nywea
Mandhari
Nywea ni kitenzi
Sielekezi
Maana ya kwanza ya nywea ni kunjamana na kauka kwa kukosa maji; sinyaa.
Maana ya pili ya nywea ni jikunyata kwa hofu au wasiwasi.
Maana ya tatu ya nywea ni kuwa katika hali ya kukosa nguvu; dhii, dhoofu, fifia.
Maana ya nne ya nywea ni pungua uvimbe au ukubwa; kuwa dogo kuliko ilivyokuwa; pwea au pojaa.
Nywea inaweza kunyambulika na kuwa nyweka, nywelea na nywesha.
Nywea ni neno halisi la Kiswahili.
Marejeleo
Said H. K. et al.(2014), "Kamusi ya Kiswahili Sanifu. TOLEO LA 3. TATAKI iliyokuwa TUKI." OXFORD UNIVERSITY PRESS. uk. 447.