Nenda kwa yaliyomo

nomino za pekee

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru

Nomino za pekee pia huitwa nomino za maalum nomino hizi ni majina mahususi ambayo yanatambulisha viumbe,mahali,au vitu mf. Abdi, Nairobi, Bahari Hindi, Ziwa viktoria,

Mifano ya nomino za pekee ni pamoja na

1.Nomino zunazotaja majina ya watu:John,Mary,Martin

2.Nomino zinazotaja majina ya siku za wiki mf. Ijumaa, Alhamisi, Jumapili.

3.Nomino zinazotaja majina ya miezi: Julai, Mei

4.Nomino zinazotaja majina ya Mlima: Mlima Kenya, Mlima Longonot

5.Nomino zinazotaja majina ya nchi: Kenya, Uganda, Tanzania

6.Nomino zinazotaja majina ya mito: Mto Yala, Mto Nyamidi, Mto Nzoia

7.Nomino zinazotaja majina ya Maziwa Ziwa turkana Zima Nakuru

8.Nomino zinazotaja lugha: Kiswahili, Kiingerza

Kiswahili

[hariri]
  1. Nomino za pekee ni maneno yanayotaja majina mahususi ya watu, mahali au vitu ambavyo vina sifa ya pekee. Maneno hayo yanapoandikwa lazima yaanze na herufi kubwa mwanzoni.

Tafsiri

[hariri]
ina makala kuhusu:

Ingizo hili ni sehemu ya mradi wa Kuboresha Wikipedia na Wikamusi ya Kiswahili. Unaweza kusaidia kuihariri na kuongeza maana.