alika
Mandhari
Kiswahili
[hariri]kitenzi
[hariri]alika
- toa sauti ya kishindo kama vile mfyatuko wa risasi au mpasuko wa kitu
- ita watu waje kwenye sherehe; karibisha
- tangaza
- pia alisa; weka mgonjwa, mwari, na kadhalika mahali kwa sababu maalum; tawisha
misemo
[hariri]alika mgonjwa- tawisha mgonjwa ili kumfanyia dawa
alika mwari- weka mwanawari ndani kwa muda wa siku kadhaa kabla ya kuolewa
alika mvulana/msichana- weka ndani mvulana au msichana ili kumfunda jandoni au unyagoni
nomino
[hariri]alika pia arika mwanamke au mwanaume ambaye amepata mafunzo jandoni au unyagoni