Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-02-17

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aidha
Alisema utata uliopo katika sheria hiyo unatokana na watumishi aidha kuachishwa kazi au kujiuzulu. [1]
aina
Vifaa ilivyokabidhiwa ni pamoja na sare za makocha, jezi seti moja aina ya Umbro pamoja na jezi maalum kwa ajili ya mazoezi ya timu hiyo ambayo hufanyika katika Uwanja wa Chuo cha Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam. [2]
ajue
Kwanza, Dk Slaa ajiulize ni mara ya kwanza kuwekewa kadude ka tekinolojia ya kisasa chumbani kwake? Kama hivyo ndivyo, basi ajue hiyo ni Happenstance ya James Bond. [3]
akisema
Ungemsikia mmoja wetu akisema: “Huwa inaanza na namba zinajihesabu kurudi chini. [4]
albino
NI ukweli usiofichika kuwa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, albino, na haikushangaza kuona kwamba wamefikia hatua hata ya kuamuru hatua kali zilizotiliwa shaka na baadhi ya wananchi zichukuliwe dhidi yao ya wauaji hao. [5]
ama
Hata hivyo Ngawaiya ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM mkoani Kilimanjaro, alilikataa ushauri huo wa Mrema na kwamba ilikuwa mapema kwake kuzungumzia ama atawania au hatawania ubunge katika jimbo hilo. [6]
amani
Bilikesi alisema kuwa walimu walikuwa wamepanga kufanya maandamano ya amani kulaani kitendo cha mkuu huyo wa wilaya ya Bukoba cha kuwachapa walimu viboko, na kuwa kunyimwa kibali cha kufanya hivyo ni kunyimwa haki yao ya kujieleza na kutoa hisia zao. [7]
ambao
Kuhusu hatua za kisheria ambazo anaweza kuchukua dhidi ya watu ambao anadai walilenga kumchafua, Masha alisema hadi sasa ameshawasiliana na kampuni ya Uwakili ya Emma, kufanya uchambuzi wa kisheria kuona namna ya kushughulikia jambo hilo. [8]
anapata
Lengo la mahakama hapa lilikuwa ni kuona mrufani anapata haki zake zote stahili ambazo angezipata kwa mrufaniwa wa kwanza baada ya kufuata utaratibu muafaka kuvunja mkataba wa kazi. [9]
atakuwa
Makamu Mwenyekiti wa Chaneta, Shyrose Bhanji aliiambia Mwananchi jana kuwa katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Emmanuel Nchimbi atakuwa mgeni rasmi. [10]
au
MKURUGENZI wa zamani wa utawala na utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, Amatus Liyumba, ambaye anakabiliwa na kesi ya kutumia vibaya madaraka na kuisababishia serikali hasara, jana alilazimika kurejea kulala mahabusu kutokana na kasoro zilizobainika kwenye hati za mali, ikiwa ni pamoja na kama neno "ship" linamaanisha kondoo au meli. [11]
baina
Awali Jintao alisema kwamba mbali ya mabadiliko yanayoikumba dunia katika nyanja mbalimbali, uhusiano na urafiki baina ya nchi hizo ulioanzishwa mwaka 1964, umeendelea kukua na kuneemeka. [12]
bali
Kuhusu kilichoitupa nje Sagem Securite katika hatua ya awali ya mchakato, Masha alisema hiyo haikutokana na kukosa sifa au uwezo, bali ni kuvuja kwa taarifa kutokana na nyaraka iliyonyofolewa hivyo kuathiri taratibu za kisheria za zabuni ambazo ni siri. [13]
bara
China itatekeleza ahadi yake ya kutopunguza msaada wake kwa Afrika na kuishawishi jumuiya ya kimataifa kuheshimu ahadi zao kwa bara hili,"alisema Jintao akirejea mwelekeo wa mataifa mengi makubwa, kufikiria kupunguza misaada yao kwa nchi zinazoendelea kutokana na matatizo makubwa ya kiuchumi yaliyozikumba nchi hizo. [14]
bila
Kufuatia mkanganyiko huo wa kiutawala, walimu kumi waliotambuliwa na utumishi waliingizwa kwenye kompyuta na kulipwa mishahara yao ambapo wengine 32, walijukuta wakiishi maisha magumu bila mshahara hadi sasa. [15]
bosi
Kuhusu barua ambayo alimwandikia Waziri Mkuu Mizengo Pinda Desemba mwaka jana, alisema: "Ilikuwa ni kutoa taarifa kwa waziri mkuu ambaye ni bosi wangu katika shughuli za kila siku za kiserikali. [16]
cha
Baadhi ya masharti ya dhamana kwa washitakiwa hao ni kutoa nusu ya pesa zilizoibwa kama dhamana ambayo ni zaidi ya Sh55 bilioni kwa kila mmoja au hati ya mali yenye thamani ya kiasi hicho cha pesa. [17]
chao
Joseph Kuzilwa aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa taarifa hizo si za kweli na kwamba taratibu zote za kisheria na kiithibati zilifuatwa katika uanzishwaji wa chuo chao. [18]
cheti
Inakuwa utata zaidi pale halmashauri hiyo inapokuwa na mtu anayekaimu kama wala hana cheti cha uhasibu. [19]
dhati
Aliongeza kuwa uhusiano huo wa dhati na wa kujivunia unaonyesha mfano wa mshikamano na ushirikiano kati ya China na bara la Afrika na kati ya nchi mbili hizo katika nyanja mbalimbali. [20]
dhehebu
Katiba ya Bolivia inatambua dhehebu la Katoliki kuwa ndio dhehebu pekee linalotambulika nchini lakini katika marekebisho ya katiba madhehebu mengine yatatambuliwa. [21]
dunia
Alisema mabadiliko ya hali ya hewa duniani ni wastani wa mabadiliko hayo kwa muda mrefu kutokana na shughuli za binadamu na kwamba yanatishia maisha ya mwanadamu, si Tanzania pekee bali dunia nzima. [22]
endapo
Nilichojaribu kufanya ni kuepusha lawama kutoka kwa Watanzania hapo baadaye endapo mambo yangeharibika. [23]
enzi
ZIARA ya Rais wa China, Hu Jintao nchini, imekuja na neema ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili uliojengwa tangu enzi za Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na kiongozi wa kwanza na muasisi wa China, Mao Tse Tung. [24]
es
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika mkutano maalumu na wahariri na wawakilishi wa wahariri wa vyombo vya habari, Masha alisema ameamua kuvunja ukimya baada ya kuona mchakato huo sasa unazungumzika hadharani na kwamba yuko tayari kujiuzulu kama kuna uthibitisho wa yeye kuingilia zabuni. [25]
eti
Mimi sioni sababu ya kumwadhibu DC eti kwa sababu kawapiga walimu, ni haki yao,” alisema Lianda. [26]
fainali
Bhanji alisema kuwa wachezaji na viongozi wa JKT watatuzwa kwa kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati baada ya kuifunga NIC ya Uganda katika fainali kwenye Uwanja wa Zimamoto, Zanzibar. [27]
feki
Kuzilwa amekanusha taarifa za kuwepo kwa wahadhiri wenye vyeti feki vya uzamivu katika chuo chake na kuongeza kuwa habari hizo hazikufanyiwa uchunguzi. [28]
gani
Vifaa hivyo vilikabidhiwa jana kwa uongozi wa Taswa FC na kupokelewa na mwenyekiti wake, Majuto Omary ambaye alisema uamuzi huo wa kampuni ya Vuvuzela kuwasaidia uomeonyesha namna gani inavyojali michezo. [29]
gesi
Muyungi alisema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea duniani hivi sasa, yametokana na shughuli mbalimbali za binadamu, zikiwemo za viwanda vinavyozalisha gesi zenye sumu zinazochangia mabadiliko hayo. [30]
gharama
Gharama nyingi na kwa mantiki hiyo rasilimali muhimu za taifa zinaishia kwenye majengo, mishahara na gharama nyingine za uendeshaji ambazo kwa hivi leo kuporomoka kwa uchumi wa dunia kunadhihirisha hazihitajiki na hazistahili kukubalika. [31]
hafla
CHAMA cha Netiboli Tanzania, Chaneta, leo kitatoa zawadi mbalimbali kwa wachezaji na viongozi wa JKT Mbweni kwa kutwaa ubingwa wa netiboli Afrika Mashariki, hafla itakayofanyiuka kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. [32]
haina
Mapinduzi ya TEKNOHAMA yanaandikwa kwenye ukuta kwamba: "Benki kama zilivyo leo zimepitwa na wakati na kuwa ni sawa na ile mijusi mikubwa 'dinosaurs' na haina tena nafasi katika karne ya 22 hapa duniani. [33]
hakimu
Wakili Membar alihoji ni kwa nini kesi hiyo imekuwa ikicheleweshwa kuanza kusikilizwa bila sababu za msingi na kumwomba hakimu Euphemia Mingi kuifuta. [34]
halifai
Matumizi ya neno uhalisia halifai kutumika hapa. [35]
hana
Hata hivyo Ngawaiya alipohojiwa jana kwa njia ya simu na Mwananchi,alisema yuko tayari kuhojiwa na kikao chochote cha chama chake (CCM) kwa sababu hana kosa lolote alilofanya na wala hajamdhalilisha kiongozi yeyote kupitia vyombo vya habari. [36]
hao
Ijumaa, rufaa ya Liyumba na mwenzake ya kutaka wapunguziwe masharti ya dhamana ilitupwa Mahakama Kuu na washtakiwa hao wakarudi mahabusu na jana Liyumba alionekana kujiandaa kurudi uraiani, lakini kasoro hizo zilimrejesha rumande. [37]
hapa
Walimu mkoani hapa walikuwa wamepanga kuandamana jana lakini maandamano hayo hayakufanyika kutokana na kutopata kibali cha Jeshi la Polisi, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Chama cha Walimu cha Kagera, Dauda Bilikesi. [38]
hasa
Alisema ni vigumu kuweza kubaini nani hasa amenyofoa nyaraka hiyo ya siri, kwani hupita katika mikono ya watu wengi, lakini akaonya kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua. [39]
hatua
Kampuni zilizovuka hatua ya awali ya mchujo ni Unisys ya Afrika Kusini, Giesecke& Devrient Fze ya Dubai na Iris Corporation Berhad ya Malysia. [40]
hawa
Wataingia mkataba na wachezaji hawa kwa nyakati tofauti, Henry baada ya kumalizika faibnali za CHAN wakati Izuchukwu atasajiliwa baada ya makubaliano na klabu ya Simba na pia baada ya kufikisha miaka 18,î alisema. [41]
hawezi
Hata hivyo, Waziri Masha alisema Mpigachapa wa Serikali hawezi kupewa tenda hiyo kwa kuwa hakujaza fomu za maombi. [42]
hayo
Zipo taarifa kuwa maeneo hayo kuna wakimbizi wananunua vyeti vya kuzaliwa. [43]
hewa
MAISHA ya Watanzania yamo hatarini kukumbwa na magonjwa, kutokana na ongezeko la kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani. [44]
hii
Mheshimiwa hakimu, mimi naona kesi hii imekuwa ikicheleweshwa kwa makusudi na upande wa mashtaka, hivyo nakuomba uifute endapo watashindwa tena kuleta vielelezo", aliomba wakili Membar. [45]
hiki
Kusema kuwa chuo hiki hakikufuata utaratibu wakati wa kuanzishwa kwake kuwa Chuo Kikuu ni kudharau mamlaka za kitaifa na kimataifa ikiwamo Kamisheni ya Vyuo Vikuu (TCU) na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema. [46]
hili
Alisema habari zilizochapishwa katika gazeti moja litolewalo kila siku (siyo hili) siyo sahihi na kwamba zinaweza kupotosha umma kuhusu chuo hicho. [47]
hizi
Akithibitisha kutokea kwa mgongano huo, Afisa elimu wa wilaya ya Same, Deosdedit Bimbalirwa alimwambia mwandishi wa habari hizi jana ofisini kwake kuwa kweli walimu hao hawajalipwa, lakini akadai wanaohusika na tatizo hilo siyo wilaya yake. [48]
huduma
Kiwanda cha Sukari TPC na kuboresha huduma za elimu na afya. [49]
humo
Hata balozi wa Nigeria nchini alithibitisha kuwa kampuni hiyo iliwahi kukumbwa na matatizo, lakini akasema bado inafanya miradi mingi mikubwa nchini humo. [50]
huo
Masha ameibuka kuzungumzia tuhuma zake siku moja baada ya Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani kutaja kampuni sita zilizopita ngwe ya kwanza ya mradi huo uliotengezewa zaidi ya Sh200 bilioni, huku Sagem Securite ikiwa imetupwa nje ya mchakato. [51]
husika
Ni Chuo Kikuu halali kinachotambulika na mamlaka husika za kitaifa na kimataifa,” alisema Prof. [52]
huu
Liyumba na Kweka walipandishwa kizimbani Januari 27 mwaka huu kwa kutuma za kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia seriakli hasara ya zaidi ya Sh221 bilioni na hadi leo bado hawajapata dhamana. [53]
huwa
Mapinduzi yoyote makubwa yanapotokea wale waliokuwepo huwa vipofu na wamefungwa fungwa na mazoea na desturi kiasi cha kutojua au kuamini kuwa kile kinachotokea kweli kinatokea na kitatokea. [54]
huyo
Kuhusu safari yake Geneva, Uswisi iliyoripotiwa kuwa ilikuwa Oktoba mosi, waziri huyo alisema siku hiyo alikuwa akitokea Hong kong kupitia Dubai kurejea nchini. [55]
ibilisi
Tunaona nchi nyingine zikielekea kukutana na ibilisi lakini sisi ni tofauti. [56]
idadi
Mbali na mataifa hayo kufikiria kupunguza misaada yao kwa nchi changa, miradi mingi ya uwekezaji inaweza kupungua kutokana na msukosuko wa kifedha, hali kadhalika kupungua kwa idadi ya watalii ambao huziingizia nchi changa, hasa za Afrika mashariki fedha nyingi. [57]
ikawa
Ikawa asubuhi ikawa jioni siku ya kwanza. [58]
ikishirikiana
Nyingine ni Madras Security Printers ya India, Maruben Corporation ikishirikiana na Zetes na Nec ya Japan na Tata Consultancy Services ikishirikiana na na Ontrack Innovatives Limited ya India. [59]
ila
Unajua sisi kama wilaya walipokuja hao walimu, kabla ya kuanza kulipwa tuliwapatia posho ya kujikimu na kuwakopesha mishahara ya miezi miwili ya mwanzo, ila tulipoona mishahara inazidi kuchelewa na hazina yetu inazidi kukauka tulishindwa, tukaamua kuwapumzisha nyumbani wasubiri," alisema Afisa Elimu wa wilaya ya Same, Deosdedit Bimbalirwa. [60]
ile
WAZIRI wa Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) , Ally Juma Shamhuna amezitaka klabu za Miembeni na Mundu za visiwani humo kujifunza kutokana makosa baada ya kutolewa mapema katika Michuano ya Klabu Bingwa Afrika na ile ya Kombe la Shirikisho. [61]
ili
Maana, nilikaa kimya kuanzia katika mchakato na hadi katika kamati za bunge, ili kuheshimu sheria na taratibu, lakini akina Dk. [62]
iliyopo
Hatari iliyopo na ambayo bado inastahili kutathminiwa kwa mapana na marefu zaidi ni kwamba haiwezekani kuwa na wakuu wa mabenki ambao wanawategemea watu wa Teknohama kuelewa kile kinachoendelea katika biashara zao. [63]
in
Enemy in action). [64]
insha
Ninaitunuku makala hii kwa Leah Bourne rafiki katika mtandao na ambaye insha yake ya mwaka 1998 iliwaonya Wamarekani lakini hakuna aliyemjali wala kuzingatia aliyoyaandika wakati huo. [65]
iwe
Au kwa maneno mengine benki lazima iwe Teknohama, na Teknohama lazima iwe benki. [66]
japo
Kwa mara ya kwanza ningependa niwe tofauti na Waafrika wenzangu kwa kuthubutu kuchangia japo kwa ufinyu wa fikira na uzoefu wangu ninachoamini ndio njia sahihi ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya uchumi duniani leo. [67]
je
Cha kujiuliza hapa ni je, ndio mwisho wa safari? Na hivi kweli fedha za sarafu na karatasi bado zinahitajika kwa matumizi yote ya kiuchumi na kifedha. [68]
jumla
MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga wameendeleza ubabe wake dhidi ya timu ya Comoro, Etoile d'Or Mironsty kuisambaratisha kwa jumla ya mabao 14-1, baada ya jana ushindi wake wa 6-0 ugenini. [69]
juu
Ligi hiyo inashirikisha timu tisa ambapo timu tatu za juu zitafuzu moja kwa moja kucheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao. [70]
ka
Juzi huko Dodoma kulikuwa na habari kwamba kamekutwa kadude ka kisasa ka kunasia sauti vyumbani mwa wabunge wawili wa upinzani. [71]
kabla
Alifafanua kwamba alipata malalamiko kutoka kwa baadhi ya makampuni, ikiwemo Sagem Securite zikidai kwamba zimeenguliwa katika zabuni kabla ya mchakato kumalizika. [72]
kadhaa
Imani yetu ni kwamba, Vuvuzela imejitolea na kuna wadau kadhaa wanaweza kuendelea kusaidia michezo. [73]
kali
Ninachokiona mimi ni kuwa Obama, Brown na wenzake wanampa mgonjwa wa malaria kali panadol ya kutuliza maumivu kwa muda. [74]
karatasi
Baada ya hapo mwanadamu akagundua kuwa anaweza kutumia karatasi au sarafu kuwakilisha fedha fulani. [75]
karibu
WAKATI mgogoro wa kiuchumi ukiyasumbua mataifa makubwa na madogo duniani, Rais Hu Jintao wa China amesema nchi yake itaimarisha mawasiliano na ushirikiano wa karibu na Tanzania na nchi nyingine za Afrika, kwa lengo la kupunguza athari za mgogoro huo, huku akitangaza msaada wa kifedha, kielimu. [76]
kata
Helleni Lianda, mkazi wa kata Kashai katika manispaa ya Bukoba, alisema kuwa wapo baadhi ya walimu ambao wanafanya kazi zao kwa kufuata misingi na taratibu za kazi, lakini walimu walio wengi wamejiingiza katika biashara na kuwa wanapaswa kuchagua moja, kama kuingia madarasani kufundisha au kufanya biashara. [77]
kati
Kwa mwaka 2007 peke yake, biashara kati ya mataifa hayo mawili ilikuwa kwa asilimia 48 na kufikia Dola 800 milioni za Kimarekani (sawa na karibu Sh1 trilioni). [78]
kauli
MWENYEKITI wa chama TLP,Augustine Mrema, amemzulia matatizo mbunge wa zamani wa Moshi Vijijini kwa tiketi ya chama hicho, Thomas Ngawaiya, kufuatia kauli za kiongozi huyo wakati akimuomba Ngawaiya, ajiondoe CCM na kurudi TLP, ili awanie ubunge wa jimbo hilo. [79]
kijamii
Kuna viongozi wachache sana ambao wanakaa wakawaza na kuwazua ni nini kinachoweza kufanywa na Teknohama leo na kesho katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi, kijamii, kiteknolojia na kiutamaduni. [80]
kile
CHAMA cha Wanafunzi wa Shule za Sekondari Tanzania (TASSA), kimeandaa maandamano makubwa yenye lengo la kushinikiza kuvunjwa kwa Baraza la Taifa la Mitihani, kwa kile kilichodaiwa kuwa ni, utendaji mbovu unaosababisha lishindwe kudhibiti wizi wa mitihani. [81]
kilimo
Kwa mujibu wa mchanganuo wa fedha hizo, Sh20 bilioni zitatumika katika kuimarisha kilimo, elimu na miundombinu Tanzania Bara na Sh4.5 bilioni kuendeleza miundombinu na teknolojia ya habari Zanzibar. [82]
kimsingi
Wakala wa wachezaji hao, Meddy Remtullah alisema jana kuwa kimsingi wachezaji wake wamefanikiwa katika majaribio na kitakachofuata ni uamuzi wa viongozi wa klabu. [83]
kinachoendelea
Inawalazimu rais au waziri mkuu wa nchi angalau kwa mwezi kama sio wiki kujua ni nini kinachoendelea. [84]
kipekee
Naye Rais Jakaya Kikwete alisema Tanzania na China zimenufaika kutokana na uhusiano baina ya nchi hizo, ulioanzishwa na viongozi watangulizi na kwamba, Tanzania itaendeleza uhusiano huo wa kipekee na China ili kujenga mshikamano zaidi. [85]
kocha
KUREJEA nchini kwa nahodha wa Taifa Stars, Henry Joseph na kuanza mazoezi kiungo Athuman Iddi 'Chuji' kumempa ahueni kocha Marcio Maximo aliyekuwa na kazi ya kuteua wachezaji wa kuziba pengo la nyota hao kabla ya kuelekea Ivory Coast kwenye michuano ya CHAN mwisho wa wiki. [86]
kote
Kwa mujibu wa Matefu leo zimebaki siku kumi, ili muda ambao chama hicho kiliutoa Alielezea matumaini yake kuwa maandamano hayo yataungwa mkono na watu wengi kote nchini wakiwemo wazazi na wadau wa elimu. [87]
kuandika
Katika mazungumzo ulinganishi wa mambo mabaya na madudu unaweza kukubalika kwenye mazungumzo lakini katika maandishi ya kawaida haikuwa lazima kuandika madudu badala ya mambo mabaya. [88]
kuandikwa
Limelazimishwa kwa kufanywa jina na kuandikwa kutokana na neno kudorora kwa maana ya kuharibika. [89]
kudai
Mwenyekiti huyo aliwaomba wadau mbalimbali wa elimu, wanasiasa na wazazi, kusaidia harakati hizo za kudai haki ikiwa ni pamoja na kuwaunga mkono wanafunzi katika maandamano yao. [90]
kueleza
Msomaji wa kawaida anapata tabu kidogo kumwelewa mwandishi anachokusudia kueleza. [91]
kujua
Kwa sababu za nafasi katika makala haya nitaongelea tu juu ya mfumo wa benki, mathalani, katika nchi yetu na fursa za kipekee zilizoletwa na Teknolojia ya habari na mawasiliano (Teknohama) bila wengi wetu kujua kuwa benki zinastahili kuwa teknohama na yenyewe inastahili kuwa benki. [92]
kuliko
Kuna ukweli kiasi fulani lakini ninaamini kuwa Teknohama ni kubwa kuliko benki zote zikiwekwa pamoja. [93]
kumi
Mwaka jana ,ofisi ya elimu mkoa wa Kilimanjaro ilielekeza walimu 42 kupangiwa vituo vya kazi katika wilaya hiyo, lakini baadaye Idara ya Utumishi ikadai kuwa walimu hao walipangwa kwa makosa badala yake walitakiwa kupangwa walimu kumi pekee wilayani hapo. [94]
kumpa
Chuji na Henry ambao walikosa mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na Zimbabwe iliyochezwa Jumatato iliyopita na kumalizika kwa suluhu, nafasi zao katika kiungo zilionekana kuwa wazi na kuifanya Stars kupwaya na kumpa wakati mgumu Maximo wa nani wa kufiti katika nafasi hizo. [95]
kundi
Imeelezwa kuwa mpasuko huo unatokana kuwepo kwa kundi la wanachama linaloafikiana na Mrema kuhusu Ngawaiya kufanya kazi nzuri katika kuwahudumia wapiga kura wakati akiwa mbunge wa Moshi wa Vijijini. [96]
kupoteza
SEKTA ya afya ni moja ya eneo ambalo watumishi wake wanatuhumiwa kuendekeza rushwa na kusababisha watu wengi kupoteza maisha kwa kukosa huduma muhimu ya matibabu. [97]
kuu
Baya zaidi ni kuwa kuna baadhi ya benki kuu ambazo bado hazijakubali kuwa Teknohama ni rasilimali muhimu wanayostahili kuwa nayo, kuitumia kikamilifu na kuienzi na kwamba asilimia kubwa ya watu wao wanastahili kuwa wale wanaojua Teknohama na Taaluma ya Fedha kwa pamoja. [98]
kuwepo
Kuhusu taarifa za kuwepo tuhuma za utapeli kwa kampuni ya Sagem Securite, alikiri kuzitambua baada ya kufanya uchunguzi. [99]
kwa
Hata hivyo, upande wa mashitaka ulioongozwa na wakili wa serikali, Justus Mulokozi ulipinga kupokelewa kwa hati hizo kwa madai kuwa zina kasoro. [100]
kwao
Ni viongozi wachache sana wanaojua kwa uhakika kila shilingi inayoingia na kutoka nchini kwao. [101]
kwenda
Dibo alifungiwa mwaka mmoja kutocheza mpira wa kikapu ndani na nje ya nchi na Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD) kwa kuikacha timu ya mkoa huo na kwenda kuchezea Mwanza katika mashindano ya taifa yaliyofanyika Oktoba mwaka jana. [102]
kwetu
Amekuja kwetu tumekaa naye na ameomba msamaha na tumefikiria tukaona kwa sababu amekubali kosa tumsamehe ili kunusuru kiwango chake. [103]
la
Kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea Liyumba, Profesa Mgongo Fimbo aliwasilisha hati hizo mbele ya Hakimu Mkazi Hadija Msongo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. [104]
leo
Hakimu Msongo aliahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea kusikilizwa kwa kuwa muda wa mahakama ulikuwa umekwisha. [105]
ligi
Tutapigana kadri ya uwezo wetu kuhakikisha tunashinda hiyo kesho (leo) mbali ya kuwa timu zote zinazoshiriki ligi hii zimeajiandaa," alisema Kanakamfumu ambaye hana muda mrefu tangu alipochukua jukumu hilo. [106]
liko
Niliona ni vema wenzetu PPRA watupe ushauri wa kitaalamu; watusaidie maana ni jambo ambalo lilikuwa liko ndani kwa ndani ya serikali," alisema. [107]
lipo
Tunataka Ngawaiya ahojiwe na vikao vya wilaya au mkoa,aseme ni kwa nini alizungumza na Mrema, lakini pia aeleze ni kwa nini amemdharau kiongozi wetu (jina lipo) wa wananchi mbele ya Mrema na waandishi wa habari"alisema Eliabu Damas. [108]
lugha
Kwanza hatukujua lugha waliyokuwa wakizungumza katika sinema zile. [109]
maana
Ndiyo maana haya nayaeleza leo. [110]
mabao
Miembeni ilitolewa katika Michuano hiyo na Monamotapa ya Zimbabwe kwa mabao 3-2 wakati Mundu iliondolewa mashindanoni baada ya kuchapwa mabao 7-0 na Red Arrows ya Zambia. [111]
mabaya
Na bila sisi kushirikishwa kwa ukamilifu na kwa uhakika mambo pengine yanaweza yakawa mabaya zaidi. [112]
machache
Nitawachokoza katika haya machache. [113]
madudu
Tunashuhudia madudu mengi sana hasa katika Kamati ya Uchaguzi na Kamati ya Nidhamu ambazo zilijikuta zikifanya uamuzi ambao unapingana na kanuni za soka. [114]
maeneo
Hapa nchini bado kuna wakimbizi hasa maeneo ya mipakani kama Kibondo, Karagwe na sehemu nyingine. [115]
magofu
Akaona kwamba watoto wengi walikuwa wanakufa hata kabla ya kufika kwenye magofu yale yaliyoitwa shule. [116]
makusudio
Pengine walioianzisha siku hii walikuwa na makusudio mazuri tu. [117]
maombi
Wiki iliyopita Jaji Projest Rugazia wa Mahakama Kuu alitupilia mbali maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na washitakiwa hao ya kutaka kulegezwa kwa masharti ya dhamana. [118]
mara
Mkuu huyo wa wilaya, alisema Wasomali hao, awatafikishwa mahakamani mara baada ya polisi kukamilisha uchunguzi wao, kuhusu kitendo chao cha kuingia nchini, isivyo halali. [119]
masuala
Tatizo ni serikali na udhibiti wa masuala ya kifedha. [120]
matokeo
Akizungumza na Shirka la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuhusiana na matokeo hayo, Shamhuna ambaye pia ni Naibu Waziri Kiongozi wa SMZ, alisema kuwa kimsingi kutolewa kwa timu hizo kunatokana na maandalizi hafifu. [121]
matukio
Anasema katika juhudi hizo, sekta ya ulinzi binafsi ipo tayari kuwalinda albino bila malipo kwa sababu imeguswa na matukio hayo. [122]
mauji
Mashirika mbalimbali ya kijamii yamekuwa yakipigia kelele na kukemea mauji hayo bila ya mafanikio huku matamko ya kulaani vitendo hivyo kutoka kwa viongozi wa dini yakigonga mwamba kwani vimekuwa vikizidi kuendelea kuripotiwa. [123]
mfuatano
Pili ni mfuatano wa maneno mpango mkakati. [124]
mimi
Lakini, kumbuka, mimi ni waziri wa mambo ya ndani, nina dhamana ya vitambulisho vya taifa, nisingeweza kukaa kimya wakati naona mambo yameharibika. [125]
miradi
Masha aliongeza kwamba, mwaka 2004, kampuni hiyo ilipewa miradi mbalimbali ndani na nje ya nchi hiyo. [126]
miungu
Ni wapendwa wa Mungu, ni wapenzi wa Mungu, ni miungu kabisa na sisi. [127]
mjini
WAKATI walimu wa mkoani Kagera wamenyimwa kibali cha kuandamana kuunga mkono uamuzi wa Rais Kikwete wa kumvua madaraka mkuu wa wilaya aliyechapa viboko walimu, wakazi wa mjini Bukoba wamedai hatua ya DC huyo ilikuwa sahihi katika kukomesha utoro uliokithiri wakati wa kazi. [128]
mkakati
Katika hatua za awali za kuwadhibiti wanyama hao, serikaki nchini Kenya inaandaa mpango mkakati unaolenga kujenga ukuta maalum. [129]
mpango
Mwenyekiti wa TSIA, Almasi Maige anasema askari wake wote wanaofikia milioni moja kutoka katika makampuni 460 nchini kote watahusishwa katika mpango huo wa ulinzi na kuongeza kuwa askari hao watafanya kazi hiyo sambamba na shughuli zao za kawaida katika malindo. [130]
msomaji
Sentensi hii haina maana na msomaji hataweza kuelewa kilichokusudiwa. [131]
mwa
Hata hivyo kauli hizo, zimezua mpasuko miongoni mwa wanachama wa CCM wa Wilaya ya Moshi Vijijini. [132]
mwajiri
Sasa basi, sheria zote hizi mbili zinakataza na kukemea kwa sauti kuu ya pamoja kwa mwajiri kumwachisha kazi mwajiriwa wake, au mwajiriwa kuacha kazi kienyeji tu bila ya kufuata taratibu za sheria. [133]
mzima
Tulijua sinema ingerudi tena kijijini kwetu baada ya mwaka mzima. [134]
nao
Marwa alisema katika mahojiano nao, watu hao wengine wakiwa na mikuki, walisema wametokea Kenya na kwamba waliingia katika hifadhi hiyo, katika jitihada zao za kutafuta ng'ombe wao walioibiwa hivi karibuni nchini humo. [135]
navigator
MSIE = navigator. [136]
naye
Mkuu huyo alienda kwenye shule tatu za Kansenene, Katerero na Kanazi na kumuamuru koplo wa jeshi aliyeambatana naye kuwachapa walimu hao viboko kwa makosa ya uzembe na kuchelewa kazini. [137]
ndio
Mimi nafikiri tatizo hapa ni maandali hafifu na ukosefu wa fedha, lakini kama unajua kabisa kwamba unatakiwa kushiriki michuano fulani basi unatakiwa kujiandaa mapema si unasubiri mpaka dakika ya mwisho ndio unaanza kuhangaika. [138]
ndizo
Manyema na Majimaji ndizo timu pekee katika ligi hiyo zilizowahi kushiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara. [139]
ng
Kama ambavyo kwa dini ya Wamaasai, Mmaasai hawezi kuiba ng’ombe kwa sababu Mungu wake kasema ng’ombe wote ni mali yake, vivyo hivyo hata kwa wanene wetu. [140]
ngozi
Kwa mujibu wa Richard Muyungi, Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), athari za mabadiliko ya hali ya hewa yakiwemo magonjwa ya ngozi, yanaweza kuwakumba Watanzania. [141]
nia
Tunapongeza na kuishukuru serikali ya China kwa msaada wake na nia yake ya kuendeleza ushirikiano wa kindugu baina ya watu wake na Watanzania ulioanza muda mrefu na kuinufaisha nchi hii katika maeneo mbali mbali ikiwamo ujenzi wa Reli ya Uhuru ya Tanzania na Zambia (Tazara), ambayo mpaka sasa inaashiria upendo wa ndugu zetu hao kwetu. [142]
nini
Najua linaweza kujitokeza swali la kwa nini sasa. [143]
nyuma
Sio tu kwamba Teknohama imewaacha nyuma viongozi wetu bali pia kile wanachokijua ni kile wanachoambiwa tu na wataalamu wa Teknohama. [144]
of
Mathalan, katika shauri la rufaa la mwaka 1996 kati ya Georgia Celestine Mtikila dhidi ya Registered Trastees of Dar es Salaam Nursery School na International School of Tanganyika Ltd. [145]
papo
Kuendelea kwa mauaji hayo kumefikia hatua ya kuwagawa hata wananchi, wengine wakitaka wauaji hao wachukuliwe hatua kwa kuuawa papo hapo na wengine wakipinga hatua hiyo kwa kusema inakwenda kinyume cha sheria za nchi. [146]
pia
Alisema pia hata hati ya kusafiria iliyotolewa mahakamani hapo inaonyesha kuwa imeisha muda wake wa kutumika. [147]
pili
HATUA ya pili ya Ligi ya Soka Daraja la Kwanza inaanza kutimua vumbi leo katika Uwanja wa Uhuru (zamani Taifa) jijini Dar es Salaam kwa kuzikutanisha Kijiweni ya Mbeya na Polisi Iringa, Manyema na Majimaji kwenye mechi ya ufunguzi. [148]
polisi
Taarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi zimesema kuwa, walimu hao walinyimwa kibali kutokana na kuhofia kuvunjika kwa amani. [149]
potofu
Mauaji hayo ambayo yanasababishwa na imani potofu za ushirikina si tu yanawafanya watu wenye ulemavu wa ngozi kuishi kwa shaka na kutokuwa na amani katika nchi yao, yanachafua kabisa taswira ya Tanzania kimataifa na kupoteza sifa ya kuwa kisiwa cha amani. [150]
raia
POLISI wilayani Same mkoani Kilimanjaro, wamewatia mbaroni raia tisa wa Somalia, wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, kinyume cha sheria. [151]
rais
Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti, wakazi hao walisema kuwa adhabu aliyoitoa rais kwa mkuu huyo haistahili, wakisema kuwa walimu hao walistahili adhabu hiyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya utovu wa nidhamu. [152]
roho
Tengeneza pesa, utapata mbingu yako papo hapo na kisha utafurahia mbinguni zaidi baada ya kukata roho. [153]
saa
Wakazi hao waliitupia lawama serikali iliyopitisha utaratibu wa walimu kupewa mikopo ambao wamesema umechangia kwa asilimia kubwa walimu kukiuka maadili ya kazi yao, ikiwemo kufanya biashara saa za kazi na kushindwa kufundisha. [154]
sana
Tumeziangalia hati lakini ni mapema sana kusema kuwa hatuna pingamizi kwa sababu lazima tufike na kuona mali au nyumba na kujiridhisha kama thamani iliyotajwa ni ya kweli,” alisema Mulokozi. [155]
sawa
Rais Jintao alikabidhi msaada wa Yuan 150 milioni sawa na zaidi ya Sh28 bilioni kusaidia Tanzania wakati huu ambao nchi mbalimbali duniani zimekumbwa na tatizo la kuyumba kwa uchumi. [156]
screen
Width = screen. [157]
sh
Alizitaja baadhi ya kazi hizo kuwa ni pamoja na kutetea maslahi ya wakulima wa kahawa, kuishawishi serikali kujenge ya Barabara ya Kibosho na kusaidia kulipwa kwa deni la sh. [158]
shaka
Mbunge huyo anafahamika sana kwa uzalendo wake usiotiliwa shaka na ujasiri wake katika kupigania yale anayoyasimamia. [159]
si
Waziri Masha pia alisema kuwa taarifa za vyombo vya habari kuwa alikuwa nchini Uswisi Oktoba mosi kuzungumzia tenda hiyo, si sahihi na kuonyesha nyaraka za kusafiria zinazoeleza kuwa siku hiyo alikuwa akitokea Hong Kong kuja Tanzania. [160]
sinema
WAKATI ule tukiwa wadogo tulipenda sana kufuatilia mambo ya sinema. [161]
sio
Mbali na asilimia kubwa ya watu waliohojiwa kuonekana kumuunga mkono mkuu huyo wa wilaya, wapo baadhi ambao wamesema kitendo cha kuwachapa viboko walimu sio cha kiungwana maana zipo taratibu za kumwajibisha mtumishi wa serikali anayeenda kinyume na taratibu za kazi, sio kumchapa viboko. [162]
soka
Henry alikuwa nchini Norway akifanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa na klabu ya Molde FC, wakati Iddi 'Chuji' alikuwa akisumbuliwa na majeruhi wa nyama ya paja. [163]
tangu
Wakazi hao wanadai kuwa walimu wengi wamejitumbukiza kwenye biashara binafsi tangu waanze kupata mikopo kutoka kwenye mabenki na hivyo kutumia muda wa kazi kwa shughuli zao binafsi badala ya kufundisha. [164]
tatu
Masha alisema katika jambo hilo, wanasheria wake wataangalia kama kuna ushahidi wa mtu wa tatu ukiacha mchapishaji na mhariri, ambaye amekuwa akichochea habari hizo alizoziita zimelenga kumchafua. [165]
tena
Mapema mwezi huu,Mrema akiwa ameongozana na wafuasi wake, alikwenda katika mgahawa wa Central Garden wa mjini Moshi, ambako alimkuta Ngawaiya na kumuomba mbele ya waandishi wa habari, arudi TLP na kuwania tena ubunge wa Moshi Vijijni, kupitia tiketi ya chama hicho. [166]
trekta
Mungu akaagiza, trekta ziwepo. [167]
tu
Hata hivyo, msaada huo si tu kwamba, umetolewa kwa ajili ya kutusaidia kukabiliana na hali ngumu ya maisha, bali ni changamoto kwa serikali yetu kutumia vizuri fedha hizo katika maeneo zilikoelekezwa na si kuziingiza kwenye miradi yenye mianya ya kifisadi. [168]
tusio
Na hata sisi tusio na uwezo ni sehemu ya ufumbuzi wa tatizo lililopo. [169]
uamuzi
Masha, ambaye alionekana kutokuwa na wasiwasi, alichambua tuhuma moja baada ya nyingine na kusema hajawahi kuwa na ukaribu na Sagem Securite ya Hispania zaidi ya kupokea malalamiko yao na kuongeza kwamba uamuzi wa kutaka ushauri wa Mamlaka ya Umma (PPRA), wakati mchakato ukiendelea, haukuingilia mchakato. [170]
ujao
Awali, mwendesha mashtaka wa serikali, Francis Mboya akitoa maelezo yake kwa hakimu mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Euphenia Mingi aliomba kesi hiyo isogeze mbele hadi mwezi ujao kwa kuwa jalada bado lipo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). [171]
ukata
Naam! Sisi maskini tutakatika na ukata tu hata baada ya kukata roho lakini matajiri wataukata kama walivyoukata hapahapa. [172]
ule
Rais Jintao alitia saini mikataba ya kiuchumi na Rais Kikwete, ukiwamo ule wa Tanzania na benki kubwa ya Exima ya China utakaotoa mikopo kwa miradi ambayo bado haijawekwa wazi. [173]
upya
Lakini Jintao alisema matatizo hayo hayataifanya China ifikirie upya uhusiano wake na nchi hizo na badala yake itaendeleza mikakati yake barani Afrika na kutimiza ahadi zake. [174]
ushindi
Akizungumza na Mwananchi, kocha mkuu wa Polisi Iringa, Joseph Kanakamfumu alisema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi. [175]
uwanja
Hivi karibuni ilijenga uwanja wa kimataifa wa michezo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 waliokaa, ukiwa umegharimu zaidi ya Sh53 bilioni. [176]
vifaa
Kweli tunajivunia hali hii, Vuvuzela imeonyesha uungwana wa hali ya juu kutokana na kutoa vifaa hivi ambavyo vitatusaidia kwa kiasi kikubwa katika maandalizi yetu ya mechi mbalimbali za ndani na nje ya Dar es Salaam. [177]
vijana
Kabwe alisema Masha anapaswa kujiuzulu ili kujenga heshima ya vijana kwani ameichafua na kuwafanya wasiweze kuaminika. [178]
vile
Kesho (leo) tunataka kuwapongeza wachezaji na viongozi wa JKT kwa kazi nzuri, lakini vile vile hatutaacha kuwapongeza Jeshi Stars kwa kucheza kwa nguvu vile vile hatutaacha kuwapongeza Polisi kwa kutwaa ubingwa kwa wanaume,î alisema Shyrose ambaye aliahidi kutoa Sh1milioni kwa timu bingwa kati ya hizo. [179]
vizazi
Rasilimali za ni kitu muhimu maendeleo endelevu ya vizazi vilivyopo na vijavyo katika jamii yoyote duniani. [180]
vokali
Kimsingi maneno ya Kiswahili yanatakiwa yaishie na vokali. [181]
vya
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha jana alivunja ukimya dhidi ya tuhuma zinazomwandama kuwa aliingilia mchakato wa zabuni ya mradi wa uchapishaji vitambulisho vya taifa, alipokanusha kuwa na uhusiano wowote na kampuni ya Sagem Securite na kusema kuwa yuko tayari kujiuzulu iwapo itathibitika kuwa alifanya kosa hilo au alipokea rushwa. [182]
wakuu
Baada ya kusoma na kutafakari kwa mapana na marefu, ninadiriki kuyakinisha kwamba pengo la elimu ya teknohama kati ya viongozi wakuu wa makampuni na wataalamu wa teknohama lilisababisha kufanya watalaamu mengi—wakuu wa makampuni husika hawakuyafahamu na kama walikuwa wakihisi lolote hawakuwa na namna ya kuyakinisha. [183]
walinzi
Hata hivyo, hakutaja aina ya zawadi itakayotolewa kwa walinzi watakaofanikisha kutoa taarifa za kukamatwa kwa wauaji hao. [184]
wao
Naye Beatrice Mshumbusi, mkazi wa kata Hamugembe, alisema walimu walistahili kuchapwa viboko, akidai kuwa wamekuwa kero hasa kutokana na vitendo vyao vya kulewa saa za kazi, hali inayosababisha wengi wao kuwa wachafu kupindukia. [185]
wapi
Kama tulivyosoma kwenye magazeti kuwa Mrema amemuomba Ngawaiya ajiunge TLP,Ngawaiya kagoma lakini kakiri kuwa akiwa mbunge aliwafanyia wananchi kazi nzuri sasa tatizo liko wapi," alihoji Kidaya. [186]
watu
Unaweza kukaa kimya kuachia watu waseme, lakini wakapotosha kama ilivyofanyika. [187]
waume
Na hii inabaki kuwa sababu ndoa nyingi zinaterereka kwa kuwa wanawake wanashindwa kujipendekeza na kuwanyenyekea waume zao kila siku kama vile ambavyo wengi wanafanya katika siku kama hii. [188]
wazazi
Baadhi ya wazazi walisema wanaandaa maandamano kupinga kitendo cha kumwajibisha mkuu wa wilaya ya Bukoba kwa sababu ya kuwapiga walimu viboko. [189]
wewe
Mfumo wa benki kama ninavyoujua na kama wewe unavyoujua umekaa kwa namna ambayo jamaa hawa wanakusanya fedha kutoka kwa wengi na kuzikopesha kwa wachache kwa faida kubwa. [190]
wiki
Wasomali hao walikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita na kuna madai kuwa walikuwa na bunduki. [191]
wote
Nahodha Joseph pamoja na Mnigeria Emeh Izuchukwu, wote wa Simba walirejea nchini Jumamosi usiku wakisubiri hatma yao ya kusakata kandanda la kulipwa. [192]
yale
Jintao alisema taifa lake litachukua mtazamo mpana, wenye uwiano, endelevu na unaotekelezeka katika kuweza kubadilisha mfumo wa fedha wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuongeza uwakilishi wa mataifa ya kiafrika na yale yanayoendelea pamoja na sauti zao katika mabadiliko hayo. [193]
yangu
Huo ndiyo ukweli wa tuhuma zinazotolewa dhidi yangu. [194]
yao
Liyumba na mshtakiwa mwenzake, Deograthias Kweka wanatakiwa kuweka dhamana ya fedha taslimu au mali zenye thamani ya Sh55 bilioni kila mmoja, ikiwa ni nusu ya Sh221 bilioni ambazo wanadaiwa kuipotezea serikali kutokana na kutumia vibaya madaraka yao. [195]
yote
Hatima ya yote mgonjwa atapaswa kuwekewa dripu ya kwinini. [196]
yule
Tusije tukashangaa kuwa yule Mjapani aliyeanzisha benki yake na aina yake ya fedha digiti au elektroniki pengine ndiye binadamu mwenye akili timamu kuliko wote duniani hivi leo. [197]
zile
Taswa ambayo ni timu ya waandishi wa habari, imekuwa ikitoa upinzani kwa timu mbalimbali zikiwamo zile zinazoshiriki ligi mbalimbali za ushindani. [198]
ziote
Akaamuru shule ziote kama uyoga, zisambae kila kata hadi kila kijiji, zikasambaa, zikasambaa hadi zikasambaratika. [199]
ziwepo
Basi Mungu akaamuru ziwepo shule zikawepo. [200]