Biogesi

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru

Kiswahili[hariri]

Mchoro wa biogesi

Nomino[hariri]

  1. Biogesi ni gesi inayozalishwa na bacteria wanapovunjavunja malighafi zinazooza kwa urahisi kama vile kinyesi cha ng’ombe na mifugo wengine, na mabaki ya jikoni, yanapowekwa kwenye sehemu isiyokuwa na hewa ya oksijeni. Nishati hii inaweza kutumika kwa kupikia pamoja na kuwasha taa majumbani.
  2. Biogesi, chanzo cha nishati na mbolea hai.Hii ni aina ya nishati inayosaidia kupunguza uharibifu wa mazingira na inazalisha mbolea ya mboji ambayo imethibitishwa kurutubisha udongo.

Soma zaidi[hariri]