Nenda kwa yaliyomo

fasihi

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru

aina za fasihi

[hariri]
  1. fasihi simulizi
  2. fasihi andishi

fasihi simulizi

[hariri]

fasihi simulizi ni kazi ya sanaa iliyohifadhiwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo(ni sanaa ya kimapokezi) kama vile hadithi, ngano, maigizo na vitendawili. Fasihi simulizi hutumia ishara ili kupitusha ujumbe kwa wanajamii. Fasihi simulizi uhusisha fanani(mtendaji), utendaji na hadhira.

maigizo au sanaa za maonyesho au michezo

[hariri]
Aina ya neno
[hariri]

Nomino

Umoja
[hariri]

Igizo

Wingi
[hariri]

Maigizo

Ngeli
[hariri]

i-zi(kamusi teule ya kiswahili) li-ya(kamusi ya kuswahili sanifu)

Maana
[hariri]

Tendo la kufanya afanyavyo mwengine. Kuiga maneno au matendo au yote. Maigizo hushirikisha michezo ya kuigiza na maonyesho au maonesho ambayo huigizwa kimyakimya au kwa kusimulia mambo fulani yanayomhusu binadamu. Lengo moja huwa ni kuonesha utamaduni wa jamii fulani. Huweza kutokea mahali popote , wakati wowote bila uwepo na maandalizi ya mapema.

Michezo huweza kuwasilishwa kupitia ushairi wa utendaji wa mambo ya kijamii inayohusisha utumiaji wa viungo vya mwili na maneno kuwasilisha habari.

Maigizo huwa na umbo la tamthilia.

Maneno au/na matendo ya binadamu hutokea kwa wingi katika maigizo na hupewa umuhimu mkubwa.

fasihi andishi

[hariri]

fasihi andishi ni kazi ya sanaa katika maandishi kama vile riwaya na tamthilia.

chanzo cha neno

[hariri]

Kiarabu

aina ya neno

[hariri]
  1. kivumishi
  2. nomino

maana kama kivumishi

[hariri]

-enye lugha safi;-enye kutumia lugha safi na nzuri

Nomino

[hariri]

ngeli

[hariri]

i-zi

maana

[hariri]
  1. funzo la ujuzi wa lugha
  2. somo au funzo au taaluma inayohusu tungo za sanaa au kisanaa kama vile ushairi, riwaya, tamthilia, tenzi, semi, vitendawili, hadithi, ngano, khurafa, maigizo, majigambo, vitanza ndimi, misemo, methali, riwaya na kadhalika.

Tafsiri

[hariri]