Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-24

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


adhma
Baada ya kushindwa kutimiza adhma yao ya kumwondoa Nkunda madarakani. [1]
aheri
Lakini aheri hata siasa. [2]
aina
Alisema matatizo hayo yalianza tangu lilipofanyika tamasha la Mkali Nani walipopata zawadi ya gari aina ya Toyota Hiace iliyosababisha Y dashi kupelekwa polisi walipokuwa wakigombea fedha hizo kwa ajili ya haki. [3]
ama
Inaonekana kama TFF ama wadau ama wahusika wa moja kwa moja na wachezaji hawana mikakati mizuri ya kuwaandaa wanasoka wetu wanaopata bahati ya kwenda kujaribu soka la kulipwa. [4]
amani
Huko ni kukosa uongozi bora na kuhatarisha amani na uhuru wa kweli wa wananchi kwa njia ya demokrasia ya uchaguzi. [5]
ambacho
Mwakilishi wa NCCR Mageuzi Peterson Mushenyera, alilalamika kwamba, Afisa Mtendaji wa kata ya Iyunga Mapinduzi alishusha bei ya mbolea kutoka shilingi 100,000 hadi shilingi 45,000/ kitu ambacho alisema ni rushwa katika uchaguzi. [6]
amefariki
Mwanamume mmoja anayefahamika kama kwa jina la Khalfani Sheriveji amefariki dunia baada ya kujinyonga. [7]
ana
Alisema mpaka sasa Karijo ana mkataba na FM Academia wa miaka miwili, lakini pamoja na kuwa na mkataba huo karijo hataondoka FM Academia. [8]
anaripoti
Naye Leon Bahati anaripoti kuwa Dk. [9]
au
Aliongeza kwamba kwa kauli hiyo Kikwete haitofautiani na kiongozi wa utawala wa kikoloni wa Rhodesia (Zimbabwe) Mwingereza Ian Smith ambaye aliwahi kutamka kuwa Waafrika hawawezi kujitawala hadi baada ya miaka 50 au 100, jambo ambalo Lipumba alisema halikuwezekana baada ya wananchi wa Zimbabwe kutokubali na kupigania uhuru wao hadi walipoupata. [10]
azidi
Naomba Mungu azidi kuwajaalia nguvu, maisha marefu na mafanikio kwa mwaka huu mpya. [11]
azma
Kwa namna hiyo, Mamlaka inatarajiwa kuendelea kutoa mchango unaostahili zaidi ya ule iliokwisha utoa katika kufikia azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania. [12]
bado
Wilbroad Slaa amesema bado haamini kama Rais Kikwete anaweza kutoa kauli hiyo, lakini akasema kama rais ametamka hayo, basi nchi imekosa utawala wa sheria. [13]
bali
Wazanzibari hawana haki ya kujichagulia rais wanayemtaka bali CCM na Serikali ya Muungano ndiyo itawachagulia rais wa kuwaongoza. [14]
bar
Wakati mke wake alikuwa amlala na yeye alikuwa bar akipiga pombe. [15]
bila
Januari 12 mwaka huu gazeti la Taifa Huru lilipigwa marufuku kusambazwa wakati wa kilele cha sherehe za miaka 45 ya Mapinduzi Zanzibar kisiwani Pemba bila ya kutolewa kwa taarifa rasmi kwa wamiliki wake, ambao walipanga kugawa bure gazeti hilo uwanjani. [16]
binadamu
Sasa, salaam ni salaam tu lakini bado ni mwanzo wa kumbagua binadamu mwenzio. [17]
bomu
Ili aamini kwamba kweli kuna mpango wa kulipua bomu ndani ya Nchi Tawala itabidi amwone huyu gaidi akiingia bungeni huko akiwa amebeba bomu mkononi. [18]
chako
Hakikisha kuwa besela ya kitanda ni imara unapotandika kitanda chako. [19]
chao
Kitu ambacho wananchi wa Pemba walivutiwa nacho sio tu kumwona Waziri Mkuu bali pia ni vile alivyoanza kuwashukuru wananchi waliojitokeza kumpokea na baadaye kutoa hotuba yake ya kuwataka wananchi washirikiane katika kuleta maendeleo katika kisiwa chao na mwisho alimalizia kwa kutoa fursa ya kuulizwa maswali. [20]
chongo
Kweli ushabiki ni chongo. [21]
dansi
Wageni waalikwa waliselebuka muziki wa dansi. [22]
daraja
Leo kamati ya mashindano itakutana na uongozi kuzungumzia maendeleo ya mchezo wa ligi kwa mzunguko wa pili pamoja na mashindano ya ligi daraja la kwanza na mashindano ya fainali za CHAN,"alisema Kaijage. [23]
duni
Mkapa alisema teknolojia duni za utunzaji wa kumbukumbu zilisababisha kampuni ya mshitakiwa wa kwanza kushindwa kuhakikiwa. [24]
dunia
Uamuzi huo wa serikali umekuja huku dunia nzima ikiwa na upungufu wa chakula na kwamba, bila ya jitihada za makusudi, janga la njaa litaikumba nchi yetu na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya nchi. [25]
es
Karibu wanafunzi 2,000 hawataweza kuendelea na masomo yao kwenye Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kurudi chuoni, ikiwa ni pamoja na kulipia sehemu za gharama ya elimu ya juu. [26]
eti
Tunaona ushabiki mtupu tunapoona hawa wanaojidai waumini wakitetea yasiyoteteka eti kwa sababu aliyetenda ni ‘mwenzetu’ wa dini yetu. [27]
fyongo
Mchezaji kiungo wa timu ya taifa alipiga fyongo na mpira ukatoka nje. [28]
hadhari
Kabla ya majina haya kuwekwa hadhari kwa mara ya kwanza. [29]
haijawahi
Alisema tangu kampuni hiyo isajiliwe mwaka 2003 haijawahi kuhakikiwa ili kujua taarifa za maendeleo yake. [30]
hakuna
Alisema kama kweli atakuwa ametamka hayo basi nchi itasambaratika kwa sababu kutakuwa hakuna uhuru wa utawala wa sheria. [31]
halina
Kwa hiyo hili neno hadhari halina maana iliyokusadiwa. [32]
hana
Rais hana nia njema na demokrasia," alisema Profesa Lipumba. [33]
hao
Wakati viongozi hao wakisema hayo, katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. [34]
hapa
Hata hivyo, barua hiyo imeonya kwamba haitakuwa sahihi kuendelea kuchapisha na kusambaza gazeti hilo hadi hapo taratibu za kisheria za usajili zitakapokamilika na kuruhusiwa rasmi kuchapishwa na kusambazwa Visiwani hapa. [35]
hapo
Alisema migogoro inayotokea chuoni hapo inatokana na itikadi za kisiasa ambazo huingizwa katika taaluma na kusababisha vurugu, migomo na matatizo mengine. [36]
haramu
Kwa hiyo ni sahihi kuandika, Mwanamume mmoja anayefahamika kwa jina la Khalfani Sheriveji amefariki dunia kwa Watu 120 wanaosadikiwa kuwa ni wahamiaji haramu wamekamatwa. [37]
hatua
Tunaitaka serikali kumchukulia hatua cha kisheria na kumwajibisha kwa kuwa anapotosha ukweli kuhusu suala la uchangiaji elimu ya juu," alisema Charles. [38]
hawa
Natoa shukrani sana kwa wasomaji na waandishi hawa na nawasihi waendelee na juhudi zao. [39]
hewa
Majukumu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ni pamoja na kuchunguza, kukusanya, kuhakiki na kuratibu taarifa za hali ya hewa na kuzisambaza nchini. [40]
hicho
Lipumba alisema kauli ya rais, ambaye aliahidi kushughulikia mpasuko uliotokana na kutangazwa kwa matokeo ya urais katika uchaguzi wa mwaka 2005, imekivunja moyo chama hicho kwa kuwa inapingana na wajibu wake. [41]
hiki
Aliwataka wakazi wa Kata hiyo ambao hawakuwepo kwenye mkutano kukubaliana na maamuzi hayo, ili kufanikisha malengo ya maendeleo ya kata kwa faida ya kizazi hiki na cha baadaye. [42]
hilo
Slaa amesema haamini kuwa Rais Kikwete ametoa tamko hilo na kama ametamka basi nchi imekosa utawala wa sheria. [43]
hivi
Alisema hivi sasa kiwanda hicho tayari kimeshafunga mashine hizo hivyo kitaanza kununua pamba kutoka kwa wakulima, tayari kwa kutengeneza vitambaa vipana, jambo ambalo ni ukombozi kwa mkulima. [44]
hofu
Lipumba alisema katika shahada nambari 44347062 alijiandikisha kwa jina la Wiliam Sisala Simwali ikionyesha tarehe ya kuzaliwa 13/10/1968 katika kata ya Ilembo na kwamba hali hiyo inaleta hofu kwao na kuamini kuwa hizo ni mbinu za CCM katika kujihakikishia inapata ushindi katika jimbo hilo. [45]
hotuba
Katika hotuba yake baada ya kuingia madarakani Rais Jakaya Kiwete, pamoja na mambo mengine aliahidi kuushughulikia mpasuko wa kisiasa uliopo visiwani Zanzibar, lakini jitihada zake za serikali yake kutafuta muafaka zimeishia kwa CUF kutangaza kujitoa kwenye mazungumzo. [46]
huku
SHIRIKA la Posta Tanzania (TPC), linajiendesha katika mazingira magumu kimtaji huku likilemewa na mzigo wa deni la zaidi ya Sh 17 bilioni. [47]
huo
UMOJA wa Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu vya Umma (Uvejuta), umemtaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jumanne Maghembe, kushtakiwa kwa kutumia vibaya madaraka yake kama ilivyokuwa kwa mawaziri wastaafu, Basil Mramba na Daniel Yona Mramba na Yona, ambao walikuwa mawaziri katika serikali ya awamu ya tatu, wameshtakiwa kwa tuhuma za kutumia vibaya ofisi zao, na umoja huo wa wanafunzi unamuona Maghembe kuwa naye ametumia vibaya ofisi. [48]
huu
Aliongeza kuwa kwa sasa menejimenti ya chuo haijazungumzia suala hilo na kwamba idadi ya wanafunzi inazidi kuongezeka kwani wameongeza muda wa udahili hadi Januari 29 mwaka huu. [49]
huyu
Kwanza ya yote kuna vitu shostito vya kuangalia; huyu mtu anakuheshimu kiasi gani anakupenda kiasi gani na anakujali kiasi gani. [50]
ijayo
Taarifa zilizopatika katika kilele cha miaka 15 ya shirika hilo, zilisema tangu kuanzishwa kwake mwaka 1994 hadi sasa, TPC inadaiwa zaidi ya Sh17 bilioni na bado linahitaji mtaji wa Sh 30 bilioni, kutekeleza mkakati wake wa kipindi cha miaka mitano ijayo. [51]
ikawa
Mfano zipo meseji watu wanatumiana "Vipi Dear!" unakuja, na hii ikawa ni meseji ya kawaida kabisa kwa mtu na mfanyakazi mwenzake kazini lakini kwako ikawa na sura nyingine tofauti kabisa na makusudiao yenyewe. [52]
iko
Mbali na gazeti la Taifa Huru, kampuni ya Zanzibar Media Cooperation pia inamiliki kituo cha redio cha Zenj FM na iko katika mchakato wa kuanzisha kituo cha televisheni Visiwani Zanzibar. [53]
ila
Lakini ukimwacha yeye, hakuna waziri mkuu mwingine aliyewahi kutembelea kisiwani Pemba na kulala hadi asubuhi ila John Malecela ambaye alitembelea kwa kutwa moja tu. [54]
ile
Hata hivyo alisema baada ya masuala ya EPA kuanza, majalada ya makampuni yaliyotajwa yalichukuliwa na ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na ile ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) na kwamba hadi leo hayajarudishwa. [55]
ili
Alifafanua kuwa ili kutatua matatizo hayo, uongozi wa UDSM hauna budi kusimama katika taaluma, badala ya kukiendesha chuo kisiasa. [56]
iliamua
Kutokana na utafiti huo Serikali ya Mtaa wa Makangarawe baada ya kupewa kipaumbele na serikali kuu, uwezo wa kuwa karibu na watoto wanaoishi katika mazingira magumu, iliamua kujikita zaidi katika mpango wa kuwasaidia watoto hao. [57]
imara
KOCHA Manyema, Abdalah Kibadeni 'King' amesema kwa sasa anaaindaa kikosi chake kwa kucheza mechi nyingi za kujipima nguvu kwa lengo kutegeneza timu imara zaidi. [58]
ina
Nondo alisema kata hiyo ina shule ya Sekondari iliyopo Mtaa wa Tubuyu ndani ya Manispaa ,lakini ujenzi wake unasuasua kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo yasiyoeleweka. [59]
inashiriki
Timu ya Miembeni inashiriki michuano ya Klabu bingwa Afrika wakati timu ya Mundu yenyewe inashiriki michuano ya Shirikisho. [60]
inaweza
Kwa hiyo baada ya kulijadili menejimenti inaweza kutoa tamko juu ya suala hilo lakini uongozi hauna nia mbaya katika udahili mpya wa wanafunzi," alisema Prof Lihamba. [61]
isiwe
Waziri Mkuu amesema tofauti za kisiasa na kiitikadi isiwe sababu ya kutofanya shughuli za maendeleo kwani ikitokea hivyo nchi haiwezi kwenda kwa mtindo huo na wanaoumia kwa kukosa maendeleo ni wananchi ambao ndio waliowaweka viongozi madarakani kwa kuwachagua na kuwaamini kuwa viongozi hao watawaletea maendeleo. [62]
iwe
Kwa nini iwe kwa wachezaji wetu kila mara tuambiwe wanashindwa? Ni jukumu la TFF kuangalia pale wachezaji hao walipojikwaa ili kuzuia wengine wasijikwae tena. [63]
je
Ikiwa hata ofisi hamna hii mliyonayo mmekodi, je, wakikatisha misaada yao wapi mtapata fedha au ndo na hii ofisi mtairudisha kwa mwenyewe," alihoji Mhagama. [64]
jipya
Wasanii hao wamejitoa rasmi na kuanzisha kundi lao jipya linaloitwa Temeke Unit chini ya meneja wao mpya Issa Abdalah ambaye wamemtaja kuwa ndiye pendekezo lao na mtetezi wa maslahi yao. [65]
juu
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa juu wa CUF- mwenyekiti Prof. [66]
kabla
Barua hiyo pia imeeleza kwamba awali msajili wa magazeti wa Idara ya Habari alikiri kupokea barua ya kuomba kubadilisha jina la gazeti la kutoka Asumin, ambalo pia lilikuwa linamilikiwa na kampuni hiyo, kwenda Taifa Huru, lakini kabla ya kukubaliwa kusajiliwa, gazeti hilo lilichapishwa na kusambazwa. [67]
kadhaa
MARA baada ya timu yetu ya soka ya taifa kuanza kufanya vizuri na kuonyesha kiwango cha kuvutia, mawakala wa soka kutoka sehemu kadhaa duniani, baadhi ya wachezaji walioonyesha kujituma katika michezo mbalimbali wameanza kufuatwa na mawakala hao kwa lengo la kuwapeleka kwenye vilabu nje ya nchi. [68]
karibu
Aidha wapinzani hao wa Tanzania Prisons wanatarajia kuwasili nchini Alhamisi kwa ndege maalamu, na TFF wakiahidi kufuatilia kwa karibu maendeleo ya wawakilishi hao wa nchi ili waweze kupata matokeo mazuri. [69]
kasi
Kipindi cha pili kilianza kwa timu kushambuliana kwa zamu ambapo dakika ya 48 Khalfan aliongeza bao la tatu kwa upande wa Moro baada ya kukimbia kwa kasi na kupiga shuti lililoenda moja kwa moja wavuni. [70]
kata
Malange alisema kuwa, amewaandikia waraka watendaji wa kata na vijiji kuwakataza kutumia mbolea hiyo kuwabagua wanachama wa vyama mbali mbali vya siasa. [71]
kiasi
Aidha alisema kuwa katika eneo walilopanga kwa ajili ya ofisi yao wanalipa kiasi cha dola 3,000 za Kimarekani. [72]
kidogo
Lakini hata hao wana CCM kidogo waliopo wanapaswa kutunzwa na kuthaminiwa ili nao wajisikie wana thamani katika ujenzi wa demokrasia kwa kuchagua chama wanachokitaka badala ya kupuuzwa na kuonekana kuwa ni wachache hivyo hawana mchango katika gurudumu la kuendeleza demokrasia nchini. [73]
kila
Akizungumza kwa njia ya simu jana Ismail alisema amepokea barua kutoka SMZ ya kulipiga marufuku gazeti hilo ambalo linatakiwa kutoka kila Jumanne. [74]
kilimo
MSIMAMIZI wa uchaguzi mkoani Mbeya, Juliana Malange, ametetea matumizi ya vitambulisho vya kupigia kura katika ununuzi wa pembejeo za kilimo na mbolea mkoani humo. [75]
kitendo
Hivi karibuni vyama vya CUF, NCCR Mageuzi, TLP na TPPPMaendeleo walilalamikia kitendo cha watendaji wa kata kuchukua vitambulisho vya wapigakura wao kwa kisingizio cha kununulia Mbolea. [76]
kocha
Katika michuano hiyo inayoanza Februari 22, Stars imepangwa kundi A na wenyeji Ivory Coast, Senegal na Zambia ambayo kocha wake, Mfaransa Herve Renald amechanganyikiwa baada kwa nyota wake aliowatengeneza kwenye kombe la chalenji Jijini Uganda, kukimbilia Ulaya. [77]
kote
Mimi sikisemi chama chochote kile maana ushabiki huo uko kote kote, kwa chama cha zama zile hadi chama cha zama hizi. [78]
kuandika
Hata hivyo sitachoka kuandika makala pale inapobidi. [79]
kubuni
Kama hatuna mikakati hiyo, basi sasa ni wakati mwafaka kwa TFF, na wadau wa soka kwa ujumla kubuni mikakati hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho kuna dalili za soka letu kuanza kupanda huku kukiwa na ligi ya taifa inayolenga kuinua vipaji na viwango vya soka. [80]
kuchokwa
Afadhali hata mpira maana hatimaye mashabiki wataanza kudai mabadiliko lakini katika siasa, watu watashabikia weeeeeeeeeeeee huku chama fulani kimeshapondwa badala ya kupendwa, kimechekwa na kuchokwa na hata kuchukiwa kutokana na kuchakaa kwake. [81]
kudai
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum, Malange ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halamshauri ya mkoa wa Mbeya, alisema kwa kuwa wananchi hawana vitambulisho vya uraia, ofisi yake imewaagiza watendaji wa vijiji kudai vitambulisho hivyo kwa ajili ya kuwatambua wakulima. [82]
kujua
Alisema walishaiandikia barua Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar kuielezea masikitiko yao ya kuzuiwa kusambaza gazeti la Taifa Huru pamoja na kujua sababu za msingi zilizosababisha kuzuiwa. [83]
kule
Tanzania nimeona ina wachezaji wengi sana wazuri na kikosi chake nilichokiona kule kwenye Chalenji Uganda ni kizuri nakiamini,"alisema Baraza. [84]
kuleta
Kesi hiyo jana ilikuwa iendelee kusikilizwa kwa mashahidi wengine kutoa ushahidi, lakini iliahirishwa baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuleta mashahidi wawili. [85]
kuliko
Baada ya kushindwa kufikia makubaliano na kampuni ambayo waliomba iwasaidie mchakato huo na wao kutaka fedha nyingi kuliko walizopewa na wadhamini wao TBL waliamua kutuma maombi kwa wadhamini wao iliwaweze kuwasaidia mchakato huo lakini bado hawajajibiwa. [86]
kuna
Alisema tayari wamo katika mchakato wa kuomba usajili Tanzania Bara baada ya kubaini kuwa Zanzibar kuna matatizo katika suala zima la demokrasia ya uhuru wa habari. [87]
kuondoa
Hatupingi hatua hizo, lakini tunadhani hazisaidii kuzuia mauaji wala kuondoa fikra za ushirikina kwenye akili za watu. [88]
kupata
Utaratibu huu umewekwa ili kuwawezesha wakulima kupata mbolea kwa bei rahisi. [89]
kupimia
Kinachotia moyo zaidi ni kufungwa kwa vituo vya kupimia hali ya hewa vinavyojiendesha vyenyewe katika maeneo ya Mtwara, Bukoba, Babati, Tabora, Kigoma na Kibondo. [90]
kupotosha
Hapa tena kuna matatizo ya kuchanganya /r/ na /l/ katika maandishi na kupotosha maana inayokusudiwa. [91]
kusema
Siamini kwamba Rais anaweza kusema hayo. [92]
kuua
Mikakati ya maandalizi ya TFF, mawakala wa ndani na klabu husika ihusishe pia nchi ambayo wachezaji hao wanakwenda kwa sababu nchi nyingine hazisaidii kuinua kiwango cha uchezaji na badala yake wahusika wanakwenda huko kuua vipaji vyao. [93]
kuuza
Mhariri huyo mtendaji alisema SMZ pia imewafungia milango ya kufanya biashara kwa kuuza gazeti ambalo walishaingia mkataba na baadhi ya makampuni kwa ajili ya kutoa matangazo yao. [94]
kuvuruga
Baadaye viatu hivi vitatolewa kwa watoto yatima ili na wao waweze kumkumbuka aliyefanikiwa sana kuvuruga amani ya dunia, uchumi wa dunia na mazingira ya dunia, baada ya kuvuruga demokrasia ya dunia ndani ya nchi yake mwenyewe wakati wa ‘kuchaguliwa’ mara ya kwanza. [95]
kuwekwa
Kikwete anamaanisha serikali itaendelea kuwekwa na wao. [96]
kuweza
Sekondari ya kata yao na kuweza kuwapokea wanafunzi mapema iwezekanavyo. [97]
kwao
Wakili wa serikali Boniface Stanslaus alisema walienda kuwafuatilia mashahidi nyubani kwao, lakini hawakuwakuta. [98]
la
Akitoa tamko la umoja huo jana, rais wa Uvejuta, Godbless Charles alisema jana Maghembe anatakiwa kushtakiwa kwa kutokana na kauli yake kwamba sera ya uchangiaji elimu vyuo vikuu haina mapungufu na kuwataka wanafunzi kuikubali, akisema kauli hiyo inaonyesha jinsi asivyowajibika. [99]
labda
Neno gungulika halimo katika Kiswahili labda linatokana na lugha ya kikabila. [100]
lao
Ismail alisema kuzuiwa kusambazwa kwa gazeti lao kuliwafanya waingie hasara kubwa, akisema zaidi ya Sh12 milioni zilipotea ikiwemo gharama za kuchapisha nakala 3,000, kuchapisha fulana 1,500 kati ya hizo fulana 300 zilikuwa zigawiwe bure kwa wasikilizaji wa redio ya Zenj FM, kuchukua wafanyakazi sita kutoka Dar es salaam kwenda Pemba, pamoja na gharama nyingine za kusafirisha magazeti kutoka Dar es salaam hadi Pemba. [101]
leo
Naye Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam Suleiman Kova jana alizungumza na waandishi wa habari kueleza sababu zilizomfanya azuie maandamano ya wanafunzi wa UDSM yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo. [102]
licha
Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, kocha huyo maarufu katika medani ya soka nchini alisema kuwa licha ya kuwa timu hiyo imesajili wachezaji 30, lakini anataka kutengeza kikosi cha wachezaji 22 wenye uwezo sawa. [103]
ligi
Naamini kwamba ikienda kwenye mashindano ya CHAN mwezi ujao itafanya vizuri, wachezaji wake wanaweza kushindana hata kwenye ligi za ndani wanafanya vizuri sana ni matokeo mazuri. [104]
lina
Haifai kuandika jambo ambalo lina utata. [105]
linalofaa
Hapa neno linalofaa ni kushadidia maana yake ni kufanya kuwa imara au madhubuti, kushikilia jambo kwa nguvu. [106]
lugha
Katika lugha ya Kiswahili neno shadadia halimo na ni makosa kubuni neno ambalo siyo la Kiswahili na kulitumia bila ya uangalifu na kwa kuzingatia taratibu za uandishi. [107]
lukuki
MALALAMIKO juu ya ukosefu wa maji safi na salama kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, yamezidi kuwa mengi huku lawama lukuki zikipelekwa kwa Kmpuni ya Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (Dawasco). [108]
maandishi
Maneno yanayofaa hapa ni mchanganuo wa mradi, kwa maana kwamba hakuna nchi hata moja iliyopeleka uchambuzi wa maandishi wa mradi ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya nchi. [109]
makala
KWA kipindi kirefu sasa nimekuwa nikiandika makala kuhusu matumizi bora ya Kiswahili katika magazeti yanayochapishwa hapa nchini. [110]
makubwa
Anatonesha vidonda na majeraha makubwa ya kisiasa. [111]
mara
Ibrahimu lipumba alisema kuwa baada ya kufanya uchunguzi katika daftari la wapiga kura walibaini Mwenyekiti huyo akiwa amejiandikisha mara mbili ambapo katika shahada namba 0255615 amejiandikisha kwa jina la Wiliamu Sisala Simwali ikionyesha kwa maneno kuwa ni mtu mzima. [112]
matarajio
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ni miongoni mwa taasisi za umma ambazo, kwa kipindi kilichopita, zilikuwa zinalalamikiwa sana na wananchi kutokana na huduma duni zisizokidhi matarajio ya wananchi zilizokuwa zikitolewa na taasisi hizo. [113]
mawili
Chuo cha Hali ya Hewa Kigoma, kimeendelea kuboreshwa kwa kujengewa madarasa mawili zaidi. [114]
mbovu
Alisema sera hiyo ni mbovu, ya kibaguzi na inawakandamiza watoto wa maskini na kuwabeba watoto wa matajiri, hivyo inatakiwa kufanyiwa marekebisho. [115]
mdogo
Katika hatua nyingine jumla ya wananchi 127,780 Kesho wanatarajia kupiga kura za kumchagua mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini katika uchaguzi mdogo kutokana na nafasi ilyoachwa wazi baada ya kifo cha Mbuge Richard Nyuala. [116]
mfumo
CUF na CCM zimekuwa zikichuana vikali kwenye chaguzi za urais visiwani humo na tangu kuruhusiwa kwa mfumo wa vyama vingi, CCM imekuwa ikishinda kwa tofauti ndogo, matokeo ambayo yamekuwa yakizusha utata mkubwa na kusababisha ghasia, ambazo zilifanya baadhi ya wananchi wa Pemba kwenda Mombasa kuishi kama wakimbizi mwaka 2000 baada ya watu zaidi ya 27 kuuawa. [117]
mfupi
Renard alisema; "Siogopi lakini inasumbua kupoteza wachezaji watano tegemeo mwezi mmoja kabla ya CHAN. Ni vigumu kufanya kazi na wachezaji wapya ukiwa na muda mfupi. [118]
mhariri
Sikupewa sababu wala sikupewa barua rasmi,” alisema Daud Ismail, ambaye ni mhariri mtendaji wa gazeti hilo. [119]
mikoa
Mauaji ya aina hiyo yalienea pia katika mikoa mingine. [120]
mimi
Alisema katika kundi lao jipya wameshafanikiwa kufanya ziara ya miezi mitatu katika nchi za Burundi, Rwanda, Uganda na Kongo huku wakifanikiwa kurekodi nyimbo mbalimbali ikiwemo ya More Fare ambayo waliirekodi wakiwa Rwanda wakimshirikisha Sister mimi. [121]
mishale
Amesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana mishale ya saa 10:30 katika eneo la Sabasaba. [122]
mitaani
Aliandika neno kulingana na jinsi linavyotumika mitaani. [123]
mke
Amesema CCM ni chama jeuri na kikubwa hivyo bila ya kuwa na ofisi inayoonekana ni sawa na baba mwenye mke aliyekosa kuwa na nyumba. [124]
mpango
Nawapa nafasi kubwa kwenye kundi lao,"aliongeza mchezaji huyo huku akisisitiza kuwa hana mpango wa kuondoka Yanga hadi atimize malengo yake. [125]
mradi
Kwa mfano: Hakuna hata serikali moja katika nchi za SADC ambayo imeleta mchakato wa mradi. [126]
mtaa
Alisema ili kufanikisha suala hilo la kijamii la uchangiaji watoto wanaoishi katika mazingira magumu, ofisi ya mtendaji kata pamoja na kamati ya mazingira hatarishi mtaa wa Makangarawe zinatakiwa kushirikiana na mratibu wa mpango huo ili kuwawezesha kupata wafadhili. [127]
mto
MAMLAKA ya Maji safi na Maji taka ya Dar es Salaam (DAWASCO), imetahadharisha uwezekano wa mto Ruvu kukauka ndani ya siku 14 zijazo endapo mvua hatanyesha jambo ambalona kusababisha ukosefu wa maji jijini, ikiwa mvua hazitanyesha. [128]
muhimu
Ziara ya Pinda imefichua jambo moja muhimu ambalo nadhani viongozi wengi hawalifahamu na iwapo litafanyiwa kazi basi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaweza kujipatia wafuasi wengi lakini kutokana na kupuuzwa kwa wanachama hao wachache waliopo ndio sababu kubwa inayofanya wananchi wa kisiwani Pemba kukosa maamuzi ya kukipenda chama hicho kama alivyobainisha Mzee Ahmad Ali Mussa ambaye alisimama kutoa maelezo wakati Waziri Mkuu alipotoa fursa ya kuuliza maswali. [129]
mwa
Alisema malengo ni kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo,unakamilika mwishoni mwa mwezi Februari ili wanafunzi waanze masomo mapema mwezi Machi mwaka huu. [130]
mwezi
Tangu mwaka 2006 bei ya maji haijapanda, lakini gharama za uendeshaji ikiwemo umeme zimekuwa zikipanda mara kwa mara, hali hii inafanya Dawasco ijiendeshe kwa gharama kubwa," alisema Kaaya Alisema Mamlaka yake imekuwa ikilipa zaidi ya Shilingi milioni 6 kwa mwezi zikiwa ni gharama za uendeshaji wa mitambo ya Ruvu chini na ruvu juu. [131]
na
KAULI ya Rais Jakaya Kikwete kuwa wapinzani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) watalazimika kusubiri kwa muda mrefu na pengine wasipate nafasi ya kushika madaraka visiwani humo, imewasha moto mpya baada ya Chama cha Wananchi (CUF), kuielezea kuwa imetonesha vidonda vya kisiasa. [132]
namba
Alisema wanafunzi hao waliliandikia barua jeshi hilo Januari 19, ikiwa haina namba ya kumbukumbu. [133]
nao
Akijibu hoja za wabunge Mariki alikiri kuwa mtikisiko huo umewagusa na kwamba wameshapewa tahadhari na wahisani hasa kwa miradi ambayo hawajaingia nao mikataba. [134]
ndio
Mshambuliaji Rodger Kola wa Zanaco ndio wa mwisho kuondoka juzi kuelekea Sweden huku wachezaji tegemeo, kwenye ulinzi, Emmanuel Mbola, Francis Kasonde, kiungo William Njobvu na mshambuliaji matata Given Singuluma wakiwa wameshatua Ulaya. [135]
ndipo
Shahidi huyo, Andrew Mkapa ambaye ni Msajili Msaidizi wa Wakala wa Usajili wa Makampuni (Brela), alisema masuala ya EPA yalipoanza na majina ya makampuni kutangazwa kwenye vyombo vya habari ndipo waligundua mmiliki wa kampuni ya Rashhaz ambayo ni ya mshitakiwa wa kwanza, Rajabu Maranda. [136]
ngozi
Mwishoni mwa miaka ya 1990 yalizuka mauaji ya watu ambao ngozi zao zilichunwa na kuuzwa na katika siku za hivi karibuni yamejitokeza mauaji ya kutisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino. [137]
ni
Kikwete alitoa kauli hiyo juzi katika siku ya mwisho ya ziara yake kisiwani Pemba ambako ni ngome kuu ya CUF, aliposema kuwa ni bora wanaouwanga mkono wapinzani wakashirikiana na serikali ya CCM kuweka maendeleo visiwani humo kwa kuwa itawachukua muda na pengine iusiwezekane kabisa kutwaa madaraka. [138]
nia
Hana nia ya kuziba mpasuko wa kisiasa ulio Zanzibar ambao alisema anaushughulikia. [139]
nyuma
Alisema hatua ya kurudisha mchezo huo nyuma imekuja baada ya TFF kuarifiwa na uongozi wa uwanja wa Taifa kuwa Jumapili uwanja utakuwa unatumika kwa ajili ya shughuli nyingine. [140]
papo
Waziri Mkuu alisema amepata uzoefu mkubwa akiwa bungeni katika kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo. [141]
pia
Kiongozi huyo wa wanafunzi pia aliutaka uongozi wa UDSM kuacha kukiendesha chuo hicho kwa itikadi za vyama vya siasa, badala yake itafute njia ya kutatua matatizo, ikiwemo migomo. [142]
pili
SHAHIDI wa pili katika kesi ya wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inayomkabili Kada wa Chama Cha Mapinduzi na wafanyakazi watatu wa BoT amesema vyombo vya habari ndivyo vilivyowasaidia kugundua Kampuni ya mshitakiwa wa kwanza. [143]
poa
Na kwa kuwa Makengeza Enterprises haitaki watu wapekue baadaye na kupata funza badala ya mafunzo, viatu maalum vitauzwa kwa bei poa hapohapo kwenye tamasha. [144]
rafiki
Ninaye rafiki yangu ambaye alikuwa mpigania uhuru wa Afrika Kusini. [145]
rasmi
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imelipiga marufuku rasmi gazeti ya la Taifa Huru linalotolewa na kampuni ya Zanzibar Media Cooperation (ZMC) inayomilikiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -Muungano, Seif Muhammad Khatib, kuingia visiwa vya Zanzibar. [146]
roho
Huku wachezaji hao ambao ni roho ya Zambia wakipepea na Tanzania ikichekelea, Baraza amesema kwamba anaamini uwezo wa wachezaji wa Tanzania hivyo hana wasiwasi na utendaji wa kikosi hicho. [147]
saa
Hatukuona sababu za msingi za kuzuiwa kusambaza gazeti letu lakini kwa kuwa nilipigiwa simu saa 6:30 usiku, ilinibidi nikubali agizo la Naibu Katibu Mkuu Said Shaaban. [148]
sare
Timu hizo leo zitakutana tena kwa mara ya tatu ambapo Azam Fc ikishinda mchezo mmoja dhidi ya Polisi Dodoma na kutoka sare na Moro UTD huku JKT Ruvu ikiifunga Toto African ya Mwanza na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Yanga. [149]
sasa
Basi sasa tusubiri tuone," alisema Maalim Seif. [150]
sawa
Alisema, mpaka sasa, zaidi ya wanafunzi 27,289 hawajaweza kulipa gharama za masomo na kwamba pamoja na waliosimamishwa jumla ya wanafunzi 31,443 hawako chuoni, ambayo ni sawa na asilimia 87 ya wanafunzi wote. [151]
sekta
Wakati rais akitoa maelekezo kama hayo, ni vyema viongozi wengine wenye majukumu ya kusimamia kilimo, wakajiunga pamoja na jitihada za rais ili zoezi la kuimarisha sekta ya kilimo likafanikiwa na hivyo kuwaletea neema wakulima ambao ni wengi, lakini wanaongoza kwa umasikini nchini. [152]
shaka
WABUNGE wameutilia shaka uendelevu na utendaji kazi wa Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya Wanyama (WWF) kufuatia kubainika kuwa asilimia 95 ya bajeti yake, inatoka kwa wahisani wa kimataifa. [153]
shirika
Hayo yalikuja baada ya wabunge wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii kutembelea ofisi za shirika hilo na kuelezwa kuwa asilimia 95 ya bajeti yake, inatokana wahisani wa kimataifa. [154]
shule
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amir Nondo alisema uamuzi wa wazazi kuchangia kiasi hicho cha fedha ulifikiwa hivi karibuni na unalenga kukamilisha ujenzi wa madarasa sita yatakayowawezesha wanafunzi kuanza masomo katika shule hiyo. [155]
si
Kauli hiyo itazidisha mpasuko uliopo kwa kuwa inamaanisha wananchi wa Zanzibar waishie kuchagua, madiwani, wawakilishi na wabunge lakini si serikali," alisema akirejea kauli ya Kikwete kuwa wabunge hawana serikali hivyo hawawezi kuwajengea barabara wala huduma nyingine za jamii. [156]
sio
Kwa kweli sisi tulikuwa tumo katika process za kuomba usajili upande wa Tanzania Bara maana tumebaini kuwa huko kwenu kuna matatizo makubwa katika suala zima la uhuru wa habari, lakini pia tuliamua kulileta gazeti letu hivyo hivyo ili tuone tutachukuliwa hatua gani maana sioni kama tumevunja sheria na kama tumevunja sheria basi tupelekwe mahakamani sio kutishana," alisema Ismail. [157]
siyo
Alisema serikali inapaswa kutumia pesa zake yenyewe ili kusaidia huduma ya maji na siyo kusubiri fedha za wafadhili. [158]
tamaa
MWENYEKITI wa Prisons, Salum Chambusha amesema kuwa wameshakata tamaa ya kuitetea nafasi yao ya pili msimu huu kutokana na kiwango kinachoonyeshwa na timu yake. [159]
tegemezi
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa WWF (T) Hermen Mwageni, alikiri kuwa na bajeti tegemezi, lakini alisema huo ni utamduni kwa kuwa hata serikali ni tegemezi katika bajeti yake. [160]
tena
Amesema hatua hiyo imekuja kufuatia kushuka kwa bei ya pamba duniani na kwamba kama viwanda vikiendelea kuagiza pamba kutoka nje, wakulima wataathirika zaidi na hatimaye, kutotamani tena kulima zao hilo, jambo ambalo ni hatari kwa uchumi wa taifa. [161]
tu
Hata hivyo Nagu aliwataka wamiliki wa kiwanda hicho kuboresha maslahi na hali za wafanyakazi wao kwa kuwafungulia saccos ili waweze kukopa na kujikwamua kiuchumi badala ya kuendelea kutegemea mishahara tu, mshahara tu. [162]
tuseme
Tuondoshe tofauti zetu na tukubali kusema ukweli pale penye ukweli jitihada zisipuuzwe tutende zaidi na tuseme kidogo dhamira yetu njema itaonekana," amesisitiza Waziri Mkuu. [163]
udahili
Alisema umoja huo pia unapinga hatua ya UDSM kuwafutia udahili baadhi ya wanafunzi kwa kushindwa kutimiza masharti yaliyowekwa na uongozi wa chuo hicho, kuwataka wakubali sera ya uchangiaji elimu ya juu, jambo ambalo linapingwa na wanafunzi hao. [164]
ujinga
Tunashauri zitafutwe njia nyingine ukiwepo mjadala wa kitaifa kuzungumzia tatizo hilo, kubuni mikakati ya kuondoa ujinga, kuongeza elimu, kuongeza kipato na maisha bora ya watu kwa njia halali. [165]
ule
Akijibu swali la Hakimu Mkuu Mkazi, John Utamwa (Naibu Msajili wa Mahakama Kuu) shahidi huyo alisema utunzaji wa kumbukumbu za makampuni Brela ni ule wa mifumo ya kizamani. [166]
ulikuwa
MCHEZO kati ya timu ya Azam FC na JKT Ruvu ambao ulikuwa ufanyike kesho Jumapili, sasa utachezwa leo katika uwanja wa Taifa baada ya shirikisho la soka kualifiwa na uongozi wa uwanja kuwa siku hiyo utatumika kwa shughuli nyingine. [167]
umuhimu
Akizungumzia hali hiyo Mwenyeki wa Kamati ya Bunge ya Kilimo na Aridhi, Gidioni Cheyo, alisema wananchi wanapaswa kujua kuwa kuna umuhimu wa kulipia huduma ya maji kutokana na ukweli kuwa uzalishaji wake ni wagharama. [168]
una
Tusingetoa lawama kwani mwanzo wa kila kitu una ugumu wake na hasa kwa nchi zinazoendelea Tanzania ikiwa mojawapo. [169]
upya
Alisema Uvejuta inaliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali kuipitia upya sera ya uchangiaji wa elimu kwa vyuo vikuu ili waweze kubaini mapungufu yaliyopo na kuirekebisha ili iweze kuwasaidia watoto wa maskini. [170]
usafiri
Miongoni mwa sekta zinazonufaika na taarifa za TMA ni sekta za kiuchumi na kijamii kama vile sekta za usafiri, kilimo, maji, mazingira na ujenzi. [171]
vifaa
Jitihada nyingine za Mamlaka katika kuboresha huduma hizo, zinadhihirishwa na kufungwa kwa mitambo na vifaa mbalimbali katika baadhi ya maeneo hapa nchini. [172]
vijana
Chambusha alisema kuwa timu yake kwa sasa imekuwa ikifanya vibaya kutokana na kuwa na wachezaji wengi vijana ambao bado hawajazoeana. [173]
vingine
Na cha kufurahisha zaidi ni kufufuliwa kwa vituo 360 na kuanzishwa kwa vingine vipya 197 vya kupimia mvua nchini. [174]
vituo
Kwa mujibu wa msimaizi wa uchaguzi mdogo jimbo la Mbeya vijijini Juliana Malange jumla ya vituo 395 vitatumika katika kupigia kura na kwamba wanatatumia daftari la wapiga kura lilofanyiwa maboresho mwaka jana. [175]
vyao
Mwenyekiti wa TPP Maendeleo alisema wananchi wa kata ya Isupo walitakiwa kukabidhi vitambulisho vyao vya kupigia kura na hadi juzi vilikuwa havijarudishwa. [176]
wakuu
TBL ambao ndio wadhamini wakuu wa Simba na Yanga waliwataka kutafuta Katibu na Mhazini wa kuajiliwa. [177]
wale
Sisi tusonge mbele na wale wakorofi tuachane nao tuwabakishe nyuma maana tukiwafuata tutapotea," alisisitiza. [178]
wana
Mzee Mussa alisema Pemba wapo wana CCM tena wenye kuumwa na chama chao isipokuwa uongozi uliopo ni mbovu na haufai kutokana na kuwa wadanganyifu na hawataki kuwashirikisha wananchi wa ngazi za chini katika maamuzi ya kichama. [179]
wanaendelea
Katika kipindi husika, wanafunzi 120 wamemaliza mafunzo ya Utabiri Daraja la Tatu katika Chuo cha Hali ya Hewa cha Kigoma wakati wengine 43 wanaendelea na masomo. [180]
wanaishi
Sio mtoto huyo tu, wapo watoto wengi katika maeneo hayo ya Makangarawe ambao wanaishi katika mazingira magumu na ambao wanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa jamii. [181]
wangu
Wazazi wangu wameshafariki mimi naishi na dada yangu ambaye anafanya biasahara ndogondogo ya kuuza karanga," anasema Hassan Mohamed mmoja kati ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu huko Makangarawe Wilaya ya Temeke. [182]
wasio
Maamuzi ya zimamoto hayatawasaidia albino KUANZIA miaka ya 1970 jamii yetu imekumbwa na wimbi la mauaji ya watu wasio na hatia kutokana na kile kinachodaiwa imani za kishirikina. [183]
watano
ZAMBIA ikijiandaa na fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(CHAN), imekimbiwa na wachezaji watano tegemeo, huku Mike Baraza wa Kenya akisisitiza kwamba Taifa Stars itafanya maajabu Ivory Coast. [184]
wateja
Mamlaka pia imeanzisha Mkataba wa Huduma kwa Wateja, Clients Service Charter, katika jitihada za kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa na Mamlaka zinafikia viwango kulingana na matarajio ya wateja wake. [185]
watu
Kauli ya Rais Kikwete ni tatizo linaloongeza matatizo, rais lazima asimamie demokrasia na nafasi ya uhuru wa nchi na watu wake, lakini badala yake yupo kinyume," alisema. [186]
wawe
Na sasa si suala la Waislamu tu, wawe Waislamu wenzetu au Waislamu waleee. [187]
wetu
Mchakato huo unagharimu kama Mil 30 ilikufanya zoezi hilo kuanzia awali mpaka kumpata Katibu na Mhazini wa kuajiliwa kama wadhamini wetu walivyotuagiza na kama unavyojua Simba sasa hatuna fedha kabisa ndio maana tumeamua kuomba msaada, alisema Hassanoo. [188]
wiki
Kaaya alisema kiasi cha maji katika mto Ruvu ambao ni chanzo cha maji yanayotumiwa na wakazi zaidi ya milioni tatu wa Dar es Salaam, kinaonyesha dalili mbaya za madhara kutokea, iwapo mvua hazitanyesha katika kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa. [189]
yanaweza
Maneno kupiga fyongo yanaweza kumbabaisha msomaji. [190]
yao
Profesa Lipumba alisema kauli hiyo imemsikitisha kwa kuwa inaonyesha nia ya Kikwete na chama chake kuwanyima wananchi uhuru na haki yao ya kuchagua kile wanachopenda kwa manufaa yao na nchi yao. [191]
yetu
Wakati tunasajili tuliangalia mbele zaidi na sasa tunajipanga vizuri ilituakikishe tukikosa kutetea nafasi yetu basi tunabaki kwenye ligi ili mwakani tuweze kufanya maajabu kwani tutakuwa tumeshaiandaa timu nzuri kwa muda mrefu, alisema Chambusho. [192]
yeye
Kwa Pinda hii ilikuwa ziara yake ya kwanza Kisiwani Pemba tokea ateuliwe kuwa Waziri Mkuu lakini pia yeye ni waziri mkuu wa pili kulala katika kisiwa hicho ukiacha aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo Dk Salim Ahmed Salim (kwao) ambaye aliwahi kutembelea maeneo mbalimbali na kulala. [193]
yote
Tumeshapewa tahadhari kwamba tunaweza kukosa fedha tulizoahidiwa za miradi yote ambayo tulikuwa hatujaingia mikataba" alisema Mariki. [194]
yoyote
Alisema wanafunzi hao hawana haki kuandamana, kukusanyika wala kufanya mikutano yoyote kisheria kwa kuwa si taasisi. [195]
za
Lipumba alidai kuwa chama chake kilishinda katika chaguzi za mwaka 1995, 2000 (ambao ulirudiwa katika baadhi ya majimbo) na 2005, lakini iliibiwa kura zake na kwamba kauli ya Kikwete inaonyesha mapema nia mbaya kwa Zanzibar, jambo ambalo Lipumba alisema ni hatari. [196]
zetu
Tutahakikisha timu zetu zinashiriki vizuri katika michezo hii ya ngazi za klabu na tutakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha wanafanya vizuri kwa maendeleo ya mpira hapa nchini,"Alisema Kaijage. [197]
zile
Tumeshangazwa na baadhi ya taarifa hasa kuhusu fedha zilizopatikana kutokana na zile zilizorudishwa na watuhumiwa wa EPA, ambazo zilikusudiwa kuwasaidia wakulima kuchelewa kuwafikia wahusika na hivyo kufanya nia njema ya Rais Kikwete kukumbwa na upinzani usiotarajiwa. [198]
zipo
SAUTI za huzuni kama hizi zipo nyingi ili hazipapata fursa ya kusikika. [199]
zote
Wahadhiri hao walisema kuwa wanasikitishwa kuona uongozi wa UDSM kushindwa kuwarejesha wanafunzi wote na kwamba walio wengi wanaonekana kutokuwa na uwezo wa kulipia gharama zote za masomo. [200]