matamshi

Ufafanuzi kutoka Wiktionary, kamusi iliyo huru

Kiswahili[hariri]

Nomino[hariri]

matamshi

  1. jinsi mtu anavyoongea au jinsi au namna ya kutamka.

Matamshi yako katika ngeli ya ya-.

Matamshi ndiyo hatua ya kwanza ya kuongea.

Matamshi huhusisha hewa inayotoka mapafuni. Mapafu husukuma hewa katika mkondo wa hewa na kuielekeza kooni. Kooni, hewa hupitia nyuzisauti. Nyuzisauti hutetemeka na kutoa sauti hewa inapozipitia. Nyuzisauti ndizo chanzi cha sauti zote zinazotamkwa na binadamu. Baada ya kupitia nyuzisauti, hewa huelekea kinywani. Katika kinywa, hewa hukumbana na viungo mbalimbali ambavyo ndivyo misingi ya matamshi, viungo hivi hujulikana kama alasauti.

Tafsiri[hariri]