Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-10

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
aende
Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [2]
aina
Hivyo, kuna haja kuwa na utaratibu au kampeni maalumu ya kuwasaka watu wa aina hiyo kuanzia kwenye maduka ya dawa hadi kwa waganga wa jadi na wanaopatikana navyo wachukuliwe hatua za kisheria. [3]
akawa
Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [4]
alifika
Muda mfupi baadaye waziri alifika hapo hospitalini, kwani si mbali sana kutoka kwenye ofisi yake. [5]
alisoma
Siku moja baada ya kukutana na jamaa huyo alisoma taarifa kwenye gazeti moja kwamba kuna biashara kubwa ya kununua viungo vya albino kwa ajili ya machimbo ya madini na biashara ya uvuvi. [6]
aliweza
Chuji aliweza kuibuka mshindi baada ya kupata kura 104 zilizopigwa na waandishi wa habari. [7]
aliyekuwa
Jukwaa la Wahariri lilianzishwa Mei 2007 na kuzinduliwa na aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wakati huo, Muhammed Seif Khatib. [8]
ambae
Unajua kwenye klabu yangu kuna wachezaji wengi wazuri sana na kila mmoja amesajili kwa kazi yake kwenye nafasi yake,î alisema Mrwanda ambae amewahi kuichezea Simba. [9]
ambako
Nyakiroto alisema maeneo yanayoongoza kwa maambukizo ya ugonjwa huo ni vya Muluseni, Nansio mjini, Nantare, Mahande, Bukondo na Ngoma ambako ugonjwa ulianzia. [10]
ambaye
Ole Milia, ambaye ni mwanasheria, alikanusha tuhuma hizo za kutumia mada yake kumshambulia Ole Sendeka, akisema alilenga kuzungumzia matatizo ya ardhi na Sheria ya Ardhi. [11]
ambayo
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga alisema kuwa, usajili huo utasukuma mbele maendeleo ya wanahabari nchini ambayo ndio msingi wa kuanzishwa kwa jukwaa hilo. [12]
ana
Hivyo hatukumwalika katika kikao hicho kwa kuwa hatujui nia yake, kama ana nia ya kutuunga mkono au la," alisema Profesa Lipumba. [13]
anayo
Msimu mwingine wa Mashindano ya Miss Tanzania ndio unaanza Fay anayo machache kwa wasichana waliojipanga kwania mataji mbalimbali ya mashindano hayo,...... ndiyo ukiachilia wanaoshinda kwa kuamini wanavyo vigezo na wanalihitaji taji wapo wanaotaka kushikiri kwasababu zao binafsi. [14]
anga
Pamoja na kuingilia kati utendaji mbovu unaodaiwa kusababisha shirika hilo kupoteza muelekeo, imekubali kutoa ruzuku ya Sh2.5 bilioni ili liweze kuanza kutoa huduma zake baada ya Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini (TCAA), kuirejeshea ATCL leseni ya kutoa huduma ya usafiri wa anga iliyokuwa imenyang'anywa kutokana na kukosa baadhi ya vigezo muhimu, ambavyo sasa vimerekebishwa. [15]
angalia
Nasikia unamjua, ni huyu hapa angalia vizuri picha, kama unajua anapatikana wapi, nitaagiza hata magari mengine yamsake maeneo hayo, nitaomba hata jamaa yangu mmoja usalama wa taifa mstaafu mwenye uwezo mkubwa katika masuala ya kupeleleza atusaidie kumpata,” alisema waziri. [16]
angekuwa
Akizungumza mwanamuziki huyo alisema kuwa yeye binafsi kama isingekuwa kujituma na moyo wa uvumilivu basi angekuwa ameshapotea kama wanavyopotea wasanii wengine wanaokuja na kuondoka. [17]
au
Alisema wahariri waliamua kusajili jukwaa hilo kama kampuni ili kuepuka watu, makundi au vyombo visivyohusika na taaluma hiyo kuingilia masuala ya wahariri. [18]
baadaye
Alisema baadhi ya watu katika maeneo ya mradi, wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kufukua mabomba ya chuma na baadaye kuyauza kwa wafanyabiashara wanaonunua chuma chakavu. [19]
bado
Sheikh Yahya alisema CCM mwakani haitakuwa na nafasi kutawala peke yake ingawa Rais Jakaya Kikwete bado ataendelea na wadhifa wake wa urais. [20]
baina
Akizungumza na waandishi wa habari katika hotel ya Lamada jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa timu hiyo Iman Madega alisema hakuna mgogoro wowote unaoendelea ndani ya Yanga baina ya uongozi na mwalimu. [21]
bila
Alifafanua kwamba CCM haiwezi kuyumba kwa sababu yoyote na itaendelea kutawala bila kushirikiana na vyama vingine. [22]
cha
Kwani utajiri na mali ni kigezo cha kupatikana Serikali ya vyama vyote. [23]
chakavu
Njwayo alisema biashara ya chuma chakavu, inaathiri kwa kiasi kikubwa, utekelezaji wa mipango ya kuboresha huduma za maji kwa wananchi wa Wilaya za Newala, Tandahimba na Mtwara Vijijini, wanaohudumiwa na mamlaka hiyo. [24]
chake
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema katika kikao hicho kuwa Alimwandikia barua mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kutaka chama chake kimwunge mkono mgombea wa CUF, lakini Mbowe hakujibu barua hiyo. [25]
chanjo
Chanjo ya kipindupindu isiwalemaze wananchi JUZI Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ilitangaza kuwa Januari17, mwaka huu itaanza kuifanyia majaribio chanjo mpya ya ugonjwa wa kipindupindu katika visiwa vya Unguja na Pemba, ikiwa ni juhudi zake za kutokomeza ugonjwa huo visiwani humo. [26]
chiki
Tofauti na wasanii wengine ambao wanapenda kufanya mambo kwasababu fulani kafanya nitofauti kwa Mr chiki ambaye mbali na kukaa kwenye sanaa ya maigizo kwa muda mrefu bado ajaamuwa kujikita kwenye utengenezaji wa filam. [27]
dunia
CUF na Chama Cha Mapinduzi (CCM), vilimwekea pingamizi mgombea wa Chadema na kufanikiwa kumwondoa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi huo ulioitishwa kuziba pengo lililoachwa wazi na Richard Nyaulawa aliyefariki dunia baada ya kuugua muda mrefu. [28]
enka
Meshack Abel anasumbuliwa na enka na hatacheza leo lakini nafasi yake imezibwa kikamilifu na Kelvin Yondani ambae amekuwa kama pacha wa Salum Sued. [29]
es
HATIMAYE jukwaa la wahariri nchini limepata usajili wake kuanzia Jumatano wiki hii chini ya sheria ya makampuni ya mwaka 2002. Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Sakina Datoo, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kwamba, jukwaa hilo limesajiliwa na Msajili wa Makampuni (Brela). [30]
eti
Haya, haya, haya, wapo ambao wamediriki hata kutuita sisi waishiwa kuwa ni mafisadi, eti tumekunywa na kunywaga ushuru wa watu hadi asubuhi siku ya mwaka mpya. [31]
foleni
Kumbe jamaa mwenyewe alikuwa anatafuta nishani ya kiatu peke yake kwa kujaribu kuzuia kila gari linalotaka kuruka foleni. [32]
fulani
Danny ana maumivu fulani nina wasiwasi sana na lakini mpaka kesho (leo) asubuhi nitajua lakini hana hali mbaya sana,î anasema Daktari wa timu, Juma Sufian. [33]
game
Alizidi kufafanua kuwa ni kipindi kirefu sana alikaa pembeni kidogo japokuwa aliweza kuwafahamisha mashabiki kuwa wampe muda kwani yupo katika masuala mengine na bado yupo katika game. [34]
gani
Kukubalika na watu inahitaji moyo na uvumilivu, waliongea sana baada ya mimi kubadili mfumo wangu wa uimbaji lakini kila siku nilikuwa nasema naweza na nashukuru sana walionipa faraja kipindi chote mpaka mashabiki wamenikubali, sasa nawaacha wachague jinsi gani nawashika mashabiki na wakiendelea kushangaa nateleza" alisema. [35]
hadi
Fedha kutokana na misaada na mikopo zilipungua kutoka dola 717 milioni (Sh960 bilioni) na hadi dola 518 milioni (Sh694 bilioni) katika mwaka huo. [36]
hajui
Kauli hiyo ilionekana kumchanganya sana Kazim, akawa hajui la kufanya. [37]
hakika
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alisema, hana hakika kama chama chake kimealikwa kwenye mkutano huo, lakini hata kama wangealikwa wasingehudhuria kwa kuwa ndoa hiyo ni ya kinafiki. [38]
halafu
Nimewaambia wachezaji kila mtu asimame na mtu kuanzia mwanzo mpaka mwisho, wasitoe nafasi wachezee mpira, watulie halafu wanapanga mashambulizi. [39]
hamsini
Katika mchezo wa kuwania kufuzu nusu fainali ya kombe la Chalenji, ambao asilimia hamsini ya Stars wana malaria, Uganda haina cha kupoteza lakini Stars inahitaji ushindi huku ikisikilizia matokeo ya mechi ya nyingine. [40]
hana
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Elimu kwa vyombo vyahabari jana na kutiwa sanini na Kaimu Katibu Mkuu, S.Gesimba imeonyesha kwamba, watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo mwaka hana walikuwa 414,375, wasichana wakiwa 192,218 sawa na asilimia 46.4 na wavulana asilimia 222,157 (asilimia 53.6 ). [41]
hao
Wenyeviti hao waliokutana ni Profesa Lipumba (CUF), James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Agostine Mrema (TLP); na Peter Mzirai (PPT Maendeleo) huku Freeman Mbowe ambaye awali alikuwa hakosi katika vikao kama hivyo kutoonekana. [42]
hapa
Uuzaji wa bidhaa nje ulipanda kutoka dola 3.69 bilioni mwaka mmoja uliopita hadi dola 4.47 bilioni, ikiwa imesaidiwa na bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini, ambazo zilipanda kwa asilimia 97 hadi kufikia dola 564 milioni. [43]
hapo
Madega aliongeza kuwa kama uongozi wake ni mbaya Yanga isingefikia hapo ilipofikia kwani hivi sasa timu inacheza mpira safi, na sasa nguvu zao wanazielekeza kwenye mzunguko wa pili wa ligi na kasi ni ileile ya mzunguko wa kwanza na mashambulizi ni yale yale. [44]
hasa
Mhadhiri mwingine wa chuo hicho, Dk Haji Semboja ameeleza kuwa, tatizo hilo linaweza limesababishwa na matatizo mbalimbali yaliyojitokeza nchini na hasa ikiwa ni kipindi cha kutoka kwenye bajeti ambapo serikali haikuwa na fedha za kutosha kufanya manunuzi mengi muhimu. [45]
hata
Datoo alisema kimsingi hata kabla ya kusajiliwa, wahariri walikuwa na haki kukutana kujadili masuala ya taaluma ya uandishi wa habari na kwamba kusajiliwa ni hatua muhimu zaidi kisheria. [46]
hatua
Nitamchukulia hatua za kisheria," alisema Ole Milia wakati akipata matibabu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Monduli. [47]
hawa
Ni baadhi tu ya wanachama wanaipaka matope klabu kwa maslahi yao binafsi, lakini sisi viongozi tunafanya uchunguzi mkali ili kuwabaini watu hawa na tukiwabaini tutawachukulia hatua kali na itakuwa fundisho kwa wengine"alisema Madega. [48]
hawana
Zanzibar ina mategemeo makubwa ya kufuzu hatua ya pili na wachezaji wake walisema jana kwamba hawana presha yoyote na Rwanda. [49]
hayo
Kufuatia mafanikio hayo, Benki Kuu imepongeza juhudi zinazofanywa na sekta hiyo katika kukuza uchumi wa taifa. [50]
hii
Mimi pia ninatabiri kwamba CCM haitapasuka bali itaendelea kutawala nchi hii milele," alisema Makamba kwa kejeli. [51]
hiki
Katika vikao vya namna ile utasikia wazee wakisema kikao hiki kinabaraka! baraka ile ni ya wele wawili wanaojaribu kuzungumza mambo yaliyo jaa vifuani kwao na kisha kuunganisha tena wakiwa wanaanza maisha mapya yaliyokunjua vifua vyao. [52]
hivi
Ndio maana tulihitaji fedha nyingi za kigeni kununua bidhaa kutoka nje," alisema Prof Mabere na kuonya: "Hali hii ikiendelea hivi, ni ishara kuwa uchumi unaporomoka. [53]
hizi
Ndugu yenu kutoka pande hizi naomba niendelee kuwashukuru ninyi wasomaji wangu kwa hamasa na changamoto mnnazonipa. [54]
hizo
Taarifa hiyo imeeleza kuwa uagizaji wa bidhaa kutoka nje uliongezeka kwa asilimia 36 na kufanya jumla ya fedha zilizotumika kuagiza bidhaa hizo kuwa dola 6.36 bilioni kulinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka jana. [55]
hofu
UONGOZI wa klabu ya Yanga umewatoa hofu wanachama wake kuwa hakuna migogoro ndani ya timu hiyo ambavyo imesikika siku za hivi karibuni na kocha mkuu wa timu hiyo Dusan Kondic ataendelea kukinoa kikosi iko katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu unaoanza leo. [56]
huko
Safari ikandelea mpaka Miss Kinondoni, huko nako alilinyakua taji kubwa lililokuwa likishikiliwa na Miss Tanzania wa wakati huo, Richa Maria Adhia. [57]
huu
Hata hivyo, baada ya watu 21 kufunguliwa mashtaka ya tuhuma za wizi wa jumla ya Sh133 bilioni, nchi kadhaa ziliwasilisha michango yao kwa bajeti ya mwaka huu. [58]
huyu
Jamaa kumbe wanastuana bwana, alipoenda huku kwingine wakaambiana kaja huku, na huyu naye akapiga, mchizi akaaga kuna ishu anafuata ofisini akarudi kwingine. [59]
idadi
Kwa mujibu wa Semkondo, mitambo minne katika hiyo, itatumika kusukuma maji kutoka katika chanzo cha Mkunya na idadi kama hiyo katika chanzo cha maji cha Mitema, Kitangali. [60]
iende
Lakini waishiwa walikubaliana kwa kauli moja tuzo ya tako ya juu kabisa iende kwa wenye makampuni ya mafuta. [61]
iko
Tuligundua kuwa, CUF iko juu Mbeya na ina kura nyingi sasa sisi kazi yetu ni kuongezea tu katika zile kura za CUF ili Mponzi ashinde. [62]
ila
Siyo kuwa msanii huyu pamoja na kutopenda mfumo ulio kwernye soko la filamu hajawahi kucheza kabisa filamu la hasha alishashirikishwa kwenye filamu kadhaa kama vile filamu iliyojulikana kwa jina la Subrina na Sakata, ila kutoka na mambo yake mwenyewe ametuahidi mwaka 2010 tutaanza kumshuu udia kwenye filamu za ukweli zenye character wenye sifa zote. [63]
ile
Unaweza ukajifanya kama wewe Mastaplani, ukaunganisha ishu zako dabo, labda mara ya kwanza ishu ikawa poa, lakini biliv'mi, lazima zitakuwa zina hitilafu mbili tatu, sababu umakini wake unakuwa sio kiviiiile, si unashtukia ile? Na afadhali zisaksidi kimagumashi lakini samtaimz zote zinazingua, unabaki unang'aang'aa macho. [64]
ili
Alisema Jukwaa hilo lililoanza mwaka 2007 lilikuwa linaendeshwa na kamati ya muda iliyopewa jukumu na Wahariri kuhakikisha pamoja na mambo mengine linapata usajili ili kukifanya chombo hicho kitambuliwe kisheria. [65]
iliyopo
Kocha huyo aliyasema hayo jana mara baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari katika mkutano uliowakutanisha waandishi wa habari na viongozi wa klabu hiyo uliofanyika katika Hotel ya Lamada iliyopo Jijini Dar es salaam. [66]
imetoa
SEKTA binafsi nchini imetoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa kwa kipindi kilichoishia Oktoba mwaka jana, taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeeleza. [67]
iwe
Aidha aliongeza kuwa ni baadhi tu ya wanachama wanaichafulia jina klabu na wao viongozi wapo katika uchunguzi mkali ili kuwabaini watu hao ambao hawaitakii mema Yanga na wakibainika watachukuliwa hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo. [68]
jamani
HAYA haya jamani. [69]
japo
Pia msanii huyu anasema kuwa kati ya malengo aliyonayo ambayo anaamini nimwongozo wa sanaa ya uigizaji nipamoja na kuanzisha chama kitakacho wasimamia wasanii japo kuwa wasanii wengi hawapendi kitu hicho. [70]
jua
Na kama hato jua basi hawezi kukuridhisha na kama hatokuridhisha jua hutofurahisha na kama hatofurahia basi mengine ndiyo haya yatokanayo. [71]
juu
Suala la CCM kushirikiana na Chama cha Demokrasia (DP), katika uchaguzi mdogo wa Tarime ni udhaifu na dalili tosha juu ya kushindwa kwake," alisema Sheikh Yahya. [72]
kansa
Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [73]
kasi
Huku wakishambulia kwa kasi na kutawala kipindi cha kwanza, The Cranes walipata bao la pili katika dakika ya 28, kupitia Steven Bengo aliyekuwa akiisumbua ngome ya Bara baada ya kupiga faulo iliyojaa moja kwa moja wavuni. [74]
kati
Kwa mujibu wa matokeo hayo, watahiniwa waliofauru walikuwa 283,278 sawa na asilimia 73.5 kati yao wasichana 121,619 sawa na asilimia 31.6 na wavulana 161,659 sawa na asilimia 41.9 waliofanya mtihani huo. [75]
kijana
Hela nyingi sana hizo analipwa Maximo inaonekana mnapenda sana michezo namna viongozi wazuri,"alisema kocha huyo kijana. [76]
kila
Sheikh Yahya alisema kila kitu kina dalili zake na kwamba dalili ya CCM kukwama katika uchaguzi wa 2010 zimekwishaonekana. [77]
kile
Na mara nyingine vikao kama vile vinakosea na ikaja kuwa sababu kuwa waliopatanishwa jana wamegombana tena kwa sababu katika hili kikao kile yalizumzwa mengi yatokanayo, na kiini haswa kikaachwa, mathalan mambo ya kitandani. [78]
kipindupindu
Mkoa wa Mara kwa uchunguzi vimethibitisha kuwa ugonjwa huo, ni kipindupindu. [79]
kirefu
Njwayo ambaye pia ni Mbunge wa Tandahimba, alisema wananchi wa maeneo yanayonufaika na Mradi wa Maji wa Makonde, wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuulinda, ili uendelee kuwasaidia kwa kipindi kirefu. [80]
kombe
Nguvu zetu tumezielekeza kwenye mzunguko wa pili wa ligi na tutafanya vizuri kama tulivyofanya vizuri kwenye mzunguko wa kwanza na naamini tutatwaa kombe,"alijigamba Madega. [81]
kufa
Wakati wanaendelea kuangalia ile picha aliingia daktari aliyekuwa akimwangalia Kazim na kumwomba waziri afupishe mazungumzo, badala yake wamsake yule mvumbuzi wa dawa kwani isingepita saa 12 kabla ya Kazim kufa ikiwa hatapata ile dawa. [82]
kufuzu
Chuji ameweza kuibuka mwanamichezo bora baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN na kusaidia timu yake kutinga fainali hizo zitakazofanyika nchini Ivory Coast mapema mwaka huu. [83]
kukaa
Twende na wakati kwa kuacha kukaa ofisini, badala yake, tifanye kazi kwa kuona na kuhakikisha," alisema. [84]
kukagua
Mhandisi Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Ogare Salu alisema juzi katika majumuisho ya ziara yake ya kukagua majengo hayo kuwa, madhara yanayoweza kuwapata wakazi hao, ni kifo na uharibifu wa mali. [85]
kula
Profesa Laswai alisema endapo wananchi mkoani hapa, watakuwa na juhudi na malengo mazuri na kutumia elimu ya kutokomeza utapiamlo, wanaweza kuutokomeza kabisa utapiamlo kwa kula mlo uliokamilika. [86]
kulazwa
Hadi sasa zaidi ya wagonjwa 105 wamepokelewa na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe wakisumbuliwa na maradhi hayo. [87]
kule
Akazuga kuna kitu anaenda kuchukua samwea, akaenda kule kwingine. [88]
kulia
Badala yake viongozi nao waliungana na wananchi kulia kuwa wafanyabishara hawa ndio chanzo cha kupanda kwa gharama za maisha. [89]
kumuua
Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [90]
kuna
Alisema katika mtaa wa Amani kuna jengo limejengwa chini ya kiwango ambalo sasa limeanza kuathiri majengo mengine yaliyo karibu yake kwa kuyabomoa kuta. [91]
kutwaa
Herve ambae timu yake ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, alisema kwamba anaelekeza nguvu zake kwenye michuano ya CHAN mwezi ujao. [92]
kuua
Tunapongeza juhudi zilizofanywa na SMZ kukabiliana na kipindupindu kwa kutafuta njia moja wapo ya kudumu dhidi ya ugonjwa huo sugu unaoendelea kuua watu, hasa katika maeneo yanayotawaliwa na uchafu. [93]
kuuza
Mmbaga alisema zao hilo, likitumika ipasavyo litasaidia watoto wadogo kuondoa tatizo la utapia mlo na kuwapatia wakulima mapato baada ya kuuza soya na kwamba soya inaongeza virutubisho vingi vya protini kwa wagonjwa wa ukimwi. [94]
kwao
Naye Mwenyekiti wa TLP, Agostine Mrema alisema, uchaguzi wa Mbeya ni mtihani wao wote na si wa CUF pekee kwani aibu ya kushindwa ikitokea si ya kwao tu bali ni ya wapinzani wote. [95]
la
Kama Sheikh Yahya ametoa utabiri huo na mimi ninatabiri hivyo sasa tuone nani mkweli katika utabiri wake," alisema Makamba na kuongeza: "Huu sio wakati wa kutabiri ni wakati wa kuzungumzia maendeleo ya chama lakini kama unaona suala la utabiri wa Sheikh Yahya ndiyo la muhimu, ukaandike kwamba Makamba kasema Sheikh Yahya sio Mungu na siwezi kukubaliana na utabiri wake. [96]
lake
Stars ilizawazisha bao lake katika dakika ya 48 kwa mkwaju wa penalti mfungaji akiwa Salum Sued baada ya Sali Edward kumwangusha Danny Mrwanda wakati akienda kufunga. [97]
langu
Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni,” alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [98]
lengo
Tutaitisha kikao haraka ili kuamua kwa pamoja jambo la kufanya kwa lengo la kuokoa maisha ya wakazi hao kabla ajali hazijatokea,"alisema Lufungulo. [99]
leo
Kilomita chache kutoka eneo hilo, mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete alikuwa akizindua nyumba za wanajeshi wa kambi ya Monduli, akiwa ameongozana na viongozi wengi wa chama hicho na leo anatarajiwa kuja mjini hapa kuendelea na ziara yake. [100]
licha
Hata hivyo, kitendo cha hivi sasa cha wafanyabiashara hao kuendelea kukaidi amri ya serikali kushusha bei ya mafuta kimeonyesha kwamba licha ya chombo hicho kupewa meno inawezekana kilikuwa bado kikijihisi ni kibogoyo kama zamani. [101]
lita
Kiwango hicho ni cha chini kulinganisha na bei ya sasa ambayo ni kati ya Sh1,400 na Sh 1,600 kwa lita moja ya petroli na kati ya Sh1,300 na Sh1,400 kwa lita moja ya dizeli. [102]
lolote
Nasema hili kwa sababu inashangaza kuona kundi ndogo la wafanyabiashara wa mafuta nchini limeigeuza serikali kama mtoto anavyoweza kumchezea babu yake akijua kwamba hawezi kuadhibiwa kwa kosa lolote analoweza kumfanyia. [103]
mada
Alitumia mada yake kunishambulia," alisema Ole Sendeka akizungumzia mada iliyowasilishwa na Ole Milya kwenye semina hiyo kuhusu matumizi ya ardhi na jinsi wanasiasa wanavyotumia Sheria ya Ardhi kudhulumu wafugaji iliyofanyika kwenye Chuo cha Elimu Monduli. [104]
madai
Kutokana na pendekezo la mwalimu mstaafu, nafasi ya nne katika tuzo inaenda kwa wale wote ambao wanawarusha wengine kwa madai kwamba na wao wanarushwa na wakubwa zaidi. [105]
mafisadi
Huyu anatumiwa na mafisadi kunimaliza. [106]
magari
Watu wanapita kwa kasi ya alQaeda, na kuzuia magari upande wa pili na pia kufanya hata foleni ya kwenda mjini ikwamekwame. [107]
magumu
Maisha yamezidi kuwa magumu na nadhani hata waajiri wetu hawaongezi mishahara kwa sababu wanajua tutajitafutia kwa hizi njia nyingine. [108]
mara
Akizungumza katika mkutano huo, Meya wa Manispaa ya Ilala, Abuu Jumaa, aliwataka watendaji kukagua maeneo ya ujenzi kwanza kabla ya kutoa vibali, na kuendelea kuyakagua majengo hayo mara kwa mara kuona kama vipimo vimefuatwa. [109]
mbele
Amenijeruhi na amenidhalilisha mbele ya watu, hivyo ni lazima nimchukulie hatua za kisheria. [110]
meno
Baada ya serikali kuunda Ewura ilionekana kuwa haina meno na kwamba haingeweza kuwa na nguvu za kufanya kazi zake vyema, hata hivyo, serikali ilisikia kilio cha wananchi kuipatia meno Ewura baada ya kufanyia marekebisho sheria ya nishati bungeni. [111]
mgumu
Kocha wa Tanzania, Marcio Maximo alisema mchezo ulikuwa mgumu sana kwa vijana wake katika kipindi cha kwanza lakini walirekebisha makosa na kupata bao lilowapeleka fainali. [112]
miji
Naye mwenyekiti wa Mipango miji wa Manispaa ya Ilala, Magina Lufungulo alisema, baada ya kugundua kasoro hizo, manispaa itaitisha kikao cha wahandisi wanaosimamia shughuli za ujenzi maeneo hayo, kujadili hatima ya tatizo hilo. [113]
mikopo
BoT pia imeeleza kuwa sababu nyingine iliyochangia nakisi hiyo ni kupungua kwa fedha za misaada na mikopo. [114]
mingi
Tuna mikakati mingi kidogo na mizuri sana nina kila sababu ya kusema sisi ni bora na hilo kila mmoja analitambua kwahiyo kama tutakuwa hatuendi sehemu mbali mbali wengine hawatapata fursa ya kuona ubora wetu, kwahiyo tutafanya kila liwezekanalo kuwafurahisha mashabiki wetu" alisema Nyoshi. [115]
mji
Kiongozi wa kundi hilo Nyoshi alisema tangu wawepo nchini hawajawahi kutoka nje ya nchi kwenda mji wowote mkubwa hivyo wataitumia fursa hiyo walioipata kujitangaza vizuri ili wawe wanapata mialiko mara kwa mara na pia kuipa utambulisho bendi hiyo. [116]
mkuu
Hata hivyo ofisi ya mkemia mkuu wa serikali Kanda ya Mwanza, imetuma mwakilishi wake kwenda Ukerewe kuchukua upya, sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa kina. [117]
mlo
WANANCHI mkoani Morogoro wametakiwa kutumia kwa wingi zao la soya ili kutokomeza kabisa tatizo la utapia mlo mkoani humo. [118]
mno
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [119]
moto
Baadaye wakiwa njiani wanampeleka kituoni, walipigiwa simu na Ikulu kuwa kuna watu wamechoma moto kwa pasi Ikulu. [120]
mtindo
Wangekamata magari na kuyakalisha pale nusu saa, huu mtindo ungekoma papohapo. [121]
mumewe
Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [122]
mwa
Watu watano miongoni mwa hao, wamekwishapoteza maisha. [123]
mwenye
Mwenyewe anajiita Super Model mwenye ndoto kubwa za kuwa mwanamitindo mkubwa kama kina Oluchi. [124]
mwezi
KIUNGO wa Taifa Stars na Yanga, Athuman Iddi 'Chuji' amechaguliwa kuwa mwanamichezo bora wa mwezi Disemba na Chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani (Taswa). [125]
mwishiwa
Lakini mwishiwa mmoja alisema. [126]
mzuri
CUF na TLP vina mtandao mzuri sana Mbeya Vijijini hivyo cha msingi ni kushirikiana wote ili kuimarisha mtandao huo badala ya kupoteza kura kwa hasira za kijinga na ubabe, tunaomba wananchi wasipige kura za maruhani na wasigomee uchaguzi bali tumpigie Mponzi," alisisitiza Mrema. [127]
na
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeuponda utabiri uliotolewa juzi na Mnajimu Sheikh Yahya Hussein na kusema, sheikh huyo sio Mungu kutabiri mpasuko ndani ya chama hicho. [128]
nami
Ndugu yangu nakupa pole sana, yaani ni bora ungewasiliana nami kabla ya kwenda huko, kwani ukweli ni kwamba dawa imegunduliwa nchini na jamaa mmoja tena ni albino, rudi wahi mapema usipoteze muda wako huko,” alimsisitizia. [129]
nao
Siwezi kukubaliana na utabiri wa Sheikh Yahya kwa sababu yeye sio Mungu na kama watu wanaweza kuamini utabiri wake na kukubaliana nao basi. [130]
ndefu
Alisema, kazi ni ngumu na safari bado ni ndefu kuelekea Ikulu kwa hiyo tusijisahau CCM hatujaikamata popote kinachoendelea ni sawa na siafu aliyepanda mgongo wa tembo. [131]
ndio
Naye Prof Mabere Robert wa chuo hicho alisema inawezekana kipindi hicho hakikuwa cha mauzo ya bidhaa nje ndio maana kumekuwa na nakisi kubwa kiasi hicho. [132]
ndiye
Simanjiro wakati akijua mimi ndiye mbunge wa jimbo hilo. [133]
ni
Katibu Mkuu Yusuf Makamba aliliambia gazeti hili jana kuwa, CCM haiwezi kuvunjwa moyo na utabiri huo kwa kuwa Sheikh Yahya ni binadamu anayeweza kutumia busara zake kusema anachoamini kuwa kweli. [134]
nia
Wakati vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi, Tanzania Labour (TLP) na PPT Maendeleo vikikutana jana na kutangaza nia ya kumwunga mkono mgombea wa CUF katika uchaguzi mdogo wa Mbeya Vijijini, Daudi Mponzi, Chadema imesema haipo tayari kuungana navyo kwa kuwa umoja huo ni wa kinafiki. [135]
nina
Kutokana na kusajili katika mamlaka ambayo itawafanya wafanye kazi bila ya kuingiliwa na mtu mwingine wa pembeni, nina uhakika wahariri sasa watakuwa wamepewa walichokuwa wanakitaka," alisema Kajubi. [136]
nini
Kocha huyo baada ya kuambiwa kwamba Maximo mkataba wake unamalizika Julai na amegoma kuongeza, aliomba namba ya Rais wa TFF, Leodegar Tenga, lakini hakutaka kuweka bayana ni ya nini. [137]
njama
Kitendo cha askari yule kumpiga mumewe na muda mfupi baadaye kukara roho, kilimfanya aamini kuwa kama vile kuna njama za kumuua zilifanyika. [138]
njano
Mawazo yao ni kwamba Haruna Moshi na Shadrack Nsajigwa hawatacheza leo kwa kuwa wanakadi mbili za njano kila mmoja kitu ambacho si sahihi na kitawashangaza uwanjani. [139]
nusu
KILIMANJARO Stars imefanikiwa kusonga kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la Chalenji kwa bahati baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa wenyeji Uganda (The Cranes), huku ndugu zao wa Zanzibar wakiyaanga mashindano hayo baada ya kufungwa 3-0 na Rwanda. [140]
nyingi
Lakini pia katika kipindi hicho bei ya petroli duniani ilikuwa imepanda sana, hivyo fedha nyingi zilitumika tofauti na ilivyokusudiwa," anasema Dk Semboja. [141]
nyinyi
Sijui kama nyinyi waishiwa ni wasomi au la. [142]
nyuma
Nimefurahi kurejea tena Tanzania nikiwa kocha wa Simba, nilifurahia sana maisha wakati nilipokuwa na timu hii miaka ya nyuma ambapo tuliweza kutwaa ubingwa wa ligina michuano ya Tusker," alisema Phiri. [143]
nzuri
Azam ni timu nzuri na kila siku inazidi kufanya vizuri ukilinganisha na timu nyingine. [144]
pale
Alisema kuwa hiyo iwe ni changamoto kwa watu wengi pia kuona umuhimu wa kufanya hivyo na kuthibitisha utamaduni wa Mtanzania wa kupingezana pale linapotokea jambo zuri. [145]
polisi
Tayari mwenyekiti huyo wa UV-CCM amesharipoti tukio hilo polisi na sasa anasubiri kesi. [146]
raia
Herve Renard ambae ni raia wa Ufaransa, timu yake ilitolewa juzi katika hatua ya makundi ya kombe la chalenji baada ya kufungwa mabao 2-0 na Sudan. [147]
rais
Lakini wanaoruka hivi wanaona kwamba kila mtu ana haki ya kuruka foleni apendavyo kwa sababu yeye ni rais mtarajiwa hata kama ni rais wa mende nyumbani kwake. [148]
roho
Nakufa, mkuu wa polisi unaniua, sawa mimi nimemuua albino, lakini wewe unaniua mimi kwa kunipiga kibao, imeandika wapi kwamba muharifu apigwe, kabla ya kufikishwa mahakamani,” alisema Kazim huku akikata roho. [149]
saa
Kufutuati matokeo hayo Tanzania sasa itakutana na vinara wa kundi B, Kenya, Harambee Stars kesho Jumapili saa 12:30 mchana kwenye Uwanja wa Nambolee. [150]
saini
Kocha mpya wa timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi Mzambia, Patrick Phiri jana alitia saini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha timu hiyo huku akiwahakikishia wapenzi na wanachama sasa Simba itarudi kwenye nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi. [151]
sana
Sheikh Yahya pia katika utabiri wake alisema uchaguzi wa mwaka 2010 hautakuwa na wizi wa kura kwa kuwa watu wamekuwa wajanja na vyama vya siasa nchini vina nguvu sana. [152]
sanaa
Jina lake kamili ni Salum Mchoma lakini katika tasinia ya sanaa ya maigizo anajulikana zaidi kama Mr Chiki. [153]
sare
Naamini vijana wangu na najua watafanya kazi niliyowaagiza, ni kama tumeshaingia nusu fainali sare ni nzuri kwetu lakini nimewaambia wachezaji wangu washinde kwa vile sielewi nini kinaweza kutokea. [154]
shida
Umempata?” alidakia Kazim, aliyekuwa akizungumza kwa shida. [155]
shule
Sasa juzi mimi nilikuwa kijijini wakati matokeo ya shule za msingi yalipotangazwa. [156]
si
Uuzwaji nje wa bidhaa ambazo si asili ulipanda kwa asilimia 25 na kufikia dola 2.12 bilioni (Sh2.8) ikilinganisha na mwaka jana. [157]
sifa
Taarifa zilizoenea sehemu mbalimbali nchini; na hata kukamatwa na kushtakiwa mahakamani kwa mganga mmoja wa jadi kwa tuhuma za kukutwa na vifaa mbalimbali vya hospitalini na madawa kadhaa, zinadhihirisha kuwa vifaa hivyo sasa vinatumiwa na watu wasio na sifa kutumia vifaa hivyo kutibu wagonjwa. [158]
sisi
Siwezi kuzungumzia suala la kualikwa au kutoalikwa, lakini hata kama tungealikwa tusingehudhuria kwa sababu sisi tunaungana na vyama makini vyenye ukweli na sio muungano wa kinafiki, kudanganyana na kuwadanganya Watanzania, muungano wa kuchekeana mchana na kupigana visu usiku," alisema Dk Slaa. [159]
soka
Naye Kocha wa mabingwa hao Mserbia Dusan Kondic amesema timu nyingi za hapa nyumbani zinakosa viongozi wenye ujuzi wa soka ndio chanzo kikubwa cha kusababisha timu kufanya vibaya kwenye mashindano mbalimbali. [160]
soko
Mbali na kasoro hizo zilizopo kwenye tasinia ya filamu alizozibainisha Mr chiki, amejiwekea malengo na anasema kuna watu anataka ajiunge nao ili ifikapo mwaka 2010 aweze kuingia rasmi kwenye soko la flamu na anaamini watafanya maajabu na kulipandisha soko hilo. [161]
sugu
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na SMZ, chanjo hiyo ni ya kwanza kutolewa nchini Tanzania na kwamba, wameshaandaa maeneo maalumu ya kufanyia majaribio hayo, ambayo ni yale yenye matatizo sugu ya ugonjwa huo visiwani humo na watu 5,000 wakiwemo watu wazima na watoto wanaotarajiwa kuchanjwa. [162]
tena
Tuna uhakika kupitia ushirikiano huu kwamba, CCM haina tena chochoro za kupenyea Mbeya Vijijini na Daudi Mponzi atakuwa mbunge wa jimbo hilo," alijigamba Profesa Lipumba. [163]
tiba
VIFAA vya tiba hospitalini sasa inaonekana kutumbukia mikononi mwa watu wasiostahili ambao hawana ujuzi wa taaluma ya uganga na udaktari wa kusomea kutoka taasisi zinazotambulika. [164]
tishio
Wachezaji asilimia hamsini wana malaria, ukianzia Nurdin Bakar, Kiggi Makasi, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Bonny lakini si tishio sana ambayo inaweza kuwazuia wasicheze. [165]
tu
Dhahabu na utalii ulichangia kwa asilimi 47 tu katika mapato yatokanayo na bidhaa zilizouzwa nje. [166]
tuko
Lakini sisi tuko nyumbani tunapaswa kuwaonyesha mashabiki wetu kwamba tuko tayari kwa ubingwa na matokeo mazuri ya kuwafurahisha kama wenyeji,îalisema kocha huyo na kusisitiza kwamba hawataki kupoteza uelekeo wao. [167]
tumekuwa
KWA muda mrefu Watanzania tumekuwa katika matatizo makubwa ya kupanda kwa bei ya mafuta, ambayo ilisababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la duniani. [168]
tuzo
Lakini kwa kuwa sisi ni watu wa ukweli na uwazi, tumejiweka wenyewe ndani ya tuzo la tako. [169]
uchungu
Kwa nini wengine wafaidi tu, sisi waishiwa tusifaidi? Tumefurahi kuona kwamba wako wengi wenye uchungu wa nchi yao. [170]
ujao
Alifafanua kuwa, Serikali ya miaka ya 2010 ni ya muungano wa vyama, uchaguzi ujao hautakuwa na wizi wa kura kama vile ilivyokuwa awali, vyama vya Upinzani kulaumiana na chama tawala. [171]
uko
UHAI wa wakazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam, uko shakani baada ya utafiti wa kitalaam kuonyesha kuwa asilimia 90 ya majengo yote ya eneo hilo, ni mabovu kutokana na kasoro za kiufundi. [172]
umri
Hivyo washindi wote watacheza fainali leo ikiwa umri wa miaka 14 Mtanzania Shaaban Ibrahim atapambana na Guyorly Irudukunda kutoka Burundi na umri wa miaka 16 kwa wasichana Syori Laura wa Burundi atacheza na Shufaa Changawa kutoka Kenya na miaka 16 wavulana ndugu wawili Waburundi wakimenyana nao ni Idrissa Ndayisenga atacheza na Hassani Ndayishimiye. [173]
una
Mbali na kugoma kuhudhuria kikao cha vyama hivyo kilichofanyika Buguruni makao makuu ya CUF, Chadema ilieleza msimamo wake kwamba kamwe hakitamwunga mkono mgombea huyo wa CUF kwa kuwa umoja huo una mashaka. [174]
uwazi
Kikubwa katika kikao cha usuluhisho ni kuwapa nafasi wawili kuwasilisha mambo yao kwa uwazi na baadaye kushawishi wawili wale kurudiana baada ya kusafisha vifua vyao. [175]
uwezo
Ni kweli ninafanya kazi, lakini si yangu, utajiri wangu umepungua, nilikuwa nataka kununuaq ndege binafsi ya kutembelea, kwa hali ya kipato changu cha sasa, sina uwezo wa kufanya hivyo, mbaya zaidi tayari nilishatamba kwa watu kwamba nitanunua ndege, nisipomnunua wataniona mimi ni maskini” alijisemea. [176]
vibali
Ramani wanazoombea vibali vya ujenzi, sio wanazotumia kujenga. [177]
vifaa
Uagizaji wa bidhaa kama vifaa vya usafiri na ujenzi na mafuta ulipanda katika kipindi hicho, benki hiyo ilisema. [178]
vitendo
Alibainisha kuwa lengo kubwa la kusambaza elimu kwa vitendo ni , kuendeleza zao la soya mkoani Morogoro kwa kutumia teknolojia zilizobuniwa. [179]
vyakula
Wanaendelea vizuri, wanakula sawasawa vyakula ambavyo vina asili ya Tanzania ingawa maandalizi yake kwa hapa hotelini si mazuri kwa kiasi tunachotaka,îalisema daktari wa Stars, Juma Sufian. [180]
wa
Kauli ya Makamba imekuja siku moja baada ya Sheikh Yahya Hussein kuitabiria CCM mpasuko na kueleza kuwa Serikali itakayoundwa mwakani, itakuwa ya umoja wa vyama vya siasa. [181]
wako
Peter Mzirai, Mwenyekiti wa PPT Maendeleo taifa, alitamka wazi kuwa chama chake kina muunga mkono Mponzi na kwamba wako tayari kushirikiana katika kampeni Mbeya Vijijini. [182]
wale
Lakini nikaja kugundua kuwa ile ya wale kuongea ndiyo dawa yenyewe tofauti tu ni kwamba huenda hawa watu hawakuwa wawazi baina yao wakiwa pekee yao, labda mmoja alishindwa kujieleza. [183]
walimu
Na siyo walimu tu. [184]
wameleta
Watu wameleta mapendekezo yao. [185]
wao
Alifafanua kwamba, wao walishasema na hawatabadilisha msimamo wao wa kutoshiriki vikao vya muungano huo kwa kuwa hakuna umoja wa dhati. [186]
wapi
Pale unatakiwa mstari mmoja tu wa kwenda mjini lakini wapi. [187]
waziwazi
Alisema waziwazi kuwa baadhi ya wanasiasa wanatumia Sheria ya Ardhi kudhulumu wafugaji. [188]
wetu
Tulikuwa ugenini kila mtu alikuwa akiwashangiliwa wapinzani wetu na kuwapa wakati mgumu wachezaji wangu tunashukuru tumefuzu kwa hatua ya nusu fainali. [189]
wote
Jumla ya watahiniwa 102,184 sawa na asilimia 26 ,5 walishindwa mtihani wakiwemo wasichana 57,461 sawa na asilimia 14.9 na wavulana walikuwa 44,723 sawa na asilimia 11.6 ya watahiniwa wote. [190]
yenye
Alisema timu ya Azam ni mfano mzuri wa kuigwa na timu nyingine kutokana na uongozi wake kufanya vizuri na ni timu yenye viongozi wazuri kuanzia kocha mpaka benchi la ufundi ndio sababu inayofanya vizuri kila siku. [191]
yetu
Maana yake ni kwamba, katika kipindi hicho kulikuwa na mahitaji makubwa ya fedha za kigeni na hii inasababisha fedha yetu kuporomoka na kuibuka kwa mfumuko wa bei. [192]
yuko
Mchizi fundi bwana, mambo ya wayaringi kwenye mabangaluu ya walioshtuka kujenga mwaka huu, mchizi anarekebisha na kusema kweli kazi anainyaka, yuko freshi lakini sasa kitu kimoja kikamshinda mwanangu, hawezi kukataa ishu, yaani kila simu anayopigiwa, watu wakimuuliza una chansi mchizi anajibu ndio. [193]
yule
Hakuna jambo la kukufanya tusikutangaze kama mgunduzi wa dawa kuponya kansa kwenye moyo, dawa yako tulimpa hadi mtoto wa rais na amepona, rais anataka akuone kukushukuru na kupanga sherehe kubwa ya uzinduzi wa dawa hii ya aina yake,” alisema waziri wa afya wa nchi hiyo siku moja alipokutana na kijana yule mwenye ulemavu wa ngozi. [194]
yupo
Hakuna mgogoro wowote kati ya uongozi na mwalimu kila kitu kinakwenda kama kilivyo na mwalimu yupo ataendelea kuwepo na atakinoa kikosi kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, kwa kifupi Yanga ni shwari,"alisema Madega. [195]
za
Maeneo yaliyotoa mchango mkubwa katika sekta hiyo ni huduma za kifedha, viwanda na mawasiliano. [196]
zangu
Ndugu zangu wajumbe, tujitahidi kuwaelimisha wananchi na viongozi wa serikali za vijiji, ili wasaidie kukomesha vitendo vya baadhi yetu kufukua mabomba ya chuma na kuyauza kama chuma chakavu," alinena Njwayo. [197]
zenu
Zaidi nataka niwatakie mwaka mwema wenye baraka kwenu na kwa familia zenu, nataka pia niwakumbushe kuwa huu unaweza kuwa mwaka wa neema kwa watakao jishughulisha. [198]
zetu
Tunaogopa kuingiliwa, ndio maana tukaamua kusajili jukwaa kama kampuni kwani tutafanya kazi zetu kwa nafasi kubwa bila ya kupata bughudha kutoka kwa yeyote," alisema. [199]
zote
Kocha wa Uganda, Bobby Williamson alisema mchezo wa leo utakuwa hasa kutokana na morali ya timu zote mbili lakini atatumia kikamilifu viungo wake. [200]