Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-16

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aina
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Jamal Rwambow amethibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kuwa gari hilo aina ya Toyota Chaser limetambulika kuwa na namba za usajiri T 706 ABY na linakisiwa kuwa lilikuwa likiegeshwa maeneo ya Butimba Mkuyuni. [1]
akaanza
Wakati bado tunacheka akaanza. [2]
akawa
Tena kichekesho ni kwamba kila mwishiwa akawa amebeba bahasha lililotuna. [3]
aliyeingia
Mgosi aliyeingia kipindi cha pili pamoja na Orji Obina kuchukua nafasi za Mohamed Kijuso na Mohaed Banka walibadilisha sura ya mchezo huku wakishambulia mfululizo. [4]
ambazo
Katika michuano hiyo Emirates imeandaa shughuli mbalimbali ambazo zitawashirikiwa watazamaji na wageni waalikwa kutoka makampuni mbalimbali. [5]
ana
KOCHA Mkuu wa mabingwa wa soka wa Zambia, Zesco, Fighton Simkonda amesema Simba ni timu nzuri lakini kocha wa timu hiyo Patric Phirri ana kazi kubwa kusuka ukuta wake na kutengeneza kiungo. [6]
anaweza
Hata hivyo, imeelezwa kuwa mchezaji huyo anaweza kutimka ebndapo tu baadhi ya mambo hayatatimizwa. [7]
anywa
Rushwa pia ni tatizo kubwa, kwa sababu wengi waliopewa tenda za ujenzi hukutwa na makosa mbalimbali hapo kabla, lakini ni jambo la kushangaza kuwa hupewa tenda zaidi na zaidi, huku kimsingi walipaswa kuchukuliwa hatua ikiwemo kunyang’anywa leseni," anasema. [8]
anywe
Inashauriwa pia mtu anywe angalau lita tano za maji kwa siku. [9]
au
Tunazingatia uwezo wao kiuchumi wa mwombaji ikiwa pamoja na historia ya elimu ya mwombaji, kiwango cha elimu ya wazazi ama walezi wake, shughuli za kiuchumi za mwombaji na wazazi au walezi," alisema Nyatega. [10]
bado
Kama mnavyofahamu nchi yetu iko kwenye malengo ya Milenia ya Maendelo na katika baadhi ya malengo hayo bado tuko nyuma. [11]
baina
Katibu mkuu wizara hiyo, Dk Florens Turuka aliridhia kufanyika kwa vikao vya ziada baina ya wabunge wa kamati, serikali na wadau wa habari lakini akataka kusiwe na shinikizo kutoka kwa wadau na wanaharakati. [12]
bandari
Ili kutekeleza jambo hilo la kuhakikisha kuwa mizigo inaondolewa bandari haraka, aliziagiza TPA na TRA kuhakikisha kuwa zinapiga mnada kiasi cha asilimia 30 ya makontena yaliyokaa bandarini zaidi ya siku 21, ikiwa ni njia ya haraka ya kupunguza mlundikano wa mizigo. [13]
beki
Katika dakika za 15 na 22 beki wa Yanga, Amir Maftah kama angekuwa makini, angeweza kuiandikia Yanga bao kabla ya Gaudence Mwaikimba naye kukosa bao katika dakika ya 33 akiwa karibu kabisa na lango. [14]
bila
Mikopo inatolewa bila kutoza riba na urejeshwaji wake huchukua muda mrefu (hadi miaka 10) ni dhahiri kwamba thamani yake inapungua. [15]
bin
Wababe wa kivita walifanikiwa kuuondoa utawala wa kijeshi wa Kirusi hadi pale kundi la Watalebani lilipoitwaa nchi hiyo mwaka 1996. Utawala huo wa Watalebani ulifikia tamati mwaka 2001 kutokana na nguvu kubwa za kijeshi za Marekani, iliyokuwa ikimuunga mkono Osama bin Laden wakati huo. [16]
binamu
Mdogo wake, Amanullah alitwaa madaraka hadi mwaka 1929 madaraka yake yalipochukuliwa na binamu yake Nadir Khan aliyeongoza kwa miaka minne kabla ya kuuawa. [17]
bondia
Alisema mbali ya pambano hilo kutakuwa na pambano lingine kati ya Mtanzania Khalid Mkasa dhidi ya bondia Dan Agar wa Ufaransa kuwania ubingwa wa mabara. [18]
cha
Ingawa sera ya kuchangia huduma ni jambo la msingi katika jamii, kitendo cha Bodi ya Mikopo kuwagawa wanafunzi katika makundi sita kinaigawa nchi katika makundi mawili na inawaongezea wazazi mzigo. [19]
chake
Lakini jana, Rais Kikwete, ambaye alikuwa na mkutano na viongozi wa Wizara ya Miundombinu, wa Mamlaka ya Bandari (TPA) na uongozi wa Bandari ya Dar es salaam uliofanyika Ikulu, aliitaka TICTS kutekeleza wajibu wake ipasavyo kwa mujibu wa mkataba wake kwa kuongeza ufanisi na kuboresha kiwango chake cha utendaji kwa lengo la kupunguza mlundikano wa meli bandarini. [20]
dhidi
Naye kocha wa Zesco, Fighton Simukonda aliwasifu wachezaji wake kuwa pamoja na uchovu wa safari na mechi dhidi ya Simba, wamechoka lakini wamejitahidi kwa kiasi kikubwa. [21]
don
Suti hilo! Yaani suruali ilikuwa mfano wa ‘don’t touch’ na tai ilikuwa inajikunja kutokana na kutumika miaka si chini ya ishirini. [22]
duni
Kwa hiyo tukiwa wadau muhimu wa elimu tunona kwamba, wanafunzi hao dhaifu ambao hufundishwa katika mazingira duni na walimu wasio na uwezo, ndiyo sababu za msingi za kushuka kwa ufaulu, hivyo tatizo hilo litafutiwe ufumbuzi. [23]
dunia
BINGWA wa Mabara wa mchezo wa kickboxing, Japhet Kaseba atapanda ulingoni Machi Mosi kuzipiga na Digregorio Cosimo wa Italia katika pambano la kuwania ubingwa wa dunia (WKN) litakalofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. [24]
duniani
SHIRIKA la Ndege la Emirates ambalo linafahamika zaidi kwa udhamini wa michezo duniani, limedhamini kwa mara ya pili mfululizo michuano ya Wazi ya Gofu Afrika inayofanyika Afrika Kusini. [25]
es
Alisisitiza kuwa gazeti la The Citizen si tu kwamba halihaririwi Nairobi, bali hata mhariri wake mtendaji, mhariri wa habari, msanifu mkuu, wahariri wengine na waandishi wote ni Watanzania na kazi zote za kuandaa, kuhariri na kuchapa gazeti hilo zinafanyika Dar es Salaam. [26]
faida
Kabla sijaeleza sababu ambazo naona zinasababisha kushuka kwa e-government nchini, labda nitaje faida za mpango huu. [27]
fanya
Ni wachezaji wachache hapa nchini ambao hakika wanaweza kufanya kama alivyo fanya Mgosi, tena ukizingatia mechi yenyewe ilikuwa ya kirafiki. [28]
fulani
Kwa kawaida mtu unapoumwa, mwili unakuwa umekosa viasili fulani vinavyohitajika mwilini. [29]
gani
Kama idara haina fedha ya kufanya vikao hivyo, basi mkurugenzi aandae bajeti kwa katibu wa kamati hii na yeye atajua ni jinsi gani ya kupata fedha za kufanyia vikao na wadau. [30]
gofu
Jinsi tunavyoendelea kupanua uwepo wetu Afrika Kusini, kudhamini michuano mikubwa ya gofu kama michuano ya wazi ya gofu Afrka ni fursa ya kusaidia maendeleo ya mchezo huu wa gofu. [31]
haja
Naye mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Habari (Maelezo), Habib Nyundo alikiri kuwepo kwa upungufu na changamoto katika sheria hiyo na kuongeza kwamba kuna haja kubwa ya kuifanyia marekebisho. [32]
hana
Hata hivyo, Sir Alex Ferguson alisema kuwa hana mpango wa kumwachia mchezaji huyo kutimka. [33]
hasa
Alisema, Tanzania ni miongoni mwa mataifa mengi yanayokabiliwa na changamoto ya wingi wa vifo vya akinamama wajawazito hasa wakati wa kujifungua na hii ni kwa sababu, wauguzi na wakunga hawajawajibika vilivyo. [34]
hata
Katika hatua nyingine, Kwaang' alisema utaratibu huo haustahili hata kidogo kwa sababu inawaongezea wazazi mizigo ambayo haistahili na kwamba inawafanya washindwe kuwasomesha watoto. [35]
hatari
Kwa sasa tunafanya utafiti wa kuweza kuponya ugonjwa hatari wa Ukimwi kwa kutumia hivi hivi vyakula. [36]
hawana
Wachezaji wana miili lakini wanaonekana hawana nguvu. [37]
hicho
Ukaguzi uliofanywa jana katika kituo hicho na maafisa wa Jeshi la Polisi ulibaini kuwa, mabasi hayo yaliyokuwa yanaelekea mikoani yalikuwa na matatizo ya kiufundi hivyo kuyaamuru yasiondoke mpaka yatakapotengenezwa. [38]
hii
Wageni wanamiliki hisa nyingi zaidi ya asilimia 60 kuliko mzawa na hii ni kwa sababu wazawa waliokuwa na hisa katika kampuni hiyo waliamua kuuza hisa zao kwa wageni. [39]
hisa
Tumebaini kuwa mwekezaji wa kigeni anamiliki hisa nyingi zaidi kuliko mzawa mzalendo," alisema mkurugenzi huyo. [40]
hivi
Naye bondia Japhet Kaseba alisema hivi sasa yuko katika maandalizi makubwa kujiandaa na mpambano huo na akawashukuru mashabiki wake kwa kumpa sapoti na ushirikiano kwani ndio siri ya ushindi wake. [41]
hizi
Lakini pamoja na hayo, serikali imefanya jitihada kuhakikisha kwamba huduma hizi zinakuwa juu lakini baadhi ya watendaji wake wanazembea. [42]
hujui
Utamaduni huu shostito ni wa pwani, kama ulikuwa hujui chukua hiyo, Na ukweli ni kwamba wanawake wengi wa pwani wanajua maana ya chai ya jioni na ndiyo maana wanasifiwa kuwa wanayajua mambo. [43]
huko
Taifa hili la Kiislamu linaloongozwa na Rais Hamid Karzai, linalokadiriwa kuwa na jumla ya watu milioni 32.7, ikiwemo wengine milioni 3.5 wanaoishi kama wakimbizi huko ughaibuni, lilianza kuvamiwa na Himaya ya Median (Iran) iliyojipanua na kuingia katika eneo la nchi hiyo miaka 700 kabla ya kuzaliwa Kristo. [44]
hupewa
Hadi sasa hakuna dawa ya hospitalini inayotibu kisukari, sana sana wagonjwa hupewa dawa maalumu ya kuongeza insulini mwilini ili sukari iweze kuchujwa. [45]
huu
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa vyumba vya madarasa ,Mwambungu aliwataka viongozi wa ngazi zote kuhamasisha wazazi na wakazi wa Manispaa hiyo washiriki katika kazi ya ujenzi huo na kwamba mwisho ni Machi mwaka huu. [46]
huwa
Kwa mfano, mtu anayeumwa tezi la shingo (goitre), huwa amepungukiwa na madini joto yaliyomo kwenye chumvi," anasema Kikao. [47]
huyo
Mwenyekiti huyo alitoa kauli hiyo siku moja baada ya vyuo vikuu mbalimbali nchini, kutangaza utaratibu mpya wa kuwarejesha wanafunzi waliofukuzwa mapema mwaka jana kwa sababu za mgomo vyuoni. [48]
ikiwemo
Kwa mfano, mwaka 2000, serikali kupitia wahisani mbalimbali ilianzisha Programu ya Maboresho ya Huduma za Serikali (PSRP), ambayo moja ya malengo yake ilikuwa ni kuiwezesha kutumia kompyuta katika shughuli zake za kila siku ikiwemo matrumizi ya mtandao. [49]
iko
Hata hivyo Kwaang' alifafanua kwamba sera ya kuchangia iko katika sekta zote, lakini tatizo ni namna ya kuitekeleza kwani utekelezaji wake inachangia kuwagawa wanafunzi na kwamba, hali hiyo ikiachwa iendelee itawagawa watoto wa Kitanzania kwa maana kwamba kutakuwa na tabaka la watu wenye elimu na wasiokuwa na elimu ndani ya nchi moja. [50]
ile
Kutokana na ugumu wa masharti hayo na kwa kuwa mkazo wa uongozi wa UDSM uko katika kupata pesa kwa asilimia ile ambayo kila mwanafunzi anapaswa kutoa, ni asilimia 33 tu ya wanafunzi wote wa shahada ya kwanza waliotekeleza na ambao kimsingi ndio wataruhusiwa kuingia darasani kuanzia Jumatatu. [51]
ili
Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo, George Nyatega alisema ili kukuza kiwango cha fedha zinazotolewa wakati wa mikopo, inapaswa fedha hizo zitozwe riba. [52]
imara
Huku kocha wake Patrick Phiri akiwa anasimama mara kwa mara kutoa maelekezo, Simba ilijitahidi kupanga mashambulizi lakini hata hivyo ngome ya Zesco ilikuwa imara. [53]
ina
MKURUGENZI msaidizi wa Maelezo, Raphael Hokororo ameieleza Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii kuwa, serikali ina mgogoro na kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), inayochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, kuhusu umiliki wake. [54]
ini
WAKATI serikali na wadau mbalimbali wakihangaika kutafuta dawa za magonjwa sugu kama vile kisukari, pumu, moyo, ini, malaria na mengineyo, kiasi cha kuwafanya wengine kwenda kutibiwa nje ya nchi, imeelezwa kwamba chakula hiki tunachokula kila siku ni dawa ya magonjwa hayo. [55]
ipo
Kuhusu muswada wa sheria ya habari, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera alisema marekebisho ya sheria hiyo namba tatu ya mwaka 1976 ya magazeti ipo jikoni na itawasilishwa bungeni kujadiliwa wakati wowote itakapokamilika. [56]
iwapo
Alifafanua kwamba, malipo wanayotoa kwa walimu wa nje ni madogo na iwapo yatakatwa kodi, walimu hao watagoma na kuilazimu serikali kuongeza. [57]
jengo
Kumekuwa na hamaki kubwa ya kuhimiza utafiti na kutaka hatua zichukuliwe pindi inapotokea jengo kuporomoka lakini baada ya muda mfupi kupita, shime hiyo husahaulika. [58]
jingine
Alitaka hilo lifanyike kwa kutafuta eneo jingine la kuhifadhia magari nje ya bandari. [59]
jipya
SI jambo jipya kwa wananchi kujichukulia sheria mkononi na kumuadhibu, hata kumuua, mtu wanayemtuhumu kwa wizi, lakini wakazi wa Buhongwa jijini Mwanza walienda mbali zaidi walipogawana mali waliyodai iliibiwa na baadaye kuliteketeza gari la mtuhumiwa. [60]
juu
Hii ni kodi ya kiuzushi," alisema Prof Mbwette katika mahojiano na Mwananchi na kufafanua kuwa, alifanya vikao kadhaa na viongozi wa juu wa TRA kuhusiana na suala hilo, lakini cha kushangaza wanashikilia msimamo kuwa malipo hayo ni ya kisheria hivyo ni lazima walipwe. [61]
juzi
Nyoni alitoa wito huo juzi katika sherehe za uzinduzi wa Baraza hilo zilizofanyika jijini Dar es Salaam. [62]
kadhaa
Sheria pia haifafanui mambo kadhaa muhimu yanayohitajika katika uendeshaji wa sekta nzima ya habari nchini," alisema Nyundo. [63]
kali
Mwanza alifumania nyavu kwa shuti kali baada ya ngome ya Simba kujichanganya. [64]
kama
Akihitimisha semina ya kamati hiyo ya bunge, Bendera alisema: “Kwa sasa rasimu iko jikoni inachapwa kwa wataalamu wa ICT na ikimaliza hapo itapelekwa wizarani na baadaye bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na hatimaye kupitishwa kama sheria. [65]
kansa
Akieleza magonjwa ambayo huyatibu katika kituo chake, Kikao anasema: "Ninatibu ugonjwa wa ini, kifafa, kisukari, kansa na mengineyo. [66]
kasi
RAIS Jakaya Kikwete jana aliiagiza kampuni inayolalamikiwa ya upakiaji na upakuaji mizigo bandarini ya TICTS, kuhakikisha inafanya kazi zake kwa mujibu wa mkataba na kuongeza kasi ya kupunguza tatizo la mlundikano wa mizigo kwenye Bandari ya Dar es salaam. [67]
kati
Dereva mmoja anayeendesha basi linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Dodoma alisema ajira ni tatizo kubwa kwao. [68]
kemikali
Vyakula tunavyokula kila siku ni dawa, na kama watu wangefahamu siri hii kusingekuwa na haja ya watu kutumia dawa za kemikali zinazotolewa hospitalini. [69]
kidato
Alisema kila kata ilipangiwa kujenga vyumba vitano vya madarasa ili kukidhi mahitaji ya upungufu wa vyumba 101 vya madarasa na kuwawezesha wanafunzi wote waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza. [70]
kikao
KAMATI ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuacha kigugumizi na kutoa tamko kuhusu mkataba wake na Wakala wa Utoaji Mizingo Bandarini (TICTS) katika kikao kijacho cha Bunge. [71]
kimoja
Anapenda, muwekee na kibiskuti kimoja cha tangawizi pembeni. [72]
kivita
Mataifa haya yalianza kuivamia nchi hii miaka 700 kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo, yakiwa na nia tofauti, lakini kikubwa zaidi kujilinda kivita kutokana na nchi hiyo kuwa kiungo cha mataifa ya Asia ya Kati, sehemu ya India na Mashariki ya Kati. [73]
kontena
Aliwataka kuchukua hatua hiyo kwa kutumia taratibu muhimu zilizopo, ikiwa ni pamoja na kontena kupigwa mnada baada ya kuwa zimekaa bandarini kwa siku 21 kama sheria inavyotaka. [74]
kuanguka
Athari kubwa ya ugonjwa huu ni mtu kuanguka kila mara. [75]
kufa
Walipogundua wamevamiwa na wananchi walitoka ndani ya gari na kuanza kukimbia wote na dereva wa taksi aliingia mtaroni na kupita katika kalvati la maji kutoka upande wa pili, lakini alionekana na alipotakiwa ajisalimishe, alionyesha ukaidi na ndipo alipomshambulia kwa mapanga na marungu hadi kufa. [76]
kuimba
Kweli wanaweza kuingia hivihivi? Kweli wataingia kama milolongo ya vijana wanaotafuta nafasi moja ya Ustaa wakati ambapo hata wenzao wa mitaani wanawacheka wakijaribu kuimba. [77]
kuitwaa
Historia ya taifa hilo kuendelea kuvamiwa kwa sababu za kujiimarisha kivita kwa mataifa yenye nguvu, inaonyesha kuwa mataifa mengine mengi yalijitokeza kutaka kuitwaa nchi hiyo. [78]
kuja
Mchezaji huyo amekuwa hapangwi mara kwa mara Old Trafford hasa baada ya kuja Dimitar Berbatov. [79]
kujengwa
Meya wa Manispaa ya Ilala, Abuu Jumaa, anasema kuwa Kamati ya Vibali na Ujenzi ya Manispaa ya Ilala inapaswa kusimamisha utoaji wa vibali hivyo kiholela bila ya kuangalia kitu kinachotakiwa kujengwa kwani kwa kufanya hivyo ni kuendelea kuhatarisha maisha ya watu. [80]
kujua
Msajili wa baraza hilo Gustav Moyo alisema mfumo huo utasaidia kupata taarifa sahihi za wauguzi na kujua mwenendo wao wa kazi Alisema katika kusimamia maadili ya wakunga na wauguzi baraza limefanya ukaguzi nchi nzima na kubaini makosa mbalimbali likiwenmo la wauguzi kugushi vyeti vya taaluma. [81]
kukaa
Umoja wa Wazalishaji wa Kahawa nchini (TCA) umedai kwamba, kutokana na ucheleweshaji huo, katika kila magunia 300 ya kahawa, 100 hupotea kwa kuoza kutokana na kukaa muda mrefu ndani ya kontena yakisubiri kusafirishwa. [82]
kumi
Ama baada ya salaam kwa idhini yenu naomba niweke mezani mada hii iliyoko mbele yetu hii leo; Chai ya saa kumi. [83]
kunywa
Kwa mfano, ugonjwa wa malaria ambao unaongoza kwa vifo nchini, unaweza kutibiwa kwa kunywa maji tu. [84]
kupitia
Kauli hiyo imetolewa na kamati hiyo kupitia Mwenyekiti wake, Mohamed Missanga jijini Dar es Salaam juzi. [85]
kutaka
Kwa sasa, Majeshi ya Umoja wa Kujihami wa nchi za Magharibi (Nato) yanakalia sehemu kubwa ya nchi hii kwa madai ya kutaka kuyaondoa makundi ya kigaidi ya Al – Qaeda. [86]
kutibu
Mtaalamu wa tiba za vyakula wa kituo cha tiba ya chakula cha Kikao Natural Food Therapist Clinic (KNFTC), kilichopo Turiani mkoani Morogoro, John Kikao anaeleza jinsi chakula kinavyoweza kutibu magonjwa hayo. [87]
kutoa
Hatujakaa na serikali na wadau kujadili na kutoa mapendekezo ya sheria hii. [88]
kutwaa
Polisi waliofika eneo la tuikio alfajiri kwa ajili ya kutwaa mwili wa marehemu pamoja na vielelezo vingine katika eneo la tukio, walikuta wananchi wakiwa wanakata gari hilo vipande kwa ajili ya kuviuza kama chuma chakavu na walipotaka nyama iliyokamtwa katika gari hilo, walizidiwa nguvu na wananchi na kufanikiwa kutwaa kiasi kidogo cha nyama huku kingine wakigawana wananchi. [89]
kuwa
Sababu kubwa iliyofanya wanafunzi hao kuanzisha migomo hiyo ni kupinga sera ya uchangiaji wa elimu, wakidai kuwa inawapa upendeleo wanafunzi wanaotoka katika familia zenye uwezo na kuwabana wale wanaotoka katika familia zisizokuwa na uwezo. [90]
kuwepo
Pia sheria hiyo inazungumzia kuwepo kwa viwango vya elimu kwa waandishi, na umiliki wa vyombo vya habari. [91]
la
WABUINGE wameitaka serikali isimamie zoezi la kuwarejesha wanafunzi wa vyuo vikuu waliofukuzwa na kuhakikisha kwamba wote wanarudishwa masomoni. [92]
lake
Walikuwa wamefanikisha mtego wao wa wizi wa ng'ombe uliomnasa dereva wa taksi anayejulikana kwa jina la Johnson Chacha, ambaye anadaiwa kuiba nyama ambayo ilikutwa kwenye gari lake na kusababisha wananchi hao kuamua kutoa kipigo hicho cha kikatili kilichokatisha maisha yake. [93]
leo
Semina hiyo inaendelea tena leo kwenye ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora uliopo jijini hapa. [94]
letu
Kama sisi tulijitahidi sana kwa sababu tulichoka lakini ingekuwa tumefika siku mbili kabla ungeona soka letu, tuliwazidi Simba wanavyonekana bado kuna attizo na wanahitaji mazoezi ya nguvu. [95]
licha
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Wilson Masilingi alisema kuwa Ikuli imewathibitishia kuwa hali ya ulinzi na usalama nchini ni shwari licha ya matatizo madogo madogo ya kijamii. [96]
ligi
Nimeambiwa wengine hawakuwepo hivyo sijawaona lakini marekebisho ni muhimu huo ni ushauri wangi, kwani wakati niko Zambia niliambiwa hii timu haifanyi vizuri kwenye ligi lakini sioni sababu inayowafanya wakashindwa kuwika kama Simba ninayoifahamu. [97]
lita
Kwanza unapoamka asubuhi kabla hata hujapiga mswaki unakunywa lita moja ya maji. [98]
maalum
Baada ya wanafunzi kusimamishwa, uongozi wa vyuo uliweka masharti magumu zaidi ya kurejea kwao kama vile kujaza fomu maalum. [99]
madaktari
Tunakabiliwa pia na tatizo la vifaa na madaktari. [100]
madhubuti
Vile vile sababu nyingine ambayo inasababisha teknolojia hii muhimu kutotumika ipasavyo ni pamoja na kukosekana kwa sera na mipango madhubuti ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama), katika taasisi za serikali. [101]
magari
Rais pia alizungumzia mlundikano wa magari yanayosubiri kuchukuliwa na wenyewe bandarini, akitaka kutafutwa maarifa ya kuyaondoa ili kupatikane nafasi zaidi ndani ya eneo la bandari hiyo kwa shughuli na mizigo mingine. [102]
mahaba
Chai iliyoandaliwa kwa mahaba huamsha mahaba. [103]
mara
Tunakagua mabasi yote kabla ya kuanza safari mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa, maisha ya abiria yanakuwa salama," alieleza Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Awadhi Haji. [104]
masikini
Lakini badala yake wameyatupa kiasi kwamba asilimia 67 ya wanafunzi wengi wao kutoka familia masikini wanatarajiwa kukosa elimu ya juu kwa sababu ya umasikini wao. [105]
mazao
Harakati za Pinda zisiishie jukwaani KATIKA harakati za kuboresha kilimo nchini, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameendelea na kampeni yake ya kufufua uzalishaji wa mazao mbalimbali kwa kuwataka viongozi wote wa serikali ‘kujinyonga’ kwa lengo la kumsaidia mkulima wa kawaida. [106]
mbele
Alisema basi la Sumry lililokuwa likiondoka kituoni hapo lilikutwa likiwa na hitilafu kwenye kioo cha mbele ambayo ingeweza kusababisha ajali hivyo walilizuia kuondoka. [107]
mdomoni
Hiyo itawezesha ule uchafu wa mdomoni kurudi tumboni na kufyonzwa na mishipa ya damu. [108]
mengine
Aliyataja mabasi mengine yaliyozuiliwa kusafirisha abiria kuwa ni Akamba lililokuwa likielekea Nairobi, Super Feo na Alsaeidy yaliyokuwa yakielekea Kahama. [109]
mfumo
Katika hatua nyingine TNMC, imeanzisha mfumo wa kukusanya na kuhifadhi taarifa za wauguzi na wakunga wote unaotambulika kama (Data Bank) kwa lengo la kuwa na kumbukumbu sahihi za wauguzi wote nchini. [110]
mganga
Mzee Kikao alianzaje kuwa mganga?: "Kabla ya kuanza shughuli za uganga kwa kutumia vyakula, nilikuwa mwalimu wa shule za msingi hapa wilayani Turiani. [111]
mifuko
Badala ya kukaa na kufurahia kutoboka kwa mifuko na kupasuka kwa suruali yenye mifuko, kila mara wanatafuta kazi zingine za kufanya. [112]
minne
Ripoti hiyo ya miaka minne iliyopita inaonyesha kuwa Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya 127 mwaka 2005 hadi 147 mwaka jana. [113]
miti
JANUARI Mosi mwaka huu ilikuwa ni siku ya taifa ya kupanda miti. [114]
mkazi
Mmiliki wa ng'ombe aliyeibwa, William Luchemba, 50, mkazi wa kijiji cha Idetemya, alisema ingawa hakubaliani na kitendo cha kumuua mtuhumiwa, amefarijika na kubainika kwa wezi hao kwa kuwa limekuwa ni tatizo kubwa. [115]
moyo
WANACHAMA wa klabu ya Simba wamempongeza mshambuliaji wa timu hiyo, Mussa Hassan Mgosi kwa kuwa na moyo wa kujituma kutetea klabu yake bila kujali kuwa na majukumu ya timu ya taifa. [116]
msimu
Mchezaji huyo anamaliza mkataba wake Old Trafford mwishoni mwa msimu. [117]
mtindo
Mwambungu, alisema umezuka mtindo kwa baadhi ya walimu wakuu kuwafukuza wanafunzi wa sekondari na za msingi kwa kisingizio cha kutolipa ada na michango jambo ambalo alisema halitakiwi. [118]
mwa
Alisema taarifa hizo ni za kusikitisha kwa kuwa hazina ukweli wowote kutokana na ukweli kuwa, gazeti hilo liko mikononi mwa Watanzania ambao ni wazawa. [119]
mwalimu
Lakini kama wakizingatia haya, na wakafuata ushauri wa mwalimu wao, Patrick Phiri, naamini watafanya vizuri. [120]
mwingine
Wakati mwingine huwabadilishia vyakula wagonjwa hadi wanapopona. [121]
mwishiwa
Si kila mtu anaweza kuchekesha? Kwa nini tusifanye na sisi?’ ‘Kweli kabisa mwishiwa Supu. [122]
mzuri
Akizungumzia mchezo huo, Kondic alisema kuwa vijana wake wamecheza vile ambavyo hakutarajia, lakini aliwasifu kutokana na mchezo mzuri. [123]
nao
Singida vijijini na wilaya ya Manyoni, ingawa hawajaniletea orodha ya waombaji, lakini nilipoongea nao kwa simu, Singida vijijini wamesema watu tisa na Manyoni wanane, wameomba kupatiwa mafunzo ya awali ya waamuzi wa soka"alisema Magazi. [124]
nauli
Dereva wa basi linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Tanga alidai kuwa analipwa posho ya Sh20,000 na nauli ya abiria mmoja kulitoa gari Dar es Salaam kwenda Tanga. [125]
nayo
Alisema fedha zitakazoongezeka zitatoka serikalini ili ziende TRA ambayo nayo itazirejesha tena kwa serikali, jambo ambalo halitakuwa na maana yoyote bali ni kuifanya mamlaka hiyo kujipalilia sifa kwamba, ina makusanyo makubwa wakati si kweli. [126]
ndio
Najua kuwa sheria hii imepitwa na wakati na ndio maana tunataka kuileta bungeni ijadiliwe. [127]
ndiyo
Nampongeza Mussa Hassan Mgosi kwa kufika na kucheza, hii ndiyo inayotakiwa kwa mchezaji, naamini wachezaji wengine wataiga mfano huu. [128]
ndizo
Uchunguzi uliofanywa na vyombo vya habari kwa muda mrefu na ambao unaendelea kufanywa kila siku kwa kufika shuleni kushuhudia hali halisi, unaonyesha shule nyingi hasa zilizoanzishwa kisiasa chini ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) yaani sekondari za kata, ndizo zinaongoza kwa matokeo mabaya. [129]
ng
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa walipata taarifa ya simu ya mkononi usiku wa saa 9: 38 kutoka kijiji cha Idetemya, kata ya Usagara wilayani Misungwi, ikiwajulisha kuwa kulikuwa na wizi wa ng’ombe na hivyo wakaandaa mtego. [130]
ni
Moja ya taratibu hizo ni suala la kujaza fomu na kujiandikisha upya huku wakitakiwa kulipa madeni yote wanayodaiwa chuoni hapo. [131]
nia
Lakini hawakuishia hapo, wananchi hao wagawana kitoweo hicho na baadaye kuliteketeza gari lake kwa moto kabla ya kulikata vipande vipande na kila mtu kuondoka na sehemu yake, wengi wakionekana kuwa na nia ya kuuza kama chuma chakavu. [132]
nini
Kuna baadhi ya wasomaji wataanza kujiuliza e-government ni nini? Hizi ni huduma ambazo zinatolewa na serikali kwa wananchi wake kwa njia ya kompyuta ambayo imeunganishwa katika mtandao wa internet. [133]
nyongo
Ugonjwa huo pia huandamana na kuathirika kwa bandama na nyongo. [134]
ovyo
Alisistiza kuwa wao wabunge kwa kuwa wana dhamana kubwa kwa wananchi, hawapaswi kuachia mambo nyeti yaende ovyo ovyo kwa kuwa wakifanya hivyo nchi haitatawalika. [135]
pale
Moja kati ya mafanikio aliyoyapata Kaseba ni kutwaa ubingwa wa Dunia, Mabara, Afrika na Tanzania na akiwa na rekodi ya pekee ya kuwagalagaza wapinzni wake katika dakika za awali za mchezo moja likiwa ni pambano la kuwania ubingwa wa dunia mwaka jana pale alipomchapa Abjeeht Petkar wa India na kisha kumtwanga Ricky Agays wa Phillipins katika raundi ya kwanza tu ya mchezo. [136]
peke
Wanakunywa peke yao huko wazee, na hata wake na watoto wanaachwa peke yao. [137]
pekee
Pia walihoji uwezo wa kampuni hiyo katika kutatua tatizo la mlundikano wa mizigo bandarini, wakidai kuwa imeonyesha haina uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa ufanisi au inafanya kwa kusuasua, ili iendelee na tenda hiyo, wakati wabunge wengine walihoji sababu za TICTS kupewa haki pekee ya kufanya kazi hiyo. [138]
pia
Kwaang' pia alisema hakuna sababu ya nchi kuendelea kubeba mzigo wa kusomesha watoto wanaotoka familia zenye uwezo wakati kuna watoto wanaohitaji msaada wa serikali. [139]
pikipiki
IBRSPJBO-48 900772 inayodaiwa kuwa ya pikipiki iliyokuwa haijapata usajili hapa nchini," alieleza Kamanda Rwambow. [140]
pili
Haya makundi ya wanafunzi wanaopewa mikopo yanaongeza mzigo kwa wazazi na pili yanaleta tabaka la elimu ndani ya nchi kiasi ambacho kinatufanya tujiulize maswali mengi," alisema. [141]
pindi
Vyombo vya habari haviitaki kabisa sheria namba 3 ya 1976 kwa sababu vinadai serikali imepewa uwezo mkubwa wa kuviingilia, kuvifungia na hata kuchukua mali zao pindi vinapokosea," alisema. [142]
posho
Alisema madereva wengi, wanalipwa posho badala ya mshahara hivyo kuwafanya washindwe katika kazi zao. [143]
programu
Hadi awamu ya kwanza ya programu hiyo ilipomalizika mwaka jana, mafanikio yaliyopatikana na kidogo. [144]
ripoti
UTAFITI uliofanywa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa (UN) kuhusiana na masuala ya e-government na ripoti yake kutolewa mwaka jana, Tanzania imeshuka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mwaka 2005, ripoti hiyo ilipotolewa mara ya mwisho. [145]
saa
Ili kufanikisha uharaka huo, aliwaagiza TRA kuhakikisha kuwa sehemu ya kushughulikia nyaraka ya long-room inafanywa kuwa short-room kwa maofisa wa mamlaka hayo kufanya kazi kwa saa 24, ikiwa ni pamoja na siku za Jumapili. [146]
sare
Huo ulikuwa mchezo wa pili wa Zesco ambayo iliwasili nchini siku nne zilizopita na ilianza kwa kutoka sare ya bao 1-1 na Simba katika mchezo wa kwanza uliofanyika juzi kwenye uwanja huo. [147]
sawa
Hapa tunaanza kushuhudia ubaguzi ukianza kujitokeza katika sekta ya elimu kwamba, watoto wa masikini hawana nafasi tena ya kupata elimu ya juu, ikimaanisha kuwa vyuo vya umma sasa ni sawa na vyuo binafsi ambako mwanafuzi asiyelipa ada hufukuzwa. [148]
shule
SERIKALI wilayani Morogoro imewataka walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari kuacha kuwazuia wanafunzi kuingia darasani, kwa madai kuwa wazazi wao wameshindwa kulipa michango mbalimbali na ada ya shule. [149]
soka
MABINGWA wa soka Tanzania, Yanga na mabingwa wa soka wa Zambia, Zesco wameshindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu, katika mchezo mkali wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. [150]
sumu
Dawa za kemikali ni sumu kwa hiyo mtu akizitumia sana huleta madhara makubwa mwilini ikiwamo kuharibu ini. [151]
tabia
Nyoni alilitaka Baraza hilo kusimamia na kuhakikisha viwango vya elimu na tabia ya wauguzi vinazingatiwa na kudumishwa na kulitaka kuchukua hatua za kinidhamu kwa wanaokiuka maadili ya kazi. [152]
tabu
Gazeti la Kingereza la TheCitizen linalochapishwa na kampuni ya mwananchi linahaririwa jijini Nairobi Kenya na kuchapwa Tanzania na wala wenyewe hawaoni tabu,” alisistiza. [153]
tatu
Katika kundi la tatu, mwanafunzi hupata mkopo kwa asilia 40 na kundi la mwisho linahusu wanafunzi ambao hawapati mkopo kabisa. [154]
tiba
Hii ni tiba muafaka ya usumbufu, urasimu, rushwa na gharama za uendeshaji wa shughuli za serikali. [155]
ufaulu
MAPEMA mwaka jana, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ililiambia Bunge ilivyosikitishwa na kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa wanafunzi na kwamba, ilikuwa inafanya utafiti kujua sababu zake. [156]
uhaba
Vile vile kuna uhaba wa vifaa mbalimbali vya maabara. [157]
ule
Katika mkutano wake wa pili, Rais Kikwete alitarajiwa kukutana jana jioni na uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), na ule wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA). [158]
umekuwa
Alisema hatua hiyo itaiwezesha Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), hata kampuni nyingine kufanya kazi hiyo ili kuondoa msongamano wa mizigo bandarini ambao katika siku za karibuni umekuwa ni mkubwa na unaotia aibu Taifa. [159]
umma
MWISHONI mwa mwaka jana wanafunzi wa shahada ya kwanza kutoka vyuo vikuu saba vya umma nchini, walisimamishwa masomo kutokana na mgomo wao wa kupinga sera ya uchangiaji elimu ya juu. [160]
umuhimu
Kaimu mwenyekiti wa kamati hiyo ya bunge ya Maendeleo ya Jamii, Haroub Said (Mbunge) alisisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wadau katika kujadili marekebisho ya sheria hiyo. [161]
usanii
Ni kupoteza muda kabisa hata watumie usanii namna gani. [162]
usio
Anasema kuwa, serikali inapaswa kuwachukulia hatua kali makandarasi waliokutwa na hatia ya kufanya ujenzi usio kuwa na tija kwa wananchi. [163]
utawala
Miaka 150 baada ya uvamizi wa Iran, waliokuwa wapinzani wao wakubwa, Persian waliivamia na kuwaondoa Wairan hao na kuanzisha utawala wa aina yake ulioitwa Achaemenid Dynasty. [164]
uti
Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Cheju, Zanzibar juzi baada ya kukagua kilimo cha mpunga katika eneo hilo, alifahamisha kuwa anaposema viongozi wajinyonge anamaanisha kwamba, wabadilike na kuacha maneno badala yake wajitoe kikamilifu kufanikisha azma ya serikali katika kufufua kilimo, vinginevyo kilimo hakiwezi kuwa uti wa mgongo wa taifa hili na mkombozi wa wanyonge ambao kazi yao kubwa ni kulima. [165]
utoaji
Alibainisha kuwa kuna tatizo kubwa katika suala la utoaji wa vibali kwa kufuata masharti ya vibali vya ujenzi. [166]
utundu
Lakini bado nafikiri huu unaweza kuwa utundu unaoweza kukutumia ukakusaidia. [167]
uwanjani
Wakati mchezo unaendelea, mshambuliaji wa Simba na Kilimanjaro Stars, Mussa Hassan Mgosi aliingia uwanjani na kushangiliwa na mashabiki wachache waliofika uwanjani hapo. [168]
uwe
Chai hii shosti haihitaji digrii, au lazima uwe umezaliwa na hotelia, laahasha na wala si ngumu kutengeneza almuhimu hapa ni makusudio yaliyolengwa. [169]
vibaya
Ni dhahiri kuwa itajisikia vibaya hivyo kuboresha na kuongeza juhudi ili ripoti nyingine itakapotolewa iweze kufanya vizuri. [170]
vifaa
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Rais Kikwete ameitaka TICTS kununua vifaa zaidi na pia kuhakikisha kuwa vifaa vya TPA vinatumika. [171]
vile
Akizungumza kwenye semina ya kamati hiyo iliyofanyika ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Hokororo alisema serikali ina mgogoro na kampuni hiyo kwa vile inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na wageni, kitu ambacho alisema hakitakiwi. [172]
vipaja
Siku ya vipaja? Mwishiwa Supu unawaita waamuzi kwa ajili ya siku ya vipaja? Hata sisi tunaweza kuamua. [173]
vipaji
Usiku wa vipaji mwishiwa. [174]
vipimo
Hospitali zingebaki tu na kazi za vipimo na ushauri, lakini vyakula hasa vya mimea ni dawa za magonjwa sugu. [175]
vita
Hata hivyo, kwa kuwa waziri mkuu ameanzisha vita, tunaomba aweke utaratibu wa kuwafuatilia wasaidizi wake wote, ili waweze kutekeleza wajibu wao ipasavyo, vinginevyo zitakuwa porojo za kisiasa zinazoishia kwenye majukwaa ya kisiasa na ambazo mwisho hakuna anayehoji wala kuchukuliwa hatua. [176]
vya
Alisema vyombo vya habari ni kama bomu na kwamba kama umakini hautakuwepo katika marekebisho ya sheria hiyo, nchi haitatawalika. [177]
vyenu
Hapa nawalinda kabisa na vijisenti vyenu. [178]
waamuzi
Hayo yalisemwa juzi na mwenyekiti wa chama cha waamuzi mkoani hapa, Josephat Magazi, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati inayochuliwa na chama hicho ya kuondoa tatizo kubwa la waamuzi wa soka mkoani Singida. [179]
wagonjwa
Mpaka sasa nimeshatibu zaidi ya wagonjwa 10 wa ugonjwa wa ini. [180]
waishiwa
Lo! Mimi nilidhani waishiwa watacheka na kuendelea na kujiliwaza kwao. [181]
wamekuwa
Usafirishaji wa mazao bandarini uboreshwe WAKATI serikali inakazana kuboresha kilimo nchini, baadhi ya wadau wa sekta hiyo wamekuwa wakikwamisha juhudi hizo kwa kutowajibika ipasavyo katika nafasi zao. [182]
wanachuma
Lakini wakati huu wengine wanachuma hivi hivi. [183]
wanene
Au milolongo ya wakereketwa wa nafasi ya utawala wanaoamua kugombea nafasi ndani ya chama cha wanene huku hawajulikani kabisa. [184]
wapi
Utadhani bingo! Lakini wapi! Maisha yamekuwa lotto na Mungu mkubwa siku yangu itakuwapo. [185]
wapo
Alisema kuwa wilaya ya Iramba wamejitokeza waombaji 30 ambao kati yao wapo wanawake tisa na waombaji wote ni walimu kutoka shule za msingi na sekondari. [186]
wasiwe
Aliongeza kuwa serikali inadhibiti ulinzi na usalama wa nchi na kwamba wananchi wasiwe na wasiwasi juu ya usalama wa nchi yao. [187]
wengine
Hatuoni sababu ya baadhi ya wanafunzi kurejeshwa na wengine kukataliwa. [188]
wenzangu
Waishiwa wenzangu. [189]
wetu
Makamu wa Rais wa Emirates anayeshughulikia Afrika, Asia Magharibi na India, Salem Obaidalla, alisema: "Gofu imekuwa mtindo wa maisha unaopendendwa na abiria wetu wengi. [190]
wewe
Kwa kumtengea chai mumeo kama ni wadizaini hii utaonyesha mapenzi makubwa na wewe pia kupata nafasi ya kuzungumza naye mipango yenu ya baadaye kama si kupenyeza zako hoja. [191]
wezi
Tuliweka mtego eneo hili kwa vile tunajua kuwa kila siku wezi wanapoiba, hukipitia eneo hili kukwepa kizuizi cha polisi. [192]
wiki
Najisikia kama nitacheza vizuri sana zaidi ya nilivyocheza wiki hii. [193]
ya
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwa niaba ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, mwenyekiti wa kamati hiyo, Omary Kwaang’ alisema serikali inatakiwa iwe makini katika suala hilo la kurejesha wanafunzi hao chuoni. [194]
yako
Andaa chai yako kwa umakini, chai shurti iandaliwe ikiwa na kila kikorombwezo kumpumbaza. [195]
yana
ASKARI wa Kikosi cha Usalama Barabarani wameyazuia mabasi matano kutoka katika Kituo Kikuuu ya Mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo (UBT), jijini Dar es Salaam kusafiri baada ya kubainika kwamba, yana hitilafu mbalimbali. [196]
yangu
Akizungumzia mchezo huo, Phiri alisema: "Timu yangu imecheza vizuri, wachezaji wamebadilika katika kipindi kifupi na nataraji mabadiliko zaidi ya uwanjani. [197]
yao
Katika hatua nyingine Prof Mbwette alisema baadhi ya walimu wa nje ambao hawajalipwa malimbikizo ya malipo yao, wamegoma kutoa matokeo ya mitihani ya wanafunzi kadhaa wa chuo hicho. [198]
ziara
Onyo hilo lilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mwambungu katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu, ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, katika shule za sekondari za kata za Manispaa ya Morogoro. [199]
zile
Afghanistan ni eneo linaloelezwa kuwa ni makutano ya nchi za Mashariki na zile za Magharibi, eneo maalum la kuanzia mapambano dhidi ya mataifa yasiyotabirika kama Iran, Iraq, Pakistan, India, China na mengineyo. [200]