Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-02-11

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


adha
Hata hivyo Shule ya Sekondari ya Azania iliyopo Ilala, Dar es Salaam imeamua kuondoa adha ya mabaki kwa kubuni matumizi mengine mazuri kwa maslahi yao. [1]
aina
Mbunge huyo pia aliomba serikali itoe tamko kama polisi wanaofanya kazi ya kuchoma bangi hiyo wanadhurika au hapana kutokana na ukweli kuwa bangi ni aina ya magugu hivyo yanapochomwa moto yanakuwa na moshi mkubwa. [2]
ajabu
Tena niliota ndoto ya ajabu sana na nawaomba waishiwa wasomaji wangu wanisaidie kuelewa ndoto hii. [3]
akioza
Samaki mmoja akioza, wote wameoza. [4]
akiwa
Siku hiyo niliitwa kwa mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali (IGP), Saidi Mwema na nilimkuta akiwa na makamishna wawili. [5]
al
Muammar Abu Minyar al Gaddafi, amekuwa kiongozi wa kidikteta tangu alipofanya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1969. Ingawa Gaddafi hakushika ofisi au cheo tangu mwaka 1979, ana heshima ya kuwa msimamizi wa Mapinduzi ya Kijamaa ya Waarabu wa Libya. [6]
alitaka
Owenya alitaka kujua sababu za hali hiyo kuwepo na alitaka serikali kueleza ni watuhumiwa wangapi wa mihadarati waliotajwa na Hayati Amina Chifupa walishachukuliwa hatua hadi sasa. [7]
alitoa
Slaa alitoa kauli hiyo juzi wakati anachangia kuhusu mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya serikali kwa kipindi cha mwaka 2009/10 hadi 2011/2012 iliyotolewa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. [8]
ama
Wasaidizi wa RPC ni OCD. Katika utaratibu wetu kama kuna tatizo kuna mawili ama kumwita aenda mwenyewe au kumwita ofisini,” alijibu Zombe. [9]
ambalo
Hata hivyo, Zombe aliieleza mahakama kuwa siku hiyo alikwenda kituoni hapo baada ya kuitwa na OCD wa Magomeni, SSP Matage kuwa kuna tatizo ambalo alikuwa akihitaji msaada wake. [10]
ambayo
Alisema barua hiyo, ambayo ilikuwa ikijibu barua ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ya Mei 31 mwaka 2006, ilieleza kuwa baada ya kukamilisha mambo kadhaa ya kiupelelezi na kwa ushahidi ulioko katika jalada tumefikia maamuzi kuwa Zombe aunganishwe katika kesi hiyo. [11]
ana
Na kwa sababu hiyo, mbunge yeyote anapokuwa akisema Bungeni ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyewe anaamini kuwa ni la ukweli na siyo jambo la kubuni au kubahatisha tu. [12]
as
Binamu yake Sayyid Hassan ar-Rida al Mahd as Sanussi akawa mfalme badala yake. [13]
au
Bila shaka maelekezo ya DPP hakuyapata au aliyemfundisha hakumuelewa vema,” alidai. [14]
awe
Slaa aliendelea kusisitiza kutofuta kauli hiyo kwa maelezo kuwa itabidi asome hansadi za bunge ili kuhakiki ukweli juu ya kauli hiyo na atathmini kulingana na makusudio ya ujumbe ya hoja aliyokuwa anaitoa ili awe na maamuzi sahihi. [15]
baadaye
Alidai walizumgumzia tukio la Bidco na kuwapongeza askari waliohusika kwa kuwatoa kimasomaso na kwamba pesa hizo zilifikishwa na kwamba ndipo baadaye aliwaita waandishi wa habari ili kuwaeleza tukio hilo na kuwaonyesha fedha hizo na bastola hiyo. [16]
bali
Alisema kuwa bendi hiyo haijavunjika kama watu wengi wanavyofikiria, isipokuwa hivi sasa haitakuwa tena chini ya shirika hilo bali itafanya shughuli zake kwa kujitegemea. [17]
bara
MWENYEKITI wa Umoja wa Afrika aliyemaliza muda wake, Rais Jakaya Kikwete pamoja na mambo mengine ya kuyashughulikia barani Afrika hususan yale ya migogoro lakini pia amemkabidhi Mwenyekiti mpya wa Umoja huo, kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, kazi ya kuliunganisha bara la Afrika. [18]
bastola
Sh4 milioni na bastola. [19]
bendera
WAKATI Prisons ya Mbeya ikiagwa kwa kukabidhiwa bendera ya taifa na Kanali Mstaafu Iddi Kipingu, wawakilishi wengine wa Zanzibar, Mundu huenda wakajitoa kufuatia ukosefu wa fedha kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF). [20]
bila
Asubuhi hiyo hiyo akawaita OCD wa wilaya zote lakini na askari wa chuo kikuu tu ambapo walizungumza hali ya uhalifu maana kwa kuwa wakati huo kulikuwa na ujambazi sana watu walikuwa wakiuawa bila sababu. [21]
bodi
Liyumba na Kweka wanadaiwa kuwa kati ya mwaka 2001 na 2006 wakiwa waajiriwa wa serikali walitumia madaraka yao vibaya na kuidhinisha malipo ya ujenzi wa minara pacha bila idhini ya bodi ya wakurugenzi wa BoT na kuisababishia serikali hasara kubwa. [22]
bomba
Nchi hizo mbili pia zimekubaliana kushirikiana katika kuboresha huduma nyingine za kiuchumi zinazomilikiwa na kuendeshwa kwa pamoja kati ya nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na bomba la TAZAMA ili kuharakisha mafuta kufika nchini Zambia. [23]
bungeni
Akitoa taarifa bungeni jana, Sitta alisema kuwa Dk. [24]
cha
Kutokana na kilio hicho cha kimya kimya, mara nyingine alijikuta akikabwa na kigugumizi cha uchungu kiasi cha kushindwa hata kuzungumza. [25]
chake
Kwa ujumla, inasikitisha kuona shule za serikali ambazo zilitazamiwa kuonyesha mfano mzuri, zikiwemo zinazoitwa za vipaji maalumu zimeshukuka, hivyo kuondoa thamani ya kiwango chake. [26]
chako
Anakuwa mwema zaidi anapokuwa na shida, katika kipindi chako cha mafanikio urafiki wenu utanoga, ukifilisika atakugeuka. [27]
chenye
Taasisi ya kitengo cha ujasusi wa kiuchumi duniani (Economist Intelligence Unit) chenye makao yake makuu nchini Uingereza kimetabiri kwamba uchumi wa Tanzania utakuwa kwa asilimia 6.9 mwaka huu na asilimia 7.1 mwaka ujao. [28]
dhamira
Akizungumzia uamuzi wake wa kuchukua fomu Ngabo alisema kuwa hilo limetokana dhamira yake ya kweli ya kurudisha heshima ya mchezo huo nchini. [29]
es
MSHTAKIWA wa kwanza katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka mjini Mahenge, Morogoro na dereva teksi wa Manzese jijini Dar es Salaam, Abdallah Zombe jana alijitetea kwa zaidi ya saa tatu huku akimwaga machozi wakati akiwasilisha utetezi wake. [30]
familia
Alizaliwa mwaka 1942 katika familia ya wakulima. [31]
fani
Mwanafunzi George Thomas wa mwaka wa tatu anayesomea fani ya sayansi ya utafiti wa ardhi, alisema utaratibu wa udahili uliopangwa unaenda vizuri na wengi wao wameufurahia na hakuna fujo yoyote ambayo imetokea tangu kuanza kwa zoezi hilo. [32]
furaha
Hapo namaanisha kwamba watu wanaamini kwamba ukipata mafanikio kinachofuata ni furaha. [33]
gani
Nilimuuliza alikuwa na jambo gani na kama kulikuwa na umuhimu wa mimi kwenda, akasema ilikuwa ni muhimu. [34]
gesi
Miradi mipya ya uwekezaji, ikiwemo mradi wa gesi na kilimo, inaweza kuchelewa. [35]
hao
Hatua ya kupanda kizimbani jana na kuanza kujitetea ilikuja baada ya mahakama hiyo kuridhika kuwa Zombe, ambaye wakati wa mauaji hayo alikuwa akikaimu nafasi ya kamanda wa kanda ya Dar es salaam, pamoja na wenzake wana kesi ya kujibu kuhusu mauaji ya watu hao kulingana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo. [36]
hapa
Shahidi katika ushahidi uliotolewa hapa ni kwamba wewe ulikwenda katika kituo cha Polisi Urafiki, hebu iambie mahakama ni lini ulikwenda kwama RPC na kwa nini?” aliuliza Wakili Msemwa. [37]
harakati
Mwaka 1961, Gaddafi akafukuzwa kutoka Sebha kutokana na harakati zake za kisiasa. [38]
hatimaye
Na hatimaye baada ya vita kuu ya pili, sababu ikapatikana ya kulazimisha kuwa na taifa la Waisrael. [39]
hatutaki
Sisi hatutaki, hatutaki lakini tutatupwa kama hao. [40]
hatutoki
Hapa hatutoki, huko hatutaki. [41]
hawa
Matage aliniambia kuwa hawa ofisa wa polisi (Bageni na Makelle) wanatoka kwenye tukio la uporaji wa pesa za Bidco ambako zimeokolewa Sh5,750,000, lakini Sh. [42]
hiki
Atataka umfanyie hiki umfanyie hiki lakini yeye hayuko tayari kwa lolote juu yako. [43]
hili
Hata zinapofika kwa RPC huzinakili kama zilivyo bila kuongeza ili kama likitokea jambo kama hili lililotuweka hapa, tunarudi kwenye taarifa hiyo,” alisisitiza. [44]
hivi
Alisema miaka ya hivi karibuni, Tanzania imekuwa ni moja ya nchi vinara, katika ukamataji na uteketezaji wa bangi , hivyo alikanusha kuwa Tanzania ni moja ya nchi vinara wa kulima bangi kwa wingi. [45]
hizo
Zombe, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) ambaye alikuwa mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Dar es Salaam, alijikuta akimwaga machozi mara kadhaa wakati akijitetea mbele ya Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Salum Masatti kuhusu tuhuma hizo dhidi yake pamoja na askari wenzake tisa. [46]
huduma
Sekta ambazo zinatabiriwa kufanya vizuri ni pamoja na ujenzi, madini na huduma, wakati kilimo kinatarajiwa kufanya vibaya ikiwa serikali itaendelea kuchelewesha mabadiliko yanayotakiwa. [47]
huenda
Maximo huenda akakichezesha kikosi kinachoundwa na kipa Shaaban Dihile, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Swed, Shadrack Nsajingwa, na Juma Jabu kama mabeki, viungo, Godfrey Bonny, Haruna Moshi ( Boban), Nurdin Bakari na washambuliaji Jerry Tegete, Mrisho Ngassa na Mussa Hassan Mgosi. [48]
huko
Tutafanya kama tulivyofanya mara hii kisiwani Zanzibar kwani Watanzania wa huko walituunga mkono kwa kiasi kikubwa na tutaania Arusha na kisha katika mikoa mingine,alisema kocha huyo. [49]
huo
Kuhusu kuhusika katika tukio hilo, Zombe alidai siku hiyo alikuwa na shughuli maalumu ya kuongoza msafara wa Rais Jakaya Kikwete ambaye wakati huo alikuwa na ziara za kutembelea wizara mbalimbali na kutoa maelekezo ya utendaji na kwamba majukumu yake aliyakabidhi kwa SSP Mafie. [50]
husika
OCD wa eneo husika pia aliandika taarifa ya tukio hilo. [51]
huu
Kwa mujibu wa IMF ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika ulifikia asilimia 8 hadi mwaka jana, lakini hali inaonyesha kuwa kasi hiyo ya ukuaji itapungua kwa mwaka huu kutokana na matatizo mbalimbali, yakiwemo ya mgogoro wa kifedha ulioikumba dunia kwa sasa, ukiwa umeanzia kwenye mataifa tajiri duniani. [52]
huyu
Barua hii imeandikwa tofauti na nyingine zote sababu kwa sababu mshtakiwa huyu anakaa Segerea (mahabusu). [53]
ikawa
Na alipouruhusu umiliki binafsi wa makampuni madogo, Serikali ikawa ikimiliki makampuni makubwa. [54]
ikiwa
UKUAJI wa uchumi wa Tanzania umetabiririwa kuwa utaanguka mwaka huu kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na matatizo ya ndani na mgororo wa kifedha duniani. [55]
ile
Tena nakumbuka gazeti la Mwananchi lilinionyesha nikiwa nimeshika hizo fedha na nikiwa nimeshika ile bastola. [56]
ili
Wakili Msemwa alikuwa akijaribu kumzuia kwa ishara wakati fulani, lakini Zombe alionekana kumbishia kwa ishara na wakati fulani kulazimika kuomba ruhusa kwa jaji ili aendelee kutoa maelezo yake. [57]
imara
Wanadai japokuwa ujenzi wake ulichukua wiki mbili, kwa uzoefu wao sasa mtambo huo unaweza kutengenezwa kwa siku tatu na ukakamilika kuwa imara kwa matumizi. [58]
ina
Hata hivyo, wizara bado ina matumaini ya uchumi kukukua hadi kufikia asilimia 9.2 mwaka 2011. wizara imejiridhisha kwamba kushuka kwa mazao makuu ya biashara katika masoko ya Ulaya na Marekani kama ni tatizo. [59]
iwapo
Katika kipengele cha pili, inaelezwa: “Mbunge yeyote anapokuwa akisema bungeni hatachukuliwa kuwa anasema uongo iwapo anafanya rejea ya habari kuhusu jambo fulani lililotangazwa au lililoandikwa na vyombo vya habari. [60]
iwe
Kuhusu uboreshwaji wa bomba la Tazama, Rais Banda alisema kuwa serikali yake itafanya jitihada za kutoa fedha ili kuweza kuhakikisha miundombinu ya bomba hilo inaboreshwa ili iwe ya kisasa. [61]
iweje
Kama samaki mmoja aliyeoza anaozesha tenga zima, iweje kama karibu samaki wote wameoza? Yupo samaki mwingine atakayepona kweli? Ataozeshwa na yeye. [62]
joto
Mmoja wa wapishi wa shule hiyo, Stella James anasema mtambo huo umesaidia kwa kiasi kukubwa kupunguza adha na joto ambalo lilikuwa linawatesa wakati wa kupika vyakula. [63]
jukumu
Aliongeza kuwa kwa nafasi ya RCO, jukumu hilo alilikabidhi kwa SSP Mkumbo na kwamba alikuwa ingawa wasaidizi hao walikuwa wakimuelezea yaliyokuwa yakitokea jijini, lakini wakati mwingine alikuwa akichelewa kurudi na hivyo alikuwa akienda nyumbani moja kwa moja. [64]
juu
Alidai taarifa za matukio yote huandaliwa tangu ngazi ya chini na kutumwa kwa viongozi wa juu hatua kwa hatua hadi kwa IGP kupitia katika mitambo maalumu na kwamba hata Ikulu kuna mtambo huo ambao ni mkubwa unaopokea matukio hayo yote. [65]
juzi
Willbrod Slaa baada ya kusita kutolea maamuzi sakata alilolitangaza juzi na kumtaka kulithibitishia bunge kwamba serikali inawapa leseni za ualimu wanafunzi waliofeli kidato cha sita, baada ya kuwasilisha vielelezo vinavyohitaji kufanyiwa uchunguzi. [66]
kaa
Kwa maana hiyo kama nafsi yako inakusuta kweli utaweza kujiamini? Siamini kamwe! Na kibaya zaidi ni kwamba kaa ukisubiri siku moja kuumbuliwa kwa sababu uovu wowote siku zote huacha nyayo nyuma yake. [67]
kamwe
Kwa maana hiyo watu kama hao hata kama watapata utajiri wa kiwango gani, hawataweza kamwe kujiamini, kwa sababu tayari wamekengeuka kimaadili na dhambi hiyo inaweza kutenguliwa kwa wao kukiri hadharani dhambi hiyo. [68]
kata
Kuanzishwa kwa sekondari za kata, kulikolazimu kuwahamisha walimu wengi wazoefu kwenda kuwa walimu wakuu wa shule hizo, pamoja na waliohamia sekondari za binafsi zikiwamo seminari kufuata masilahi, kumechangia kwa kiasi kikubwa kudhoofisha ubora wa elimu katika shule za umma. [69]
kauli
Slaa awasilishe vielelezo vinavyothibitisha kauli hiyo na kwamba asipofanya hivyo bunge litatumia kanuni zake ili kumuadhibu kutokana na kulidanganya. [70]
kigumu
Mgogoro wa walimu uliotokea Agosti hadi Oktoba, mwaka jana wakati watoto wanajiandaa na mitihani, pia umechangia kwa kiasi kikubwa matokeo kuwa mabaya, kwani wanafunzi walikosa maandalizi ya kutosha kutokana na kukosa walimu wa kuwasaidia katika kipindi hicho kigumu. [71]
kila
Tunaomba hata sharti la kutakiwa kuripoti ofisi ya mwendesha mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kila Ijumaa liondolewe kwani ni kama adhabu kwa washitakiwa,” alidai Nyange. [72]
kile
Hata hivyo, Stars nao wakiwa na kikosi kile kile kilichofuzu kwa fainali hizo, chenye wachezaji machachari kama vile, Mrisho Ngassa, Kigi Makasi, Jerry Tegete , Mussa Hassan Mgosi na wengineo, wana na hamu ya kuwafunga Wazimbabwe ili kuwaonyesha Watanzania kuwa safari ya kuelekea Ivory Coast imeiva. [73]
kilo
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk James Wanyancha alisema jana kwamba hali ya machinjio kwa jiji hilo ni mbaya licha ya idadi kubwa ya ulaji wa nyama unaozidi wastani wa kilo 10 kwa mtu mmoja kwa mwaka. [74]
kipigo
Wakati timu hiyo ikitoka sare wawakirishi wengine wa Tanzania Bara timu ya Jeshi Stars imekubali kipigo cha goli 37-30 dhidi ya JKU ya Zanzibar. [75]
kitengo
Miongoni mwa wasaidizi hao wa RCO aliwataja kuwa ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Charles Mkumbo ambaye aliyekuwa mkuu wa kitengo cha ujambazi na uhalifu mbalimbali Dar es Salaam. [76]
kuanzia
Alisema bendi hiyo haitakuwa tena chini ya shirika hilo kuanzia Machi Mosi mwaka huu, hivyo mkataba huo utaisaidia bendi hiyo kujiendesha yenyewe. [77]
kuficha
Anadiriki kutoa aibu zako nje na kuficha za kwake. [78]
kule
Hata mimi nimekusikia ukisema kuwa kuwa kule Karatu kuna vijana waliofeli na wamepewa leseni za uwalimu,” alibainisha Spika Sitta. [79]
kumaliza
Baada ya kumaliza kuchangia, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margereth Sitta alisimama na kumtaka Dk. [80]
kumbe
Atakufundisha mambo mabaya na kukufanya uamini ni mwenzie kumbe nia yake ni kukuharibia. [81]
kunuka
Na watu katika kutafuta samaki asiyeoza walianza kunuka na wao. [82]
kuongea
Na wakati naangalia hivi nikasikia ghafla kama samaki wa chini wanaanza kuongea. [83]
kutafakari
Nikajaribu kutafakari. [84]
kuu
Viongozi hao wawili pia walijadili huduma nyingine za kiuchumi zinazomilikiwa na kuendeshwa kwa pamoja na nchi hizo mbili, ikiwemo barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam hadi Lusaka. [85]
kuwepo
Alidai walimueleza kuwa moja ya tatizo ni kuwepo kwa walimu ambao wanapewa leseni za kufundisha huku wakati walifeli mitihani ya kidato cha sita. [86]
kwake
Akizungumza na Mwananchi jana ofisini kwake, makamu mkuu wa chuo, Profesa Idrissa Mshoro alisema wanafunzi bado wanaendelea na udahili baada ya kufanya malipo kwa utaratibu ambao baraza la chuo limeweka. [87]
kwako
Na wanakuja kwako wakiwa wanapeperusha hii bendera ya urafiki. [88]
kwao
Kama Walibya walifanikiwa kutufunga katika uwanja wetu wa nyumbani kwa ushindi wa 2-0 kwanini sisi tushindwe kuwafunga 3-0 kwao? alihoji Kipingu. [89]
kwenye
Nilikwenda tukaingia na mke wangu kwenye gari nikamuuliza OCD Matage mahali alikokuwa akaniambai alikuwa Kituo cha Urafiki. [90]
la
Akiongozwa na wakili wake, Jerome Memwa katika utetezi wake uliochukua saa 3:38, Zombe alikanusha ushahidi wote uliotolewa mahakamani hapo kuwa si wa kweli na kwamba ulipangwa tu kwa lengo la kummaliza kwa sababu ambazo hata hivyo hakuweza kuzieleza. [91]
lake
Anaelewa kwamba amepoteza, ndiyo maana ametoka akiwa hivyo," alisema mwanadiplomasia mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe. [92]
leo
Hadi leo, washitakiwa hao, ambao walifikishwa mahakamani Januari 27 mwaka huu, bado wako rumande kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. [93]
ligi
RAIS Jakaya Kikwete amewataka wachezaji wa Taifa Stars kutobweteka na ushindi walioupata dhidi ya Sudan na kupata tiketi ya fainali za Afrika au kuogopa majina makubwa ya timu wanazokwenda kushindana nazo nchini Ivory Coast, badala yake waende wakifahamu kuwa wana changamoto ya kutakiwa kufanya vizuri katika fainali za Mataifa za wachezaji wa ligi za ndani (CHAN). [94]
likioza
Tenga moja likioza, litenge, tenga moja likioza, litenge, lituuupe. [95]
lita
Mtambo huu una uwezo wa kuchukua kilo 12 za mabaki ya chakula na lita 40 za maji asubuhi, na jioni huwekwa kiasi hicho hicho. [96]
lolote
Tuko tayari kwa lolote juu yao na tunawafanya kuwa ni wenzetu. [97]
maalum
Alikuwa akijibu swali la Lucy Owenya (Viti maalum Chadema) aliyetaka kujua juhudi zinazofanywa na serikali katika kupambana na tatizo la mihadarati nchini. [98]
mabao
Katika mchezo wa kwanza , Prisons walipoteza kwa kipigo cha mabao 2-0 jijini Dar es Salaam. [99]
mada
Ni dhahiri wengi wa wasomaji wameridhishwa na mada yenyewe ambayo leo itazungumzia sehemu ya pili kabla ya kuanza kujadili mada nyingine. [100]
maeneo
Alieleza sababu zinazosababisha kuongezeka kwa kilimo na matumizi ya bangi hapa nchini kuwa ni pamoja na mazingira ya kijiografia kwa kilimo cha bangi kinafanyika katika maeneo ya milima na misitu minene ya asili kusikofikika kirahisi. [101]
mafunzo
Baada ya kuhitimu mwaka 1965, alipelekwa Uingereza kwa mafunzo zaidi katika chuo cha British Army Staff College. [102]
makabila
Waisraeli wapigana wakawashinda hawa wa makabila mengine lakini Wafilisti walidinda. [103]
makala
Mtambo huu unatumia mabaki ya chakula kama vile wali, ugali, makande na aina mbalimbali za vyakula anavyokula binadamu pamoja na matunda," anasema Mkuu wa shule hiyo Donald Sigodalilwa alipohojiwa na mwandishi wa makala haya hivi karibuni. [104]
makao
Mimi nilikamatwa Juni 6 mwaka 2006 nikiwa makao makuu ya Jeshi la Polisi. [105]
malengo
Hali hii itafanya serikali kutofikia malengo yake ya kutokomeza umasikini. [106]
mapema
Prisons inashiriki michuano hiyo ya CAF kwa mara ya tatu ambapo mara ya yake ya kwanza ilikuwa mwaka 1999 wakati mara ya pili ilikuwa mwaka 2005, hata hivyo timu hiyo imekuwa ikiondolewa mapema katika michuano hiyo. [107]
matenga
Kandokando yake yalikuwepo matenga ya samaki na mchuuzi alikuwa anayakagua moja moja. [108]
mbali
Hata hivyo, upande wa serikali uliokuwa ukiongozwa na wakili wa serikali, Joseph Maugo uliiomba mahakama itupilie mbali hoja hizo kwa maelezo kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilifuata taratibu zote za kisheria katika kuweka masharti hayo ya dhamana. [109]
mbinu
Baada ya kupata nafasi hiyo, tunaamini Banda alipata muda muafaka wa kuzungumza na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete juu ya nini kifanyike katika kuliokoa shirika hilo lililokumbwa na ubadhirifu, uongozi mbovu, wizi na matatizo ya miundo mbinu yake. [110]
mbovu
Ukiacha bomba la Tazama, suala la huduma mbovu za Tazara limekuwa likiumiza wengi hasa kutokana na ukweli kuwa usafiri huo ulikuwa ukitegemewa sana na wananchi wa mataifa haya mawili kwa kusafiri wao au kusafirisha mizigo yao. [111]
mchuuzi
Kwanza nilimwona mchuuzi wa samaki akiwa amesimama mbele ya meza yake ya biashara. [112]
mdomo
Hawezi kufunga mdomo wake kuzungumza mambo yako. [113]
mema
Kwa imani hiyo inafuata kwamba iwapo watu watafanya mambo mema kwa lengo la kulinda furaha ya wenzao na wakafanya hivyo kwa nia njema hakuna yeyote awaye wala mamlaka yoyote iwezayo kuwakwaza watu wa aina hiyo. [114]
mfumo
Akizungumza na Mwananchi jijini jana, Maximo alisema mfumo huo utakuwa ni njia nzuri ya kuwapa Watanzania nafasi ya kuiona timu yao ya taifa ikicheza. [115]
michepuo
Kwa mujibu wa wanafunzi hao, mtambo huo umekuwa kichocheo kikubwa kwa wanafunzi kuchukua masomo ya sayansi tofauti na awali wakati bado haujatengenezwa, kwani wengi walikuwa wanakimbia masomo ya sayansi na kuchukua michepuo mingine. [116]
midogo
Ana miradi midogo midogo inayoweza kumfanya asiuguse hata mshahara wake. [117]
miezi
Scolari, aliyeiongoza Brazil kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 2004, alitimuliwa kazi Jumatatu ikiwa ni miezi manane katika mkataba wake wa miaka mitatu uliokuwa ukimwingizia pauni milioni sita kwa mwaka. [118]
miji
Marais hao, pia walijadili namna ya kurahisisha uvukaji mpaka wa Nakonde hasa kwa malori makubwa ya mizigo na pia kukubaliana namna ya kumaliza matatizo ya umeme ambao Zambia inatoa kwa Tanzania kwa miji ya Mbeya na Sumbawanga. [119]
mikondo
Mwaka 1967 shule hiyo ilitaifishwa na mwaka 1987 ilipanuliwa zaidi na kuwa na mikondo 28 ikiwemo 24 ya sekondari ya kawaida (O- Level) na minne ya sekondari ya juu (A-Level). [120]
mimi
Kama Mtukufu Jaji alivyosema, hii ni moja ya sababu ya kunibakisha mimi katika kesi hii ili nisaidie kutoa ushahidi. [121]
minne
Uamuzi wa bilionea wa Russia, Roman Abramovich kumtimua Jose Mourinho mwaka 2007 na Avram Grant mwezi mmoja baada ya Muisraeli huyo kusaini maktaba wa miaka minne umekuwa ni mzigo mkubwa kwake. [122]
miradi
EIU imebainisha kwamba uwekezaji utapungua isipokuwa kwa miradi mikubwa iliyopo. [123]
mkaa
Wapishi wanaipenda kazi yao kwani sasa wanapika chakula kingi bila kuungua na joto ikilinganishwa na wanavyopikia majiko mengine ya mkaa. [124]
mke
Siku hiyo nilikuwa nimekwenda kumchukua mke wangu Hospitali ya TMJ katikati ya jiji. [125]
mnuko
Au hata akibaki hajaoza, bado atanuka kama wenzie maana amekaa kwenye tenga la mnuko mtupu. [126]
mosi
SEPTEMBA mosi, 1969, kikundi kidogo cha maofisa wa kijeshi wakiongozwa na Gaddafi kilifanya Mapinduzi ya kijeshi yaliyomwaga damu, na kumwangusha Mfalme Idris wa kwanza aliyekuwa Kamena Vourla, Ugiriki akitibiwa. [127]
mradi
MAOMBI ya kulegezewa kwa masharti ya dhamana katika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh221 bilioni inayomkabili aliyekuwa mkurugenzi wa utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Joachimu Liyumba na meneja mradi, Deograthias Kweka yatatolewa uamuzi keshokutwa. [128]
mrefu
Ni kiongozi wa nne aliyeongoza taifa hilo kwa muda mrefu. [129]
msafi
Usijidai msafi. [130]
msingi
Alijiunga na shule ya msingi Bugobwa mwaka 1968 na kuhitimu elimu yake ya msingi mwaka 1975 ambapo alijiunga na shule ya ufundi Ifunda mpaka mwaka 1978 alipohamia Dar es Salaam. [131]
muda
Jana Sitta alifafanua kuwa ameamua kutoa muda wa uchunguzi wa vielelezo vya Dk. [132]
mwepesi
Rafiki huyu ni mwepesi kuchukua ya kwako na kukuletea ya watu. [133]
mzito
Mjadala huu ni mzito sana. [134]
nafuu
SPIKA wa Bunge, Samweli Sitta amempa nafuu mbunge wa Karatu kwa tiketi ya Chadema, Dk. [135]
nao
Pia, aliwashukuru wadhamini mbalimbali ambao wamekuwa bega kwa bega na timu hiyo hadi kufikia mafanikio iliyoyapata kwa sasa, lakini TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) nao wasibweteke kwani fedha zikiwamo wanazozipata katika viingilio vya michezo mbalimbali vitumike kuiendesha timu na kuiandalia michezo ya kujipima nguvu ili kupata uzoefu. [136]
naye
UAMUZI wa Chelsea kumtimua kocha wake, Luiz Felipe Scolari utaigharimu timu hiyo kiasi cha pauni milioni 15 kama fidia ya kuvunja mkataba naye, imefahamika. [137]
nayo
Lakini, Zimbabwe ambayo pia imefuzu nayo ni nzuri na katika michuano hiyo imepangwa Kundi B lenye timu za DRC, Libya na Ghana. [138]
ndani
Dereva wangu aliyekuwa amebaki katika gari alikuja ndani akanitaarifu kuwa OCD Matage alikuwa akiniita," alidai Zombe. [139]
ndio
ASILIMIA 66 ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi waliofanyiwa udahili jana, ndio waliokubaliwa kurudishwa chuoni baada ya kusimamishwa masomo kwa kosa la kugomea masomo, wanafunzi 30 hawakujaza fomu za kuomba kurudi chuoni. [140]
ndivyo
Mtambo huu ukipewa chakula na maji kama inavyotakiwa ndivyo unavyotoa gesi kwa wingi na ukizidishiwa chakula unavimbiwa na hivyo kushindwa kutoa gesi inayotakiwa kwa matumizi ya kawaida," anaeleza. [141]
ndoo
Wakati niliona siwezi kuvumilia tena na imebaki kuoza na mimi, wakaja watu wenye ndoo za maji na kuanza kuwamwagia watu wote huku wakiimba. [142]
ng
JIJI la Dar es Salaam linahitaji ng’ombe 800 na mbuzi/kondoo 1500 kwa siku moja ili kuweza kukidhi hali ya upatikanaji wa nyama kwa wakazi wa jiji hilo, bunge lilielezwa jana. [143]
ngozi
Ukweli ni kwamba wapo pia katika kundi la marafiki, 'marafiki maadui' waliojivika ngozi ya urafiki. [144]
ngumi
KAMPUNI ya Simu za Mkononi, Vodacom Tanzania imetoa Shilingi milioni 6 kwa ajili ya udhamini wa pambano la ngumi za kulipwa kati ya Rashid Matumla na Francis Cheka utakaofanyika Ijumaa katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. [145]
ni
Katika hali hiyo Zombe alimtupia lawama Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuwa ni miongoni mwa watu waliohusika katika kupanga ushahidi kwa lengo la kummaliza katika hali ya kutapatapa baada ya kuona kuwa hawana ushahidi wa kumhusisha na tukio hilo. [146]
nia
Katika mkutano huo, Gaddafi alisisitiza nia yake ya kutaka Muungano wa Afrika kwa Waafrika wote kwa kila hali. [147]
nimeloa
Lakini wale samaki wakanicheka tu na mimi nikakuta wenye ndoo wakinilenga na mimi hadi nilijikuta nimeloa. [148]
nusu
Mmoja wa mawakili wanaowatetea washitakiwa hao, Hubert Nyange jana aliiomba mahakama iondoe sharti la dhamana la kuwataka washitakiwa watoe nusu ya fedha wanazodaiwa kuzipoteza, akisema kiwango hicho ni kikubwa na hakitakuwa cha haki kwa washitakiwa. [149]
nyuma
Big Phil' amefukuzwa baada ya Chelsea kuwa nyuma kwa pointi saba dhidi ya vinara Manchester United na kuporomoka hadi nafasi ya nne baada ya kutoka suluhu na timu mpya kwenye ligi hiyo, Hull City kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, Jumamosi na kusababisha timu hiyo kuzomewa na mashabiki wake. [150]
paa
Ndipo hapo nikastuka na kukuta huko nje mvua inyesha na paa yangu inavuja kwa nguvu zote hadi kweli nimeloa. [151]
pale
Anakuwa rafiki yako pale anapohisi unaweza kumsaidia. [152]
pekee
Sisi kama wanafunzi wa Azania tunajivunia kuwa na mtambo mkubwa kama huu na tunamshukuru Mkuu wa shule kwa kukubali na kuruhusu kujegwa mtambo huo shuleni hapa jambo ambalo limetusaidia hasa tunaochukua masomo ya sayansi," anaongeza Mnaku ambaye anahisi ni shule yao pekee yenye mtambo kama huo Dar es Salaam. [153]
pengo
Katika mchezo wa leo, Maximo anaweza kuwatumia baadhi ya wachezaji wapya ili kuziba pengo la nahodha, Henry Joseph aliyeko kwenye majaribio nchini Norway, ingawa kiungo wa Mtibwa Shaaban Nditi anaweza kutumiwa zaidi. [154]
pia
Zombe, ambaye jana alisimama pia kama shahidi wa kwanza upande wa utetezi dhidi yake (Dw1), alibubujikwa na machozi wakati akitoa ushahidi wake na kujifuta kwa kitambaa mara kadhaa huku akigeukia pembeni. [155]
pili
Alisema walipofika ofisini walimkuta mkuu wa kituo hicho, SP Juma Ndaki, OCD Matage, SP Mkumbo, mshtakiwa wa pili, SP Christopher Bageni na mshtakiwa wa tatu, ASP Ahmed Makelle. [156]
rais
Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mwandamizi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja aliwataja mabondia wa zamani waliojitokeza kuwa ni pamoja na Hezron Kigonda anayewania nafasi ya makamu wa rais pamoja na Herman Mabula anayewania nafasi ya ukatibu mkuu. [157]
reli
Viongozi hao wawili walijadili hali ya Reli ya Tazara inayomilikiwa kwa pamoja na nchi hizo mbili na kukubaliana kuwa yatafutwe majibu ya matatizo yanayolikabili shirika hilo kwa sasa ili kuweza kuboresha miundombinu na kuunganisha reli hiyo na Bandari ya Dar es Salaam. [158]
safi
Zimbabwe, maarufu Warriors, ambao wanatamba kwa kosa safi na la uhakika, kiasi cha kuwa tishio katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika waliwasili nchini jana. [159]
sare
TIMU ya netiboli ya JKT Mbweni walitoka sare kwa kufungana 32 Shirika la Bima la Uganda katika mechi ya ufunguzi ya michuano ya Klabu bingwa Afrika Mashariki. [160]
sasa
Hawa ni maofisa wakubwa sasa nisaidie tufanyeje," alidai Zombe akimkariri Matage. [161]
shaba
Rais huyo alikuwa kwenye ziara ya kwanza nchini tangu achaguliwe kuongoza taifa hilo, ambalo uchumi wake mkubwa unategemea madini ya shaba, ambayo husafirishwa kupitia Bandari ya Dar es salaam. [162]
shosti
Na ushauri wa kupewaaa shosti. [163]
shule
Matokeo hayo yameathiriwa vibaya na shule za serikali ambazo nyingi zimeboronga na kuwafanya wadau wengi wa elimu, pengine hata serikali yenyewe kuhoji sababu za shule zake kufanya vibaya ikilinganishwa na za binafsi. [164]
sio
Katika historia ya hivi karibuni mgogoro kati ya Waisraeli (sio Israeli kama nchi) na Wapalestina ulianza katimk miaka ya 1920 baada ya vita kuu ya pili. [165]
sisi
Mmeonyesha mafundisho mliyoyapata kutoka kwa mwalimu wenu (Marcio Maximo) yamezaa matunda kwa kiasi kikubwa na sisi Watanzania tumepayaona na juhudi zenu zinaonekana kila siku. [166]
soka
Akizungumza na wachezaji na makocha wao Ikulu, Dar es Salaam jana wakati wa chakula cha mchana alichowaandalia, Kikwete alisema wachezaji hao wamefikia kiwango kizuri cha kuitangaza soka ya Tanzania, lakini wafahamu bado wana safari ndefu ikiwamo ya kuhakikisha wanafanya vyema katika fainali za Mataifa ya Afrika yanayoanza baadaye mwezi huu. [167]
somo
Timu hiyo imesheheni wachezaji wengi, wazoefu na wenye vipaji vikubwa na iliwasili nchini ikijigamba kuwa leo kuwa itatoa somo la jinsi ya kucheza kandanda na kuishinda Stars. [168]
tayari
Hadi sasa, tayari mashahidi watatu wametoa ushahidi katika kesi hiyo. [169]
tena
Wizara ya Fedha na Uchumi itafikiria kufanya tathimini tena kujua ukuaji halisi. [170]
tenga
Lakini alipofika kwenye tenga la tatu akaanza kutupa samaki mmoja baada ya mwingine, maana kila mmoja alionekana kuoza. [171]
toka
KIONGOZI wa bendi ya DDC Mlimani Park Orchestra, Shaaban Dede amewataka wabunge pamoja na serikali kuisaidia bendi hiyo ili kuhakikisha inapata haki zake stahiki toka kwa Shirika la Uchumi la jiji la Dar es Salaam (DDC). [172]
tuna
Sisi tunashukuru kuwepo kwa mtambo huu ambao unatusaidia katika mazoezi ya vitendo na hivi sasa hakuna kitu ambacho hatukijui kuhusu biogas na tuna uwezo wa kutengeneza mahali popote tukipelekwa. [173]
ujao
Rais Jakaya Kikwete amewaalika mawaziri wa fedha na magavana wa nchi zote za Afrika katika mkutano mkubwa utakaofanyika jijini Dar es salaam mwezi ujao kujadili mafanikio ambayo Afrika imepata na athari za mtikisiko wa kiuchumi duniani. [174]
ulafi
Hatuna ulafi, tuwatafute wasafi, hatuna ulafi tuwatafute wasafi. [175]
ule
Zambia yenyewe imejikuta ikifanya biashara ya shaba bila ya faida kubwa kwa kuwa inalazimika kusafirisha mali hiyo ghafi kwa usafiri wa barabara badala ya ule wa bei nafuu wa reli. [176]
una
SERIKALI haijafanya utafiti wa ili kujua kama moshi wa bangi inayoteketezwa na polisi una madhara au la kwa watu wanaokuwa karibu na moshi huo, bunge liliambiwa jana. [177]
uovu
Wapo wanaotafuta umaarufu kwa kutoa michango hadharani kwa lengo la kujitangaza lakini wengi wao ni waathirika wa maradhi ya kutojiamini, dhamira zao zinawasuta kwa uovu wao. [178]
uozo
Na hapo nikajikuta nimekaa chini huku harufu ya uozo ikiwa imeniletea kizunguzungu. [179]
usiku
Baada ya mkutano huo, Gaddafi alitoka mkutanoni akiwa kimya, na baadaye viongozi wengine walitoka mkutanoni saa 9 usiku huku wakiwa wameuacha kiporo mjadala huo kwa siku inayofuata. [180]
utu
Athari za kutanguliza vitu ni kuondoa utu, kwa hakika tamaa ya vitu siku zote huondosha utu. [181]
uweze
Lakini pia mgogoro wa dini unaingizwa ili uweze kutuzuga tusiweze kuona ukweli. [182]
uwezo
Dk Wanyancha alisema kuwa serikali inatazama uwezekano wa kujenga machinjio ya kisasa zaidi katika Jiji hilo ambayo yatakuwa na uwezo wa kuchinja kati ya ng’ombe 500 na mbuzi/Kondoo 1,400 kwa siku. [183]
vigumu
Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Kibira, aliliambia Mwananchi jana kuwa mashindano hayo yameanza vizuri na vigumu kutabiri kama timu za Tanzania Bara zinawe kufanya vizuri katika michuano hiyo. [184]
vya
Spika Sitta hakuridhika na maelezo hayo, akisema kuwa hakujibu kulingana na maagizo aliyopewa ya ama kukubali kufuta kauli ama kuwasilisha vielelezo vya maelezo yake, hasa ikizingatia kuwa hata yeye mwenyewe (Spika) alimsikia akieleza hivyo. [185]
vyake
Kwa hiyo ni lazima mtambo ulishwe chakula kulingana na vipimo vyake bila kuzidisha ili uweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. [186]
wakoloni
Waingereza walikuwa wakoloni kule Palestina, Iran na Iraq na maeneo mengine ya Mashariki ya mbali, India, Afghanistan. [187]
wala
Hawakuwa na nchi, serikali, wala dola. [188]
wale
Na kichekesho zaidi ni kuwa Yesu na Mtume walipingwa zaidi kiimani na watu wa mataifa yao kuliko wale wa makabila mengine. [189]
waliooza
Ilionekana wazi kwamba waliooza zaidi ni wale wa juu, kisha wale wa juu walikuwa wameambukiza wale wa chini uozo wao. [190]
wananuka
Na hata wachuuzi wenyewe walikuwa wananuka. [191]
wao
Zombe alikanusha ushahidi wote hasa kuwa aliwavamia baadhi ya ndugu wa marehemu Muhimbili na kuwatishia na kwamba hata maelezo yao yanatofautiana jambo ambalo alisema linaashiria ushahidi wao si kwa kweli. [192]
wapo
Anasema Watanzania wanatamani siku moja waone mabadiliko ya kweli katika maisha yao, waondokane na hali ngumu ya maisha lakini bahati mbaya ndoto zao hizo inakuwa vigumu kutimizwa kwa sababu wapo baadhi ya viongozi wasio wawajibikaji badala yake wamekuwa wababaishaji na walaji wa mali ya umma kwa maslahi yao binafsi. [193]
wiki
Maximo, anataka kushinda katika mechi hiyo ili kuweza kujua ni kiasi gani wachezaji wake wameiva, hasa baada ya kuwaandaa kwa zaisdi ya wiki ikiwamo ziara ya Zanzibar. [194]
yangu
Historia inaonesha kwamba siyo lazima kila mwenye mafanikio awe na furaha hapo maana yangu ni kwamba mafanikio ya mtu ni kitu cha binafsi kuliko mtazamo wa jamii au wa nje yake mhusika. [195]
yetu
Ni natumaini yetu kuwa tutafanya vizuri katika mechi hiyo kama wao waliwaza kutufunga nyumbani basi hata sisi tunaweza kufanya maajabu nyumbani kwani soka ni mchezo wa makosa," alisema. [196]
za
Naomba hii ya mshtakiwa wa tano niizungumzie kidogo na ninaomba busara za mahakama na za wazee wa baraza zitumike. [197]
zake
Mtazamo wa msukosuko wa kifedha wa sasa umekuwa kwenye nchi zilizoendelea kiuchumi na zile zinazoibukia, lakini athari zake kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara zitakuwa mbaya. [198]
zangu
Naomba nichukue furasa hii kuwasabahi marafiki zangu popote mlipo. [199]
zetu
Utaratibu ni mzuri na hauna fujo, lakini nauomba uongozi wa chuo kila wamalizapo kutoa majina ya wanafunzi waliofanyiwa udahili ,wayapeleke bodi ya mkopo ili tupate fedha zetu za kujikimu kwani tunazidi kuwa na maisha magumu kwa kuwa hatuna fedha za chakula na malazi,” alisema George. [200]