Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-19

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


aaah
Yaani niue albino ndio niwe tajiri, aaah hapana sitaki kuwa kwenye orodha ya wauaji, kama ni umaskini acha niwe, hata kama watu watasema nimeporomoka sawa tu,” alijisemea Kazim. [1]
aende
Kuna baadhi na wataalam kule alikokwenda kuhangaika walimshauri labda aende nje ya nchi. [2]
aina
Huwezi kumtoza kodi raia na kisha unamtaka achangie huduma hizo kwa shuruti",alisema Ruhuza na kusisitiza kuwa kodi wanayotozwa wananchi si kwa ajili ya kununulia magari ya kifahari (mashangingi) wala kufanyia starehe za aina yoyote bali ni kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wake. [3]
akawa
Kweli walifanya hivyo, wiki moja baadaye walirudi, Kazim akawa amekubali kwamba angependa kufanya biashara zote mbili yaani ya uvuvi na uchimbaji madini. [4]
akiwa
Mshambuliaji wa Polisi, Nicolaus Kapipe alikosa bao la wazi katika dakika ya 28 na Mokil Lambo naye akipaisha mpira akiwa karibu na lango. [5]
alifoka
Sasa huo si ujinga, picha ndio nini? Picha ndio dawa,” alifoka Kazim hali iliyomfanya waziri aendelee kufadhaika na kumueleza kuwa watakachokifanya ni kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari. [6]
ama
Naamini wakaguzi wa serikali wakatakapokagua upya mahesabu kama Cegodeta ilivyoomba, ukweli ama kuna ubadhirifu au hapana, utajulikana," alisisitiza Ngawaiya. [7]
amani
Mgeni rasmi katika pambano hilo alikuwa mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye aliwasifu mabondia wote kwa kumaliza mpambano kwa amani na aliwasifu kwa uwezo mkubwa waliouonyesha. [8]
ambao
Katika uchunguzi wake, Mwananchi ilizungumza na maofisa mbalimbali wa elimu katika mikoa tofauti pamoja na wakaguzi, ambao wengi walieleza kuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu, ambayo hayatoi mwanga katika mkakati wa kuinua kiwango cha elimu. [9]
ana
Alisema tatizo kubwa ni kwamba, serikali imeshindwa kuweka vipaumbele vya taifa na badala yake imekuwa ikiendeshwa kwa matukio, hisia na dharura na kuongeza kuwa viongozi wa CCM wameshindwa kufikiri kwa pamoja na badala yake, kila kiongozi ana mtizamo wake anaotaka ndio uwe dira ya kuongoza taifa. [10]
au
Sababu kubwa za upungufu huo zimetajwa kuwa ni baadhi yao kustaafu au kufariki dunia wakati serikali inashindwa kuziba mapengo kutokana na uhaba wa walimu wenye sifa za kuteuliwa kujaza nafasi hizo katika ngazi mbalimbali. [11]
baadaye
Dakika tatu baadaye, Mgosi akaipatia Simba bao la tatu baada ya kupata pasi ya Nyagawa. [12]
badala
Wakati huohuo, CUF imeishutumu serikali ya awamu ya nne kwa kushindwa kuwafikisha mahakamani wahusika wa kashfa ya Richmond, badala yake inawapeleka mahakamani watu wasiohusika na kashfa hiyo. [13]
bado
Katika hatua nyingine, mjumbe wa kikundi cha wazee hao, Ally Makame alisema bado wanaendelea kuzitaka jumuiya za kimataifa kushughulikia suala la kisiwa hicho kujitenga na kuwa na dola yake kwani hatua iliyopo hivi sasa inaonyesha dhahiri kuwa watu wake wameendelea kudhalilishwa kila siku. [14]
bwana
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na bwana mmoja aitwaye John Gottman unasema: namna vile watu wanavyogombana unaweza kujua ni kiasi gani watu wanapendana halikadhalika utaweza kujua ni maamuzi yatokanayo. [15]
chaguzi
Kwa mujibu wa mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa CUF, Jussa Ismail Jussa, marekebisho hayo yatakuwa katika vipengele vya namna ya kupata wagombea wa chama katika chaguzi na kuongeza uwakilishi wa wanawake ndani na nje ya chama kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa. [16]
chake
Pia alidai kuwa mwenyekiti wa chama hicho alipopata safari za nje ya nchi mwaka 2008 ambaye aliambatana na mjumbe wa CUF, Mustafa Wandwi, katika safari hiyo alidai mwenyekiti huyo alimshawishi ajiunge na chama chake kwa kumuahidi kiasi cha Sh1 milioni. [17]
chao
Juni mwaka jana kikundi cha wazee 12 wa Kisiwa cha Pemba waliibuka na kuzua hoja ya kutaka kujitenga kwa kisiwa chao kwa madai kuwa, serikali ya CCM inawabagua kimaendeleo. [18]
chongo
Kweli ushabiki ni chongo. [19]
chuoni
Chama hicho pia kimeitaka serikali ichukue hatua za haraka kuhakikisha kuwa, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) zaidi ya 2000 walioachwa kwa sababu ya kushindwa kutimiza masharti, hasa kulipa madeni wanayodaiwa, wanarejeshwa chuoni na kuendelea na masomo. [20]
dhana
Epuka dhana na kusikiliza maneno ya watu. [21]
duni
Mama huyo ambaye ni mbunifu wa mitindo aliyedumu katika fani hiyo kwa muda mrefu zaidi, anasema elimu duni na kutoelewa umuhimu wa mitindo nchini ndiyo tatizo kubwa, kwani jamii ya kitanzania haina uelewa kabisa. [22]
es
Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, katibu mtendaji wa wazee hao, Hamad Ali Musa, alisema tayari walishafikisha suala hilo kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa kwani mauaji hayo yalitokea wakati viongozi hao wakiwa madarakani. [23]
fani
Kwenye kila fani kunakuwa na kanuni na taratibu zake za kutekeleza majukumu, fani nyingi zinazingatia elimu ya juu lakini kwenye michezo cha msingi ni nidhamu, siyo kwamba mwenye elimu ahitajiki la hasha ila ukiwa na elimu itakuwa ni faida kubwa. [24]
fidia
MWENYEKITI wa Taasisi ya Utawala Bora na Maendeleo (Cegodeta), Thomas Ngawaiya amesema hayuko tayari kumuomba radhi na kumlipa fidia ya Sh120 milioni, Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Philemon Ndesamburo, anayedai kukashifiwa. [25]
gani
Sasa kumlipa mkulima Sh100,000 bila kujali ameathirika kwa kiasi gani, ni kummaliza kabisa," alisema Tara. [26]
haina
Alisema mapema mwezi uliopita walipeleka maombi yao ya kutaka kujitenga katika ofisi za Umoja wa Mataifa, lakini walijibiwa kuwa Pemba haina sababu za kujitenga kutokana na ukweli wa mambo kwamba, Rais Jakaya Kikwete anashughulikia mpasuko uliopo ndani ya Zanzibar. [27]
haja
Ni vema viongozi wetu wakaelewa kuwa hakuna haja ya kuwafumba midomo watu wanapotafuta haki zao za msingi. [28]
hajui
Kauli hiyo ilionekana kumchanganya sana Kazim, akawa hajui la kufanya. [29]
hapa
WADHAMINI mbalimbnali wameshauriwa kutoangalia mchezo wa soka na kuacha michezo mingine, hali inayofanya kudumaa kwa michezo mingine hapa nchini. [30]
hapo
Akizungumzia msimamo wa serikali kuhusu masharti ya kuwarejesha chuoni hapo wanafunzi hao Ruhuza alisema hata hao walioweza kulipa si kwamba nao wana uwezo, bali wameamua kujinyima na hata kwa kukopa jambo ambalo limewaongezea mzigo. [31]
hasa
Maofisa hao waliohojiwa na Mwananchi kwa siku kadhaa sasa katika wilaya, mikoa na kanda mbalimbali, wamethibitisha kuwa, mbali ya upungufu wa wakaguzi, baadhi ya kanda hazina ofisi na vitendea kazi kama magari, fedha na vifaa vya ofisini hali inayosababisha wakaguzi waliopo kushindwa kuzifikia shule nyingi hasa za vijijini. [32]
hata
Kati ya halmashauri saba za mkoa huo, halmashauri za Kibaha Mjini na Vijijini ambako ndiyo makao makuu ya mkoa, ndizo zina hali mbaya zaidi, kwani wakaguzi wake hawana hata chombo kimoja cha usafiri. [33]
hawezi
Alisema katika salaam hizo za Mwaka Mpya, hakuna sehemu yoyote ambayo amemtaja Ndesamburo kama mtu binafsi na kwamba kwa msingi huo, hawezi kumuomba radhi na kumlipa fidia. [34]
hii
Hali kama hii inasababisha kushuka kwa kiwango cha elimu kwani kama shule haifanyiwi ukaguzi wa mara kwa mara, walimu hujisahau na kufanya wanavyotaka," alieleza mkaguzi huyo. [35]
hiki
Katika Kanda ya Magharibi, mahitaji halisi ya mjini Tabora ni wakaguzi 54, lakini wapo 36 hivyo upungufu ni wakaguzi 18. Upungufu huo, mtoa habari huyo anasema, unatokana na sababu kwamba, wakaguzi lazima wawe walimu, lakini kwa kipindi hiki kuna uhaba mkubwa wa walimu. [36]
hizi
Nasi tunajipanga kwenda DRC lengo hasa ni kudumisha ushirikiano na kuendeleza mchezo huu kwa nchi hizi”, alisema Mihayo. [37]
hofu
Katika muswaada mpya wa wanyamapori jambo hili lipo na hivi karibuni tutalifikisha bungeni hivyo msiwe na hofu na serikali inatambua shida ambazo mnapata," alisema Maige. [38]
hospitali
Alihangahaika kwenye hospitali nyingi bila mafanikio. [39]
hujui
Kwa kuwa hujui aliyekuletea ana nia gani na mumeo. [40]
hujuma
Kwa kutumia mwanya huo huo wa serikali kulala kusimamia mambo mengi muhimu, watumishi wengi wa umma wamejipata madaraka ya kufanya mambo ambayo kwa uhakika ni hujuma dhidi ya serikali yao. [41]
huko
Baada ya kumaliza elimu ya sekondari alijiunga na chuo uhazili huko huko ambapo baada ya kumaliza alifanikiwa kufanya kazi katika ofisi mbalimbali kama katibu muhutasi. [42]
huna
Ama unaota unahisi unakusaliti na huna uhakika, na huenda hujamuuliza. [43]
husika
Tunawatakia Yanga na Prisons maandalizi mazuri na kutumia kipindi kilichobakia kutengeneza timu ya ushindi ambayo matokeo yake ni sifa kwa Tanzania na si kwa klabu husika. [44]
hutumia
Sasa ukikuta timu ambazo saikolojia yao ipo katika hali nzuri hutumia nafasi hiyo kujipanga na hatimaye kupata ushindi kirahisi"anasema Maximo. [45]
huu
Katika suala la kumfikisha Waziri Seif Khatib mahakamani, Musa alisema kuwa, mapema mwishoni mwa mwezi huu mchakato huo utakuwa umekamilika, kwani mawakili wa kusimamia kesi hiyo tayari wameshapatikana. [46]
huwa
Alisema viongozi wengi wa CCM huwa hawaendi kuwatembelea wanachama wao, waliopo kwenye matawi na hivyo kuonekana chama ni cha viongozi wakati ni cha wanachama. [47]
huyu
Hivi sasa mama huyu ameolewa na ana watoto wanne, watatu wakike na wa kiume mmoja. [48]
idadi
Wilaya zinazokabiliwa na upungufu huo na idadi yake kwenye mabano ni Mwanga (4), Moshi vijijini (1), Same (1), Siha (9) zote za mkoani Kilimanjaro. [49]
ikawa
Na inawezekana ikawa hujui nini kamwambia mumeo kuhusu wewe. [50]
ila
Ninasema hivyo kwa sababu nchi yetu ina idadi kubwa ya wanamichezo lakini maandalizi yao huwa ni ya muda mfupi ila inapokaribia michezo mikubwa ndiyo mchezaji hupewa mazoezi mengi ili aweze kukabiliana na timu pinzani ambayo huwa imeishaandaliwa kwa mambo matatu niliyoyataja. [51]
ile
KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Villa Squad, Kenny Mwaisabula 'Mzazi' amesema ushindi wa mabo 2-0 walioupata Ijumaa iliyopita dhidi ya Prisons ni onyo kwa timu zote watakazokutana nazo kwani hivi sasa timu hiyo sio ile ya mzunguko uliopita. [52]
ili
Alitoa mfano kuwa katika wakati huu wa vita dhidi ya mafisadi, mmoja wa wabunge wa chama hicho alipeleka gari mahakamani, ili likamsaidie usafiri mmoja wa watuhumiwa wa kesi za ufisadi. [53]
ina
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango, Mwaimu Mntangi imeeleza kuwa, idara ya ukaguzi wa shule ina wakaguzi 1,094 nchi nzima na kati yao 976 ni wa shule za msingi, 132 wa sekondari na 23 wa vyuo vya ualimu. [54]
ipo
Laikini pamoja na hayo, bado tunadhani nafasi ipo kwa makocha kutumia wiki mbili zilizobakia kuwajenga wachezaji kisaikolojia na hata kuwapa nguvu ya ushindi. [55]
jengo
Wakaguzi hao pia hawana ofisi, badala yake wamekuwa wakijishikiza kwenye ofisi ya jengo la mkuu wa mkoa wa Pwani. [56]
juu
Alisema NCCR-Mageuzi kinaamini kuwa serikali ina uwezo wa kuwalipia wanafunzi wote wa elimu ya juu ada ya masomo, lakini serikali ya CCM kwa makusudi haitaki kufanya hivyo, kwa sababu inachukulia ujinga kama mtaji wa kuendelea kubaki madarakani, maana inajua wakielimika katu hawataruhusu watawala mafisadi kubaki madarakani. [57]
juzi
Shutuma hizo zimekuja baada ya serikali hiyo juzi kumfikisha mahakamani Naeem Gire, aliyedaiwa kuhusika na kashfa ya Richmond. [58]
kamati
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Babati Vijijini walitoa wito huo juzi wakati wakizungumza na wabunge wa kamati ya maliasili, utalii na Mazingira ambao walitembelea wilaya hiyo. [59]
kansa
Zaidi ya kuwa msaidizi wake, jamaa huyo albino, alikuwa ni mvumbuzi wa dawa kutibu kansa ya moyo, hata hivyo hakuwahi kumwambia Kazim. [60]
karibu
Tatizo jingine kubwa kwa kanda hiyo ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya kuendeshea mafunzo ya kitaalam na kitaaluma kwa walimu, hali ambayo imeelezwa kuwa imeathiri kwa kiasi fulani ushirikiano wa karibu kati ya Idara ya Elimu, Utawala na Ukaguzi wa shule. [61]
kasi
Kwa mujibu wa Kandihabi polisi inaendelea kupambana na kundi hilo lililoibuka kwa kasi na kutishia usalama wa maisha na mali za wakazi wa maeneo ya Mbagala kwa kufanya uhalifu wa kutumia silaha. [62]
kata
Madiwani hao,Laurent Tara wa kata ya Bashinet, Silas Uwema wa kata ya Galapo na John Kanda wa kata ya Kash, walisema, viwango vya fidia au pole ambayo inatolewa na serikali kwa waathirika wa manyama pori ni ndogo sana. [63]
kibao
Jamaa kauaaaa, kabakaaaaa, kafisadiiiiiii, kafanya kufuru kibao zinazopingana kabisa na msahafu wa dini yake, lakini badala ya kumkemea twamtetea. [64]
kikubwa
Alisema kuwa ushindi uliopatikana utaendelea, lakini kikubwa ni kulinda hadhi na heshima ya klabu. [65]
kile
Wote tunafahamu umuhimu wa kusikiliza kwa makini na kuelewa kile ambacho mtu unaambiwa au unaelimishwa. [66]
kipaji
Mwanamichezo lazima akubali wapo wanamichezo mbalimbali wanaocheza mchezo kama anaocheza yeye, ila wanatofautiana kwenye kipaji, mazingira na nidhamu kwa hiyo juhudi na maarifa ni kitu muhimu katika kuboresha akili ya mchezo nje ya uwanja na ndani ya uwanja. [67]
kitakuwa
Naye mkurugenzi wa msanii huyo, Hartmann Mbilinyi anasema Steve anatarajia kutengenezewa kipindi ambacho kitakuwa ni fungakazi kwa sanaa ya vichekesho ambayo inaonekana kupata umaarufu mkubwa hapa nchini. [68]
kitendo
FANI ya mitindo imekuwa ikichukuliwa kama burudani, hasa pale wabunifu wanaponadi kazi zao, kitendo ambacho kimekuwa kikichangia kupotosha maana yake halisi. [69]
km
Shule hizo ni Itandamilo iliyopo umbali wa km 142, Mwitiko km 185, Majojo km 200 na Kilumbi km 296 ambazo zote zipo mbali na makao makuu ya wilaya ya Sikonge; Tura km 149, Kizengi km 170, Kalangale km 212 na Migongwa km 209 kutoka Wilaya ya Uyui. [70]
kuambiwa
Ugomvi mwingi wa wanawake wengi unatokana na maneno ya kuambiwa ama kudhania. [71]
kucheza
Amewahakikisha ushindi mashabiki wake katika mechi yao dhidi ya Yanga wanayotarajia kucheza januari 31 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. [72]
kufa
Alisema wananchi ndio wa kwanza katika suala la kuhifadhi na kutunza hifadhi hizo, lakini akashangaa kwamba inapotokea tatizo la kujeruhiwa au kufa serikali inakuwa na kigugumizi katika kutekeleza hilo. [73]
kuhusu
Kuwashughulikia wahusika wa Richmond haitakiwi kuwa kificho kwa sababu Mheshimiwa Harrison Mwakyembe alishamaliza kila kitu kuhusu wahusika," alisema Atik. [74]
kujaribu
Kujua na kujaribu kutumia njia sahihi ya kugombana kutasaidia kutatua migogoro yenu. [75]
kujua
Kutokana na tatizo hilo, ofisi ya ukaguzi kanda imeamua kukagua shule maalum kama vile zile zenye malalamiko na ambazo wanafunzi wake wameonekana hawajafanya vizuri kwenye mitihani yao, lengo likiwa ni kujua tatizo la kufeli. [76]
kule
KOCHA Marcio Maximo anasema sasa anaelekeza nguvu zake katika kuiandaa vema Timu ya Taifa, Taifa Stars ili iweze kukabiliana na mikiki mikiki ya Michuano ya Mataifa ya Afrika inayotarajia kupingwa kule Ivory Coast Februari. [77]
kuliko
Alisema umefika wakati Wizara ya Mali Asili na Utalii kujali watu zaidi kuliko inavyojali wanyama. [78]
kumbe
Zaidi ya yote kumbe alikuwa amechukua mkopo benki baada ya biashara zake kumchanganyia, ili kuboresha zaidi, akiamini kuwa kwa namna alivyokuwa akipata fedha angeweza kulipa deni ndani ya muda mfupi. [79]
kumpa
Alisema kuwa ameamua kuiunga mkono CUF kwa sababu watendaji wake ni majasiri na wana uwezo mkubwa na kwamba CUF ni chama cha ukombozi hivyo kinastahili kuungwa mkono na wananchi wote, ikiwa ni pamoja na wa Mbeya Vijijini ambao alisema wanatakiwa kumpa kura za Mponzi. [80]
kumuua
Ndio akaona ni bora awapigie simu wale jamaa zake na kuangalia ni namna gani wanaweza kumuua albino ili waendelee na biashara ile ya madini na uvuvi wa samaki. [81]
kuna
Hata hivyo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetoa taarifa kuwa, kuna wakaguzi wa kutosha. [82]
kundi
JESHI la polisi mkoani Temeke, limewakata watu 100 kwa tuhuma za kujihusisha na kundi haramu la kihalifu linalojiita Mbwa Mwitu. [83]
kuona
Kwa upande wake Ofisa Elimu Mkoa wa Mtwara, Hipson Kipenya alilishukuru shirika hilo kwa kuona umuhimu wa kuinua michezo mashuleni ambapo kwa kufanya hivyo watoto wengi wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika masomo na vipaji vyao kupanda na maendeleo yao yanapanda vizuri. [84]
kupingwa
Jussa alisema wanatarajia kuwa mapendekezo hayo ya marekebisho yatapita bila ya kupingwa katika mkutano huo. [85]
kusaidia
Akikabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Shirika hilo, Chigogoro Mohamed alisema kuwa lengo la kutoa mipira hiyo ni kusaidia kuendeleza michezo katika shule za msingi zilizopo katika mkoa wa Mtwara hususan wasichana. [86]
kushona
Amefahamisha kuwa amekuwa akichora kila anachobuni na kisha kushona mavazi yanayowezatumika katika shughuli mbalimbali. [87]
kutoa
Alisema NCCR-kinaamini kuwa suala la elimu ni huduma ya jamii, hivyo serikali kama mkusanyaji wa kodi ni wajibu wake kutoa huduma za jamii kwa wananchi wake. [88]
kuu
Sio siri mwandishi, tupo katika mazingira magumu sana katika utendaji kazi zetu, maana changamoto ndiyo kama hizo tulizokueleza ambazo tunaamini ndizo kuu katika kazi zetu. [89]
kuua
Kutokana na mfumo mbovu wa elimu ikiwemo sera ya uchangiaji wa elimu ya juu Ruhuza alituhumu serikali kuwa, ina mkakati wa kuua elimu nchini tangu shule za msingi hadi vyuo vikuu hususan kwa watoto wa masikini. [90]
kuzidi
Makamba ambaye pia ni mbunge wa kuteuliwa na rais, amehimiza ushirikiano kati ya viongozi na wanachama kwa lengo la kuzidi kukijenga Chama Cha Mapinduzi. [91]
kweli
Katika taarifa hiyo, Ngawaiya anasema ni kweli kwamba Desemba 29 mwaka jana, aliitisha mkutano wa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kutoa salamu za mwaka mpya za taasisi yake kwa wananchi. [92]
la
Musa pia alisema wanakusudia kumfikisha katika mahakama hiyo aliyekuwa mkuu wa Jeshi la Polisi, Omary Mahita wakidai kuwa, damu iliyomwagika bila hatia katika kipindi hicho haiwezi kufumbiwa macho na hivyo ni muhimu haki itendeke na sheria kuchukua mkondo wake. [93]
labda
Kabla sijaeleza sababu ambazo naona zinasababisha kushuka kwa e-government nchini, labda nitaje faida za mpango huu. [94]
lake
Msemaji wa timu hiyo, Idd Godigodi alisema kuwa kuundwa kwa kamati maalum, lengo lake ni kuhakikisha timu inafanya vizuri. [95]
langu
Huku sasa ni kuzinguana, kumbe hata mawaziri nao huwa wanakuwa wasanii, inawezekanaje niwasiliane na wewe nikiwa nje ya nchi uniambia yuko mvumbuzi wa dawa ya kuponya tatizo langu halafu sasa aniambie hajui atampata vipi, huu ni uhuni,” alijisemea Kazim akiwa mwenye hasira na kuwaza kuwa kama asingempa dawa hiyo angefanya mpango wa kumuua kwa sababu naye alikuwa albino. [96]
leo
Masuala ya ufisadi wa rada, ununuzi wa ndege ya rais pamoja na suala la kampuni hewa ya ufuaji umeme nchini ya Richmond hayakuanza leo, bali yalikuwapo tangu utawala wa awamu ya tatu, lakini Chadema imeshupalia suala la ufisadi huku ikionekana kuwatetea mafisadi," alisema Jussa. [97]
licha
Katika mchezo huo, timu zote hazikuonyesha ushindani hasa kipindi cha kwanza, licha ya kuwa Simba ilizinduka dakika 20 za mwisho na kuonyesha uhai wa mashambulizi. [98]
maana
Waziri Khatib alitufumba midomo kwa kutumia nguvu za dola na ndiyo maana tukawekwa ndani," alisema Musa. [99]
maelekezo
Wachezaji wangu walifuata maelekezo niliyowapa ndiyo maana walicheza vizuri kuliko Prisons, ukiangalia ile mechi tulitawala sana. [100]
maeneo
Hata kanda moja ilipotaka kuazima wakaguzi kutoka maeneo mengine yenye wakaguzi wengi, imeshindikana kutokana na ukosefu wa pesa. [101]
mafuta
Kivipi? Kama unavyojua kusema maneno yanayoudhi ni kama kumtupia kijinga cha moto mtu ambaye tayari ameshaoga mafuta ya taa. [102]
makao
Mathalani Idara ya Ukaguzi Kanda ya Ziwa yenye makao yake mjini Mwanza ina upungufu wa watumishi 89 wakiwemo wakaguzi. [103]
makini
Alitoa changamoto kwa wananchi kuwa makini na kundi hilo linalokua kwa kasi hususani maeneo ya Mbagala na kuwataka washirikiane na polisi kwa kutoa taarifa ili kulidhibiti. [104]
matatu
Alikuwa akituambia kuhusu masuala matatu muhimu yafuatayo ambayo itakuwa vizuri nikiyaelezea ili tuweze kuayafuatilia na kuelewa msingi wa mwanamichezo mwenye nidhamu : kwanza kuna suala la akili ya mchezo, pili ni suala la stamina na tatu ni kuutunza mwili. [105]
mbinu
Tunaamini, kwa siku hizi zilizobakia, makocha na madawati ya ufundi, watawapa wachezaji mbinu sahihi na kuwaandaa wachezaji wetu kisaikolojia kwani mafanikio ya Yanga au Prisons ni mafanikio ya Taifa. [106]
miaka
Sambamba na hilo la kupokea na kujadili taarifa hiyo, pia baraza kuu litaandaa kazi za chama kwa miaka mingine mitano kuanzia mwaka 2009 hadi 2014," alisema Jussa. [107]
migogoro
Ni aibu kwa sababu ripoti ya mwisho inaonyesha kuwa hata nchi ya Zimbabwe ambayo ina migogoro ya kiuchumi na kisiasa ipo juu yetu. [108]
mikiki
Alisema mbali na yeye pia Moro United kuna wachezaji wazuri na wenye uwezo mkubwa wa kuweza kuhimili mikiki ya mzunguko wa pili kwa ufanisi mkubwa. [109]
mimi
Ndesamburo wala kumlipa fidia anayotaka ya Sh 120,000,000 kwa sababu sijawahi kumkashifu mbunge huyo wa Moshi Mjini ambaye pia ni mbunge wangu kwa kuwa mimi pia ni mkazi wa Moshi Mjini. [110]
minne
Ripoti hiyo ya miaka minne iliyopita inaonyesha kuwa Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya 127 mwaka 2005 hadi 147 mwaka jana. [111]
mipango
Stive Nyerere nimemuandalia mipango ya mwaka mpya ambayo itakuwa na mafaniko makubwa katika sanaa yake, kwani kutokana na uzoefu wangu katika nchi nyingi za Ulaya nilizotembelea, hivyo naamini kuwa uwezo wa kukamata soko la dunia upo," anasema Mbilinyi. [112]
mipira
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mipira 500 ya mchezo wa wavu, na netiboli yenye thamani ya shilingi 1 milioni. [113]
miti
JANUARI Mosi mwaka huu ilikuwa ni siku ya taifa ya kupanda miti. [114]
mkoani
Taarifa kutoka mkoani Pwani zinaeleza kuwa wakaguzi wapo katika mazingira magumu ya kutekeleza majukumu yao kutokana na uhaba mkubwa wa vitendea kazi. [115]
mno
Anasema kuwa muda uliopo ni mfupi mno kabla ya kwenda Afrika Magharibi hivyo ni muhimu basi wachezaji waliomo katika kikosi chake wakaishi kulingana na maadali ya mchezaji soka ili kulinda viwango vyao lakini pia kwavile muda mwingi watakuwa katika klabu zao ni muhimu wakafata maelekezo ya walimu wao kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamemsaidia kwa kiasi kikubwa. [116]
msaidizi
Jamaa huyo ambaye alikuwa kama msaidizi wake wa karibu, alikuwa akimuwakilisha katika kazi mbalimbali na ndiye aliyekuwa ana siri zake nyingi. [117]
mtandao
Kuna baadhi ya wasomaji wataanza kujiuliza e-government ni nini? Hizi ni huduma ambazo zinatolewa na serikali kwa wananchi wake kwa njia ya kompyuta ambayo imeunganishwa katika mtandao wa internet. [118]
muda
Upungufu huo umesababisha shule nyingi kutokaguliwa kwa muda mrefu. [119]
mumewe
Mkewe Kazim, hajui chochote kuhusu mumewe kuua albino; ni mwanamke ambaye anafanya kazi ofisi ya usalama wa taifa na zaidi ya yote anaijua vizuri sheria. [120]
mwaka
Baada ya vurugu hizo za mwaka, watu kadhaa kutoka Pemba walikimbilia Shimoni, Mombasa wakisaka hifadhi ya kisiasa. [121]
mwalimu
Kocha alipenda sana kuzingatia mahudhurio, sababu alikuwa akiamini ili tuelewane vizuri sana ni lazima afikeshe mafunzo yake kwa njia ya uso kwa uso, sawa zipo njia nyingi za kujifunza lakini njia hii ya kuhudhuria mafunzo na kumsikiliza mwalimu ilitusaidia sana. [122]
na
Mauaji ya Wapemba hao yalitokea mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais wa Zanzibar wakati Amaan Abeid Karume alipotangazwa mshindi na kusababisha wapinzani kuandamana kupinga ushindi huo. [123]
naibu
Mrema aliendelea kuwavutia wananchi hao aliposema kuwa alipokuwa naibu waziri mkuu alifanya kazi zake vizuri, ikiwa ni pamoja na kukamata ndege iliyokuwa na dhahabu zenye thamani ya Sh175 milioni, lakini waziri mkuu wa wakati huo hakufanya lolote zaidi ya propaganda. [124]
nami
Hivyo ndiyo nami nikafikia hatua ya kujiuliza swali hili kuhusiana na nchi yetu kushuka. [125]
nani
Tunaamini CAF ilitoa ratiba mapema ili klabu zinazoshiriki ziweze kuweka mikakati imara ikiwa ni pamoja na kutambua zitapambana na nani, timu inayokutana nayo inachezaje, watachezea wapi na itakuwa ni wakati gani. [126]
nao
Aliwataka viongozi wa CCM nchini kujenga tabia ya kutembelea wanachama wao waliopo katika ngazi za chini, ili kuwa karibu nao na kuwafanya wakione chama ni chao na sio cha viongozi. [127]
naye
Aliongeza kuwa "kumfikisha mtu ambaye hahusiki na Richmond hakuonyeshi ukweli wowote katika kuwashughulikia wahusika wa kashfa hiyo". Atik alimgeukia Waziri Mkuu Mizengo Pinda akieleza kuwa naye haeleweki katika kuwashughulikia wahusika wa kashfa hiyo. [128]
nayo
MENEJA wa timu ya Mtibwa Sugar ya Turiani Mkoani Morogoro, David Bugoya ametamba na timu yake kutoa vipigo kwa kila timu itakayokutana nayo na hasa ikiwa kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa Manungu. [129]
nchini
Wapemba hawatakubali kuendelea kufedheheshwa kama wakimbizi, hivyo ni vema mashirika ya UN yakaanza kujiandaa mapema kupokea wakimbizi nchini Kenya wakati wa uchaguzi," alisema Makame. [130]
ndio
Upungufu huo ndio unachangia kushuka kiwango cha ufaulu wa wanafunzi shuleni, kutokana na walimu kufundisha kwa mazoea bila kukaguliwa. [131]
ngumu
Alisema mechi yetu inayofuata ni ngumu lakini muda wa kufanya maandalizi waliokuwa nao bado ni mwingi hivyo wanataka kuutumia muda huo kwa kufanya marekebisho madogomadogo na kusema kwa sasa wanamshukuru Mungu kwani timu haina majeruhi. [132]
ni
Mkapa alisema katika kipindi hicho cha Hard Talk kuwa, anashangaa waandishi kuokota habari wakati mtoaji rasmi wa taarifa kama hizo ni serikali. [133]
nina
Pia nina matatizo makubwa ya gharama za uendeshaji ofisi kama vile vifaa vya ofisini," alisema ofisa huyo. [134]
nini
Mbrazil huyo anasema kuwa soka ya dunia ya sasa imebadilika mpira hauchezwi kwa kuangalia rekodi za nyuma kwamba nani na nani wamefanya nini siku zilizopita kwani kila mmoja hutaka kufikia malengo aliyojiwekea. [135]
nzuri
Nitatumia uwezo wangu kuhahakisha timu yangu ya Maro United inafanikiwa kushika nafasi nzuri za juu kama alivyosema kocha wangu Minziro," alisema Nizar. [136]
pale
Hatuna shaka kabisa kwamba viongozi wa timu zetu za Yanga na Prisons wamechukua hatua za ziada na kutumia kufanya maandalizi ya hapa na pale kujiweka sawa kwa mechi hizo. [137]
pande
Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 48 lililofungwa na Obina kwa shuti la umbali wa mita 40 baada ya kupata pande la Mussa Hassan Mgosi. [138]
picha
Ikabidi kwa kumtia moyo, ikabidi aende kwenye ofisi ambayo alikuwa akifanyia utafiti huo na kufanikiwa kupata picha yake. [139]
pili
SIMBA ya Dar es Salaam, imeanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa ushindi wa mbinde, baada ya kuifunga Polisi Moro mabao 3-2, mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. [140]
poa
Na kwa kuwa Makengeza Enterprises haitaki watu wapekue baadaye na kupata funza badala ya mafunzo, viatu maalum vitauzwa kwa bei poa hapohapo kwenye tamasha. [141]
pole
Katika hatua nyingine, Wizara ya Mali Asili na Utalii imeshauriwa kuongeza viwango vya fidia na pole kwa watu na mashamba ambayo yanaharibiwa na wanyamapori hasa katika maeneo yanayopakana na hifadhi za taifa. [142]
pumzi
Mchezaji akiwa na pumzi ya kutosha atakuwa amepanua mapafu yake vizuri na kumuwezesha kuwa na stamina itakayomfanya kuomba mipira uwanjani, kutuliza vizuri na kutoa pasi kama mchezaji mwenzake anavyotaka, hataweza kutegea, atajituma na kuweza kucheza kitimu. [143]
rafiki
Ninaye rafiki yangu ambaye alikuwa mpigania uhuru wa Afrika Kusini. [144]
ripoti
UTAFITI uliofanywa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa (UN) kuhusiana na masuala ya e-government na ripoti yake kutolewa mwaka jana, Tanzania imeshuka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mwaka 2005, ripoti hiyo ilipotolewa mara ya mwisho. [145]
roho
Nakufa, mkuu wa polisi unaniua, sawa mimi nimemuua albino, lakini wewe unaniua mimi kwa kunipiga kibao, imeandika wapi kwamba muharifu apigwe, kabla ya kufikishwa mahakamani,” alisema Kazim huku akikata roho. [146]
saa
Mpambano huo wa raundi 12 ulioanza saa nne usiku, mabondia wote walionyesha kiwango cha juu kiasi cha kuwavutia mashabiki waliohudhuria pambano hilo. [147]
salaam
Ngawaiya, ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM mkoani Kilimanjaro, alisema katika salaam hizo pia aliiomba serikali kuzifanyia marekebisho sheria za vyama vya siasa na vyama vya ushirika. [148]
sanaa
Anasema yeye binafsi amepania kuboresha sanaa yake na kuipenyeza katika soko la kimataifa. [149]
sauti
Jina laStive Nyerere limetokana na sanaa yake kwa kuwa alianza usanii kwa kuingiza sauti ya Baba wa Taifa ,Mwalimu Julius Nyerere. [150]
sawa
Hiyo ni sawa na wakaguzi watano kustaafu, sita wapya kuajiriwa. [151]
sekta
Maadhimisho ya siku hiyo yaliyoanza kuadhimishwa mwaka 2001 yamekuja huku kukiwa na taarifa kuwa sekta ya misitu imekuwa ikikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo upoteaji wa miti. [152]
sera
Akitoa msimamo wa chama hicho jana kuhusu suala la wanafunzi hao, Katibu Mkuu wa chama hicho, Samuel Ruhuza alisema NCCR-Mageuzi kimeitaka serikali kuachana na sera ya uchangiaji wa elimu kwa kuwa ni mbovu na imepitwa na wakati. [153]
shida
Wananchi hao walianza kuonyesha kuvutiwa na Mrema mara aliposimama jukwaani wakati alipomshangilia na kupiga kelele kuonyesha kumkubali na bila kuchelewa waziri huyo wa zamani wa mambo ya ndani alianza hotuba yake kwa kuwaambia wananchi kuwa shida na maisha magumu waliyonayo wamejitakia. [154]
si
Jambo hili ni uongo kwani suala letu halihusiani kabisa na masuala ya siasa, katika suala la kutaka Pemba iwe na dola yake si suala la CUF, ni suala letu wananchi, hivyo ni vema viongozi wakafahamu jambo hili," alisema Makame. [155]
sina
Mimi sina sababu ya kuomumba radhi Mh. [156]
sisi
Alisisitiza kuwa serikali ya sasa inapaswa kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuwekeza katika elimu, kwa kuzingatia falsafa yake kama alivyowahi kusema kuwa, "Tunampa vitu vingi mwanafunzi anayesoma katika chuo kikuu, ili na sisi tuweze kupata vingi kutoka kwake atakapomaliza chuo kikuu. [157]
siyo
Dhana ya Cegodeta haimlengi mtu binafsi na wala sheria inayomuomba siyo kwa ajili ya kumkomoa mtu binafsi, bali ni kwa manufaa ya umma," alisema. [158]
soko
Idarous anapendekeza kuwa vianzishwe vyuo vya ubunifu wa mitindo katika ngazi mbalimbali ili kupata watu wenye ujuzi kamaili ambao wataweza kutengeneza bidhaa zitakazoweza kushindana katika soko la kimataifa. [159]
tajiri
Huku akiendelea na kazi Kazim alikuwa ni mtu tajiri kwa muda mfupi mno. [160]
tamaa
Alisema mkakati huu unajidhihirisha katika mazingira mabovu ya kujifunzia yanayowakatisha tamaa walimu na wanafunzi wao kwa ujumla, huku watoto wachache wenye uwezo wakisoma katika shule zenye mazingira mazuri ya kujifunzia. [161]
tena
Katika dakika ya 61, Obina aliwanyanyua tena mashabiki wa Simba kwa kuandika bao la pili baada ya kuuwahi mpira wa mbali wa Ulimboka Mwakingwe ambaye alitengenezewa mpira na Nico Nyagawa. [162]
tu
Kwa mujibu wa mtoa habari hizo, Kanda ya Ziwa, ambayo inahudumia mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera ina wilaya 20 ambazo zina upungufu mkubwa wa watumishi, huku Ukerewe ikiwa na mkaguzi mmoja tu. [163]
tulikuwa
Nilifikiri sisi tulikuwa tunanyanyaswa lakini nilichoona huko ni zaidi. [164]
tuna
Nimeridhishwa na kiwango cha wachezaji wangu licha ya kwamba hatukufanikiwa kutwaa ubingwa kule Uganda hii inanipa imani ya kwamba ikiwa tutajiandaa vya kutosha basi tuna nafasi ya kufanya vizuri kule Ivory Coast," anasema. [165]
tunaona
Mara nyingi watu wakubwa tunaona vipaji lakini tunapuuza sababu hatujali kuendeleza vipaji hata kwa ushauri unaofaa tu. [166]
ubia
Akizungumza kwenye mkutano huo, mwenyekiti wa chama hicho wilayani Kinondoni, Abdulkarim Atik alisema Rais Jakaya Kikwete alipoingia madarakani mwaka 2005 alisema urais wake hauna ubia na mtu yeyote. [167]
ubora
IDARA ya ukaguzi, inayopaswa kukagua kazi, ufundishaji wa walimu darasani, kiwango cha ubora wa mazingira ya kujifunzia na vitendea kazi, inakabiliwa na uhaba mkubwa wa wafanyakazi, uchunguzi wa Mwananchi umebaini. [168]
uchumi
Baadaye viatu hivi vitatolewa kwa watoto yatima ili na wao waweze kumkumbuka aliyefanikiwa sana kuvuruga amani ya dunia, uchumi wa dunia na mazingira ya dunia, baada ya kuvuruga demokrasia ya dunia ndani ya nchi yake mwenyewe wakati wa ‘kuchaguliwa’ mara ya kwanza. [169]
uelewa
Mwaisabula alisema nidhamu na uelewa wa wachezaji wake ndiyo uliochangia ushindi huo na hali hiyo itaendelea katika mechi zote zinazofuata. [170]
uhuru
Kiongozi huyo wa Cegodeta alisema: "Sitamuomba radhi (Ndesamburo) wala kumlipa fidia na ana uhuru na haki ya kwenda mahakamani kama akipenda. [171]
uko
Mimi sikisemi chama chochote kile maana ushabiki huo uko kote kote, kwa chama cha zama zile hadi chama cha zama hizi. [172]
umma
Alisema pamoja na mambo mengine, katika risala yake ya maandishi, alizungumzia utawala bora na maendeleo na kuiomba serikali iongeze nguvu na kudhibiti wizi na ubadhirifu wa fedha za umma, katika vyama vya ushirika na vyama vya siasa. [173]
upo
Aliongeza kuwa ' Sina uoga wala mshituko kukutana na Yanga kwani uhakika wa ushindi upo, tunajiamini kwani mapumziko ya maandalizi ya mzunguko wa pili tulisahihisha makosa yote hivyo ni imani yangu kuwa tutafanya vizuri. [174]
upya
Hivyo niliomba tuhuma hizo zichunguzwe na mahesababu yakaguliwe upya na mkaguzi mkuu wa serikali ili ukweli ujulikane. [175]
uso
Miyeyusho naye alijibu mapigo katika raundi ya sita hadi ya tisa kwa kumpa mpinzani wake makonde ya uso na kumfanya kuchanganyikiwa huku mashabiki waliogawanyika pande mbili ikiwemo kambi ya Temeke ambayo anatoka Matumla na kambi ya Kinondoni anayotokea Miyeyusho wakishangilia kwa nguvu huku kila mmoja akivutia upande wake, lakini kiburudisho ilikuwa kambi ya TMK iliyokuwa ikiongozwa ushangiliaji na msanii Juma Nature. [176]
viatu
Kutakuwepo na sanamu kubwa ya Kichaka na wote mtapewa nafasi ya kuitupia viatu kwa nguvu zote. [177]
vibaya
Ni dhahiri kuwa itajisikia vibaya hivyo kuboresha na kuongeza juhudi ili ripoti nyingine itakapotolewa iweze kufanya vizuri. [178]
vile
Mkaguzi huyo alisema kwa vile sheria ya ukaguzi inazuia ukaguzi kufanywa na mtu mmoja, wilaya nyingi zimekuwa hazifanyiwi ukaguzi na zile ambazo zimekuwa zikifanyiwa ziko jirani na ofisi za ukaguzi ambazo usafiri pekee wa kuzifikia eneo hilo ni kwa miguu tu. [179]
vipaji
SHIRIKA la kuendeleza michezo na kuinua vipaji kwa vijana katika Mkoa wa Mtwara la Sport Development limetoa msaada wa vifaa vya michezo kwa ofisi ya elimu ya mkoa. [180]
vipi
Mambo vipi mashosto. [181]
vya
Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika jana kwenye viwanja vya Manzese Bakhresa, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa CUF, Ismail Jussa aliituhumu Chadema kuwa harakati zake za kupinga ufisadi hazina ukweli wowote. [182]
vyake
Kweli wale watu walimuua yule albino na kwenda na viungo vyake kwenye maeneo ya biashara. [183]
vyema
Steve Mengere maarufu kwa jina la Stive Nyerere, anasema mwaka mpya wa 2009 ni mwaka wa mabadiliko kwake na anasema ni vyema kwa wasanii wenzake kuboresha kila kitu katika maisha kuanzia katika kazi za usanii, maisha, tabia na mavazi. [184]
vyote
Hivi vyote vinapungua kwa kiasi kikubwa chini ya utaratibu huu. [185]
wageni
Alisema mkutano utakuwa na wageni kutoka katika taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi ili kushuhudia demokrasia inavyofanya kazi ndani ya chama chao na kwamba hadi sasa wanatarijia ushiriki wa wajumbe 700 katika mkutano huo. [186]
wako
Yanga tunaweza kusema wako pazuri, kwa kuwa wachezaji wake wengi walikuwa kwenye timu ya taifa iliyoshiriki mashindano mbalimbali ikiwemo Kombe la Chalenji katika siku za karibuni. [187]
wana
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, amewataka wana CCM kutolumbana kwa lugha mbaya na wanachama wa vyama vingine vya siasa nchini. [188]
wao
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakitembea nchi nzima kutangaza Operesheni Sangara, wao CCM wanatengeneza nyavu za kumnasa huyo sangara. [189]
wiki
Msimamo huo wa Ngawaiya, ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini kwa tiketi ya TLP kabla ya kujiunga na CCM, umekuja wiki moja tu baada ya Ndesemburo kutoa siku 14 kwa mwenyekiti huyo kuomba radhi na kumlipa fidia ya Sh120 milioni kwa madai kuwa alimkashifu na kwamba asipofanya hivyo atafikishwa mahakamani. [190]
yaani
Sasa hivi nakuja kivingine yaani hata umma wa Watanzania utashangaa kwani nitakuwa sikamatiki kabisa, nina uhakika huo kwani meneja wangu kaniandalia mambo mazuri ya kufanya,” anasema Stive Nyerere. [191]
yako
Unapoanza kufungwa sio kwamba tayari umepoteza mchezo unatakiwa kutulia na kurekebisha makosa yako na baadaye kuangalia ni namna gani unaweza kupata ushindi hivi ndivyo ninavyotaka tukafanye hata tutakapoenda Ivory Coast. [192]
yao
Kiongozi huyo alisema, hivi sasa wapo katika mchakato wa mwisho wa kutafuta mawakili watakaosimamia kesi yao ipasavyo wakati itakapoanza kusikilizwa. [193]
yenu
Inachokupasa ufahamu kuwa kuziba kauli katika suala ambalo limekuudhi hupelekea madhara makubwa mbeleni katika mahusiano yenu na huenda ikaathirika afya yako. [194]
yeye
Hoja ya kutaja majumba na helikopta kwenye taarifa yangu haikummaanisha mtu, kwani si yeye pekee mwenye nyumba na helikopta nchini mwetu. [195]
yote
Kandihabi alisema polisi imejipanga kukabiliana na kundi hilo kwa kuanzisha operesheni maalum kuwasaka katika maeneo yote ya Manispaa ya Temeke. [196]
yuko
Huyu yuko kwenye upande wa madini. [197]
yule
Kwani bila kusikiliza kwa makini kile ambacho unaambiwa au unafundishwa ni sawa na kumdharau yule ambaye anajitahidi kukupa suala muhimu ambalo litakuelimisha au kukusaidia. [198]
zako
Zipo hizi hisia wakati mwingine za kumchukia bila kujua sababu, lakini sababu ni kwamba dhana zako ndizo zinakupeleka huko. [199]
zetu
Kwa kawaida kila wilaya inapaswa kuwa na wakaguzi tisa, lakini katika kanda yangu wapo wakaguzi chini ya watano hivyo ukiangalia utaona upungufu tulionao katika wilaya zetu ni mkubwa kwa upande wa wakaguzi," alieleza mtoa habari huyo na akaongeza kuwa tatizo limekuwa kubwa zaidi baada ya wakaguzi sita kustaafu na wengine watatu kufariki dunia ilhali serikali imeshindwa kuteua wengine. [200]