Nenda kwa yaliyomo

tabianchi

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru

Kiswahili

[hariri]
Ramani ya dunia inayoonyesha kanda za tabianchi kuanzia ikweta: tropiki, yabisi, wastani, kibara na baridi.

Nomino

[hariri]

tabianchi

Pronunciation

[hariri]

  1. Tabianchi (Kiing. climate) inamaanisha jumla ya halijoto, unyevuanga, kanieneo ya angahewa, upepo, usimbishaji na tabia nyingine zinazoathiri hali ya hewa katika sehemu fulani ya uso wa dunia kwa muda mrefu.
  2. Tabianchi ni tofauti na halihewa ikitazama vipindi virefu lakini halihewa inatazama hali ya sasa au katika muda mfupi. Kwa lugha nyingine tunaweza kusema: Tabianchi ni jumla ya halihewa zote zinazoweza kutokea mahali pamoja duniani katika kipindi kisichopungua miaka 30.

Tafsiri

[hariri]