Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2009-01-17

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


afanye 
Huenda unadhani hafanyi vile unataka afanye na hujamuambia au hujui unataka afanye nini. [1]
aina 
Sendeka, mmoja wa wabunge machachari, aliwasili mahakamani hapo kwa gari aina ya Land Rover, Defender ya polisi na kupelekwa katika chumba cha mapumziko kabla ya kupandishwa kizimbani. [2]
akaanza 
Wakati bado tunacheka akaanza. [3]
ama 
Wizara yangu haijatamka wala haijamtuma mtu ama taasisi yoyote kumchunguza au kumtisha wala haihusiki na upelelezi. [4]
ambalo 
Baadhi ya ofisi za serikali ambazo zimebahatika kuwa na kurugenzi za ICT/IT nyingi zimekuwa hazitumiki ipasavyo kwani zimekuwa zikitumika kwa kutoa ushauri butu na kushauri manunuzi ya vifaa mbalimbali vya kompyuta (hardware na software) kiholela bila kuzingatia mahitaji halisi jambo ambalo linapoteza fedha nyingi za serikali. [5]
ambazo 
Na jana, Rais Kikwete alionekana kuyajua hayo mapema na maagizo yake mengi yalilenga sehemu zote ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wadau kuhusu utendaji wa kampuni hiyo. [6]
ana 
Akizungumza na Mwananchi jijini jana, Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega alisema mazungumzo baina ya timu hizo mbili yapo katika hatua ya awali, lakini alisema ana imani watafikia makubaliano. [7]
anywa 
Rushwa pia ni tatizo kubwa, kwa sababu wengi waliopewa tenda za ujenzi hukutwa na makosa mbalimbali hapo kabla, lakini ni jambo la kushangaza kuwa hupewa tenda zaidi na zaidi, huku kimsingi walipaswa kuchukuliwa hatua ikiwemo kunyang’anywa leseni," anasema. [8]
au 
Baada ya tathmini hiyo, huruma stahiki itatolewa kwa wale ambao itabainika kwamba, kwa sababu moja au nyingine, hawana kabisa uwezo wa kuchangia kwa kiwango walichopangiwa, baada ya tathmini hiyo kukamilika, kundi hili pia litaruhusiwa kurudi vyuoni. [9]
baada 
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, ameamua kuitua mzigo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na kujitwisha baada ya kueleza kuwa, wanafunzi watakaojiona kuwa wameshindwa kuchangia gharama za elimu, wakate rufaa kwake. [10]
badala 
Baadaye, mfanyabishara wa madini ya Tanzanite, Baraka Kanunga alijitokeza badala yake na kuungana na mfanyabiashara mwenzake Joel Sabore Lesirya ambao wote kwa pamoja walifanikiwa kumdhamini mbunge huyo wa Simanjiro. [11]
bado 
Akizungumza mahakamani hapo wakili wa upande wa mashitaka, Ngole aliiomba mahakama kuwapa muda wa kukamilisha upelelezi wa keshi hiyo kwa kuwa bado haujakamilika na kuomba mahakama hiyo kuipangia tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo. [12]
baina 
Florens Turuka, aliridhia kufanyika kwa vikao vya ziada baina ya wabunge wa kamati, serikali na wadau wa habari lakini isiwe kwa shinikizo kutoka kwa wadau na wanaharakati. [13]
bali 
Hata hivyo, alisema si jukumu lake kumchunguza mtu bali vipo vyombo vinavyohusika, ambavyo vinastahili kuulizwa kuhusu suala la Jaji Warioba kuchunguzwa, na kwamba iwapo vitafanya hivyo Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), ndiye mwenye mamlaka ya kuamua kumfikisha mtu mahakamani ikiwa ataridhishwa na ushahidi alionao. [14]
bila 
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, inaonekana mafuvu na mifupa hiyo ya watu wasiofahamika, imekuwapo eneo hilo muda mrefu bila kujulikana. [15]
bin 
Wababe wa kivita walifanikiwa kuuondoa utawala wa kijeshi wa Kirusi hadi pale kundi la Watalebani lilipoitwaa nchi hiyo mwaka 1996. Utawala huo wa Watalebani ulifikia tamati mwaka 2001 kutokana na nguvu kubwa za kijeshi za Marekani, iliyokuwa ikimuunga mkono Osama bin Laden wakati huo. [16]
binafsi 
Hapa tunaanza kushuhudia ubaguzi ukianza kujitokeza katika sekta ya elimu kwamba, watoto wa masikini hawana nafasi tena ya kupata elimu ya juu, ikimaanisha kuwa vyuo vya umma sasa ni sawa na vyuo binafsi ambako mwanafuzi asiyelipa ada hufukuzwa. [17]
binamu 
Mdogo wake, Amanullah alitwaa madaraka hadi mwaka 1929 madaraka yake yalipochukuliwa na binamu yake Nadir Khan aliyeongoza kwa miaka minne kabla ya kuuawa. [18]
butu 
Mziba aliisema safu ya usjambuilii wa timu hiyo imeonekana kuwa butu hivyo kukosa magoli mengi kwenye mechi ya Jumatatu iliyopita dhidi ya Azam. [19]
bwana 
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na bwana mmoja aitwaye John Gottman unasema: namna vile watu wanavyogombana unaweza kujua ni kiasi gani watu wanapendana halikadhalika utaweza kujua ni maamuzi yatokanayo. [20]
chake 
Oluoch alisema chama chake kinasubiri utekelezaji wa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kufanya uhakiki wa mwalimu mmoja baada ya mwingine. [21]
chetu 
Leo tutacheza mchezo wa kirafiki baina yetu kwa kuwashirikisha wachezaji ambao ni waanzilishi wa Taswa Fc wa siku nyingi ambao watacheza na wageni katika chama chetu na timu yetu lengo likiwa ni kuleta maendeleo na kupanua zaidi chama chetu ili kiendelee kukua zaidi na kujul;ikana ndani na nje ya nchi," alisema Majuto. [22]
dhana 
Naye Mwenyekiti wa Yanga Imani Madega alisema udhamini wa TBL mbali na kuwa na faida ya kuongeza kipato katika timu lakini pia umeweka historia mpya kwa kuziunganisha timu hizo kubwa nchini na kuondoa dhana ya uadui ambayo ilianza kujengeka. [23]
dhidi 
Akizungumza nje ya mahakama, Sendeka aliwashukuru wote waliofika mahakamani hapo na kuwataka kuliacha suala hilo kwenye vyombo vya sheria ili vifanye kazi yake na kuwatahadharisha dhidi ya maneno machafu na kuwatuhumu watu kuhusu suala hilo pamoja na kuacha kufanya maandamamo wakati wanapotoka mahakamani hapo. [24]
dogo 
Yanga iliwasajili wachezaji hao kutoka Tusker wakati dirisha dogo la usajili likiwa tayari limefungwa hivyo Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuiwekea ngumu kutowatumia wachezaji hao kwenye michuano yoyote. [25]
don 
Suti hilo! Yaani suruali ilikuwa mfano wa ‘don’t touch’ na tai ilikuwa inajikunja kutokana na kutumika miaka si chini ya ishirini. [26]
duni 
Kwa hiyo tukiwa wadau muhimu wa elimu tunona kwamba, wanafunzi hao dhaifu ambao hufundishwa katika mazingira duni na walimu wasio na uwezo, ndiyo sababu za msingi za kushuka kwa ufaulu, hivyo tatizo hilo litafutiwe ufumbuzi. [27]
dunia 
Alisema uzoefu na ukomavu wa wachezaji katika mashindano mbalimbali utawapa changamoto zaidi hivyo kuweza kushiriki kombe la dunia. [28]
duniani 
Baada ya teknolojia ya kompyuta na internet kusambaa duniani, nchi nyingi sasa zinatumia kompyuta na internet katika kutoa huduma zake mbalimbali kwa wananchi. [29]
es 
Mbunge Sendeka anatetewa na mawakili, Michael Ngalo wa kampuni ya Ngalo and Company yenye ofisi zake jijini Dar es salaam na Arusha akisaidiwa na wakili wa kujitegemea, Neema Mtayangula huku upande wa mashitaka unaongozwa na wakili Hashimu Ngole akisaidiwa na wakili Augustino Kombe. [30]
familia 
Lakini badala yake wameyatupa kiasi kwamba asilimia 67 ya wanafunzi wengi wao kutoka familia masikini wanatarajiwa kukosa elimu ya juu kwa sababu ya umasikini wao. [31]
fulani 
Kwa kawaida mtu unapoumwa, mwili unakuwa umekosa viasili fulani vinavyohitajika mwilini. [32]
hadi 
Prof Maghembe alisema, hadi kufikia juzi jioni wanafunzi wengi walikuwa wametimiza masharti yote waliyopewa na wameshaitwa kuendelea na masomo kutegemeana na ratiba ya vyuo husika. [33]
haina 
Kilango alisema wamebaini kwamba TCRA haina wataalam wakutosha katika suala la mawasiliano na ndiyo maana hawajaingia kwa undani zaidi katika kutambua kipato cha wawekezaji hao. [34]
haja 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Habib Nyundo, alikiri kuepo kwa upungufu na changamoto katika sheria hiyo na kwamba kuna haja kubwa ya kuifanyia marekebisho. [35]
hapa 
WAFANYABIASHARA wa nishati ya mafuta wa mjini hapa wamebuni njia mpya ya kuuza nishati ya mafuta kwa bei ya juu ikilinganishwa na bei inayosisitizwa na serikali kupitia mamlaka mbalimbali. [36]
hatari 
Mashimo mengine hutokana na watu kutafuta maji wakati wa kiangaz na hivyo kuwa hatari wakati mvua zinapoanza. [37]
hatua 
Alisema pamoja na hatua za kidhamu, walimu waliodanganywa pia watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka. [38]
hii 
Tangu mapema wiki hii, kumekuwa kukiripotiwa habari kadhaa kuwa Ole Sendeka amepandishwa kizimbani kwa madai ya kufanya kosa hilo, lakini suala lake lilikuwa polisi hadi jana wakati mbunge huyo alipofikishwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha akikabiliwa na shitaka la shambulio la kudhuru mwili. [39]
hisa 
Rais alisema kuwa maamuzi yote makubwa kuhusu reli hiyo, lazima yafanywe kwa kuishirikisha Serikali ya Tanzania ambayo inamiliki asilimia 49 ya hisa za TRL. Kampuni ya RITES ya India inamiliki asilimia 51 ya hisa katika kampuni hiyo. [40]
hivi 
Wakati huohuo, Waziri Chikawe amesema serikali itatoa taarifa kuhusu ufumbuzi wa suala la kuwepo au kutokuwepo kwa Kadhi Mkuu hivi karibuni. [41]
hospitali 
Hata hivyo, Kikao hawakatazi watu kutumia dawa za hospitali: "Dawa za hospitali zitumike tu pale inapolazimika, lakini siyo kila mara. [42]
huenda 
Inachokupasa ufahamu kuwa kuziba kauli katika suala ambalo limekuudhi hupelekea madhara makubwa mbeleni katika mahusiano yenu na huenda ikaathirika afya yako. [43]
hujui 
Kwa kuwa hujui aliyekuletea ana nia gani na mumeo. [44]
huko 
Taifa hili la Kiislamu linaloongozwa na Rais Hamid Karzai, linalokadiriwa kuwa na jumla ya watu milioni 32.7, ikiwemo wengine milioni 3.5 wanaoishi kama wakimbizi huko ughaibuni, lilianza kuvamiwa na Himaya ya Median (Iran) iliyojipanua na kuingia katika eneo la nchi hiyo miaka 700 kabla ya kuzaliwa Kristo. [45]
huku 
MAfuvu hayo yamechukuliwa na kuhifadhiwa kwenye kituo cha polisi cha mkoa jana huku polisi hao wakiwa na vikao kadhaa vya ndani kujadili suala hilo. [46]
huo 
Uchunguzi huo, ulioendeshwa kwa muda wiki moja umebaini kuwa lita moja ya ya petroli inauzwa kati ya Sh 1500 na 2000 hadi Sh 2200 kwa lita, tofauti na bei halisi iliyoandikwa katika baadhi ya vituo hivyo ya Sh 1274 kwa lita moja na hivyo kusababisha malalamiko kutoka kwa madereva teksi, daladala na watumiaji wengine. [47]
hupewa 
Hadi sasa hakuna dawa ya hospitalini inayotibu kisukari, sana sana wagonjwa hupewa dawa maalumu ya kuongeza insulini mwilini ili sukari iweze kuchujwa. [48]
husika 
Ni matarajio ya serikali kwamba, wanafunzi watarejea vyuoni kwa kuzingatia taratibu zilizotangazwa na vyuo husika. [49]
huu 
Akisomamewa hati ya mashitaka mahakamani hapo mbele ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, James Kalayamaha, mbunge huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 9 mwaka huu majira ya saa 10:30 wilayani Monduli wakati alipompiga Mallya kibao upande wa shavu la kulia na kumsababishia maumivu mwilini mwake. [50]
huwa 
Kwa mfano, mtu anayeumwa tezi la shingo (goitre), huwa amepungukiwa na madini joto yaliyomo kwenye chumvi," anasema Kikao. [51]
ikawa 
Inaweza hiyo ikawa sababu, lakini si kubwa kiasi hicho. [52]
ila 
Ni kweli tuna mpango wa kuwarudisha Tusker kwa mkopo na mazungumzo tayari yameanza ila yapo katika hatua ya awali tutaendelea kuwafahamisha yakikamilika" alisema Madega. [53]
ile 
Kutokana na ugumu wa masharti hayo na kwa kuwa mkazo wa uongozi wa UDSM uko katika kupata pesa kwa asilimia ile ambayo kila mwanafunzi anapaswa kutoa, ni asilimia 33 tu ya wanafunzi wote wa shahada ya kwanza waliotekeleza na ambao kimsingi ndio wataruhusiwa kuingia darasani kuanzia Jumatatu. [54]
iliyopo 
Lakini pamoja na maelezo hayo mazuri, bado kuna walakini katika utekelezaji wa mapendekezo hayo kutokana na kasumba iliyopo ya kusubiri hadi hali iwe mbaya ndipo hatua zichukuliwe. [55]
ina 
Hapana shaka Yanga leo ina kila sababu ya kuibuka na ushindi kutokana na silaha zake zote zilizokuwa timu ya Taifa kurejea tayari kwa mchezo huo licha ya kuwa JKT Ruvu nayo si timu ya kubeza. [56]
ini 
WAKATI serikali na wadau mbalimbali wakihangaika kutafuta dawa za magonjwa sugu kama vile kisukari, pumu, moyo, ini, malaria na mengineyo, kiasi cha kuwafanya wengine kwenda kutibiwa nje ya nchi, imeelezwa kwamba chakula hiki tunachokula kila siku ni dawa ya magonjwa hayo. [57]
ipo 
Chikawe alisema kuwa mbali na suala hilo serikali ipo katika mchakato wa kutoa waraka wa serikali namba moja kuhusu marekebisho ya Sheria ya Ndoa na Sheria ya Mirathi na kwamba wizara yake imekuwa ikifanya kazi kutekeleza matamko ya ilani ya Chama Cha mapinduzi katika sekta ya sheria. [58]
iwe 
Matatizo hayo si tu kuwa yanawakwamisha wakulima, bali pia juhudi za serikali za kufufua kilimo chenye tija katika kukuza uchumi wa taifa, hivyo tunaomba juhudi zifanyike kuboresha huduma hiyo ya bandari na iwe kwa mazao mengine ambayo tunaamini yanakumbana na tatizo hilo. [59]
jengo 
Kumekuwa na hamaki kubwa ya kuhimiza utafiti na kutaka hatua zichukuliwe pindi inapotokea jengo kuporomoka lakini baada ya muda mfupi kupita, shime hiyo husahaulika. [60]
jirani 
Alisisitiza kuwa ni muhimu kwa Tanzania kuendelea kuwa na njia za reli zinazoungana na za nchi nyingine za jirani. [61]
jua 
Kama wewe ni mmoja ya wale watu ambao huchagua kunyamaza ama kununa kuliko kutatua tatizo jua wewe ni chanzo cha kuzidi kwa matatizo mbeleni. [62]
juu 
Tatizo la uchangiaji wa elimu ya juu lilisababisha migomo ya wanafunzi sehemu mbalimbali mwishoni mwa mwaka jana na kusababisha serikali kufunga vyuo vyake vikuu saba baada ya wanafunzi kugoma kuingia darasani wakipinga sera ya uchangiaji kwa madai kuwa inabagua. [63]
kadi 
Katika hatua nyingine, Salim Said, anaripoti kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema haina uwezo wa kudhibiti kadi (laini) za simu za mkononi kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili. [64]
kali 
Mara nyingi ini huathirika hasa baada ya mtu kunywa sumu au kutumia dawa nyingi kwa muda mrefu au kutumia sana pombe kali. [65]
kansa 
Akieleza magonjwa ambayo huyatibu katika kituo chake, Kikao anasema: "Ninatibu ugonjwa wa ini, kifafa, kisukari, kansa na mengineyo. [66]
karne 
Ukiachilia mbali himaya mbalimbali zilizokuwa zikipigana kikumbo kuitwaa Afghanistan, karne ya 19 ilishuhudiwa mapambano mengi zaidi kutokana na mataifa yenye nguvu kujikita zaidi katika kujipanua na kulinda maslahi yao katika Asia ya Kati. [67]
kasi 
Kocha mkuu wa timu hiyo, Dusan Kondic anaweza kapanga kikosi imara kukabiliana na mafande hao wenye kasi, nguvu na wanaomiliki mpira vema katika kuhakikisha anavuna pointi tatu muhimu. [68]
kata 
Uchunguzi uliofanywa na vyombo vya habari kwa muda mrefu na ambao unaendelea kufanywa kila siku kwa kufika shuleni kushuhudia hali halisi, unaonyesha shule nyingi hasa zilizoanzishwa kisiasa chini ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) yaani sekondari za kata, ndizo zinaongoza kwa matokeo mabaya. [69]
kemikali 
Vyakula tunavyokula kila siku ni dawa, na kama watu wangefahamu siri hii kusingekuwa na haja ya watu kutumia dawa za kemikali zinazotolewa hospitalini. [70]
kidogo 
Hadi awamu ya kwanza ya programu hiyo ilipomalizika mwaka jana, mafanikio yaliyopatikana na kidogo. [71]
kigaidi 
Kwa sasa, Majeshi ya Umoja wa Kujihami wa nchi za Magharibi (Nato) yanakalia sehemu kubwa ya nchi hii kwa madai ya kutaka kuyaondoa makundi ya kigaidi ya Al – Qaeda. [72]
kikubwa 
Waheshimiwa wabunge suala la kudhibiti kadi za simu ni gumu sana kwa sababu halijawekewa sheria na serikali inajipatia kipato kikubwa kutoka kwa watumiaji," alisema Mungy. [73]
kila 
Hakimu aliikubali hoja hiyo kwa masharti ya kudhaminiwa na watu wawili ambao kila mmoja anatakiwa adhamini kwa Sh500,000 na kuhakikisha mtuhumiwa anafika mahakamani pindi atakapohitajika. [74]
kile 
Kutoa vibali kabla ya kuangalia kwa makini nini kinachotakiwa kujengwa ni hatari, kwani kwa kufanya hivyo kunatoa mwanya kwa wajenzi wasiokuwa waaminifu kufanya kile wanachotaka kwa kutumia ujanja ujanja," anasema Jumaa. [75]
kina 
JESHI la Polisi mkoani Kagera linaendelea na uchunguzi wa kina kuwabaini watu waliohusika na mauaji ya mtoto wa miaka sita, Michael Petro ambaye alikuwa albino. [76]
kocha 
Shadrack Nsajigwa anacheza kulia huku kushoto kocha akitarajia kumchezesha yoyote kati ya Nurdin Bakari, Abuu Mtiro kutokana na Amir Maftah kuumia katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Zesco ya Zambia juzi. [77]
kuandika 
BFT ilifutiwa uanachama na shirikisho hilo la Kimataifa baada ya baadhi ya viongozi kuandika barua ya kujiuzulu kwa viongozi wake kitu ambacho kilipingwa na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo na hivyo kupelekea kufutiwa uanachama hadi hapo watakapochagua viongozi wengine ndani ya mwezi mmoja. [78]
kuanguka 
Athari kubwa ya ugonjwa huu ni mtu kuanguka kila mara. [79]
kuimba 
Kweli wanaweza kuingia hivihivi? Kweli wataingia kama milolongo ya vijana wanaotafuta nafasi moja ya Ustaa wakati ambapo hata wenzao wa mitaani wanawacheka wakijaribu kuimba. [80]
kuishi 
Hiyo itasaidia kuwadumaza wadudu wa malaria, kwa sababu wadudu hao hawawezi kuishi kwenye mwili wenye maji mengi. [81]
kuitwaa 
Historia ya taifa hilo kuendelea kuvamiwa kwa sababu za kujiimarisha kivita kwa mataifa yenye nguvu, inaonyesha kuwa mataifa mengine mengi yalijitokeza kutaka kuitwaa nchi hiyo. [82]
kuja 
Kituo changu hakina mashine za kuwapimia wagonjwa, hivyo hulazimika kwenda hospitali kwana kabla ya kuja hapa. [83]
kujengwa 
Meya wa Manispaa ya Ilala, Abuu Jumaa, anasema kuwa Kamati ya Vibali na Ujenzi ya Manispaa ya Ilala inapaswa kusimamisha utoaji wa vibali hivyo kiholela bila ya kuangalia kitu kinachotakiwa kujengwa kwani kwa kufanya hivyo ni kuendelea kuhatarisha maisha ya watu. [84]
kujua 
Hayo yaliibuka jana katika mjadala wa semina ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, baada ya wabunge kutaka kujua hatua zinazochukuliwa na serikali, kudhibiti matumizi mabaya ya kadi hizo. [85]
kukaa 
Umoja wa Wazalishaji wa Kahawa nchini (TCA) umedai kwamba, kutokana na ucheleweshaji huo, katika kila magunia 300 ya kahawa, 100 hupotea kwa kuoza kutokana na kukaa muda mrefu ndani ya kontena yakisubiri kusafirishwa. [86]
kumaliza 
Kilinda alisema wameuanza mzunguko huo kwa kasi na wanataka kumaliza kwa kazi hivyo hawaihofii timu yoyote watakayokutana nayo. [87]
kumsikiliza 
Ongeza umakini katika kumsikiliza. [88]
kuna 
Ila kuna watu wanataka tupigane, hivyo tumieni busara zenu ili sheria hii iweze kuwa nzuri," alisisitiza Bendera. [89]
kuona 
Alisema wabunge wanataka kuona kuwa mwananchi wote wakiemo wa maeneo ya vijijini, wananufaika na huduma za simu kuliko ilivyo sasa. [90]
kupanda 
Mratibu wa pambano hilo Abdul Kipenga alisema maandalizi ya pambano hilo yamekamilika na kinachosubiriwa ni mabondia kupanda ulingoni kupambana. [91]
kupewa 
Pia alisema Chama cha Tenisi, kupewa hadhi ya kuwa mwenyeji wa mashindano yaliyomalizika, kriketi, riadha kwa kuwasilisha mikakati yao kwa amendeleo ya mchezo wa riadha pamoja na chama cha kuogelea. [92]
kusikiliza 
Epuka dhana na kusikiliza maneno ya watu. [93]
kutibu 
Mtaalamu wa tiba za vyakula wa kituo cha tiba ya chakula cha Kikao Natural Food Therapist Clinic (KNFTC), kilichopo Turiani mkoani Morogoro, John Kikao anaeleza jinsi chakula kinavyoweza kutibu magonjwa hayo. [94]
kwani 
Kondic alisema anauchukulia uzito mkubwa mchezo huo kwani anachotaka ni kutoka na pointi zote uwanjani. [95]
kwao 
Katika hatua nyingine Madega alisema wachezaji Mike Baraza, George Owino ambao waliokuwa na timu ya taifa ya Kenya kwenye michuano ya Chalenji walitarajia kuwasili nchini jana usiku kutoka kwao tayari kwa mchezo wa leo dhidi ya JKT Ruvu. [96]
kweli 
Kung’oa sehemu yoyote ya reli ni kutuambia kuwa hamuijali nchi hii na kwa kweli hatuwezi kuwa na washirika wa namna hiyo. [97]
la 
KATIKA tukio lisilo la kawaida nchini, mafuvu 40 ya vichwa vya watu yamegundulika yakiwa yamefukiwa ndani ya pango lililo chini ya mti wa mbuyu, kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga. [98]
leo 
Hata hivyo, baada ya Maghembe kutoa taarifa hiyo alikataa kujibu maswali ya waandishi wa habari kwa kuahidi kuwa atakuwa tayari kufanya hivyo leo. [99]
ligi 
Yanga inayoongoza ligi hiyo inahitaji kushinda michezo mitano tu ili itangaze ubingwa mapema kabla ya ligi kuisha. [100]
maalum 
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alisema hayo jana alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano maalum aliouitisha kuelezea mafanikio ya wizara yake katika miaka mitatu ya serikali ya awamu ya nne. [101]
mabaki 
Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, ACP Shaibu Ibrahim alisema jana kuwa mafuvu hayo yalikutwa pamoja na mabaki mengine ya miili ya binadamu. [102]
madaktari 
Tunakabiliwa pia na tatizo la vifaa na madaktari. [103]
madhubuti 
Vile vile sababu nyingine ambayo inasababisha teknolojia hii muhimu kutotumika ipasavyo ni pamoja na kukosekana kwa sera na mipango madhubuti ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama), katika taasisi za serikali. [104]
maelezo 
Alisema tayari maelezo ya mama wa marehemu na baba huyo yamechukuliwa na kwamba mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu na jamaa wa marehemu kwa ajili ya mazishi, wakati polisi ikiendelea na upelelezi. [105]
magari 
Pamoja na hayo, alisema kuna umuhimu wa kuachana na mtindo wa viongozi wa serikali kununua magari ya kifahari yanayogharimu fedha nyingi, ambazo zingeweza kusaidia kufanikisha harakati za kuboresha kilimo nchini na hasa kukabiliana na kilimo cha jembe la mkono ambacho kimepitwa na wakati. [106]
mahusiano 
Tunahitaji mahusiano na nchi nyingine. [107]
majengo 
Naye mwenyekiti wa Simba Hassan Dalali aliiomba TBL kuharakisha baadhi ya makubaliano yaliyomo kwenye mkataba likiwemo suala la usafiri na ukarabati wa majengo ya klabu hizo. [108]
makundi 
Wanafunzi hao walikuwa wanapinga utaratibu wa sasa wa kuwatenga kwenye makundi, wengine kupewa mikopo kwa asilimia 100 na wengine hadi asilimia 20 tu. [109]
mara 
Kombani alisema mara baada ya kupokea madia hayo, serikali ilifanya uhakiki na kubaini kuwa walimu walio wengi walighushi nyakara mbalimbali kuidanganya na kujipatia fedha wasizostahiki. [110]
matokeo 
Moro iliwashangaza mashabiki wengi kwenye mechi dhidi ya Azam Jumatatu baada ya kuibuka na kusawazisha goli mbili na kuyafanya matokeo kuwa sare. [111]
mawazo 
Haya ni mawazo ya kushangaza kabisa. [112]
mazao 
Harakati za Pinda zisiishie jukwaani KATIKA harakati za kuboresha kilimo nchini, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameendelea na kampeni yake ya kufufua uzalishaji wa mazao mbalimbali kwa kuwataka viongozi wote wa serikali ‘kujinyonga’ kwa lengo la kumsaidia mkulima wa kawaida. [113]
mazuri 
Aidha Kipingu alisifia vyama vya michezo mbalimbali ambayo imeweza kufanya vizuri kwa mwaka uliopita na amesema ili kuboresha zaidi michezo hapa nchini ni pamoja na kujenga mahusiano mazuri ya mipango ya pamoja kwa viongozi wa michezo wa Bara na visiwani. [114]
mbali 
SERIKALI imetupilia mbali' madai ya kwamba walimu wanaidai Sh 21 bilioni zinazotokana na stahili mbali'mbali. [115]
mganga 
Mzee Kikao alianzaje kuwa mganga?: "Kabla ya kuanza shughuli za uganga kwa kutumia vyakula, nilikuwa mwalimu wa shule za msingi hapa wilayani Turiani. [116]
mgumu 
Sisi hatuiogopi timu yoyote na wala hatuidharau yoyote tunachotaka ni kuingia uwanjani na kusomba pointi zote, mchezo dhidi ya Yanga leo utakuwa mgumu sana lakini tutawafunga na zaidi tunataka kulipiza kisasi," alisema. [117]
mifuko 
Badala ya kukaa na kufurahia kutoboka kwa mifuko na kupasuka kwa suruali yenye mifuko, kila mara wanatafuta kazi zingine za kufanya. [118]
mimi 
Kwa sasa mimi sina taarifa kuhusu hilo na kwanza ofisini kwangu hatuna utaratibu wa kutisha watu. [119]
minne 
Ripoti hiyo ya miaka minne iliyopita inaonyesha kuwa Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya 127 mwaka 2005 hadi 147 mwaka jana. [120]
mkutano 
Akizungumza na katika mkutano wa watumishi wa Jiji la Dar es Salaam Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) Celina Kombani, alisema kuwa madai hayo si halali. [121]
mkuu 
Hata hivyo Naibu katibu mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT),Ezekiah Oluoch, alikanusha kauli ya waziri Kombani na kwamba lengo la waziri ni kutaka kupotosha umma. [122]
mwishiwa 
Si kila mtu anaweza kuchekesha? Kwa nini tusifanye na sisi?’ ‘Kweli kabisa mwishiwa Supu. [123]
na 
Matukio kama hayo yamekuwa yakiripotiwa kwenye nchi zilizowahi kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini Jeshi la Polisi limeeleza kuwa limegundua mafuvu hayo katika kijiji cha Mayangi kilicho katika Kata ya Ukenyenge tarafa ya Negezi wilayani Kishapu. [124]
nani 
Nakuambia nani hajui lakini yeye anakunja manoti yake safi wakati sisi tunakaa tunaangalia meza tupu. [125]
naona 
Kabla sijaeleza sababu ambazo naona zinasababisha kushuka kwa e-government nchini, labda nitaje faida za mpango huu. [126]
naye 
Kamanda Salewi alisema baada ya kufanikiwa kuvunja mlango, walimfunika kwa blanketi mama wa mtoto huyo, Grace Philemon, 38, na baba anayedaiwa kuwa ni mpenzi wa mama huyo na baadaye kumchukua mtoto huyo na kutoka naye nje, ambako walimuua na kumkata mikono yote miwili na miguu na kutoweka nayo na kuelekea kusikojulikana. [127]
ndio 
Sisi ndio wamiliki wa reli hiyo kwa asilimia 100. Nyie tumewaajiri tu kama waendeshaji tu," amesisitiza Rais Kikwete katika mkutano huo uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam. [128]
ndiye 
Alisema kuwa anamfahamu na kumheshimu Jaji Warioba kwa kuwa ndiye alimpokea na kufundisha kazi alipojiunga na Wizara ya Sheria mwaka 1975, wakati huo Warioba alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. [129]
ndugu 
Kingorwila, Abdulatifu Twaribu ambaye alidai ni ndugu ambaye ni mmiliki wa kituo cha MT Mohamed Twaribu alisema wafanyakazi wao wanafanya ujanja wa kuuza mafuta kwa bei ya juu ikilinganishwa na bei halisi waliyokuwa wameiandika katika mabango. [130]
ngumi 
BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) leo linatarajia kukutana na uongozi wa Shirikisho la ngumi za ridhaa BFT kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusiana shirikisho hilo ikiwemo kutoa maelekezo yaliyotolewa na TOC kutoka Shirikisho la Kimataifa la ngumi kuhusiana na uongozi usiotambulika wa shirikisho hilo. [131]
ni 
Hata hivyo, idadi ya mafuvu hayo ni kubwa. [132]
nia 
Mataifa haya yalianza kuivamia nchi hii miaka 700 kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo, yakiwa na nia tofauti, lakini kikubwa zaidi kujilinda kivita kutokana na nchi hiyo kuwa kiungo cha mataifa ya Asia ya Kati, sehemu ya India na Mashariki ya Kati. [133]
nini 
Kuna baadhi ya wasomaji wataanza kujiuliza e-government ni nini? Hizi ni huduma ambazo zinatolewa na serikali kwa wananchi wake kwa njia ya kompyuta ambayo imeunganishwa katika mtandao wa internet. [134]
nyama 
Kuna mambo mbali mbali yanayosababisha ugonjwa wa kansa ikiwamo ulaji wa nyama kwa wingi, sukari nyeupe na mafuta ya wanyama. [135]
nyeti 
Aidha, wabunge wametakiwa kutumia busara na nafasi zao kuweza kujadili kwa makini rasimu hiyo watakapopelekewa kwa kuwa suala la habari ni nyeti katika usalama wa taifa. [136]
nyingi 
Tunaheshimu mchango wa TBL katika maendeleo ya soka nchini, lakini ningependa kushauri watakapoboresha mkataba waweke programu maalum kwa ajili ya kuinua vipaji vya vijana ambao watazitumikia timu hizi badala ya kutumia fedha nyingi kwenye usajili," alisema Nyamlani. [137]
nyongo 
Ugonjwa huo pia huandamana na kuathirika kwa bandama na nyongo. [138]
oa 
Miongoni mwa mipango hiyo ni kujaribu kupata mkopo mkubwa wa kuendesha shughuli za reli hiyo bila ridhaa ya serikali, mipango ya kuacha kutoa huduma kwenye baadhi ya vipande vya reli kwa madai kuwa, havina faida, hali ya usalama wa reli yenyewe, maombi ya TRL kuzidi kupunguziwa kodi; na hata kutaka mipango ya kung’oa kipande cha reli kati ya Tanzania na Kenya kwa madai kuwa hakina faida. [139]
ovyo 
Hatuwezi kufanya jambo la ovyo kiasi hicho. [140]
rais 
Kuhusu hisia za kutaka kung’oa reli kwa sababu ya kutopata faida, rais alisema: "Hili litachukuliwa kama hujuma. [141]
rasimu 
SERIKALI imesema rasimu ya marekebisho ya Sheria namba 3 ya mwaka 1976 ya Magazeti ipo jikoni na inatarajiwa kufikishwa bungeni kujadiliwa mara itakapokamilika. [142]
reli 
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete, jana aliicharukia Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), akiitaka kuacha kuchukua maamuzi makubwa katika uendeshaji wa usafiri wa Reli ya Kati bila kuishirikisha serikali, akisema "reli si mali ya TRL, bali ni ya serikali ya Tanzania na Watanzania. [143]
ridhaa 
Alisema kwa wale wanafunzi ambao hawakujaza kabisa fomu za maombi ya kudahiliwa upya watakuwa wameamua kwa ridhaa yao wenyewe kutokurejea vyuoni. [144]
ripoti 
UTAFITI uliofanywa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa (UN) kuhusiana na masuala ya e-government na ripoti yake kutolewa mwaka jana, Tanzania imeshuka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mwaka 2005, ripoti hiyo ilipotolewa mara ya mwisho. [145]
saa 
Alisema tukio polisi walibaini mabaki hayo ya binadamu Januari 13 wakati walipoenda kwenye eneo hilo majira ya saa 10:35, ingawa taarifa yake haikueleza kiini cha kwenda eneo la tukio kufanya uchunguzi uliosababisha kugundulika kwa mabaki hayo. [146]
sana 
BAADA ya kuripotiwa sana kwamba angefikishwa mahakamani, hatimaye mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka jana alipandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kumshambulia mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) mkoani Arusha, James Ole Milya. [147]
sare 
Akizungumza na Mwananchi jana jiji Dar es Salaam katika uwanja wa Shule ya sekondari ya Benjamini Mkapa alisema pamoja na sare katika mechi zote, bado viwango vya timu hizo kubwa hapa nchini ni tofauti na Zesco. [148]
sasa 
Lakini sasa, wale ambao wanaamini kuwa hawana uwezo wa kuchangia wamepewa mwanya wa kukata rufaa kwa waziri, uamuzi ambao unaonyesha kuwa serikali imelegeza masharti. [149]
si 
Iwapo si mauaji ya watu wengi, mabaki hayo yanaweza kuwa yanatokana na imani za watu wengi kuwa wakoloni walipoondoka waliacha madini, na hasa rubi, chini ya miti ya mibuyu, imani ambayo hufanya watu wengi wanaoishi kwenye maeneo yenye madini kuchimba mashimo marefu karibu na mibuyu kusaka vito hivyo. [150]
sifa 
Vyombo vya habari vimebaini shule takriban zote za kata nchini, zinakabiliwa na matatizo kadhaa; hazina walimu wenye sifa na waliopo, wengi wao waliajiriwa kisiasa, hivyo wanaingia darasani kama walimu lakini si walimu. [151]
sisi 
Na kama unataka msimamo wetu kuhusu maombi ya mkopo bila kutushirikisha, sisi basi ni kwamba hatuukubali mkopo huo. [152]
siyo 
Sisi kama Serikali ya Tanzania ni mbia-mwenza na siyo mshirika mdogo katika makubaliano ya kuendesha reli hii. [153]
sumu 
Dawa za kemikali ni sumu kwa hiyo mtu akizitumia sana huleta madhara makubwa mwilini ikiwamo kuharibu ini. [154]
tena 
Semina hiyo inaendelea tena leo katika ukumbi wa tume ya haki za binadamu na utawala bora jijini hapa ambapo mjadala wa sheria hiyo na utendaji wa magazeti utaendelea. [155]
tiba 
Hii ni tiba muafaka ya usumbufu, urasimu, rushwa na gharama za uendeshaji wa shughuli za serikali. [156]
tu 
Alisema nyaraka hizo ni pamoja na vyeti vya ndoa vilivyoonyesha mikoa waliyodai kuwa wametoka ili tu wajipatie fedha. [157]
ubora 
Khamis Dogo anayeegesha teksi katika kituo cha Kosovo na Bob Ommy walilalamikia bei na kufafanua kuwa ubora wa nishati hiyo, mafuta yanayouzwa hayana ubora unaotakiwa kutokana na kuchanganywa na mafuta ya taa. [158]
ufaulu 
MAPEMA mwaka jana, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ililiambia Bunge ilivyosikitishwa na kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa wanafunzi na kwamba, ilikuwa inafanya utafiti kujua sababu zake. [159]
uharibifu 
Kuhusu usalama wa reli, Rais Kikwete alisisitiza: "Kuna uharibifu mkubwa katika baadhi ya maeneo ya reli. [160]
uhusiano 
Akijibu maswali ya wabunge hao, Ofisa uhusiano wa TCRA, Innocent Mungy, alisema, suala hilo ni gumu kwa kuwa halijaandaliwa mazingira. [161]
ujao 
Alisema leo watakutana na viongozi wote wa BFT kwa ajili ya kuwapa taarifa hiyo rasmi ya IBA na wao kama viongozi wana wajibu wa kutoa mapendekezo yao juu ya uongozi ujao na ulipita ikiwemo makabidhiano ya mali za chama na Januari 31 kutakuwa na mkutano na wanachama wote kwa ajili ya kuzungumzia mchakato mzima uliopo katika shirikisho hilo. [162]
ujenzi 
Tume hiyo ya kuchunguza ujenzi wa maghorofa katika Jiji la Dar es Salaam, iliundwa baada ya kuanguka kwa jengo moja huko Chang'ombe na kusababisha kifo cha mtu mmoja. [163]
umma 
Profesa Maghembe alisema hayo alipokuwa akitoa taarifa ya kufunguliwa kwa vyuo vikuu vya umma vilivyofungwa Novemba mwaka jana kutokana na migomo. [164]
upya 
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Profesa Maghembe alisema kuwa watakaokata rufaa itabidi wafanyiwe tathmini upya. [165]
usanii 
Ni kupoteza muda kabisa hata watumie usanii namna gani. [166]
utafiti 
Kuhusu suala la kuwepo au kutokuwepo Kadhi Mkuu, utafiti tayari umefanyika na umekabidhiwa serikalini. [167]
uti 
Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Cheju, Zanzibar juzi baada ya kukagua kilimo cha mpunga katika eneo hilo, alifahamisha kuwa anaposema viongozi wajinyonge anamaanisha kwamba, wabadilike na kuacha maneno badala yake wajitoe kikamilifu kufanikisha azma ya serikali katika kufufua kilimo, vinginevyo kilimo hakiwezi kuwa uti wa mgongo wa taifa hili na mkombozi wa wanyonge ambao kazi yao kubwa ni kulima. [168]
utoaji 
Alibainisha kuwa kuna tatizo kubwa katika suala la utoaji wa vibali kwa kufuata masharti ya vibali vya ujenzi. [169]
uwanja 
Wakati Yanga ikicheza leo, mahasimu wao, Simba watashuka uwanjani kesho kucheza na Polisi Morogoro kwenye uwanja huo. [170]
vifaa 
Mbali ya ukosefu wa walimu shule hizo zimejengwa chini ya kiwango, hazina majengo yaliyokamilika kwa ajili ya mabweni, ofisi za walimu, maktaba, maabara na madarasa pamoja na vifaa na huduma nyingine muhimu kwa wanafunzi. [171]
vijana 
SHIRIKISHO la soka Tanzania, TFF, limeishauri Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuweka programu za kuinua vipaji kwa vijana kwa klabu za Simba na Yanga ili kupunguza gharama kubwa za usajili katika timu hizo. [172]
vile 
Hali ya usalama wa reli inaonekana kuwa hatarini kwa sababu nyie mnaonekana kama vile hamjali. [173]
vipimo 
Hospitali zingebaki tu na kazi za vipimo na ushauri, lakini vyakula hasa vya mimea ni dawa za magonjwa sugu. [174]
vituo 
Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa habari katika vituo mbalimbali vya mafuta mjini hapa, umebaini petroli inauzwa kwa bei ya juu tofauti na bei halisi wanayoiandika katika mabango ya vituo vya mafuta. [175]
vocha 
Ndugu wajumbe hakuna maendeleo yasiyo na madhara yake lakini pia serikali inajikusanyia mapato makubwa katika kila vocha inayonunuliwa. [176]
vyao 
Alisema wameamua kuwarudisha wakacheze Tusker kwa mkopo ili waweze kulinda viwango vyao ambavyo vingeweza kushuka endapo wasingecheza mpira wa ushindani kwa muda mrefu. [177]
vyenu 
Hapa nawalinda kabisa na vijisenti vyenu. [178]
wagonjwa 
Mpaka sasa nimeshatibu zaidi ya wagonjwa 10 wa ugonjwa wa ini. [179]
waishiwa 
Lo! Mimi nilidhani waishiwa watacheka na kuendelea na kujiliwaza kwao. [180]
wake 
Badala yake imesema katika uhakiki wake, serikali imeibaini kuwa madai halali ya walimu hao ni Sh 9 bilioni. [181]
wala 
SERIKALI imesema haina taarifa za kuchunguzwa na mpango wa kufikishwa mahakamani kwa waziri mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba na kwamba wala haihusika na suala hilo. [182]
wanachuma 
Lakini wakati huu wengine wanachuma hivi hivi. [183]
wanatoka 
Maafande hao wa JKT watakuwa wakiwatumaini Bakari Kondo, Sostenes Manyasi, Haruna Adolph,Rashid Matambo, George Minja na Kessy Mapande kuhakikisha Yanga haifurukuti mbele yao na wanatoka na pointi tatu muhimu. [184]
wao 
Kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na watoto wao hasa katika kipindi hiki cha mvua, akitaka wasiwaruhusu kwenda kuchota maji peke yao. [185]
wazee 
Inadaiwa kuwa tukio hilo lilitokea wakati Ole Sendeka pamoja na Mallya wakiwa katika semina ya wazee wa kimila iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Monduli. [186]
wenu 
Wakati mwingine unaweza kukuta jambo kubwa mliligombania linakuwa dogo kutokana na uelewa wenu kwa kila moja wenu. [187]
wenye 
Alisistiza kuwa, wao kama wabunge wenye dhamana kubwa kwa wananchi, hawapaswi kuachia mambo nyeti yaende ovyo ovyo. [188]
wenzangu 
Waishiwa wenzangu. [189]
wote 
Wanafunzi ambao hawataweza kabisa kutimiza sharti la kulipa mchango wao wote wa gharama za masomo kwa sababu za msingi, wanashauriwa kukata rufaa kwa maandishi kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili uwezo wao wa kuchangia utathminiwe upya," alisema Prof Maghembe akisoma taarifa yake kwa vyombo vya habari. [190]
yako 
Hakimu alikubali na kusema masharti ya dhamana yako wazi na hivyo wadhamini kujitokeza, akiwemo meneja wa Bonite mkoani Arusha, Mwangole Segule ambae alipingwa kuwa mdhamini kutokana na hati yake kukosa muhuri wa uongozi wa kampuni hiyo. [191]
yenu 
Nyie hamna haki na hamwezi kutoa maamuzi yenu pekee bila kuishirikisha serikali. [192]
yetu 
Reli ni mali yetu. [193]
yeye 
Waziri Chikawe alisema kuwa taarifa zinazomhusu yeye kuzungumzia Jaji Warioba zilizoandikwa na gazeti moja la kila siku (si Mwananchi) kuwa si za kweni na zimejaa ushabiki. [194]
za 
Pia hatukuweza kufahamu mifupa na mafuvu haya na ya watu wa jinsia gani lakini tumeyahifadhi kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kubaini umri na jinsia za watu hao," alisema. [195]
zamani 
Warioba amekuwa akibashiriwa na vyombo vya habari kuwa angefikishwa mahakamani kuhusu kampuni ya Mwananchi Gold ambayo inahusishwa na usafidi na ubashiri ulipozidi, kiongozi huyo wa zamani aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kufafanua kuhusu kampuni hiyo. [196]
zenye 
Hivyo UN ikaona kuna haja ya kufanya utafiti ili kujua nchi zilizopiga hatua katika matumizi ya kompyuta na internet katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wake na zenye ubora. [197]
zetu 
Timu zetu bado, kiwango kilichoonyeshwa kinasikitisha uwezo wa Zesco uwezi kulinganishwa na Yanga au Simba, inaonekana wazi kuwa wanaufahamu mpira, lakini timu zetu zimekalili sasa hiyo ni mbaya katika soka," alisema Abeid Mziba. [198]
zile 
Afghanistan ni eneo linaloelezwa kuwa ni makutano ya nchi za Mashariki na zile za Magharibi, eneo maalum la kuanzia mapambano dhidi ya mataifa yasiyotabirika kama Iran, Iraq, Pakistan, India, China na mengineyo. [199]
zote 
Alisema tayari serikali imeunda tume ya kuchunguza walimu wote waliodanganya na kwamba wakurugenzi wa halmashauri zote nchini wameagizwa kushirikiana na tume hiyo, ili kuhakikisha kuwa kazi hiyo inafanyika kwa ufanisi. [200]