Nenda kwa yaliyomo

daladala

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru

Swahili[hariri]

Nomino[hariri]

Kiswahili

daladala (wingi daladala)

  1. Basi dogo la abiria linalotumika kama njia ya usafiri wa umma katika baadhi ya nchi, hasa katika maeneo ya Afrika Mashariki.

Asili ya neno[hariri]

Miaka ya 1980 kulikuwa na usafiri huu. Bei yake ilikuwa shilingi tano ya Tanzania kutoka Kariakoo hadi Temeke Mwembeyanga. Kondakta alikuwa akitangaza dala dala kwenda Kariakoo. Dala ni kisawe cha shilingi tano. Baadaye ikatoka kuwa pesa hadi gari.

Mifano[hariri]

  • Nilisafiri kwa daladala kwenda kazini leo asubuhi.