Mtumiaji:Robert Ullmann/Mwananchi/2008-12-31

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru
Jump to navigation Jump to search

Mwananchi, Dar es Salaam, http://www.mwananchi.co.tz


achukue
Haisemi nani achukue hatua, wala kwa vipi. [1]
ajira
Nimekuwa nikitumikia halmashauri hii kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi sasa kwa ajira ya kibarua huku nikilipwa Sh 50,000 kwa mwezi, sasa nimechoka nataka kuajiriwa sitaki danadana,"alisema Megiroo. [2]
ama
Katibu wa matajiri hao wa mafuta nchini, Bisarara alisema akiba yao inatosha na kwamba hakuna haja ya wananchi ama serikali kuwa na wasiwasi kwamba bidhaa hiyo inaweza kupungua. [3]
ambapo
Kutokana na ajali hiyo treni ya abiria iliyokuwa iondoke jana jioni kuelekea bara haikuondoka ambapo inatarajiwa kuondoka leo saa sita mchana. [4]
ana
Siku chache kabla ya sikukuu ya Krismasi baadhi ya wafanyabiashara walihofia kutokea kwa uhaba wa mafuta baada ya kuwepo taarifa kwamba nchi jirani hazina mafuta, hivyo wakalazimika kupandisha bei ya bidhaa hiyo kiholela ingawa sisi kwa ujumla wetu kila mmoja ana akiba itakayoweza kutumika kwa siku 25 na kabla hayajamalizika meli za mafuta zitakuwa zimeshawasili nchini," alisema Hirani. [5]
ari
Kwa upande wake kocha wa timu hiyo, Marcio Maximo alisema yeye na pamoja wachezaji wake wana ari na imani kubwa ya kufanya vizuri kutokanana na maandalizi mazuri waliyoyapata ili kilichobaki ni kwa Watanzania kujitokeza na kuwaunga mkono. [6]
au
Public and Commissiners for Oath, CAP 12 RE 2002) inaeleza wazi wazi kwamba hakuna kizuizi chochote dhidi ya kiapo cha wakili au kamishina yoyote wa viapo. [7]
azma
Alisema kuwa kwa ufafanuzi Operesheni Sangara ni ziara maalum za kujenga Chadema, kuhamasisha uwajibikaji wa viongozi na kutetea rasilimali za taifa na kwamba neno Sangara ni jina la samaki ambalo linawasilisha azma ya chama kuweka mkazo wa kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha Watanzania. [8]
bara
ABIRIA kutoka sehemu mbalimbali nchini waliokuwa wasafiri jana na juzi kwenda bara wamekwama katika stesheni ya treni ya reli ya kati jijini Dar es Saalam kutokana na ajali iliyotokea katika stesheni ya Tura na Karangasi mkoani Tabora. [9]
baraza
Kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri Baada ya Waziri Mkuu kujiuzulu, Rais Jakaya Kikwete alilazimika kulivunja baraza lake la mawaziri na baada ya kutafakari kwa kipindi cha zaidi ya wiki moja, hatimaye Rais aliunda Baraza jipya la mawaziri na kumteua Mizengo Peter Pinda kuwa Waziri Mkuu. [10]
barua
Akizungumza na waandishi wa habari msimamizi huyo alisema mgombea wa Chadema na DP wana haki ya kukata rufaa Tume ya uchaguzi taifa kwa muda wa saa 48 kuanzia juzi walipokabidhiwa barua ya kuenguliwa kushiriki katika uchaguzi kutokana na pingamizi lililotolewa na dhidi yao kupokelewa na msimamizi. [11]
basi
Hivyo kama Mzee Mwinyi naye alitenda kosa wakati wa utawala wake, basi atachukuliwa hatua. [12]
bila
Nilifurahi kumsikia Rais Kikwete akisema hatamshitaki Mkapa, bila shaka aliona mbali. [13]
bora
Alisema ili kutekeleza mpango huo, wamependekeza kuwe na viwanja bora, muundo wa mashindano ya kila mwaka kuanzia ngazi ya shule, kuendeleza walimu wa riadha, kufanya semina ndogo za uongozi, pamoja na namna ya kufundisha timu ya taifa katika sura ya kitaifa. [14]
chao
Katika tukio hilo vibarua hao walikwenda katika halmashauri hiyo, na kutaka waonane na Mkurugenzi wa manispaa, Raphael Mbunda, ili wamweleza kilio chao cha kulipwa mishahara midogo. [15]
chuo
Mwezi mmoja baadaye uongozi wa chuo uliwarejesha wanafunzi wote isipokuwa wanafunzi 56 walioesemekana kuwa vinara wa kuwashinikiza wenzao kugoma. [16]
dana
Kwa mujibu wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo wanafunzi hao walitaka kukabidhiwa rasmi hosteli za chuo hicho zilizopo mtaa wa Chole jijini Dar es Salaam ambazo kwa muda mrefu uongozi wa chuo umekuwa ukiwapiga dana dana na kushindwa kuwakabidhi kama yalivyokuwa makubaliano ya awali. [17]
dhati
Na hapa ndipo kunapokuja umuhimu wa kuwa na ushirikiano katika taasisi za siasa, hasa vyama vya upinzani kama kweli vinania ya dhati ya kukiondoa CCM madarakani. [18]
dola
Wakati bei ya mafuta ikipanda nchini, hali ni tofauti katika soko la dunia ambako nishati hiyo imeshuka kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita baada ya kupanda kwa kasi hadi kufikia dola 140 za Kimarekani kwa pipa mwezi Julai. [19]
elimu
Lakini jitihada hizo zinapaswa kwenda sambamba na mambo mengine muhimu ili kufanikisha lengo la kuwapatia vijana wengi zaidi elimu ya sekondari. [20]
email
Binafsi kwa wale wote walionikumbuka kwa mwaka mzima iwe ni kwa email, barua, kwa kupigia simu, kunitumia meseji ama hata hao walio nibip nikapata hisia kuwa walikuwa wananifikiria na wananikumbuka kwa namna moja ama nyingine imenionyesha wanajali kiasi kama hicho, naomba niseme ahsanteni sana. [21]
endapo
Kuhusu suala la upangaji wa bei ya mafuta, Bisarara alisema kwamba wameshakubaliana na Ewura namna watakavyofanya endapo itabidi bei ya mafuta ipande. [22]
es
Akizungumza na gazeti hili, Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Cosmas Mogella alisema kuwa, ukiukwaji wa makusudi wa sheria mbalimbali za nchi ndio sababu iliyopelekea kuenguliwa kwa mgombea huyo wa Chadema. [23]
fomu
Pia mgombea huyo alisema kuwa yeye binafsi anaamini kuwa maelezo yake ni sahihi na kwamba hakuna kipengele ambacho alikikiuka katika kujaza fomu hiyo na ndiyo maana amechukua uamuzi wa kukata rufaa Tume ya Uchaguzi Taifa. [24]
furaha
Tuna furaha kuona wenzetu Zambia wamekubali mwaliko wetu licha ya kualikwa dakika za mwisho baada ya Eritrea kujitoa," alieleza Musonye. [25]
gani
Fikiria inapoteza kiasi gani? alihoji mtoa habari huyo na kuongeza kuwa "Hivi sasa kuna idadi kubwa ya wahamiaji haramu walio magerezani ambao kutokana na uwezo mdogo serikali inashindwa kuwarejesha kwao. [26]
gari
Mtapendekezaje kwamba sisi tupewe tuzo ya tako kwa kuthamini gari kuliko kompyuta. [27]
gumzo
Michuano hiyo inafunguliwa rasmi mjini hapa, mahali ambako gumzo katika mitaa na mabasi ya abiria ni kuhusu mashindano hayo ambayo timu ya Tanzania, Kilimanjaro Stars imekuwa gumzo. [28]
hadi
Alisema kutoka na utendaji aliouita kuwa mahiri wa Mkapa wakati wa uongozi wake, umewafanya Watanzania wengi kumuunga mkono hadi sasa na kwamba kitendo cha kumshitaki ni udhalilishaji ambao unaweza kuleta mgawanyiko katika umoja wa kitaifa uliopo. [29]
haki
Chadema watakuwa wamenyimwa haki ya kupiga kura endapo mgombea wao ataondolewa katika Kinyan'anyiro hicho. [30]
halisi
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Haruna Lipumba anasema, ripoti hiyo si sahihi kulingana na hali halisi ya maisha ya Watanzania na kwamba imelenga zaidi katika kupotosha. [31]
hamu
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alieleza kuwa timu zote, isipokuwa Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) inayosubiriwa kwa hamu baada ya kufanya vizuri kwa siku za karibuni barani Afrika na kufuzu kwa michuano ya wachezaji wa ligi za ndani (CHAN), zimewasili. [32]
hana
Semboja Hajji kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam anasema, hana hakika kuwa takwimu hizo ni sahihi, lakini anasema hata kama ni sahihi hakuna tofauti yoyote kwa kuwa hata katika bajeti zilizopita takwimu hizo za kukua kwa uchumi zilitajwa. [33]
hao
Kauli ya waagizaji hao imekuja siku moja baada ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima kueleza kuwa akiba ya mafuta iliyopo ni kubwa ya kuweza kutosheleza mwzi mzima na kushangazwa na hatua ya wafanyabiashara hao kupandisha bei ya mafuta kwa madai kuwa ni adimu. [34]
hapa
Hata wewe nikikuuliza hapo unajua sheria za vyama?...mimi sioni kama kuna lolote la kuongea hapa, wao wameenda kinyume cha sheria na uamuzi huo uliotolewa hauna mashaka yoyote yale," aliongeza kusema. [35]
hapo
Wafuasi hao walisema kwa sasa hawatatoa maamuzi yao mpaka hapo watakapo pata majibu ya rufaa mbayo mgombea wao ameikata na kuiwasilisha tume ya uchaguzi Taifa ndipo watakuwa na jambo la kuamua ambalo wanadhani kuwa litakuwa sahihi kwao. [36]
hasa
Sisi Wabunge tupo kwa ajili ya kuifanyia marekebisho katiba, kutunga sera na sheria," alisema Sinani na akaongeza kusema: "(Suala la hoja binafsi) Likiletwa tutalijadili, lakini pamoja na majukumu hayo sidhani kama ni busara kuifanyia marekebisho katiba kila kukicha, hasa pale unapomlenga mtu fulani. [37]
hata
Mkazi mwingine aliyetoa maoni alisema kwa kuwa sheria ni msumeno na kwamba ni matarajio yake kuwa kuondolewa kwa kinga hiyo haitakuwa kwa Mkapa, bali hata rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na kwamba vinginevyo madai hayo yatakuwa yamelenga kumchafua Mkapa kisiasa. [38]
hawana
Semboja anafafanua kuwa, kukua kwa mauzo ya nje nchini Tanzania si jambo la kujisifu kwamba serikali imepiga hatua, kwa sababu bidhaa nyingi zinazouzwa nje ni za kampuni za nje na kwamba Watanzania hawana bidhaa wanazouza nje ya nchi. [39]
haya
Tumeyapa uzito mashindano haya, ni kufa au kupona. [40]
hii
Leo hii tukisema wangapi wanamuunga mkono Mkapa tutawapata wengi kuliko wachache wanavyofikiri. [41]
hiki
Nimewaeleza wachezaji wangu wawe makini kwani hiki ni kipimo kikubwa kwao kwa michuano ijayo iliyo mbele yao. [42]
hili
Jamani Mkapa amelitumikia taifa hili na kuliacha katika hali nzuri. [43]
hilo
Mbunge wa jimbo la Mtwara, Mohamed Sinani alizungumzia suala hilo kidiplomasia zaidi, lakini akashindwa kuficha msimamo wake kwa Rais Mkapa, ambaye aliteuliwa na CCM kuwania urais baada ya kumshinda Rais Jakaya Kikwete katika marudio ya kura za maoni. [44]
hivi
Opareshen Sangara inakwenda sambamba na kuhamasisha wananchi kujiunga na Chadema na inasimamiwa na uongozi wa taifa na ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Chadema wa mwaka 2006 mpaka 2010 wa kueneza chama na sera zake kwa umma na kuhamsisha mabadiliko kwa lengo kuweka tumaini jipya la demokrasia ya maendeleo, kufanya hivi siyo kudhalilisha wananchi nadhani wanapungukiwa uelewa," alieleza. [45]
hivyo
Bei ya mafuta ilipanda ghafla usiku wa siku moja kabla ya Krismasi huku baadhi ya vituo vikifungwa kwa maelezo kuwa kuongezeka kwa vitendo vya maharamia wa Kisomali kuteka meli za mizigo kwenye pwani ya Somalia kumefanya meli zilizobeba shehena za mafuta yanayokuja nchini kushindwa kupita na hivyo kusababisha uhaba wa nishati hiyo muhimu. [46]
hizo
Alifafanua kwamba ingawa mafuta yapo ya kutosha nchini, pia wameshalipa gharama za kuleta mafuta mengine na kwamba meli hizo ziko njiani na zitawasili muda wowote kuanzia Januari mwakani. [47]
hofu
Kitendo cha wamiliki wa vituo vya mafuta kinapaswa kukemewa kwani wanawasababishia wananchi hofu ya maisha. [48]
huduma
Alisema watu wenye mamlaka serikalini, wamekuwa wakijilimbikia bila aibu utajiri wa kutisha na kuufuja wakati wananchi walio wengi wakiteseka kwa kukosa chakula na huduma nyingine muhimu. [49]
huenda
Hakuna mpenda mageuzi ambaye hakufurahia uamuzi huo wabusara uliooneshwa na upinzani, na hali ya matumaini kuwa huenda uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 utakuwa na mabadiliko makubwa katika medani ya siasa hapa nchini kwa upinzani kushika hatamu za uongozi wa nchi hii. [50]
huko
Haina maana ya kuwadharilisha wananchi," alieleza na kufafanua kuwa tayari operesheni hiyo imeshafanyika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na kuhamia mkoani Mbeya katika kampeni za uchaguzi mdogo wa huko. [51]
huo
Wakati huo ukinipigia (simu) nitakuwa katika nafasi nzuri ya kutoa maoni yangu, kwa sasa ni mapema mono," alisema Njwayo aliyehojiwa kwa njia ya simu. [52]
huu
Awali msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mbeya vijijini Juliana Malange alitoa saa 48 kuanzia juzi jioni kwa wagombea wa vyama vya Chadema na DP kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya kuenguliwa kushiriki uchaguzi mdogo unaotarajia kufanyika Januari 25 mwaka huu. [53]
huyu
Lakini kwa bahati mbaya huyu aliyependekeza tuzo ya tako kwa wanaoazimia kwenye mawarsha yeye mwenyewe amependekeza tu hatua zichukuliwe bila kuonyesha nani achukue hatua hii. [54]
idadi
Kwa mujibu wa habari hizo serikali inatumia Sh500,000 kugharimia safari ya mhamiaji haramu mmoja kurejeshwa kwao na kwamba kuna idadi kubwa ya wahamiaji ambao hadi sasa wako katika magereza ya Tanzania. [55]
ikiwemo
Rais alisema, mwendelezo huo wa hali ya mambo ilivyo kwa sasa, utaathiri mpango huo wa kuleta amani katika mgogoro wa Palestina na Israel na kuongeza kwamba, ameungana na Jumuiya ya Kimataifa ikiwemo ya wapenda amani kupinga mauaji hayo. [56]
ile
Alisema wamiliki hao wako chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) na ndiyo waliowapa leseni ya kufanya biashara kama ambavyo mamlaka hiyo ilivyotoa leseni kwa waagizaji hao hivyo bado wana mamlaka ya kuwadhibiti kwa namna yoyote ile ili tatizo la aina hiyo isije ikajitokeza tena. [57]
ili
Wilbroad Slaa ameahidi kuwasilisha hoja ya kutaka Mkapa, aliyeongoza nchi kwa vipindi viwili (1995-2005), apandishwe kizimbani kujibu tuhuma za kufanya makosa wakati akiwa Ikulu, huku kiongozi wa upinzani Bungeni, Hamad Rashid, akiahidi kuwasilisha hoja ya kutaka kiongozi huyo aondolewe kinga ili aweze kupandishwe kizimbani. [58]
imara
Bwalya, nahodha wa zamani wa Zambia aliyecheza soka ya kulipwa nchini Ubelgiji , Amerika Kusini, alisema kuwa huo utakuwa mtihani mzuri kwa vijana wake ambao watacheza na timu imara kama Tanzania, Uganda, Sudan, Rwanda na Kenya. [59]
inadai
Ripoti hiyo, ambayo imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu na kuchapishwa katika Magazeti ya serikali, inadai kuwa uchumi wa Tanzania ndani ya kipindi cha miaka miatatu ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete unapeta kulingana na viashiria kadhaa ambavyo inavitaja. [60]
iwe
Kama ambavyo wanasiasa wamekuwa wakisisitiza kuwa viongozi wanaoingia madarakani kwa rushwa au ghilba zozote ni dhahiri serikali watakayoiunda haitaweza kuwa na ujasiri wa kupambana na rushwa na ufisadi kwani ni lazima iwe sehemu ya maisha na ni shamba la wanasiasa kuvuna mamlioni ya fedha kila wakati wa uchaguzi unapofika. [61]
jimbo
Huo ni upuuzi na nitaupinga kokote," alisema mbunge wa jimbo la Masasi, Raynald Mrope. [62]
jiti
Nafasi ni ndogo mno kwa kuwa tayari wameshajitia jiti la roho na ukishajitia jiti la roho sauti haitoki tena," alisema Duni. [63]
juu
Aidha, Duni alikilalamikia Chadema kuwa hakina ushirikiano na nia nzuri juu ya CUF kwa kukataa wito wa kuombwa kushirikiana na kusimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi huo. [64]
kadhaa
Rubeya hakupatikana licha ya kutafutwa mara kadhaa. [65]
kali
Dakika mbili baadaye, Solomon Philipo wa Manyoni aliisawazishia timu yake baada ya kufunga goli safi baada ya kuachia shuti kali akiwa mita 30 na mpira kujaa ndani ya nyavu upande wa kulia wa lango la Toto. [66]
kati
Bei kwa sasa dola 40 za Kimarekani kwa pipa, wakati bei ya mafuta ambayo yanatakiwa kuwa yanauzwa nchini kwa sasa ni ile iliyokuwa duniani miezi miwili iliyopita ambayo ni kati ya dola 50 na 60 za Kimarekani kwa pipa. [67]
kauli
Na hilo ndilo linaloonekana hivi sasa, kwani tangu uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime upite kumekuwa na kauli za kujichanganya za viongozi wa vyama vya upinzani, leo huyo kasema hivi, kesho mwingine kakanusha na kadhalika. [68]
kazi
Ingawa sisi kama Ewura kazi yetu ni kulinda maslahi ya watumiaji na wenye mali na kuhakikisha kwamba hakuna atakayeumia kati yao na kuhusu ongezeko la bei ya bidhaa hiyo inasababishwa na wafanyabiashara kuwa na hofu ya kukosekana kwa mafuta,"alisema Ngamlagosi. [69]
kidogo
Aliongeza kuwa moja ya sababu zinazoongeza hofu ya kukosekana kwa mafuta ni hatua ya waagizaji na wamiliki wa vituo vya mafuta nchini kuagiza mafuta kidogo kutokana na bei ya bidhaa hiyo kuyumba. [70]
kilieleza
Chanzo kimoja kilieleza kuwa mchezaji huyo amekuwa ni mtovu wa nidhamu, kitu ambacho kimewakela sana viongozi hao na kuchukua jukumu la kumsimamisha kwa muda usiojulikana. [71]
kimoja
Alisema kuwa mafanikio ya soka ya Tanzania yaliyopatikana kwa siku za karibuni yamewaunganisha Watanzania na kuwa kitu kimoja na kuongeza kuwa ni muhimu wachezaji wa timu hiyo wakadumisha jambo hilo. [72]
kisiwa
Katibu wa Ujumbe wa watu walikwenda kuwasilisha barua ya madai hayo kwenye Ofisi za Mwakilishi Mkazai Umoja wa Mataifa, Hamad Ali Mussa alisema wanataka kisiwa hicho kiwe na mamlaka yake kama vilivyo visiwa vinavyounda utawala wa Comoro. [73]
kiti
KUENGULIWA kwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Sabwee Shitambala katika kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Mbeya Vijijini kumepokewa kwa hisia tofauti na wadau mbalimbali wa siasa nchini. [74]
kiwe
Zaidi ya wananchi 10,000 wa Kisiwa cha Pemba, wameuomba Umoja wa Mataifa (UN) uilazimishe Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibadili muundo wa sasa wa serikali utakaoruhusu visiwa vya Unguja na Pemba, kila kimoja kiwe na serikali yake. [75]
klabu
Kufukuzwa au kusimamishwa kwa wachezaji kulifichuliwa juzi na kuthibitishwa na uongozi wa klabu hiyo kongwe ya Mtaa wa Msimbazi. [76]
kodi
Mara baada ya Uchaguzi mkuu wa 1995 waliokuwa mawaziri wa fedha Simon Mbilinyi na Naibu wake Kilontsi Mporogomyi walilazimika kung'oka kwa kilichodaiwa kutoa misamaha ya kodi. [77]
koo
Na kama desturi ilivyo, mwenye pendekezo lazima alainishe koo za waishiwa, pamoja na kutoa posho la tako (si tuzo la tako). [78]
kuahidi
Rais Kikwete alibaini na kutamka wazi ni lazima viongozi watenganishe biashara na siasa na kuahidi kuanza mara moja kushughulikia suala hili. [79]
kufoka
Bila hata kutoa tuzo ya tume kwa ajili yetu, alianza kufoka moja kwa moja. [80]
kuja
Zimeongeza kuwa ni wazi lipo tatizo katika mipaka wa nchi jirani ambao huwapitisha wahamiaji hao kuja nchini kukwepesha mzigo huo kwa serikali za nchi zao. [81]
kukiuka
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Juma Duni Haji alisema, wao ndio waliokiengua Chadema katika uchaguzi huo mdogo kwa kukiuka taratibu na sheria ya uchaguzi. [82]
kukusanya
Serikali ilisema imefanikiwa kukusanya zaidi ya Sh 50 bilioni zilizorejeshwa na watuhumiwa wa ufisadi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT). [83]
kule
Miaka michache iliyopita tulikuwa tunakwenda kwenye mashindano kwa ajili ya kushiriki, lakini sasa hivi tunakwenda kupambana ili tuweze kutwaa ubingwa na ubingwa huo utakuwa ni ishara nzuri ya kufanya vizuri kule Ivory Coast, "alisema Kandoro. [84]
kulipa
Anakubali kuwa, kiwango cha mauzo ya nje kimeongezeka, lakini anasema, kinatokana na madini hasa dhahabu na bei yake katika soko la dunia jambo ambalo halimfaidishi hata kidogo raia wa kawaida kwa kuwa makampuni yanayozalisha na kuuza madini nchini yanakwepa kulipa kodi. [85]
kuomba
Aidha Rais Kikwete alisema Kingunge na Mungai, wameondolewa katika orodha ya mawaziri baada ya kuomba kupumzika kutokana na kufanya kazi serikali kwa muda mrefu. [86]
kupata
Habari zaidi zinasema kuwa Idara ya Uhamiaji imekuwa ikiwasiliana na mabalozi wa nchi husika kuhusu wahamiaji hao bila kupata ufumbuzi sahihi wa tatizo hilo. [87]
kupitia
Hali kadhalika msimamizi huyo alisema kuwa amepokea pingamizi kutoka kwa mgombea wa CCM, Luckson Mwanjali dhidi ya mgombea wa Chadema Sambwee Shitambala na kwamba baada ya kupitia pingamizi hizo na maelezo ya utetezi ofisi ya msimaizi imeyapokea mapingamizi hayo. [88]
kusoma
Mbeya Vijijini, Juliana Malange hakuweza kusoma kwa makini sheria hiyo na kuzingatia kikamilifu kabla ya kufanya maamuzi ya kumuengua. [89]
kutuliza
Oktoba 18 askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) mkoa wa Iringa walilazimika kutumia mabomu ya machozi kutuliza vurugu za wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mkwawa (MUCE). [90]
kuu
Alisema baada ya uongozi wa timu hiyo kukutana wiki iliyopita na kuiweka wazi mikakati ya timu hiyo kwa wanachama ana hakika mikakati hiyo ikitekelezwa ipasavyo timu hiyo itafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu na kuepuka kushuka daraja. [91]
kuuza
WAAGIZAJI wakubwa wa mafuta nchini wamewakana na wamiliki wa vituo vya kuuza nishati hiyo na kushangazwa na kitendo cha kupandisha bei kiholela wakati wa sikukuu ya Krismas kwa kisingizio cha uadimu wa mafuta baada ya meli kuzuiwa na maharamia wa Kisomali. [92]
kwake
Pia alielezea kukerwa kwake juu ya kukithiri kwa maovu mengine na kwamba wakati umefika wa wananchi kushirikiana katika kukemea na kutokomeza maovu hayo. [93]
kwako
Kwa niaba ya serikali, watu wa Tanzania na kwa niaba yangu, ningependa kutuma salamu kwako na watu wa Palestina na familia za wapendwa wetu, kueleza majonzi na simanzi kwa hasara iliyotokea," ilisema taarifa hiyo ikimnukuu Rais Kikwete. [94]
kwenu
Na kwa maana hiyo naomba nichukue fursa hii tena kuwashukuru wasomaji wote wa makala zangu na zaidi niseme ni fahari iliyoje kupata kusikia kutoka kwenu. [95]
la
Wakati shinikizao la kutaka Mkapa aondolewe kinga na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za makosa anayodaiwa kufanya akiwa Ikulu, wabunge na wananchi wa mkoani Mtwara na wananchi kuibuka na kumtetea. [96]
lake
Hata hivyo, Gabriel ambaye inasemekana uongozi wa Simba umemuza kisirisiri lakini yeye amekataa kuuzwa huko kwa timu hiyo ambayo si chaguo lake. [97]
leo
Sisi tumewaachia Kiteto na Tarime kwa kuwa tuliona wao ndio wenye nguvu, lakini wao wanakuwa wagumu, Tunduru na Tanga madiwani ambako sisi ndio tulio na nguvu na tuliwaomba walikataa kutuachia na leo Mbeya ni sisi, pia wamekataa" alilaumu Duni. [98]
letu
Tatizo letu hatujui sheria za nchi zinasemaje na wala hatupendi kujua, hili ni tatizo sugu tulilo nalo Watanzania wengi," alisema Dk Mogella. [99]
licha
Sisi hatuwezi kuchukua polisi na kwenda kuwakamata licha ya ukweli kuwa ongezeko hilo linawaumiza wananchi. [100]
ligi
KOCHA wa Taifa Stars, Marcio Maximo amesema kuwa majina ya nchi na historia zao za nyuma hazimpi taAbu kiasi cha kumfanya ashindwe kufanya vizuri wakati wa michuano ya Afrika ya wachezaji wa ligi za ndani(CHAN) iliyopangwa kufanyika Februari mwakani nchini Ivory Coast. [101]
mabaya
Novemba 25 Watanzania wakalisikia jingine kubwa, Mawaziri wawili waliowahi kuongoza wizara mbalimbali ikiwamo nyeti ya fedha katika serikali ya awamu tatu, Basil Mramba na Daniel Yona wamefikishwa kortini kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh11.7 bilioni. [102]
macho
Inasikitisha kuona watu wenye mamlaka wakijilimbikizia mali huku wengine wakiteseka kwa kusoka chakula na huduma za matibabu, vitendo hivi havifai kufumbiwa macho hata kidogo, kwa sababu vinahatarisha usalama na amani ya taifa letu," alisema Askofu Mtenga. [103]
madeni
Ni mwezi huo huo wa Februari, baada ya sakata la Richmond, lilizuka kwa kasi kubwa suala la wale waliochota fedha kutoka akaunti ya madeni ya nje ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA). [104]
mali
Alifafanua kuwa wajibu wao ni kulinda maslahi ya watumiaji na wenye mali na kwamba wata hakikisha kwamba akuna atakayeumia kati yao. [105]
manaibu
Alipotangaza Baraza jipya iligundulika kuwa Mawaziri tisa na manaibu mawaziri nane, walipoteza nyadhifa zao. [106]
mara
Lakini wakizungumza kwa nyakati tofauti kabla ya katibu wa umoja wa waagizaji mafuta, Salum Bisarara kutoa msimamo wao, wafanyabiasahara hao walisema ingawa serikali imeruhusu mfumo huria wa biashara, hatua ya wenye vituo kupandisha bei mara kwa mara si ya kistaarabu. [107]
marufuku
Kwa sababu kauli hii ya Pinda kupiga marufuku matumizi ya mashangingi serikalini ilishawahi kuzungumzwa mno huko nyuma na mawaziri wengine, lakini tunaendelea kushuhudia yakiendelea kutumika. [108]
matukio
Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Edward Lowassa Mwaka 2008 utakumbukwa kuwa ulikuwa na matukio ambayo yameweka historia katika siasa za nchi hii. [109]
matunda
Walisema pamoja na kulipwa ujira mdogo, pia wamekuwa wakiahidiwa kuajiriwa, lakini ahadi hiyo, haijazaa matunda. [110]
mbele
Alitoa mfano wa wanafunzi wanapopeleka fomu za uthibitisho wa kuzaliwa (Affidavit) kiapo kinachotolewa mbele ya mwanasheria au wakili hukubaliwa kisheria. [111]
mbunge
Tayari mbunge wa Karatu, Dk. [112]
mchezo
WAKATI Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) likikamilisha mpango maalum wa kuinua kiwango cha mchezo huo, utekelezaji wake unatarajia kukamilika baada ya miaka nane, imeelezwa. [113]
mfumuko
Profesa Lipumba anasema kwamba hali ya mfumuko wa bei inayotangazwa katika ripoti mbalimbali za serikali ni mara mbili zaidi ya hali halisi ya mfumuko wa bei za bidhaa muhimu nchini. [114]
mgomo
Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, latangaza kuwasimamisha masomo kwa muda usiojulikana, wanafunzi wa shahada ya kwanza kufuatia mgomo waliouitisha kuishinikiza serikali iwaongezee fedha za mikopo. [115]
mhuri
Sheria inasema ukaape mahakamani na upate mhuri wa mahakama, lakini mgombea wa Chadema ameapa kwa wakili na kwa kuwa yeye mwenyewe ni wakili akaamua kuchukua mhuri wa kampuni yake, hizo si taratibu wala sheria ya uchaguzi isemavyo," alisema Duni. [116]
milioni
Lipumba anafafanua kuwa, ripoti hiyo inatofautiana na ripoti ya serikali ya Novemba/Desemba mwaka huu, ambayo yenyewe inaonyesha kuwa watu masikini wameongezeka kutoka 11.7 milioni 2005 hadi 12.7 milioni 2007, na kuongeza kuwa kuna ongezeko la watu milioni moja ambao ni masikini. [117]
mimi
Nilivyoelewa mimi ni kwamba kinga ikiondolewa ni kwa marais wote waliomaliza muda wao kwa kuwa katiba ni moja. [118]
mistari
Rais Kikwete kupitia hotuba yake hiyo alisema kuwa amedhamiria kumaliza kabisa mpasuko wa kisiasa katika visiwa vya Unguja na Pemba ambapo alisema kuwa unatokana na sababu za kihistoria za wananchi wa kisiwa hicho kusimama kwenye mistari yao ya kihistoria wakati wa mapambano ya kujitawala. [119]
mjini
Watanzania wenzangu tusiwe na shukrani za Punda," alisema Ibrahim Mchopa mkazi wa mjini Mtwara. [120]
mkesha
Aliongeza kuwa siku hiyo ya mkesha wa mwaka mpya wameandaa zawadi mbalimbali ambazo zitakuwa zikitolewa kwa sababu maalum, muda maalum na zitatolewa na mtu maalum. [121]
mkoa
KIKAO cha Baraza la Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza (UVCCM) kimeilaani mikutano ya hadhara ya Chadema iliyopewa jina la Operesheni Sangara na kudai kuwa ilikuwa ikiwadhalilisha wananchi. [122]
mkongwe
SIKU moja baada ya Kamati ya Utendaji ya Simba iliyokutana juzi kumsimamisha Orji Obina na kumtimua mshambuliaji mkongwe Emmanuel Gabriel, wachezaji hao wamesema hawajapata taarifa yoyote kutoka kwa uongozi kuhusiana na adhabu hiyo. [123]
mkuu
Akizungumza jana na Mwananchi, msemaji mkuu wa timu hiyo, Idd Godigodi alisema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kumpa mwalimu muda wa kutosha kurekabisha makosa ambayo yalijitokeza katika mzunguko wa kwanza. [124]
mno
Mbunge wa Tandahimba, Juma Njwayo aliamua kutoweka bayana msimamo wake na akazungumzia suala hilo kiufundi zaidi, akisema ni mapema mno kulizungumzia na kwamba anasubiri kwanza liwasilishwe kama hoja binafsi Bungeni. [125]
mpya
Akizungumza na viongozi wapya wa UVCCM walioteuliwa katika uchaguzi mpya wa chama mwaka huu, kamanda wa vijana ambaye pia ni rais wa bunge la Afirika Balozi Gerturde Mongella aliwapongeza vijana kwa kutoa tamkio hilo la kulaani wananchi kudharirishwa na kuitwa sangara. [126]
mrefu
Serikali hutumia Sh500,000 kumrejesha kwao mhamiaji haramu mmoja, na imekuwa ikifanya hivyo muda mrefu. [127]
mtovu
Kamati hiyo ilimsimamisha mshambuliaji huyo wa Kinigeria kwa madai kuwa ni mtovu wa nidhamu na kumtimua Gabriel kwa madai kuwa si mchezaji wao kwa sababu walikwishamuuza Oman. [128]
mzunguko
Toto ipo kwenye maandalizi mazito ya kujiandaa kushiriki mzunguko wa pili wa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza Januari 10 mwakani. [129]
na
Ndivyo unavyoweza kufupisha kitendo cha baadhi ya wabunge na wananchi wa mkoani Mtwara kujitokeza hadharani na kumtetea rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa. [130]
nao
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona kuwa hata baadhi ya mapadri, watawa,maketikista na wamisionari, nao wanajihusisha na maovu hayo wakati wakijua wazi kuwa yanamchukiza Mungu. [131]
naomba
Mwaka mpya naomba tumshukuru Mungu, maisha yanaendelea. [132]
nayo
Habari hizo zilieleza kuwa, hata treni ya abiria iliyokuwa iondoke Jumapili kuelekea bara haikuondoka kwa sababu ilichelewa kufika na hivyo kulazimika kuondoka juzi mchana ambapo nayo kama ikifika maeneo ya ajali na kukuta marekebisho hayajafanyika italazimika kusubiri mpaka mafundi watakapomaliza kurekebisha reli. [133]
ndani
Habari za uhakika kutoka ndani ya kampuni ya reli nchini (TRL), zinasema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi katikati ya stesheni ya Tura na Karangasi baada ya mabehewa matatu ya treni ya mizigo kuacha njia. [134]
ndivyo
Lakini ndivyo tulivyo. [135]
ndugu
Lakini pia ndugu zangu waumini tunapaswa kuendelea kuliombea taifa letu bila kukoma ili tatizo hili liishe, tusichoke kumuomba Mungu atusaidie kutuondolea matatizo na majanga mbali mbali katika nchi yetu ,"alisisitiza kiongozi huyo wa kidini. [136]
ngumu
Kibarua mwingine, Issa Mulla, alisema amekuwa akifanya kazi ngumu lakini akiwa kibarua na kwamba sasa amechoshwa na hali hiyo. [137]
ni
Miongoni mwa tuhuma za Mkapa, ambaye anasifika kwa kuinua uchumi baada ya kuukuta kwenye hali mbaya, ni kujiuzia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya kwa bei nafuu akitumia kampuni ya Tan Power Resources anayoimulika pamoja na waziri wa zamani wa nishati na madini, Daniel Yona wakati akiwa rais. [138]
niaba
Rais Kikwete katika salamu zake hizo kwa niaba ya serikali na Watanzania, zilizotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alisema licha ya kushtushwa, lakini hali ilivyo sasa inaweza kuathiri mpango wa kutafuta amani Mashariki ya Kati maarufu kama Road Map. [139]
nini
Mimi nashindwa kuelewa ni kwa nini msimamizi alitoa uamuzi huo. [140]
njaa
Alipokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Henry Shekifu kuwa watu hao walikuwa wakikabiliwa na njaa kali baada ya ukame uliosababisha kupungua kwa matunda na mizizi wanayoitegemea kwa chakula. [141]
nje
Joshua alipiga adhabu ndogo na mpira ulienda moja kwa moja na kujaa upande wa kushoto wa lango la Manyoni huku kipa Usega Mgogo akiukodolea macho kwa imani kuwa unatoka nje ya lango. [142]
nne
Hatari yake ni kwamba wanafunzi watakaopitia mazingira hayo watamaliza kidato cha nne bila ya kuwa na elimu inayolingana na kiwango hicho. [143]
nyeti
Hali hiyo ilisababisha Rais Kikwete kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, Daudi Ballali kutokana na kushindwa kudhibiti upotevu wa fedha hizo akiwa kama kiongozi mkuu wa taasisi hiyo nyeti ya umma. [144]
ovyo
Uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 aliyekuwa Waziri wa Biashara na Viwanda Iddi Simba aliondolewa madarakani baada ya kubainika alitoa ovyo vibali vya uagizaji sukari nje ya nchi. [145]
papo
Waziri Mkuu aliyasema hayo wakati akijibu maswali ya papo kwa papo. [146]
pato
Baadhi ya viashiria vilivyoainishwa katika ripoti hiyo kuwa vimefanikiwa sana ni pamoja pato la taifa, pato la serikali, mauzo ya nje, pato la mtu mmoja mmoja na miradi mipya iliyofunguliwa na kusajiliwa. [147]
pia
Baadhi ya wananchi wa mikoa hiyo walihojiwa na Mwananchi walionekana kupinga hoja hiyo, wakitaka Mkapa aangaliwe pia kwa mazuri aliyofanya. [148]
raia
Katika kuonyesha msisitizo, rais alifafanua kwamba, alisoma kwa mshtuko na huzuni taarifa za mashambulizi mfululizo ya ndege za Israel katika Ukanda wa Gaza ambayo yaliua zaidi ya raia wa Palestina 375, huku yakiacha wengine majeruhi ambao ni pamoja na wanafunzi. [149]
ratiba
Baadhi ya abiria waliozungumza na Mwananchi jana walisema kuwa, kwa sasa safari za treni hiyo hazieleweki hivyo hawashangai walivyofika stesheni hapo na kukuta matangazo kuwa jana hawatasafiri kama kawaida bila kuambiwa sababu yoyote ya mabadiliko ya ratiba za treni hiyo. [150]
ripoti
Kwa mujibu wa ripoti hiyo serikali inajigamba na kujinasibu kuwa uchumi wa Tanzania unapeta ndani ya kipindi hicho cha miaka mitatu. [151]
rufaa
Akizungumza na waandishi baada ya kuwasilisha rufaa, mgombea huyo alisema kuwa msimamizi wa uchaguzi hakusoma kwa makini maelezo yake na kuyazingatia kikamilifu kabla ya kufanya maamuzi ya kumuengua. [152]
sana
Alisema nafasi ya Chadema kushiriki katika uchaguzi huo ni mdogo sana kwa sasa ingawa wamepewa muda wa saa 48 kukata rufaa iwapo hawakuridhika na maamuzi hayo. [153]
sasa
Siasa za sasa ni za kuchafuana. [154]
si
Kimsingi siungi mkono si tu kwa sababu Mkapa ni wa kusini bali alivyoliongoza taifa," alisema Athumani akimzungumzia Mkapa ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Lupaso wilayani Masasi. [155]
sifa
Kisheria wagombea wanapaswa kuapa kwa hakimu ambaye kwa mujibu wa sheria za viapo ya mwaka 1966 ni kamishna wa viapo, lakini hata wakili pia anatambulika kwa sifa hiyo, hivyo mtu anaweza kuapa hata kwa wakili,"alisema. [156]
siyo
Mongella alisema kuwa wao kama wanasiasa wanakubaliana na siasa za hoja na wala siyo siasa za kudhalilisha wananchi na kuwaita sangara. [157]
soka
Rais Jakaya Kikwete mara ya mwisho alipokuwa akilihutubia bunge mwezi Agosti mwaka huu, alisema baada ya kusaidia kuinua kiango cha soka sasa anaigeukia riadha na kuwataka viongozi wa RT kuandaa mikakati itakayosadia kufikia lengo hilo. [158]
sote
Jahazi letu limeandaliwa vema kwa ajili ya kuwapandisha mashabiki wetu na kuwapeleka Zanzibar, na mwaka mpya utatukuta sisi sote tukiwa ndani ya jahazi tukila raha za uhakika,î alisema Mzee Yusufu. [159]
taji
Tumekuja na ndoto, tuna shinikizo la kutwaa tena taji letu, tuna kikosi kizuri na imara," alieleza kocha wao, Yusuf Burhane. [160]
tako
HE jamani, mambo ya nishani ya viatu na tuzo la tako yameleta ubishi mkubwa sana. [161]
tamaa
Msemo huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuinua maendeleo ya watu mbalimbali hasa pale kunapoonekana kuna vikwazo ambavyo vinakatisha tamaa, na hivyo kufanya baadhi ya watu au kikundi cha watu kuanza kujitenga kwa ama kukatishwa tamaa, ama kuona mambo hayatakuwa kama wanavyofikiria. [162]
tano
Naye alipotafutwa, Kaduguda aliieleza Mwananchi kuwa apigiwe simu baada ya dakika tano na alipotafutwa baadaye alishauri atafutwe Katibu Mwenezi, Said Rubeya. [163]
tathmini
Wenzetu Rwanda, Kenya, Uganda wanakimbia wakati sisi ndio kwanza tunajikongoja na tunajisifu uchumi unakua, lakini ukifanya tathmini ya kina utagundua kuwa badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma," anasema Dk. [164]
tu
Si hilo tu amefanya mengi ambayo anastahili kuheshimiwa na kuachwa apumzike. [165]
tume
Katika hatua nyingine kumekuwepo na makundi ya wafuasi wa Chadema katika maeneo ya Mbalizi Mbeya Vijijini ambao wamekuwa wakijaribu kuzunguka wakiimba nyimbo kushinikiza tume kumrudisha mgombea wao kurudishwa katika kinyang'anyiro cha ubunge Mbeya vijijini huku wakiwa wameshika bendera za chama hicho. [166]
tuna
Wanajidai tuna operesheni sangara lakini ile ni operesheni ua CUF, habari ndio hiyo, na kilichobaki ni kuthibitisha ukichelewa umefungwa tatu bila," alituhumu Duni. [167]
uhalisia
Ripoti hiyo imewashitua wadau mbalimbali wa masuala ya kisiasa, kidiplomasia na kiuchumi nchini ambao wanasema kuwa ripoti hiyo inapotosha umma wa Watanzania kwa kuwa haijazungumzia uhalisia wa uchumi wa nchi. [168]
ule
Ni kipindi ambacho kilikuwa na shinikizo, wasiwasi mkubwa nchini, lakini sasa taifa limerudia hali yake kawaida," alisema Rais Kikwete na kuongeza: "Uamuzi ule ulileta mashaka makubwa sana, ulileta mtikisiko nchini. [169]
umma
Oparesheni sangara ni mkakati ambao chama chetu kimeubuni kwa lengo la kuikomboa nchi kutoka mikononi mwa mafisadi wakubwa tuliowafananisha na sangara, ilizinduliwa katika siku ya kuadhimisha tarehe ya kutangazwa kwa orodha ya mafisadi wanaoitafuna nchi na ambao baadhi yao wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za wizi wa fedha za umma. [170]
usalama
Hata hivyo alipotakiwa kutoa takwimu za tatizo hilo alikataa akisema suala hilo linaweza kuhatarisha usalama wa taifa. [171]
uwezo
Watu hao walipewa leseni na Ewura kama tulivyopewa sisi hivyo mamlaka ndiyo yenye uwezo wa kuwadhibiti, hasa ikizingatiwa kwamba ni chombo cha serikali na chenye maamuzi mazito. [172]
vibarua
ZAIDI ya vibarua 30 wa Idara ya Afya (Mazingira) katika Halmashauri ya Manispaa ya Arusha, jana waliandamana ili kushinikiza kuongezewa mishahara. [173]
vibaya
Mramba, waziri mkongwe aliyepata kushika wizara nyeti kwenye serikali za awamu zote nne, na Yona, aliyeshika wizara kwenye serikali za awamu mbili, walipandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kutumia vibaya ofisi kwa kuiruhusu kampuni ya M/S Alex Stewart (Assayers) ya Uingereza kuingia mkataba wa kudhibiti madini ya dhahabu kinyume cha sheria. [174]
vifaa
Haitoshi kuwa na vyumba vya madarasa kama vifaa vya kufundishia havipo au havitoshi, na hakuna walimu wa kutosha. [175]
virago
UONGOZI wa Klabu ya Simba umemsimamisha mshambuliaji wake wa kulipwa kutoka Nigeria, Orji Obina na kumtupia virago mkongwe, Emannuel Gabriel. [176]
vya
Ndugu yangu hili suala ni la Kikatiba, tusubiri walete hoja na vielelezo vya ushahidi, tutalijadili kuona uzito wake. [177]
vyake
Akizungumza na Mwananchi jana jijini Dar es Salaam, Mzee Yusufu alisema wameamua kuwapelekea Jahazi mashabiki wao wa Tabata na viunga vyake ili wawe pamoja katika kuuaga na kuukaribisha mwaka mpya ambapo kwa pamoja wataupokea wakiwa ndani ya jahazi. [178]
waishiwa
Hata hivyo sisi waishiwa tulifaidi sana maana tulikuwa tumeshajiteua kuwa tume ya tuzo. [179]
wakisema
Watu waliotoa maoni yao kuhusu hilo walionyesha kuridhishwa kwao na kitendo cha serikali kuwapandisha kizimbani mawaziri wawili wa zamani wanaotuhumiwa kwa vitendo vya ufisadi, huku baadhi wakisema kuwa bado wengi zaidi wanatakiwa kufikishwa mbele ya mkono wa sheria. [180]
wala
Suala la mafuta kupanda ni suala la wamiliki wa vituo vya mafuta wala halihusiani na sikukuu za Krismas ama sisi kufunga ofisi wakati wa sikukuu na wala lisihusishwe na suala la maharamia wa Kisomali, bali ni maamuzi ya wamiliki wa vituo vya mafuta ya kupandisha bei kwa sababu wanazozifahamu. [181]
wale
Hata hivyo, kocha huyo alisema pamoja na matumaini makubwa aliyonayo kwa kikosi chake, bado Watanzania watatakiwa kuiunga mkono hata pale michuano hiyo itakapoanza akiwataka wale wenye uwezo wa kusafiri kufanya hivyo ili kwenda kuishangilia timu hiyo. [182]
walio
WIMBI la wahamiaji haramu wanaoingia nchini kutoka mataifa mbalimbali linaelezwa kuigharimu serikali mamilioni ya fedha katika kuwarejesha makwao na kuwahudumia walio magerezani imeelezwa. [183]
wangu
Wakati naanza kuifundisha Stars wachezaji wangu walikuwa na hofu pale watakapokutana na Cameroon au timu yoyote, lakini niliwaambaia waondoe kitu hicho na kusikiliza maelekezo yangu, nafikiri walifanya nini kwenye michezo iliyiopita,"alisema. [184]
wao
Mkazi mwingine Rashidi Athuman alisema kuondolewa kwa kinga kwa marais waliomaliza muda wao kutasababisha machafuko ya kisiasa na hatimaye kuvunjika kwa amani na utulivu. [185]
wapo
Kwa faida yako na wengine ikibidi fuatilia zaidi kwa wahusika, wahamiaji haramu wapo na ni tatizo kubwa. [186]
watu
Ni lazima watu wawe na mtazamo wa mbali. [187]
wenyeji
Katika michuano hiyo, Stars imepangwa Kundi A ikiwa na wenyeji wa michuano hiyo, Ivory Coast pamoja na Senegal na Zambia. [188]
wetu
Hali kadhalika kwa rais wetu atakapomaliza muda wake, kama alitenda kosa naye atashitakiwa," alisema Mohammed Omari. [189]
wiki
Katika makubaliano yetu ya kupanga bei tumeafikiana mambo mawili moja ni kukutana na Ewura kwa ajili ya kubadili takwimu za bei ya mafuta nchini na suala la pili ni kukutana kila wiki mara mbili - Alhamisi na Jumatatu- kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali, likiwemo suala la hali ya bidhaa hiyo," alifafanua Bisarara. [190]
yetu
Tunakiri kwamba akiba yetu inatosha hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi. [191]
yote
Ingawaje Rais mwenyewe amekuwa akipita na kujigamba kuwa wananchi wasiwe na hofu itakapofika 2010 yote aliyoyaahidi yatatekelezwa lakini muda umeshakuwa kikwazo kwake. [192]
zake
SIKU chache baada ya Israel kufanya mauaji ya kinyama dhidi ya Wapalestina zaidi ya 370 kwa kutumia ndege zake za kivita katika Ukanda wa Gaza, Rais Jakaya Kikwete, ametuma salamu za rambi rambi kwa Rais wa taifa hilo, Mahmoud Abbas, akieleza kushtushwa na mauaji hayo. [193]
zao
Mmiliki wa kampuni inayoagiza mafuta ya GBP, Salim Baabde alisema kuwa walifunga ofisi katika kipindi cha sikukuu ili kuwapa wafanyakazi wao fursa ya kusheherekea Krismasi na familia zao. [194]
zenu
Meseji zenu, email zenu zilinipa nguvu ya kuendelea na kila siku nilikuwa nasema hilo. [195]
zichukuliwe
Hatua zichukuliwe dhidi ya warsha zisizo na maana. [196]
zile
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Muhammed Seif Khatib alisema harakati hizo hazina tofauti na zile zilizoongozwa na Kanal Bacar wa visiwa vya Anjourn nchini Comoro. [197]
zinadai
Lakini kompyuta zinadai maamuzi ya papo kwa papo. [198]
zisizo
Anasema kuwa, serikali inapoangalia kipengele cha ajira huangalia zaidi katika ajira zisizo rasmi, jambo ambalo ni kinyume na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwapatia Watanzania ajira milioni mbili. [199]
zote
Kocha huyo aliyeshiriki upangaji wa ratiba hiyo jijini Abidjan, Ivory Coast Alhamisi iliyopita alisema kuwa siku zote amekuwa akiwakumbusha wachezaji wake kucheza kwa kujituma bila ya kuangalia aina ya timu, kitu ambacho anasema wamemwelewa na kuondoa hofu waliyokuwa nayo awali. [200]