Nenda kwa yaliyomo

kistari kifupi

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru

Kisawe cha kistari kifupi ni kistari. Kistari ni nomino. Kistari kiko katika ngeli ya ki-/vi-. Kistari ni mstari mfupi unaotumika kuunganisha maneno mawili au unaotiwa mwishoni mwa mstari kuonyesha neno linamalizikia mstari unaofuata.

Matumizi ya kistari kifupi. 1. Kuunganisha maneno au kutenganisha maneno yanayoandikwa kwa mwambatano. Kwa mfano: isimu-jamii. 2. Hutumiwa mwishoni mwa mstari kuonyesha neno linamalizikia mstari unaofuata. Hapa silabi ndizo hutenganishwa. Kwa mfano:Jana nilimwona mwalimu wetu huko so-

koni. 3. Kutenganisha silabi. Kwa mfano:Ni-na-so-ma. 4. Kudokeza jambo muhimu kuhusu neno, kama vile mzizi. Kwa mfano: -eusi. 5. Kudumisha sauti wakati neno linapotamkwa kwa kuvutwa. Kwa mfano: masala-a-a-a-le! 6. Hutumika katika tarakimu kuonyeasha mwanzo hadi mwisho. Kwa mfano: mwaka 1914-1918.