na mahitaji makubwa ya umeme na uchakavu wa majenereta hayo, tatizo la umeme limeshazoeleka kisiwani humo. [74]
kiti 
Katika chaguzi hizo chama cha Mapinduzi kimekuwa kikifanya vibaya kwa kupata wabunge wachache au kukosa kabisa kiti katika kisiwa cha Pemba. [75]
kuajili 
Yanga ni taasisi kubwa na ina utaratibu wake wa kuajili, kulikuwepo na mgongano wa katiba na mkataba, lakini baada ya kuifanya marekebisho katiba yetu, sasa kila kitu kinaenda sawa na mchakato unaendelea," alisema Madega. [76]
kuiba 
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kituo cha Polisi cha Kati na kutiwa saini na Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova zinasema, majambazi hao hawakufanikiwa kuiba fedha hizo na kwamba jambazi mmoja alijeruhiwa kwa silaha mgongoni. [77]
kuimba 
Kweli wanaweza kuingia hivihivi? Kweli wataingia kama milolongo ya vijana wanaotafuta nafasi moja ya Ustaa wakati ambapo hata wenzao wa mitaani wanawacheka wakijaribu kuimba. [78]
kuja 
Historia yake ni mbali, na kwa Wakristo ilikuwepo na sasa hivi uhafidhina unaanza kuja upya na kuna sababu nyingi. [79]
kukataa 
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, amemshutumu Mkuu wa Wilaya Kilwa mkoani Lindi, Nurudin Babu kwa kukataa kuonana naye alipokwenda ofisini kwake kujitambulisha. [80]
kukosa 
Aidha, alisema kuwa anawashangaa wapinzani wanavyozunguka na kuwaambia wananchi kuwa, CCM haijafanya kitu katika uongozi wake, kwamba siyo kweli bali ni kukosa akili na kwamba wote wanaosema hivyo ni wajinga na CCM haiwezi kuubeba ujinga huo mgongoni. [81]
kule 
Tanzania Bara hakuna wabunge na hata wabunge wao walioko kule bungeni wanaongea upuuzi mpaka tunasinzia na kufikia sisi kama akina Malecela kunyosha mkono na Spika wa bunge akituruhusu tunaomba tuzipigie kura hizo hoja zao," alisema. [82]
kulevya 
Inasidikiwa mitambo ya kusafishia madawa ya kulevya kule mpakani mwa Pakistani na Afghanistani ilisimikwa kwa msaada wa majasusi wa Marekani. [83]
kumi 
Hata kitendo cha Rais Karume kufanya sherehe za Mapinduzi kisiwani Pemba mara moja tu kwa miaka yote kumi tangu aingie madarakani ni kitendo cha kibaguzi. [84]
kuna 
Akijibu maswali ya waandishi wa habri jana kwenye mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa na Ewura, mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya uagizaji wa mafuta nchini (Taomac), Salum Bisarara alisema tayari kuna meli za mafuta ambazo zitaingia na kushusha mafuta bandarini wakati wowote. [85]
kununua 
Anatolea mfano wa Jimbo lake la Wawi kuwa kuna shule za sekondari saba ambazo zote hazina vifaa muhimu katika kufundishia kama vile maabara na anasema kuwa ilimlazimu yeye mwenyewe kama mbunge kununua vifaa hivyo kwa ajili ya wanafunzi wa shule za jimbo lake. [86]
kurudi 
Okello aliondoka kuelekea Tanganyika na kuanzia wakati huo alizuiwa kurudi Zanzibar na alipigwa marufuku pia asionekane Tanganyika na Kenya. [87]
kusema 
Mbali na kusema hivyo Kondic aliisifu timu ya soka ya Azam kwa kuwa na viongozi waliobobea katika masuala ya soka tofauti na timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu. [88]
kutoka 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeeleza kuwa, ilimnyima ruhusa ya kutoka nje ya mkoa, Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja kutokana na kubaini mapungufu kwenye barua yake ya maombi ya ruhusa hiyo. [89]
kutwaa 
Kwa ushindi huo Stars imejinyakulia dola 10,000 tofauti na awali ilivyotuwa jijini hapa ambapo mashabiki walikuwa wakiipa nafasin kubwa ya kutwaa ubingwa. [90]
kuutumia 
Wana nguvu, uwezo na nyenzo za kuutumia uhuru wao. [91]
kuuza 
Bisarara alitumia nafasi hiyo kukanusha taarifa kuwa wafanyabiashara wa mafuta wanaihujumu serikali kwa kugoma kuuza mafuta kama njia ya kupinga bei elekezi zinazotolewa na Ewura kwa madai kuwa wanapata hasara. [92]
kwa 
Tayari serikali imeshawafikisha mahakamani watuhumiwa 21 kwenye sakata la wizi wa jumla ya Sh133 bilioni, mawaziri wawili wa zamani na katibu mkuu wa wizara kwa makosa ya kutumia vibaya ofisi; na jana ilikuwa zamu ya kashfa iliyoitikisa nchi mwaka jana kuhusu utoaji wa zabuni ya ufuaji umeme wa dharura kwa Richmond. [93]
kwao 
Walikuwa wamezoea kukariri lakini kutokana na mabadiliko ya kutahini, hili naona limekuwa gumu kwao. [94]
la 
SASA ni dhahiri kwamba, serikali ya Rais Jakaya Kikwete haina mzaha katika kushughulikia tuhuma za ufisadi baada ya kumfikisha mahakamani mfanyabiashara, Naeem Adam Gire kujibu shtaka la kughushi na kutoa taarifa za uongo kuhusu uwezo wa Kampuni ya Richmond. [95]
lao 
Alifafanua kwamba Mafisadi hao wasipodhibitiwa kikamilifu hali itazidi kuwa mbaya ndani ya CCM kwani lengo lao ni kutetea ufisadi ndiyo maana alipozungumzia suala la ufisadi katika semina hiyo, Millya alisimama na kuanza kumshambuliwa. [96]
lazima 
Tatizo kila Waziri anayekuja anakuja na lake, kwa hali hii unategemea utafika wapi? Ni lazima mtaanguka tu kama tungekuwa na mfumo unaoleweka sekta hii muhimu ingekuwa ya mafanikio zaidi," anafafanua. [97]
leo 
Baada ya kusikiliza hoja zote, Hakimu Lema aliahirisha kesi hiyo hadi leo atakapotoa uamuzi wa dhamana. [98]
ligi 
Mwenyekiti wa Yanga Imani Madega aliishukuru TBL kwa kutimiza masharti yaliyopo kwenye mkataba huo na kudai kuwa udhamini huo umekuwa chachu kwa timu yake kufanya vizuri kwenye ligi ambapo imekuwa ikiongoza ligi tangu ilipoanza mwezi septemba mwaka jana. [99]
likiwa 
Kufuatia tukio hilo magari mawili Toyota Mark II likiwa na vielelezo mbalimbali vilivyoachwa na majambazi hao na la pili Toyota Cresta likiwa na simu ya mkononi, yalitelekezwa. [100]
mada 
Ole Sendeka alimtwanga ngumi Millya wakati wa mapumziko ya chakula ya semina ya kimila iliyohusu matumizi ya ardhi wilayani Monduli mwishoni mwa wiki iliyopita akidai kiongozi huyo wa vijana wa CCM mkoani Arusha alikuwa akimshambulia wakati akiwasilisha mada yake kuhusu Matumizi na Sheria ya Ardhi. [101]
madrasa 
Mwaka 1970 Pakistani ilikuwa na madrasa 500 tu za serikali na 800 za binafsi. [102]
mahaba 
Chai iliyoandaliwa kwa mahaba huamsha mahaba. [103]
makala 
Elias Msuya ni mwandishi wa makala wa gazeti la Mwananchi. [104]
malengo 
Vunjo (VICOBA) kushirikiana ili vifanikishe malengo ya kuwasaidia wananchi kupambana na umasikini. [105]
mara 
Kashfa hiyo ilitokana na tatizo kubwa la umeme lililoibuka miaka miwili iliyopita, mara baada ya serikali ya awamu ya nne kuingia madarakani. [106]
matokeo 
Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam, jana, Naibu Mkurugenzi wa Elimu Kanda ya Mashariki, Delux Lyimo alisema kiwango cha kufaulu kwa wanafunzi kimeshuka kutoka asilimia 96.17 mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 77.6 mwaka jana. [107]
mazuri 
Pamoja na kuomba mazingira ya kufundishia yaboreshwa tunawasihi walimu na wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto na kuwajengea maandalizi mazuri ya kufanya vizuri katika mitihani yao. [108]
mbali 
Lakini mbali na timu hizo kuishukuru TBL kwa vifaa hivyo, pia waliiomba kampuni hiyo kuharakisha suala la mabasi ili kuzirahisishia timu hizo usafiri wa kwenda mikoani kucheza mechi. [109]
mipira 
Mrwanda ambaye alifikisha mabao matatu katika mchezo huo, alionekana kuichachafya safu ulinzi ya Burundi sambamba na Ngassa lakini viungo walikuwa wakiwapandishia mipira ya juu ambayo mara nyingi haikuwa na madhara kwa Burundi. [110]
mjini 
Kocha huyo akizungumza mjini hapa jana alisema kwamba amezungumza na klabu mbili za Ligi Kuu za nje, lakini akaziambia zisubiri kwanza mkataba wake umalizike. [111]
mkwezi 
Yule mkwezi na mkulima aliyelengwa kukombolewa, ndiye yule yule leo anayejikuta akidharauliwa na kudhalilika. [112]
mmoja 
MGANGA mmoja wa jadi wilayani Chamwino amekamatwa akiwa na orodha ya watu walio na ulemavu wa ngozi (albino). [113]
moto 
Kwa mama na dada yangu ningependa kuwaambi sasa moto umeweka. [114]
msingi 
Maximo alisema kwamba ameanzisha msingi mzuri ambao anahitaji mtu mwenye mtazamo mwingine kuuendeleza. [115]
mujibu 
Kwa mujibu wa wakili huyo, mshtakiwa huyo anadaiwa katika shtaka la tano kuwa mwezi Juni mwaka 2006, alitoa nyaraka za kughushi akionyesha kwamba Mohamed Gire amezisaini kumuidhinisha mshtakiwa kufanya shughuli za kampuni hiyo Tanzania. [116]
mwendo 
Huo ndio mwendo wa Mbwa Kachoka. [117]
mwishiwa 
Si kila mtu anaweza kuchekesha? Kwa nini tusifanye na sisi?’ ‘Kweli kabisa mwishiwa Supu. [118]
mzima 
Alisema changamoto hiyo iliyotolewa na Kondic inapaswa kutekelezwa na timu zote za Ligi Kuu ili kuimarisha mfumo mzima wa uongozi na benchi la ufundi kwa ujumla. [119]
nafuu 
Wakili anayemtetea mshtakiwa huyo, Kato Zake aliiomba mahakama kutoa masharti nafuu ya dhamana kwa kuwa makosa anayotuhumiwa yanaruhusu kupata dhamana. [120]
namba 
Kamanda Kova alimtaja dereva aliyefariki kuwa ni Omary Single, huku mhazini Halima Salum na askari namba F8186 walijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kwamba hali zao zinaendelea vizuri. [121]
nao 
Baadaye mawaziri wawili wa serikali ya awamu ya nne, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha, nao waliachia ngazi. [122]
nayo 
MBUNGE wa Simanjiro kwa tiketi ya CCM, Christopher Ole Sendeka amesema matatizo anayokabiliana nayo kwa sasa na yaliyomsababisha amtandike ngumi mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) mkoani Arusha, James Millya ni mkakati maalum wa mafisadi unaolenga kumfuta katika uwanja wa siasa na kuonya kuwa wakiachiwa, chama kitakwenda pabaya. [123]
nazo 
Askari hao walikuja na silaha nyepesi ambazo hazikuweza kushinda zile walizokuwa nazo wafuasi wa Okello. [124]
ndilo 
Hilo ndilo lilikuwa tendo la kwanza la Mapinduzi. [125]
ndugu 
Na hii si chai tu kwa maana ya chai ndugu yangu, hii ni nafasi nyingine unayoweza kujipa kupata wasaa wa kuwa karibu na mumeo kuzungumza, kumuonyesha unajali na kuamsha hisia zilizojificha ndani yake. [126]
nia 
Pia alidai haikuwa nia ya Millya kulifikisha suala lake mahakamani bali msukumo wa mafisadi, ambao bado hajawaweka hadharani. [127]
nini 
JIBU: Wale walioshiriki katika Mapinduzi mpaka leo hawatuambii kwa undani nini ulikuwa mchango wa John Okello katika Mapinduzi yale. [128]
nyingine 
Katika hatua nyingine, Lyimo alisema kuwa wanafunzi 120 kutoka sekondari 32 walifutiwa matokeo yao baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu wakati watahiniwa 13 kutoka katika shule saba matokeo yao yamesimamishwa hadi hapo uchunguzi utakapokamilika. [129]
pale 
Malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar yalielezwa vizuri na Sheikh Karume katika mkutano wa hadhara pale viwanja vya Maisara, Unguja, tarehe 8 Machi 1964, kuwa ni kuondosha ubaguzi wa aina zote, kuleta umoja wa kitaifa, kuleta usawa miongoni mwa jamii na wananchi. [130]
pasi 
Burundi ambayo ilikuwa ikishangiliwa sana na mashabiki wa Uganda ilitawala idara zote kwa takribani dakika 60 za mchezo huku wakipiga pasi nyingi kadri wanavyotaka. [131]
peke 
Kwa hiyo siyo suala la Waislamu peke yao kuwa wahafidhina. [132]
pekee 
Vituo vingi vilikuwa vimebandika bei ya mafuta iliyotangazwa na Ewura, lakini ni dizeli pekee iliyopatikana katika vituo hivyo na kusababisha misululu mirefu kwenye vituo vichache vilivyokuwa vikiuza mafuta. [133]
pia 
Wakili huyo pia alidai mshtakiwa huyo alikuwa anafuatilia hati yake ya kusafiria kwa ajili ya kwenda kwenye matibabu na kwamba ameshatoa baadhi ya hati zake za nyumba kwa Jeshi la Polisi. [134]
pita 
Wakati huu wa kusherehekea miaka hii 45 ya Mapinduzi, pita mitaani kwa makabwela ushuhudie hali ilivyo. [135]
polisi 
Juhudi za kumpata kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Omary Mganga hazikufanikiwa, lakini taarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi mkoani hapa zilithibitisha kukamatwa kwa mganga huyo. [136]
rangi 
Akiwa Zanzibar, Okello alikuwa mwanachama wa chama cha wapiga rangi -akiwa anapaka rangi majumba mbalimbali. [137]
safi 
Pamoja na umeme, Pemba pia kuna matatizo ya ubovu wa barabara, uhaba wa maji safi, uchakavu wa bandari na miundombinu ya shule. [138]
sasa 
Kufikishwa mahakamani kwa Gire kunathibitisha kauli hiyo ya Pinda na sasa mambo mengi mapya yanasubiriwa katika kashfa hiyo iliyowekwa hadharani na Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa mbunge wa Kyela, Harrison Mwakyembe. [139]
sawa 
Alisema wanafunzi 64,422 wa sekondari 535 za mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro zilifanya mtihani huo ambapo 14,430 sawa na asilimia 22.4 walifeli. [140]
sekta 
Tatizo kubwa linalotukabili ni serikali kukosa mipango endelevu ya kuendeleza sekta ya elimu, kama serikali ingekuwa na mipango madhubuti haya yote yasingekuwapo, watoto wetu wangesoma katika mazingira mazuri na wangefaulu vizuri tu. [141]
sheria 
Ole Sendeka alidai kuwa Millya alidai katika mada yake kuwa wanasiasa wanadhulumu wafugaji ardhi kwa kutumia sheria na kutoa mfano wa Simanjiro, kitu alichotafsiri kuwa alikuwa akinangwa. [142]
shuti 
Burundi ambao bado walionekana kutulia na kupanga mashabulizi ya hatari kimahesabu, walikuwa wakimiliki mpira kwa kiasi kikubwa lakini Nsajigwa aliwaponyoka dakika ya 16 na kupandisha shambulizi kali lakini shuti lake likapaa. [143]
si 
Ni ukweli usiopingika kwamba, watoto wengi siku hizi, wasipofuatiliwa hawajali kabisa shule, hivyo wazazi muwe mstari wa mbele kuwahimiza kusoma, si tu kwa kuwapeleka tuisheni, kwani huko pia hufanya mambo yao wasipofuatiliwa maendeleo yao. [144]
sio 
Tunaomba masharti nafuu ya dhamana kwa sababu mshtakiwa wakati wote amekuwa akitoa ushirikiano katika upelelezi na afya yake sio nzuri," alisema Zake. [145]
siwezi 
Ukichunguza mtiririko wa mambo na ukisikiliza yasemwayo na wale waliokuwa karibu na mapinduzi unapata hisia kuwa mchango wa Okello ulikuwa mkubwa, lakini siwezi kusema kuwa kuliko Sheikh Abeid Karume hakutoa mchango wowote. [146]
soka 
KILIMANJARO Stars jana jioni iliwafariji Watanzania baada ya kuifunga Burundi mabao 3-2 huku ikicheza soka lisilovutia na kuchukua ushindi wa tatu wa Kombe la Chalenji. [147]
tangu 
Awali Kaimu Mkurugenzi wa Ewura, Anastas Mbawala, akielezea hali halisi ya uhaba wa mafuta ulioikumba nchi tangu Jumamosi, alisema hali hiyo imetokana na makampuni ya mafuta kuogopa kuagiza mafuta mengi wakihofia kupata hasara kufuatia hatua ya Ewura kutangaza bei elekezi kila wiki. [148]
tatu 
Katika shtaka la tatu mshtakiwa huyo anadaiwa kutoa taarifa za uongo kwa wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kwamba Kampuni ya Richmond ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme nchini. [149]
tu 
Lakini alidai kuwa Millya hajaandaliwa kugombea ubunge wa jimbo hilo, bali kumchafua tu. [150]
tupu 
Hawa wafanyabisahara ni wahujumu wa nchi kwa kuwa katika biashara wanayoifanya wanataka kupata faida ya asilimia 100 na kuacha nchi tupu," alisema Sakaya. [151]
uhaba 
Wakati huo huo waandishi Tumsifu Sanga na James Magai wanaripoti kuwa makampuni ya mafuta yanatarajia kuingiza shehena kubwa mafuta nchini ambayo itaondoa uhaba wa mafuta ulioikumba nchi kwa takribani siku nne sasa. [152]
uhuru 
Mapinduzi hayo pia yalitangaza uhuru mpya kwa Wazanzibari badala ya uhuru wa kwanza uliotolewa na Wakoloni wa Kiingereza tarehe 10 Desemba, 1963 uhuru ambao ulimwacha Sultani akiendelea kuitawala nchi hiyo kwa mlango wa nyuma. [153]
ulikuwa 
Ronaldo aliongeza: ìMwaka jana ulikuwa mzuri kwangu, lakini kushinda tuzo hii kumeniongezea heshima ya pekee. [154]
umri 
Kipindi cha pili kilianza kwa Burundi kuingia kwa kasi na kukosa nafasitatu za wazi, lakini Stars ilijipanga na kusawazisha dakika 68 kupitia kwa Jerry Tegete ambae alipokea krosi Shadrack Nsajigwa,mchezaji mwenye umri mkubwa kwenye kikosi cha Stars. [155]
umuhimu 
Alinijulisha umuhimu wa kuwa kwenye historia ya klabu kubwa kama hii katika maisha. [156]
usanii 
Ni kupoteza muda kabisa hata watumie usanii namna gani. [157]
usawa 
Hili Karume hakulizungumzia kwenye hotuba yake lakini ni changamoto kubwa katika kuleta usawa kwa Wazanzibari. [158]
usiku 
CRISTIANO RONALDO juzi usiku alitangazwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka 2008 na kubwaga mpinzani wake mkuu Liones Messi. [159]
utundu 
Lakini bado nafikiri huu unaweza kuwa utundu unaoweza kukutumia ukakusaidia. [160]
uwe 
Chai hii shosti haihitaji digrii, au lazima uwe umezaliwa na hotelia, laahasha na wala si ngumu kutengeneza almuhimu hapa ni makusudio yaliyolengwa. [161]
vema 
Tunapoadhimisha Mapinduzi haya, ni vema tuangalie suala la usawa kati ya Wazanzibari. [162]
vile 
Kila mmoja alikuwa akitaka nivunje mkataba huku halafu niende nikakataa kwa vile niliwaambia tatizo sifedha. [163]
vipaji 
Usiku wa vipaji mwishiwa. [164]
visiwa 
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ihakikishe kunakuwa na usawa kati wananchi wa visiwa vyote viwili kisiasa, kiuchumi na kijamii. [165]
vitabu 
Anaongeza kuwa kukosekana kwa vifaa vya kufundishia kama vitabu, maabara katika shule za sekondari ni tatizo kubwa ambalo Serikali ya Mapinduzi imeshindwa kulipatia ufumbuzi kwa kipindi chote hicho. [166]
vya 
WAKATI tatizo la upungufu wa mafuta likionekana kutopata ufumbuzi, wabunge wameitaka serikali kuchukua hatua kali, ikiwa ni pamoja na kuwanyang'anya leseni wamiliki wa vituo vya mafuta waliodiriki kuficha nishati hiyo muhimu na kusababisha usumbufu mkubwa. [167]
vyenu 
Hapa nawalinda kabisa na vijisenti vyenu. [168]
vyote 
Kuficha mafuta ni hujuma kwa uchumi, taifa na kwa wanajamii wote walio katika nchi hiyo kwani hutegemea mafuta, hivyo katika harakati za kuokoa hali hiyo, ni muhimu kufungia vituo vyote vinavyoficha mafuta na kuwapokonya leseni wamiliki wa vituo hivyo," alisema Sakaya. [169]
waamuzi 
Nafurahi kuwatangazia kwamba nimeongea na wahusika wakuu na wamekubali kuja hapa kuwa waamuzi. [170]
waishiwa 
Lo! Mimi nilidhani waishiwa watacheka na kuendelea na kujiliwaza kwao. [171]
wake 
Alisema Mgonja aliwasilisha barua ya kuomba ruhusa kwa ajili ya kwenda kuwaona wazazi wake wanaoishi mkoani Kilimanjaro na Arusha, lakini hakueleza anataka ruhusa ya siku ngapi. [172]
wakuu 
Hiyo ni kuanzia kwa mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na wataalamu mbali mbali. [173]
wakwezi 
Wao, wakulima na wakwezi, wanatakiwa kununua dawa za zaidi ya Sh5000, pato lao la mwezi mzima. [174]
wala 
Hata hivyo, alisema kuwa matokeo ya mtihani huo hautaathiri ama kumzuia mwanafunzi yeyote katika kuendelea na masomo kidato cha tatu wala kumlazimu kurudia kidato. [175]
wale 
Hivyo kuna wale ambao waliacha kufanya manunuzi makubwa ili kutosheleza siku za mwisho wa wiki pamoja na sikukuu ya Mapinduzi," alifafanua Mbawala. [176]
walijaribu 
Askari waliokuwa wamelala ghorofani bila ya kuwa na silaha, walijaribu kushuka chini. [177]
wanachuma 
Lakini wakati huu wengine wanachuma hivi hivi. [178]
wanajua 
Watakatifu hawa wanajua namna ya kuufaidi uhuru na ‘wako huru’ kufanya hivyo. [179]
wanatoka 
Kwa zaidi ya asilimia 80 ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanatoka Unguja. [180]
wangu 
Nimezungumza na klabu moja ya China na nyingine ya Afrika Kusini wote wananihitaji, lakini nimewaambia wasubiri kwanza nimalize mkataba wangu nikabidhi majukumu niliyopewa,"alisema Maximo. [181]
wao 
Wauzaji wa mafuta ni wezi na mafisadi, angalia leo serikali inafanya jitihada za kushusha bei wao wanaficha mafuta. [182]
wapi 
Hivi mafuta wanasema hawana kweli inaingia akilini wameuza wapi wakati kulikuwa na akiba ya siku nyingi. [183]
wapo 
Unajua tumeandaa mpambano huu ili kuwainua mabondia wa mikoani kama unavyojua wapo wazuri tu, lakini hawapati mapambano makubwa. [184]
watu 
MBUNGE wa Vunjo(CCM) Aloyce Kimaro amepiga marufuku tabia ya baadhi watu wa jimbo hilo kuishi maisha ya kuombaomba, badala yake amewataka wafanye kazi itakayowapatia kipato. [185]
wenyewe 
Lakini imani hizi zimeanza kujengea watu hali ya utengano kati ya Wakristo wenyewe, na kati ya Wakristo na Watu wa dini zingine. [186]
wenzangu 
Ningependa kuwashukuru wachezaji wenzangu kwa mchango wao. [187]
wewe 
Kwa kumtengea chai mumeo kama ni wadizaini hii utaonyesha mapenzi makubwa na wewe pia kupata nafasi ya kuzungumza naye mipango yenu ya baadaye kama si kupenyeza zako hoja. [188]
wezi 
Akizungumzia sakata hilo, mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli alisema wauzaji hao wanastahili kuitwa wezi na mafisadi kwa kuwa wamejipatia fedha nyingi kutokana na kuficha mafuta na baadaye kuyauza kwa bei ya juu katika siku hizo mbili, tofauti na ilivyokusudiwa. [189]
wimbo 
Aliwataka wananchi kutojengeka na kudanganywa na wimbo wa mafisadi unaoimbwa na viongozi wa vyama vya upinzani kwani vyama vingi vimekufa kutokana na kugombania fedha na kwamba suala la ubadhirifu wa fedha hakuna mtu anayelifurahia kwani hata CCM imeweka mikakati ya kuhakikisha inawachukulia hatua wale wote watakaohusika na suala hilo. [190]
yako 
Inashangaza sana kwa kipindi chote hicho cha miaka 45 serikali imeshindwa kutengeneza barabara zetu, sasa utajiuliza mafanikio ya Mapinduzi yako wapi kama miundombinu ya barabaara ambacho ni kiungo muhimu kabisa hakina hali nzuri?" anahoji. [191]
yao 
Kesi yao inatarajia kuendelea tena Februari 2 mwaka huu. [192]
yenu 
Ama baada ya salaam kwa idhini yenu naomba niweke mezani mada hii iliyoko mbele yetu hii leo; Chai ya saa kumi. [193]
yenye 
Baada ya Urusi kuivamia Afghanistan 1979, Marekani iliona hofu ya Ukomunisti kuitawala Asia MAshariki na hasa India, Pakistani, Uarabuni, hadi Malaysia na Indonesia yenye Waislamu wengi zaidi duniani. [194]
yeye 
Ni kweli kwamba Sheikh Karume hakuchukuwa silaha na kwenda kuvamia Ziwani, Mtoni au Stesheni ya Polisi ya Malindi, lakini yeye ndiye aliekuwa kiongozi wa siasa na waliofanya Mapinduzi yale walikuwa ni wafuasi wa chama alichokuwa anakiongoza. [195]
yote 
Hakusita kumsifia kocha wa United, Alex Ferguson kuwa ndiye siri ya mafanikio yake yote ya sasa. [196]
yule 
Hapo ndipo utamu wa mapigano uliponoga, kwani Okello alimpokonya silaha yule askari. [197]
zaidi 
Pia waziri wa zamani wa Fedha na Uchumi, Basil Mramba na waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kutumia vibaya ofisi zao na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh11 bilioni. [198]
zetu 
Ni jambo la kutia aibu kama sio kusikitisha kwa nchi kama Zanzibar kuwa na miundombinu mibovu hasa barabara wakati urefu wa barabara zetu si zaidi ya kilomita 1500 tu. [199]
ziada 
Wakati wa muda wake wa ziada alikuwa akiunda kikundi kidogo cha askari wa Kiafrika. [200]