Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-02-18

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aina
Kamanda Stephen alisema baada ya kumkabidhi viungo hivyo, watuhumiwa walikamatwa na walipopekua nyumbani kwa mmoja wao, walikuta dawa aina mbalimbali na maji ya kuchanganyia dawa hizo. [1]
ajira
KATIKA miaka ya hivi karibu baadhi ya viongozi wa dini wamejiingiza katika vitendo viovu ambavyo vinapoteza thamani ya utumishi na ushuda wao kwa wanaowaongoza, hivyo kuifanya jamii kudhani kwamba, huduma hiyo sasa ni sawa na ajira nyingine au imevamiwa na matapeli wanaotafuta mali. [2]
akakasirika
Mungu akakasirika. [3]
akawa
Jimbo la Ulanga lililokuwa likiongozwa na Marehemu Gundram Itatiro lilipogawanywa, nikawa Mbunge wa Ulanga Magharibi mwenzangu Itatiro akawa Ulanga Mashariki. [4]
albino
POLISI mkoani Mbeya inawashikilia watu wawili wakazi wa Kijiji cha Idweli, Kata ya Iyula, wilayani Mbozi, akiwemo mchungaji wa Kanisa la Pentekoste kwa tuhuma za kupatikana na viungo vya albino ambavyo vilikuwa vikiuzwa kwa Sh30milioni. [5]
alitoa
Alisema mara baada ya tukio hilo, mtoto huyo alirudi shuleni kuendelea na masomo na jioni alipofika nyumbani alimueleza mama yake aitwaye Upendo Masawe (40), ambaye alitoa taarifa kituo cha polisi kuhusiana na tukio hilo. [6]
amani
Katika kueleza umuhimu wa uhuru wa Mahakama, Jaji mkuu Augustine Ramadhan anasema;"Misingi ya katiba kama ilivyoainishwa katika utangulizi wa Katiba ya Jamhri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ni Uhuru, Haki na amani. [7]
anasema
Kwanza hakunipa fursa ya kunihoji, nashangaa juzi hapa wakati wa matatizo ya Edward Lowassa, Jaji Warioba anasema Lowassa hakuhojiwa, lakini hata yeye pia mimi hakunihoji. [8]
au
Shahidi: Ilikuwa ni majira ya saa 12:15 au 12:20 hivi. [9]
bado
Liyumba na Kweka walipandishwa kizimbani Januari 27, mwaka huu kwa tuhuma za kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia Seriakali hasara ya zaidi ya Sh221bilioni, Kweka bado hajapata dhamana. [10]
baina
Kabla ya kutolewa uamuzi huo, Hakimu Msongo aliahirisha kesi hiyo saa 6.34 mchana baada ya kutokea malumbano baina ya upande wa mashitaka na wa utetezi juu ya hati zilizowasilishwa mahakamani hapo na hati ya kusafiria. [11]
bali
Wakati wa kusoma hati hizo wakili Ndusyepo hakutaja namba wala mahali iliko bali alitaja jina lililoko kwenye hati husika. [12]
bara
JAKAYA Kikwete ameachia wadhifa wa uenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), bara lenye kila aina ya historia na linalokabiliwa na changamoto nyingi ambazo kila kunapokucha zinazidi kuongezeka na kufanya ndoto ya kufikia malengo ya maendeleo kufifia kila siku. [13]
bila
Alisema, vita hiyo inaendeshwa na baadhi ya magazeti yanayoingilia faragha za watu bila ya kuzingatia maadili na kwamba vita hiyo imechukua sura mpya baada ya magazeti mapya kuanzishwa au ya zamani kufufuliwa upya kwa lengo la kutukanana na kuchafuana. [14]
bili
Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Biashara (Dawasco), Raymond Mndolwa shirika hilo limepata hasara ya zaidi ya Sh74 milioni kutokana na mmilikiwa wa matenki hayo kutolipa bili za maji tangu Aprili 2008 licha kupelekewa Ankara. [15]
burudani
Naamini maandalizi yanakwenda kama tulivyopanga na kila mmoja atafurahi kupata burudani na neno la injili kupitia nyimbo,” alisema Msama. [16]
cha
Shahidi Jane: Nilisema nilitoa maelezo Central Police ( Kituo Kikuu cha Polisi). [17]
chake
Akizungumza na Mwananchi mjini hapa jana, Rais wa PST, Emmanuel Mlundwa alisema anaamini kinachowasukuma mabondia hao kutaka kupigana na Cheka ni njaa jambo ambalo chama chake hakipo tayari kuona linafanyika. [18]
chetu
Katika uongozi wa chama chetu, niliingia mwaka 1975, kama mjumbe wa mkutano mkuu wa TANU ambao ulikuwa ndio wa mwisho kabla ya kuunganishwa na Afro Shiraz Party. [19]
dhana
Akiizungumzia kwa kina dhana ya Uhuru wa Mahakama, Jaji Ramadhan anasema;"Mahakama inatakiwa iwe huru na mahakama ya utendaji (Executive). [20]
dhidi
Tukio hilo linalomhusisha mchungaji, limekuja wakati nchi ikiwa katika kampeni ya kupambana na ukatili dhidi ya maalbino, ambayo hupewa msukumo pia na viongozi wa dini mbalimbali. [21]
dunia
CHAMA cha ngumi Tanzania (PST), kimesema hakitakuwa tayari kuruhusu pambano kati ya bondia Francis Cheka anayeshikilia mkanda wa dunia wa ICB na mabondia Kalama Nyirawila na Mada Maugo kutokana na mabondia hao kutokuwa na uwezo. [22]
enzi
Lakini ilikuwa dhahiri kwamba zile shule nyingi za watu binafsi enzi zile zisingeweza kufanikiwa hata kidogo. [23]
es
WASHITAKIWA wa saba na wa tisa katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini wa Mahenge, mkoani Morogoro na dereva teksi wa Manzese Dar es Salaam, PCL Emmanuel Mabula na PC Michael Sonza wameieleza Mahakama Kuu kuwa ACP Abdallah Zombe, aliwapongeza kwa kuwa walikamata majambazi. [24]
for
Mradi wa majengo pacha ya BoT Makao Makuu, unaelezwa kutumia kiasi kikubwa cha fedha zaidi ya Sh500 bilioni, ambazo thamani yake (Value for Money) imejaa utata. [25]
fupi
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mohammed Babu wakati akitoa taarifa fupi ya mkoa huo kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye aliwasili mkoani hapa juzi kwa ziara ya kikazi ya siku ya tatu kumalizia maeneo ambayo alikatisha Mwezi Oktoba mwaka jana. [26]
gani
Shahidi huyo aliendelea kuieleza mahakama kuwa, habari za mauaji hayo alianza kuzisikia kwenye vyombo vya habari kati ya Jumatatu na Jumanne, lakini hakuweza kujua ni majambazi gani hasa kwa kuwa alisikiliza vichwa vya habari vya magazeti redioni kama ilivyokawaida yake kabla ya kwenda kazini. [27]
ghafla
BENDI ya Msondo Ngoma, imesimamisha maonyesho yake kwa wiki moja kufuatia kifo cha mwanamuziki wake, Joseph Maina aliyefariki ghafla jana kwenye daladala. [28]
hadi
Hata hivyo, katika ushahidi wao walioutoa mahakamani hapo, Mabula alidai yeye hakuhusika na vifo vya wafanyabiashara hao na kwamba, hakuwahi kufika eneo la tukio walikokamatwa wafanyabiashara hao na wala hawakuwahi kulijua eneo hilo hadi siku mahakama ilipotembelea. [29]
halisi
Umejengeka mtazamo usio sahihi kuwa ambao unapotosha dhana halisi na sahihi ya uhuru wa Mahakama. [30]
hao
Hata hivyo, mashahidi hao walitambua maelezo ya awali jana mbele ya Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Salum Masatti wakati wakitoa ushahidi wao. [31]
hapa
Wakili: Shahidi, IGP aliunda timu kuchunguza tukio hili iliyokuwa chini ya Mgawe na hapa kuna kielelezo Ex. [32]
haraka
Alisema, uchumi wa nchi unanyonywa kwa meli kukaa kwa siku nyingi katika bandari ya Dar es Salaam na hivyo kutakiwa kuchukua hatua za haraka kuhakikisha msongamano huo unaondolewa ili kulinda uchumi wa nchi. [33]
hata
Shahidi: Mheshimiwa Jaji hata kuitwa tu sikuitwa. [34]
hati
Uamuzi huo kwa mtuhumiwa huyo ulitolewa jana saa 8:00 mchana na Hakimu Mkazi, Hadija Msongo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambaye alisema kuwa mshitakiwa huyo atakuwa nje kwa dhamana ya Sh882milioni, wakati mahakama ikijiridhisha na hati nyingine zilizokataliwa na upande wa mashitaka. [35]
hatua
HATIMAYE aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA) katika Benki Kuu Tanzania (BoT) Amatus Liyumba, amepata dhamana ya Sh882milioni, huku serikali ikilalamika nje ya mahakama kutoridhika na hatua hiyo. [36]
hawa
Shahidi: Kwanza nilimueleza hawa watu siwatambui na sijawahi kuwaona. [37]
hicho
Alisema baada ya makubaliano ya kiasi cha Sh30 milioni kushindikana na kuahidiwa kukamilisha fedha hizo siku inayofuata (Februari 17), kachero huyo alifika na kiasi hicho cha fedha na kupeleka nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa na kukabidhiwa vipande vinne vya viungo hivyo, vikiwemo viganja vilivyohifadhiwa katika magazeti mawili tofauti. [38]
hii
Kumeanzishwa vita kupitia vyombo vya habari vinashambuliana kwa namna tofauti zinazokiuka maadili ya taaluma na ya kijamii, Baraza linaona vita hii haina tija kwa taifa na ni hujuma kwa taaluma ya uandishi wa habari” alisema Mukajanga. [39]
hiki
Tumesimamisha maonyesho yetu, kwa kipindi hiki nawataka mashabiki wetu kuwa watulivu na wastahimilivu katika kipindi hiki kigumu,” alisema Gurumo. [40]
hizi
Mshitakiwa utatakiwa kutimiza masharti ya dhamana ya kiasi kilichobaki cha Sh54,417,344,800.23 endapo mahakama itaona kuwa hati hizi zina kasoro,” alisema Msongo. [41]
hizo
Shahidi : Hizo particulars ni zangu, lakini maelezo si yangu maana hizo particulars ziko makao makuu,hivyo inawezekana waliyapata huko. [42]
hotel
Alifafanuwa kuwa, mmiliki wa maangi hayo wanafika katika eneo hilo na mgari kuchukua maji na kuyapeleka katika viwanda pamoja na hotel zake. [43]
hufanya
Kwakuwa nchi yetu ni ya Kidemokrasia mihimili hiyo hufanya kazi kwa kushrikiana. [44]
hujuma
BARAZA la Habari Tanzania (MCT), limekemea ‘vita ya magazeti’ inayoendelea kushamiri nchini na kwamba hiyo ni hujuma kwa taaluma ya uandishi wa habari. [45]
huku
Naye Sonza akihitimisha melezo yake ya ushahidi aliiomba mahakama itende haki, huku akidai kuwa katika mashahidi wote 37 waliotoa ushahidi mahakamani hapo hawakuwa kweli. [46]
huo
Ushahidi huo unawafanya Mabula na Michael, kuwa washitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo kukubali maelezo ya awali, tofauti na washitakiwa wengine wanne waliomtangulia ambao wote walikana maelezo yao, wakidai hawajawahi kuhojiwa na chombo chochote kuhusiana na mauaji hayo. [47]
huru
Katika kesi hiyo aliyekuwa mshitakiwa wa nne F.5912 PC Noel Leonard, mshitakiwa wa sita D.6440,CP Moris Nyangelela na mshitakiwa wa nane E6712 CPL Felix Cedrick, waliachiwa huru baada ya mahakama kuwaona kuwa hawana kesi ya kujibu. [48]
huu
Hakimu Msongo alitoa ruhusa ya siku mbili Februari 18 na 19 mwaka huu na kwamba wakati wa upelelezi, mshitakiwa ataruhusiwa kuwa na mawakili wake binafsi. [49]
huwa
Tatizo utaratibu huu haupo, hata wakikutana huwa ni kwa bahati tu tena kwenye matukio ya kitaifa na hawajadiliani kwa kina. [50]
ibilisi
Tunaona nchi nyingine zikielekea kukutana na ibilisi lakini sisi ni tofauti. [51]
ife
Siseme siku hii ife lakini ninachotaka kusema mimi; hivi kweli hatuwezi kusherehekea siku hii kila siku ya maisha yetu kwa kuhuisha upya ndoa zetu na waume zetu, ila kila siku iwe siku ya wapendano!? Kwa sababu ukweli utabaki kuwa wanaopendana ni wale waliooana. [52]
ile
Baada ya kuona hali ile, watu walijaa na niligeuza gari hadi kituo cha polisi Maghorofani, lakini na wao walinipa askari wakaniambia tuelekee hospitali ya Temeke," alisema Salum. [53]
ili
Katika ushahidi wao, Mabula na Michael waliieleza mahakama kuwa, waliwahi kuitwa kwenye timu zote mbili za polisi na katika Tume ya Jaji Kipenka, ili kutoa maelezo kuhusiana na tukio hilo na kwamba, maelezo hayo yaliyotolewa mahakamani hapo kama vielelezo ni sahihi. [54]
ilivyo
Kutokana na hali ilivyo sasa; viongozi wa serikali wamekuwa wakishangaa jinsi taasisi za dini zinavyoendeshwa na baadhi ya watu kinyume cha maadili yao na hatimaye kuwashauri watumishi wa Mungu kuwasaidia wenzao waache kufanya mambo ya aibu. [55]
imeweka
Katiba imeweka mamlaka tatu: Mamlaka ya utendaji, mamalaka ya ya utoaji wa haki na mamlaka ya kutunga sheria. [56]
ina
Alionya kuwa, huu si muda wa kutukanana na kuchafuana bali ni muda wa wanataaluma kukaa ili kutafakari kwa kina na kufanya uandishi makini kwa lengo la kuonyesha kwamba, taaluma hii ina watu mahiri, wakomavu, wastaarabu na wanaowajibika ipasavyo kwa jamii. [57]
inapaswa
Mahakama pia inapaswa iwe huru kwa wenye kesi, mbele yake. [58]
inazungumzia
Sura ya pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazungumzia Utawala yaani serikali. [59]
injili
TAMASHA la kila mwaka la Pasaka limepangwa kufanyika Aprili 13 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam likishrikisha waimbaji wa injili kutoka Afrika Mashariki na Kati. [60]
iwe
Awali, utekelezaji wa sheria hiyo ulianza kwa majaribio katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Shinyanga, Mwanza, Ruvuma na kwamba lengo ikifikia 2010, taasisi hiyo iwe imejikita nchi nzima. [61]
jumla
Hata hivyo, taryari jumla ya tani 1,021 zimekwishapelekwa kwa walengwa. [62]
juu
Shahidi: Kumuuliza bosi wangu aliye juu yangu zaidi ya mara 10 ni kosa la jinai. [63]
kabisa
Lakini jamii inapoona wanaowahubiria kuacha maovu wanafanya hayo hayo, huchanganyikiwa na wenye imani ndogo huachana kabisa na masuala ya dini. [64]
kadhaa
JKT Ruvu wao walionekana kubadilika sana katika mchezo wajana na kurekebisha makosa kadhaa yaliyowafanya na kuwafanya wafungwe mabao 4 - 1 katika mchezo wao uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar. [65]
kamati
Mwaka 1977 ndiyo nikawa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya Morogoro Mjini ya CCM, kamati ambazo baadaye zikabadilishwa na kuitwa Kamati za Siasa. [66]
karibu
Shahidi: Tulikuta maofisa karibu wote wa polisi wa mkoa wa Dar es Salaam. [67]
kavu
Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua Bandari za nchi kavu (ICD's) na kutathimini maagizo ya rais ya kupunguza msongamano wa makontena bandarini hapo. [68]
kidini
NADHANI wasomaji mnaelewa sasa kuwa mgogoro kati ya Waisraeli na Wapalestina msingi wake sio imani za kidini. [69]
kikao
Kauli hiyo imetolewa kufuatia kumalizika kwa kikao cha Bodi ya MCT kilichofanyika jana kujadili vita ya magazeti na uandishi wa kuchafuana ulioibuka nchini. [70]
kikosi
WAKATI Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo alitarajiwa jana kutangaza wachezaji 23 watakaounda kikosi chake kitakachoshiriki michuano ya CHAN, habari za uhakika zilizopatikana jana zilieleza kuwa wachezaji Uhuru Suleiman na Zahoro Pazi wa Mtibwa wameachwa. [71]
kikuu
Katika kuchambua hali hiyo, Mhadhiri mwandamizi katika kitivo cha sheria cha Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Chris Peter Maina anachambua mwingiliano huo na sababu zake. [72]
kila
SERIKALI inapoteza zaidi ya Sh20 milioni kila siku kutokana na kulipa fidia za meli zinazochelewa kupakuliwa katika Bandari ya Dar es Salaam, Waziri wa Miundombinu, Shukuru Kawambwa amesema. [73]
kile
Vile vile kuna matatizo ya miundombinu hayajadiliwi na kusaidiwa kutatuliwa na kamati za ushauri za mikoa na wilaya katikamaeneo yao kwa kile kinachodaiwa kuwa kufanya hivyo ni kuingilia uhuru wa mahakama. [74]
kuanzia
Alisema washiriki za mbio hizo wataanza kujiandikisha kuanzia Februari 27 na 28 katika Hoteli ya Keys na watu zaidi ya 600 kutoka nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki mbio hizo. [75]
kubadilisha
Katiba siyo ya kubadilisha kila siku. [76]
kudai
Palestina ikageuka kutoka nchi yenye dola kuwa nchi tawaliwa na ndipo makundi kama PLO ya Yassir Arafat yalianzishwa ili kudai uhuru ambao ulimezwa na upanuzi wa ardhi wa Waisraeli. [77]
kufungua
Sheria zilizokuwepo zilimtaka mtu anayekata rufaa ya matokeo ya uchjaguzi kutoa kiasi cha shilingi milioni tano kabla ya kufungua kesi. [78]
kuleta
Alisema nchi zinazotaraji kuleta wasanii wake niKenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Zanzibar. [79]
kumaliza
Jibu: Nilianza siasa kama mwanachama wa Tanganyika African Union (TANU) niliingia Novemba mwaka 1967, baada ya kumaliza Shahada yangu ya kwanza katika kilimo. [80]
kumbe
Wananchi wanaweza wakaamini kuwa mshitakiwa ni mhalifu kumbe Mahakama ikamwona siyo. [81]
kumpa
Alisema mshitakiwa huyo, alitenda kosa la kuomba rushwa kiasi cha Sh200,000 kutoka kwa ndugu wa mshitakiwa wa kesi ya kutorosha wasichana wa kike ili amsaidie kumpa hati ya kumtolea mshitakiwa huyo mahabusu. [82]
kumzika
Nilikuwa nazungumza na mwanafunzi wangu ambaye ni mtu wa imani thabiti ya Kikristo na mchungaji akanikumbusha kuwa hata ukisoma katika Biblia, Ishmael na Isaka walishirikiana katika kumzika Sarah (mama yake Isaka) na kumzika pamoja baba yao Ibrahim. [83]
kuna
Shahidi: Nilimuuliza Nyangelela kuna nini, akasema jana walikamata watu wakiwa na fedha kwenye tukio la ujambazi. [84]
kurudi
Shahidi:Tulikaa hadi saa 11:30 tulipoanza kurudi kituoni. [85]
kusema
Shahidi: Nilipokaribia alitoka ofisini na kusema haya pandeni kwenye gari askari wote mliokuwa doria. [86]
kutia
Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba, baadhi ya watumishi wa Mungu wanajiingiza katika vitendo vya ujambazi, utapeli, ushirikina, mauaji na vingine vya kutia aibu. [87]
kutoka
Akiongozwa na wakili wake Majura Magafu, Jane aliieleza mahakama kuwa alifika kwenye eneo la tukio mahali walipokamatwa wafanyabiashara hao, akiongozana na mshitakiwa wa tatu ASP Makelle na kwamba, waliwakuta askari polisi kutoka Chuo Kikuu wakiwa wamewakamata wafanyabiashara hao. [88]
kuu
Vilevile nilikuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa. [89]
kuzuia
Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Mary Moyo , mwanasheria wa Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (Takukuru) mkoa wa Iringa, Nitume Mizizi, alisema mshitakiwa huyo alikamatwa kwenye mtego uliowekwa na Takukuru baada ya kuletewa taarifa kutoka kwa mlalamikaji. [90]
kwake
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Zelothe Stephen alisema mtuhumiwa mwingine ni mkulima wilayani Mbozi. [91]
kwani
Nimeridhishwa na utekelezaji wa maagizo ya rais ya kupunguza msongamano wa makontena bandarini, kwani Serikali inapata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 20 kwa siku kama fidia wakati meli inapocheleweshwa kupakuliwa," alisema Dk. [92]
kwao
Alidai Makelle aliwaagiza askari wale wawachukue watuhumiwa hao hadi kituoni kwao kwa ajili ya kuwafanyia mahojiano, baada ya hapo Makelle aliwapeleka Ubungo Terminal ili kuungana na wenzao kwa ajili ya doria na Makelle akaondoka. [93]
la
Kwa nyakati tofauti, wakiongozwa na Wakili wao Majura Magafu, akitoa ushahidi wake, Mabula alikiri maelezo yote aliyoyatoa kwenye timu mbili za polisi na Tume ya Rais Jakaya Kikwete, iliyoongozwa na Jaji Mussa Kipenka, ambazo zote ziliundwa kwa lengo la kuchunguza ukweli wa vifo vya wafanyabiashara hao. [94]
lazima
Kiongozi wa siasa lazima uonekane safi mbele ya wananchi, kwa sababu serikali inaheshimiwa machoni mwa wananchi ikiwa safi, serikali safi lazima iongozwe na watu safi. [95]
lenye
Maina alifariki ghafla juzi asubuhi akiwa ndani ya basi la daladala lenye namba za usajili T582AFL linalofanyika safari zake, Mwenge na Temeke Mikoroshoni. [96]
leo
Habari zilizopatikana baadaye jana zilisema kuwa mwili wa Maina unatarajia kusafirishwa kwenda Tanga kwa mazishi yatakayofanyika kijijini kwao Mkuzi, Muheza Tanga baada ya heshima za mwisho zitakazotolewa leo nyumbani kwa kaka yake, Kurasini, Dar es Salaam. [97]
letu
Mambo hayo ni ulinzi na usalama, kutetea maslahi na kutafuta fursa za kiuchumi na kisiasa zitakazoleta maendeleo na ustawi wa bara letu, kushughulikia masuala ya jamii na utamaduni na kuimarisha Umoja wa Afrika na taasisi zake. [98]
linavyoingilia
Mfano mwingine kuonyesha jinsi Bunge linavyoingilia uhuru wa mahakama ni kesi ya Chumchia ya mwaka 1988 ya Deportation. [99]
lolote
Shahidi: Hapana hatukuwahi kukutana na tukio lolote. [100]
mabara
BAADA ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa dunia unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa ICB ,bondia Francis Cheka anatarajia kutetea mkanda wake wa ubingwa wa mabara wa UBO Juni mwaka huu. [101]
mafuta
Kwa mfano Spika mara moja alitoa matamshi kuhusu sakata la mafuta ya Petroli huko Morogoro pale amri ya EWURA ya kuvifungia vituo vya mafuta ilipositishwa kwa muda na mahakama ya Hakimu Mkazi. [102]
magofu
Akaona kwamba watoto wengi walikuwa wanakufa hata kabla ya kufika kwenye magofu yale yaliyoitwa shule. [103]
majaji
Vile vile Mahakimu na majaji wanatakiwa wawe huru na mahakimu na majaji wenzano. [104]
majina
Mbali ya Liyumba majina mengine yaliyoko kwenye hati hizo ni Jamila Nzota, Abubakar Ogunda, Avogati Chiwendo, Mikidadi Mtumbati, Seleman Kaboke, Justus Samson, Gideon Chipande, Hashimu Mwinyimvua na John Ngutiro. [105]
maoni
Vyombo hivyo havitofautishi kati ya ukweli na maoni. [106]
maovu
Tunaamini kwamba, wajibu wa taasisi za dini na watumishi wake ni kuwafanya watu waache matendo maovu na kuishi maisha yanayompendeza Mungu, ili baadaye wapate rehema na uzima wa milele. [107]
mapambano
Shahidi: Mambo ya mapambano hakunieleza. [108]
mbali
Katiba ni mhimili wa sheria ambao unatoa mwongozo wa sheria mbali mbali. [109]
mbio
Akisimulia mkasa huo, kijana huyo alisema mara baada ya kukamatwa na watu hao ambao anadai hawafahamu, alipita mwendesha baiskeli ambaye aliokoa uhai wake, baada ya watuhumiwa kumwona na kutimua mbio. [110]
mgao
Kupitia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea na kufikiwa makubaliano ya kugawana madaraka kati ya serikali ya ZANU PF na chama cha upinzani cha MDC, Maelewano hayo yaliingia dosari Oktoba 11, 2008 baada ya kutangazwa mgao wa wizara kwa vyama, Chama cha MDC kilielezea kutokuridhika na jinsi mgao ulivyofanywa. [111]
miaka
Maina ameongeza pengo la wanamuziki wakali wa bendi hiyo waliofariki miaka ya karibuni, akiwemo TX Moshi William, Athumani Momba na Suleiman Mbwembwe. [112]
miguu
Gurumo alisema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na miguu na bendi walikuwa wakiandaa utaratibu wa kumpatia matibabu. [113]
mihimili
MAHAKAMA ni mhilimili mmojawapo katika mihimili mitatu ya Dola. [114]
mikoa
OFISI ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) imemwaga waendesha mashtaka karibu katika mikoa yote nchini. [115]
mimi
Shahidi: Wote, mimi na Michael. [116]
mingine
Mihimili mingine ni Bunge na Serikali (Utawala). [117]
misingi
Kwa misingi ya kazi ya polisi unaweza kufukuzwa kazi. [118]
mitatu
Katika hatua nyingine, Mlundwa alisema chama chake hakipendi kuona Matumla na Cheka wakirudiana tena baada ya kupambana mara nne huku Cheka akishinda mipambano mitatu kati ya hiyo. [119]
mitihani
Kwa kweli nawashangaa wanaoshangaa matokeo ya mitihani yetu. [120]
miungu
Ni wapendwa wa Mungu, ni wapenzi wa Mungu, ni miungu kabisa na sisi. [121]
mji
Zelothe alisema kutokana na taarifa walizopata kutoka kwa raia wema, polisi waliweka mtego na kuwanasa baada ya kupatana kuuziana viungo hivyo katika mji wa Mlowo, wilayani Mbozi ambako kachero mmoja alifika Februari 16, kukamilisha mpango huo. [122]
mke
Maina ambaye ameacha mke na watoto wa wawili alitunga kibao kumuimbia mke wake, Mama Cossy ambacho hakijatoka. [123]
mkuu
Shahidi: Siwezi kumuuliza mkuu wangu wa kazi kwa nini ananipongeza. [124]
mlezi
Akijibu maswali ya Waziri Mkuu kuhusu ujenzi wa barabara ya Rombo hadi Tarakea na hali ya kilimo katika kijiji cha Kirya ambacho Waziri Mkuu alijitolea kuwa mlezi wake, Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba ujenzi wa barabara hiyo unaendelea vizuri na sasa umefikia kiwango cha changarawe. [125]
mradi
Chini ya mradi wa kuendeleza makazi bora, wilaya hiyo ilikuwa imetenga viwanja 1,000 vilivyopimwa na kuvigawa kwa wakazi wa kijiji hicho ili mradi utakapokamilika uwawezeshe wafugaji kuhama kutoka kwenye nyumba za manyasi na udongo na kuanza kuishi kwenye nyumba za tofali na mabati. [126]
muda
Baraza linashangazwa na muda uliochaguliwa na vyombo husika kuanzisha mashindano ya matusi, kwa kuwa ni kipindi muhimu katika historia ya taaluma hii nchini, ambapo mchakato wa kutunga sheria mpya za vyombo vya habari na haki ya kupata habari unaendelea” alisema Mukajanga. [127]
mujibu
Kwa mujibu wa Kamanda Stephen, watuhumiwa walipofika katika soko hilo Februari 16, walidai walikuwa wakiuza viungo vya kunguru mweupe. [128]
mwa
Kuhusu lini alihusishwa na tukio hilo, alisema siku moja ambayo hakukumbuka tarehe, lakini mwishoni mwa mwezi Januari akiwa katika mahakama ya mwanzo Kawe alipigiwa simu na Inspekta Omari (PW31), ambaye alimpa ujumbe kuwa afike Makao Makuu ya Polisi Idara ya Upelelezi. [129]
nayo
Tunaomba jumuiya ya kimataifa nayo ikiongozwa na Umoja wa Mataifa itusaidie. [130]
nazo
Akizungumza na Mwananchi jana mara baada ya mazoezi, nahodha huyo alisema hakuna kinachoshindikana na hawatishiki na majina ya timu wanazokwenda kucheza nazo bali juhudi pekee ndizo zitakazowakomboa. [131]
ndefu
Dhamana kwa Liyumba na wenzake wanaokabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh221bilioni, imekuja baada ya safari ndefu ya kujinasua na machungu ya mahabusu, ikiwa ni pamoja na kujaribu kutaka kiasi cha fedha za dhamana kipunguzwe. [132]
ndio
Shahidi: Mheshimiwa Jaji, mimi sikuhusika na kwa sababu mahakama ndio inatenda haki itaangalia. [133]
ng
Hata hivyo Wakili wa Serikali Mulokozi alipinga kupokelewa kwa hati hizo kwa madai kuwa nyingi zina mali zisizokuwa za kudumu kama vile kuku, ng’ombe na mbuzi ambazo alidai haziwezi kuwasaidia kama dhamana. [134]
ngozi
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limetoa amri ya kukamatwa kwa watu wawili wa Kata ya Ivumwe, kwa uzembe waliofanya ambao ungesababisha mtoto mlemavu wa ngozi kuuawa na watu wasiojulikana. [135]
ni
Watuhumiwa waliotangulia kutoa ushahidi wao katika kesi hiyo ni pamoja na Zombe, mshitakiwa wa pili Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni, mshitakiwa wa tatu Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na WP Jane Andrew. [136]
nia
Mlundwa alisema kumpiganisha Cheka na mabondia hao ni sawa na kumkosea heshima na hasa baada ya kutwaa ubingwa wa dunia na kuwataka mabondia hao kama wana nia ya kweli ya kupambana na bondia huyo kwanza wapambane wao na mshindia atakayepatikana ndipo aombe kucheza na Cheka. [137]
nidhamu
Akitoa pongezi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru (zamani Taifa), Naibu Waziri wa Ulinzi na JKT, Dk Emmanuel Nchimbi aliwataka wachezaji hao kuendeleza nidhamu na ushirikiano katika mashindano mbalimbali kwani ndio chanzo cha ushindi. [138]
ningewapa
Siku ya wanafunzi kuingia katika hizi shule ningewapa mtihani. [139]
nipo
Kwa hiyo kwa mimi sasa hivi naona kama jambo la faraja kuliko ningeendelea kukaa serikalini, ningeng'ang'ania watu wasingesema mimi ni msafi, kwa kweli nipo safi, na nashukuru uchunguzi ulibaini hivyo. [140]
noti
Nasikia hivi karibuni watawaomba waheshimiwa wapepee noti zao za posho za mipasho huko makalio makuu ili kuthibitisha kwamba na wao wanaelekea mbinguni potelea mbali kama sisi tusio na noti za kupepea tunafuata njia nyingine. [141]
nyumba
Dhamana hiyo ni thamani ya nyumba yake iliyoko Mbezi Juu jijini Dar es Salaam. [142]
nyumbani
Shahidi: Tulielekea nyumbani kupumzika. [143]
nzuri
Alisema wachezaji hao walionyesha nidhamu nzuri na ushirikiano wakati wa mashindano hayo ndiyo sababu wameibuka na ushindi na ameahidi kutoa ushirikiano wa kiwizara na kuzitaka taasisi na makampuni mbalimbali kujitokeza kusaidia kuinua mchezo huo hapa nchini. [144]
ofisi
Sisi kama serikali tunashangaa tutakaa kujadili suala hili na kulitolea maamuzi kupitia ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali,” alisema Mulokozi. [145]
pale
Jibu: Well, ulitia dosari pale mwanzo, ulitia dosari kwa sababu sikutarajia Jaji aseme hivyo. [146]
pengo
Maina ameongeza pengo la wanamuziki wakali wa bendi hiyo akiwemo TX Moshi William, Athumani Momba na Suleiman Mbwembwe ambao tayari wamefariki. [147]
pia
Kabla ya Mabula kutoa ushahidi wake alitanguliwa na shahidi wa nne (DW4) WP Jane Andrew, ambaye pia ni mshitakiwa wa tano katika kesi hiyo naye alifuata nyayo za wakubwa wake waliomtangulia. [148]
pigo
Kwa kweli ni pigo kubwa kwani Maina alishiriki katika nyimbo zote za Msondo walizopiga, alishiriki albam zote ni pigo kwa sasa hatuna la kusema tutatoa taarifa," alisema. [149]
rudi
Hata hivyo, baada ya safari hiyo ndefu ya nenda rudi kutoka gerezani akijaribu kutafuta dhamana huku akigonga mwamba, hatimaye jana mahakama ilimpatia dhamana hiyo. [150]
rufaa
Msekwa akiwa Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliingilia uhuru wa Mahakama ya Rufaa katika kesi ya Ndyanabo iliyofunguliwa kupinga sheria ya kukata rufaa kwa mgombea ambaye hakuridhika na matokeo ya uchaguzi. [151]
salama
Shahidi: Ilikuwa salama na hatukuwahi kuitumia. [152]
sana
Shahidi: Nilishangaa sana kwa sababu tulikuwa Makongo. [153]
sare
TIMU ya soka ya vijana ya Simba, chini ya miaka 20 jana iliendelea kutoa takrima katika mashindano ya vijana baada ya kuchapwa na JKT Ruvu mabao 4- 0 huku Polisi Moro ikilazimishwa sare ya bao 1- 1 na Mtibwa Sugar. [154]
sasa
Washitakiwa katika kesi hiyo walioko mahakamani sasa kwa mpangilio ni Abdallah Zombe, SP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, WP 4593 PC Jane Andrew, CPL Emmanuel Mabula, D8289 PC Michael Sonza, D 2300CPL Ebeneth Saro, D.9312D/C Rashid Lema, D4656 C/CPL Rajab Bakari na D.1367 D/CPL Festus Gwabisabi. [155]
sauti
Akaamuru miwarsha yote, na semina vyote vipigwe marufuku ili pesa zitumike kununua matrekta, lakini alisikia tu sauti ya vicheko ikitoka kwenye magari. [156]
semina
Bahati nzuri Mahakama haikumjibu, lakini Mawakili wa Tanganyika Law Society wakamjibu kwa kuandika na kutoa semina mbali mbali kuhusu uhuru wa Mahakama. [157]
shule
Lakini shule, zahanati na hata vituo vya polisi hujengwa na kamati hizo," anaeleza Jaji Ramadhan. [158]
si
Shahidi: Mheshimiwa Jaji haya si maelezo yangu. [159]
sifa
Pili ile hatua ya tume kuthibitisha tuhuma zile haikuwa kweli, ingawa ulikuwa uzushi lakini nilijiuzulu na Rais Mkapa aliniandikia barua kunipongeza kwa kujiuzulu na kusema nilionyesha sifa nzuri ya kuwajibika. [160]
sio
Chombo cha habari, kwanza kinapaswa kuutumikia umma na sio kusimamia maslahi ya watu binafsi, wawe wanasiasa, wamiliki, wafanyabiashara au wengineo,” alifafanua. [161]
sisi
Kwa kweli sisi tutacheza kadri ya uwezo wetu kuhakikisha tunaandika historia katika mashindano haya,hatutakiwi kutishika na ukubwa wa majina ya timu pinzani ambazo tumepangwa nazo bali iwe changamoto kwetu kuona tunaweza na tutawashinda. [162]
siyo
Hata hivyo, Meneja huyo alikutaka kuzungumzia suala la kuiba maji pamoja na kuharibu mita kwa kuwa yeye siyo msemaji wa kampuni bali alitumwa kwenda kuangalia kinafanyika katika eneo hilo. [163]
soka
Henry alikuwa Norway kwa majaribio ya soka ya kulipwa, wakati Chuji alikuwa majeruhi, sawa na Nizar Khalfan aliyeumia wakati wa mechi dhidi ya Zimbabwe wiki moja iliyopita. [164]
soko
Kamanda huyo alisema kukamatwa kwa watuhumiwa kulikuja wakati wakihaha kusaka wateja katika maeneo ya soko la Mwanjelwa jijini Mbeya. [165]
tabia
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza hilo, Kajubi Mukajanga aliwaambia wandishi wa habari jijini jana, kwamba MCT imesikitishwa sana na tabia ya baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari, kuanzisha na kuvitumia vyombo hivyo kama silaha kwa maslahi yao. [166]
tafsiri
Wakati Bunge linatunga sheria, Mahakama ina tafsiri sheria na serikali inatekeleza. [167]
tani
MKOA wa Kilimanjaro unahitaji tani za chakula 27,159 ili kukabiliana na uhaba wa chakula uliozikumba wilaya tatu za Mwanga, Rombo na Same. [168]
tena
Mtuhumiwa huyo alikana mashitaka na yuko nje kwa dhamana ya Sh500,000 na hakimu mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Mufindi Mary Moyo aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 27mwaka huu itakapotajwa tena. [169]
tishio
Manumba alisema kutokana na tishio hilo, jeshi la polisi nchini watashirikiana na majirani zao na baadhi ya nchi za nje kufuatilia tishio hilo ili kujihami na shambulio lolote kutoka kwa kundi hilo la kigaidi. [170]
trekta
Mungu akaagiza, trekta ziwepo. [171]
tu
Shahidi: Ndio walikuwemo askari wengine ila James tu ndiyo hakuwemo. [172]
tuna
Hati nyingi tulizoziangalia zina mali zisizodumu kama kuku, ng’ombe na mbuzi na hazimtambulishi mtu aliyefanya uthamini hakuna hata mihuri tuna wasiwasi zisije zikawa za mitaani,” alisema Mulokozi. [173]
ukata
Naam! Sisi maskini tutakatika na ukata tu hata baada ya kukata roho lakini matajiri wataukata kama walivyoukata hapahapa. [174]
usio
Lakini ni kweli vilevile kwamba siku zote kuna 'miss match' kati ya mipango safi na utekelezaji, tofauti hii inatokana kwanza na uwezo wa serikali, serikali inaweza ikawa na mipango safi lakini ikawa na utekelezaji usio mzuri, kwanza kwa ajili ya fedha hazitoshi, lakini pia kwamba inawezekana kuna watendaji wa serikali ambao si makini. [175]
utoaji
Zaidi ya hapo, tunaomba mamlaka zinazohusika kuweka utaratibu unaoelweka kwa ajili ya kudhibiti na kusimamia utoaji wa huduma hiyo, ili jamii inufaike na isaidie kuongeza kasi ya maendele nchini. [176]
uwezo
Alli Husein Lillan alisema kuwa wanauwezo uwezo mkubwa wa kutatua tatizo la msongano lakini wanakwazwa na miundombinu. [177]
vita
Kamanda Stephen alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa na polisi kutokana na uzembe wa kushindwa kuimarisha ulinzi wa watu waliokuwa na ulemavu wa ngozi kwa kuunga mkono jitihada za serikali kupiga vita mauji hayo. [178]
vyema
Mungu akaangalia akaona ni vyema. [179]
wako
Feleshi alifafanua kwamba, hata katika mahakama za Dar es Salaam ikiwemo Kisutu wapo waendesha mashitaka kutoka ofisi hiyo ambao wako chini ya mpanmgo huo wa mabadiliko ya sheria. [180]
wakuu
Katika hotuba yake wakati wa kukabidhi kiti hicho kwenye mkutano wa 12 wa wakuu wa nchi na serikali wanachama wa AU, Kikwete anasema anaamini kumekuwa na mafanikio kadhaa katika baadhi ya maeneo yenye matatizo. [181]
walio
Watu wengi wanadhani kwamba wapendanao ni wale tu walio katika mapenzi yaani boyfriend na girlfriend pekee. [182]
waliyo
Wanajua wazi kama wataibadilisha katiba watapoteza mamlaka waliyo nayo. [183]
wangu
Shahidi: Tuliwakuta maofisa wengi lakini niliweza kumtambua OCD wangu tu wa Kinondoni SSP Maro. [184]
wapi
Shahidi: Sikujua tunaelekea wapi. [185]
waume
Na hii inabaki kuwa sababu ndoa nyingi zinaterereka kwa kuwa wanawake wanashindwa kujipendekeza na kuwanyenyekea waume zao kila siku kama vile ambavyo wengi wanafanya katika siku kama hii. [186]
wawili
Wakati akitoa ushahidi wake mshitakiwa wa pili, SP Bageni aliieleza mahakama kuwa mshitakiwa wa saba (Mabula na wenzake wawili hawakuwepo kwenye eneo la tukio walikokamatiwa wafanyabiashara hao, kwa kuwa wao siku hiyo walikuwa kwenye doria Makongo. [187]
wazo
Kwa bahati nzuri wazo hilo halikufanikiwa. [188]
wenye
Alisema Chama chake hakitakuwa tayari kuona mabondia wanapigana kwa ajili ya njaa na badala yake watahakikisha mabondia wenye uwezo ndio wanaopewa kipaumbele katika kuandaliwa mapambano. [189]
wewe
Sisi wanasiasa tuna kitu ambacho tunasema 'kuwajibika kwa heshima ya serikali,’ kwa sababu wewe kama unatuhumiwa, umefikishwa mahakamani, bado unang'ang'ania uwaziri, sasa hiyo si sawa. [190]
wiki
Hivi karibuni TPA ilitangaza mafanikio makubwa katika kupunguza msongamano wa makontena ambapo ndani wiki mbili tayari makontena zaidi ya 1800 yalikuwa yameondoshwa katika Bandari ya Dar es Salaam tangu zoezi hilo la dharula lilipoanza mapema Januari mwaka huu. [191]
wowote
Kwa mujibu wa kamanda Stephen, watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya uchunguzi kukamilika. [192]
yale
Jibu: Well, inatia mashaka, kwa sababu unamtuhumu mtu kama alifanya ufisadi, bora iwe kweli, lakini inataka kuwa makini kidogo kwa sababu pale serikalini mtu anaweza kufanya maamuzi pengine si kwa sababu alikuwa na dhamira ya kufanya ufisadi, alifanya kwa sababu katika hali ile alilazimika kufanya maamuzi yale. [193]
yenye
Mmoja wa mawakili wanaomtetea Liyumba, Hudson Ndusyepo alisoma hati na leseni za makazi kwa maeneo ambayo hayajapimwa lakini upande wa mashitaka ulikubali hati moja ambayo ni ya nyumba ya Liyumba iliyoko Mbezi Juu yenye thamani ya Sh 882 milioni. [194]
yetu
Mteja amabaye aliomba maji kwa matumizi ya nyumbani ni Sureshi Daudi na mara ya mwisho alilipa bili Aprili 2008, na ameharibu mita yetu,” alidai Mndolwa na kwamba watamfikisha mahakamani. [195]
zake
Alidai kuwa mteja wao ambaye ni Sureshi Dauda aliomba maji kwa matumizi ya nyumbani, lakini alibadilisha matumizi bila kibali na kuanza kutumia katika viwanda pamoja hoteli zake. [196]
zetu
Tutachukua tahadhari na tunafuatilia ili kujihami, tutashirikiana na majirani zetu na baadhi ya nchi za nje kukabiliana na shambulio lolote," alisema Manumba. [197]
zile
Alisema kuwa wageni mbalimbali mashuhuri kutoka taasisi mbalimbali za dini pamoja na zile za kijamii, zitakuwa miongoni mwa waalikwa katika kulitia nakshi tamasha hilo. [198]
ziote
Akaamuru shule ziote kama uyoga, zisambae kila kata hadi kila kijiji, zikasambaa, zikasambaa hadi zikasambaratika. [199]
ziwepo
Basi Mungu akaamuru ziwepo shule zikawepo. [200]