mawaidha

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru

Kiswahili[hariri]

Nomino[hariri]

mawaidha

  1. maneno ya kumpa mtu mwelekeo mzuri

Ni maneno ya maonyo au mafunzo.

Visawe vyake ni mausia, mashauri na waadhi.

Mfano:

Ipe maisha yako msingi madhubuti kwa sababu maisha ni kama jengo na jengo likikosa msingi madhubuti hutetereka na hatimaye huanguka.

Kuwa kielelezo kwa taifa zima.

Tamu ikizidi tamu huwa si tamu tena. Yaani usifanye israfu.

Kuwa na bidii katika kazi ili upate kufurahi.

Kuwa tulivu.

Kuwa makini.

Kuwa na nidhamu kwani kijengacho mtu ni utu au ubinadamu au uja.

Zingatia adabu na matumizi mazuri ya lugha.

Jiweke katika hali nadhifu.

Kuwa mwangalifu katika kuwachagua marafiki zenu. Mcheza na tope humruka.

Kuwa na udugu. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.

Ukilima pantosha, utavuna pankwisha.

Tafsiri[hariri]