Nenda kwa yaliyomo

kinyota

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru

Kinyota ni nomino. Wingi wa kinyota ni vinyota. Kinyota kiko katika ngeli ya ki- /vi-. Kinyota ni ishara inayofanana na nyota iwekwayo juu ya neno kuonyesha haja ya kulizingatia wakati wa kuandika.

Matumizi ya kinyota. 1. Kuonyesha kuwa maendelezo ya neno fulani yana makosa. Kwa mfano: *kitaabu. 2. Kuashiria kuwa mpangilio wa maneno katika sentensi una makosa. Kwa mfano: *mamangu sokoni leo amekwenda saa sita. 3. Kuashiria msomaji kuhusu jambo fulani ambalo maelezo yake yanapatikana sehemu ya chini ya ukurasa huo. Kwa mfano: *liwato. 4. Kuonyesha kuwa sentensi au fungu la maneno lina makosa ya kisarufi. Kwa mfano: *mtoto chetu kinalia.

.....................................................................................................................................................................................................................

  • tako la bunduki.