Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-20

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


afanye
Huenda unadhani hafanyi vile unataka afanye na hujamuambia au hujui unataka afanye nini. [1]
aheri
Lakini aheri hata siasa. [2]
aina
Mfano, Kanda ya Magharibi ina upungufu wa wakaguzi 28 kati ya 54 wanaotakiwa, Kanda ya Magharibi inapungukiwa 15 na nyinginezo pia zina upungufu wa aina hiyo. [3]
ajira
Waziri Kapuya alisema kuwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2008 jumla ya ajira mpya 1,271,923 tayari zimepatikana kutoka sekta mbalimbali. [4]
akiwa
Dk Ngasongwa alisema: "Ukimshtaki mtu kwa maamuzi aliyoyafanya akiwa madarakani, ukweli inatia mashaka. [5]
ama
Wanadai kuwa mfumo unaotumiwa kuchambua uwezo wa kiuchumi wa mwanafunzi na familia yake (means testing), unawabagua na hivyo kutaka sera hiyo isitishwe ama wanafunzi wote wapewe mkopo kamili ili wamudu kusoma bila ya matatizo. [6]
amani
SERIKALI itapeleka askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika eneo Darfur, kujiunga na vikosi vingine vya askari wa Umoja wa Mataifa (UN), kulinda amani katika eneo hilo. [7]
ana
Na juzi, Obama, ambaye ana mvuto wa kipekee kwa watu mbalimbali, alishiriki kwenye shughuli za kijamii jijini Washington kumuenzi Mchungaji Luther King, ambaye aliuawa mwaka 1968, wakati jana ilikuwa siku ya kitaifa ya kumkumbuka King, ambaye alipigania usawa wa rangi zote bila ya kutumia vurugu. [8]
anahitaji
Nadhani anahitaji kupunguza matarajio. [9]
asasi
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema wakati wowote kuanzia sasa kitamburuza mahakamani Mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali ya Cegodeta, Thomas Ngawaiya, kwa kutoa kauli za uongo dhidi ya viongozi wa chama hicho. [10]
au
Aliongeza kuwa, kipo chama cha wahadhiri cha Udasa, lakini mara nyingi maoni ya chama hicho hayapewi uzito wowote na uongozi wa Chuo na badala yake huchukuliwa kama ushauri ambao unaweza kutumika au kutotumika. [11]
bado
Wakulima wawili waliotajwa kuuawa kwa kuchinjwa na kuchomwa mikuki yenye sumu katika mgogoro huo ni pamoja na Magome Said(35) na Mfundo Malekela (37) na wengine wawili ambao ni wafugaji wa jamii ya kimasai bado hawajafahamika majina yao. [12]
baina
MAPIGANO makali yamezuka baina ya wafugaji wa asili ya kimasai na wakulima wa Vijiji vya Kata ya Pagwi Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga na kusababisha watu wanne kuuawa na nyumba zaidi ya 45 kuchomwa moto. [13]
bali
Masharti waliyowekewa wanafunzi ya kuingia chuoni hapo hayakuwa kero kwao tu, bali wakazi wa maeneo jirani kama Changanyikeni na Makongo na wanajamii wa chuo hicho ambao walilazimika kutumia vitambulisho maalum kuweza kuingia ndani ya uzio. [14]
bodi
Mwananchi ilishuhudia wanafunzi wakilalamikia fomu za kujiunga upya na chuo hicho na kudai kwamba wanatakiwa kulipia gharama ambazo zilikuwa zinalipwa na bodi ya mikopo, miongoni mwa gharama hizo ni pamoja na hela ya mitihani, matibabu na udahili. [15]
bomu
Nao Ellen Manyangu na Winfrida Mtoi wanaripoti kuwa, baadhi ya wahadhiri wa Udsm wamelaani kitendo cha uongozi wa chuo kufunga baadhi ya njia na kusema kitendo hicho ni kutengeneza bomu ambalo hawajui litalipukia upande gani. [16]
bwana
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na bwana mmoja aitwaye John Gottman unasema: namna vile watu wanavyogombana unaweza kujua ni kiasi gani watu wanapendana halikadhalika utaweza kujua ni maamuzi yatokanayo. [17]
chake
Mkurugenzi huyo alisema chama chake kinathamini mchango wa asasi zisizo za serikali katika ujenzi wa taifa kama Haki Elimu, lakini kinashangazwa na Cegodeta ambayo inapambana na wanaharakati wa upinzani na kutetea ufisadi na mafisadi. [18]
chongo
Kweli ushabiki ni chongo. [19]
dhana
Epuka dhana na kusikiliza maneno ya watu. [20]
duni
Mama huyo ambaye ni mbunifu wa mitindo aliyedumu katika fani hiyo kwa muda mrefu zaidi, anasema elimu duni na kutoelewa umuhimu wa mitindo nchini ndiyo tatizo kubwa, kwani jamii ya kitanzania haina uelewa kabisa. [21]
es
JESHI la Polisi jana lililazimika kuvunja maandamano ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yaliyokuwa yameandaliwa na serikali ya wanafunzi iliyoripotiwa kuvunjwa, lakini zoezi la udahili likafanyika huku likisababisha adha kubwa kwa wasafiri na wakazi wa maeneo yanayopakana na chuo hicho. [22]
eti
Hata wale waliotishia kuwashitaki viongozi wa CHADEMA eti kwa kuwadhalilisha sasa wamebaki vichwa chini. [23]
faida
Kabla sijaeleza sababu ambazo naona zinasababisha kushuka kwa e-government nchini, labda nitaje faida za mpango huu. [24]
fani
Asia Idarous ambaye ni mkongwe katika fani ya ubunifu wa mitindo hapa nchini, anasema hiyo fani inayoweza kutumika kama shughuli ya kujikwamua kiuchumi, ikiwa muhusika atakuwa makini katika kufanya kazi zake. [25]
fimbo
Diwani wa Kata hiyo Pagwi Mapombe Tutilo alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa mgogoro huo,ulianza rasmi Januari 15 mwaka huu baada ya mkulima mmoja aliyetambulika kwa jina la Dotto akiwa maeneo ya shambani kwake kumuadhibu kwa kumpiga fimbo mtoto wa Kimasai aliyekuwa akichunga mifugo jirani na shamba lake wakati mtoto huyo akijaribu kuindoa mifugo huyo ili isiharibu mazao kwenye shamba hilo. [26]
hadi
Nchini Japan, mwezi huu maduka mengi ya vitabu yameweka sehemu maalumu kwa ajili ya siku ya kuapishwa kwa Obama, mkusanyiko wa hotuba zake, kuanzia hotuba inayoelezewa kuwa ya "kigwiji" ya mwaka 2004 aliyoitoa kwenye mkutano mkuu wa Democtrats hadi hotuba aliyoitoa baada ya kushinda uchaguzi mwezi Novemba. [27]
haja
Anaongeza kwamba, ipo haja ya kutoa elimu kwa walengwa wabunifu ili waweze kufanya kazi zao vizuri na kwa tija zaidi na hatimaye kuwasaidia kujikwamua kiuchumi kama wanavyofanya jirani zetu wa Kenya na Uganda. [28]
hakina
Baada ya pingamizi kukubalika na Sambwe Shitambala kuenguliwa, sasa CUF na CCM wamebaki ulingoni huku kukiwa na msindikizaji SAU, chama ambacho hakina ushawishi wa kutosha kwa wananchi. [29]
hakuna
Hata ukizunguka duniani kote hakuna helkopta inayouzwa kwa kiasi hicho kwani zingekuwepo watu wengi wangeweza kumiliki," alisema. [30]
hao
Wazee hao ambao wamekaa katika vikao mara tatu kumjadili, walikuwa wakijadili juu ya Mbunge huyo wa Monduli kupewa cheo kikubwa `ukuu wa malaigwanani``cheo ambacho walidai kuwa hakipo na kwamba hata walipompa cheo hicho walikiuka miiko ya kimila. [31]
hapa
Hakuna mzaha hapa," alisema Karunguyeye. [32]
hapo
Mara baada ya kuzuiwa kufanya maandamano chuoni hapo, uongozi wa Daruso ulienda katika baa moja iliyo jirani na mlango wa kuingilia chuoni hapo na kuzungumza na waandishi wa habari. [33]
haraka
DC na RPC hakikisheni wote wanarejea makwao haraka sana ”,alisema Abdulaziz. [34]
hasa
Mgosi alisema mzunguko huu wamepanga kufanya maajabu kwani wamejipanga vizuri na lengo lao ni kulipiza kisasi hasa kwa mahasimu wao wakubwa Yanga ambao katika mzunguko wa kwanza walionekana kucheza kwa kasi sana. [35]
hauna
Ufundishaji bila ukaguzi hauna tija kwani ni rahisi walimu kufundisha bila kufuata mitaala ya elimu iliyowekwa na serikali. [36]
hawa
Hakuna ukweli wa hilo, sisi tunachokijua ni kwamba hawa ni wachezaji wetu wanashughulikia tiketi zao na tunao kwenye timu yetu, sasa kama watatoroka uwezekano wao wa kucheza soka ni mdogo kama yaliyowakuta akina Kabanda (Laurent) na Mwaipopo (Credo),” alisema Kisasa. [37]
hawezi
Fyatu mwenzio wa Marekani, Michael Moore, alisema kwamba baada ya kuambiwa uongo mwingi kuhusu silaha za maangamizi na kadhalika, hawezi kuamini neno lolote linalotolewa na serikali yake. [38]
hayo
Hata hivyo, Jeshi la Polisi lilivunja maandamano hayo na kuwakamata wanafunzi wanne, ambao ilisemekana kwamba walikuwa wakiongoza maandamano hayo. [39]
hewa
Alieleza kuwa upandaji miti ni muhimu kwa vile inaweza kutumika kama njia nzuri ya kudhibiti mabadiliko ya tabianchi na hewa chafu ambavyo kwa pamoja huchangia uchafuzi wa mazingira hasa upande wa ongezeko la joto duniani na uharibifu wa tabaka la Ozoni. [40]
hili
Ngasongwa alitoa kauli hiyo alipozungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake jijini Dar es Salam jana. [41]
hilo
KWA Wamarekani wengi, kutawazwa kwa Rais Mteule, Barack Obama kuwa rais wa kwanza mweusi kuliongoza taifa hilo kubwa duniani, ni matumaini mapya kwao; dunia nzima inaamini hivyo. [42]
hizi
Akizungumza na waandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama hicho, Erasto Tumbo, alisema Ngawaiya kupitia asasi yake alidai kuwa Mbunge wa Moshi Mjini, Phillimoni Ndesamburo, amechota kiasi cha Sh milioni 100 za Chadema na helikopta yake binafsi. [43]
hizo
Kitabu cha hotuba hizo kimekuwa na mauzo makubwa. [44]
hofu
WAZIRI wa zamani wa Mipango, Uchumi na Uwekezaji katika utawala wa awamu ya tatu, Dk Juma Ngasongwa amesema hatua ya serikali kuwafikisha mahakamani viongozi waandamizi wa serikali, wakiwemo mawaziri kwa makosa waliyofanya wakiwa madarakani, inatia hofu. [45]
hujuma
Kwa kutumia mwanya huo huo wa serikali kulala kusimamia mambo mengi muhimu, watumishi wengi wa umma wamejipata madaraka ya kufanya mambo ambayo kwa uhakika ni hujuma dhidi ya serikali yao. [46]
huku
Hotuba ya kwanza kuandikwa ilikuwa tayari Desemba na kazi iliendelea katika wiki zilizofuata, huku Obama akiandika sana na kuhariri mwenyewe. [47]
humo
Membe alisema Kamati hiyo ya bunge imeridhia hatua ya kupeleka askari Darfur na kufafanua kuwa bataliani moja itapelekwa kuungana na askari wengine 17,000 waliopo mjini humo. [48]
huo
Aidha, kwa upande mwingine wahadhiri hao walisema wanashangazwa na kauli ya uongozi huo wa Chuo kuwataka kuanza kufundisha mara tu wanafunzi watakapofungua chuo licha ya wanafunzi wengi kutoripoti kwa siku hiyo. [49]
huu
Anakupa hisia kuwa yeye ni nani, anaonaje wakati huu na wapi anadhani tunahitaji kwenda. [50]
huwa
Tunalipia fedha za mitihani Sh12,000, kulipia matibabu Sh50,000 na udahili tunalipia Sh5,000, hela ambazo huwa zinalipwa kupitia bodi," alisema mwanafunzi Mary Lucas. [51]
huyu
Kitendo cha huyu mganga kuwachanja chale na kuwapa imani kuwa hahwezi kudhulika kimesababisha wakulima wa kabila la wakaguru kupata nguvu ya kupambana na wamasaia lakini hofu yetu ni kwamba wamasai wanatumia silaha kali yasije kutokea mauaji mengi zaidi,"alisema Dumba. [52]
ikawa
Na inawezekana ikawa hujui nini kamwambia mumeo kuhusu wewe. [53]
ikiwa
Simba ambayo kesho inakutana na Villa Squad ikiwa ni mchezo wa pili tangu mzunguko wa pili uanze. [54]
iko
Wananchi naomba mtulie na mpeleke taarifa kwa wenzenu walioko msituni waambie warudi, hali iko shwari, serikali inafanyia kazi mgogoro huo na hivi karibuni tutafanya mkutano wa usuluhishi"alisema Abdulaziz. [55]
ila
Inashangaza sana kwa uongozi wa chuo unaosimamiwa na wataalamu wa utawala na siasa na wapigania demokrasia nchini, kufanya maamuzi yanayowanyima wanafunzi wengi haki ya kusoma hata ambao hawakuhusika kuandaa mgomo au vurugu, ila tu kwa sababu ya umaskini wao. [56]
ilivyo
Hakuna mabasi ya usafiri (daladala) yaliyoruhusiwa kuingia eneo la chuo kama ilivyo kawaida yao ya kubeba abiria kutoka Mwenge kwenda Ubungo kupitia Chuo Kikuu na mengine kuelekea Changanyikeni. [57]
imeshuka
UTAFITI uliofanywa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa (UN) kuhusiana na masuala ya e-government na ripoti yake kutolewa mwaka jana, Tanzania imeshuka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mwaka 2005, ripoti hiyo ilipotolewa mara ya mwisho. [58]
in
Nilianzisha rasmi utaratibu wa kuonyesha mitindo ya mavazi mwaka 1986. Mara ya kwanza zaidi ya wanamitindo kumi walipanda jukwaani kunadi mavazi yangu,” anafahamisha na kuongeza kuwa hadi kufikia wakati huu, ameishafanya maonyesho 71 na kwamba, February 6,2009 anatarajia kufanya onyesho la 72 litakalofahamika kama Lady in red, likiwa maalum kwa sikukuu ya wapendanao (Valentines day). [59]
ina
Licha ya serikali kusema kuwa ina wakaguzi wa kutosha kwa shule za Msingi, sekondari ya vyuo vya elimu, utafiti uliofanywa hivi karibu na gazeti hili sehemu mbalimbali nchini umebaini kwamba, karibu kanda zote zinakabiliwa na upungufu wa wakaguzi. [60]
internet
Kuna baadhi ya wasomaji wataanza kujiuliza e-government ni nini? Hizi ni huduma ambazo zinatolewa na serikali kwa wananchi wake kwa njia ya kompyuta ambayo imeunganishwa katika mtandao wa internet. [61]
ipasavyo
Vile vile sababu nyingine ambayo inasababisha teknolojia hii muhimu kutotumika ipasavyo ni pamoja na kukosekana kwa sera na mipango madhubuti ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama), katika taasisi za serikali. [62]
ipo
Sasa ukikuta timu ambazo saikolojia yao ipo katika hali nzuri hutumia nafasi hiyo kujipanga na hatimaye kupata ushindi kirahisi"anasema Maximo. [63]
je
Haya, na hapa je? Mimi sikatai ni dhahiri kwamba wanene wa mafuta walitaka kutunyonya mwisho. [64]
jua
Anaongoza kundi kubwa na ana mashabiki wenye msimamo mkali ambao wanadhani jua litashuka Januari 20 na dunia itakuwa tofauti kabisa," alisema Anthon. [65]
jumla
Vita ya ufisadi hadi sasa imechukua sura tatu kuu; watu wanaotuhumiwa kuiba jumla ya Sh133 bilioni katika Akaunti ya Malipo ya Malimbikizo ya Madeni ya Nje (EPA), mawaziri wanaotuhumiwa kutumia vibaya ofisi zao na kutumia uongo ili kupata tenda ya serikali ya ufuaji umeme wa dharura. [66]
kamati
Alibainisha kuwa wizara yake imewasilisha kwa kamati hiyo taarifa ya mafanikio katika utendaji wake na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)na kuanisha maeneo mbalimbali aliyoyaita ya ushindi. [67]
kampuni
Mwenyekiti wa kamati ya ushindi ya klabu ya Simba, Hassan Othman Hassanoo alisema tayari wametuma barua kwa wadhamini wao kampuni ya Bia Tanzania, TBL, ili wawasaidie katika mchakato wa uendeshaji wa zoezi hilo ambalo alisema linagharimu fedha nyingi. [68]
kanuni
Hotuba ya siku ya kuapishwa ni hotuba inayoanza kwa kanuni za kwanza na kuweka mwelekeo wa nchi," alisema mwandishi wa hotuba wa zamani wa Rais Bill Clinton, Jeff Shesol. [69]
kasi
Waziri Kapuya alifafanua kuwa kasi ya utatuzi wa migogoro imeongezeka kutoka wastani wa kipindi cha miaka mitatu hadi mitano na kuwa siku 21 hadi 30 tangu kupokewa kwa migogoro. [70]
kati
Mimi nina darasa la wanafunzi 200 na walioruhusiwa ni 45 kati ya hao walioripoti kwa siku ya leo ni watano unategemea niwafundishe hao kisha nifanyeje juu wengine watakaoripoti baada ya hapo? Huku ni kuwekana katika wakati mgumu,” alisema mhadhiri huyo. [71]
kiasi
Hatakiwi kuanza na hotuba ya kumponda Bush kupita kiasi," alisema Schwartz. [72]
kidogo
Inatakiwa kuwa makini kidogo katika kulitazama suala hilo. [73]
kifuani
Mshtakiwa huyo ambaye ni mmoja kati ya raia wawili wa Kenya wanaotuhumiwa kupambana na Polisi Jijini Arusha kwa saa sita, aliiambia mahakama kuwa, hiyo jana alifanyiwa upekuzi mkali kwa kuvuliwa nguo zote na kupigwa kichwani na kifuani. [74]
kila
CAF ilisema kuwa timu mbili kutoka kila kundi ndizo zitakazocheza nusu fainali. [75]
kile
Hata hivyo CHADEMA wamekataa ombi hilo kwa kile walichosema kuwa, ushirikianao wa vyama hivyo ulishakufa tangu wakati wa uchaguzi wa Tarime. [76]
kisiasa
Alisema Ngawaiya anafanya hivyo kwa malengo yake ya kisiasa katika kukisafisha Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kupambana na viongozi makini wa upinzani. [77]
kitakuwa
Naye mkurugenzi wa msanii huyo, Hartmann Mbilinyi anasema Steve anatarajia kutengenezewa kipindi ambacho kitakuwa ni fungakazi kwa sanaa ya vichekesho ambayo inaonekana kupata umaarufu mkubwa hapa nchini. [78]
kitendo
Boma` na kitendo cha Lowassa kupewa cheo cha ukuu wa `Malaigwanani ` kimewashangaza wazee hao. [79]
kote
Naye katibu wa mtandao wa wanafunzi nchini, TSNP, Owawa Steven alisema wakishapangilia namna ya kuandamana nchini kote, watawafahamisha wanafunzi wote ili wajumuike katika kudai haki zao. [80]
kuambiwa
Ugomvi mwingi wa wanawake wengi unatokana na maneno ya kuambiwa ama kudhania. [81]
kuandaa
Muda na jitihada kubwa zimetumika katika kuandaa hotuba ya Obama. [82]
kuandika
Hata hivyo Hakimu Kente alisema kwa kuwa washtakiwa hao hawawataji kwa majina askari hao wa Magereza, mahakama hiyo isingeweza kutoa onyo kwa askari wote hata wasiohusika, bali itakachokifanya ni kuandika barua ikimwelekeza Mkuu wa Magereza kuhakikisha mshtakiwa huyo wa kwanza anapatiwa matibabu. [83]
kuchokwa
Afadhali hata mpira maana hatimaye mashabiki wataanza kudai mabadiliko lakini katika siasa, watu watashabikia weeeeeeeeeeeee huku chama fulani kimeshapondwa badala ya kupendwa, kimechekwa na kuchokwa na hata kuchukiwa kutokana na kuchakaa kwake. [84]
kugombea
Lakini ulipofika uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime mwaka jana kila chama kikajitosa kugombea licha ya kwamba CHADEMA ilikuwa na nafasi kubwa zaidi ya kushinda. [85]
kuiunga
Katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiteto, CUF ilikubali kuiunga mkono CHADEMA ambayo hata hivyo haikushinda. [86]
kuja
Inadaiwa kuwa Dotto ana kawaida kwa makusudi ya kulazimisha mifugo ya watu iingine shambani mwake kwa lengo la kuja kudai alipwe fidia ya fedha kwa madai ya kuharibiwa mazao yake. [87]
kujua
Na kwa sababu ya kukosa ubunifu, vyama hivi vya upinzani vinajikuta vikifanya kazi ya CCM. Yaani vinatumiwa kwa kujua au kwa kutokujua na CCM ili kuangamiza upinzani nchini. [88]
kukuza
UTARATIBU mpya wa kuwarejesha wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliokuwa wamesimamishwa kutokana na mgogoro uliosababishwa na sera ya uchangiaji elimu, haulisaidii taifa kufikia lengo lake la kukuza elimu na kupata wataalamu wa kutosha. [89]
kule
KOCHA Marcio Maximo anasema sasa anaelekeza nguvu zake katika kuiandaa vema Timu ya Taifa, Taifa Stars ili iweze kukabiliana na mikiki mikiki ya Michuano ya Mataifa ya Afrika inayotarajia kupingwa kule Ivory Coast Februari. [90]
kumsikiliza
Ongeza umakini katika kumsikiliza. [91]
kuona
Baada ya kipindi kirefu cha maandalizi ya kuingia na kutoka Ikulu, hatimaye siku imewadia kwa Wamarekani kuona ndoto iliyotangazwa miaka mingi iliyopita na mpigania haki maarufu, Dk Martin Luther King, ikitimia kwa mtu mweusi kuongoza taifa hilo. [92]
kupiga
Wanasiasa wasio na ubunifu wala mwelekeo, kazi ni kupiga siasa za mezani tu. [93]
kushona
Amefahamisha kuwa amekuwa akichora kila anachobuni na kisha kushona mavazi yanayowezatumika katika shughuli mbalimbali. [94]
kutoa
Michael Anton, ambaye alikuwa mwandishi wa hotuba wa Rais George W Bush, alisema Obama atahitaji kuepuka kutoa ahadi nyingi. [95]
kuu
Wakati huo huo, wakazi wa Changanyikeni wamelaani kitendo cha kufungiwa njia na kusema kuwa, huo ni ukiukwaji wa haki za binadamu, kwa kuwa njia hiyo ndiyo njia kuu waliyokuwa wakitumia hata kabla ya chuo hicho kuwepo. [96]
kuvuruga
Baadaye viatu hivi vitatolewa kwa watoto yatima ili na wao waweze kumkumbuka aliyefanikiwa sana kuvuruga amani ya dunia, uchumi wa dunia na mazingira ya dunia, baada ya kuvuruga demokrasia ya dunia ndani ya nchi yake mwenyewe wakati wa ‘kuchaguliwa’ mara ya kwanza. [97]
kuwaua
Alisema jambo linalozidi kuwatia hofu ni kutokana na kwamba Wakulima hao kuwa na imani potufu baada ya kuchanjwa na mganga wa jadi aliyetoka kijiji cha Idibo wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro na kufahamika kwa jina la Kilongola Jenga kuwaahidi Wakaguru hao kuingia msituni bila hofu kwani hakuna silaha yoyote ya moto itakayoweza kuwaua. [98]
kuzidi
Lakini mara nyingi kunyamaza ni kuzidi kuzidisha matatizo. [99]
kweli
Kama mtu kweli alifanya ufisadi, basi hilo sawa. [100]
la
ALIYEWAHI kuwa waziri mkuu Edward Lowassa huenda akavuliwa cheo cha ukuu wa kimila (Olaigwanani) na ukuu wa `malaigwanani baada ya jopo la wazee wa kimila kukaa vikao na kupanga siku ya kumuita na kumvua cheo hicho kikubwa kwa mila za kimaasai. [101]
lango
Wanafunzi walitakiwa kufanyiwa udahili kwenye lango la chuo linalotazamana na Chuo cha Maji cha Rwegalulila, lakini nje ya lango hilo ndiko baadhi ya wanafunzi waliona sehemu nzuri ya kuanzia maandamano yao. [102]
leo
Obama anaapishwa rasmi leo kuwa rais wa Marekani baada ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana, ushindi ambao ulipokewa kwa shangwe karibu dunia nzima, yakiwemo mataifa ya Kiarabu ambayo yana upinzani mkubwa na Marekani. [103]
lolote
Habari zilisema kuwa baada ya uongozi wa Yanga kuelezwa kuwa KFF imeshatoa tiketi kwa wachezaji hao, waliomba kupewa namba za tiketi ili wajaribu kufuatilia endapo kutakuwa na tatizo lolote lililosababisha wachezaji hao kukwama jijini Nairobi lakini bado hawajazipata. [104]
maana
Akizungumzia mchezo huo, kocha wa Simba, Patrick Phiri alisema kuwa, wachezaji wake wamecheza kitimu na ndiyo maana wakaibuka washindi. [105]
mabao
MABAO mawili yaliyofungwa na Said Dilunga katika kipindi cha pili yameiwezesha Toto African kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Moro United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. [106]
mabeki
Ni matokeo inabidi tuyakubali kwani ni sehemu ya mchezo lakini mabeki ndio wamesababisha yote haya hawakuwa makini kabisa, walipoteana. [107]
mabomba
Hata hivyo alisema tatizo hilo bado litayasumbua baadhi ya maeneo kutokana na uharibifu miundombinu ya Dawasco unaotokana na wizi na ukataji wa mabomba ya maji. [108]
madeni
Kwa mfano, kitendo cha uongozi wa vyuo vikuu kutangaza utaratibu mpya wa kuwarejesha wanafunzi waliofukuzwa mapema mwaka jana kwa sababu za mgomo vyuoni wakiwataka wajaze fomu za kujiandikisha upya pamoja na kulipa madeni yote wanayodaiwa chuoni hapo, ni hujuma dhidi ya maendeleo ya elimu nchini. [109]
madogo
Hata wamiliki wa magari madogo walilazimika kusimama langoni kukaguliwa na kuonyesha vitambulisho kabla ya kuingia. [110]
maelekezo
Kocha wa Toto African, Mbwana Makata alisema kuwa wachezaji wake walitulia na kupata ushindi baada ya maelekezo. [111]
mafuta
Kivipi? Kama unavyojua kusema maneno yanayoudhi ni kama kumtupia kijinga cha moto mtu ambaye tayari ameshaoga mafuta ya taa. [112]
majina
Alisema Jeshi la Polisi limewakamata wanafunzi wanne ambao walikuwa vinara wa maandamo hayo jana; na kuwataja majina kuwa ni pamoja na Bahati Arone, Issa Paul, Titus Ndula na Sabinian Priuspius. [113]
mapema
Alisema uamuzi huo umeridhiwa pia na Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na kwamba askari hao wanatarajiwa kuondoka nchini mapema mwezi Machi. [114]
mbali
Hata hivyo, mbali na kuwasiliana na wachezaji hao, Kisasa alisema kuwa kuna taarifa za vyombo vya habari kuwa wachezaji hao wametimkia Misri kucheza soka ya kulipwa. [115]
mbaya
Akizungumzia suala la ajira mbaya kwa watoto, Waziri Kapuya alisema kuwa wizara yake inatekeleza mpango wa kutokomeza tatizo hilo katika wilaya 16 za Tanzania Bara na wilaya mbili za Tanzania Visiwani. [116]
mbele
Hotuba ya Obama itampa nafasi nzuri ya kufanikisha malengo yake atakapokuwa Ikulu wakati atakapohutubia mbele ya maelfu ya watu. [117]
mbinu
Wapinzani mnapaswa mwende kwa wananchi na kubuni mbinu ambazo zitawavutia wananchi ili kujiunga. [118]
michuano
Wachezaji hao walikuwa Kampala, Uganda wakiitumikia timu yao iliyokuwa ikishiriki michuano ya Chalenji. [119]
mipya
Anasema awali alikuwa anabuni mitindo ya mavazi kwa ajili ya watu binafsi na baadaye alianzisha maonyesho ya mavazi kwa lengo la kuonyesha mitindo mipya aliyobuni. [120]
misitu
Maadhimisho ya siku hiyo yaliyoanza kuadhimishwa mwaka 2001 yamekuja huku kukiwa na taarifa kuwa sekta ya misitu imekuwa ikikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo upoteaji wa miti. [121]
miti
JANUARI Mosi mwaka huu ilikuwa ni siku ya taifa ya kupanda miti. [122]
mitindo
FANI ya mitindo imekuwa ikichukuliwa kama burudani, hasa pale wabunifu wanaponadi kazi zao, kitendo ambacho kimekuwa kikichangia kupotosha maana yake halisi. [123]
mrefu
Kwa muda mrefu kumekuwa na hoja ya kuviunganisha vyama hivyo ili kuwa na nguvu ya pamoja ya kukishinda chama tawala CCM. Lakini hoja hii imeshindikana hasa kwa kuwa wapinzani wenyewe hawafanani kimalengo. [124]
muda
Viongozi hao walisema kuwa, pamoja na kuzuiwa kwa maandamano hayo, wanapanga mikakati mingine ya maandamano yatakayofanyika muda wowote kuanzia leo. [125]
muhimu
Walisema wanashangazwa na uongozi wa chuo kufanya maamuzi bila ya kuwashirikisha wakiwa ni wafanyakazi wa sehemu hiyo muhimu kielimu. [126]
mumeo
Kubeba ulichoambiwa ukakitumia kama fimbo ya kumhukumu mumeo ni makosa makubwa. [127]
mweka
Wiki iliyopita Makamu mwenyekiti wa Simba, Omary Gumbo aliwaambia waandishi wa habari kuwa klabu hiyo imekamilisha mchakato wa kumsaka katibu mkuu na mweka hazina wa kuajiriwa na na kudai kuwa tayari majina yao yameshakabidhiwa kwa TBL kwa ajili ya utekelezaji. [128]
namba
Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo wanaotetewa kwa pamoja na Mwale, Ruwaichi na Robert Rogathe kutoka Jijini Arusha ni Michael Kimani au Mike ambaye pamoja na mshtakiwa namba moja wanadaiwa kupambana na Polisi Jijini Arusha kwa saa sita. [129]
nao
Tumekuwa tukiwasiliana nao mara kwa mara, mara ya mwisho nilipoongea na Baraza aliniambia wanaisubiri KFF iwapatie tiketi ili waje," alisema Madega. [130]
naye
Mshambuliaji wa Polisi, Nicolaus Kapipe alikosa bao la wazi katika dakika ya 28 na Mokil Lambo naye akipaisha mpira akiwa karibu na lango. [131]
nayo
Mwenyewe anasema "Sijui ilikuwaje lakini ninachojua mimi ninamudu sauti hiyo, ninaiweza na ndiyo nilianza nayo kwenye sanaa hii-ndio maana najivunia kuitwa Steve Nyerere. [132]
ndio
Akizungumza baada ya kupewa taarifa hizo, Abdulaziz alimwagiza Mkuu wa wilaya Dumba pamoja na Kamanda Sirro kuhakikisha wavamizi wote walitoka mikoa ya jirani wanarudi kwenye maeneo yao kwa madai ndio kichocheo kikubwa cha mapigano hayo. [133]
ndiyo
Obama, ambaye ni shabiki mkubwa wa Lincoln ambaye pia alikuwa anatokea jimbo la Illinois, aliiambia USA Today kuwa, anadhani hotuba ya Lincoln ndiyo bora ikifuatiwa na ya Kennedy. [134]
ngazi
WAKATI serikali inaendelea kuhubiri juu ya kuboresha elimu nchini, juhudi zake zinaonekana kutozaa matunda kutokana na kiwango cha ufaulu wa watahiniwa katika ngazi mbalimbali kuendelea kushuka. [135]
ni
Pia wazee hao katika mukhtasari wa kikao chao walisema kuwa katika mchakato mzima wa kumpatia Lowasa ukubwa wa wazee wa ukoo ni batili na kwamba mwezi Februari mwaka 2009 wataandaa mkutano mkubwa wa kimila akiwamo Mbunge huyo na kuangalia taratibu za kumvua cheo hicho na kwamba ikibainika ni Lowassa anapaswa kupewa cheo hicho atapewa. [136]
nusu
Katika hatua nyingine, CAF imeanzisha mfumo wa kucheza nusu Fainali kwa michuano ya Shirikisho kama ilivyo kwa mechi za Ligi ya Mabingwa. [137]
nyuma
Washindi ambao walikuwa nyuma kwa bao 1-0, walianza kuhesabu bao katika dakika ya 76 baada ya kipa wa Moro United, Saleh Tendega kulitema shuti la Oscar Fanuel na Said Dilunga akauwahi na kuukwamisha mpira wavuni. [138]
onyo
Wakili Median Mwale anayewatetea baadhi ya washtakiwa katika kesi hiyo wakiwemo raia hao wa Kenya aliiambia mahakama kuwa wateja wake wamemwarifu juu ya kuwepo kikosi hicho maalumu kinachofanya mambo yote hayo ya unyanyasaji na kuiomba mahakama itoe onyo kwa Mkuu wa Gereza la Karanga kwa niaba ya askari hao. [139]
pa
Mapigano hayo yanayotokana na mgogoro wa ardhi wa baina ya wafugaji hao na wakulima wengi wao wakiwa wa kabila la Wakaguru yamedumu kwa siku tatu na kuwaacha zaidi ya watu 800 kukosa mahala pa kuishi wala chakula. [140]
pale
Cha kushangaza ni pale viongozi wa CUF, NCCR Mageuzi, TPPP Maendeleo na TLP walipoungana na kuitaka CHADEMA imuunge mkono mgombea wa CUF Daudi Mponzi katika uchaguzi wa Mbeya. [141]
pili
Wachezaji hao walikuwa wakiichezea timu ya taifa ya Kenya 'Harambee Stars' kwenye michuano ya kombe la Chalenji yaliyomalizika nchini Uganda kwa wenyeji kutwaa ubingwa huku Kenya ikishika nafasi ya pili. [142]
poa
Na kwa kuwa Makengeza Enterprises haitaki watu wapekue baadaye na kupata funza badala ya mafunzo, viatu maalum vitauzwa kwa bei poa hapohapo kwenye tamasha. [143]
polisi
Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo hilo, kamanda mkuu wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Mark Karunguyeye, alisema polisi ililazimika kuvunja maandamano ya wanafunzi hao kutokana na kwenda kinyume na sheria. [144]
programu
Hadi awamu ya kwanza ya programu hiyo ilipomalizika mwaka jana, mafanikio yaliyopatikana na kidogo. [145]
rafiki
Ninaye rafiki yangu ambaye alikuwa mpigania uhuru wa Afrika Kusini. [146]
raia
MSHTAKIWA nambari moja katika kesi ya wizi wa Sh239.4 milioni mali ya benki ya NMB Tawi la Mwanga, Samwel Saitoti, jana alitoa tuhuma nzito mahakamani akidai kuna kikosi maalumu cha askari magereza kutoka jijini Dar es Salaam ambacho kimetishia kuwaua watuhumiwa wa kesi hiyo ambao ni raia wa Kenya. [147]
ripoti
Hata hivyo, taarifa na ripoti nyingine zitakazotumwa CAF zitafanywa na chama au shirikisho husika kwa mujibu wa taratibu," ilisema barua hiyo. [148]
saa
Dumba alisema mauaji ya wakulima hao wawili yalitokea juzi alhamisi saa 12.00 asubuhi huko katika kijiji cha Makelele baada ya kundi la wafugaji kuvamia nyumba waliyokuwa wakiishi marehemu kuiwasha moto na kuwakatakata kwa mapanga hadi kufa. [149]
salaam
Stars iliyokuwa ikiitwa Kilimanjaro Stars katika michuano ya Kombe la Chalenji, iliwasili Dar es salaam wiki iliyopita ikiwa imeshika nafasi ya tatu. [150]
sana
Mtaalamu wa mambo ya marais, Thomas Schwartz, profesa kwenye Chuo Kikuu cha Vanderbilt, alisema moja ya changamoto kubwa zinazomkabili Obama ni kupendekeza mwanzo mpya bila ya kuwa tofauti sana na rais anayeondoka, Bush, ambaye atakuwa amekaa pembeni mwake. [151]
sanaa
Anasema yeye binafsi amepania kuboresha sanaa yake na kuipenyeza katika soko la kimataifa. [152]
sasa
Huku mamilioni ya Wamarekani wakiwa hawana kazi, uchumi wa Marekani ukiporomoka na majeshi ya Marekani yakiwa vitani Iraq na Afghanistan, Obama hatakosa cha kuzungumza katika hotuba yake, ambayo amekuwa akiiandaa kwa wiki kadhaa sasa. [153]
sauti
Jina laStive Nyerere limetokana na sanaa yake kwa kuwa alianza usanii kwa kuingiza sauti ya Baba wa Taifa ,Mwalimu Julius Nyerere. [154]
shule
Mpango huo umewezesha watoto wapatao 13,961 kuondolewa katika ajira mbaya na kupewa huduma mbalimbali zikiwemo elimu ya msingi kwa waliokosa (MEMKWA), elimu ya awali, ufundi, msaada wa kisaikolojia na msaada wa vifaa vya shule. [155]
si
Tumeamua kuandamana leo (jana), ili uongozi uone kwamba unachokifanya si halali kwa sababu kumrudisha mwanafunzi mwenye uwezo kuendelea na masomo na kumwacha asiye na uwezo ni sawa na ukandamizaji," alisema mmoja wa wanafunzi waliokuwa wamebeba mabango ya vitambaa kabla ya kuanza maandamano yao. [156]
sifa
Kwa hiyo, kwa sifa ya Tanzania ilivyo, tangu eeeeenzi za mwalimu, tutasimama upande gani? Upande wa wanaonyanyaswa. [157]
sisi
Kama wanataka watumalize kwa kutuua, sisi hatuogopi kwani tunatetea haki za wanyonge," alisema rais wa Daruso, Antony Machibya. [158]
soka
WAKATI viongozi wa Yanga wanalitupia lawama Shirikisho la Soka la Kenya, KFF kwa kuwachelewesha wachezaji wake, Mike Baraza na George Owino imeelezwa kuwa wachezaji hao wametimkia Misri kucheza soka ya kulipwa. [159]
soko
Idarous anapendekeza kuwa vianzishwe vyuo vya ubunifu wa mitindo katika ngazi mbalimbali ili kupata watu wenye ujuzi kamaili ambao wataweza kutengeneza bidhaa zitakazoweza kushindana katika soko la kimataifa. [160]
suala
Wakitoa maoni yao kuhusiana na suala hilo, wakazi hao walisema kitendo cha mtu au uongozi fulani kuamua kufunga njia kwa sababu ya matatizo waliyoyatengeneza bila kujali njia hiyo inayotegemewa na jamii kwa mahitaji mbalimbali ni unyanyasaji wa hali ya juu. [161]
tangu
Watoto hao ni wa mfugaji huyo mwanamke na imeelezwa kuwa pia kuna watoto wengine hawajaonekana tangu kuanza kwa mapigano hayo. [162]
tena
Wametuzuia leo, lakini aluta continua, tunapanga mipango ya kuandamana vyuo vyote vya umma kwa mara nyingine tena. [163]
tete
Mkuu huyo wa wilaya alisema hali bado ni tete licha ya jeshi la polisi mkoa wa Tanga likiongozwa na kamanda wa Polisi mkoani humo Simon Sirro kuweka kambi porini ambako zaidi ya wakulima 800 wamejificha kwa malengo ya kuwasaka wafugaji wa Kimasai ili kulipiza kisasi. [164]
tija
Jambo jingine ni pamoja na kutafsiri Kanuni za Kazi toka lugha ya Kiingereza na kuwa katika lugha ya Kiswahili ili kuongeza uelewa kwa wananchi ambapo ufanisi na tija sehemu za kazi utaongezeka. [165]
transfoma
Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasco), Mary Lyimo, aliliambia gazeti hili jana kuwa maeneo hayo yameanza kupata maji baada ya kukamilika matengenezo ya transfoma iliyoharibika. [166]
tu
Si tu Wamarekani watakaokuwa makini kusikiliza ni nini kiongozi wao mpya anasema. [167]
tuna
Nimeridhishwa na kiwango cha wachezaji wangu licha ya kwamba hatukufanikiwa kutwaa ubingwa kule Uganda hii inanipa imani ya kwamba ikiwa tutajiandaa vya kutosha basi tuna nafasi ya kufanya vizuri kule Ivory Coast," anasema. [168]
ubora
Kwa mfumo wa sasa, ni rahisi mwalimu au walimu kutomaliza mitaala au kufundisha haraka na kumaliza mapema bila kujali ubora wa elimu na hakuna atakayehoji kwa sababu hawakaguliwi. [169]
ufahamu
Anasema Stive ana kipaji ndiyo maana kampuni yake imeamua kufanya naye kazi kwa ukaribu, ili kuweza kufanya mipango yake ya kukuza sanaa yake kimataifa inafanikiwa, na ulimwengu ufahamu kuwa mbali na soka pia Tanzania kunavipaji vingine. [170]
uhuru
Pia aliongeza kuwa chama hakiwezi kupinga mwanachama au kiongozi wake kutumia fedha alizonazo kununua zana ambazo ni muhimu kwa mapambano ya harakati za kudai mabadiliko ya kweli na uhuru wa kweli nchini. [171]
ujao
Alisema maeyaona makosa hayo na atayafanyia kazi kabla ya mchezo ujao na anaamini watabadilika. [172]
uko
Imebidi muda uongezeke kwani idadi ya wanafunzi ni kubwa na kuna wale watakaokata rufaa, pia mlango wa waziri uko wazi kwa wale wasio na uwezo wa kukamilisha malipo yote," alisema. [173]
uliopo
Anaelezea wakati uliopo. [174]
unyama
Enzi zile, daima alinielezea unyama wa makaburu, unyama wa kutisha. [175]
upo
Stive Nyerere nimemuandalia mipango ya mwaka mpya ambayo itakuwa na mafaniko makubwa katika sanaa yake, kwani kutokana na uzoefu wangu katika nchi nyingi za Ulaya nilizotembelea, hivyo naamini kuwa uwezo wa kukamata soko la dunia upo," anasema Mbilinyi. [176]
upungufu
Pamoja na kuwepo changamoto nyingi zinazosababisha tatizo hilo, upungufu wa wakaguzi wa elimu unachangia kwa kiasi kikubwa kiwango cha elimu kuendelea kushuka. [177]
uwanja
Alisema katika kipindi hicho serikali imewezesha kuanzishwa kwa kituo cha michezo, (Sports Complex) ambayo ni uwanja wa kisasa wenye viwango vya olimpiki. [178]
viatu
Kutakuwepo na sanamu kubwa ya Kichaka na wote mtapewa nafasi ya kuitupia viatu kwa nguvu zote. [179]
vichwa
CCM wanakuna vichwa, hawajui jinsi ya kujibu hoja za CHADEMA. Kila kukicha mafisadi waliotajwa wanapelekwa mahakamani. [180]
vile
Naye kocha wa Moro United, Fred Minziro alisema kuwa wachezaji hawakucheza vile alivyowaelekeza. [181]
vizuri
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala alisema hali inaendelea vizuri ya kudahili wanafunzi na akasisitiza kuwa muda wa kudahili unaongezwa. [182]
vya
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma waliamua kugoma kuingia darasani mwishoni mwa mwaka jana wakipinga sera ya uchangiaji elimu. [183]
vyao
Alisema kamati hiyo imeitaka serikali kuwa makini na suala la ardhi ambalo ni rasilimali na urithi pekee wa wananchi wa Tanzania na vizazi vyao na kwamba atalifikisha suala hilo katika vyombo husika. [184]
wake
Waandishi wa hotuba wa marais wa zamani walisema wanategemea Obama ataepuka kuweka mlolongo wa mapendekezo na badala yake atatumia ustadi wake wa kuzungumza kuelezea changamoto zinazowakabili Wamarekani. [185]
wako
Sasa Chadema wameanza Operesheni Sangara, wameshavuruga mikoa ya kanda ya Ziwa na sasa wako jijini Dar es Salaam. [186]
wapo
Mbilinyi anasema kipindi hicho ambacho kitakuwa kinarushwa na kituo kimoja wapo cha televisheni hapa nchini kitakuwa kinaitwa Comed Talk Shoo. [187]
wawe
Na sasa si suala la Waislamu tu, wawe Waislamu wenzetu au Waislamu waleee. [188]
wenyewe
Baadhi ya maeneo yataendelea kukosa maji kutokana na uharibifu mkubwa uliofanywa na wananchi wenyewe kukataji mabomba na wizi wa miundombinu," alisema Lyimo. [189]
wewe
Kama wewe ni mmoja ya wale watu ambao huchagua kunyamaza ama kununa kuliko kutatua tatizo jua wewe ni chanzo cha kuzidi kwa matatizo mbeleni. [190]
yake
Lakini wakati atakapokuwa anaapishwa, Obama anakabiliwa na changamoto kubwa moja; kuwahakikishia Wamarekani kuwa wanaweza kuondokana na matatizo ya kiuchumi yanayowakabili wakati atakapokuwa akitoa hotuba yake, inayosubiriwa kwa hamu. [191]
yangu
Kazi yangu kwenye hotuba ni kukumbusha watu njia tunayopitia na mambo yasiyo ya kawaida ambayo tumeshayapita. [192]
yao
Watu wengine duniani pia watapenda kusikia hotuba hiyo na kuitafsiri kwa mazingira yao. [193]
yenu
Inachokupasa ufahamu kuwa kuziba kauli katika suala ambalo limekuudhi hupelekea madhara makubwa mbeleni katika mahusiano yenu na huenda ikaathirika afya yako. [194]
yote
Wanafunzi hao waliamua kuandaa maandamano kupinga utaratibu wa udahili ulioanza jana wa kuwapokea wanafunzi ambao wamekamilisha malipo yao yote kulingana na makundi waliyopangiwa na Bodi ya Mikopo. [195]
yule
Na ni vyema ukaongea naye ili upate ukweli kwa kusema wasiwasi wako, au kile ulichoambiwa kwa kumkutanisha na yule aliyesema itasaidia kuondoa migogoro yenu. [196]
zenye
Hivyo UN ikaona kuna haja ya kufanya utafiti ili kujua nchi zilizopiga hatua katika matumizi ya kompyuta na internet katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wake na zenye ubora. [197]
zetu
Kazi ya ukarabati imekalika kwa kiasi kikubwa niseme ni asilimia 90 mpaka sasa nafikiri ifikapo Machi tutaanza kulitumia rasmi kwa shughuli zetu za klabu"alisema Madega. [198]
zilizopo
Alifafanua kuwa kwa watendaji wa serikali, inawezekana mtu alifanya maamuzi kwa sababu alilazimika kufanya hivyo kwa sababu zilizopo wakati huo na si kwa kufikiria kufanya ufisadi. [199]
zogo
Basi ikawa zogo, zogo kubwa kabisa hadi aliingia huyu huyu rafiki yangu aliyeonjeshwa mateso huko kwa Makaburu. [200]