Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-15

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
acha
We mwishiwa supu acha roho mbaya. [2]
aende
Kila mwishiwa aende kujiandaa kuonyesha kipaji chake siku ile na mshindi atapewa nafasi ya kujaribu kipaji chake kwenye kituo cha runinga. [3]
aina
Kwa sababu hiyo, serikali iligawanya aina ya mikopo kutoka asilimia 100, 80, 60 na 40 na fomu maalumu za kuombea mkopo, ndiyo zitakazowapa picha halisi bodi, kutambua kiwango cha mkopo anachopaswa kupewa mwanafunzi husika. [4]
ajira
Alisema wizara hiyo pia inapaswa kuongeza ajira kwa maafisa michezo katika ngazi mbalimbali kuanzia ngazi za wilaya na mikoa ili kuweza kukuza michezo hususan riadha. [5]
akawa
Tena kichekesho ni kwamba kila mwishiwa akawa amebeba bahasha lililotuna. [6]
albino
Nyumbani kwake hapo alikuwa akiishi na watu kadhaa akiwemo jamaa mmoja ambaye ni mwenye ulemavu wa ngono yaani albino. [7]
ama
Mathalani yeye mumeo hana kawaida hiyo ya kurudi jioni nyumbani ama kwa necha ya kazi yake basi hulazimika kuwepo kazini muda huu wa jioni, bado unaweza kuutumia muda wa usiku baada ya chakula cha jioni. [8]
ambao
Alisema, bila kupunguza nauli za usafiri wa abiria watu wa kawaida ambao baraza linawawakilisha hawatapata faida ya punguzo hilo la mafuta. [9]
ambapo
Taarifa hiyo ya Ikulu inaonyesha ziara hiyo ya rais itasitishwa kwa muda na kuendelea tena Februari 9, ambapo Rais Kikwete atakutana na viongozi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) pamoja na Bodi ya Biashara ya Nje (BET). [10]
ambayo
Kampeni hizo zinazoendelea kati ya CCM na Chama Cha Wananchi (CUF) zinatarajiwa kumalizika Januari 25, mwaka huu, ambayo ni siku ya kupiga kura. [11]
ana
Anasema ana nyama nyingi na ni mzito kuliko kuku wa kawaida. [12]
anasema
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Taffa, Otieno Igogo anasema moja ya sababu za msongamano bandarini ni ukiritimba unaofanywa na Kampunii ya Kupakua na Kupakia Mizigo Bandarini (TICTS). [13]
atakutana
Katika ziara yake Rais Kikwete leo atakutana na uongozi wa Bandari ya Dar es Salaam na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL). [14]
au
Gire alirudishwa rumande jana majira ya saa 7:00 mchana baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana, yaliyomtaka awe na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya Sh100 milioni au mali isiyohamishika yenye thamani inayolingana na kiasi hicho cha pesa kila mmoja. [15]
bado
Kesi hiyo iliahirishwa baada ya Wakili wa Serikali, Oswald Tibabyekomya, kudai mahakamani hapo kuwa upelelezi bado haujakamilika. [16]
baina
Mathalan, tukio la hivi karibuni wilayani Kilosa lilishuhudia watu saba wakipoteza maisha baada ya kutokea mapigano baina ya wakulima na wafugaji katika Kijiji cha Kikenge Kata ya Mabwegele. [17]
bali
Aliongeza kuwa kama hakuna mchakato wa haki kama huo, basi kesi nyingi zinazofikishwa mahakamani huwa si za lazima bali hufunguliwa kwa shinikizo na maslahi ya wakubwa wa polisi tu na kwamba, hii ni kutokana na kutokuwepo na chombo cha kuthibitisha uhalali wa kesi hizo. [18]
bara
Afrika ni bara lililoshindwa kutumia njia za kisasa katika uzalishaji wa chakula hali iliyoifanya hekari moja ya ardhi huzalisha kilo 300 mpaka 500 tu za chakula hii ni tofauti na nchi nyingi duniani. [19]
chama
Katika mikutano iliyopangiliwa kwa kuanza kuhutubiwa na wagombea wa CCM walioshindwa katika kura za maoni za chama hicho, kila aliyesimama na kuzungumza na wananchi isipokuwa Tambwe Hiza, alizungumza Kisafwa. [20]
chochote
Kumbe yeyote aliyepeleka chochote kwa waamuzi alienguliwa kwenye shindano moja kwa moja. [21]
darasa
Lakini kuzuia ununuzi wa gari hilo kunafuatia upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa ambapo inasemekana asilimia 58.8 ya wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka jana watakosa nafasi za kuanza kidato cha kwanza kutokana na upungufu wa madarasa. [22]
dhidi
Polisi Morogoro katika mechi yake ya kwanza ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ilibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Kagera Sugar mchezo ulipigwa wiki iliyopita katika dimba la Jamhuri mjini Morogoro. [23]
don
Suti hilo! Yaani suruali ilikuwa mfano wa ‘don’t touch’ na tai ilikuwa inajikunja kutokana na kutumika miaka si chini ya ishirini. [24]
duni
Kwa hiyo tukiwa wadau muhimu wa elimu tunona kwamba, wanafunzi hao dhaifu ambao hufundishwa katika mazingira duni na walimu wasio na uwezo, ndiyo sababu za msingi za kushuka kwa ufaulu, hivyo tatizo hilo litafutiwe ufumbuzi. [25]
es
Masharti mengine ya dhamana ni kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha mahakama na kuripoti polisi mara moja kwa mwezi. [26]
gani
Hivi, ni nani kati yenu, anayeweza kuruhusu rafiki yake wa karibu akamatwe, hata kama amekosea?, na ni Kiongozi gani katika awamu zote tatu zilizopita aliyeweza kuwa jasiri akaruhusu marafiki na viongozi wenzake wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya dola kama si Rais Kikwete"aliwauliza wananchi Dk. [27]
haina
Serikali iliutangaza mpango huo kwa maelezo kuwa haina uwezo wa kuwapatia mkopo wanafunzi wote wa elimu ya juu na hasa ikizingatiwa kuwa idadi yao imeongezeka maradufu, kutokana na ongezeko la vyuo vya elimu ya juu nchini. [28]
hana
MBUNGE wa Jimbo la Kyela Dk Harrison Mwakyembe,amesema hana mpango na wala hafikirii kukiacha Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kujiunga vyama vya upinzani nchini. [29]
hao
Katika shitaka la nne Gire anadaiwa kuwa mwezi Juni mwaka 2006, alitoa taarifa za uongo kwa wajumbe wa Timu ya Majadiliano ya Serikali kwamba, Richmond ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme ili wajumbe hao waweze kuipendekeza. [30]
hapa
Mshitakiwa huyo anadaiwa kuwa Machi 13, 2006 akiwa jijini Dar es Salaam, alighushi nyaraka akionyesha kwamba, Mohamed Gire ambaye ni mwenyekiti wa Richmond Development Company LLC ya Texas nchini Marekani, alisaini kumruhusu kufanya shughuli za kampuni hiyo hapa nchini. [31]
hasa
Nawaombeni wazee wangu msiniangushe hasa nyie baba zangu machifu. [32]
hata
Mwaigaga alitumia mbinu mbali mbali hata kutoa historia ya baba yake mzazi kuwa, alipohamia katika kijiji hicho, alipokelewa na kati ya mmoja wa machifu waliokuwepo hapo kwenye mkutano huo, na kwamba kutokana na hali hiyo ni vema wakampigia kura mgombea wa CCM ili aweze kuwa Mbunge wa jimbo hilo. [33]
hatua
Wito huo umetolewa wakati Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini imeiomba serikali kuwa makini na suala la mafuta, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua za kisheria wafanyabiashara wa mafuta kwa sababu wanaweza kuyumbisha uchumi wa taifa. [34]
hawa
Viongozi hawa wa elimu wanataka kuficha ukweli kwamba, kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kumefungamana moja kwa moja na udhaifu katika maboresho ya elimu nchini. [35]
hayo
Wakili wa Serikali, Oswald Tibabyekomya alieleza hayo jana mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Euphamia Mingi. [36]
heka
Shirika la Utafiti wa Kilimo Kenya (Kari) ikishirikiana IAEA na FAO imeanzisha mbegu mpya ya ngano inayoitwa Njoro-BW1, mbegu hii ina uwezo wa kuvumilia ukame na kuzalisha mpaka magunia 20 kwa kila heka moja. [37]
hii
Waambieni vijana wenu waache tabia ya kumuiga Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof Ibrahimu Lipumba, kwani hajui nchi hii ilikotoka. [38]
hili
Mwenyekiti wa kamati hiyo, William Shelukindo aliliambia gazeti hili jana kuwa, wafanyabiashara hao ni wajanja na wanatakiwa kufuatiliwa kwa karibu ili kuwadhibiti kabla hawajayumbisha uchumi. [39]
hilo
Wadau hao wametoa ombi hilo kufutia kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na la ndani. [40]
hivi
Hata hivyo aliongeza kwamba, Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) pia inapaswa kuzingatia muda mwafaka wa kutoa bei elekezi na kwamba, hivi sasa wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria hivyo wanapaswa kwenda na wakati. [41]
hizi
Huu ni mfumo wa kidunia, ili kulinda haki za raia, kwani kuchanganya majukumu ya mamlaka hizi mbili ni matumizi mabaya ya madaraka," alisema Masoud huku akitaja nchi mbali mbali zinazotumia mfumo huo. [42]
hospitali
Alihangahaika kwenye hospitali nyingi bila mafanikio. [43]
hujui
Utamaduni huu shostito ni wa pwani, kama ulikuwa hujui chukua hiyo, Na ukweli ni kwamba wanawake wengi wa pwani wanajua maana ya chai ya jioni na ndiyo maana wanasifiwa kuwa wanayajua mambo. [44]
huko
Hili suala la mradi wa Kigamboni nitalitolea ufafanuzi katika kikao kijacho cha Bunge, huko nitafafanua masuala yote yanayotarajiwa kuwekwa katika mji huo mpya ikiwemo huduma za miundombinu kama usafiri wa treni," alisema Chiligati. [45]
humo
Mwenyekiti huyo alitaja mikakati mingine ya kupata fedha za dharura kuwa ni kusimamisha ujenzi wa awamu ya pili ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri,kuchukua fedha za faini za mifugo wanazotozwa wafugaji walioingiza mifugo wilayani humo, fedha kutoka mfuko wa elimu na kukusanya michango ya elimu kutoka kwa wananchi ambao hawakutoa. [46]
huna
Pumbavu kabisa, huna maana wewe, sasa ni lazima ufe, mwenye siri za dawa ni huyo albino uliyemuua, mbwa kabisa wewe,” alifoka waziri kwa hasira kisha kupiga simu kwa mkuu wa jeshi la polisi ili kumkata Kazim kwa kitendo chake. [47]
huo
Wakati huo huo, upelelezi wa kesi ya wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania inayowakabili, Johnson Lukaza na Mwesiga Lukaza umekamilika. [48]
hutumia
Ni asilimia kumi na moja tu ya mchele unaozalishwa Afrika ndiyo hutumia umwagiliaji wakati kwingineko duniani ni asilimia 53 ya uzalishaji hutumia umwagiliaji. [49]
huu
Hata hivyo Hakimu Mingi aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 27 mwaka huu washitakiwa watakaposomewa maelezo ya awali. [50]
huyu
Nasikia unamjua, ni huyu hapa angalia vizuri picha, kama unajua anapatikana wapi, nitaagiza hata magari mengine yamsake maeneo hayo, nitaomba hata jamaa yangu mmoja usalama wa taifa mstaafu mwenye uwezo mkubwa katika masuala ya kupeleleza atusaidie kumpata,” alisema waziri. [51]
ikawa
Inaweza hiyo ikawa sababu, lakini si kubwa kiasi hicho. [52]
ila
Mzee tumekuja, hali ya biashara ni mbaya sana, yaani kila kukicha ni mikosi tupu hata hatujui tufanye nini, ila tunasikia kuna mtindo umezuka siku hizi watu wanaua albino, viungo vyao vinaweza kutusaidia kupata fedha tutakapokwenda kwa mganga wa jadi” alisema na kupingwa vikali na Kazim. [53]
ile
Anasema kuwa mijadala inayotarajiwa kuanza hivi karibuni ya kufanyia mageuzi uchumi wa dunia, kama ile itakayofanyika chini ya mikutano ya nchi 20 zenye uchumi mkubwa duniani (G20), ni lazima izungumzie kwa mapana suala la mfumo wa kodi duniani. [54]
ili
Inadaiwa kuwa mshitakiwa huyo alitoa taarifa hizo, ili wajumbe wa bodi hiyo waweze kuipendekeza Kampuni ya Richmond kufanya kazi hiyo. [55]
imeshindwa
TICTS inatakiwa iwe na mshindani kwani imeshindwa kutekeleza majukumu yake na ndiyo chanzo cha mrundikano wa makontena bandarini," anasema Igogo. [56]
inaonyesha
Ratiba ya ziara hiyo inaonyesha kuwa Januari 19, Rais Kikwete atakutana na viongozi wa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA), Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Wizara ya Fedha na Uchumi pamoja na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG). [57]
ingawa
Hii inaweza kuwa siri ya mafanikio ya wanawake wengi ingawa si wanawake wote wanajua hili. [58]
iwe
Matatizo hayo si tu kuwa yanawakwamisha wakulima, bali pia juhudi za serikali za kufufua kilimo chenye tija katika kukuza uchumi wa taifa, hivyo tunaomba juhudi zifanyike kuboresha huduma hiyo ya bandari na iwe kwa mazao mengine ambayo tunaamini yanakumbana na tatizo hilo. [59]
juu
Taarifa hiyo iliyoandaliwa na kuwasilishwa kwa wadau na Timu ya Wataalamu kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ilieleza kuwa kitendo cha DPP kuwa na mamlaka ya mwisho juu ya mashtaka kwa mtu yeyote hudhoofisha nguvu ya Takukuru kupambana na rushwa. [60]
juzi
Gire alipandishwa kizimbani juzi mbele ya Hakimu Mkazi Wariyalwande Lema wa Mahakama ya Kisutu na kusomewa mashitaka matano. [61]
kahawa
Kwa mfano, juzi wadau wa zao la kahawa nchini walilalamikia ucheleweshaji wa kusafirisha zao hilo kwenda nje katika bandari ya Dar es Salaam na hatimaye kuwasababishia hasara kubwa. [62]
kali
Mwanza alifumania nyavu kwa shuti kali baada ya ngome ya Simba kujichanganya. [63]
kama
Alisema kama hatua hizo hazitachukuliwa haraka, kampuni hizo zinaweza kuyumbisha uchumi wa nchi na kusisitiza kwamba, hawatakubali kuona wafanyabiashara wanaichezea serikali. [64]
kamili
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Simba, Patrick Phiri amesema anasubiri wachezaji wake walioko kwenye timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ili kutengeneza kikosi kamili kabla ya kuanza mikiki ya Ligi Kuu. [65]
kansa
Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [66]
karibuni
Taarifa za karibuni zinaonyesha kuwa ni wanafunzi wachache walioweza kutimiza masharti ya kurejea tena Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA). [67]
kata
BARAZA la Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro limzuia ununuzi wa gari la Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo ili fedha zilizotakiwa kutumika zifanye kazi ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari za kata. [68]
kibao
Nakufa, mkuu wa polisi unaniua, sawa mimi nimemuua albino, lakini wewe unaniua mimi kwa kunipiga kibao, imeandika wapi kwamba muharifu apigwe, kabla ya kufikishwa mahakamani,” alisema Kazim huku akikata roho. [69]
kikao
Siku hiyo hiyo Rais Kikwete atakutana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA) na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ambapo Februari 12, atafanya kikao na Wizara ya Elimu, Mafunzo na Ufundi, Baraza la Mitihani, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Umoja wa Serikali za Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (Tahliso) na viongozi wa vyuo vikuu vya umma nchini. [70]
kile
Taarifa za kuhojiwa kwa bodi hiyo ni faraja kwa wanafunzi wengi wa vyuo vya elimu ya juu nchini, kwa sababu wabunge hao wanaweza kuwa watetezi wa kile wanachoamini kuwa serikali haiwatendei haki. [71]
kimoja
Anapenda, muwekee na kibiskuti kimoja cha tangawizi pembeni. [72]
kina
Wanasema kuna wakati meli hulazimika kukaa bandarini kutokana na kina cha maji kuwa chini, hali ambayo hulazimu meli kusubiri kina kipande ndipo iondoke. [73]
kisasi
BONDIA Francis Miyeyusho amesema atalipiza kisasi kwa mpinzani wake, Mbwana Matumla katika pambano la kuwania ubingwa wa juu wa dunia wa raundi 12 litakalofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee keshokutwa. [74]
kubuni
Bissio anasema moja ya hatua zinazofaa zaidi kwa serikali za nchi za Afrika ili kuharakisha maendeleo ni kubuni hatua madhubuti za kutekeleza haki za binadamu, hususan zile zenye mwelekeo wa kiuchumi na kijamii. [75]
kubwa
Wanaweza kukuambia kuwa wamefanya kazi kubwa na wamekamilisha upelelezi wao, lakini ukiangalia hakuna ushahidi wa kutosha kumfikisha mtu mahakamani. [76]
kuchi
Lakini katika kundi la kuku hao wanaoitwa wa kienyeji, kuna aina ya kuku waitwao kuchi kama anavyosimulia mfanyabiashara wa mifugo hiyo kutoka Buguruni jijini Dar es Salaam, Khamis Omar (Jeki). [77]
kudumisha
Awali, Masoud alisema hatua ya kutenganisha shughuli za upelelezi na uendeshaji mashtaka ni moja ya hatua kubwa zilizochukuliwa hapa nchini kudumisha haki. [78]
kufa
Wakati wanaendelea kuangalia ile picha aliingia daktari aliyekuwa akimwangalia Kazim na kumwomba waziri afupishe mazungumzo, badala yake wamsake yule mvumbuzi wa dawa kwani isingepita saa 12 kabla ya Kazim kufa ikiwa hatapata ile dawa. [79]
kufika
Nampongeza Mussa Hassan Mgosi kwa kufika na kucheza, hii ndiyo inayotakiwa kwa mchezaji, naamini wachezaji wengine wataiga mfano huu. [80]
kufikia
Akizungumza jijini jana, Meneja wa Bia ya Safari, Fimbo Butallah alisema wameamua kudhamini mashindano hayo kwa nia ya kuendeleza na kukuza mchezo huo kufikia katika ngazi za juu zaidi. [81]
kufuata
Alisema taasisi hizo zitapitishwa upya na baraza la chuo na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali kwa kufuata sheria zinazokiongoza chuo hicho. [82]
kuimba
Kweli wanaweza kuingia hivihivi? Kweli wataingia kama milolongo ya vijana wanaotafuta nafasi moja ya Ustaa wakati ambapo hata wenzao wa mitaani wanawacheka wakijaribu kuimba. [83]
kuja
Nafurahi kuwatangazia kwamba nimeongea na wahusika wakuu na wamekubali kuja hapa kuwa waamuzi. [84]
kujua
MAPEMA mwaka jana, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ililiambia Bunge ilivyosikitishwa na kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa wanafunzi na kwamba, ilikuwa inafanya utafiti kujua sababu zake. [85]
kukaa
Umoja wa Wazalishaji wa Kahawa nchini (TCA) umedai kwamba, kutokana na ucheleweshaji huo, katika kila magunia 300 ya kahawa, 100 hupotea kwa kuoza kutokana na kukaa muda mrefu ndani ya kontena yakisubiri kusafirishwa. [86]
kuku
KWA kawaida watu wengi wamezoea kusikia au kujua aina mbili tu za kuku. [87]
kule
Ndio ndugu, mimi naitwa Kazim ni mwenye mgodi wa madini ya almasi kule Mwadui, tatizo ni kwamba hali kwa sasa imekuwa mbaya mno, nimechanganyikiwa hapa hata sijui la kufanya,” alisema akiomba ushauri. [88]
kumbe
Zaidi ya yote kumbe alikuwa amechukua mkopo benki baada ya biashara zake kumchanganyia, ili kuboresha zaidi, akiamini kuwa kwa namna alivyokuwa akipata fedha angeweza kulipa deni ndani ya muda mfupi. [89]
kumi
Ni wastani wa kilo kumi na moja tu kwa kila heka moja tofauti na wastani wa dunia wa kilo 62 kwa kila heka. [90]
kumuua
Yalitokea mabishano na mkulima huyo kumuua mfugaji kwa bunduki. [91]
kuonana
Wapi waamuzi, wapi waamuzi! Unajua ni vizuri kuonana nao kwanza. [92]
kupitia
Pia wanadaiwa kujipatia kiasi hicho cha fedha kupitia kampuni ya Kernel Ltd ya Tanzania, baada ya kudanganya kuwa kampuni hiyo imerithishwa deni na Kampuni ya Marubeni Corporation ya nchini Japan. [93]
kutibu
Mimi sijasomea wa kuhudhuria semina yoyote kuhusu ufugaji natumia uzoefu tu lakini watu mbalimbali wanakuja kwangu kutaka ushauri wa kiufundi hususan katika matumizi ya dawa za kienyeji kutibu kuku," anasifu Omar. [94]
kutoka
Jeetu Patel na wenzake, Amit Nandy na Devendra Patel wanadaiwa kuwa mwaka 2005 waliiba Sh10,562,922,828.60 kutoka BoT, kupitia Kampuni ya Bencon International Ltd baada ya kudanganya kuwa wamerithishwa deni na Kampuni ya Marubeni Corporation. [95]
kutoza
Meneja Mawasiliano wa TPA, Franklin Mziray anasema: "TPA haijakurupuka tu kutoza gharama hizo, ilifuata taratibu zote za kisheria zinazotakiwa, na lengo siyo kukusanya mapato bali kutoa adhabu kwa wateja wanaofanya bandari sehemu ya kuhifadhia mizigo baada ya muda wanaotakiwa kuiondoa kufika. [96]
kwani
Frola Mwalyambi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumza katika mkutano huo na baadaye kuwaomba wananchi wa kijiji hicho, kumpigia kura Mchungaji Luckson Mwanjali kwani ni mtoto wao na kwamba anastahili kuwa mbunge wa jimbo hilo. [97]
kwao
Akizungumzia kuhusu Serikali ya Wanafunzi wa UDSM (Daruso), Profesa Maboko alisema taasisi zote za wanafunzi zilizokuwa zikitambuliwa na sheria ya chuo ya mwaka 2007, kabla ya kusimamishwa kwao, hazitatambuliwa tena. [98]
kwenye
Kana kwamba wananchi hao hawajui Kiswahili, utaratibu huo wa kutumia lugha la Kisafwa ulitumika pia na wanachama wengine wa CCM walioshindwa kwenye kura za maoni, ambao jana walipata nafasi kumnadi Mwanjali akiwamo Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Robert Mboma. [99]
la
Pia anadaiwa kuwa Machi 20 mwaka 2006 katika eneo la Ubungo umeme, alitoa hati za uongo ambazo zilionyesha kwamba, Mohamed Gire amezisaini kumuidhinisha yeye kufanya shughuli za kampuni hiyo nchini. [100]
leo
Kesi hiyo itaendelea leo katika mahakama hiyo. [101]
licha
Naye kocha wa Zesco, Fington Simukhonda, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia, KK Eleven alisema kuwa wachezaji wake wamecheza vizuri, licha ya kuwa wamechoka kwa safari ndefu ya kutoka Zambia. [102]
lita
Kwa mujibu wa bei hizo petroli inatakiwa kuuzwa kwa kati ya Sh1,171 na Sh 1,233 kwa lita na diseli itauzwa kwa Sh1,301 na 1,390 kwa lita katika Mkoa wa Dar es salaam. [103]
mada
Wakichangia mada iliyowasilishwa na Bodi ya Ukaguzi wa filamu nchini katika semina ya mafunzo kwa wabunge wa kamati ya maendeleo ya jamii, baadhi ya wabunge walisema sheria hiyo haina meno ya kufanya kazi. [104]
madini
Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [105]
maeneo
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati kwa Kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Mazingira iliyokuwa katika ziara ya kutembelea miradi ya Shirika la Nyumba (NHC) zilizoko maeneo ya Mbweni J.K.T, New Bagamoyo Road na Boko, jijini Dar es salaam. [106]
majengo
Tatizo hilo, limekuja baada ya Ofisa elimu mkoa kuzuia majina ya baadhi ya wanafunzi waliofaulu hakitaka baadhi ya kata zisizomalizia majengo ya shule za sekondari kukamilisha ili majina hayo yatangazwe jambo ambalo wananchi wanamlalamikia. [107]
makubwa
Mratibu wa Social Watch, Roberto Bissio anatabiri kuwa mgogoro wa fedha ulioiandama dunia na ubepari wa mataifa makubwa dhidi ya maskini mwaka 2008 utazidisha umaskini. [108]
mapato
Unajua jinsi serikali ya Tanzania inavyotufanyia siyo vizuri kwa sababu inaangalia upande wa kupata mapato tu lakini haitujali wafanyabiashara. [109]
mayai
Wale wa kienyeji na wa kisasa ambao wako wa nyama na wa mayai. [110]
mazao
Usafirishaji wa mazao bandarini uboreshwe WAKATI serikali inakazana kuboresha kilimo nchini, baadhi ya wadau wa sekta hiyo wamekuwa wakikwamisha juhudi hizo kwa kutowajibika ipasavyo katika nafasi zao. [111]
mbegu
Alitaja mambo matano yatakayopewa kipaumbele ikiwemo mbegu bora za kilimo, maafisa ugani, matumizi ya mbolea, kilimo cha umwagiliaji na upanuzi wa soko la mazao ya wakulima. [112]
mchele
Mbegu ya nerica ina uwezo wa kuzalisha mchele kwa asilimia 50 zaidi ya mbegu za kawaida, tena bila ya kutumia kilimo cha umwagiliaji pia huvunwa mwezi mmoja mapema ukilinganisha na mbegu nyingine. [113]
mfululizo
Mgosi aliyeingia kipindi cha pili pamoja na Orji Obina kuchukua nafasi za Mohamed Kijuso na Mohaed Banka walibadilisha sura ya mchezo huku wakishambulia mfululizo. [114]
mifuko
Badala ya kukaa na kufurahia kutoboka kwa mifuko na kupasuka kwa suruali yenye mifuko, kila mara wanatafuta kazi zingine za kufanya. [115]
mikoa
Katika hatua nyingine Ngao ametoa mwito kwa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kuajiri wanariadha wastaafu waliopata kutamba kitaifa na kimataifa kufundisha mchezo huo katika mikoa mbalimbali nchini ili kuweza kuukuza mchezo huo. [116]
mikopo
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Omar Kwaangw' alithibitisha jana jijini Dar es Salaam kuwa kamati hiyo tayari imeuita uongozi wa bodi ya mikopo, ili kutoa maelezo mbele ya wajumbe wa kamati. [117]
mimi
Ni kweli ninafanya kazi, lakini si yangu, utajiri wangu umepungua, nilikuwa nataka kununuaq ndege binafsi ya kutembelea, kwa hali ya kipato changu cha sasa, sina uwezo wa kufanya hivyo, mbaya zaidi tayari nilishatamba kwa watu kwamba nitanunua ndege, nisipomnunua wataniona mimi ni maskini” alijisemea. [118]
mji
SERIKALI imesema inatarajia kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu mradi wa Kigamboni katika kikao kijacho cha Bunge ili kila Mtanzania ajue mipango endelevu iliyowekwa kuboresha mji huo. [119]
mjini
Akizungumza katika kikao cha Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika juzi mjini Ifakara, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Hassan Goagoa, alisema ni aibu kwa wilaya hiyo kufaulisha wanafunzi 7,462 na kati yao wanafunzi 3064 tu ndiyo waliopata nafasi wakati wanafunzi 4,398 wanakosa nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa. [120]
mkopo
Kulingana na sera hiyo ya uchangiaji, serikali ilitangaza kuwa mkopo utakaoidhinishwa kwa mwanafunzi utategemea uwezo wa kipato wa familia anayotoka. [121]
mkuu
KOCHA mkuu wa Polisi Morogoro, John Semkoko amesema wanatakiwa kushinda mechi sita mfululizo za Ligi Kuu Bara ili kupata uhakika wa kuepuka kuwa miongoni mwa timu tatu zitakazoshuka daraja msimu huu. [122]
mno
Fikiria ujasiri unaofanywa na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete , ni mkubwa mno, lakini wapo watu wanaobeza jambo ambalo hata CCM ingefanya nini, wapo watu ambao wataendelea kubeza tuu. [123]
moto
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, mauaji hayo yalianza baada ya mkulima mmoja kuchoma moto shamba lake kwa maandalizi ya kilimo, lakini wafugaji wa jamii ya Kimasai wakadai kuwa anaharibu chakula cha mifugo. [124]
mpaka
Mwenyekiti wa Mtibwa Sugar, Ally Mhina alisema mpaka sasa shughuli ya kuwaingizia wachezaji pesa zao kwenye akaunti zao zinaendelea na wachezaji walianza kuchukua pesa zao kuanzia jana. [125]
mrefu
Bandari ya Dar es Salaam imekuwa katika matatizo ya kiutendaji kwa muda mrefu, hali iliyosababisha mrundikano wa makontena huku mkataba wa Wakala wa Upakuaji mizigo kampuni ya TICTS na serikali ukiwa katika matatizo. [126]
msaidizi
Jamaa huyo ambaye alikuwa kama msaidizi wake wa karibu, alikuwa akimuwakilisha katika kazi mbalimbali na ndiye aliyekuwa ana siri zake nyingi. [127]
mshindani
Igogo anasema kampuni hiyo inahitaji kupatiwa mshindani kibiashara hatua ambayo anaamini kuwa itapunguza ukiritimba katika bandari hiyo na kuleta ufanisi. [128]
muhimu
Leo Rais Kikwete anaanza awamu ya pili ya mikutano muhimu na wizara mbalimbali kufuatilia utendaji wa wizara hizo, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, pamoja na maagizo aliyoyatoa kwa wizara hizo wakati anaingia madarakani," imesema sehemu ya taarifa hiyo. [129]
mumewe
Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [130]
mwa
Akichangia mjadala wa taarifa hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Dar es Salaaam(DICC), mwishoni mwa juma, alisema ili kulinda haki za raia ni vema kutenganisha majukumu ya taasisi za uchunguzi na idara ya mashtaka. [131]
mwishiwa
Si kila mtu anaweza kuchekesha? Kwa nini tusifanye na sisi?’ ‘Kweli kabisa mwishiwa Supu. [132]
na
MFANYABIASHARA Naeem Adam Gire, ambaye anakabiliwa na tuhuma za kughushi na kutoa taarifa za uongo kwamba kampuni ya Richmond ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme nchini, amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. [133]
namba
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameicharukia Sheria namba 4 ya filamu na michezo ya kuigiza ya mwaka 1976 kuwa imepitwa na wakati na kwamba itaipeleka nchi pabaya ikiwa haitafanyiwa marekebisho haraka iwezekanavyo. [134]
nao
Alisema leo (jana) tumepeleka mapendekezo yetu Sumatra kurekebisha gharama za usafiri ili watu wa kawaida nao wapate matunda ya punguzo la bei ya mafuta," alisema Ngewe. [135]
naye
Kwa kumtengea chai mumeo kama ni wadizaini hii utaonyesha mapenzi makubwa na wewe pia kupata nafasi ya kuzungumza naye mipango yenu ya baadaye kama si kupenyeza zako hoja. [136]
ndizo
Uchunguzi uliofanywa na vyombo vya habari kwa muda mrefu na ambao unaendelea kufanywa kila siku kwa kufika shuleni kushuhudia hali halisi, unaonyesha shule nyingi hasa zilizoanzishwa kisiasa chini ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) yaani sekondari za kata, ndizo zinaongoza kwa matokeo mabaya. [137]
ngumi
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Rais wa wa Chama cha ngumi za kulipwa (PST) Emmanuel Mlundwa alisema mabondia hao wanatarajia kupambana kutafuta mshindi atakayecheza pambano la ubingwa wa dunia la Intenational Circuit Boxing. [138]
nia
Alisema Serikali haina nia ya kuwahamisha wakazi wa Kigamboni ndiyo maana imeshawaandaa wataalam kufanya tathmini kati ya mtu na mtu kwa lengo la kuhakikisha kila mtu ananufaika na eneo lake kimaslai. [139]
njama
Lakini hizi ni njama za waziwazi za wafanyabiashara wa baadhi ya vituo vya mafuta za kuikwamisha serikali kudhibiti upandaji holela wa bei ya nishati hiyo, kwa lengo la kutaka kujinufaisha wao wenyewe. [140]
nzuri
Hata hivyo, pamoja na kusifia mafanikio mbalimbali yaliyoletwa na Serikali ya awamu ya nne, Dk Mwakyembe alizungumzia pia kazi nzuri iliyofanywa na Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ambaye alisema aliimarisha na kuinua Uchumi wa nchi. [141]
ofisi
Mbali ya ukosefu wa walimu shule hizo zimejengwa chini ya kiwango, hazina majengo yaliyokamilika kwa ajili ya mabweni, ofisi za walimu, maktaba, maabara na madarasa pamoja na vifaa na huduma nyingine muhimu kwa wanafunzi. [142]
pale
Simba inayonolewa na Mzambia, Patrick Phiri, ilishindwa kuonyesha makucha katika kipindi cha kwanza yake huku mabingwa hao wa Zambia wakionyesha kandanda safi na pasi za hapa na pale. [143]
pia
Mshitakiwa huyo pia anadaiwa kutoa taarifa za uongo kwa wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuwa, Kampuni ya Richmond ina uwezo wa kuzalisha megawati 100 za umeme nchini Tanzania. [144]
popote
Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, anasema, taasisi mbalimbali za kimataifa zimekuwa na nia ya kukuza 'haki' za mashirika au makampuni kuwekeza mahali popote pale duniani, na kuzuia kasumba ya nchi nyingi maskini kuweka masharti magumu ya wafanyabiashara wa nje kuwekeza kwenye nchi zao. [145]
rais
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari Ikulu jijini Dar es Salaam jana, katika ziara hiyo rais pia atafuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2005 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). [146]
ripoti
UMASKINI wa kupindukia utaendelea kuiandama Afrika hususan nchi zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kipindi cha miaka mingine 200 kama hakutachukuliwa hatua za kukabiliana na kuongezeka kwake, ripoti mpya kuhusu hali ya maendeleo katika hilo imeleeza. [147]
sana
Hivyo ni hatari sana kuipa taasisi ya uchunguzi mamlaka ya kumshtaki mtu," alisisitiza Masoud. [148]
sawa
Goagoa alisema mikakati hiyo itaenda sawa na agizo la Rais la kutaka wanafunzi wote waliofaulu kuingia madarasani hivyo wilaya inahitaji kufanya juhudi binafsi ili wanafunzi wote waingie kidato cha kwanza. [149]
shida
Umempata?” alidakia Kazim, aliyekuwa akizungumza kwa shida. [150]
si
Katika kukazia hoja yake, Masoud alisema kuna tafiti nyingi zilizofanyika katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Uingereza na kubaini kuwa taa'si'si nyingi za uchunguzi zina kawaida ya kupeleka kesi mahakamani hata ambazo si za lazima. [151]
sifa
Vyombo vya habari vimebaini shule takriban zote za kata nchini, zinakabiliwa na matatizo kadhaa; hazina walimu wenye sifa na waliopo, wengi wao waliajiriwa kisiasa, hivyo wanaingia darasani kama walimu lakini si walimu. [152]
sisi
Tunafurahia kudhamini mashindano haya kwa mara ya kwanza, tumegundua kuwa ni mchezo unaopendwa sana hasa na vijana kwa hiyo tumeona na sisi tutoe mchango wetu katika kukuza na kuendeleza mchezo huu," alisema Butallah. [153]
soka
Polisi Morogoro itashuka ndimbani Jumapili kucheza na timu ya soka ya Simba katika pambano ilitakalo pigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam. [154]
tajiri
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [155]
tatu
Alisema, Rais Kikwete amefanya mambo mengi na yenye ushujaa kwa kuweza kuwafikisha viongozi waandamizi aliowahi kufanya nao kazi katika awamu mbalimbali akiwa Waziri , lakini amefanikisha kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya dola wakituhumiwa kuitia hasara Serikali ya awamu ya tatu kwa kuruhusu msamaha wa kodi ya Sh 11 bilioni. [156]
tena
Wakati huo huo, kesi ya wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) inayomkabili mfanyabiashara maarufu jijini, Jayantkumar Chandubhai Patel (Jeetu Patel) na wenzake imeahirishwa hadi Februari 13, mwaka huu itakapotajwa tena. [157]
tenisi
WACHEZAJI watatu wa mchezo wa tenisi wataiwakilisha Tanzania katika michuano ya tenisi ya vijana ya Afrika itakayofanyika nchini Morocco mapema Aprili. [158]
tu
PCCB ni mamlaka ya uchunguzi tu. [159]
tupu
Nakuambia nani hajui lakini yeye anakunja manoti yake safi wakati sisi tunakaa tunaangalia meza tupu. [160]
ufugaji
Hii ni changamoto kubwa inayotukabili katika ufugaji wa kuku hawa," anasema Jeki. [161]
ujumla
Pia mwenyekiti alizungumzia maendele ya timu kwa kuweza kufanya vizuri kwani wameandaa mikakati mikubwa ambayo wataizungumzia katika kikao cha leo na wanachama wote huku wakizungumzia maendeleo ya timu yao kwa ujumla. [162]
uko
Hata hivyo, hakuna shaka kwamba kama Rais Kikwete hata kuwa mwoga, ni wazi ushindi uko kwake kwa sababu yeye ana kila kitu kwanza, anashikilia dola, ana vyombo vya kumsaidia kuwakamata na kuwashtaki, hivyo kundi hilo la mafisadi litakwama. [163]
ukuaji
Wakati sehemu kubwa ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara imeonyesha kuwa na ukuaji mkubwa wa kiuchumi katika miaka ya karibuni, hii haichangii katika kupunguza viwango vya umaskini. [164]
uliopo
Wadau wa sekta hiyo ya uchukuzi hasa wa bandarini wanasema utekelezaji wa mkakati wa PTA ni mgumu kutokana na urasimu uliopo bandari na makosa ya kawaida ambayo hufanyika wakati wa kupakia au kupakua makontena. [165]
umma
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, leo itaiweka kitimoto Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, kutokana na malalamiko yaliyosababisha migomo ya wanafunzi na kuvifanya vyuo saba vya umma kufungwa. [166]
unaweza
Kwa hiyo wanapoleta ushahidi ni lazima kuangalia kama unaweza kukabiliana na changamoto za mahakama. [167]
upya
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimeweka masharti magumu ya kudhibiti usajili wa wanafunzi waliodahiliwa upya kuingia chuoni hapo kuanzia Januari 19, mwaka huu. [168]
ushuru
Inaeleza kwamba imefuata taratibu zote za kisheria katika kuongeza gharama za ushuru wa kuhifadhi mizigo bandarini hapo na haijalenga kukusanya mapato. [169]
usiku
PTA wanasema wanafanya kazi saa 24 ili kupunguza msongamano wa makontena lakini ukienda kulipa pesa saa sita usiku watapokea? Pia huwezi kusoma chesesi namba za magari madogo usiku, na pia kuna wakati umeme unazimika hata siku nzima na bandari haina jenereta wakati ukizingatia asilimia kubwa ya kazi zinafanywa kwa kompyuta sasa hiyo saa 24 siyo nadharia?" anasema Msanga. [170]
utundu
Lakini bado nafikiri huu unaweza kuwa utundu unaoweza kukutumia ukakusaidia. [171]
uwanja
Leo mabingwa hao wa Zambia watapambana na Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga mchezo utakaofanyika kwenye uwanja huo wa taifa. [172]
uwe
Tunaomba utekelezaji uwe wa dhati na makini. [173]
vijiji
Lugha hiyo ilianza kutumika jana katika mikutano yake ya kampeni iliyofanyika katika vijiji vya Iyela, Nyala na Itewe wilayani Mbeya Vijijini. [174]
vikuu
Kwaangw' ambaye aliongozana na wajumbe 15 wa kamati hiyo kukitembelea Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) jana, alisema kuwa katika mahojiano na bodi ya mikopo, wamealikwa wajumbe kadhaa kutoka vyuo vikuu nchini. [175]
vile
Vile vile, kimetangaza rasmi kufutwa kwa sheria za chuo zinazotambua kuwepo kwa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho (Daruso). [176]
vipi
Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni,” alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [177]
vya
Kutokana na vipengele vingine vya usafiri wa nchi kavu na majini, tunapendekeza vipungue asilimia tano," alisema Ngewe Ngewe alisema gharama nyingine za nauli zinapanda kutokana na wapiga debe na watu wanaokata tiketi kuwalangua abiria wanaosafiri kwenda mikoani. [178]
vyenu
Hapa nawalinda kabisa na vijisenti vyenu. [179]
waishiwa
Lo! Mimi nilidhani waishiwa watacheka na kuendelea na kujiliwaza kwao. [180]
wake
KATIKA kuongoza mbinu za kuwashawishi wapigakura, Chama Cha Mapinduzi (CCM)kimeanza kutumia lugha ya kabila la Wasafwa kumnadi mgombea wake wa ubunge jimbo la Mbeya vijijini, Mchungaji Luckson Mwanjali. [181]
wakiwa
Alifahamisha kuwa kampeni hiyo itakwenda sambamba na kutoa elimu kwa madereva na kuhakikisha, madereva wanapimwa kiasi cha pombe walichokunywa wakiwa wanaendesha gari. [182]
wale
Vyuo saba vya elimu ya juu nchini vilifungwa kwa muda usiojulikana tangu Novemba mwaka jana, lakini baadaye vilitoa masharti ya wanafunzi kurejea kwa kujaza fomu na kulipa kiwango cha fedha wanachotakiwa kuchangia kwa mhula, pamoja na malimbikizo kwa wale ambao hawajalipa. [183]
wanachuma
Lakini wakati huu wengine wanachuma hivi hivi. [184]
wanasubiri
Akizungumza jana, kocha huyo alisema kutokana na mchezo uliopita dhidi ya Azam kuwa na makosa mengi tayari wamerekebisha makosa yao na wanasubiri mchezo huo kwa hamu. [185]
wao
Watoa huduma zote za usafiri wanatakiwa kuongeza juhudi katika kutoa elimu kwa madereva na watumishi wao wengine, ili kupunguza ajali za barabarani zinazotokea mara kwa mara na kuua watu wengi," alisema Ngewe. [186]
wenzangu
Waishiwa wenzangu. [187]
wiki
Kocha wa tenisi wa klabu ya Gymkhana, Majuto Majaliwa alisema wachezaji hao wameteuliwa baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa ya tenisi iliyomalizika wiki iliyoipita jijini Dar es Salaam. [188]
wote
Hata hivyo, baadhi ya vyama vya wanafunzi vilitaka wanafunzi wote kurejeshwa vyuoni bila masharti, jambo ambalo linaonekana kuzusha mvutano mwingine na menejimenti za vyuo. [189]
yako
Ukitaka kufanya mambo yako vizuri,na unataka usikilizwe, uishi maisha marefu ni bora, ubaki CCM kuliko ukawa kwenye upinzani na kupayuka mambo bila ushahidi wa kutosha. [190]
yangu
Akizungumzia mchezo huo, Phiri alisema: "Timu yangu imecheza vizuri, wachezaji wamebadilika katika kipindi kifupi na nataraji mabadiliko zaidi ya uwanjani. [191]
yao
Akizungumza na Mwananchi mara baada ya semina hiyo kumalizika Masoud alisema wao kama waendesha mashtaka ndio wanaojua changamoto wanazokabiliana nazo mahakamani, na si Takukuru na kwamba Takukuru kama wapelelezi mafunzo yao huwaelekeza kukabiliana na changamoto katika uchunguzi. [192]
yenyewe
Kesho Rais Kikwete ataendelea na ziara katika wizara hiyo na kukutana na viongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ambayo pia ina matatizo, wizara yenyewe, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Wakala wa Majengo ya Serikali, Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) na Mamlaka ya Udhibiti wa usafiri wa Nchi Kavua na Majini (Sumatra). [193]
yoyote
Hata hivyo, wizara haikutoa taarifa yoyote juu ya utafiti huo hadi wiki hii maofisa elimu wa kanda walipoeleza wanachodhani kimesababisha ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha pili kushuka nchini. [194]
yuko
Huyu yuko kwenye upande wa madini. [195]
yule
Kwa jamii ya Wasukuma kuku kuchi ni yule ambaye hana mbawa nyingi, asilimia kubwa ya mwili wake unakuwa hauna mbawa na ngozi yake inakuwa nyekundu," anasema. [196]
zaidi
Alitoa mfano katika Mahakama za Wilaya ya Mwanakwere kwa kuwa mara baada ya utaratibu wa kutenganisha shughuli za upelelezi na uendeshaji mashtaka walikuta kesi zaidi ya 1000, ambazo hazikuwa za msingi. [197]
ziara
RAIS Jakaya Kikwete leo anaanza ziara ya kutembelea wizara mbalimbali za serikali yake kufuatilia maagizo aliyoyatoa kwa wizara hizo, alipoingia madarakani mwaka 2005 na ataanzia Wizara ya Miundombinu. [198]
zile
Kuna uwezekano wa nchi maskini kuumia zaidi kutokana na mgogoro huo wa fedha," anasema, akionyesha kuwa vyanzo muhimu vya fedha kama vile fedha zinazotumwa nchi maskini kutoka kwa ndugu au jamaa zao wanaoishi nje hasa zile za Ulaya pengine zitashuka. [199]
zote
Ngewe alisema ili kuondokana na matatizo hayo baraza linatoa wito kwa taasisi zote zinazuhusika na sekta ya usafiri, kuanza kuandaa mchakato wa kuendesha usafiri kwa njia ya makampuni. [200]