Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-02-02

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
acha
Kama hii hapa chini We Makengeza, Wewe ni mwanamume au la? Kama ni mwanamume, acha kutoa viliovilio vyako vya kipuuzi kila siku maana naona unaanza kuwaambukiza hata wengine. [2]
aende
Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [3]
akawa
Mchizi kabla ya kuingia biznes kubwa kama za kuwa na butiki hivi, ..alikuwa mtu wa mishen'tauni, lakini mara mbili tatu hivi akawa kadakwa na ma'afande, akatia akili, akaanza kuuza mitumba, ndio mambo yakaenda, ..mdogo mdogo mpaka kapata butiki. [4]
akiishi
Nyumbani kwake hapo alikuwa akiishi na watu kadhaa akiwemo jamaa mmoja ambaye ni mwenye ulemavu wa ngono yaani albino. [5]
akilia
Baba mmoja akaniambia mtoto wake akamshtukiza akilia mbele ya luninga kwa kuona maelfu ya maiti yaliyorundikana. [6]
akiwa
Kauli hiyo ya Dk Mvungi, inakuja wakati kukiwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya wanasiana na wanaharakati, kutaka kiongozi huyo aondolewe kinga ili ashitakiwe kwa tuhuma za kufanya biashara akiwa Ikulu. [7]
albino
WAPO watu wanaosema kwamba machozi aliyomwaga bungeni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Alhamisi wiki hii wakati akielezea mauaji ya albino nchini yalikuwa ni machozi ya mamba. [8]
alichukua
Lakini ikaelezwa kuwa Maximo alichukua uamuzi huo kutokana na mchezaji huyo kutokuwepo nchini. [9]
alidakia
Mwishiwa mwingine alidakia. [10]
alifika
Muda mfupi baadaye waziri alifika hapo hospitalini, kwani si mbali sana kutoka kwenye ofisi yake. [11]
alionekana
Katika mechi hiyo, Haruna alishirikiana vizuri na Nizar Khalfan, Erasto Nyoni na Said Maulid ‘SMG’, alionekana kuwa katika kiwango bora na alitengeneza nafasi kadhaa za uhakika. [12]
ama
Alisema kuwa kama klabu wamekwishaanza mazungumzo na wenzao, Lov-Ham ya Norway kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo ambaye imeelezwa kuwa alikuwa anatakiwa kwenye majaribio ya wiki moja Januari ama Februari. [13]
amani
Hata hivyo walilalamikia upotoshwaji wa taarifa juu ya uamuzi wa kesi zilizofutwa na Jaji Chocha mwishoni mwa wiki iliyopita ambao walidai umekuwa ukifanywa na watu wachache wasioutakia amani na utulivu msikiti huo wa Arusha. [14]
ambalo
Kwa zaidi ya miaka miaka mitano msikiti mkuu wa Arusha umekuwa na migogoro ambayo inatokana na viongozi wa BAKWATA mkoa wa Arusha kudai msikiti huo ni mali ya mkoa na hivyo wamekuwa wakiteua uongozi jambo ambalo linapingwa na waumini wa msikiti huo. [15]
ameweza
Manji anaidhamini Yanga kwa miaka mitatu sasa na ameweza kulikarabati jengo la klabu hiyo ililopo mtaa wa Jangwani na Twiga ambalo hivi karibuni litaanza kutumika na mambo mengi kama kusajili wachezaji a kwa gharama kubwa na kuwalipa misharaha mikubwa. [16]
ana
Alisema ana matumaini makubwa ya Yanga kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa na hawaihofii timu yoyote ile. [17]
anasema
Baada ya kumuita na kumchezesha mechi kadhaa, Maximo anasema kuwa anajivuna na kiungo huyo, kwa kuwa hucheza kwa umakini uwanjani. [18]
angalia
Hebu angalia kadi za wenyewe. [19]
au
Milipuko ya aina hiyo ni ya kawaida nchini Nigeria, ambako watu hutoboa mabomba kwa ajili ya kwenda kupikia au kuuza kwa magendo. [20]
badala
Kwa upande wa wakulima, mkuu wa wilaya alisema wanapaswa kurejea katika maeneo yao ya asili badala ya kuvamia hifadhi kwa kisingizio cha kukosa ardhi. [21]
bado
Saa mbili baada ya kutokea kwa tukio hilo la gari hiyo kupinduka na kulipuka, bado juhudi za kuwasaidia angalau kuwaokoa watu waliokuwa hadi umbali wa mita 50 kutoka lilipokuwa lori hilo, baada ya eneo lote hilo kushika moto. [22]
bahati
Akafunga ofisi hizo za kuziweka kwenye majengo yake ambayo kwa bahati mbaya yalikuwa nje ya mji. [23]
bali
Kanali mstaafu Machibya pia aliwahakikisha wawekezaji hao kwamba michango ya elimu haitatoka kwao tu bali, wanaandaa harambee kubwa ya kuchangia mfuko wa elimu ya wilaya hiyo. [24]
biznes
Yaani kwa kuwa washkaji zake wengi mademu, kutokana na biznes anayofanya. [25]
chacha
Nilikuwa nafanya muziki huku nasoma, na bendi yangu ya kwanza ilikuwa nikilimanjaro chacha bendi, ambayo nilianza kuimba mwaka 1961" anafafanuwa Gurumo. [26]
chake
KAMATI mpya ya utendaji ya TFF imekaa kikao chake na kupitisha majina na wajumbe wa kamati ndogo, ambazo wajibu wake ni kusaidia kamati ya utendaji kutekeleza majukumu yake kikatiba. [27]
chochote
Ila tu sijasikia kadi ya kaka wala kadi ya dada dada kwa hiyo nitawaachia wanaharakati wa vijana wanishambulie badala yake maana, kama kawaida, hawajaambulia chochote. [28]
chozi
Chukua mfano wa huyu aliyedondosha chozi juzi. [29]
dhidi
Awali, waumini 10 waliokuwa wamefungua kesi dhidi ya BAKWATA namba 5/2006,waliokuwa wakiomba uchaguzi katika msikiti huo, pia walipongeza hukumu iliyotolewa kwa kuzingatia sheria za nchi kuacha masuala ya dini yamalizwe na katiba za taasisi za dini. [30]
es
MHADHIRI maarufu wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. [31]
fulani
Tujadili mambo ya maana ya kujikomboa na kujua haki za zetu za msingi, sio kuongea ya fulani, kwakuwa ni dhahiri hayakusaidii. [32]
gani
Kama wanasema ni kosa basi wanieleze hapa kosa ni lipi na wanioneshe ni sheria gani inayomshitaki,"alisisitiza Dk. [33]
gavana
Taarifa kutoka BoT ambazo zimethibitishwa na Gavana Profesa Benno Ndulu, zimesema chini ya mchakato huo wa awali utahusisha mabadiliko ya saini za waziri wa fedha na gavana wa BoT katika noti ya Sh2,000 tu. [34]
hajui
Kauli hiyo ilionekana kumchanganya sana Kazim, akawa hajui la kufanya. [35]
hana
Wana unaambiwa wanaenda kwa washua TRA kumchoma kwamba, kamchekini yule, mzee wa magumashi, huenda akawa hana leseni. [36]
hao
Ajali hiyo inadhaniwa kuwa ilitokana na mmoja wa wananchi hao wanaodaiwa kuwa walikuwa wanaiba mafuta, kuwasha sigara katika eneo hilo. [37]
hapana
Ila, sisi waishiwa tunamwomba, hapana hatuombi, tunamwagiza aendelee kutoa chozi la huzuni, chozi la hasira, kwa Watanzania wote wengine wanaonyanyaswa kutokana na vitendo vya wenzake 'Sema Mwishiwa Supu, sema. [38]
hasa
Alipoulizwa ni lini hasa saini hizo zitabadilishwa, alisema mchakato huo uko katika hatua za mwisho. [39]
hasira
Tunafurahi sana kuona kwamba angalau mmoja wa wale tuliowaona kuwa na roho ya korosho, ambao hawajali mateso ya wananchi ili mradi wanapata posho zao, na marupurupu kibao, na uwezo wa kufisadi wapendavyo, tunafurahi kuona kwamba angalau mmoja wao ameonyesha hali ya kuhuzunika, hata hali ya kushikwa na hasira kutokana na hali hii. [40]
hata
Profesa Ndulu alisema hata noti ya Sh2,000 baadaye inaweza kuingizwa katika mpango wa kufanya mabadiliko. [41]
hawa
Na kuna kauzu watakuja kukuletea kwamba Ooh, f'lani kasema hivi, hawa pia usiwape chansi, watakupotezea taimu yako wakati dili zinakusubiri kitaa. [42]
hayo
Muda mfupi baada ya kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha usiku wa kuamkia jana, taarifa ya shirika la Msalaba Mwekundu ilieleza kuwa miili ya watu 91 ilikutwa ikiwa imeteketea kwa moto wa mafuta hayo mara waokoaji walipowasili kwenye eneo hilo, idadi ambayo iliendelea kuongezeka kadiri muda ulivyoendelea kutokana na majeruhi wengi kuzidi kufariki dunia. [43]
hazina
Mvungi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, aliliambia Mwananchi kuwa watu wanaomjadili Mkapa wanajadili kwa hoja nyepesi tu ambazo hazina nguvu za kisheria. [44]
hicho
Makamba alitoa jana katika uwanja wa Pasua, mjini Moshi wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 32 ya chama hicho ambayo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Aman Abeid Karume. [45]
hili
Alisema ingawa Mkapa wakati wa utawala wake aliwaminya na kuwakandamiza wapinzani, lakini kwa hili yeye kama mtaalamu wa sheria hawezi kutumia kigezo hicho cha uhasama wa kisiasa,wala taaluma yake kama silaha kushinikiza kumwangamiza na kwamba anazungumza kisheria. [46]
hiyo
Waathirika wa ajali hiyo walikuwa wamelazwa kwenye sakafu ya hospitali, huku wakiwa wamewekewa chupa za maji. [47]
hizi
Katika kuthibisha hali hiyo tete ndani ya klabu hiyo iliyosajili wachezaji kwa zaidi ya shilingi milioni 500, baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo wakilalamika kuwa hawapati posho za kutosha siku hizi kila wanapocheza mechi. [48]
hizo
Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga pamoja na mawaziri kadhaa wa serikali ya Kenya akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani, George Saitoti, Waziri wa Afya, Beth Mugo na Waziri wa Elimu, Sam Ongeri walilazimika kutembelea eneo hilo baada ya taarifa hizo kutolewa jana asubuhi. [49]
humo
Akihutubia wananchi wa Kata ya Mtimbira wilayani humo juzi, Dk Rutengwe, alisema wafugaji waliovamia eneo hilo, wanapaswa kuondoka mara moja na mifugo yao na kwenda katika maeneo yaliyotengwa kitaifa, kwa ajili ya shughuli za mifugo. [50]
huo
Patrick Nyongesa, mkurugenzi wa shirika hilo la Msalaba Mwekundu katika eneo hilo alieleza kuwa hospitali zilizoko karibu zimejaa watu waliounguzwa vibaya na moto huo, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto. [51]
huu
Katika tamko lake lililosomwa na Katibu wa mkoa, Mauldine Kastico, CCM mkoa Kilimanjaro ilisema imejipanga kikamilifu na kiko makini kushinda chaguzi za serikali za mitaa mwishoni mwa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa 2010 kwa kishindo. [52]
huwa
Kukosekana kwa mchezaji huyo, kulikuwa kukiwauma sana mashabiki wa si wa Simba pekee, bali hata wapinzani, kwani kiwango cha mchezaji mara nyingi huwa akijifichi. [53]
huyo
Mmoja wa mashuhuda alieleza kuwa mmoja wa maafisa wa kikosi maalum cha polisi (GSU), aliwahi kufika katika eneo hilo mara baada ya ajali ya lori hilo kutokea, ambapo alidai kuwa afisa huyo alianza kudai ada kwa watu waliokuwa wakitaka kuchota mafuta yaliyokuwa yakimwagika. [54]
huyu
Mimi pia nilikuwa mmoja kati ya wengi tuliyosikia majigambo hayo, nanukuu: "Sasa hivi tumejiandaa kufanya vizuri katika mashindano ya dunia hatuna wasiwasi tunaamini huyu mrembo atatuwakilisha vizuri, tuwe na mategemeo ya kupata mataji mbalimbali," alisema mmoja wa viongozi. [55]
ibada
Maana, jamani, hizi kadi za biashara ni kama ibada ya dini. [56]
ile
Kwa upande wake Rais Karume, alisema licha ya kuwepo kwa majimbo na kata zenye wabunge au madiwani wa upinzani, ni lazima viongozi hao wafahamu kuwa Tanzania inaongozwa na serikali zote mbili ya Muungano na ile ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ), ambazo zitahudumia majimbo yote bila kuchoka. [57]
ili
BAKWATA mkoa wataheshimu mamlaka yetu ili tupate viongozi halali wa msikiti huu"alisema Sheikh Salum. [58]
ina
Hiyo ya Sh500 bado tunaifanyia kazi, tunajua ina uchakavu, lakini hakuna uamuzi hadi sasa, inaweza kuja kuingizwa katika mchakato huo mpya baada ya kuamuliwa," alifafanua. [59]
iwe
Ili mwisho wa siku sauti iwe kweli kutoka jela. [60]
jazi
Gurumo alikaa kilimanjaro chacha bendi kwa takribani miaka mitatu ambapo mwaka 1963 alijiunga na kilwa jazi, ambapo alikaa kwa mwaka mmoja. [61]
juu
Alisema katika zabuni mpya, BoT imeweka vigezo vya kumpata mzabuni mwenye sifa za hali ya juu. [62]
kabisa
Kaimu Mkuu wa Polisi katika eneo hilo Molo, Daniel Kamanza alisema waliweza kukuta miili ya watu 50 ambayo ilikuwa imeungua katika kiwango cha kutotambulika kabisa, "idadi inaweza kuongezeka zaidi. [63]
kabla
Alisema wanaojadili suala la Mkapa kabla ya kwenda mahakamani kumfungulia mashitaka kwa kufanya biashara Ikulu inabidi kwanza waangalie Katiba ya nchi, Sheria ya Mambo ya Urais (Presidential Affairs Act) na Sheria ya Huduma za Jamii (Public Service Act). [64]
kadi
Kukosekana kwa mazoezi ya kutosha, yalipelekea wachezaji wa Tanzania kukosa nidhamu na kupata kadi nyingi za njano na nyekundu na wengine kuugua kila kukicha. [65]
kali
Baada ya kusubiri kwa kipindi kirefu sana, na zoezi kali la kufa mtu kufanywa katikati ya kitongoji kilichobeba jina la wilaya, hatimaye ngoma uwanjani leo, watu wanatarajia kupata mambo ambayo walikata tamaa kabisa kuyapata. [66]
kama
Makamba ambaye hupenda siasa za vijembe, kama kawaida yake alisema kwa ukiwafunga paka wanne pamoja mikiani na kisha kuwawekea panya mbele yao, wote watakatika mikia kwa kila mmoja kukimbilia panya huyo. [67]
kanda
KUFUATIA Mahakama kuu kanda ya Arusha, kufuta kesi zote zilizokuwa zimefunguliwa na baraza kuu la Waislam(BAKWATA) na baadhi ya waumini juu ya uongozi wa msikiti mkuu wa Arusha,mchakato wa uchaguzi mkuu wa msikiti huo umetangazwa na jana fomu zimeanza kutolewa. [68]
kansa
Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [69]
kasi
Kamanda wa Polsi wa eneo la Rift Valley, Hassan Noor Hassan alieleza jana kuwa aliagiza mifuko 150 ya kuhifadhia maiti kwenye eneo hilo, kwa kuwa idadi ya vifo imekuwa ikiongezeka kwa kasi miongoni mwa majeruhi. [70]
katikati
Akizungumza na Mwananchi mwishoni mwa wiki, Kisasa alisema: "Kumekuwa na watu hapa katikati, sasa sisi hatutakuwa tayari kumsikiliza mtu zaidi ya klabu. [71]
kidini
Watu wengi ambao wamekuwa wakimtetea Mkapa dhidi ya tuhuma hizo,wakiwemo wabunge,wanaharakati viongozi wa kidini na wananchi wa kawaida wamekuwa wakimtetea Mkapa kwa hoja za kiutendaji wake tu kuwa amelileta taifa heshima na si kwa misingi ya kisheria. [72]
kipaji
Akizungumza na Mwananchi jijini jana Rais wa Shirikisho hilo Leodegar Tenga alisema kwa kupitia mashule tutategemea kupata wachezaji wazuri wenye vipaji kwani kipaji cha mtu huonekana tangu anapokuwa mtoto. [73]
kiroho
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, ametaja 'mwarobaini' wa ufisadi nchini kuwa ni wazazi kuwaandalia maisha ya baadaye watoto wao kwa kuwapatia elimu inayokwenda pamoja na maadili ya kiroho. [74]
kisha
Nilisikia mtu mmoja akisema kuwa watakwenda kutafuta ada hiyo kwa kutumia moto, kisha akaondoka kwenye eneo hilo, nilianza kupata mashaka. [75]
kombe
Awali mechi hiyo ilikuwa ichezwe jana, lakini ilisogezwa mbele kupisha mechi ya kuwania kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Prisons dhidi ya Khalij Sert ya Libya. [76]
kote
Duniani kote kabla ya kijana huyo albino kugundua hiyo dawa, ilikuwa inajulikana kuwa ukiwa na kansa ya moyo hakuna dawa ni kifo tu. [77]
kuishi
Siku moja usiku akiwa nyumbani alitafakari sana hali ngumu ya maisha ambayo angeanza kuishi. [78]
kuitwa
Tuwaombe wanachama na wakereketwa wetu wakatae kuitwa mafisadi," alisema Makamba huku akishangiliwa. [79]
kukutana
Akizungumzia mechi na Al Ahly, mabingwa wa Afrika, Kondic alisema kuwa anafurahi kukutana nao na hata hivyo alisema watajiandaa kwa nguvu zote waweze kushinda mchezo huo. [80]
kule
Emanule Ole Naiko alisema: "Nimemwangalia Nasreem kwa muda mrefu tangu kule kwenye mashindano ya Kanda ya Ziwa mpaka huku kwenye mashindano makubwa nchini kwetu, naona anaweza kutuwakilisha vyema. [81]
kuliko
Muda uliobaki ni mfupi kabla ya fainali hizo, tunawataka wachezaji wote ambao watatajwa kufanya mazoezi kwa nguvu na moyo, kuliko walivyokuwa wakifanya kabla, ili kutengeneza timu yenye wachezaji imara na walio tayari kucheza mechi za mashindano. [82]
kulikuwa
Alisema kuwa, muda huo kulikuwa na basi la abiria lililokuwa likipita eneo hilo na liliacha pia njia kutokana na moto huo. [83]
kulinda
Wajumbe wapya wa kamati ndogo lazima waelewe kazi iliyopo mbele yao, ni kulinda mafanikio yaliyopatikana katika kipindi kilichopita na kufanya kazi maradufu ya kipindi kilichopita, ili kuendeleza maendeleo ya mpira wa miguu nchini. [84]
kumsaidia
Wapo watendaji wachache katika baraza la mawaziri la Kikwete ambao wanaweza kumsaidia, lakini wengi hivi sasa ni mzigo kwa serikali yake. [85]
kumtia
Mvungi ambaye ni mtaalamu wa Sheria na Katiba, alisisitiza kuwa hakuna sheria yoyote inayoweza kumtia hatia Mkapa. [86]
kumuua
Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [87]
kuna
Kwanza nilikuwa mgonjwa hivyo sijarudi katika kiwango changu halafu hao wanaosema mpira hawajui, mpira ndivyo ulivyo kuna kipindi unakukubali kuna muda mwingine unakukataa hivyo watu wajue hilo. [88]
kuona
Kisasa alisema kuwa klabu yake inafurahi kuona wachezaji wananunuliwa. [89]
kupiga
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko, ilimwingiza Jerry Tegete badala ya Mwalala ambaye naye alifunga bao katika dakika ya 53 baada ya kazi nzuri ya Nurdin Bakari aliyepanda na kupiga mpira uliogonga mabeki kabla ya kumkuta mfungaji. [90]
kupingwa
Mambo kama hayo na mengineyo ndiyo yanayoibuliwa na kupingwa kwa nguvu zote katika siku ya wanawake duniani. [91]
kusaka
Mwanasiasa anapaswa kuwa chizi ya kusaka michuzi siyo kuwa mpuuzi wa kutoa chozi mbele ya kadamnasi. [92]
kushindwa
Tumeona makosa mengi na kushindwa kwenda na kasi ya mashindano kwa Taifa Stars wakati wa Kombe la Chalenji, mashindano yaliyomalizika nchini Uganda mwanzoni mwa mwezi uliopita. [93]
kusikia
Maelezo haya ya askari huyu, yalinishangaza, sikutegemea kusikia kwamba kumbe mauaji haya yanaendelea kuwepo kutokana na uzembe wa watendaji wetu kusimamia majukumu yao. [94]
kuu
Taarifa kutoka katika hospitali kuu ya Jimbo la Nakuru zilieleza kuwa, zaidi ya wahanga 100 wa tukio hilo walifikishwa hapo. [95]
kuua
Ni suala la kawaida kuua albino na damu zao au viungo vyao tunavitumia kwenye shughuli hizo za uchimbaji madini na uvuvi, watu wengi wanafanya hivyo. [96]
kuwapa
SHIRIKISHO la soka nchini TFF limeamua kuweka kipaumbele kwa kuwapa mafunzo walimu wote wa soka wanaofundisha mchezo huo mashuleni ili kupata wachezaji wazuri wenye vipaji. [97]
kwake
Kuna habari kutoka kwake kwenyewe kiongozi wa Bendi, ambaye bado hajaamua kujiita Rais bado lakini kuna a. [98]
la
ZAIDI ya watu 100 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa, baada ya lori la mafuta ya petroli kupinduka na kulipuka katika mji wa Molo kwenye mkoa wa Rift Valley nchini Kenya. [99]
lengo
Taarifa za awali zilizotolewa jana zilieleza kuwa lori hilo la mafuta lilipoteza mwelekeo na kuacha barabara karibu na mji wa Molo ambapo mamia ya watu walijitokeza na kulizunguka lori kwa lengo la kuchota mafuta yaliyokuwa yakimwagika. [100]
leo
SIMBA yenye pointi 23 na inayofukuzia nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara inashuka uwanjani leo kuvaana na maafande wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. [101]
live
Vitu live, sauti mwanana na vitu kibao vya kushangaza. [102]
maambukizi
Mradi huo utaendeshwa kwa kuzingatia juhudi za serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa vijana wanalindwa dhidi ya maambukizi ya ukimwi. [103]
maana
Kocha wa Yanga, Dusan Kondic alisema kuwa timu yake imecheza vizuri ndiyo maana imeshinda lakini akasema kipindi cha kwanza walicheza vibaya. [104]
mabao
Mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi anaweza akaendeleza kasi yake ya upachikaji mabao akisaidiana na Orji Obina na Ulimboka Mwakingwe ambaye alikosa mchezo uliopita dhidi ya Prisons kutokana na kuwa mgonjwa. [105]
madai
Mbunge huyo aliaahidi 'kuwashtaki' Mkuu wa Wilaya ya Uranga, Dk Rutengwe na Mkuu wa polisi wa wilaya hiyo Abeid Sanje, kwa madai kuwa wamekuwa wakiwanyanyasa wapiga kura wake. [106]
madini
Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [107]
mafanikio
Wote tunafahamu siri ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi kilichopita, ni ushirikiano wa viongozi wa TFF na kamati zake, pia ushirikiano waliouonyesha kwa wadau wa mpira wa miguu nchini. [108]
makao
Hivi karibuni nilifanya mazungumzo na askari polisi mmoja aliyekuwa ametumwa kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam kupelelezi mauaji ya albino mikoa ya kanda ya Ziwa, aliniambia kwamba askari polisi katika kila wilaya wanawajua wauaji wote na wafadhili mauaji haya. [109]
mamba
Akitoa maelezo hayo kwa wawekezaji wa ndani na nje waliomo ndani ya wilaya ya Serengeti katika ukumbi wa mikutano wa Mawalla Trust, Arusha, mkuu huyo wa mkoa kanali mstaafu, Mchibya, alisema wakati umefika wa kuzuia suala hilo kwa kuweka mikakati ya kushughulikia vyanzo vinavyopelekea wanafunzi hao kupata mamba. [110]
mara
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufika katika eneo hilo, Raila alitoa pole kwa watu wote waliopoteza ndugu zao katika tukio hilo la kutatanisha, huku akitoa wito kwa mamlaka zinazohusika kutoa elimu ya kutosha kwa umma kuhusu umuhimu wa watu kutokusanyika kwenye maeneo ya ajali za namna hiyo. [111]
mauaji
Nakumbuka wakati wa mauaji ya Rwanda. [112]
mbaya
HALI mbaya ya mgogoro wa fedha dunia unakaribia kuikuta klabu ya Yanga baada ya kudaiwa kuwa mdhamini wake Yusuph Manji kuikopesha timu hiyo fedha za maandalizi ya mechi yao ya juzi na Etoile d'Or Mirontsy ya Comoro. [113]
mbinu
MKUU wa mkoa wa Mara, Kanali mstaafu, Issa Machibya amesema kuwa kiwango cha wanafunzi wa kike kupata mimba wilayani Serengeti ni cha hali ya kutisha kutokana na miundo mbinu mibovu ya elimu wilayani humo. [114]
mguu
Unakutana na mtu aliyekatwa mguu au mkono. [115]
mimi
Unajua madra huwa tunafundishwa mambo mengi ikiwemo kuimba, kwa hiyo mimi ndiko hasa nilipo jifunzia mambo ya muziki" anasema Gurumo Lakini mbali na Madrasa Gurumo anasema, muziki nikipaji alichorithi kutoka kwa mama yake mzazi ambaye alikuwa mwimbaji wa ngoma za asili. [116]
mlo
Pia alisema wao kama TFF watawashauri wachezaji kujiweka katika hali ya kimazoezi kujitunza vizuri kwa kuepuka vishawishi vyovyote wawapo katika mazoezi kula vizuri yaani mlo uliokamilika pamoja na kulala mapema ili kuweza kufanya vizuri. [117]
mno
Habari za awali zilisema watu wa makundi hayo, wamevamia mno eneo la kitalu cha kampuni ya uwindaji ya Wildlife Footprint, jambo lililoilazimisha serikali wilayani humo kuwaktia mbaroni baadhi ya wananchi. [118]
mradi
Taarifa iliyotolewa na shirika hilo Jijini Dar es Salaam jana ilisema kwamba ruzuku hiyo itatumika kuendeshea mradi wa kukabiliana na ukimwi ujulikanao kama:"Mradi wa kuhusisha wazazi kuzuia ngono zembe kwa vijana. [119]
mrefu
Beki anayecheza vyema George Minja atakuwa na kazi moja tu leo kuwazuia Mgosi na Obina hawamsogelei kipa wao Shaban Dihile huku beki mwingine Rashid Matambo ambaye alikuwa majeruhi kwa muda mrefu akitarajia kurejea dimbani. [120]
msaidizi
Jamaa huyo ambaye alikuwa kama msaidizi wake wa karibu, alikuwa akimuwakilisha katika kazi mbalimbali na ndiye aliyekuwa ana siri zake nyingi. [121]
mstaafu
Sengondo Mvungi, amesema hakuna sheria inayoweza kutumika kumshitaki Rais mstaafu Benjamin Mkapa, kwa mambo anayotuhumiwa. [122]
mtaa
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa BAKWATA wa mtaa wa Bondeni,Sheikh Abdalah Salum alisema kamati ya muda iliyokuwa inaongoza msikiti huo itaendelea hadi hapo uchaguzi utakapofanyika wiki ijayo. [123]
mumewe
Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [124]
mwa
Maafisa watatu wa polisi wameripotiwa kuwa miongoni mwa watu walioteketezwa na moto huo, wakati walipokuwa wakijaribu kutekeleza majukumu yao kwa kuwazuia watu waliokuwa na nia ya kuchota mafuta hayo kulizonga gari hilo wakati lilipolipuka. [125]
mzuri
Kufanya vizuri kwa wachezaj kunatokana na kupata mlo uliokamilika na kupata muda mzuri wa mapumziko,alisema Tenga. [126]
nami
Ndugu yangu nakupa pole sana, yaani ni bora ungewasiliana nami kabla ya kwenda huko, kwani ukweli ni kwamba dawa imegunduliwa nchini na jamaa mmoja tena ni albino, rudi wahi mapema usipoteze muda wako huko,” alimsisitizia. [127]
nao
Baada ya wao kugundua kuwa 'walichemka' wakarudi nyuma na tumeanza nao mazungumzo, yanakwenda vizuri kwa kweli. [128]
naye
Wacomoro walionana vema katika dakika ya 20, Mikdad Daoud alitoa pande kwa Aboubakar Ally ambaye naye aliwatoka Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Maftah na kumvuta Juma Kaseja aliyetoka langoni na kusawazisha bao hilo. [129]
nayo
Alifafanua kwamba, inawezekana nayo itabadilishwa kuingizwa katika mabadiliko yajayo, baada ya kupatikana mzabuni atakayekidhi viwango. [130]
ndani
Mkapa anaweza kuitwa kwenye Tume ya Maadili ya viongozi na kuhojiwa kama kweli alifanya biashara ndani ya Ikulu,na hata kama akikiri bado hatuwezi kumfungulia mashitaka" ,alisema Dk Mvungi. [131]
ndio
Sheikh Salum alisema kwa mujibu wa Katiba ya BAKWATA ya mwaka 1999, kifungu ya 17 hadi 24, uongozi wa mtaa ndio ambao unajukumu la kutangaza taratibu zote za uchaguzi katika msitiki huo ikiwepo kutoa fomu za wagombea na kuwachuja. [132]
ndivyo
Ambani alisema nawasikia tu watu wanavyochonga kuwa amekwisha, lakini watambue kuwa mpira ndivyo ulivyo. [133]
ndiye
Mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya kumtafuta mrembo wa Tanzania, ambaye ndiye anayekuwa na jukumu la kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia mengi yalisemwa na waandaaji wa mashindano hayo kwa kujigamba kuwa sasa watafanya vizuri. [134]
ndiyo
Kwa ufafanuzi, alisema kampuni hiyo ndiyo ambayo imekuwa ikifanya kazi hiyo kwa kipindi cha miaka saba nyuma. [135]
ngozi
Najua na mimi sitaki watu wavamiwe na kuuawa kama wenzetu wenye ulemavu wa ngozi wanavyouawa . Lazima sheria ifanye kazi. [136]
ni
Taarifa kufikia jana jioni zilieleza kuwa vifo vinavyotokana na tukio hilo vilifikia 111, likiwa ni tukio la pili la moto kubwa kwa wiki hii, baada ya kuungua duka la kujihudumia vyakula na bidhaa (Supermarket) la Nakumat Downtown, Jumatano wiki iliyopita. [137]
nini
Sisi timu yoyote tutachapa tu kwa nini tuogope wakati sisi ni wapambanani, ubingwa wa ligi tunachukua, klabu bingwa tutaendelea kufanya vizuri na hata tukikutana na hao wa Misri sisi ni kazi tu," alisema. [138]
niwe
Lakini wangapi wameonyesha nia ya kwenda kuona hawa wahanga wenyewe na kutafuta usuluhisho? Nakumbuka msemo mmoja wa hayati Trevor Huddleston aliyekuwa mstari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi 'bora niwe na damu mkononi kuliko maji kama Pilato'.’ 'Una maana gani?' 'Namaanisha hivyo. [139]
ofisi
Aliwaomba wawekezaji hao pia kusaidia katika ujenzi wa madarasa 105, Nyumba za walimu 278, maktaba 21 pamoja na ofisi 8 za utawala. [140]
pale
ILIKUWA ni Shangwe na ndelemo kwa Nasreem Karimu katika ukumbi wa Diamondi Jubilee pale Richa Adhia alipomvika taji la urembo wa Tanzania huku akishuhudiwa na mamilioni ya Watanzania waliokuwepo ukumbini na wengine waliokuwa wakifuatilia tukio hilo kupitia televisheni. [141]
pepe
Zaina Malongo ni mwandishi wa mwananchi anapatikana kwa barua pepe zill20032000@yahoo. [142]
pia
Alisema kuwa baadhi ya pikipiki na magari mawili yaliyokuwa yakipita katika eneo hilo pia yalikumbwa na moto huo. [143]
picha
Ikabidi kwa kumtia moyo, ikabidi aende kwenye ofisi ambayo alikuwa akifanyia utafiti huo na kufanikiwa kupata picha yake. [144]
raia
Mvungi alisema yako mambo mengi tu ambayo hayafai kufanywa na na kiongozi au raia yeyote kimaadili, lakini si kinyume cha sheria na hivyo mtu hawezi kushitakiwa kwa kuwa hakuna sheria inayovunjwa. [145]
rais
Ingawa alikiri kuwa kitendo cha Mkapa kufanya biashara akiwa rais wa nchi hakifai, lakini alisema kisheria rais kufanya biashara si kosa na kwamba hakuna sheria inayomzuia kufanya biashara. [146]
rangi
Awali kabla ya mchezo huo, mashabiki kadhaa wa Simba, walionekana kuishangilia Yanga huku wengine wakiwa na mavazi ya rangi za wapinzani wao. [147]
roho
Wanaume wa kweli tutamwelewaje? Narudia kusema, mwanasiasa anapaswa kuwa na roho ngumu kama jabali ya Mwanza. [148]
rudi
Mimi sikatai, kupeana kadi kwaweza kusaidia lakini nadhani kila mtu anajua kwamba asilimia 90 au zaidi ya hizi kadi ama zitatupwa ama zitakusanya vumbi miaka nenda rudi kwenye kona ya ofisi au chumba. [149]
saa
Mwendesha mashitaka wa polisi Benedict Nyagabona alidai mbele ya Hakimu Aniseta Wambura wa mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Januari 20 mwaka huu saa 07:15 asubuhi huko Kijitonyama kwa Ali Maua. [150]
safi
Mchezo huo unaotarajia kuwa mgumu kwa timu zote mbili kutokana na JKT kucheza soka safi na la kueleweka huku wachezaji wake wakiwa na nguvu ambazo huwafanya wasichoke mapema. [151]
saini
Katika mabadiliko hayo saini za Basil Mramba na marehemu Dk. [152]
sana
Nina majeruhi wengi sana na wa kikosi cha kwanza inaumiza huwezi kufanya lolote lakini hilo halituzuii sisi kuibuka na ushindi dhidi ya Simba leo. [153]
sare
Haruna, mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya 1-1, ilikuwa mechi ya pili ya kimataifa tangu aitwe na Mbrazil, Marcio Maximo. [154]
sasa
Alisema hayo akimaanisha kuwa, muungano wa upinzani sasa umevunjika kutokana na kila chama kutaka maslahi katika uchaguzi huo. [155]
sawa
BAADA ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushinda uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Katibu Mkuu wake, Yusuph Makamba amesema muungano wa vyama vya upinzani hauna mwelekeo sawa paka wanne waliofungwa kamba mikiani. [156]
sema
Tangu alipokuwa katika shindano la BSS Aboubakar Mzuri alikuwa akiota kuimba mpaka kufikia kiwango cha Q Chief, umeona bwana, na kwa kweli akiimba huyu mtoto, kuanzia sura yake sauti na hata kule kunata na sauti yake kama uko nje ya ukumbi waweza sema mtoto wa kibondei Q Chief anaimba ndani huko, na ukiingia utamkuta kijana ambaye ghafla waweza sema, ..labda mdogo wake wanavyoshabihiana. [157]
shida
Mwaka 1917 kwa mara ya kwanza siku ya wanawake duniani iliadhimishwa Machi 8, siku hiyo wanawake waliandamana kwa madai ya kutaka ëamani na mkate,í kwa kuwa kulikuwa na vita hakukuwa na amani, hivyo hata upatikanaji wa chakula ulikuwa wa shida. [158]
si
Hili ni pigo kubwa kwa taifa la Kenya," alisema Raila huku akirejea kumbukumbu kuwa hiyo si mara ya kwanza kutokea tukio la aina hiyo, akiwaomba wananchi wa Kenya kujifunza kukaa mbali mara matukio ya magari yenye mafuta kupinduka yanapotokea. [159]
sijui
Ndio ndugu, mimi naitwa Kazim ni mwenye mgodi wa madini ya almasi kule Mwadui, tatizo ni kwamba hali kwa sasa imekuwa mbaya mno, nimechanganyikiwa hapa hata sijui la kufanya,” alisema akiomba ushauri. [160]
sio
Wapo wanawake wengi hapa Tanzania wenye elimu bora, walio katika fani ya urembo na mitindo ya mavazi, hao wanatakiwa kupewa kipaumbele katika suala la urembo na sio wanaume. [161]
suala
Kuhusu uchakavu wa noti za Sh500, alisema suala hilo bado linafanyiwa kazi na kuongeza kwamba, hapo baadaye itaamuliwa cha kufanya. [162]
tajiri
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [163]
tamaa
Ajali hizo za moto zinaashiria hali ya kukata tamaa kwa watu wanaoishi katika maeneo masikini barani Afrika. [164]
tangu
Mvungi anakuwa ni mwanasiasa wa kwanza kumtetea Mkapa kwa hoja za kitaalam, tangu tuhuma dhidi yake zilipoibuliwa na wanasiasa kuanza kujadiliwa kwa mtizamo wa kutaka kumshitaki. [165]
tatu
MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Nyamwezi iliyopo mkoani Tabora, Meshack Athuman (18) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu mkazi Kinondoni akituhumiwa kuiba vitu vyenye thamani ya Sh 8,875,000 mali ya Said Abdallah. [166]
tena
Meshack alikiri shitaka na kesi itatajwa tena Februari 12 mwaka huu kwani upelelezi bado haujakamilika hivyo amerudishwa mahabusu kwa kukosa wadhamini. [167]
tu
Umasikini umekuwa ukiwasukuma watu kujiingiza katika matukio ya ajabu, ilimradi tu waweze kuiona siku inayofuata," alisema Odinga katika hospitali ya Odinga ya Nakuru, karibu na Molo. [168]
udume
Waishiwa wengine waliodumaa na udume wao walimlaani pia msaliti wa udume. [169]
uhakika
Habari za uhakika kutoka kwa chanzo cha habari kilieleza kuwa mdhamini huyo amamepunguza udhamini wake katika klabu kwa sasa iliiweze kujiendesha yenyewe. [170]
uko
MWEZI mmoja baada ya Benki Kuu Tanzania (BoT), kutangaza zabuni ya uchipashaji noti zake, mchakato wa zabuni ya awali uko katika hatua ya mwisho. [171]
ulikuwa
Kocha wa Prison, James Nestori alisema kuwa mchezo huo ulikuwa mgumu kutokana na kuwa na wachezaji wengi vijana ambao bado awajazoea mechi. [172]
uliopita
Mwezi uliopita BoT ilitangaza zabuni mpya ya kutafuta kampuni itakayofanya mabadiliko ya noti zake. [173]
umri
Ngurumo ambaye pamamoja na umri wake kwa sasa kuwa ni takiribani miaka 69 lakini ukweli wa mambo awapo jukwaani utadhani nikijana tena wa miaka 30, kutokana na umahiri wake wa kuimba. [174]
upya
Ni Top Band Jumamosi hii inajimwaga uwanjani, kukuletea songi mpya na zile ulizozizoea, huku ikiwa imesukwa upya na kuwekwa vionjo ambavyo vitakusababisha wewe na wenzio wawili watatu kutothubutu kuiulizia ilipo itakapofika siku ya wikiendi. [175]
uteuzi
Kwa mujibu wa TFF, uteuzi wa wajumbe wa kamati ndogo unazingatia malengo ya TFF, pamoja na utaalamu walionao wadau na wapenzi wa mpira wa miguu nchini, kwani uongozi wa mpira wa miguu wa dunia ya leo, unahitaji utaalamu wa hali ya juu kufanikisha malengo. [176]
vema
Baada ya bao hilo, Yanga ilianza kushambulia kwa nguvu ambapo Ambani, Amir Maftah na Wisdom Ndhlovu walionana vema lakini mmaliziaji, Mrisho Ngassa alipiga nje huku Ben Mwalala akikosa mabao mfululizo. [177]
vifaa
T-MARC itajihusisha na menejimenti ya mradi huo na mandeleo ya mtaala na vifaa vya kufundishia. [178]
vile
Baadhi ya vyanazo hivyo vilitajwa na mkuu wa mkoa kuwa ni pamona na, kutokuwepo kwa mabweni, umbali pamoja na mazingira yenyewe ya shule ambayo yanapelekea vishawishi kwa wanafunzi hao kama vile kupangisha nyumba mitaani kutokana na ukosefu wa mabweni. [179]
vingi
Naungana na Mwenyekiti huyo lakini, nafikiri maandalizi yetu ni ya zimamoto sidhani kama tunakuwa na maandalizi ya kutosha ili kuhakikisha kuwa wawakilishi wetu katika kuwania taji la dunia wanafanya vizuri ukiachia mbali Nancy Sumari, ambaye alijitutumua na kufanya vizuri hapo nyuma, lakini warembo wetu wengine wengi wamekuwa wakirudi na visingizio vingi juu ya uendeshwaji wa shindano la Miss World. [180]
vipi
Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni,” alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [181]
vita
Siku ya wanawake Duniani ilipata msukumo mpya mwaka 1915 yalipofanywa maandamano makubwa huko Bern Switzerland yakishinikiza kumalizika kwa vita ya kwanza ya dunia. [182]
vya
Mwaka 2006, bomba la mafuta liliripuka na kusababisha vifo vya watu 200 nchini Nigeria. [183]
vyake
Kweli wale watu walimuua yule albino na kwenda na viungo vyake kwenye maeneo ya biashara. [184]
vyote
MENEJA wa timu ya Mtibwa Sugar, David Bugoya ameuomba uongozi wa Shirikisho la Soka nchini kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa kutosha katika viwanja vyote vinavyotumika kuchezea Ligi Kuu ya Vodacom. [185]
wako
Makamba alirejea maagizo ya Karume alipozungumza na wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) mjini Dodoma, ambako aliwataka wasihofu Operesheni Sangara iliyotangazwa na Chadema kwani wako imara kujibu mapigo. [186]
wale
Leo mwezi unatimia shosti ushajiuliza umefanya nini cha maana? Au wewe ni kati ya wale wanaoka chobiso kuchunguza ya watu wakati yakwao yanawashinda. [187]
wana
Makamu mwenyekiti wa TAA, Oswald Urassa alisema kuwa wana mikakati ya kuendeleza michezo hiyo kila mwaka. [188]
wapi
Kama semina hiyo ingekuwa na matunda tugeona mawaziri wakifanya kazi kama mchwa kumsaidia rais, lakini wapi hawana lolote wamebaki kupiga siasa tu. [189]
wauaji
Pili kama waziri katika mkutano wake na makamanda hao wageamua kutoa kiasi fulani cha pesa kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwa wauaji au waganga wa kienyeji, naamini wote wangenaswa kirahisi mno. [190]
wazima
Hawa ndio wanastahili kuandaa mashindano hayo kwa sasa pia kuchagua warembo wenye sifa na si watu wazima. [191]
wenye
Alisema kwa kuzingatia katiba hiyo, tayari wameanza kutoa fomu na akawaomba waumini wote wa msikiti huo wenye sifa stahili kwa kila nafasi kuchukuwa fomu za kugombea uongozi. [192]
wetu
Mwandishi wetu alishuhudia gari la kuzima moto kutoka Manispaa ya Nakuru likiwasili kwenye eneo hilo la Molo kwa kuchelewa, kutokana na eneo la mji wa Molo kutokuwa na gari la zimamoto. [193]
wimbo
Ngwea alisema kuwa hivi sasa tayari amesharekodi nyimbo kadhaa ambazo ni kali na mpaka sasa amebakiza wimbo mmoja tu ambao ataupa jina la ‘weekend’ ambayo atamshirikisha Joseph Chameleone ambaye ni mgonjwa kwa hivi sasa. [194]
yangu
Kuna wengine wanaweza kurejea dimbani kutokanana na afya zao kuimarika, lakini wengi wao bado hali zao si nzuri na hili limeiathiri sana timu yangu kwani tunashindwa kupata ushindi mara kwa mara kutokana na tatizo la maheruhi," alisema kocha huyo. [195]
yuko
Haruna ni mchezaji mwenye akili na kipaji kizuri cha soka, hatumii nguvu sana, yeye anatumia akili yuko taratibu uwanjani lakini anafanya mambo ya ajabu na ya uhakika. [196]
yule
Aliongeza kuwa ikiwa Mkapa atakiri mbele ya tume hiyo, itakuwa nafasi ya kurekebisha sheria za nchi kwa ajili ya kukabiliana na rais ajaye na si kurudi nyuma hata kwa yule aliyefanya mambo kama hayo kabla ya marekebisho ya sheria hiyo. [197]
za
Katika tukio hilo la awali, zaidi ya watu 50 walipotea wakiwa hawajulikani waliko, lakini siku mbili baadaye miili ya watu 27 ikiwa imepatikana katika mabaki ya jengo la duka hilo huku juhudi za kutafuta miili zaidi zikiendelea, mingi kati ya iliyopatikana ikiwa imeteketea kiasi cha kutotambulika. [198]
zake
Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa, Katibu Mwenezi, John Chiligati, Rais Karume alipokea wanachama wapya 1,321 waliojiunga na chama hicho na jumuiya zake. [199]
zangu
Sikiliza Kazim, usinitukane tafadhari, mimi ni mtu mwenye heshima zangu, nakusaidia tu, usiniletee shida, kama vipi rudi kule India tuone kama utapona, kosa langu ni nini?” alijibu waziri kwa sauti ya hasira. [200]