Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2008-12-30

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


afya
Alisema kuwa cha msingi anamwomba Mungu awasaidie na waendeendelee kuwa na afya njema ili wajipange upya kwa umakini zaidi na kukiimarisha kikosi chao. [1]
aina
Hili linaweza kuwa tukio kubwa na la aina yake si tu kwa mwaka huu bali pia katika historia ya matukio ya uchomaji shule nchini. [2]
ajabu
Kuhusu taarifa kuwa bodi ya NDC haikuidhinisha fedha hizo kuidhamini Uhuru Capital Management, Kanali Simbakalia alisema itakuwa ni jambo la ajabu. [3]
akawa
Maisha ya Kazim yalibadilika ghafla, akawa ni mtoto wa kutoka familia ya kitajiri, sio maskini tena. [4]
akiwa
Kamanda mganga alisema tukio hilo lilitokea Desema 27 Mwaka huu mara baada ya kumalizika kwa maziko ya marehemu Athumani, aliyefariki dunia akiwa amelazwa katika Hospitali ya Misheni Mvumi, wilayani Chamwino. [5]
alionekana
Walimu waliokuwa wakimfundisha walimshangaa sana Kazim, kwani alionekana ni mwenye uwezo wa ajabu wa kuelewa mambo. [6]
alipokuwa
Kama ilivyo kwa wakati ule alipokuwa shule ya msingi, uwezo wake haukupungua bali uliendelea. [7]
aliuliza
Ni kweli kwamba hakuwahi kabisa kusoma shule yoyote?” aliuliza mwalimu Tito aliyekuwa na kazi ya kumfindisha somo la Hesabu. [8]
ama
Anaongeza kuwa kutokana na wazazi wengi kutokuwa na uwezo wa kifedha watoto wengi hawana mabegi ya shule hivyo wanapata wakati mgumu kubeba vipande hivyo wanapokwenda ama kurudi kutoka shule jambo ambalo linawafedhehesha sana na kuwakosesha amani. [9]
ambao
Akisimulia tukio hilo, Andingenye alisema kutokana na mtoto huyo kuchoshwa na kusumbuliwa na ustaadh huyo aliamua kumshtaki kwa wazazi wake, ambao kwanza walimuonya, lakini mwalimu huyo wa dini alikana kufanya kitendo hicho. [10]
ambapo
Mgulani walipata vikapu vyao kupitia kwa wachezaji wao Ibrahim Dua na Edmund Pastory ambapo kila mmoja aliweza kuonyesha umahiri wake katika mchezo huo. [11]
ambazo
Mahitaji ya mafuta katika nchi zenye viwanda, ambazo ndio wateja wakubwa wa bidhaa hiyo, yamekuwa yakishuka siku hadi siku kutokana na msukosuko huo, huku serikali za nchi hizo zikitaka mabadiliko katika teknolojia ya nishati inayotumika kuendeshea viwanda na magari. [12]
au
Karibu mwaka wa 20 sasa kama sio zaidi mazungumzo ni hayo kwa hayo hivi leo ukifika bandarini dare s salaam ukitokea Zanzibar unapekuliwa na ukionekana na doti mbili tu za kanga au televisheni moja kwa ajili ya matumizi yao unalipishwa licha ya kuwa na vielelezo vyote," alisema Salim Turky ambaye ni Mwekezaji wa ndani. [13]
awali
Akizungumzia nafasi ya Zanzibar katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Waziri Khatibu alisema ili kufaidi matunda ya ushirikiano huo kwa sasa Zanziba itakuwa na sehemu yake inayotegemea tofauti na awali ilipokuwa ikishiriki kupitia Serikali ya Muungano. [14]
awamu
Kiongozi huyo alisema kwamba lengo la upanuzi huo ni kuwezesha wanafunzi 13,480 kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika uteuzi wa awamu ya pili ambao wataungana na wenzao 10,600 walioteuliwa katika awamu ya kwanza. [15]
awe
Kwanza tabia ya kuwavamia wafanyabiashara ni imepitwa na wakati na kuwapiga faini ya laki tatu awe nazo au asiwe nazo ni mbaya sana kwa sababu kunawaumiza sana kiuchumi unamrudisha alipotoka kiuchumi ifike pahala mlipa kodi awe rafiki awe ni mdau mkuu wa uchumi katika nchi," alisema Rais wa Chama hicho. [16]
baadhi
POLISI mkoani Dodoma, wanawashikilia wakazi sita wa kijiji cha Chilembe wilayani Chamino,kwa tuhuma za kuhamasisha baadhi ya watu na kuchoma moto nyumba ya mwenzao anayehusishwa na kifo cha mtu aliyetambuliwa kuwa ni, Athumani Timetheo(18). [17]
baina
Hata hivyo, alisema bado kuna changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja malumbano baina ya viongozi wa serikali zote kwa kutumia vyombo vya habari badala ya kutumia vikao kutatua tofauti zinazojitokeza, akisema jambo hilo linawachanganya wananchi. [18]
bali
Tunakwenda Uganda si kwa ajili ya kusindikiza, bali kupambana na kuhakikisha tunafanya vizuri katika michuano hiyo kwani michuano hiyo ni kipimo tosha kwa timu yetu inayojiandaa kwa fainali za wachezaji wanaocheza ligi ya ndani itakayofanyika Ivory Coast mwezi Februari. [19]
bara
Tanzania bara wakati wenzetu wa bara wanaingiza bidhaa zao bila vikwazo," alisema Rais huyo. [20]
basi
Meneja wa bendi hiyo, Hassan Rehani alisema jumla ya wanamuziki 25 na viongozi watandoka kwa basi maalum la kukodi tayari kwa onyesho hilo la funga mwaka lililoandaliwa na Hoteli ya Safari Park. [21]
bei
SERIKALI imeshangazwa na kitendo cha wafanyabiashara wa mafuta nchini cha kupandisha bei ya bidhaa hiyo wakati kuna akiba ya kutosha inayoweza kutumika katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia sasa. [22]
benki
Ni kweli urasimu mkubwa umejitokeza kati ya taasisi husika iliyopewa jukumu la kutoa fedha hizo pamoja na benki ambayo itatoa mikopo hiyo na ndio maana hadi sasa tumeshindwa kutoa mikopo kwa walengwa. [23]
bibi
Kwanza akawa anaishi na bibi yake kijijini, hakuna simu wala aina yoyote ya mawasiliano. [24]
binti
Kamanda Andingenye alisema awali wazazi wa binti huyo mara baada ya mtoto wao kurudi likizo walimuomba ustaadh huyo amsaidie masuala ya kidini katika madrasa yake na ndipo ustaadh huyo alipoanza kushikwa na tamaa na kuanza kumlaghai ili afanye mapenzi na mwanafunzi huyo. [25]
bora
TIMU ya soka ya African Lyon(zamani Mbagala Market) itaingia kambini Januari 2 kwenye Chuo cha Ualimu cha Vikindu, Kisarawe ili kujiandaa na hatua ya pili ya tisa bora ya Ligi Daraja la Kwanza itakayoanza mapema Januari. [26]
bure
Inawezekana kuwa TBL wameshawaona viongozi wa BD kuwa ni wababaishaji kwani tangu chama hicho kianze kusimamia mchezo huo hakijawahi kuwa na ofisi hata ya kupewa bure, jambo ambalo TBL kama mdhamini anaweza kuwa na wasiwasi. [27]
chache
Kwa baadhi ya shule matukio ya moto yaliweza kutokea zaidi ya mara moja tena ndani ya muda wa siku chache. [28]
chuo
Kamanda Andingenye alisema tukio hilo lilitokea Desemba 26 saa 4:00 usiku katika maeneo ya karibu na chuo hicho. [29]
dawa
Kwa mujibu wa kamanda Mganga akiwa huko,mganga alimpa marehemu dawa ya kutapika ili imsaidie kupunguza uvimbe wa tumboni, lakini hali ilikuwa ilizidi kuwa mbaya. [30]
dini
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Thobias Andingenye alisema mwalimu huyo wa dini alikamatwa Desemba 24 majira ya saa 6:00 mchana kwenye nyumba ya kulala wageni ya Bembea iliyo maeneo ya Kiwanja cha Ndege mkoani hapa. [31]
dola
Katika soko la dunia, bei ya nishati hiyo imeshuka kiasi cha kugota kwenye dola 40 za Kimarekani kwa pipa kutokana na msukosuko wa kifedha ulioikumba dunia, kiasi cha kusababisha nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi dunia chini ya umoja wao wa Opec kukubaliana kupunguza uzalishaji wa nishati hiyo ili bei isioendelee kushuka. [32]
elimu
Lakini jitihada hizo zinapaswa kwenda sambamba na mambo mengine muhimu ili kufanikisha lengo la kuwapatia vijana wengi zaidi elimu ya sekondari. [33]
email
Binafsi kwa wale wote walionikumbuka kwa mwaka mzima iwe ni kwa email, barua, kwa kupigia simu, kunitumia meseji ama hata hao walio nibip nikapata hisia kuwa walikuwa wananifikiria na wananikumbuka kwa namna moja ama nyingine imenionyesha wanajali kiasi kama hicho, naomba niseme ahsanteni sana. [34]
eneo
Alisema kutokana na wizi huo wananchi wa eneo la Sota waliwabaini watu na kuwashambulia kwa kuwapiga mawe na marungu na kusababisha vifo vyao na pia kuwachoma moto. [35]
es
Jana, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa serikali haifahamu sababu za wafanyabiashara hao kupandisha bei ya mafuta. [36]
eti
Yaani watu wanafurika kupendekeza majina ya watu wanaostahili nishani ya viatu, kama yule mwandishi asiyeogopeshwa hata na asidi, na yule mtoto aliyemuuliza swali waziri mkuu aliyepitwa na wakati hadi akaandamwa na mashushushu eti mtoto hana akili ya kuuliza maswali kama hayo, na wale waliokaa barabarani mbele ya magari hadi shida zao ziliposikilizwa. [37]
fedha
Maharamia hao wa Kisomali wamesababisha hofu kwenye Bahari ya Hindi kutokana na kuendeleza vitendo vya utekaji meli na kudai fedha nyingi ili waziachie. [38]
fomu
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha fomu ya pingamizi hilo, mjumbe wa tume ya uchaguzi ya CUF, Hussein Mmasi alisema chama chake kiliamua kumwekea pingamizi Shitambala kutokana na kuapa katika kampuni ya uwakili badala ya Mahakama ya Wilaya. [39]
gani
Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Meja Jenerali Mstaafu, Said Kalembo aliipongeza timu hiyo kwa kutwaa ubingwa huo ambao utaurudisha katika ramani ya soka mkoa wa Morogoro na kuahidi kukaa na uongozi wa MRFA kuangalia jinsi gani ya kuwapongeza. [40]
gari
Mtapendekezaje kwamba sisi tupewe tuzo ya tako kwa kuthamini gari kuliko kompyuta. [41]
hadi
Awali wafanyabiashara hao walikuwa wakiuza mafuta hayo kati ya Sh1,300 na Sh1,400 lakini hivi katika kipindi cha kuelekea sikukuu ya Krismasi, yalipanda ghafla hadi kufikia bei ya kati ya Sh1,700 na Sh2,000 kwa petroli katika sehemu mbalimbali nchini. [42]
haki
Tunajiandaa kukata rufaa ndani ya masaa 48 yajayo ili tuweze kupata haki yetu ya msingi dhidi ya mgombea wetu ambaye tunaamini kuwa alikuwa na vigezo vyote vtya kushiriki kwenye uchaguzi," alisema Dk. [43]
hamu
Ninajivuna kuwa kwa sasa nina kikosi kizuri ambacho kinaweza kufanya makubwa ambayo wapenzi wa soka na Watanzania wanayasubiri kwa hamu," alieleza. [44]
hao
Serikali imetoa kauli hiyo wiki moja baada ya wafanyabiashara hao kupandisha bei ya mafuta ghafla kwa madai kuwa shehena walizokuwa wakitegemea zinashindwa kuja kutokana na utekaji wa meli unaofanywa na maharamia wa Kisomali kwenye Bahari ya Hindi. [45]
hasa
Kwa ujumla ZNCCIA inasema kwamba bado Zanzibar inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kubadilika kwa fikra za watendaji wa serikali hasa wanaosimamia shughuoi za biashara pamoja na wakusanyaji wa kodi wanahitaji kufanya kazi aktika ulimwengu wa sasa. [46]
hata
Alisema sababu nyingi zinaweza kujitokeza katika kipindi hiki, lakini ukweli ni kwamba sababu zote hizo hazina ushahidi hata kidogo hivyo haziwezi kuwa sababu ya kupanda kwa bei ya mafuta katika vituo vya kuuza mafuta sehemu yoyote nchini. [47]
hatutaki
Tumeanza mchakato wa kutoa fedha kwa wafanyabiashara wadogo kwa sababu hatutaki kupoteza muda. [48]
haya
Watu waje waone miondoko tofauti kama vile mganda katoka baharini , samaki ,wanaona haya wamefanywa vibaya ,taratibu usimkanyage na nyingine kibao. [49]
hedhi
Sababu ya hali hii ni nyingi ikiwemo ukweli kuwa baadhi yao hupata shida wanapokuwa katika vipindi vya hedhi. [50]
hekima
Mimi nilidhani nguvu inatokana na hekima na maarifa ya yanayosemwa. [51]
hii
Ninapenda kuchukua fursa hii kuwahakikishia wananchi kwamba serikali inafuatilia kwa karibu suala hili na itachukua hatua muafaka kila inapobidi ili kuhakikisha kuwa upatikanaji wa bidhaa za mafuta nchini unakuwa wa uhakika," alisema naibu waziri huyo. [52]
hisa
HATIMAYE hoteli ya Embassy, iliyo katikati ya Jiji la Dar es salaam, sasa iko chini ya milki ya watu binafsi baada ya serikali kuuza hisa zake kwa mtu binafsi kufuatia kutofanya kazi kwa takriban miaka mitano. [53]
hizo
Mbinu zote hizo zinazotumiwa na CCM zina lengo la kuwaibia kura wapinzani huku wakijua mshindi anapotangazwa, wapinzani huenda mahakamani, lakini hurudi mikono mitupu kwa kuwa wao ndio serikali," alisema. [54]
hoja
Nitatoaje hoja za nguvu huko sina gari la nguvu. [55]
humo
BAADA ya timu ya soka ya Mtibwa Sugar kutwaa Kombe la Tusker, Chama cha Soka mkoani humo (MRFA) kinatarajia kukaa na uongozi wa serikali ya mkoa ili kuangalia namna ya kuienzi timu hiyo kutokana na kuutangaza vyema mkoa wa Morogoro. [56]
huo
Kwa mujibu wa barua iliyotolewa na kusainiwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi jimboni hapo, Juliana Malange mgombea huyo wa Chadema hataruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi huo ulioandaliwa kuziba pengo lililoachwa na Mbunge Richard Nyaulawa aliyefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. [57]
huruma
Yule mzee alimuonea huruma, kwa namna ambavyo amekuwa akiishi maisha ya shida. [58]
huu
Desemba 28 mwaka huu majira ya saa 4.30 Asubuhi. [59]
huwa
Duni alisema kuwa CCM huvuruga daftari na kuongeza idadi ya wapiga kura kimiujiza na mwisho wake huwa ni matokeo ya kura kuonyeha idadi kubwa tofauti na idadi ya waliojiandikisha. [60]
huyu
Lakini kwa bahati mbaya huyu aliyependekeza tuzo ya tako kwa wanaoazimia kwenye mawarsha yeye mwenyewe amependekeza tu hatua zichukuliwe bila kuonyesha nani achukue hatua hii. [61]
ikiwemo
Rais Karume na tayari kazi imeanza ikiwemo kufanya uchambuzi yakinifu katika fomu mbali mbali za maombi tulizozipokea kutoka kwa wajasiriamali wetu," alisema. [62]
iko
Akizungumza na waandishi wa habari jana juu ya mafaniko na changamoto kwa wizara yake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mambo ya Muungano, Mohamed Seif Khatib alisema taarifa ya mshauri huyo kwa sasa iko katika hatua nzuri ya utekelezaji wa mapendekezo. [63]
ile
Naibu katibu huyo alifafanua kuwa mbinu nyingine ni ile ya kumwaga polisi vijijini ili kuwajengea hofu wananchi. [64]
ili
Uongozi wa Chadema mkoani Mbeya ulithibitisha kupokea barua yenye maamuzi hayo na kusema kuwa wanatarajia kukaa kikao baadaye jana usiku ili kujua hatima ya chama chao. [65]
ina
Hata hivyo, alisema matokeo hayo yanadhihirisha kuwa bado kuna kazi ya kufanywa na Ewura katika kusimamia mifumuko mikubwa kama hiyo ya bei ambayo ina athari kwa uchumi na kwamba wizara yake kwa kushirikiana na chombo hicho na taasisi nyingine watalitafutia ufumbuzi suala hilo ikiwa sambamba na kulipatia utaratibu wa kisheria utakaoimarisha utekelezaji na usimamizi wa sheria na kanuni zake. [66]
inafaa
Ili kufikia malengo kama ya Ligi ya mpira wa Kikapu Marekani (NBA) licha ya kuwa ligi yetu ni ya ridhaa, inafaa BD wajirekebishe ikiwa ni pamoja na kuachana na tabia ya kung'ang'ania mdhamini mmoja pamoja na kuweka programu za kueleweka ili waweze kurudisha matumaini yaliyopotea kuanzia kwa wadhamini wa ligi hiyo mpaka kwa wachezaji wa mchezo huo. [67]
ipo
Kwa vile bodi ya shirika haijawahi kuruhusu dhamana hiyo, serikali imeona ipo haja ya kuchunguza kwa kina matumizi ya fedha hizo na iwapo umetokea uvunjaji wowote wa sheria hatua mwafaka zichukuliwe haraka kwa watakaobainika kuhusika. [68]
juhudi
Maisha haya hayaridhishi hata kidogo na ndio maana kumekuwepo na juhudi za muda mrefu za serikali na hata wadau wa maendeleo kuwatoa Wahadzabe porini na kuwaleta karibu na huduma za kijamii kama elimu, maji na mengineyo. [69]
juu
Alisema kuwa pamoja na CCM kutumia mbinu hizo chafu, bado CUF haitakata tama kudai haki na kuendelea kuwaelimisha wananchi juu ya kuacha tabia ya kuuza shahada zao. [70]
juzi
WANANCHI wenye hasira kali juzi walichukua uamuzi usio wa kawaida wakati walipovamia ofisi ya mtendaji wa kijiji na kata ya Kanyerere wilayani Misungwi mkoani hapa na kuwaua watuhumiwa wawili wa ujambazi na baadaye kuchoma moto miili yao. [71]
kabisa
Kwa hali hiyo, wasichana wengi wa Kiafrika walio shuleni wanalazimika kuchagua kati ya kuhimili aibu inayotokana na kuhangaika kujihifadhi na hedhi katika mazingira ya shule na hasa hali hiyo inapotokea wakati ambao hawakutegemea au kukataa kwenda shule kabisa kuepusha aibu. [72]
kabla
Alisema kabla ya kumfikisha binti huyo katika nyumba ya wageni, ustaadh huyo alimpeleka kwenye duka la nguo na kumchagulia nguo za sikukuu na kisha kuziacha dukani huku akiahidi kuzifuata baadaye. [73]
kadhaa
Rubeya hakupatikana licha ya kutafutwa mara kadhaa. [74]
kale
Alisema wafanyabiashara wasionekane kuwa wakorofi na badala yake watendaji wa ZRB waachane na ufanyaji kazi wa kale na kucha vitisho na mawazo yasio sahihi na badala yake kushirikiana katika ukusanyaji wa kodi. [75]
kama
Lakini kama imeshindwa kuweka ukomo wa bei ya bidhaa hiyo muhimu, na badala yake imeiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) kukutana na wafanyabiashara wa mafuta kujadili suala hilo na kulitafutia ufumbuzi. [76]
kero
Mbali na vikwazo hivyo lakini pia wafanyabiashara wa Zanzibar wanailalmikia serikali kwa kutokuonesha umakini kushughulikia kero zinazowasumbua wananchi na wafanyabiashara kwa jumla ikiwemo wasafiri wanaotokea visiwani Zanzibar ambao tayari huwa wameshafanyiwa upekuzi lakini wanapofika badanri ya Dar es salaam hupekuliwa tena kama vile wanatoka nje ya nchi. [77]
kike
Uwepo wake katika eneo la Kakola lililo karibu na mgodi wa Bulyanhulu wenye pilika pilika nyingi za kimaisha na hata idadi kubwa ya watu kumeifanya shule hiyo kukumbwa na tatizo tete la utoro kwa wanafunzi linalosababishwa na wanafunzi kukacha shule ili kutafuta maisha kwa haraka na ujauzito kwa wanafunzi wa kike. [78]
kimapenzi
Lingine lililostua watu wengi walileleza kuwa walichoshwa na tabia za baadhi ya walimu kuwataka na kuwalazimisha kuwa na uhusiano wa kimapenzi. [79]
kisiwa
Alisema kwamba matatizo mengine yanayochangia kuwakimbiza wafanyabiashara wa kizanzibari kuwekeza visiwani hapa ni kuwepo kwa taasisi nyingi zinazosimamia masuala ya kodi katika kisiwa kidogo kama Zanzibar na kuitolea mfano TRA na ZRB kuwa zinaongeza urasimu kwa wafanyabiashara. [80]
kitita
Serikali imeagiza kufanyika kwa uchunguzi huo kwa lengo la kubaini walioidhinisha dhamana, kubaini wamiliki wa kampuni iliyodhaminiwa na kubaini uhusiano wa kampuni ya Uhuru Capital Management PTE iliyodhaminiwa na NDC kwa kutumia kitita hicho cha fedha. [81]
klabu
Habari za uhakika kutoka katika vyanzo vyetu na ambazo zilithibitishwa jana na uongozi wa klabu hiyo zilieleza kuwa uongozi wa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi umemsimamisha mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu. [82]
kodi
Rais huyo alisema kwamba mikakati ya muda mrefu ya kuimaliza Zanzibar kibiashara imetimia kwani licha ya kuwepo kwa vikwazo visivyo vya kodi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mashaka mengine mapya yataikumba Zanzibar chini ya soko la pamoja la Afrika Mashariki. [83]
koo
Na kama desturi ilivyo, mwenye pendekezo lazima alainishe koo za waishiwa, pamoja na kutoa posho la tako (si tuzo la tako). [84]
kozi
Kweli alipomaliza kidato cha sita, alifaulu kusomea kozi ambayo Mkurugenzi wa RaidMed aliipenda yaani ya utaalam wa kutengeneza simu, hata hivyo alimshauri ni vizuri aende kusomea nchini Finland ambako ndiko kwenye umaarufu wa kutengeneza simu duniani. [85]
kufaulu
Kuna wakati aliwahi kupewa mtihani wa kidato cha sita, alifanya na kufaulu vizuri. [86]
kufoka
Bila hata kutoa tuzo ya tume kwa ajili yetu, alianza kufoka moja kwa moja. [87]
kuiba
Huwezi kuiba fedha ukazificha Singapore. [88]
kula
Alisema hata hivyo mgonjwa aliwaambia watu waliokuwa wanakwenda kuona kuwa ugomjwa wake, ulitokana na kula chakula nyumbani kwa Yaledi ambaye ni jirani yake. [89]
kuomba
Kila alichofundishwa kilikuwa ni kama vile alishawahi kufundishwa mara nyingi, kwani alikuwa ana uwezo wa ajabu mno darasani, hadi wanafunzi wa madarasa ya juu wakawa wanakwenda kwake kuomba kufundishwa baadhi ya mambo ambayo hawakuwa wakiyajua. [90]
kuona
Kamanda huyo alisema baada ya kuona hali hiyo, mganga, alishauri mgonjwa apelekwe hospitalini kwa matibabu zaidi. [91]
kuonekana
Hata hivyo wengi walimsifia kwa kuonekana mwenye hekima. [92]
kura
Wakati huohuo, CUF imesema kuwa kinazitambua mbinu zinazotumiwa na CCM katika kuhakikisha kinapata ushindi kwa kuvuruga daftari la wapiga kura na kuongeza idadi watu kwa miujiza, ikidai kuwa hiyo ndiyo silaha yao kubwa. [93]
kusoma
KUNA mtu mmoja alinitumia meseji katika simu yangu Ijumaa ya wiki hii baada ya kusoma habari za maaskofu kukemea ufisadi, alishangaa kuona viongozi hao wa dini wanapoteza nguvu zao nyingi kukemea ufisadi wakati serikali haiwezi kuwabana mafisadi. [94]
kutishia
Hali hii ya ubabaishaji ilisababisha viongozi wa timu mbalimbali zinazoshiriki ligi hiyo kutishia kutoingiza timu zao uwanjani mpaka watakapopewa zawadi sasa hili ni tatizo jingine ambalo lisipoangaliwa litaupeleka mchezo huu katika hatua mbaya. [95]
kutoa
Waziri Asha alisema tangu viongozi hao kutoa ahadi za watoe fedha hizo, vijana wa Zanzibar hawajazipata kutokana na kuwepo kwa urasimu huo. [96]
kuu
Tunachosubiri ni mzunguko wa pili wa ligi kuu,î alisema. [97]
kwani
Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa Chama hicho Abdallah Abass amesema kwamba sasa hivi kilichobakia kwa wazanzibari ni maneno matupu yasioonesha dalili kwa kufufuka kwa uchumi kwani biashara ndio imefikia kikomo chake. [98]
kwao
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF), Florian Kaijage alisema timu hiyo inaondoka kesho jioni kwa ndege ya Kenya Airways ikiwa na wachezaji 20 na viongozi wanne na itaagwa leo hotelini kwao, FNJ , Msasani tayari kwa kwenda uganda kwa ajili ya michuano hiyo. [99]
kwenu
Na kwa maana hiyo naomba nichukue fursa hii tena kuwashukuru wasomaji wote wa makala zangu na zaidi niseme ni fahari iliyoje kupata kusikia kutoka kwenu. [100]
la
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeenguliwa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Mbeya Vijijini baada ya mgombea wake, Sabwee Shitambala kuondolewa katika orodha ya wagombea kutokana na Tume ya Uchaguzi kukubali pingamizi dhidi yake lililowekwa na vyama viwili. [101]
lake
Hata hivyo, Bhai alisema kuwa wanamsaka mtendaji wa kijiji hicho ambaye hakumtaja jina lake kwa mahojiano zaidi. [102]
laki
Alilalamikia kitendo cha operesheni za kivamizi kinachofanywa na maafisa wa ZRB kwa kisingizio cha kuwatafuta walipa kodi wasiolipa na kuwapiga faini ya laki tatu kila mmoja kuwa kinawerejesha nyuma wafanyabiashara. [103]
leo
Akizungumzia jitihada za serikali kukabiliana na tatizo hilo, Waziri Malima alisema kupanda kwa bei kunaathiri uchumi wa nchi na hivyo wizara yake imeiagiza Ewura kukutana na wafanyabiasha leo na kujadili suala hilo na baadaye mamlaka hiyo ipeleke maelezo kamili kuhusu suala hilo. [104]
lililo
Lakini ni suala lililo wazi kuwa miaka ya hivi karibuni ligi hiyo imekuwa taabani ambapo katika msimu wa 2008-2009, imeanza bila wadhamini hao kutoa fedha wala zawadi kwa timu shiriki hali inayofanya timu kucheza ligi hiyo kwa mkopo. [105]
mafanikio
Ligi hiyo kwa zaidi ya miaka sita inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) tena kwa mafanikio makubwa. [106]
maji
Bidhaa inayozalishwa na mtu mmoja kama umeme na maji ndiyo rahisi kuipangia bei na kuidhibiti ili wasifanye biashara ya kuwaumiza watumiaji wa mwisho. [107]
malengo
Tuliitumia kwa malengo maalum," alisema Kanali Simbakalia. [108]
mali
Baadaye tarehe 18 wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika na Stadi za Biashara (MUCCoBs) cha mjini Moshi nao walitangaza mgomo kwa kususa kuingia darasani na kufanya uharibifu wa mali pamoja na kuwashambuliwa kwa mawe na mchanga wahadhiri wa chuo. [109]
mama
Wanaharakati wa masuala ya elimu kwa wanawake nchini Zambia, Daphne Chimuka wa Jukwaa la Wanawake Wasomi Zambia (FAWEZA) na Barbara Chilangwa wa Kampeni ya Elimu kwa Wanawake (CAMFED) wanasema kipindi cha hedhi kinaweza kusababisha unyayapaa kwa watoto wa kike shuleni kwa kuwa katika tamaduni nyingi za Kiafrika mwanamke anachukuliwa kama mama wa familia. [110]
maskini
Sasa wanatoa msaada kwa sisi maskini wenye saa za Kiafrika bado. [111]
mawasiliano
Hata wao wanahitaji kuongeza maarifa na kufanya mawasiliano ya haraka. [112]
mazao
Anaeleza kuwa kwa kushirikiana na wafadhili mbalimbali wameweza kuwasaidia vifaa vya kilimo, nguo, vyakula, vyombo vya matumizi ya ndani, kuwafundisha kupika na kupanda mazao. [113]
mazoezi
Kocha mkuu wa timu hiyo, Marcio Maximo alisema jana kuwa wachezaji wote tayari wamewasili kambini na wameanza mazoezi tangu juzi kwa ajili ya michuano hiyo. [114]
mazuri
Mahudhurio katika Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam ambao hutumiwa kila mwaka na BD kwa ajili ya michezo ya ligi hiyo yalikuwa mazuri. [115]
mbili
Baada ya kugombana kwa muda mrefu kuhusu uchimbaji wa nishati hiyo, serikali ilimtafuta mshauri mwelekezi kwa lengo la kutushauri namna ya kugawana raslimali hiyo na kwa sasa tayari amekwishawasilisha taarifa rasmi ya mapendekezo katika serikali zote mbili namna ya kugawana raslimali hiyo," alisema Khatib. [116]
mengi
Ukiachia hilo yapo mambo mengi ambayo serikali imeahidi kuyatekeleza mwakani, ninaamini kwamba haitafanya makosa yale yale ambayo imekuwa ikifanya kila mara ya kuahidi bila ya kuwapo utekelezaji. [117]
mfano
Kisheria hatuwezi kupanga bei ya mafuta kwa sababu haizalishwi na mtu mmoja mfano. [118]
mgomo
Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, latangaza kuwasimamisha masomo kwa muda usiojulikana, wanafunzi wa shahada ya kwanza kufuatia mgomo waliouitisha kuishinikiza serikali iwaongezee fedha za mikopo. [119]
mgumu
Kwa watawala mwaka 2008 ulikuwa mgumu kwao. [120]
migodi
ILIJENGWA na kuanza masomo mwaka 2005 kama shule ya sekondari ya kata kwa ushirikiano wa nguvu za wananchi wa kata ya Bugarama iliyopo wilaya ya Kahama na kampuni ya Barrick Tanzania inayomiliki migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi, North Mara na Tulawaka. [121]
mingi
Katika Ligi ya Vodacom kuna mizunguko mingi na wachezaji hubadilisha mazingira mara kwa mara, wengi huugua kutokana na mazingira mageni lakini michuano ya Tasker tulikaa sehemu moja na kuzoea mazingira, alisema. [122]
miradi
Alisema wananchi wamekuwa na shauku kubwa ya fedha hizo ili waanzishie miradi yao na kujiunua kiuchumi. [123]
mjini
Akizungumza mjini hapa jana, Katibu Mkuu wa MRFA, Aristo Nikitas alisema chama chake kimepokea ushindi huo kwa furaha kubwa huku akidai kwa kiasi kikubwa ubingwa huo umetokana na chama hicho kuiandalia michezo mingi ya kirafiki timu hiyo kabla ya kuanza kwa michuano hiyo. [124]
mkoa
Akizungumza na Mwananchi kutoka Kigoma, mkurugenzi mkuu wa NDC wa wakati huo, Kanali Joseph Simbakalia, ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa huo, alisema taarifa hizo zinalenga kuchafuana na kwamba mambo yote yako bayana. [125]
mkononi
Angalia simu za mkononi. [126]
mkubwa
MABILIONI ya fedha zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kusaidia wafanyabiashara wadogo yamekwama kutokana na urasimu mkubwa unaodaiwa kuigubika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeelezwa. [127]
mkuu
Katibu mkuu wa Chadema, Dk. [128]
mlevi
Kwani ni lazima urudi kwa mama yako kama ni mlevi kiasi hicho na anayeishi mitaani,” alihoji. [129]
mno
Kwa sababu kauli hii ya Pinda kupiga marufuku matumizi ya mashangingi serikalini ilishawahi kuzungumzwa mno huko nyuma na mawaziri wengine, lakini tunaendelea kushuhudia yakiendelea kutumika. [130]
mpya
WASHAMBULIAJI wawili wa kimataifa wa Tanzania wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, Athumani Machuppa na Said Maulid watakuwa wageni rasmi katika uzinduzi wa albamu ya Dogo Mfaume iitwayo Kazi ya Dukanii utakaofanyika siku ya mkesha wa mwaka mpya, Desemba 31,2008 kwenye Ukumbi wa Luxury Pub Temeke Jijini Dar es Salaam. [131]
msaada
Katika mpango huo, vifaa hivyo vya kujisitiri vitakuwa vikitoka Marekani kama msaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali na kisha kusambazwa katika mashirika ya kujitolea yanayofanya kazi za kuwahudumia wasichana shuleni. [132]
mtihani
Christine Ishengoma kwa kuwa yalitokea wakati wanafunzi wa kidato cha nne wakiwa katika maandalizi ya kufanya mtihani wa mwisho wa kumaliza kidato cha nne. [133]
mvua
Nyumba ya nyasi aliyoachiwa na marehemu bibi yake ilikuwa ni kero nyingine, kwani kuna wakati mvua zilipokuwa zikinyesha, ilikuwa ikiingiza mvua. [134]
mwa
BAADA ya mizengwe ya hapa na pale iliyokuwa ikitolewa na Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD), hatimaye ligi hiyo maarufu mkoani humo ya Kili RBA imeanza mwishoni mwa wiki iliyopita ikizishirikisha timu 16, nne kati ya hizo zikiwa ni za wanawake. [135]
mwizi
Asubuhi ya siku iliyofuata Kazim alipata kipigo kikali kisha akaeleza ukweli kwamba yeye ni mtoto wa mitaani, hana baba na mama yake ni mwizi na mtumiaji wa dawa za kulevya mkubwa. [136]
mzima
Uongozi wa mgodi ulitoa ahadi mwaka jana mbele ya Rais Kikwete kuwa ingejenga maabara, mwaka mzima sasa, hakuna hatua yoyote iliyokwisha chukuliwa hali ambayo inawaathiri wanafunzi". Hata walimu nao ni wa mashaka. [137]
nani
Ismail aliongeza kuwa vikundi mbalimbali vya burudani ikiwemo wakali mbalimbali na TMK Squad vitaonyeshana nani mkali siku hiyo. [138]
nao
Kutokana na muda mfupi tulio nao, timu yangu itaendelea na mazoezi mpaka kesho asubuhi kabla ya jioni kuanza safari. [139]
naomba
Mwaka mpya naomba tumshukuru Mungu, maisha yanaendelea. [140]
naye
Wale wezi wenzake walipoona hakuna mawasiliano yoyote kutoka kwa Kazim waliondoka, hawakuwa na habari naye tena. [141]
nayo
Pia Waziri Khatib alizungumzia manufaa ya misaada ya kiuchumi na ya maendeleo inayotolewa na wafadhili kwa Serikali ya Muungano akisema umewekwa utaratibu wa kuhakikisha kwamba Zanzibar nayo inapata mgawo wake. [142]
ndivyo
Lakini ndivyo tulivyo. [143]
nguo
Alisema pamoja na ustaadh huyo kuonywa na wazazi, aliendelea na ushawishi wake na safari hii akaamua kutumia mbinu ya kumnunulia binti huyo nguo kwa ajili ya sikukuu ya Krismasi. [144]
nguvu
Ni kweli wahenga walisema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, lakini hatua hii ya NCCR-Mageuzi kujitoa kwa kuwa tu vyama vya upinzani havikuungana kusimamisha mgombea mmoja haikuwapa haki wanachama wake ya kuchagua au kugombea kiti hicho. [145]
ni
Taarifa dhidi ya pingamizi ya mgombea wa chama hicho ziliwakilishwa kwa msimamizi huyo wa uchaguzi jimboni hapo zikieleza kuwa Shitambala alikwenda kuapa katika kampuni ya uwakili badala ya mahakama ya wilaya, kitendo ambacho kimeelezwa kuwa ni kinyume cha sheria. [146]
nini
Waishiwa wateule, kwa nini hapa Tanzania, daima tuko upande wa watendewa kuliko watendaji? Hebu angalia maazimio mwisho wa warsha zote ambazo hatimaye mnene kwenye nguvu amesimamisha. [147]
njaa
Alipokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Henry Shekifu kuwa watu hao walikuwa wakikabiliwa na njaa kali baada ya ukame uliosababisha kupungua kwa matunda na mizizi wanayoitegemea kwa chakula. [148]
nje
Alifafanua kwamba haiwezekani mafuta yakapanda hapa nchini peke yake wakati nje ya nchi yanakotolewa bei yake inazidi kushuka hivyo ni lazima Ewura itoe maelezo ya kutosha ya sababu za bei ya bidhaa hiyo kuzidi kwenda juu. [149]
njia
Idrissa Mshoro uamuzi huo ulifikiwa na baraza la chuo kama njia ya kuepusha hatari chuoni hapo kufuatia mfululizo wa migomo wa zaidi ya siku tatu uliofanywa na wanafunzi hao wakiushinikiza uongozi pamoja na mambo mengine kutoa matokeo ya wanafunzi 227 yanayoshikiliwa na chuo. [150]
nne
Alisema kuwa hii ni mara ya tano kwa Twanga Pepeta kutumbuiza Kenya ambapo mara ya kwanza ilikuwa wakati wa uzinduzi maalum wa vituo vya huduma ya tiba, mara ya pili ilikua kwa ajli ya kusheherekea Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, mara ya tatu ilikuwa ya kuadhimisha miaka mitatu ya Mandao wa Kimataifa unao jishughulisha na tafiti za Uchumi na mara ya nne kwa ajili ya uzinduzi wa mtandao wa simu wa Orange. [151]
nzima
Ofisi nzima. [152]
pa
Tarehe 2 mwezi huu wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Muhimbili(MUHAS) watangaza mgomo usio na kikomo wakishinikiza uongozi wa chuo hicho kuwatekelezea madai yao ya kuwapatia mahala pa kuishi. [153]
papo
Lakini kompyuta zinadai maamuzi ya papo kwa papo. [154]
pedi
Hata hivyo hali hiyo inaweza isiendelee tena kwa watoto wa kike nchini Zambia kushindwa kwenda shule kwa kuwa wapo katika mzunguko wa siku zao kwani mpango wa kusambaza pedi kwa wanafunzi wa kike kunaweza kubadilisha hali hiyo kabisa na kuwafanya waweze kuhudhuria masomo na kujiendeleza zaidi. [155]
pepe
Mwanadishi wa safu hii, anapatikana kupitia barua pepe, juliusmagodi@yahoo. [156]
pia
Madai hayo ndio pia yaliyoifanya CCM kumwekea pingamizi mgombea huyo. [157]
pili
Katika tukio jingine jeshi la Polisi mkoani hapa linawashikilia wanafunzi wawili wa mwaka wa pili wa Chuo Kikuu cha Kiislam, Sadi Ayubu, 23, na Joseph Mwinjake, 27, kwa kuwashambulia na kuwajeruhi Abdul Mhanga, 22, na Mussa Rajabu wakiwatuhumu kuwa ni vibaka. [158]
sawa
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa serikali iliuza hisa zake zote 40 kwa gharama ya dola 538,640 za Kimarekani (sawa na zaidi ya Sh550 milioni za Kitanzania) kwa KJ ambaye sasa atakuwa anamiliki asilimia 80 ya hisa zote za hoteli hiyo wakati asilimia 20 imebaki kwa Kibo Hotels. [159]
si
Naibu waziri huyo pia alikanusha madai kwamba kupanda kwa bei ya mafuta kunasababishwa na meli zenye shehena ya mafuta kushindwa kufika nchini kwa kuhofia kutekwa na maharamia wa Kisomali na kusema kwamba madai hayo si kweli na hayana uhusiano na suala la kupanga kwa bei hapa nchini. [160]
siri
Hii haiingii akilini hata kidogo, iweje uongozi mpya ndio ucheleweshe vitu hivyo inawezekana viongozi wa BD walikuwa na agenda ya siri na huo uongozi wa TBL uliobadilishwa ndio maana huo mpya uliongia madarakani ukastukia mchezo huo na kuamua kutotoa vifaa ndani ya muda mwafaka. [161]
sisi
Hata hivyo sisi waishiwa tulifaidi sana maana tulikuwa tumeshajiteua kuwa tume ya tuzo. [162]
sita
JESHI la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia ustaadh wa madrasa, Dadi Ramadhani, 35, ambaye ni mkazi wa Mafiga mkoani hapa kwa tuhuma za kujaribu kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita wa Shule ya Msingi Kinondoni jijini Dar es Salaam. [163]
sura
Kwa sura hii wanaume wakware na wenye fedha zao wamekuwa wakiitumia hii kama fursa ya kuwarubuni na mwisho wa siku kuwapa ujauzito na kuwatelekeza. [164]
swali
Pengine, swali ni kuwa kwanini BD wawang'ang'anie udhamini pekee wa TBL wakati yapo makampuni makubwa nchini ambayo yakiombwa yanaweza kudhamini mchezo huo. [165]
taifa
Alitaja mafaniko mengine ya wizara yake kuwa ni kuundwa kwa Tume ya Fedha ya pamoja kwa lengo la kuhakikisha kwamba Zanzibar inachangia na kunufaika na mapato ya taifa. [166]
tako
HE jamani, mambo ya nishani ya viatu na tuzo la tako yameleta ubishi mkubwa sana. [167]
tano
Naye alipotafutwa, Kaduguda aliieleza Mwananchi kuwa apigiwe simu baada ya dakika tano na alipotafutwa baadaye alishauri atafutwe Katibu Mwenezi, Said Rubeya. [168]
tawi
Fedha hizo ziliwekwa kwenye tawi la benki ya Barclays la London. [169]
timu
Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa uongozi huo umeamua kumtupia virago Gabriel kwa madai kuwa si mchezaji wao kwani tayari alishauzwa katika timu ya Fanja iliyopo Oman. [170]
tuhuma
Sengerema wamewashambulia na kuwaua watu wawili kwa tuhuma za wizi. [171]
tukio
Bhai alisema kuwa siku ya tukio wananchi hao walivamia ofisi ya mtendaji wa Kanyerere na kuwashambulia kwa mawe na marungu watu hao wawili, Ben Saganya, 30, na Bundara Ruben, 26, na baadaye kuchoma moto miili yao. [172]
tume
Mamia ya mashabiki wa Chadema waliokuwa wamejikusanya katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi walionekana kujikusanya katika makundi baada ya uamuzi huo kutolewa, wengi wakiilaani hatua hiyo ya tume ya uchaguzi. [173]
uja
Mama yake, Joyce alikuwa akiishi mitaani baada ya kufukuzwa kutoka kwa wazazi wake baada ya kupewa uja uzito akiwa mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Sandara iliyoko katika kisiwa cha Bahe. [174]
ujana
IMEKUWA ni jambo lililozoeleka kwa wasichana wengi barani Afrika kuwa kipindi cha ujana ndicho kipindi ambacho hulazimika kukaa nyumbani kwa muda badala ya kwenda shule. [175]
ujenzi
Taasisi imeanzisha vituo nane vya elimu ya awali, ujenzi wa madarasa kwa elimu ajili ya elimu ya watu wazima na mabweni kwa wanafunzi wanaotoka mbali na vituo vya elimu. [176]
ule
KASHFA za ufisadi zimezidi kutanda baada ya serikali kuliagiza Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), kufanya uchunguzi wa matumizi ya zaidi ya Sh1.5 bilioni zilizotolewa kama mkopo kwa ajili ya upembuzi wa mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma na ule wa chuma wa Liganga. [177]
umma
Migomo, maandamano na hata vurugu kutoka kwa watumishi wa umma hasa walimu na walimu vimeandika ukurasa mpya wa historia ya Tanzania. [178]
upande
Chama Cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar (ZNCCIA) kimesema Zanzibar imemalizwa kiuchumi na Tanzania Bara na sasa wafanyabiashara wakubwa wanahamishia shughuli zao upande wa pili wa Muungano. [179]
utu
Kutokana na elimu kwa mtoto wa kike kutothaminiwa na kuheshimiwa, wamekuwa wakichukuliwa kama watu watakao kuja kuwa walezi tu wa watoto nyumbani” anasema Chimuka na kuongeza kuwa sheria za kimila zinachukulia kipindi cha ujana kwa msichana kama kiashiria cha utu uzima na hivyo kujiandaa kuolewa. [180]
uvuvi
Mbali na taarifa hiyo ya mafuta na gesi asilia, Waziri Khatib alisema serikali zote mbili zimeona umuhimu wa kuratibu shughuli za uvuvi kwa kuunda chombo maalum kwa lengo kuweka utaratibu wa kugawana mapato yanayotokana na uvuvi kwa ajili ya kuzinufaisha serikali zote mbili. [181]
vifaa
Haitoshi kuwa na vyumba vya madarasa kama vifaa vya kufundishia havipo au havitoshi, na hakuna walimu wa kutosha. [182]
vikapu
JKT ilimaliza kipindi cha kwanza ikiongoza kwa kuwa na vikapu 45 dhidi ya 26 vya Mgulani. [183]
virago
UONGOZI wa Klabu ya Simba umemsimamisha mshambuliaji wake wa kulipwa kutoka Nigeria, Orji Obina na kumtupia virago mkongwe, Emannuel Gabriel. [184]
vitu
Pia thamani ya hoteli hiyo inadaiwa kuwa sawa na dola 1.3 milioni za Kimarekani (sawa na zaidi ya Sh1.5 bilioni za Kitanzania), ikiwa ni majengo na vitu vyote vilivyo ndani ya hoteli hiyo. [185]
vya
Juzi Shitambala aliwekewa pingamizi na vyama vya CUF na CCM. Chadema ilimwekea pingamizi mgombea wa CCM kwa madai kuwa alisema uongo kuhusu mahali alipozaliwa. [186]
wako
Akizungumza na Mwananchi jana, kocha wa timu hiyo, Salum Mayanga alisema timu yake imejidhatiti kikamilifu na wachezaji wake wako katika hali nzuri. [187]
wala
Na wala hatuwezi kukubaliana na madai kwamba maharamia wa Kisomali ni chanzo cha kupanda bei mafuta. [188]
wale
Wachezaji wa timu hiyo ni Shaaban Nditi na Salum Swed na wale wa Zanzibar kama Soud Abdi na Abdalah Juma. [189]
wao
Alisema tayari wameshapata taarifa za pingamizi dhidi ya mgombea wao kwamba limetupiliwa mbali na lile la CUF na CCM kukubalika jambo ambalo alisema limezua utata ndani ya chama chake. [190]
wazi
Hatua hiyo ya NCCR-Mageuzi imekuja baada ya Chadema na CUF kushindwa kuafikiana kuhusu kusimamisha mgombea mmoja wa ubunge katika jimbo hilo lililoachwa wazi na marehemu Richard Nyaulawa aliyefariki dunia mwezi uliopita. [191]
wewe
Hiyo itakupa nafasi ya kuona wewe ni mtu muhimu kiasi gani na huenda ikawa nafasi nyingine kwako kumshukuru tena Muumba. [192]
wote
Hata hivyo, Mapunda alitetea kuwa wanahisa wote wawili wa hoteli hiyo ni Watanzania ambao ni wafanyabiashara wa muda mrefu hapa nchini. [193]
yale
Tukio hili na yale ya Lugoba yalimsikitisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dk. [194]
yapo
Pamoja na kwamba mafuta bado yapo ya kutosha nchini, sababu ya msingi iliyowafanya wapandishe bei hiyo haijulikani. [195]
yeye
Hata hivyo, Gabriel ambaye inasemekana uongozi wa Simba umemuza kisirisiri lakini yeye amekataa kuuzwa huko kwa timu hiyo ambayo si chaguo lake. [196]
yote
Alisema kuwa katika matukio yote mawili hakuna mtu anayeshikiliwa na kwamba Polisi itamuhoji Mathayo kuhusu tukio hilo. [197]
za
Kutokana na pingamizi lililowekwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) maombi yao yamezingatiwa na hivyo mgombea wa Chadema hataweza kuendelea na kampeni zozote za uchaguzi," inaeleza sehemu ya barua hiyo. [198]
zenu
Meseji zenu, email zenu zilinipa nguvu ya kuendelea na kila siku nilikuwa nasema hilo. [199]
zipo
Kama hiyo haitoshi timu zilizoonekana kuwa king'ang'anizi katika kudai vifaa hivyo, zilipozwa kwa kupewa mipira miwili huku zikiahidiwa kupatiwa jezi kwa madai kuwa ugawaji umechelewa kwa sababu jezi hizo zipo katika utaratibu wa kuandikwa majina ya timu pamoja na namba. [200]